Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
6Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1031

ANNUUR 1031

Ratings: (0)|Views: 4,701|Likes:
Published by MZALENDO.NET

More info:

Published by: MZALENDO.NET on Aug 24, 2012
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

10/30/2012

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1031 SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
Sensa ya Watu na Makazi 26 Agosti 2012:
Serikali yalikorogadakika za majeruhi
Ni Sensa ya liwalo na liwe-Ponda
Serikali, Waislamu bado ngoma nzito keshoWaazimia kukaa Itiqaf Misikitini. Bukoba wasema…Serikali isipate tabu itangaze waje wenyewe jela
MCHUNGAJI amekasirika.Anahoji maamuzi yetuWazanzibari kupitia Waziriwetu wa KATIBA na SHERIA,na WAZIRI wa UtamaduniUtalii na Michezo.
Anataka ufutwe nautokemezwe kwa mbali uleustaarabu wa Wazanzibari wakuheshimu Mwezi Mtukufu waRamadhani.Anafoka na kuhoji ni kwa ninini marufuku kutembea nusu uchi,kula chakula hadharani, kuvutasigara na kupigana mabusu ovyo barabarani, unywaji wa pombe
Wachungaji ni keroMuungano Zanzibar
Wanataka waingie Barazani Chukwani…Wakatoe hoja kuzika ustaarabu wa KiislamKama ndio gharama ya muungano, hatulipi
kiholela kwa kipindi cha Mwezimtukufu wa Ramadhani!Kuvunjika Muungano niJambo la hatari. Lakini Zanzibar kumezwa na kupoteza uwezo wakujiamulia mambo yake kitaifana kimataifa na kupotea katikaramani ya dunia, ni Jambo lahatari zaidi. Ni nani anaeridhia kuonamamlaka ya familia yakeyanamilikiwa na ndugu yakealie jirani?
Hiyo ni kashfa! Haikubaliki.(Soma Uk. 7)
Mh. Waziri Mkuu hii
nyumba ni yetu sote
Kudhani Kelele za mpangaji…ni kujidanganyaSana mnachelewesha tu muda wa kulipuka bomuTutahaha kutafuta mchawi wakati mchawi serikali
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda SHEIKH Alhad Mussa
 www.tawheedtz.orgUnakuhimiza ufanye Ibada ya Hijja 2012Fanyeni Haraka Kuhiji. Maana HajuiMmoja Wenu Kitakachomtokea – IbnAbbasMkabala na Msikiti wa Makonde,Kariakoo,Dar es Salaam022 2182068; 0776 070770; 0719 689528
Mtandao wa Tawheed
WAISLAMU Mjini Arusha wakiwa katika swala ya pamoja ya Eid iliyofanyika Msikiti Mkuu Arusha Jumapili iliyopita.
Mratibu azuiya Waislamu kuswali IddUmati wakusanyika Polisi TangaWawatoa Masheikh waliokamatwaKwa Waziri Mkuu Pinda futari yadoda
Waislam kukaa Itqaf siku saba za sensa - Uk. 3
 
2
 AN-NUUR
SHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0652 849227, 0713 110148, DSM.
www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
Tahariri/Habari
ULE mwezi mtukufuwa Ramadhani, mweziwa swaumu, mweziwa toba, umepita.Waislamu kote dunianiwamehitimisha nguzo hiiya nne ya Uislamu kwakusherehekea Sikukuuya Eid Fitr mwishonimwa wiki.
Wakati Ramadhaniikiondoka, tunaaminikuwa Waislamu watakuwawameiva baada ya kuhitimumafunzo ya mwezi mmojaya ucha Mungu.Mwenyezi Munguameeleza katika Qur’an,“Enyi mlioaminiimelazimishwakwenu funga kamailivyolazimishwa kwawale ambao waliopitakabla yenu ili mpate uchaMungu.” (Baqara: 183).Hivyo tunataraji kwambaUmma wa Kiislamu kwadarsa lililopatikana ndaniya Ramadhani, utaendeleakumcha Mwenyezi Mungukwa usahihi na kwataqwa zaidi hata katikamiezi mingine iliyosalia. Na hili hasa ndio lengola Ramadhani kwaWaislamu.Wakati wa Ramadhani, bila ya shaka sotetulishuhudia jinsi misikitiilivyokuwa ikijaa wauminikatika muda wa swala.Qur’ani Tukufuilikuwa ikisomwa kwawingi Misikitini na hatamajumbani, hali kadhalikana tasbihi, ibada za Tahajud,tarawehe, witir, kukeshausiku wa Lailatul Kadir nk.Ilimradi kilikuwa kipindicha ibada zaidi.Hofu yetu ni iwapoumma wa Kiislamuutadumu katika kumchaMungu kama ilivyokuwakatika Ramadhani. Kunahatari kwamba baada yaWaislamu kukamilishaRamadhani, mambo yotemema na mazuri yataishia
Waliokuwa wakiabuduRamadhani imeondoka
hapo. Ramadhani inawezakuondoka na ucha Munguwake.Umefika muda wakuacha mazoea haya yakuabudu Ramadhani badalaya Mwenyezi Mungu(sw). Kweli Ramadhaniimekwisha hadi mwakani,lakini tuliyekuwa tunafungana kuswali kwa ajili yakeyu hai milele, hamalizikina wala haishi kamailivyokwisha Ramadhani.Badala ya Muislamukuharibu funga yake kwakuasi baada ya Ramadhani,ni vyema akafungamanana marejeo ya mkufunziRamadhani (reference) ilikujiepusha na hasara kubwainayoweza kupatikana.Kufunga sita katikamfungo Mosi inawezakuwa msaada mkubwawa kutoharibu yaletuliyojifunza ndani yaRamadhani na itamsaidiamuumini kuzoea kudumukatika ibada sikuzinazofuata.Kama Muislamukaweza kufunga mwezimzima, ni aibu na fedhehakwamba Muislamu huyuatashindwa kulinda yalealiyokuwa akiyafanyandani ya Ramadhani nakurejea kwenye uchafualiokuwa akiishi nao kablaya Ramadhani.Tulilo na uhakika nalosote ni kwamba, Muislamuatakayeshindwa kulindaucha Mungu alioupatandani ya Ramadhani kwakuendelea nao katika mudaunaoendelea, huyo ndiyealiyeshindwa vibaya kabisakatika mafunzo ya ChuoKikuu Cha Ucha-Mungu,Ramadani. Atakuwaameambulia sifuri.Mwenyezi Munguatuwezeshe tudumu katikaucha Mungu na kuujengeaheshima Uislamu hapaulimwenguni. Amiin.
Serikali yalikoroga dakika za majeruhi
IKIWA ndio siku yasensa imewadia, badohali si shwari Waislamuwakibaki na msimamo wakutokuhesabiwa.
Katika kukabiliana nahali hiyo, kumekuwa nakamatakamata wakiandamwawale wanaotuhumiwakusambaza vipeperushivinavyowakataza Waislamukuhesabiwa au kuwashawishikwa namna yoyote.Habari kutoa mikoa,wilaya na vijiji mbalimbali,zinaonyesha kuwa badala yaserikali kutafuta namna yakutuliza mambo, imekuwaikichukua hatua ambazozinawafanya hata waleWaislamu ambao walikuwahawana msimamo juu yaususiaji huo, sasa waunganena wenzao.Habari kutoka Tangazinafahamisha kuwa janaumati mkubwa wa Waislamuulifurika katika kituo chaPolisi Chumbageni kujuahatma ya Masheikh waliokuwawamekamatwa wakidaiwakuhamasisha watu kususiasensa.Waliokamatwa walikuwani Sheikh Chambuso, UstadhHamad Ayoub, FadhilChambo, Hussein Idd naMwalimu Kassim Amar.“Mfumokristo upo kazini,Sheikh Chambuso na MwalimuKassim Amar wamekamatwakwa kuwaeleza Waislamu waTanga vijijini dhulma iliyoponchini dhidi ya Waislamu.Wameshikiliwa katika kituocha Polisi Mtandikeni, DugaMaforoni toka jana usiku wasaa tatu. Waislamu simamenikuwahami Askari hawa waAllah, Makamanda wa Mtume(s.a.w). Fikisha ujumbe huukwa nduguzo Waislamu.”Ujumbe huu wa manenoulioanza kusambaa jana saanne usiku, ndio uliowavutamamia ya Waislamu jijiniTanga leo asubuhi baada yakupata taarifa kuwa Masheikhhao walikuwa wameletwaChumbageni.Hadi tukienda mitamboni,Masheikh hao walikuwawameachiwa na kusindikizwakwa maandamano hadi MasjidQubah ambapo Waislamuwalikariri msimamo wao wakususia sensa.Katika maelezoyao walisema kuwawalimfahamisha wazi Mkuuwa Kituo cha Polisi kuwasi kweli kuwa serikali hainadini, bali dini ni ya serikaliipo na ndiyo hiyo ya watuambao wao ndio wenyekusikilizwa, huku Waislamu
Na Mwandishi Wetu
wakipuuzwa, kubaguliwa nakudharauliwa.Kwa mtindo huo ndiomaana Waislamu wameonaserikali iendelee na haoinaowathamini katika zoezihili la sensa.Kwa upande wa WilayaniSame, habari zinafahamishakuwa Mratibu wa Sensa aliyekatika kituo cha Kisiwani‘amelikoroga’ baada yakuwakosesha Walimu kuswaliswala ya Idd.Habari zinasema kuwailitolewa maelekezo kuwahakuna cha kuswali Idd, bali semina kwa walimuwaliopangwa kuhesabuwatu itaendelea kamakawaida wakati swala ya Iddinaendelea.Hata baada ya WalimuWaislamu kulalamika, badoMratibu alisisitiza hakuna chakuswali Idd.Habari zilizokuwa zimevujazilisema kuwa huo ulikuwamkakati uliowekwa tokaWilayani kuwa wakikosa kujakatika semina hiyo iwe sababuya kuondolewa.Walimu hao walifika nakwa mshangao, Mratibualipoita majina na kuonaWaislamu wapo akasemahakuna semina watu warudinyumbani wakale Idd.Hata hivyo, wakati huoswala ilikuwa ishamalizikawatu wanarejea kutokamisikitini.Mpasha habari wetuanafahamisha kuwa walimuWaislamu walikuja juu nawakataka kuwa maadhaliwamekoseshwa swala, basisemina iendelee.Tukio hilo limewafanyaWaislamu wengi kuona kuwakuna njama dhidi ya Waislamuna hivi sasa gumzo ni jinsi idadikubwa ya Walimu Waislamumjini Same walioomba kuwawahesabuji walivyoachwana kuchukuliwa Wakristowatupu.Kwa upande mwingineinafahamishwa kuwa hali sishwari Sumbawanga ambapofutari iliyoandaliwa na Mkuuwa Mkoa ilidoda baadakususiwa na Waislamu.Tukio hilo lilitanguliwa nalile la futari iliyoandaliwa naKatibu Tawala wa Mkoa (RAS)16 Agosti, 2012 ambapo baadaya watu kumaliza maakuli,Mkuu wa Wilaya ya Nkasialisimama na kuzungumzalakini akabaki akishangaa baada ya kujikuta akiachwa pweke baada ya kundi laWaislamu kunyanyuka nakuondoka mara tu alipoanzakuzungumzia sensa.Habari za tukio hilo laWaislamu kugomea Sensambele ya Mkuu wa Wilaya naRAS katika hafla ya mwalikowa futari, zilisambaa kwa kasina kuwa mada ya Khutba zaIjumaa takribani kwa Misikitiyote Sumbawanga mjinimsisitizo ukiwa Waislamukukataa kuhesabiwa.Khatibu wa Ijumaa Msikitiwa Qiblatain, AbdillahSalim Kanazawa, alielekezaWaislamu nini umuhimu waShura na nini madhara yakupinga Shura.Baadhi ya Maimamuakiwemo Imam Rajabwaliwasisitiza Waislamu kuwakinachohitajika ni umoja nakupigania haki na heshima yaUislamu na Waislamu.Katika kuhakikisha wapo pamoja na wanasaidianakwa lolote litakalotokea,kumetolewa namba za simukwamba mahali popote mtuatakapobughudhiwa kwakukataa kuhesabiwa apigeili ipigwe Adhana katikaMisikiti mbalimbali Waislamuwakusanyike na kuamua lakufanya.Ilikuwa ni baada ya tukiohilo Mkuu wa Mkoa nayeakaandaa futari katika jitihadaza kupoza mambo.Hata hivyo pamoja nakuandaliwa watu wa TV namagazeti, futari ilidoda baadaya Waalikwa Waislamu waliowengi kususia kwa kujuakuwa agenda itakuwa sensa.Futari hiyo ilifanyika Agosti18, 2012.Katika tukio jingine kutokaSumbawanga Mjini, mtotommoja wa chini ya miaka10 aliwaacha hoi wahesabujiwaliokuwa katika zoezi lamajaribio baada ya kukataakuhesabiwa na kusema kuwaakihesabiwa atakuwa kafiri.“Baba kasema sisiWaislamu hatuhesabiwi! Babakasema ambaye atahesabiwaatakuwa kafiri.”Alisema mtoto huyoaliyekutwa akiwa pekenyumbani na kutimua mbioakiwacha maofisa wa sensawakishangaa.
WAZIRI Mkuu Pinda
 
3
 AN-NUUR
SHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012
Habari
Ni Sensa ya liwalo na liwe-Ponda
ITAKUWA ni sensa yaliwalo na liwe, baada yaserikali kugoma kusikilizamadai ya waislamu.
Hiyo ni Kauli ya SheikhPonda Issa Ponda wakatiakisoma risala ya BarazaKuu la Jumuiya na Taasisiza Kiislamu katika Barazala Idd.Ponda amesema kuwa, bado wanaishauri Serikalikuakhirisha Sensa mpakamwakani ili iweze kufanyaSensa ya Kitaifa badala yakufanya Sensa ya ‘Liwalo nalilwe’.Kwa upande mwingine,kwa wanaokataa sensamsimamo umekuwa kuwakama ni kuwafunga, serikaliisipate tabu, itangazewatakuja wenyewe katikavituo vya Polisi na magerezakama itaona kwa busara zakekuwa hiyo ndiyo stahiki yawasiotaka kuhesabiwa.Wameyasema hayo baadhi ya Waislamu kutokamaeneo mbalimbali nchiniwakiitaka Serikali kuachakutumia vitisho kuhusu sualala Sensa ya watu na makazi na badala yake kujenga tabia yakuwasikiliza Waislamu kamainavyofanya kwa maaskofu.Katika tamko lililotolewawakati wa sherehe za Barazala Idd ambalo liliandaliwa naBaraza Kuu la Jumuiya naTaasisi za Kiislam Tanzaniana kufanyika katika viwanjavya Mwembeyanga JijiniDar es Salaam, Baraza Kuulimesisitiza kuwa Waislamuhawatashiriki zoezi hilo laSensa na kwamba siku yaSensa Waislamu wanatakiwakubaki Misikitini katika Ibadaya Itiqaaf na hata ikiwawatafungwa jela watakuwatayari, kuliko kukubalikuhesabiwa.Akisoma tamko hilombele ya umati mkubwawa Waislamu waliohudhuriasherehe hizo, SheikhPonda Issa Ponda alisemaingawa Serikali kupitiavyombo vyake vya habariimeendeleza propaganda zakuwa wamekubaliana naWaislamu juu ya kushirikiSensa, ukweli ni kwambahawajakubaliana popote juuya hilo.Kuhusu taarifazilizochapishwa magazetiniza Mkurugenzi wa TBC1kuwaomba radhi Waislamukwa kutoa takwimu zauwongo zinazowahujumu,na hiyo ndiyo kuwa sababu yawao kuachana na madai yao,Sheikh Ponda alisema TBC1ni kama mtoto, na hivyomalalamiko yao yalikuwani kwa Serikali inayomilikichombo hicho cha habari.“Madai ya mapendekezo
Na Bakari Mwakangwale
ya Waislamu kuhusu namnaya kuzuia hujuma katikaSensa ya watu na makazihayakuelekezwa kwa walewalioghushi takwimu(TBC1) na wenzake, bali nikwa Serikali kupitia Idara yaTakwimu ya Taifa”, alisema.Akasema kufuatiataarifa hizo zinazodaiwakusambazwa kwamba etimuafaka baina ya Serikali naWaislamu umekwishapatikanana kwamba sasa Waislamuwatashiriki Sensa ya watuna makazi inayotarajiwakuanza Agosti 26, 2012, badomsimamo wa Waislamu wakutoshiriki uko palepale.“Tunatamka kuwa, pamojana propaganda za TBC1kuomba radhi na vitishovya Serikali, msimamo waWaislamu wa kutoshirikizoezi la Sensa Agost 26, 2012upo palepale”, lilisema tamkohilo la Waislamu lenye kurasatatu.Katika hatua nyinginemwandishi wa habari hizialishuhudia mwamko waumati huo wa Waislamu wakususia zoezi hilo la Sensakwa kugombania vipeperushivilivyoandikwa kwa herufikubwa kuwa, “NYUMBAHII NI YA WAISLAMU,HATUANDIKISHWISENSA”.Mbali ya suala la Sensaya watu na makazi, jambo jingine ambalo lilivuta hisia zaWaislamu mkutanoni hapo nilile linalohusiana na mchakatowa maoni juu ya Katiba mpyaambayo ilihudhurishwa naSheikh Kondo Juma Bungo.Katika mkutano huo, SheikhBungo alisisitiza umuhimuwa Waislamu kushirikivema katika kuhakikishawanawasilisha maoni yaokuhusiana na masualambalimbali yanayowagusa.“Katiba ndiyo sheria mamaambayo inaelekeza namnaviongozi watakavyoongoza naraia wanavyotakiwa kufuatasheria hizo. Sasa kanunimojawapo ya sheria dunianikote ni kwamba haiwezikufanya kazi mahala ambaposheria zilizopo zinakinzanana sheria hiyo”, alisema hukuakitoa mifano kadhaa kutokakwenye Qur’an na Sunnah.Habari kutoka Bukobazinasema kuwa serikaliimetakiwa kutokupata tabukusambaza Polisi kukamataMuislamu mmoja mmoja, baliiseme wale wote wasiotakakuhesabiwa waje jela gani naWaislamu watafika.Maoni hayo yametolewana Masheikh na Maimamumbalimbali baada ya kutokeahali ya kusumbuliwa kwa baadhi ya viongozi waKiislamu wakidaiwakuhamasisha waumini waokukataa sensa.
WAISLAMU wametakiwakufurika misikitini kwa ajiliya ibada ya Itiqaf na Duakuanzia usiku wa Jumamosiya Agosti 25 siku ya sensana kufunga swaumu sikutatu kuanzia tarehe hiyokumuomba Allah juu yakadhia inazowakabili hivisasa.
Wito huo umetolewa naBaraza Kuu la Jumuiya naTaasisi za Kiislamu janaAgosti 24, 2012.“Ndugu Waislamu,tumuogope Allah na kamwetusiogope vitisho. Sote kwa pamoja tutekeleze maazimiohaya ili historia ituandikekuwa tulipigania haki zaWaislamu Tanzania”. Ilielezataarifa ya Jumuia hiyo.Akizungumza katika kikaokilichoandaliwa na Jumuiahiyo na kuhudhuriwa naMaimamu kutoka misikitimbalimbali ya jijini Dar esSalaam, kilichofanyika katikaukumbi wa Makao Makuu yaTAMPRO Magomeni Mapipa jana, Katibu wa Jumuia naTaasisi za Kiislamu nchini,Sheikh Ponda Issa Ponda,amesema Masheikh waJumuia na Taasisi 63 nchinikwa pamoja wamekubalianaWaislamu nchini kutekelezaibada hizo kufuatia kitendocha serikali kwa makusudikupuuza madai ya Waislamu.Ponda amesema hakuna
Waislam kukaa Itqaf siku saba za sensa
Watafunga siku tatu, kusoma KunutiMufti, RC wapata wakati mgumu SongeaDC, Madiwani, Waziri Malima hoi Mkuranga
Na Shaaban Rajab,Bakari Mwakangale
kiongozi wa Jumuia naTaasisi ya Kiislamu aliyewahikuhubiri kuwa sensa niharamu, bali wametoa sababuzao za msingi za kususia zoezihilo ambazo wamezieleza nakuzifafanua vizuri, ila serikaliinapotosha kwa makusudi.Akasema, Viongozi waJumuiya wametaja baadhiya madai ya Waislamu kuwani suala la wanafunzi waKiislamu wa kidato cha sitakufelishwa kwa makusudi naBaraza la Mitihani la Taifa nahakuna hatua zilizochukuliwadhidi ya wahusika.Tukio jingine ambaolimepuuzwa ni Waislamukuletewa Kadhi asiye nanguvu za kisheria.Taarifa ya Jumuia hiyoimeeleza kuwa Waislamuwanataka Kadhi aliyeteuliwana Jumuia zote za Kiislamuna ambaye anatambuliwa naKatiba ya nchi.Suala la tatu limetajwakuwa ni sensa ya watu namakazi ambapo Waislamuwanataka kiwepo kipengelecha dini kwenye dodoso lasensa ili kujua idadi kamili yawatu na dini zao, lengo likiwani kuondoa takwimu potofuzinazoendelea kutumiwa naserikali na taasisi zisizo zakiserikali kwa maslahi yao nakwa hasara ya Uislamu.Aidha, Waislamu kwamuda mrefu wametakaserikali kujiunga na Jumuiaya Kiuchumi ya Kiislamu yaOIC, lakini licha ya serikaliyenyewe kukiri kuwa hakunaathari mbaya kwa nchikujiunga na jumuia hiyo, badohaitaki kwa sababu Maaskofuhawataki.Alisema, inasikitishakwamba hata wasomiwalishiriki kupotosha sualahili katika jitihada za kuzimahoja ya Waislamu kuitakaserikali kujinga na OIC.Akakumbusha kuwa Prof.Mwesiga Baregu aliwahikutetea hatua ya serikalikuzima uwezekano wakujiunga na Jumuia hiyo palealiponukuliwa akisema kuwamoja ya kanuni na masharti yaOIC ya kujiunga mwanachamampya, ni lazima mwanachamahuyo (nchi) iwe na idadikubwa ya Waislamu, kinyumena hapo mwanachama huyoatakuwa hajakidhi kigezo chakujiunga na jumuia hiyo.Alisema, umefika wakatiWaislamu wa Tanzania kuwana msimamo na kushikamana pamoja katika masuala yamsingi yanayohusu maslahiya Waislamu na Uislamu.“Ndugu Waislamutumuogope Allah na kamwetusiogope vitisho. Sote kwa pamoja tutekeleze maazimiohaya ili historia ituandikekuwa tulipigania haki zaWaislamu Tanzania, usiku waterehe 25 kuamkia 26 Agostisote tuelekee katika misikitiya jirani kwa ajili ya ibada zaitiqaf na kunut. Kwa pamojatutekeleze maazimio hayaili historia idhihiri”, ilisemasehemu ya azimio hilo laJumuia na Taasisi za Kiislamunchini.Aidha imefahamishwakuwa Mufti wa BakwataIssa Shaaban Simba akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoawa Ruvuma Bw. SaidKalembo, wametahayarimjini Songea pale Waislamuwalipowahakikishia kwambawao hawahesabiwi.Mufti Simba amekuwaSongea akishirikiana naMkuu wa mkoa kuhamasishaWaislamu kushiriki katikasensa.Wakati Mufti na baadhiya Masheikh wa Bakwatawakifanya ziara za mikoanikushinikiza Waislamukushiriki sensa, hukoMkuranga wamedhihirishahadharani kwambahawatoshiriki zoezi hilo.Hayo yamejiri katikamkutano uliohudhuriwa naMadiwani pamoja na NaibuWaziri wa Kilimo Bw. AdamMalima, ambao walihamasishaWaislamu kushiriki zoezi lasensa na kukemea vipeperushivilivyokuwa vikielezea sababuza Waislamu kugomea sensahiyo.Tukio hilo lilikuja baadaya Ust. Abdulswamad kutokaBaraza Kuu kupewa nafasiya kuhutubia katika mkutanohuo huku wageni wenginewakidhani kuwa anatokaBAKWATA baada ya kusikiakuwa anatoka Baraza Kuu.Ust. Abdulswamad baada yakupata nafasi hiyo alibainishakuwa yeye ni miongoni mwawalioandaa kipeperushihicho na kuwataka Waislamukupima yale waliyoelezwakatika kipeperushi na yalewaliyoelezwa na mawakalawa serikali kujua ukweli.Hata baaada ya kutoa nasahazake Waislamu walisisitizakwamba hawatashiriki zoezila sensa mbele ya mawakalahao wa serikali.

Activity (6)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 hundred reads
1 thousand reads
Salum Ussi liked this

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->