Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword
Like this
10Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1037

ANNUUR 1037

Ratings: (0)|Views: 9,376 |Likes:
Published by Hassan Mussa Khamis

More info:

Published by: Hassan Mussa Khamis on Oct 06, 2012
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

07/19/2014

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1037
Dhuul-Qaad
1434, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
Rungu la NECTA lawaponda tena Waislamu
Safari hii ni kwa Walimu wa StashahadaNi mchezo wa kuondoa Dini baada ya Qubah (?)Zanzibar nayo kubanwa au wawe na NECZA yao
 DKT. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania.
WITO umetolewa kwaWaisamu Jijini Dar esSalaam, kujitoa na kwenda
Sensa ilikuwa Baraka
Kumbe ilisilimisha Mkristo mmojaWaislamu watakiwa kutembelea wafungwa
Inaendelea Uk. 3
Ubaya Ubaya sasa
kuleta balaa Unguja
Uamsho watakiwa kuanzia Jihad Jang’ombeWaje kwa Baraza la Mji Zanzibar ing’are
Uk. 3
Na Bakari MwakangwaleMagerezani kuwatembeleaWaislamu, kwa ajili yakuwasaidia kwani wengiwalioko huko wanahitaji
Washenga wa maadui wa
Zanzibar watolewe serikalini
 Aanze kuondoka Mwinyihaji Makame Au aseme Bububu adui alikuwa nani?Wanadhani fitna, farka itawapa Urais 2015
Uk. 4
 MWENYEKITI wa CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Julius Mtatiro katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanjavya Levolosi, Jijini Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita. Habari kamili Uk. 16.
Tapeli ajizolea fedhakutoka kwa Waislam
Uk. 7
 
2
 AN-NUUR
Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM.
www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
Tahariri/Tangazo
P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0754 260241Fax: 2450822 Dar es SalaamE-mail: ipcubungoislamic@gmail.com
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL
Maandalizi ya Kidatocha Kwanza 2013
Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic HighSchool) inatangaza
PROGRAMU
maalum ya maandaliziya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunziWaislamu.Programu hii itaanza tarehe
15/09/2012
hadi tarehe
10/12/2012
Jumatatu hadi Jumamosi saa
3:00
asubuhihadi saa
8:30
mchana.Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni:1. Elimu ya Dini ya Kiislamu2. English Language3. Arabic Language4. Mathematics6. Introduction to Computer Ni programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi10/12/2012) Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs
50,000/=
inalipwa yote mwanzoni mwa programu.Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BUREKwa mawasiliano zaidi:
0714 888557, 0659 204013,0717 295107
MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU
Wabillah Tawfiiq
MKUU WA SHULE
Bismillahir Rahmaanir Rahiim
HIVI sasa Waislamu,wake kwa waume kutokanchi mbalimbali dunianiwanaelekea nchini SaudiArabia kwa ajili yakutekeleza nguzo ya tanoya Uislamu, ambayo niibada ya Hija.
Hapa kwetu Tanzaniakadhalika, ndugu zetuwa Kiislamu ambaowamejaaliwa kupatamasurufu ya kutekelezaibada hiyo, nao wamekuwakatika hatua za mwishokuelekea Saudia kwa lengohilo hilo.Uislamu umejengwakatika nguzo tano.Kushuhudia kwambahakuna Mola anayestahikikuabudiwa kwa hakiisipokuwa Allah na BwanaMtume Muhammad(SAW) ni mjumbe wake,kusimamisha sala tano,kutoa zaka, kufunga mwezimtukufu wa Ramadhani nakwenda Hijja. (Bukhari naMuslim).Kwa bahati mbayaWaislamu wengi tunazisomana kuzikariri nguzo hizi bila ya kuzingatia uzitona umuhimu wake katikamaisha yetu ya kila siku.Uislamu haumkubali mtuyoyote ambaye hakutimizanguzo za Dini, inapokuwamtu huyo amepewa naMwenyezi Mungu uwezowa kuzitimiza.Mwenyezi Mungu (SW)anaamuru ifuatavyo: “Natimizeni Hijja na Umra kwaajili ya Mwenyezi Mungu”(Al-Baqara, 2:196)Hapa Mwenyezi Mungu(SW) anataka Waislamuwaitekeleze ibada nanguzo ya Hijja. Na kwawale wanaokwenda Hijja,anawataka waitimize ibadahiyo kwa ukamilifu. Na kwa ajili ya MwenyeziMungu imewawajibikiawatu wafanye Hijjakatika nyumba hiyo kwayule awezaye kwendahuko. Na atakayekufuru(atakayekanusha) basi
Kila la kherimahujaii wetu
Mwenyezi Mungu si mhitajikuwahitaji walimwengu.”(Al Imran, 3:97)Kwa maneno mengine,ni wajibu kwa kila mwenyeuwezo kwenda Hijja kwa ajiliya Mola wake. MwenyeziMungu (SW) anaichukuliaHijja kuwa ni haki yakekutoka kwa viumbe vyakewaliomuamini na ambaoamewapa uwezo. Na kwakuwa anayetoa uwezo niyeye Mwenyewe (SW), basi anamjua kila aliyempauwezo na asiyempa. Hivyo,kwa ambaye amepewauwezo na kwa sababu yoyoteile, hakwenda kuhiji Makka, basi ajue kuwa Mola wakehamuhitajii kwa lolote.Tuna hakika kwambaWaislamu wengi wanajuafaida za Hijja. HivyoMuislamu hana budikutanguliza kwenda Hijjakwanza kuliko kwa mfano,kufanya harusi inayogharimuthamani ya Hijja zaidi yamoja.Katika Hadithiiliyopokelewa na AbuHuraira (RA), Mtume(SAW) amesema: “Mwenyekufanya Hijja bila ya kusemamaneno machafu na bila yakufanya vitendo vichafu,atasamehewa madhambiyeke atakaporudi kama sikualiyozaliwa na mama yake.”(Bukhari, Muslim).Kwa mapenzi yakesubhanahu Wataala, Rehemaza Allah hazisimami kwayule anayekwenda kuhiji peke yake. Bali wapenzi wotewa Mahujaji wananufaikakwa uhakika kutokana nadua watakazoombewa naHajji.Hoja hii imebainishwana Mjumbe wa MwenyeziMungu (SAW) katikaHadithi iliyopokelewa naAbu Huraira (RA) kamaifuatavyo:“Husamehewa madhambiyake mwenye kuhiji pamojana wale watakao-ombewana mwenye kuhiji.” (Al-Bazzari, At-tabraany, IbnKhuzaimah, na Al-Hakim).Wako miongoni mwetuWaislamu wanaojizuiliakwenda Hijja kwa dhana yakuwa wanachohitaji kutoani kingi na hakirudi. Hii nidhana potofu haiendani namafundisho ya Dini. Ni potofukwa sababu lengo la Uislamuni kupata radhi za Mola,kuepukana na moto, na kupata pepo. Hijja inamhakikishiaMuislamu haya yote kwampigo.Lakini pia dhana hiyo ni potofu kwa sababu anachokitoamtu kwa kufunga safari yaHijja au Umra hakipotei;kinarudishwa na kuzidishwa.Katika Hadithi iliyopokelewana Anas bin Malik (RA),Mtume(SAW) amesema:“Mwenye kufanya Hijjana mwenye kufanya Umrani wageni wa MwenyeziMungu Mtukufu. Hupewawanachoomba, na (Allah)anajibu dua zao, nahurudishiwa walivyotoa,dirham (au shilingi) moja kwadirham (au shilingi) milionimoja”. (Al-Baihaqy). Nguzo ya kwanza katikanguzo za Hijja ni kuhirimia.Wanaume wote kubadili nguona kuvaa nguo za aina moja.Mashuka mawili meupe,moja juu mabegani na la pilikufunga kiunoni.Hapa tunajifunza kitukimoja muhimu. Nacho niusawa kwa binadamu. Hakunanafasi ya kuwepo alamaalama zinazowatofautishawatu kwa mataifa yao, utajiriwao, vyeo vyao, n.k. nazinazowafanya wajinasibishena cheo, kabila, mali, utaifa aukundi fulani. Hali hii inatoanafasi ya mtu kujijua zaidi.Kiburi, majivuno, kujiona,chuki, miongoni mwa maasiyaliyo ndani ya moyo wa mtuyanakuwa havana nafasi.Mtu anapata nafasi yakupata hisia ya utu wake,na hali itakavyokuwa sikuya kufufuliwa. HivyoHijja ni fursa kubwa sanainayomsaidia mtu katikakukumbuka mwisho wake,kujenga Uislamu wake, nakumkumbuka sana Molawake.Kisimamo cha Arafakinatoa wasaa zaidi watumilioni tatu hukutana katikauwanja mmoja. Huo ni mfanowa siku ya Qiyama ambapoAllah atatukusanya wanadamuwote walioumbwa na kuishikatika uso wa ardhi pamojakatika uwanja mmoja. Wenyeakili wanatakiwa wanufaikena mkusanyiko huo kwakuikumbuka siku hiyo yakiyama.Watu wote wanaokwendaHijja kwa ajili ya Allah(SW) ni vyema wakawekamapatano baina ya watuwaliokuwa wamekhasimiana.Haji mtarajiwa anatakiwaasuluhishane na kila Mwislamualiyekuwa amekhasimiananaye. Kwa maneno mengine,anatakiwa akamilishe imaniyake kwa kuondoa chuki,hasama, kuondosheanakinyongo, kusuluhishana nakupeana radhi na Waislamuwenzake ambao ndio nduguzake wa kiroho.Ibada ya Hijja inaanzia mtuanapokuwa nyumbani kwakena katika nchi yake. Muislamuanatakiwa aondoke kwa safariya Hijja akiwa amelipa madeniyake yote anayodaiwa, naamewaridhisha watu wakewa nyumbani kwa kuwaachiamahitaji yao ya maisha kwamuda wote anaotarajiwakuweko safarini.Hivi ndivyo Muislamuanatakiwa anapoondokakuelekea Makka kuitikia witowa Mola wake, anatakiwaaondoke huku ndani ya moyowake ukiwa umejaza mapenzikwa Mola wake (SW), Mtumewake Muhammad (SAW), nandugu zake Waislamu wote. Ni dhahiri kuwa MwenyeziMungu (SW) ametuwekeaHijja ili tujenge umoja waKiislamu kimataifa. Swali lakujiuliza ni je, sisi tunaotokanchi moja tunajuana? Je,tunashirikiana? Je, tunamshikamano? Ni vyema safari hiimahujaji wakajenga umojana kufahamiana kabla yakuondoka kwenda Hijja ilikujenga umoja unaofahamikakatika nchi yetu kwanza. Niajabu taasisi za kusafirishana kuhudumia mahujajinchini kusafirisha Mahujajina kutekeleza ibada zotehuko Makka na kurejeanyumbani bila ya Mahujajiwa taasisi moja kujuana nawa taasisi nyingine hali yakuwa wanatoka Taifa moja.Si kisimamo cha Arafa walaMinna, kote huko kupishanatu. Hutokezea wachachemiongoni mwao wakajuanakwa bahati. Lakini badohakuna juhudi inayochukuliwakujenga mtandao angalau wawale waliobahatika kwendaHijja wakafahamiana vizuri.Katika hali hii kwelilile lengo kuu la Hijjalinapatikana? Vipi kuhusufalsafa ya Hijja tunaifahamu?Kuna haja ya waandaaji waHija kulishughulikia tatizohili. Mahujaji wafahamianena kushikamana tangunyumbani.Tumalizie kwa kusema,kama ambavyo MwenyeziMungu amewajaalia afyanjema, masurufu na wasaakwa ajili ya kutekelezaibada ya Hija, tunamuombaawajaalie pia Hija njemana iliyokamilika. Hija maq buul.
 
3
 AN-NUUR
Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012
Habari
Rungu la NECTA lawaponda tena Waislamu
MGOGORO kati yaWaislamu na Baraza laMitihani Tanzania unazidikupanuka baada ya Barazahilo kuzuiya matokeoya baadhi ya wanachuokwa madai kuwa NECTAhaitambui somo la Maarifaya Uislamu.
Baadhi ya wanafunziwaliozuiwa masomo yaowanasema kuwa katikamitihani yao ya kidato cha sitawalifanya masomo ya ‘arts’ pamoja na Islamic Knowledgena kufaulu kwa kiwango chakuwa na sifa za kuchukuaMafunzo ya Ualimu kiwangocha Stashahada (Diploma) nakwamba waliwalisha vielelezovyao NECTA wakasajiliwa.Hata hivyo wanasemakuwa, baada ya kufanyamtihani wa kumalizi koziyao ya masomo wakiwawamefanya masomo mawiliya kufundishia, moja likiwaElimu ya Dini ya Kiislamu,Baraza la Mitihani limezuiyamatokeo yao likidai kuwasomo la Maarifa ya Uislamuhalitambuliki.Walimu hao Tarajaliwamesema kuwawameshangazwa na hatuahiyo ya NECTA kwani tanguwakati wa Usajili mpakakufanyika mtihani Barazaliliwakubali kama wanachuowenye sifa, sasa wanashangaahii kanuni imekuja kutokawapi.Kwa upande wa baadhiya wakufunzi waliotoamaoni yao wamesema kuwawameshangazwa na kitendohicho cha NECTA kwaniilivyo Baraza hutahini mtihaniwa Maarifa ya Uislamu kwaO Level na A Level, sasa“walimu wa kufundisha somohilo watapatikana kutokawapi kama Baraza halitambuisomo hilo katika kiwangocha kusomesha walimu?”Wamehoji.“Hizi ni njama,hivi wanataka walimuwanaosomesha Elimu yaDini ya Kiislamu wasiwe naMaarifa ya Uislamu na Ualimu japo wa Diploma ili wapatekisingizio cha kuwatukanaWaislamu kuwa walimu waMadrasa ndio wanaosomeshasekondari! Kama hawatakiwasomi Waislamu, mbonakatika mitihani ya kidato channe na sita, hawachukui tuWaislamu mitaani na kuwapakutunga na kusahihishamitihani ya kidato cha nnena sita?” Alihoji Mwalimummoja ambaye hata hivyo
Na Mwandishi Wetu
hakutaka kutajwa jina lakegazetini.Mwalimu huyo anasemakuwa kisingizio cha NECTAkuwa kuna Waraka waWizara usiotambua Islamicknowledge hayana mashikokwa sababu yapo pia masomomengine ambayo hivi sasayanatambuliwa na Barazala Mitihani Tanzania kuwayanafanya miunganiko(Combinations), wakati katikaWaraka huo hayakutajwa.Kwa upande mwingineakasema kuwa katika mitihaniya kidato cha sita (ACSEE),kwa upande wa Zanzibar,wanafunzi wanafanya IslamicKnowledge kama somomojawapo katika combinationya masomo matatu yaPrincipal Pass.Swali ni je, kwa msimamohuo Baraza na kwa kuzingatiakuwa Baraza hilo ndiolinasimamia pia mitihani kwaZanzibar, kwa maana kuwani suala linalosimamiwa naSerikali ya Muungano, “je,ina maana NECTA itafutamatokeo ya wanachuo wotekutoka Zanzibar?”Kwa upande wa baadhi yaWamiliki wa Shule na Vyuovya Ualimu vya Kiislamuwamesema kuwa, waomchepuo wao mkuu ni Somola Dini ya Kiislamu kamailivyo kilimo kwa shule zakilimo.Kwa hiyo, Barazakutotambua somo hilo nisawa na kuwazuiya Waislamukusomesha walimu wenye sifawa kusomesha somo hilo.“Shule na Vyuo vyetuwamevisajili kwa kuvitambuakuwa ni vya kidini, kutotambuasomo la dini, maana yakeni kutukataza kusomeshawalimu wataalamu ili baadaewatumie kisingizio chakutokuwa na walimu wenyesifa kufunga shule na vyuovyetu.” Amesema Mkuummoja wa Chuo.Hata hivyo, baadhi yaWaislamu waliotoa maoniyao kuhusu sakata hiliwamekumbushia ule Warakaulitolewa miaka ya 1980s baada ya kuanzishwa shuleza kwanza za seminari zaKiislamu uliosema kuwa shuleza seminari si shule na kwambawanafunzi wake wakimalizakidato cha nne hata wakifauluhawatachaguliwa kuingiakidato cha tano katika shuleza seriikali.Kabla Waislamuhawajaanzisha Qubah naJabal Hira, ilikuwa wanafunzikutoka shule za seminariza Kikristo wakichaguliwakuingia High School zaserikali na kisha Chuo Kikuucha Dar es Salaam.Wanasema, ilikuwa baadaya kuona Waislamu naowanaanzisha seminari ndioWaraka huo ukatoka.Hata hivyo wanasemakuwa, Waraka huoulitelekezwa kinyemela, kwamaana kuwa haukutekelezwa baada ya kuonekana kuwahaukuwakatisha tamaaWaislamu na ‘mfumo’ ukaonakuwa watakaoathirika zaidini Wakristo kwa sababundio walikuwa na seminarinyingi.“Walidhani kuwa kwakutoa Waraka huo, Waislamuwangevunjika moyo wafungeshule zao na wazazi waKiislamu wasingepelekawatoto wao katika shule hizowakati Waraka wa Serikalihauzitambui, lakini walipoonazinaendelea wakauficha.”Amesema mwanaharakatimmoja wa Kiislamu.Kwa rekodi hiyo, baadhi yaWaislamu waliokuwa katikaharakati za kuanzisha seminariza kwanza za Kinondoni,Jumuiya, Masjid Qubahna Jabal Hira, wanasemakuwa, huenda hatua hii yaBaraza la Mitihani Tanzania,ni mkakati wa kuwakatishatamaa na kuwawekea vikwazoWaislamu wasisomeshewalimu wenye sifa zakusomesha Somo la Diniya Kiislamu katika ngaziya sekondari na hata VyuoVikuu.Taarifa tulizozipatawakati tukienda mitamboni jana zilifahamisha kuwaWalimu Tarajali ambaomatokeo yao yamezuiwa,ilikuwa wawasilishe barua yamalalamiko yao kwa KatibuMkuu, Wizara ya Elimu naMafunzo ya Ufundi.
Sensa ilikuwa Baraka
Inatoka Uk. 1msaada wa hali na mali.
Wito huo umetolewana Ustadhi Ally Mbarukuakiongea na Mwandishi wahabari hizi akielezea hali yaWaislamu magerezani nawafungwa kwa ujumla.Ust. Mbaruku amebainihayo baada ya kukamatwana Jeshi la Polisi, mweziSeptemba, mwaka huu kishakuwekwa rumande katikaGereza la Segerea kwa kilekilichodaiwa kuwa ni kosa lakugomea zoezi la Sensa yawatu na Makazi.Mbali ya Ust. Mbarukukubaini hali hiyo, lakini pia alidai yeye pamoja nawenzake watano, wakiwagerezani huko walifanikiwakumsilimisha mtuhumiwammoja waliyemtaja kwa jinala Yona Edward Pius.Mbaruku amesema, kunawatuhumiwa Waislamu wengiwanaohitaji msaada wa hali nahaswa namna ya kuwawekeadhamana ambazo anadaiwengi wao wamekwama kwahila na dhulma tu.Alisema, siku chachealizokuwa gerezani,amejifunza mengi na kubainikwamba Waislamu wengiwaliopo huko wapo kwamakosa ya kubambikiwa aukukosa uwezo wa ndugu zaokuwasimamia katika masualaya dhamana.Kwa maana hiyo, aliwatakaWaislamu wakiwemowanasheria, kuweka utaratibiwa kufika magerezani kuongeana watuhumiwa.Alisema, yeye baada yakutoka kwa dhamana nawezake kufuatia sakata hilola Sensa, ameshafanya juhudikwa kuwasimamia mahabusuWaislamu wapatao watanona kufanikiwa kuwatoa kwadhamana.Kuhusu Bw. Yona Edward,waliyemsilimisha akiwagerezani, alisema awaliwalikutana naye katika selo yakituo cha Polisi cha Oysterbay,ambapo wakijadili suala lasensa na Uislamu humo kituocha polisi, Bw. Yona, alivutikanayo.Baada ya hapo, walitoka na baadaye walikutana tena katikamahabusu ya Segerea, ambapo jamaa (Edward) aliwaelezania yake ya kusilimu, ambapowalimuona Sheikh Mkuu wamahabusu, aliyemtaja kwa jina la Sheikh Ally Jabir nakumsilimisha.Baada ya kusilimu, alisema,Yona, alichagua jina la Ismail,na kisha kuanza kumfundishamasuala ya dini huko hukogerezani na viongozi waKiislamu Mahabusu waliokohumo.Alisema, walianza kutokawao kwa dhamana kishaalimsimamia Bw. Islamil(Yona) kwa kuwafuatawazi wake ambao walitoaushirikiano hatimaye nayealitoka kwa dhamana.Bw. Ismail (Yona) ambayealipitia mafunzo ya dinikatika Chuo Cha Biblia(Bible School) na kuhitimumasomo hayo mwaka 2003,alikabidhiwa cheti chakusilimu chenye namba 1201,cha Baraza Kuu.Mbali ya cheti hichoIslamil amepata hati ya kiapocha kusilimu cha Mahakamaya Mwanzo ya Wilaya yaKinondoni, ya tarehe25.9.2012, iliyosainiwa naHakim E. M. Kihiyo.Kwa sasa Bw. Ismail,anapata elimu ya dini yakempya ya Kiislamu katikaMadrasa Istiqama, iliyopo jirani na Masjidi RahmanMakangira Msasani.
 DKT. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji NECTA.

Activity (10)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 thousand reads
1 hundred reads

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->