Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword
Like this
18Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1039

ANNUUR 1039

Ratings: (0)|Views: 10,165 |Likes:
Published by Hassan Mussa Khamis

More info:

Published by: Hassan Mussa Khamis on Oct 19, 2012
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

11/06/2012

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1039
Dhuul-Hijja
1434, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
Mansour yamemkuta
 Alisema kweli Ilunga
 Ataka kuchoma kichaka cha mfumokristoMaalim Seif naye sasa amekalia kuti kavu
Kadhia ya Ponda, Sheikh Farid:
 Vita ya Msalaba yaja kwa nguvu
Washakamata Mombasa Waislamu wanauliwaNdoto za Wazanzibari kupumua kuyeyuka pundeTusaidie serikali, Afande Mwema kuzuiya ‘mbweha’
Polisi waharibu maliMarkaz Chang’ombe
Wavunja madrisha, wapiga wanafunziMasheikh Azhar waduwaa, wafunga ChuoBakwata wazika historia ya Chang’ombe’Mpemba’ aliyenunua ajitafutia balaa
Mbagala sawa Mwembechai
Jamhuri kukosa uadilifu katika masuala ya kidiniWaislamu walishambuliwa wakienda IjumaaTatizo Polisi kupuuza malalamiko ya Waislamu
 SHEIKH Ponda Issa Ponda SHEIKH Farid Hadd 
Ni Msiba mkubwa!
Inapokuwa heri ya James Mbatia Al Had kujipendekeza mpaka lini?
Uk. 10
 BAADHI ya polisi waliovamia Chuo cha Kiislamu Markaz Chang'ombe ambapo baadhi majengo yaliharibiwa na mali kupotea wakiongea na maafisa wa Ubalozi wa Misri. Chuohicho kipo chini ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar Misri,
 
2
AN-NUUR
Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM.
www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
Tahariri/Habari
Mansour yamemkuta Alisema kweli Ilunga
Na Mwandishi Wetu
AMESEMA kweli SheikhIlunga Hassan Kapungu,ukitaka balaa hojimuungano.Mansour alitangazakutaka Zanzibar huru, yenyekiti Umoja wa Mataifa;yamemkuta.Rais Alli Mohammed Sheinamefuta uteuzi wa Mjumbe waBaraza la Mapinduzi aliokuwaamempa Mansour Yussuf Himid.Badala yake nafasi hiyoamepewa mtu ambaye kwasiku za hivi karibuni amekuwaakijipamba kwa kauli za‘Maskani ya Kisonge’ zakutaka Zanzibar iendeleekuenzi muungano wa serikalimbili.Huyu ni Shawana BukhetiHassan ambaye katika uchaguzimdogo wa hivi karibuni Jimbola Bububu anatajwa kuwammoja wa makada wa CCMwaliofanikisha kupatikanaushindi wa kibabe wa chamahicho tawala.Ukiacha aliyokwishakuyasema huko nyumakuonyesha kuwa muundowa muungano uliopo haufaina kwamba Wazanzibariwanataka kupumua, hivikaribuni katika kongamanolililofanyika katika hoteli yaBwawani, Mansur, aliwatakaWazanzibari kusimama imarakupigania uhuru wa nchiyao.“Huu ni wakati wakuzungumza kwa dhati,ni wakati wa kuzungumzaukweli, bila ya hofu wala bilawoga kwa maana hofu na wogahaukupeleki mahali, haswaunapozungumzia mustakabaliwa nchi hii.” Alisema.Kwa upande mwingineMansour aliwatakaWazanzibari kuwapuuzaviongozi wa serikali na kisiasawanaotaka kulazimishamuungano wa serikali mbiliambao alisema kuwa umefelikutatua zinazoitwa kero zamuungano.“Anaposimama kiongoziwa juu wa nchi aliyepewaimani na watu, akisimamaakasema mkitaka msitake,muungano utakuwa hivihivi (wa serikali mbili), miehuwa najiuliza, kulikoni?”“Unamlazimisha nani,wakati mwanao mwenyewendani ya nyumba zamahizi huwezi kumlazimisha,sasa utoke ukawashurutishewatu, viongozi wa namnahiyo ni waovu, na wamekosamuelekeo.”Alisema Mansour nakusisitiza kuwa Zanzibar inahitaji “viongozi ambaowana hikima, wana busara(na) wanarai watu….Kiongozihawezi kushurutisha watu.”Alichosema na kusisitizaMansour katika kongamanohilo ni kuwa mfumo wamuungano uliopo hauwasaidiiWazanzibari na kwamba hataTume na Kamati zilizowahikuundwa kuangalia matatizoya muungano, zilibaini kuwamfumo wa serikali mbilihaufai.“Miaka 48 watuwameshindwa kuzungumza,tutazungumza leo, kwa mfanokuna kamati karibia ya 25,zote hizi zimefikia maamuzimamoja tu, kwamba mfumotuliofikia haufai, hawa woteni wasomi waliobobea na timuzao ni za wasomi waliobobea,tena nyingine zinaundwamie bado mi ndogo nipo njenasoma.”“Sasa leo msitunyosheevidole kina Moyo na Mansour,wanataka kuharibu, hawandio waliosema kwambahuu mfumo sio. Sasa jamanikamati tumeziunda wenyewe,zimeundwa na Jamhuri yaMuungano wa Tanzaniana serikali ya Mapinduziya Zanzibra na kila kaziwaliyopewa jibu ni moja tu,mfumo siyo.”Hata hivyo, pamoja nakusema yale yale ambayoyalishasemwa na Tumezilizowahi kuundwa naserikali, ambayo hatahivyo hayakufanyiwa kazi,inaonekana Mansour kagusaeneo lisilotakiwa kamaalivyosema Ilunga.Amehoji muungano kitualichosema kwamba ni sawana kugusa mfumokristounaodhibiti Zanzibar kupitiamuungano huu wa serikalimbili.Katika makongamano
QUR’AN Tukufu ni kitabuambacho ndio muongoziwa Waislamu. Chenyewena Hadithi za MtumeMuhammad (s.a.w) ndiomihimili ya imani yaKiislamu.
Hivi karibuni kijanaEmannuel Josephat, mkaziwa Mbagala anadaiwamakusudi, alitemea mate nakukojolea kitabu kitukufucha Qur’an mbele yawenzake Waislamu.Kukojolewa Qur’an nidharau na tusi kubwa nauchokozi wa makusudikwa Waislamu popote pale.Lakini zaidi, kitendo hichokinatafsiri chuki kubwadhidi ya Waislamu na imaniyao.Hatua hiyo imeleta tafranikubwa ambapo Makanisayameharibiwa, misikitiimeharibiwa na Waislamuwamepigwa mabomu nakujeruhiwa.Hayo yote ni matokeo yahasira zilizosababishwa natendo hilo chafu la kukojoleakitabu cha MwenyeziMungu.Baada ya kitendo hicho,zimekuwepo kauli za utetezikwa baadhi ya watu kwambautoto ndio uliomsukumakijana Emannuel Josephat(14) kutenda uhalifu huo.Hata hivyo, wanaotoakauli hizi hatudhani kwambawatoto wao wa kikewangetokea kubakwa namtoto mwenye umri kamawa Josephati wangekuja nautetezi wa namna hii. Yaanikwamba mbakaji ni utotohivyo isieleweke vibayana huruma ichukue nafasizaidi.Swali la kujiuliza, mkosajini mtoto kwa kiwango ganikiasi kwamba ameshindwakutambua kwamba kitendoanachokifanya ni kichafu. Je,kwa utoto huo huo, anawezakukojolea Biblia yake?Yupo msanii anayeitwaElizabeth Michael (Lulu)ambaye yupo rumande hivisasa akikabiliwa na kesi yakumuua msanii mwenzakeSteven Kanumba.Pamoja na kuwepo hoja zautoto dhidi ya mtuhumiwa,
Si lazima kutukana Waislamukuzuiya Wakristo kuasi Kanisa
 bado sheria inachukuamkondo wake ili haki iwezekupatikana.Umri wa Lulu ambao badouna utata (miaka 17 au 18) naumri wa kijana aliyekojoleaQur,an (miaka 14) unawezakuwa katika kiwangocha kuitwa watoto, lakinisi watoto wa kushindwakutambua zuri na baya.Kwamba miaka 14 aliyonayo Emannuel Josephat,haiwezi kuhalalisha uhalifuwake wa makusudi dhidiya imani ya watu wengine,halafu itarajiwe kwamba umriwake mdogo unaweza kuwakinga ya kushughulikiwa aukupuuza kile alichokifanya.Kutokana na mazingiraya tukio lenyewe,Inaonekana wazi kwambachuki iliyokithiri dhidi yaUislamu na Waislamu,ndio iliyomsukuma kijanaJosephat kukojolea Qur’an.Hakununua wala kuokotakitabu hicho Qur’an, balialichukua msahafu kwamwenzie na kukikojoleahuku mwenye kitabuakishuhudia. Kwambaalikusudia kuonyesha chukialiyo nayo dhidi ya walewote wanaoamini katikakitabu hicho.Kabla ya kufanya tukiohilo, Josephat alisema kuwanyumbani kwao wanakijuakitabu cha Qur’an kuwa nikitabu cha shetani na kwambaWaislamu wanafuga majinina Qur an yao ni kitabu chamapepo.Hata hivyo, tunaaminikabisa kwamba kauli zakijana huyo hazikuja tu kwa bahati mbaya. Bali dhana hizini matokeo ya mafundisho yamiaka mingi yanayotolewaMakanisani na Mapadrina Maaskofu kwa wauminiwao.Pamoja na kuwa nimafundisho ya uongo na yakujenga mioyo ya chuki kwawaumini, lakini wenyewewanaona kuwa ndio njiasahihi ya kulinda imani zawaumini wao wasivutwekuingia katika Uislamu.Wakristo wengiwamepandikizwa dhanahii na viongozi wao tanguSunday Schools hadi kuhitimukipaimara. AliyofanyaJosephat ni matokeo yamafundisho hayo.Kwa mkristo, Muislamuni mfuasi wa shetani, lichaya kwamba huko mitaaniwanapokutana na jamaa zaoWaislamu, wanamudu kufichahisia na kuonyesha sura zaupendo wa kinafiki.Haya ndio mazingirawanayoishi Watanzania waliowengi kiimani.Hivi sasa watuwamekamatwa kwa kilekinachoitwa kuharibiwa nakuibwa mali za makanisa hukoMbagala. Viongozi wa juu waserikali na vyombo vya dolatayari wameshatoa maagizokuhakikisha waliofanyauharibifu huo wanashikishwaadabu.Viongozi wa Waislamuwanakamatwa na kuswekwandani.Katika mchakato wa namnahii, tunaona kwamba kunaudhaifu mkubwa kwa serikalina vyombo vyake vya dolakatika kukabiliana na matatizoya kiimani kwa watu wakehususan shida inapokuwa yakidini au ya kisiasa.Badala ya serikali naviongozi wake kupambana nachanzo cha tatizo, wamekuwana desturi ya kuhangaikana matokeo ya tatizo. Huuumekuwa ugonjwa wa miakamingi hasa shida yenyeweinapowahusu Waislamu.Tunavyofahamu kila jambolina chanzo chake. Na dawasahihi ya kuondoa tatizo nikushughuhulikia chazo chatatizo ili kuweza kuliondoakabisa lisijitokeze tena.Kama ni kuondoa mti, basiung’olewe na mizizi yake,sio kukata matawi yake nakuuacha, utachipua.Sote tunafahamu kuwachanzo cha tatizo Mbagalakuwa ni kukojolewa Qur’ankwa makusudi. lakini tukiolinalozungumzwa sasa nikuharibiwa mali za makanisana kuchukua hatua zakuwadhibiti Waislamu naviongozi wao.Utadhani wanaotuhumiwakuharibu makanisa hayowalikurupuka tu kama wehuna kufanya uhalifu huo.Ipo haja sasa kwa serikalikutumia busara na uadilifukatika kutanzua mizozo yakiimani nchini badala yakutumia mazoea. Siku zote nivyema kikatizamwa chanzo.Ukiingizwa udini, dharau,kibri na kujipendekeza naushabiki katika kutatua shidahatarishi kama hizi za kiimani,ni sawa na kuuteketeza mtikwa kukata matawi yake tu.Viongozi wa dini nao wanadhima ya kufundisha wauminiwao elimu sahihi ya dinikwa mujibu wa maandikoya vitabu vyao vya kiimani, badala ya kutoa mafunzoya dini kwa dhana za chukiza kiimani, kwa kuaminikuwa ndio kumjengea imanimuumini na kumlinda asijeakaasi dini.Si lazima kumjaza chukiMkristo juu ya Uislamu iliapate kuwa Mkristo mzuri naadumu katika dini hiyo.
Inaendelea Uk. 4
 
3
AN-NUUR
Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012
Habari
Ipeni elimu nafasi ya kwanzaMaendeleo yatakuja -Sheikh
Na Bakari Mwakangwale
WAISLAMU kote nchiniwametakiwa kufanya juhudikatika kuuhisha Uislamukupitia elimu ili kujileteamaendeleo katika jamii yaokwa ujumla.
Akizungumza mwishoni mwa juma lililopita katika hafla fupi yakuwaaga wanafunzi waliohitimuelimu ya msingi katika shuleya Almustaqiim iliyopo Mtonikwa Aziz Ali Temeke Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mansour  Nassor alisema hakuna jambokubwa la kuwarithisha watotokama elimu.Akikariri Aya kutoka ndani yaQur’an tukufu pamoja na Hadithza Mtume Muhammad (saw),Sheikh Nassor, alisisitiza sualala elimu na kuongeza kuwa uborawake mbele ya Mwenyezi Munguumepewa nafasi ya kwanza kablaya ibada nyingine yoyote.Alisema, suala hilo lichaya kukokotezwa sana katikamafundisho ya Kiislamu, badokuna watu wachache wamekuwawakipuuza wakati ambapo nayoni faradhi kama alivyopatakusema kiongozi wa Ummahuu.“Mtume (s a w) amesema,kutafuta elimu ni lazima kwakila Muislamu mwanaume naMuislamu mwanamke, hivyohatuwezi kudai tutafanikiwakuipigania dini hii bila yakufanya hima kuwapelekawatoto wetu wapate mafunzoyatakayowawezesha kuyakabilivema mazingira yao ya dunianina akhera”. Alisema Sheikh Nassor.Kwa upande wake, meneja waShule hiyo ambaye pia ni Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya naTaasisi za Kiislamu TanzaniaSheikh Farid Saleh, aliwatakaWaislamu kutumia fursa zakuanzisha Shule za Kiislamukwani shule zilizopo kwa sasahazitoshi.“Nawaomba wazazi naWaislamu popote pale mlipo hapanchini kuhakikisha mnazitumiavema fursa mnazozipata kwakuanzisha Shule nyingi ili vijanawetu hawa wasipate kisingizio chauchache wa Shule”, alisema.Akaongeza kuwa, kwa sasaShule zilizopo ni chache sanaukilinganisha mahitaji halisi yaWaislamu pamoja na mwamkowao kwa kupeleka vijana waokwenye Shule zinazotoa elimu yamaadili na malezi ya Kiislamu.“Mathalan, hapa kwetuMustaqiim, tayari darasa lakwanza limeshajaa na tumeanzakusimamisha usajili wawanafunzi, sasa hali itakuwajeitakapofika mwezi Desemba?”alisema na kuhoji Shekh Farid.Pamoja na nasaha hizokiongozi huyo wa Baraza KuuWilayani humo aliwataka wazazikutoa ushirikiano na uongoziwa Shule ambao wanawapelekawatoto wao ili kuleta ufanisina kupata matarajio memayaliyokusudiwa.Aidha, Sheikh Farid,aliwanasihi Waislamu kuangaliaaina ya shule za Sekondariwanazowapeleka watoto waomara baada ya kuhitimu elimuya Msingi.Alisema, ni vyema wazazikuwaendeleza watoto wao katikashule za Kiislamu, kwa maelezokuwa ni kupoteza nguvu nakumtoa mtoto katika misingi yamaadili aliyoipata kwa muda wamiaka saba iliyotumika kuwaleavijana hao katika Shule zao ikiwaatapelekwa katika shule za hovyozisizo na maadili.
Mbagala sawa Mwembechai
SERIKALI ya Jamhuriya Muungano Tanzaniana Jeshi lake la Polisi,imetuhumiwa kusababishavurugu kubwa Mbagalawiki iliyopita iliyopelekeawatu kuumizwa na baadhiya Misikiti na Makanisakuharibiwa.
Katika tuhuma hizoimeelezwa kuwa Jeshi laPolisi Wilaya ya MbagalaKanda Maalum ya KipolisiMkoa wa Temeke, ndiyosababu ya kuzuka kwa vurugueneo la Mbagala Jijini Dar esSalaam, baada ya kushindwakumchukulia hatua za harakakijana aliyekojolea Qur’ an.Baadhi ya Waislamu waMbagala wamefikia hatua yakulituhumu Jeshi hilo, wakidaikuwa walishindwa kulipauzito tukio la kunajisiwaQur an, lililofanywa siku yaJumatano wiki iliyopita nakijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Emanuel Josephat(14).Shutuma hizo zimetolewana watu waliokuwawakishughulikia suala lakunajisiwa Qur’an ambapowamesema kuwa kilichotokeaMbagala ni sawa na yaleyaliyotokea Mwembechaiambapo Waislamu waliuwawawakati serikali ikitekelezashinikizo la Paroko wa KanisaKatoliki Mburahati.Wakifafanua walisemakuwa, wakati katika kadhiaya Mwembechai shutuma
Na Bakari Mwakangwale
za Paroko zilipokewa naserikali kwa uzito mkubwana kwamba zilitosha kuwa‘agizo’ kwa serikali kuingiakazini kuwashukia Waislamukwa hasira kinyume chasheria na utawala bora, kwaMbagala Polisi walipuuzamalalamiko ya Waislamu nakwamba kulikuwa na kiladalili kwamba wanatakakulizima kinyemelea suala lakunajisiwa Qur’an.“Waislamu hawakuchukuasheria mkononi, walifuatataratibu za nchi na za kisheriahadi kumfikisha mtuhumiwa polisi, lakini polisi hawakulipauzito hali iliyowafanyaWaislamu kwenda kituonikutaka maelezo.” Anasemamkazi mmoja wa Mbagala.Akiongea na mwandishimkazi huyo anasema kuwakama Polisi wangekuwamakini, wakalipokea jambohilo kwa uzito wake, haliisingefikia hapo, lakini waoutadhani waliona hakunakilichotokea au ilikuwa kanakwamba waliona alichofanyayule kijana ni sawa au kamasio sawa basi, ama ni kwarushwa au vipi ikawa wanatakakumhami yule kijana, hilo ndiolililozua vurugu. Wameumizawatu, wameharibu Misikiti,wamesababisha vuruguzilizopelekea kushambuliwamakanisa kutokana nautendaji wao usio wa haki,wanaonekana kupendeleaWakristo na kudharauWaislamu.” Alisema mamammoja, mkazi wa Chamaziambaye hata hivyo hakutaka jina lake kutajwa gazetini.“Inaonekana saikolojiailiyojengwa kwa Polisi wetuni kuwa Mkristo katika nchihii haguswi inapotokea kuwamlalamikaji ni Muislamu,ila kwa Mkristo ni kinyumechake, akilalamika Mkristo,Polisi na serikali kwaujumla hawasubiri walakushughulika kutafuta ukweli,watawavurumisha Waislamukama wahalifu na majambaziyaliyokwisha kuhukumiwa,hili ndio lililoleta maafaMwembechai, ndio piailiyosababisha kuuliwaWaislamu Pemba Januari2001 na ndio lililoleta vuruguMbagala.” Aliongeza mamahuyo mtu mzima.Akifafanua zaidi akasemakuwa hata kauli za viongoziwa serikali akiwemoMheshimiwa Rais JakayaMrisho Khalfan Kikwete,zinaonyesha mwelekeo huohuo.Hakuna aliyeguswa nakitendo cha kunajisiwa Qur’anwala Misikiti iliyoharibiwakwa mabomu ya Polisi. Kilammoja alikimbilia kujisajilikuwa ni mtetezi wa Makanisa,Ukristo na Wakristo.“Kwa kweli kitendo chaRais Kikwete kutokuonyeshakabisa kuguswa na kitendocha Polisi kupiga mabomumisikiti, inaonyesha Wakristohawakukosea kuwa yeye nichaguo la ‘Mungu wao waUtatu’ na sasa wanafaidimatunda; ila jambo moja tulinawapa faraja Waislamukuwa hata washirikina waKiquraishi walitumia dolakumpiga vita Mtume (s.a.w),lakini hatimaye Makkahilikombolewa Abu Sufyaniakasalimu amri.”Alisema mama huyo nakuongeza kuwa hata zilekauli zilizotolewa katikazile vurugu zilizohusishwana Uamsho, Zanzibar hivikaribuni, zinathibitisha hilohilo.Ila akasema kuwawanachotakiwa Waislamukufahamu ni kuwa kilazama watalazimika kujitoamuhanga kwa namna mojaau nyingine kuhami diniyao, Dini ya Haki ambayohivi sasa nguvu za ukafirina ushirikina dunia nzimakupitia zinazoitwa jumuiyaza kimataifa zimeunganakuupiga vita.Akawapa faraja akiwaambiaWaislamu, hasa ambao hivisasa wanashikiliwa na Polisiwakiwa na kesi ya kujibukuhusiana na vurugu zaMbagala, akiwataka warejeeaya ya Qur’an inayosemakuwa makafiri watakusanya pesa, nguvu za kiuchumina maguvu yao ya kijeshina kidola kuwapiga vitaWaislamu, lakini nguvu na pesa zao zitapotea bure kwasababu hawataweza kuzima Nuru ya Uislamu huku katikavita yao hiyo wakiwarahisishiaWaislamu njia ya kupata Radhiza Mola wao.“Mazoea ya Jeshi laPolisi nchini kutokuchukuahatua inapotokea Waislamu
Inaendelea Uk. 6
 KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kushoto)akionyesha bomu waliolikuta ndani ya Msikiti katika vurugu zilizotokea Mbagala Ijumaa iliyopita.

Activity (18)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 hundred reads
1 thousand reads
Ayouun Nadhra liked this
Amran Nassor liked this

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->