Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword
Like this
5Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1040

ANNUUR 1040

Ratings: (0)|Views: 210|Likes:
Published by Hassan Mussa Khamis

More info:

Published by: Hassan Mussa Khamis on Oct 23, 2012
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

12/04/2012

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1040 DHUL-HIJJA 1433, JUMANNE OKTOBA 23 - 25, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Kariakoo mnatuma JWTZMalawi mtapeleka nini?
Waziri wetu Nchimbi chutama, usitambeMsilitumbukize Jeshi letu kwenye ‘aibu’ hiiYote haya mnafanya kwa masilahi ya nani?
Hofu ya maandamano ya Waislamu Dar:
 DKT. Emmanuel Nchimbi 
‘Simba’ Farid Ahmed
FFU walivyozidiwa
hadi kuitwa JWTZ
Polisi wasema hakutekwa, alijitekaMwenyewe asema ameongeza ujasiri Asisitiza, ni kufa au Jamhuri ya Zanzibar 
Mwingine akojolea
Qur’an Ukonga Dar
Uk. 10
 MMOJA wa raia akiwa chini ya ulinzi wa Askari katika mitaa ya Kariakoo, pia alikamatwa akiwa katika shughuli zake nakujumuishwa katika kadhia ya kamatakamata ya FFU, JWT na Mgambo Ijumaa wiki liyopita. MALORI ya JWTZ yakiwa yamewabeba Askari wa jeshi hilo kuingizwa mitaani katikakamatakamata ya raia Kariakoo, jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita.
Ni kijana mwenye miaka 20 Atoweka hajulikani alipo
 
2
 
DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25,
2012
AN-NUUR
 
TAHARIRI/HABARI
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM.
www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro,D'Salaam
MAONI YETU
Njama za kuilipua Zanzibar zakwama
Hadi sasa kinachoonekanakama njama za kuilipuaZanzibar, isikalike nakuirejesha kwenye siasa zachuki, fitna, farka na uhasama,zimefeli.
Hata hivyo, hali hiyoinaonekana kuwakasirisha baadhiya watu ambao hawakusitakujitokeza hadharani kushutumuserikali na Jeshi la Polisi kwambakwa waonavo wao, halijachukuahatua za kutosha.Pengine kilichokuwakikitarajiwa ni kuwa baada ya‘kutekwa’ Sheikh Farid, liibukezogo kubwa Polisi wapige watu‘Kijanjaweed’ na hata kuuwa haliitakayozidi kukasirisha wananchina kufanya nchi isikalike.Likitokea hilo, iwe sababukwanza ya kuvunja Serikali yaUmoja wa Kitaifa na Maridhianona kisha kuwaandama baadhiya watu pamoja na taasisi zaKiislamu.Hata hivyo, Nusra ya Allahilikuwa juu ya watu wa Zanzibar ambapo, wananchi walikuwawatulivu ukiacha zogo lililokuwalikifanywa na vijana wasiojalichochote ambao inadaiwakuwa ni wale Janjaweed ambao baada ya kuifanyia kazi CCMkatika chaguzi zilizopita,wametelekezwa.Kwa upande mwingine, Jeshila Polisi lilionekana kufanyakazi yake vizuri ambapowaliwaandama tu wale waliokuwawakileta ghasia mitaani na kwanguvu iliyokuwa ikilingana nahali halisi.Hata hivyo, hali hiyo ambayokwa hakika imekuwa ni nusrakwa nchi, inaonekana kuwahaikuwa matarajio ya baadhi yawatu ambao sasa wanailaumuserikali na hata kufikia hatua yakutoa kauli kwamba serikali yaUmoja wa Kitaifa na Maridhianoivunjikilie kwa mbali.Katika kudhihirisha kuwakuna watu wanatokota kwa hasirakuona Zanzibar ikiwa katikahali hii ya amani na utulivu,wamekuwa wakisambaza fitnakupitia vipeperushi wakidaikuwa wanaochochea fujo hadikuuwawa Polisi (FFU) kuleBububu, ni CUF. Na kwa sababu hiyo wanatakaCUF watolewe serikaliniwakisema “sisi CCM basi tenaUmoja na CUF.”“CCM kosa letu kuwatiambwa msikitini, sasa tunasemakuwa basi tena litakalo kuwana liwe. Kwa sisi CCM basi tena umoja na CUF.”Kinasema kipeperushi kimojakinachodaiwa kusambazwa na
Na Mwandishi Wetu
CCM wahafidhina.Hata hivyo, wahafidhina haohuku wakidai kuwa CUF ndiowanaochafua hali ya amani,wao wamejifanya kuwa ndiowapenda amani na watetezi waamani hiyo.Wanasema katika kipeperushihicho: “Nyie CUF/Muamsho,Abubakar Khamis Bakari, Mussa Njino na Azizi mushazoea fujona sisi CCM sera yetu amani,sasa mujiuzulu…tumechoka nanyinyi juu ya mauwaji ya askariwetu.”Kipeperushi kikamalizia kwakusema, “ondokeniii murudikwenuuuuu”, bila kufafanuawaende wapi (Pemba?).Maoni ya wengi na hata kauliza vijana katika vijiwe na maskaniza CCM ambazo mwandishiamebahatika kupita na kusikilizakauli za vijana hao ni kuwa,waliokuwa wakifanya zogo ikiwani pamoja na kuvamia maduka yaulevi na kupora masanduku ya pombe ni vijana wa Janjaweedambao wametelekezwa baada yakutiwa ununda.Vijana hao walipewamafunzo ya kijeshi, wakatiwaukatili wakawa wanapiga watumikwaju na hata kuuwa bilakuona vibaya wala hofu na bilakuchukuliwa hatua, (ufupi wamaneno waliondolewa hofu naubinadamu) wakati wa chaguzizilizopita.Baada ya kutiwa ukatilihuo na baada ya kuwaingizaCCM madarakani, wenyewewanadaiwa kusema kuwahawakupewa yale waliyoahidiwa,wametelekezwa.Inadaiwa kuwa japo ni kwelikwamba kuna vijana wengiwaliohusika katika vurugu, lakiniinaaminika kuwa ‘Ubaya ubaya’hao waliotokana na Janjaweed,ndio walioonekana mitaani bila ya hofu ya FFU wakifanyauporaji na kupiga watu.Inadhaniwa kuwa waliohusikakumteka Sheikh Farid huendawalikuwa na lengo la kuchocheaghasia nchini.Kwamba wakitaraji kuwawafuasi wake wangelipuka katikanamna ambayo ingelazimishavyombo vya dola kuchukua hatuaambazo matokeo yake ni kuletaghasia zaidi.Hoja hiyo inakuja hasa baadaya Sheikh Farid mwenyewekueleza hali ilivyokuwa ambapoinaonyesha kuwa waliomtekawalikuwa wakimhoji maswali yakawaida ya kipolisi.“Kama aliyoeleza SheikhFarid ni kweli, kwa niniwahusika wasingemwita tu Polisiau wakamkamata ikajulikanakwamba yupo Polisi anahojiwa?Kwa nini wacheze ‘drama’ hiiwakati waliyomhoji angewezakuitwa Polisi na kuhojiwa?”Haya ndiyo maswaliyanayoulizwa na watu wakijengahoja kwamba hata kamawaliohusika ni vyombo vya dola,lakini inaonyesha kuwa kunawatu walio ndani ya vyombo vyadola ambao hawafurahii hali hiiya amani na utulivu iliyopo.Inaelezwa kuwa kama mipangokama hiyo ingefanikiwa au kamaitaendelezwa na kufanikiwa,huenda ikawarahisishia kazimabeberu kupitia AFRICOMyao ambao kila penye harufu yamafuta na gesi, hutaka kupadhibitikijeshi na kikachero. Na njia nyepesi kamawalivyokwishaingia Ugandawakidai kusaidia kumsakaKonny, ni kujenga mazingiraya kuonyesha kuwa nchi inakitisho cha magaidi, Al Qaidana Al Shabab, na kwa hiyo kwavile wao washajipa ukiranjawa kupambana na ugaididuniani, basi huingia na kukaa.Wakishaingia ndio wamekaa,huna ubavu wa kuwatoa tena. Ni kwa sababu hiyo, wanaokulanjama hizi wakiangalia masilahiyao binafsi katika siasa zaZanzibar, wanatakiwa kutizamana hatari wanayoikaribishaambayo itawadhuru wao navizazi vyao vijavyo.
Wakati huo huo,
imeelezwakuwa Spika wa Baraza laWawakilishi, Mheshimiwa Ameir Kificho anastahiki pongezi zadhati kwa uzalendo wa hali ya juu alioonyesha katika kuzimahoja za waliotaka kuleta hoja binafsi ambayo ilikuwa na lengola kusambaratisha serikali yaumoja wa kitaifa.Kwa nafasi yake ya Uspikana pengeine kwa busara za uzee,Spika Kificho ilikuwa kamaanawabembeleza wajumbe nakuwakumbusha wakumbukekiapo walichochukua chakuitumikia nchi na wananchi. Namna yake ilikuwakama anawaambia kuwa waowangetakiwa kuwa watu wamwisho kuwasaliti wananchina nchi, na sio wao kuwa wamwanzo kuja na agenda zakuisambaratisha Zanzibar.Kwa upande mwingine, kwamuda wote ambao Sheikh Faridalikuwa haonekani, Masheikhwa Jumuiya ya Maimamu nawale wa Uamsho wamekuwawakifanya kazi kubwa yakuwatuliza wananchi na wakatihuo huo wakifanya vikao vya pamoja na Polisi kushauriana juuya hali ilivyo.
Inaendelea Uk. 5
USIKU wa Alhamisikuamkia Ijumaa SheikhMohammed Issa aliongeakupitia Redio Imaniakiwatuliza na kuwatakawatulie wakati viongoziwao wakishughulikiamadai yao.
Kwa waliomsikiaSheikh MohammedIssa watakuambia kuwaaliongea kwa masikitikona uchungu mkubwa hukuakitoa machozi akionyesha jinsi dhulma ilivyozidi kwaWaislamu.Alisema, inasikitishakuwa madai ya Waislamuyanapuuzwa yakiwepolile la kulalamikia dhulmainayofanywa na Barazala Mitihani Tanzania nasasa kibao kinageuzwakinachoonekana nakupigiwa zumari ni madaiya kuchomwa makanisa.Viongozi wa Waislamuwanakamatwa ili kuzimaagenda kama hiyo.Madai hayo ndiyo piayaliyotolewa na Waislamuwaliobahatika kufika katikalango la Ikulu ambapowalinukuliwa wakisemakuwa dhulma imezidi.Mtu mmoja katika walewaliofika lango la Ikulumuda mfupi kabla ya RaisKikwete kuwasili akitokeasafari alinukuliwa “live”na kamera za televisheniakisema kuwa dhulma kwaWaislamu imezidi nchini nakwamba yeye atasema kwelihata kama askari waliokuwawamemkamata watampigaau kumuuwa.Alisema, Qur’animenajisiwa lakini hilohalionekani likizungumzwa.Kinachosemwa sasa nikuharibiwa makanisa.Pamoja na nasahaalizotoa Sheikh MohammedIssa na Masheikh wengine,inawezekana kuwa kuna baadhi ya Waislamuwaliokuwa wamepaniakwamba lazima wafikeIkulu kufikisha kilio chao.Hoja yetu hapa, sio
Propaganda hazitasaidiakudumisha amani nchini
Agenda ni NECTA, MoU, OIC, Dhulma
kwamba azma ya Waislamuhao ilikuwa sahihi au la.Lakini hoja kwetu ni jinsi vyombo vya dolavilivyoshughulikia jambohilo.Kilichotokea ni kuwa badala ya vyombo vya dolakuzuiya watu wasifike Ikulu,walichofanya ni kusababishavurugu mitaani na kuletakizingizio cha kuwapakaziawatu makosa wasiyo kuwanayo.Waziri Nchimbi anasemakuwa kuna watu wanatakakuchafua amani ya nchi naanaleta hoja kuwa huendawanatumiwa na watu wanje.Mheshimiwa Nchimbi,labda tuulize, hivi nimpaka Waislamu wanchi hii watumiwe aukuchochewa na ‘watu wanje’ ndio waone dhulmainayofanywa na NECTAwanayoilalamikia? Inahitajimataifa ya nje kuona kuwatoka NECTA imeundwaimekuwa kama parokiaau kigango cha kanisa?Lile suala linalolalamikiwakwamba utunuku wamadaraja umekuwa siri nawenye walakini mkubwaikituhumiwa kuwa nikichochoro cha kufichauovu wa shule zinazotakiwakutesa kila mwaka ilizisije kuteseka, inahitajikuchochewa na Al Qaidahau Al Shabab, kuliona?Hivi inahitaji mataifaya nje kuwaonyeshaWaislamu wa Tanzaniakuwa serikali inaitumiaBakwata kuhujumu haki zaWaislamu? Hata hili la juzila Mufti Shaaban kuuwahoja ya Mahkama ya Kadhi,hawalioni? Nimegusia suala la NECTA na Bakwata kwasababu ndiyo masualamawili ambayo SheikhPonda pamoja na viongoziwengine wa Jumuiyana Taasisi za Kiislamuwalikuwa wakiyazungumziahivi karibuni.Ukiacha lile la kutakakuchochea uhasama bainaya Waislamu na Wakristo,kingine kinachoonekanakatika hatua hizizinazochukuliwa na vyombovya dola dhidi ya Waislamuni kama namna iliyobuniwaya kuzima hoja na agendaza Waislamu. Maanaukishafanikiwa kuwakamataviongozi wa Waislamu auukawapaka matope Waislamukuwa ni “Boko Haram”,hapana shaka itakuwa ninjia ya uhakika ya kuzimamadai ya Waislamu dhidiya NECTA, suala la MoU,Mahakama ya Kadhi, OIC namengine mengi.Tunachosema ni kuwaWaislamu wana madai yamsingi dhidi ya NECTA nadhidi ya serikali. Hakunanamna ya kuzima madai hayaila kuyashughulikia.Ila kama tunadhani kuwa propaganda za kuleta ugorowa Boko Haram na Botiza kukodi kuleta Uamshokuchoma makanisa Dar esSalaam zitasaidia kuzima hojaza Waisalmu na wakati huo huokudumisha amani; kwa hakikatutakuwa tunajidanganya.
 
3
DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25,
2012
AN-NUUR
 
HABARI
‘Simba’ Farid Ahmed
“MIMI msimamo wangu katikasuala la kuitetea Zanzibar upopale pale hadi Jamhuri yaWatu wa Zanzibar isimame.”
Hiyo ni kauli ya SheikhFarid Ahmed Hadi mara baadaya kuachiwa na watu aliodaiwalimteka na kumzuiya kwasiku nne.Sheikh Farid alionekanaIjumaa Usiku baada ya kupoteakwa siku nne katika visiwa vyaZanzibar huku akionekana akiwana afya njema pamoja na furaha baada ya kuonana na familiayake iliyopo Mbuyuni Mkoa waMjini Magharibi.Hata hivyo, Jeshi la Polisilimesema kuwa Sheikh Faridhakutekwa ila kinachoonekana ninjama za kujiteka mwenyewe.Kamishna wa Polisi Zanzibar,Mussa Ali Mussa amesema kuwasi kweli kwamba Sheikh Faridalitekwa bali kinachoonekana nikujiteka mwenyewe. Na kwa sababu hali hiyoya kujiteka imeleta vuruguzilizosababisha uvunjifu waamani, mali kuharibiwa na hatakuuliwa mtu, Polisi walikuwawamemshikilia Sheikh Farid pamoja na viongozi wenginewa Uamsho na walifikishwamahakamani jana na kusomewashitaka la uchochezi wanalodaiwakulifanya mwezi Agosti.Akifafanua juu ya kilealichokiita kujiteka Farid,Kamanda Mussa amesemakuwa kwa mujibu wa taarifazilizotolewa na dereva wakealiyempakia na kumwacha hukoMazizini, alimwambia aendezake wakati yeye (Sheikh Farid)akizungumza na watu waliokuwakatika gari aina ya NOAH.“Hivi tujiulize, mtu watuhuwajui unazungumza nao katika Noah kwa simu na kumwambiadereva wako aende zake, huko sikutekwa labda kujiteka. AlisemaKamishna Mussa.Hata hivyo, wakati Kamishnawa Polisi akisema hayo, SheikhFarid ameelezea alivyokamatwaambapo alisema kuwa hakutekwa bali alichukuliwa na jeshi la polisi na vikosi vya usalamawakitaka kumhoji kuhusiana naharakati zake za kuitetea Zanzibar ndani ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.“Kwa kweli inazungumzwaneno kutoweka, lakini mimisikutekwa, bali nilichukuliwana watu ambao ni polisi nawakaniingiza katika gari nakunipeleka sehemu moja ambayomimi nilikuwa siijui wakanifungakitambaa machoni na kunipelekasehemu nisiyoifahamu nakuniingiza katika nyumba mojanikiwa na kitambaa cheusiusoni”, alisema.Sheikh Farid alipatikanamajira ya saa 2:15 usiku baadaya umeme kukatika ambapokwa mujibu wa maelezo yakeanasema alishushwa ndani ya garikama mzigo kwa kusukumwasehemu ile ile ambayo awalialichukuliwa na ametambua hilo baada ya kuona ameshushwakatika msikiti ambao aliingiasiku ya kwanza alipochukuliwa.“Nilifungwa kitambaacheusi na tokea nimefungwa
Na Alghaythiyah,Zanzibar.
sikufunguliwa mpaka leo(Ijumaa) walipokuja kunitupasehemu ile ile walionichukuandio wakanifungua, na mimimwenyewe sikuwa nimewezakukifungua kwa muda wotehuo kutokana na jinsiwalivyokifunga”. Alieleza.Akizungumzia hali aliyoikutahuko ndani ya nyumba alipokuwaameingizwa, Sheikh Ahmedalisema kwa kuwa alikuwaamefungwa uso hakuwezakutembea sehemu yoyote ndaniya nyumba.Aidha alisema, hakuwahi kulakwa siku zote hizo ila kunywamaji tu aliyokuwa akinywaakienda msalani kujisaidia.“Sijala kitu chochote kwasababu hiyo nyumba haikaliwina mtu, lakini hata kamaningeletewa chakula nisingekulakwa sababu siwezi kuwaaminikula chakula chao kwa hivyonilichokuwa nafanya nikendachooni kujisaidia ndio nakunywamaji ya mferejini kwa wingi sanana Alhamdulillah (NashukuruMungu) amenisaidia”, aliongezaSheikh huyo ambaye alikuwaamezongwa na umati mkubwawa watu nyumbani kwake.Umati huo ulikusanyikanyumbani kwake kuanzia saa 3usiku mara baada ya kusambaahabari kwamba kapatikana nawengine kukesha hapo.Ilikuwa takbiira, adhkar nakasda kuonyesha furaha yawaumini hao wa dini ya Kiislamukwa kiongozi wao.Katika maelezo yake SheikhFarid amesema kuwa kwa mudawote aliokuwa akishikiliwahakuwahi kupigwa hata maramoja wala hajadhuriwa kwa haliyoyote zaidi ya kutiwa khofuwakati akifanyiwa mahojianona baadhi ya wakati alikuwaakihojiwa kwa hasira na ukali iliatoe maelezo yote.Alisema kuwa walichokuwawakitaka kujua ni kuhusianana harakati zake na masualamengi yalikuwa yakimlengayeye binafsi, uhusiano wakena Rais wa Zanzibar Dk AliMohammed Shein na uhusinowake na Makamo wa Kwanzawa Rais wa Zanzibar MaalimSeif Sharif Hamad pamoja nasafari zake za kwenda na kurudinchini Oman.“Walitaka kujua kila kituchangu na kwa kweli walikuwawanataka kujua kila kitu nailikuwa ni vitisho na baadhi yawakati walikuwa wakipiga risasimiguuni ili watimize lengo laowanalolitaka”, alisema Kiongozihuyo.Alipoulizwa juu ya watuwaliokuwa wakimhoji alisemakuwa walikuwa wakitofautinakwa kuwa kila mmoja alikuwaakitumia namna yake ya kuhojiambapo wengine wakitumiaukali na wengine wakihoji kwautaratibu na upole.Akielezea mazingira yanyumba hiyo aliyowekwa alisemani khofu ilikuwa imetanda, lakinialiweza kuvumilia katika kipindichote hicho kwa kuwa hakuwaakiona kitu chochote kwa kuwaalikuwa amefunikwa uso wote.Akitoa wito wake kwaumma aliwataka watulie nawasifanye fujo huku ombi lakekwa viongozi wa serikali likiwakuwataka kutenda uadilifu nawawe wanatekeleza kauli zaokivitendo na sio kusema bilaya kutenda haki kwani amanihaiwezi kudumishwa iwapo watuwanayimwa haki.“Naomba watu watuliewasifanye fujo na wasifanyevurugu za aina yoyote, hizi niawamu za kudai haki lakiniwawe na subra kwani hii ni nchiyetu na tunaipenda na tutaiteteakwa nguvu zote na wito wangukwa viongozi wa serikali wawewaadilifu na watende haki kwasababu hii ni nchi yetu na hizini awamu za mabadiliko naasiyetaka mabadiliko, basi wakatiutambadilisha akitaka asiteke”,alisema.Sheikh Farid alisemalicha ya vitendo vyote hivyoalivyofanyiwa, hatarejea nyumakamwe na ataitetea Zanzibar hadi pumzi yake ya mwisho kwanianachokifanya yeye na wenzake nikitendo kinachokubalika kisheriana hakuna wa kuwazuwia.“Tutaitetea nchi yetu yaZanzibar hadi tone la mwisho(la damu) kwa sababutunachokifanya hatujavunjasheria wala hatujenda kinyumena sheria za nchi kwa hivyotutaitetea Zanzibar mpaka iwe nadola kamili na mamlaka kamilihaiulizwi na mtu na irudi katikahadhi yake kama ilivyokuwamwaka 1963.” Alisema SheikhFarid.Akitoa maelezo yakukamatwa kwake alisemakwamba awali alipigiwa simuna mtu aliyejitambulisha kuwa nimwanafunzi wake wa Madrassaya Mahdi Mahfoudh kwambaanataka kuonana naye nakumtaka waonane katika eneo laMbweni karibu na duka ambapombele yake kuna msikiti mdogousiosaliwa na watu wengi.“Mimi napigiwa simu nawatu mbali mbali kwa hivyonilipopokea simu kuwamwanafunzi wangu wa MahdiMahfodh sasa wakati huo natokanyumbani nilikuwa nahitajiumeme kwa hivyo mimi nilipofika pale nikamwambia yule kijanawangu kwamba nataka kununuaumeme na nikamwambia kijananenda kanunue umeme na miminaingia humu msalani kujisaidiasasa yule kijana akaondokakwenda kununua umeme, kilekitendo cha yule kijana kuondokatu na mie ndio nimetoka chooninaona gari ndio hiyo imekujaimepaki na kuna mtu mmojaakashuka akaniita Maalim naakajitambulisha pale kwambamimi ni askari wa usalama nanaomba uingia humu ndani yagari tunataka kukuhoji na ndipowakati huo huo watu wenginewawili wakashuka ndani ya gariwakiwa wamejifunika nyusozao vitambaa vyeusi isipokuwamacho wakiwa na mashinigani(bunduki) ...sasa mimi sikutakatena nikimbie au vipi kwa sababuningekataa pengine ingekuwa nikhatari zaidi sikuwa na sababuya kukataa nikaingia ndani yagari na nilipoingia tu nikafungwakitambaa gari ikaondoka”.Alisimulia mkasa huo SheikhAhmed.Alisema baada ya kuingiandani ya gari gari hiyo haikurudinyuma ilionekana inakwenda njiaya Uwanja wa Ndege kwa kuwailikuwa imeelekeza huko na kishakupita ‘round about’ kama marasita inazunguka tu hapo roundabout, ili kumpotezea lengoasifahamu wapi anapelekwana kuanzia hapo hakuwezakujua wapi anapelekwa hadihapo alipofika katika nyumbana kuwekwa huko kwa mudawote akiwa amefunikwa usowake na hajafunguliwa hatamara moja zaidi ya siku ambayoamerudishwa sehemu ile ile nakutupwa kwa kusukumwa tundani ya gari.Muda mfupi baada ya taarifahizo kuenea kwamba SheikhFarid ameonekana, watu mbalimbali walikuwa wakitumianaujumbe kwa njia ya simu nafacebook wakiulizia alipo iliwamuone kwa macho yao.Sheikh Farid Ahmed alipotokahapo alipotupwa, alikwendamoja kwa moja hadi nyumbanikwa mama yake eneo la Malindiambapo alikutana na watu mbalimbali na kusalimiana nao nakisha kwenda nyumbani kwakeMbuyuni karibu na Msikiti waMabuyuni katika uwanja wampira wa Malindi.Muda mfupi waumini wadini ya Kiislamu walimiminikakwa wingi na kukaa nje ya getila nyumba ya Sheikh Farid hapoMbuyuni wakitaka kumuonakwani wengi wao walikuwahawaamini kama angeachiwaakiwa hai kutokana na taarifa zaawali zilizokuwa zikisambazwakwamba Sheikh huyo amefarikidunia kwa kupigwa sindano yasumu na wanajeshi.Waumini wa kike nawakiume, wakubwa na watotokwa wingi walikusanyikahuku wakisikika wakimsifuna kumshukuru Mwenye enziMungu kwa kumrejesha kiongoziwao salama wakipiga Takrbir ...yaani Mwenyeenzi MunguMkubwa na kisha kuimba wimbowa kumpongeza na kusemaSimba …...ameachiwa ...Simbaameachiwa...Simba ameachiwaambapo kulikuwa na dufuzikipigwa na wengine kuitikia.Wakati waumini hao wakiwanje ya geti na baadhi ya viongoziwa Jumuiya ya Uamsho naMihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki) wakiwa ndani, wauminihao walikuwa wakipiga malelelekila mara wakimuomba SheikhFarid atoke achungulie ili wawezekusalimiana nao ambapo baadhiya wakati walikuwa wakipenyana kuingia ndani kwa lengo lakutaka kukumbatiana naye nakupiga picha.Katika mitandao ya facebook watu wengi hasa vijana wameweka picha zao wakiwa wamepiga pamoja na Sheikh Farid hukuwengine wakibadilisha profilezao na kumuweka picha yakehuku wengine wakisema huyondio shujaa wanayemtaka kuwakiongozi wa nchi yao.Waumini walibakia hapo kwamuda na hata pale alipoambiwakwamba amechoka na hangewezakutoka nje, walisema shida yaowamuone japo achungulie nje.Kwa hiyo ikawa ni zoezila Sheikh Farid kuchunguliamara kwa mara kuwasalimiawaumini na kuwatolea mkonona kila baada ya muda alikuwaakisimama na kuchungulia hukuakishangiliwa.Ilipofika saa nane usikuwaumini walianza kuondokakidogo kidogo na kufanyamaandamano huku wakiimbawimbo wa Simba ametolewa nakuelekea katika barabara zote zaMjini huku wakipiga dufu.
 SHEIKH FAarid Hadd (wa tatu kushoto).

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->