Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
1Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
1st Tanzania Compliant

1st Tanzania Compliant

Ratings: (0)|Views: 16|Likes:
Published by Kevin Kallsen
This is the first complaint filed
This is the first complaint filed

More info:

Published by: Kevin Kallsen on Mar 07, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

12/09/2013

pdf

text

original

 
27/02/2013
Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Kanisa Anglikana TanzaniaMwenyekiti wa Nyumba ya Maaskofu,Mababa Askofu wote wa kanisa Anglikana Tanzania,Katibu Mkuu Kanisa Anglikana Tanzania,Wajumbe wote wa Sinodi Maalum ya Uchaguzi wa Askofu Mkuu wa Kanisa AnglikanaTanzania, Bwana Yesu Kristo asifiwe,
YAH: RUFAA KUHUSIANA NA KUKIUKWA KWA MAKUSUDI TARATIBUZA UCHAGUZI WA ASKOFU MKUU WA KANISA ANGLIKANA TANZANIAULIOFANYIKA KATIKA KANISA KUU LA ROHO MTAKATIFU – DODOMA,ALHAMISI TAREHE 21 FEBRUARI, 2013.
 Sisi ambao ni wajumbe halali wa Sinodi ya Uchaguzi wa Askofu Mkuu wa Kanisa AnglikanaTanzania, tunaotoka katika Madayosisi tofauti lakini tunaounganishwa na tukio la makusudila uvunjwaji wa Katiba ya Kanisa Anglikana Tanzania pamoja na ukiukwaji wa taratibu zauchaguzi uliofanywa na Profesa Palamagamba Kabudi na Rev Dr. Dickson Chilongani ambayeni Katibu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania. Yafuatayo ni maelezo yetu.
Wajibu na kazi za Msajili
Wajibu na kazi za msajili vimeelezwa vizuri katika
kanuni ya NNE (d) i, ii,iii,na iv
ya Katibaya Kanisa Anglikana Tanzania. Kwa mujibu wa Kanuni tajwa hapo juu, Msajili wa Kanisa ni:mshauri wa Askofu Mkuu katika mambo yote yanayohusu sheria; huhudhuria vikao vya Sinodiya Kanisa, Halmashauri ya kudumu na Nyumba ya Maaskofu (kama akihitajiwa); kwa niaba yaAskofu Mkuu, kutekeleza mambo ya
Kisheria
wakati wa kuamriwa Askofu au Askofu Mkuu, nawakati ambapo hati za kisheria zinahitajika na kuwa na madaraka mengine yoyote atakayopewana Katiba hii au Sinodi ya Kanisa.Tumependa kwamba turejee sehemu hiyo muhimu ya Katiba na hivi ndivyo tusemavyo; kwanzalinaweza kufanyika kosa la kutafsiri vibaya
kanuni ya TATU (a)
kwamba yeye (Msajili) nimjumbe halali wa Sinodi. Lakini, ujumbe wake ni kwa kazi maalum kama inavyotafsiriwa vizurina
Kanuni ya NNE (d)i-iv.
Yeye kwa maana hiyo sio mpiga kura katika Sinodi yoyote yaKanisa. Kitendo cha Profesa Kabudi kupiga kura kilikuwa ni makosa na hivyo kufanya uchaguzi
 
kuwa batili kwa sababu zifuatazo:
i)
Aliapa kwenye Sinodi maalum tunayoitaja, kuwa
shahidi
(Angalia kitabu chautaratibu wa uchaguzi wa Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, tarehe 21 Februari 2013, (uk.6) SEHEMU YA PILI. Kipengele na. 1 “Mwenyekiti awatakemashahidi wa uchaguzi, yaani Msajili wa Jimbo na Katibu Mkuu wa Jimbo (ambayeni Katibu wa Sinodi) watoe kiapo cha kutenda haki”
 
ii)
Tunasema kwamba Profesa na Katibu Mkuu waliapa kiapo cha kutenda haki nakusimamia zoezi zima, hawakuapa kiapo cha kupiga kura kuchagua Askofu Mkuukwa kuwa huo si wajibu, haki wala kazi yao kwa mujibu wa katiba na taratibu.Walioapa kupiga kura
(Tazama kitabu cha utaratibu wa uchaguzi wa Askofu Mkuu,Uk. 6, sehemu ya pili, kipengele namba 3)
ni Mababa Maaskofu wa KAT pamoja naWajumbe wa Sinodi Maalum ya Uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KAT toka katikaMadayosisi na waliapa kama ifuatavyo;MIMI .........................NIKIFAHAMU UMUHIMU WA DARAJA TAKATIFU LAASKOFU MKUU NA JINSI AMBAVYO SI HAKI ITOLEWE ISIVYOSTAHILI, NAAHIDI KWA DHATI KUWA SITASEMA WALA KUPIGA KURA KATIKAMKUTANO HUU KWA WOGA AU UPENDELEO, BALI KWA UAMINIFUWANGU WOTE, KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU, KWA FAIDA YAKANISA LAKE, NA MANUFAA YA WATU WAKE. EE MUNGU UNISAIDIESAHIHI ...........................................TAREHE .................................. Kipengele hicho kinaagiza wajumbe Sinodi kuapa mbele ya Msajili wa jimbo na hiyo ndiyokazi yake. Haiwezekani muapishaji, asahau ghafla na kujifanya kuwa Mjumbe wa kawaida nampiga kura, wakati hakula kiapo hicho.
Kwa Mheshimiwa wa viwango vya elimu
,
hususanProfesa
,
na mtu mwenye ufahamu mkubwa kama yeye, mtu anayetegemewa Kitaifa,na Mjumbe wa kamati muhimu sana ya kuandika Katiba ya nchi
, ni dhahiri kuwa lilelilikuwa kosa alilopanga kwa makusudi na alilifanya akiwa anajua. Profesa Kabudi alifanya kazizote zikiwemo zile ambazo kwa mujibu wa majukumu yake kikatiba hakupaswa kutia mkonowake hata kama moyoni alikuwa na chaguo lake. Profesa alisimamia, alipiga kura, alishirikikuhesabu kura, na akatangaza matokeo,tendo ambalo lilipaswa kufanywa na mwenyekiti.Tunachosema yeye sio mpiga kura! Hili lisichanganywe na mambo mengine. Hata wasajili waJimbo waliomtangulia hawakupiga kura katika chaguzi zo zote za Jimbo.
 Msajili wa Jimbo kukiuka kanuni ya KWANZA ya Kanisa Anglikana Tanzania (5) sehemuc,d,e na f.
 
Sehemu hiyo inatoa utaratibu wa namna ya upigaji kura, kwamba; kura zitapigwa kwa utaratibuwa kupunguza majina. Majina matatu tu yaliyopata kura nyingi katika kura ya awamu yakwanza yatachakuliwa na kupigiwa
kura ya
 
pili
, Jambo hilo halikufanyika, na jina la AskofuSadock Makaya aliyeshika nafasi ya tatu likatupiliwa mbali na kubakishwa majina mawili haliinayotufanya tusadiki kuwa kulikuwa na jina lengwa. Profesa Kabudi, ni mtu ambaye hatumtiliishaka katika uwezo na taaaluma yake na kwamba huyu ni mtu anayejua sana historia ya kanisana uendeshaji wake. Profesa anatufanya tuamini kuwa mambo hayo aliyatenda kwa
malengo
na
mipango maalum
na ya muda mrefu sana, tena akifahamu fika kuwa anaivunja kwa makusudiya wazi kabisa Katiba ya KAT, na kuwapotosha kwa kudhamiria wajumbe wa Sinodi maalum yaUchaguzi akidhani na kujiamini kuwa hatuoni, au hakuna hata wenye uwezo wa kuona madhambi hayo.
Kuingizwa kwa wajumbe wasiostahili kupiga kura.Kanuni ya tatu
ya Katiba ya Kanisa Anglikana Tanzania inawataja wajumbe wa Sinodi, nammoja kati ya wajumbe hao ni
Mama Mkuu wa CMM
. Mama Mkuu wa CMM ni
Sr. Gloria
 
CMM
wala sio Sr. Helena CMM aliyekuja kupiga kura na kuhesabia kura. Kuruhusiwa kupigakura na kuhesabu kura kwa Sr. Helena CMM ni kinyume cha Katiba ya Jimbo, kwani yeyesi mjumbe wa sinodi ya Uchaguzi. Katibu wa Kanisa Anglikana Tanzania pamoja na ProfesaKabudi wanalijua hilo, na kwa makusudi walilibariki jambo hilo. Sisi tunasema kwamba, kurana
uwepo wake
Sr. Helena CMM sio halali kwani yeye sio mjumbe halali wa Sinodi ya Jimbo,kwa namna yoyote ile hakupaswa kuhesabu kura katika uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KAT.Hata katika lile zoezi la kuhakiki wapiga kura kuna jina la mjumbe mmoja toka Dayosisi yaRuaha lililoingizwa palepale kwa madai kwamba lilikosewa kitu ambacho siyo sahihi. Baruaya mwaliko wa kuhudhuria Sinodi Maalum ya Uchaguzi wa Askofu Mkuu iliyoandikwana ‘Msajili’ wa Jimbo tarehe 21/11/2012 inayowaalika Wajumbe wa Sinodi ya uchaguzi waAskofu Mkuu ilisisitiza, twanukuu,
“tafadhali njoo na barua hii na igongwe muhuri waDayosisi na iwe na sahihi ya Askofu wa Dayosisi. Itakusaidia kuandikishwa ili ushirkikupiga kura”
mwisho wa kunukuu. Msajili wa jimbo alishindwa kufuatilia kwa umakini zoezihilo la kuhakiki wapiga kura kama alivyosisitiza katika barua yake. Hakuna hata mjumbe mmojawa Sinodi ya Uchaguzi aliyehakikiwa kwa barua ile ya mwaliko toka kwa ‘Msajili’ wa jimbondiyo sababu yule
mjumbe toka Dayosisi ya Ruaha aliiingizwa palepale kinyemela
. Jambohilo linaleta mashaka makubwa sana, nasi twathubutu kusema Katibu wa Jimbo na ‘Msajili’ waKanisa hawakuwa makini katika swala hilo, wamelifanya wakiwa na mkakati maalum. Ofisi yaKatibu Mkuu iliwasiliana na Madayosisi na kupewa orodha ya majina ya wajumbe wa sinodiya uchaguzi, na Madayosisi yote yalituma majina yao. Swali ni hili, iweje siku ya mwishotena wakati wa kuhakiki wajumbe liingizwe jina la mjumbe huyo, ambaye hakuwepo kwenyeorodha ya Katibu Mkuu?

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->