Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword
Like this
9Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1061.

ANNUUR 1061.

Ratings: (0)|Views: 3,579 |Likes:
Published by MZALENDO.NET
ANNUUR 1061.
ANNUUR 1061.

More info:

Published by: MZALENDO.NET on Mar 09, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

07/20/2013

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1061
RABBIUL THAN
1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
www.annuurpapers.co.tz
Hakuna kitu kinachowaliza wenye akilizaidi kuliko wasiwasi wa kuokoka naMoto na kupata Pepo! Hijja peke yakendiyo inayoweza kumsafisha muislamuna madhambi yote, akarudi kama sikualiyozaliwa na mama yake, na akapataPepo katika muda wa siku tano. Hivyohakuna matumizi bora ya fedha kulikokwenda Hijja. Wewe ndugu yetuushakwenda mara ngapi?KaribuAhluSunna wal Jamaa. Gharama zote niDola 4,300 tu. Tafadhaliwasiliananasi ifuatavyo: Tanzania Bara:0717224437; 0777462022;Unguja:0777458075;Pemba: 0776357117.
4)KUPATA PEPO KWA SIKU TANO!
Watuhumiwa Kesi ya Sheikh Ponda‘wawakaanga’ Polisi mahakamani
Wadai walivamiwa msikitini wakiwa katika ibadaWaikana BAKWATA na kudai hawazijui kazi zakeWasema kiongozi wao ni Qur’an na Sunna za Mtume
KATIBU Mkuu wa Chamacha Wananchi,CUFMaalim Seif Sharif 
Maalim Seif awakumbushaZanzibar OIC
 Mwenyekiti wa Jumuiya wa Jumuiya ya Al-Yousuf Sheikh Al-Youseif (kushoto) akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani.
Na Mwandishi Maalum,Z’bar
Hamad, amesemaZanzibar imepoteza fursanyingi kwa kutokuwamwanachama wa Jumuiyaya Maendeleo ya KiislamuDuniani (OIC).
Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye ni Makamowa Kwanza wa Rais wa
Inaendelea Uk. 3
Ni usiku wa Itiqaf T.I.C Kichangani kesho
Waislamu kukutana kutawakal kwa Allah (s.w)Masheikh kujadili kulegalega mahusiano ya kidini
Ujio wa FBI: Ni Msiba
Sasa ndio giza limetanda kweliSio alipokufa Mwalimu Nyerere
 KIKOSI Maalum cha kutuliza ghasia (FFU) kikiwa katika eneo la Markaz Chang'ombe Jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2012.
 
2
 AN-NUUR
RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
Tahariri/Tangazo
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza kozi maalum yamaandalizi kwa wanaorudia kufanya mtihani wa Kidato cha IV, 2013.Programu hii itaanza tarehe
28/02/2013
hadi tarehe
28/08/2013
 Jumatatu hadi Jumamosi saa 2:00 kamili Asubuhi hadi saa 9:10 Alasir.
Masomo yatakayofundishwa ni:-
Elimu ya Dini ya Kiislamu, English Language. Lugha ya Kiarabu. BasicMathematics, History, Geography, Civics, Physics, Chemistry, Biology,Book Keeping, Commerce.Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni kwa Tshs
10,000/=
Mlete mwanao apate Elimu bora itakayomwezesha kujiungana Kidato cha Tano.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba:
 
0714 888557/0659 204013
Wabillah Tawfiiq
MKUU WA SHULE
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL
P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0712 974428 Fax: 2450822 D’ SalaamE-mail: ipcubungoislamic@gmail.com
Maandalizi kwa wanaorudiaKidato cha IV, 2013
Kiswahili
IMETOKA taarifa yaJeshi la Polisi kuwatayari maafandewetu wanashirikianana makachero waFBI kuwanasawatuhumiwa wamauaji ya PadreEvarist Mushi.Pengine swaliambalo Watanzaniawangependa kujuani hili. Katikaushirikianao huu,nani anamtumakazi mwenzake? Autuulize vingine, huu niushirikiano au askariwetu wanatumwakazi na wageni waoFBI?
Tunauliza hivi kwasababu tuliwaonawatu hawa alipokujaBill Clinton hapa.Hawakuwaaminikabisa wanausalamawetu kiasi chakumdhalilishaaliyekuwa Rais wetuBenjamin WilliamMkapa kwa kulinusishagari lake kwa mbwa.Au Tumesahau?Alipokuja ‘MzeeMzima’ George WBush wakaweka vijanawao mpaka kwenyedari ya Ikulu yetu! Hivisisi ndio tuliowaombawapande au walipandawenyewe bila hata yakungoja ruhusa yetu?Mtu anakuja nyumbanikwako halafuanakupekuwa mpakachumbani kwako.Je, hivi tuliridhiaudhalilishwaji ule? Je,hapa kuna kushirikiana
Ujio wa FBI: Ni Msiba
Sasa ndio giza limetanda kweliSio alipokufa Mwalimu Nyerere
au wao kufanyawatakavyo?Tusisahau kuwa hawandio wale waliosemakwa kujiamini na jeurikuwa Iraq kuna silahaza maangamizi. Lakini baada ya walilokusudiakufanikiwa kwa maanakuwa baada ya kuvamianchi ya watu na kuuwamamilioni ya watu nakufanya uharibifu naufusadi wa kutisha,wenyewe hao hao bilaya aibu wakasemakuwa waliongopa,Saddam hakuwa nasilaha za maangamizi.Kama alivyosemaRais wetu MheshimiwaJakaya Mrisho Kikwetena kama alivyosemaWaziri wa Mambo ya Ndani MheshimiwaEmmanuel Nchimbina pia baadhi yamakamanda wetu waPolisi, inavyoonekanatunawaamini sana‘washirika’ wetu hawa.Lakini swali ni je, kamawatatuambia Uamshowana kiwanda chasilaha za maangamizikama walivyodaikuwa zipo kule Iraqtutaamini maadhaliwamesema wao? Tunaubavu wa kupingawatakayosema kamatutakuwa na wasiwasikuwa wanaongopa ausio sahihi? Baraza laUsalama la Umoja waMataifa na Jumuiya yaKimataifa kwa ujumlailisema Iraq hakunasilaha za maangamizina ikapinga nchi hiyokuvamiwa, lakiniMarekani ikavamiaikafanya ufisadiiliokusudia kufanya.Je, na sisi tupo tayarikubeba gharama yamatokeo ya ukacherowao kama itakuja katikasura ileile ya madai yasilaha za maangamiziIraq?Akizungumza katikamahojiano maalumu na baadhi ya vyombo vyahabari wiki iliyopita,Kamishna wa PolisiZanzibar, Musa AliMusa alithibitishakwamba jeshi lakelimekuwa likishirikianana FBI katika upelelezihuo na kwamba idadiya waliokamatwaimeongezeka.“Ni kweli tumekuwatukishirikiana na FBIkatika upelelezi ilikuhakikisha kuwa,wahusika wa tukiola kuuawa kwa PadriMushi wanakamatwa.Hii itasaidiakupunguza vitendovinavyohusishwana matukio yakigaidi yakiwamomauaji,”alisemaKamishna Musa.Labda tuulize, ujuzigani na ufahamu gani wakuwajua Wazanzibari naWatanzania waliokujanao FBI kiasi chakuwezesha kufika tuwanakamatwa watu?Au wamekuja na orodhayao na polisi wetuwanafanya kutumwa“tukamatie yule na yulena yule?”Yamewahi kufanyikamauwaji mengi sananchini hapa, yakiwemoya Kamanda wa PolisiMwanza, lakini yoteyalichukuliwa kamamatukio ya kihalifuna vyombo vyetu vyausalama na sheriavikayashughulikia kwaumakini mkubwa. Kitugani kinawafanya polisiwetu wakimbilie kuletamsamiati wa ugaidikatika tukio hili? Je,huu ni wao wenyeweau wameletewa nawashirika wao FBI?Sisi tunadhani kuwakabla ya polisi wetukukimbilia kuwa naimani na ujuzi naufanyaji kazi wa FBI,wangefanya kwanzasemina nao wawaombewawafahamishe uzurina kwa kituo kilekizungumkuti cha“Anthrax Terror Attack”kimeishia wapi?Tunasemakizungumkuti kwasababu awali wataalamuhao tuliowaagizakutoka Washington nawenzao katika ukacheronchini mwao walisemakuwa kimeta kilekilitoka kwa Al Qaidawaliotumwa na SaddamHussein. Walimwenguwakaonyeshwa na bahasha zilizoandikwaAllahu Akbar ili kukaziakuwa waliohusika niWaislamu, Al Qaida.Hata hivyo baadaewakawa wanaparuranawenyewe kwa wenyewe baada ya taarifakuvuja kuwa kimetakile kilitokea katikamaabara zao wenyewe,tena za kijeshi.Katika kitisho kile chakimeta ilielezwa kuwawatu saba walikufa.Je, sisi tumejiandaakulipa gharama kiasigani (katika sura yakuuliwa au kuteswaWatanzania wasio nahatia) kama mambotutakayofanyiwa ni sawana haya ya “AnthraxTerror Attacks” na yaleya silaha za maangamiziIraq?Kwa hakika kwa mtuyeyote mwenye akiliyake timamu na hasaakiwa na japo chembeya uzalendo na mwenyekujali ubinadamu nautu wake, akitafakari juu ya ujio huu wa FBI,hatakosa kuona kuwatumefikwa na msiba.Kama tuliambiwakuwa giza limetandaalipokufa Mwalimu Nyerere, zile zilikuwanyimbo na ngonjera tuza kuomboleza msiba,sasa ndio giza limetandakweli.
 
3
 AN-NUUR
RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013
Habari
Watuhumiwa Kesi ya Sheikh Ponda ‘wawakaanga’ Polisi mahakamani
MASHAHIDI wa upandewa utetezi katika kesiinayomkabili Sheikh PondaIssa Ponda, wamedai askariPolisi waliwavamia nakuwapiga wakiwa katikaibada ya Itiqafu, ndaniya Msikiti wa MarkazChang’ombe, jijini Dar esSalaam, usiku wa Oktoba16, 2012.
Mashahidi hao ambao niwashtakiwa katika kesi hiyonamba 145/2012, walitoamadai hayo mbele ya HakimMkazi wa Mahakama yaKisutu, Bi. Victoria Nongwa,walipokuwa wakitoa ushahidiwao mahakamani hapoJumatano wiki hii, na kuelezakuwa wanakana mashtakayote yanayowakabili.Mbali na madai hayo,washtakiwa hao ambao kilammoja alipanda kizimbanikutoa utetezi wake, kwaujumla walilikana BAKWATA,wakidai wanaisikia tu lakinihawaitambui pamoja na MuftiSheikh Shaaban Simba.Wakiongozwa na Wakiliwao Bw. Juma Nassoro,mashahidi hao walisemakwamba walifika katika Msikitiwa Markaz Chang’ombe kwalengo la kufanya ibada yaItiqafu, yenye fadhila nyingimiongoni mwa ibada zaKiislamu.Walidai pamoja na kujiandaana ibada hiyo, hawakuwezakuitekeleza kwani ilipofikamajira ya saa tisa usiku,muda ambao ndio muafakakwa ibada hiyo, walisikiavishindo, geti kuvunjwa nakisha mlango na madirishaya Msikiti kuvunjwa na askarikuingia ndani na viatu vyao nakuanza kuwashambulia.Shahidi namba moja Bi.Kulthumu Mfaume, ambaye pia ni mshtakiwa namba mbili,akiwa kizimbani aliiambiaMahakama kuwa alisikia kunaibada ya Itiqafu katika ChuoCha Kiislamu Markazi, ndipoalipolazimika kwenda kwaajili ya Ibada hiyo.“Usiku tulishtuka baadaya kusikia geti likivunjwa namara mlango wa Msikiti naoulibamizwa na kuvunjika, kishaniliona askari wakiingia ndanina mabuti yao, walitupigasana na walikuwa wanaumetupu, kisha walituingizakatika magari yao” AlisemaBi. Kulthumu.Bi. Kulthumu alisema pamoja na kujitetea kwambawapo katika ibada ya Itiqafu nakuhoji kosa lao ni nini, alidaiaskari hao hawakuwaelewana walizidisha kipigo.Akijibu maswali ya Wakili
Na Bakari Mwakangwale
wa Serikali, Bw. TumainiKweka, kwamba alipatajetaarifa za ibada hiyo ya Itiqafu,Bi. Kulthumu alisema akiwanjiani alisikia wakitangazaMsikitini, na kwa kufahamuumuhimu wa ibada hiyoalilazimika kwenda.Alipoulizwa ni nanikiongozi wake, Bi. Kulthumualijibu hana kiongozi bali yeyehuongozwa na Qur’an naSunna za Mtume Muhammad(s .a .w).Kwa upande wake, shahidinamba mbili Bi. ZainabMohammed (50), ambayekatika kesi hiyo ni mstakiwanamba tatu, akitoa ushahidiwake alisema alikamatwa naaskari Polisi akiwa katika Ibadaya Itiqaf ndani ya Msikiti waChuo Cha Kiislamu MarkaziChang’ombe, na alipata kipigokutoka kwa askari hao.Kuhusu ni wapi alipatataarifa za ibada hiyo, alisemaalipata kupitia kwa muuminimwenzake, ambapo baadaya kufika hapo Markaz,hakufanya shughuli yoyotezaidi ya kufanya ibada ndaniya Msikiti huo.Alipoulizwa ni nani mmilikiwa eneo alilokamatiwa,alisema kwa mujibu wamafundisho ya Uislamu,anafahamu kuwa Misikitiyote ni mali ya Waislamu nakila Muislamu ana haki yakufanya ibada yoyote.Shahidi namba tatu Bi.Zaidani Yusuph (66), aliilezaMahakama kuwa wakatialipokiwa ndani ya MsikitiniMarkaz Chang’ombe kwa ajiliya ibada ya Itiqaf Oktoba 16mwaka jana, aliona askariwanaume wakiingia upandewa wanawake usiku baada yakuvunja geti na mlango waMsikiti na kuanza kuwapiga.Shahidi huyo ambayeni mshatakiwa namba nne,alisema kipigo alichopatakutoka kwa Polisi, alijeruhiwakidole cha mguuni huku askarihao wakimtoa maneno yakejeli.“Kwa umri wangu huusikufanya ubishi wowote,lakini walinipiga licha yakuwauliza kosa langu ninini, walizidisha kipigo nawalifanya unyama mkubwa.”Alisema Bibi huyo.Wakili wa Serikali Bw.Tumaini Kweka, alipomuulizani nani kiongozi wake akiwakama Muislamu, Bi. Zaidanalijibu kwa kujiamini kuwakiongozi wake ni Qur’ an naSunna na hata alipoulizwanani msimamizi wake alisemahana zaidi ya Qur’ an.Wakili Kweka alipomuulizakama anaifahamu BAKWATA,Bi. Zaidani, alisema, “Siijui,sitaki kuijua wala sitakikuisikia, hata huyo Mufti,simjui.”Akitoa ushahidi wakembele ya Hakim Bi. Victoria Nongwa, shahidi namba tano,Juma (22), alisema ilimlazimukuacha ibada zake majira yasaa tisa usiku mara baada yakusikia vishindo nje, kwanigeti lilivunjwa ukafuatiamlango wa msikiti na kishaaliona askari Polisi wakiingiandani ya msikiti .Alisema mara baada yakuingia msikitini walianzakuwapiga na kuamuruwafanye wanavyotaka wao.Aliongeza kuwa Walivamia bila kutoa tangazo lolote nakwamba, vurugu zao ndizozilizokuwa ishara kuwa eneohilo kwa muda huo halikuwashwari.” Alisema Juma. Naye alipoulizwa kamaanaifahamu BAKWATA,alisema anaifahamu kuwani Taasisi ya Kiislamu kamazilivyo taasisi zingine za dini.Baada ya kuliizwa kama anamahusiano na chombo hichoalijibu kuwa haimuhusu.“Tukiwa ndani ya msikitimajira ya saa nane usikukwenda tisa, tulisikia kishindonje, kabla hatujakaa sawatulisikia mlango wa msikitiukibamizwa na mara waliingiaaskari kama wale(akionyesha baadhi ya askari FFUwaliokuwa mahakamanihapo) na waliingia viatu vyaoMsikitini.” Alisema shahidihuyo namba tano, Bi. FaridaLukoko (53).Bi. Farida ambaye nimshitakiwa namba 7,alionyesha Mahakamani hapoalama za majeraha mikononimwake, alisema kuwaalipigwa marugu mikononina mgongoni, jambo ambaloalidai kuwa hadi sasabadoanasikia maumivu makalikatika sehemu hizo.Alisema kipigo hichokilimfanya asijitambue baadaya kuanguka chini. Baadayealielezwa na wenzake kuwaalinyanyuliwa na askari haokwa kushikwa miguu namikono kisha kurushwa ndaniya gari.Shahidi mwingine ambayeni mshitakiwa namba tisaAthumani Salim, alipoulizwakama anaifaham Bakwata,alisema anaisikia tu, lakiniinajishughulisha na nini,hajui.Alipoulizwa ni wapi anaptataarifa za kuandama kwamwezi, alisema Waislamuwanafunga na kufungua kwamujibu wa Qur’an na Sunna, popote unapoandama au kwakukamilika kwa idadi ya sikukatika mwezi huo. Naye shahidi namba naneAdama Ramadhani (40),aliulizwa na mwendeshamashtaka wa Serikali Bw.Kweka, kama anafahamukazi za Bakwata, alisemaanachojua kazi yakekubwa ni kuwatangaziaWaislamu mwezi waRamadhani unapoandamana pindi unapomalizika na sivinginevyo.Kwa ujumla Mashahidiwote walidai Mahakamanihapo kuwa, hakunashahidi yeyote upandewa mashtaka aliyewatajakuwa ni wavamizi wakiwanja wanachoshutumiwakuvamia.Washatakiwa hao wameanzakutoa utetezi wao Jumatanowiki hii kufuatia HakimuMkazi wa Mahakama yaKisutu, Bi. Victoria Nongwa,Jumatatu wiki hii kusemaSheikh Ponda Issa Ponda nawenzake 49, wanakesi yakujibu.Washitakiwa wotewanakabiliwa na makosamanne, isipokuwa mshtakiwanamba moja (Sheikh Ponda)na mshtakiwa namba tano(Ust. Mukadam), ambaowanakabiliwa na mashtakamatano.Hakim Nongwa alisema pamoja na Mawakili waupande wa utetezi kutoamaelezeo ya kina katikautetezi wao juu ya shauri hilo,Mahakama imeona ni vyemaiwape nafasi washitakiwawaweze kupanda kizimbanikutoa utetezi wao.“Mahakama inaonawashtakiwa wotewaliokamatwa katikakiwanja kile, ni vyemawapande kizimbani ili watoeutetezi wao, waseme sababuzilizofanya waingie pale.”Alisema Hakimu Nongwa.Kwa mujibu wa Wakili waupande wa utetezi Bw. Juma Nassoro, ameileza mahakamahiyo kuwa jumla ya mashahidisitini watafika mahakani hapokutoa ushahidi wao upandekwa upande wa utetezi.
Maalim Seif awakumbusha Zanzibar OIC
Inatoka Uk. 1
Serikali ya Zanzibar,aliongeza kuwa iwapoZanzibar ingepata fursa yakuwa mwanachama wa OIC,ingekuwa mbali kiuchumikwa vile Jumuiya hiyoimekuwa ikichangia sanamaendeleo ya kiuchumikwa nchi wanachama.Maalim Seif alieleza hayokatika viwanja vya JamhuriJimbo la Makunduchi,wakati akihutubia mkutanowa hadhara uliotishwana Chama hicho hivikaribuni.Kielezea kusikitishwakwake na kitendo chaZanzibar kukoseshwaUanachama wa Jumuiyahiyo, alisema kitendocha Zanzibar kuzuiwakujiunga na jumuia hiyohuenda ni mpango maalumulioandaliwa wa kuipotezeaZanzibar umaarufuduniani.“Zanzibar ndio dolakongwe zaidi katikaukanda huu wa Kusini mwaAfrika, lakini tumepotezaumaarufu wetu”, alielezakwa masikitiko.Alielezea kusikitishwakwake na vitendo vya baadhiya viongozi wa upande wa pili wa Muungano, kwakutoithamini Zanzibar na kuipotezea haki zakeambazo ingepaswakuzipata.Maalim Seif alitoa mfanowa ujio wa Waziri waMambo ya Nje wa Oman,ambaye alizuru nchinisiku za hivi karibuni naalipowasili nchini RaisMwai Kibaki wa Kenya.Alisema wageni wotehao hakuna aliyepelekwaZanzibar na kuelezea kasorohiyo kuwa ni miongoni kwavitendo vinavyoinyimaZanzibar fursa.“Pamoja na yote hayo,lakini Wawakilishi waZanzibar walitakiwawaende wakatoe maoniyao mbele ya Wazirihuyo wa Oman, lakinikwa masikitiko makubwaWaziri wa Mambo ya Njewa Tanzania aliyapuuzamaoni na mapendekezoya Wazanzibari. Sijuiinakuwaje Waziri wa upandemmoja anaweza kuiamulianchi yenye Rais”, alielezana kuhoji.Maalim Seif alifahamishakuwa mambo yote hayoyanatokana na Zanzibar kutokuwa na mamlakakamili na kwamba,wakati umefika sasa kwaWazanzibari kuungana
Inaendelea Uk. 4

Activity (9)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 hundred reads
1 thousand reads
1 thousand reads
Saleh Hemed added this note
JAZAKALLAHU LKHAIR
Saidwaole liked this

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->