Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
6Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1062

ANNUUR 1062

Ratings: (0)|Views: 3,806|Likes:
Published by MZALENDO.NET
ANNUUR 1062
ANNUUR 1062

More info:

Published by: MZALENDO.NET on Mar 16, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

07/12/2014

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1062
JAMADUL AWWAL
1434, IJUMAA MACHI 15-21, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
www.annuurpapers.co.tz
Njama za kulitumbukiza Taifa
katika machafuko zafichuliwa
Vyombo vya habari, Serikali yahusishwaWaislamu watoa tamko zito, watoa onyoWaeleza Serikali inavyokoleza fitna, chuki
Ukweli wadhihiri juu ya muungano
Maoni ya Baraza yafunga mjadalaSi suala la Mzee Moyo wala UamshoNi la wananchi na Wawakilishi wao
KATIBU mkuu wa Chama chaWananchi CUF Mh. MaalimSeif Sharif Hamad amemtakaWaziri wa Mambo ya Ndani yaNchi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Nchimbi ajiuzulu- Maalim Seif
Na Mwandishi Wetu
kujiuzulu katika wadhifawake kutokana na kushindwakusimamia Wizara yake katikautekelezaji wa majukumuyake.
Akizungumza katika mkutano
Inaendelea Uk. 6
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda.WAZIRI mstaafu,Frederick Sumaye. MKUU wa Jeshi la Polisi nchini , Said MwemaWAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi 
Mtume(saw) amesema, “…Mahujajiwanarudishiwa kila walichokitumiakatika Hijja, shilingi moja kwa milionimoja.” Hivyo twende wengi,na mara nyingi kuhiji. Kadhalikatutumie mali zetu KUISIMAMISHANGUZO YA HIJJA. Jiunge na AhluSunna wal Jamaa. Gharama zoteni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliananasi ifuatavyo: Tanzania Bara:0717224437; 0777462022;Unguja:0777458075;Pemba: 0776357117.
(5) TAJIRIKA KWA KUHIJJI!
Mahakama kupitia pingamizidhamana ya Imam Hamza
Uk. 6
 
2
AN-NUUR
JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
Tahariri/Habari/Tangazo
KAULI aliyotoa Makamuwa Kwanza wa Raiswa Zanzibar, MaalimSeif Sharif Hamad hivikaribuni akitahadharishakuwa huenda kuna watuwenye nia mbaya ambaowameamua kuyatumiamatukio ya kuuawa nakujeruhiwa viongozi wakidini, kujenga chuki siya kupita bila kutiliwamkazo.
Katika kauli hiyoalipokuwa akihutubia katikahafla ya Maulid ya Kuzaliwakwa Mtume Muhammad(S.A.W), huko Mjini Kiuyu,Wilaya ya Wete, KaskaziniPemba, Maalim Seif alisemakuwa inasikitisha kuonawapo baadhi ya viongoziwenye nia chafu dhidi yaZanzibar wenye tabia yakutoa kauli za kujenga chukina fitna miongoni mwaWazanzibari.“Ni jambo la kusikitishakuna watu wenye nia chafudhidi ya Zanzibar, ambaowameamua kuyatumiamatukio haya kujenga chukimiongoni mwa Wazanzibariwenyewe kwa wenyewe”,alionya Maalim Seif.Makamu wa Kwanza waRais alisema kinachoonekanakuna ajenda imetayarishwaya kutaka kulazimisha chukiza kidini Zanzibar, licha yakuwa Zanzibar ina historia yadahari ya watu kuvumilianana kuishi kwa pamoja, pamoja na kuwepo watu waimani tafauti.Akawataka wananchiwote wa Zanzibar hivi sasawawe macho na ajendazinazolengwa kuwavurugana waendelee kuishi kwamshikamano na umojakama ambavyo wamekuwawakiishi.Maalim Seif katikanasaha zake alisema kuwawapo watu wanaolazimishakuwepo ugaidi Zanzibar iliwapate sababu ya kuwadhuruWazanzibari (Waislamu).Alisema inasikitishakuona baadhi ya viongozi namagazeti ya Tanzania Barayanachochea chuki za kidinina kusema kuwa Zanzibar kuna Ugaidi. Na kwamba halihiyo inaonesha kuwa kuna
Wanaopandikiza ugaidiTanzania ndio magaidi
Kauli ya Maalim Seif izingatiwe
ajenda imetayarishwa kutakakulazimisha chuki za kidiniZanzibar, kwa sababu hukoTanzania Bara kumetokeamatukio mabaya zaidi, lakinihayajahusishwa na ugaidi.Alitoa mfano matukio yakuuawa kwa Kamanda waPolisi Mkoa, na kuchinjwakwa Padri huko Geita, kuwani mabaya kabisa, lakinihakuna hata chombo chahabari kimoja kilichohusishamatukio hayo na Ugaidi.“Nasema Zanzibar hakunaUgaidi, hakuna ugomviwa kidini. Yanayotokeayametusikitisha sana, nimatokeo ya uhalifu wakupindukia, linalowezakufanywa lifanywekuwanasa wahalifu hawa,na kuwafikisha mbele yavyombo vya sharia”, alisemaMakamu wa Kwanza waRais.Aliwataka wananchi wotewa Zanzibar kwa wakatihuu kuwa watulivu nawasitawaliwe na jazba nawala wasichokozane, piawasikubali kuchokozeka.Sisi tungependa kutiliamkazo kwa kusema kuwakwa hakika wanaopaliliaagenda ya ugaidi ndio magaidikwa sababu wanachofanyani kujenga mazingira yakuteswa na kuuliwa watuwasio na hatia.Uzoefu unaonyeshakuwa mahali popote dunianiambapo wachafuzi, mafatanina wasaliti walifanikiwakupandikiza kitisho chaugaidi, basi kilichofuatiani mateso na mauwaji kwawananchi wasio na hatia. Ni kutokana na uzoefuhuo kama unavyodhihirikatika nchi za Afghanistan,Pakistan, Yemen, Kenya,Somali na huko Amerikaya Kusini katika miaka yanyuma, tunadhani kuwaitakuwa jambo la busarakusisitiza nasaha hizi zaMaalim Seif na kuwatakaWatanzania wote kuwazomeana kuwakomesha wale wotewanaotaka kupandikizachuki za kidini na kitisho chaugaidi miongoni mwetu.Tukifanya hivyo itakuwasalama kwetu sote, lakinitukiwafumbia macho nakuwachekea, tujue itakuwamsiba kwetu sote pia.
Ukweli wadhihiri juu ya muungano
UKWELI sasa upo wazi.Hoja ya Zanzibar kamanchi na Dola kamili, sisuala la watu wachache,bali la wananchi naWawakilishi wao katika‘Bunge’.
Hilo linadaiwakufahamika baada yakufichuka kuwa maoniya Baraza la WawakilishiZanzibar juu ya KatibaMpya yanafanana na yaleyaliyowahi kutolewa naMzee Hassan Nassor Moyo,Mansour, Masheikh waUamsho na Wazanzibariwalio wengi.Inaelezwa kuwa pamojana mambo mengine, katikamaoni yao Wawakilishiwamesisitiza hoja yakuwepo kwa Jamhuri yaMuungano wa Tanzaniainayotokana na Jamhuri yaTanganyika na Jamhuri yaWatu wa Zanzibar.Ikafafanuliwa katikanukta hiyo kuwa nilazima Katiba Mpya ijayoihakikishe kuwepo namaeneo maalum ya mamlakaambayo Zanzibar ina uwezonayo kama nchi (Mamlakaya Dola ya Zanzibar).Habari za uhakikazinafahamisha kuwa maoniyaliyowahi kutolewa na baadhi ya Wawakilishi kamaMheshimiwa Jussa juu yamuundo wa muungano nahadhi ya Zanzibar katikamuungano huo, yanajitokezakatika maoni ya pamoja yaWawakilishi katika Barazayaliyowasilishwa na SpikaPandu Ameir Kificho kwaidhini ya Kamati ya Uongozina Shughuli za Baraza yaBaraza la Wawakilishi laZanzibar.Habari hizozinafahamishakuwa Wawakilishiwanapendekeza kuwepo naMamlaka ya Zanzibar huruna Mamlaka ya Tanganyikahuru ndani ya Jamhuri yaMuungano.Katika hali hiyo,kinachosisitizwa ni kuwaMamlaka ya Muunganoyawekwe wazi nakwamba kuwe na usawawa Ushirikishwaji katikaMamlaka ya Muungano baina ya Tanganyika naZanzibar.Kwa mujibu wachanzo chetu cha habarikatika Baraza na katikaTume ya Jaji Warioba,inapendekezwa kuwa ilehali ya sasa ambapo jambolinaweza kuingizwa katikamuungano bila kupata
Na Mwandishi Wetu
ridhaa ya Zanzibar ipigwemarufuku. Na zaidi ni kuwa maadhalizilizoungana ni nchi mbilihuru, kila moja ikibakina dola yake kamili, basihata katika utoaji wa Raiswa muungano na makamowake liwe ni jambo lakupokezana.Sambamba na hilo,kinachosisitizwa ni kuwautungaji wa sera na sheria zamuungano, lisiwe ni jambola kufanyika Dodoma katikamamlaka za muungano, bali Dola mbili zihusike nakuridhia.Pamoja na maoni hayokama yanavyodaiwakuwasilishwa kwa Tume,inashauriwa pia kuwakila nchi iwe na rasilimalizake na kwamba zile zamuungano zitambuliwe nahizo ndio zitumike katikauendeshaji wa mamlaka zamuungano. Na kama kutakuwana kugawana mapatokutokana na rasilimalihizo, basi ugawaji ufanyikekwa uwiano maalumutakaokubaliwa kwa pamoja na pande mbili zaMuungano.Duru za kisiasa nchinizinafahamisha kuwa kamaTume ya Jaji Wariobaitafanya kazi yake kwauadilifu na kujali maoniya wananchi na vyombovyao vya uwakilishi,hakuna namna ya kukwepakufanya mabadilikomakubwa katika mfumowa muungano. Na kwamba hakunanamna nyingine yakufanya mabadiliko hayoyawakilishe matakwa yawananchi (Wazanzibari)na hivyo kukubalika nakupata uhalali wa kisiasa,ila kwa kufikia hatma yakurejesha nchi na Dolambili kama zilivyokuwakabla ya 1964 na ndiowatu wajadili mfumo wamuungano.“Kwa kweli kamamwisho wa yote muundohuu wa muunganohautabadilika na kuletampya ambapo kila nchi(Tanganyika na Zanzibar)zitakuwa Dola mbili zenyehaki sawa katika muunganohuo mpya, kile kinachoitwakero za muunganokitaendelea kuwepo namwishowe itakuwa zogolisilo na sababu. Borakufanya marekebishokwa njia za kiungwanana demokrasia kulikokusubiri kusambaratikakama ilivyotokea katika baadhi ya nchi la UlayaMashariki.” Alisemamchambuzi mmoja wasiasa za Zanzibar akitoamaoni yake.
Uongozi wa Masjid Tungi,Temeke jijini Dar es Salaamunawaarifu Waislamu wotekuwa, kutakuwa na Ibadamaalum ya Itqaf msikitinihapo.
Siku:
Jumamosi ijayo tarehe
23/03/2013
msikitini hapo baada ya swala ya Isha.
WOTE MNAKARIBISHWA 
WABILLAH TAWFIIQ
Itqaf Masjid Tungi
 
3
AN-NUUR
JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013
Habari
Njama za kulitumbukiza Taifa katika machafuko zafichuliwa
JUMUIYA na Taasisi zaKiislamu nchini, zimetoatamko kuelezea nakutoa tahadhari juu yakampeni zinazoendeleaza kulitumbukiza Taifakatika machafuko yakidini.
Katika tamko hiloambalo limewasilishwarasmi kwa Waziri Mkuu,Serikali ya Jamhuri yaTanzania imetuhumiwakuhusika kuchochea chukina kupandikiza farkana fitna miongoni mwaWaislamu na Wakristo jambo lililoelezwa kuwani la hatari.“Jambo la hatari sanaambalo sasa linatudhuru,ni kampeni za serikali zakuwasingizia Waislamumambo mazito yakuhatarisha amani nautulivu nchini ili kuhalalishadhana kuwa Waislamu niwatu hatari.”Imesema sehemuya tamko hilo na kutoamfano wa uzushi uliowahikutangazwa na aliyekuwaWaziri Mkuu MheshimiwaFrederick Sumaye.Ikaelezwa kuwa katikauzushi huo Sumaye alidaikuwa kuna magaidi waKiislamu waliokuwawamefuzu mafunzo njeya nchi na walikuwawamerejea nchini nakwamba shabaha yao yakwanza ilikuwa kulipuahospitali ya Muhimbili. Na kweli baada ya kaulihiyo ya Sumaye, “Waislamuwatatu wafanyakazi waMuhimbili akiwemoProfesa Jahazi, bingwa waBio-Chemistry, wakatiwambaroni kwa tuhumzaza kupanga kuilipuahospitali.”Tamko hilo laWaislamu linasema kuwa japo watuhumiwa wote“waliachiwa baada ya sikuchache, lakini tayari sumu ya propaganda chafu ilikuwaimekwishapenyezwa.”“Kwa Waziri Mkuukutangaza uzushi kamahuo, ni dhahiri kuwa lengolilikuwa ni kuwafanyawananchi wenginewawachukie Waislamukwa kukusudia kufanyauovu wa kulipua hospitali.(Na) la kuzingatia hapa nikwamba baada ya kauli
Na Mwandishi Wetu
WAKOLONI waKijerumani na waKiingereza waliaminikuwa Waislamu ni watuhatari sana, kidini nakisiasa. Hivyo waliwekamikakati kadhaa yakuwadhibiti. Imani hiyoya wakoloni ilitokanana msimamo madhubutiwa Waislamu wa kuwatayari kwa udi na ambarikupambana na wakolonihao ili nchi yetu iwehuru.
“Vema, mmetuhukumutunyongwe nasi tumekubali.Tumekubali kwa sababu nisisi wenyewe tulioendeamaji ya dawa Ngarambekwa hiari yetu; kwasababu hatukuona hakiya kutawaliwa na nyinyiwahuni. Na kwa sasakwa kuwa mmenipata, basi ninyongeni harakakusudi jina langu libakilikikumbukwa kwambanilikuwa mmojaniliyepigania nchi yangu”(Selemani Mamba, MajiMaji hero).Kauli ya shujaa SuleimanMamba aliyowaambiawakoloni wa kijerumaniwakati wa kunyongwakwake tuliyoinukuu hapo juu inaonesha msimamohuo ambao ni wa hatarikwa maslahi ya wakoloni.Ili kulinda maslahi yao,wakoloni wakaona njiarahisi ni kutugawa iliwatutawale. Kwa kuwawaliosimama kidete
Kiini cha Tatizo
kupambana nao kisiasawalikuwa ni Waislamu,wakatumia dini kutugawa.Kwa bahati mbaya, dhanahii kuwa Waislamu niwatu hatari sana kidini nakisiasa imekumbatiwa naawamu zote za serikali yaTanzania, bila kuzingatiakilichowafanya wakoloniwawachukie Waislamu. Na serikali za awamu zotezimekuwa zikihakikishakuwa zinaweka mikakatiya kuwadhibiti raia hawaambao ni hatari kwausalama wa nchi. Itoshetu kwa sasa kusema kuwakatika nchi yetu Wakristowa madhehebu mbalimbali,Walutheri, Waanglikana,Wakatoliki, Wasabato, nawengineo wanayo haki nauhuru wa kuratibu mamboyao na kuchagua viongoziwao bila ya kuingiliwa nadola. Lakini kwa Waislamusivyo. Vyombo vyaUsalama lazima vihusikekatika kuamua nani awekiongozi mkuu wa watuhawa hatari! Kwa hiyoserikali imetugawa nainaendelea kutugawa bainaya raia wapenda heri na raiawapenda shari. Tunajuakuwa wapo viongozikadhaa ambao ni Wakristowaliowahi kuishauri serikali(wakati wa uongozi waMheshimiwa Mkapa) kuwasasa Waislamu nao waachwehuru kuchagua viongoziwao kama raia wengine.Tunawashukuru kwa moyowao huo wa kizalendo, japoserikali bado inaamini njianzuri ya kuimarisha umojawetu ni kuwadhibiti nakuwadhoofisha Waislamu. Na kwa bahati mbaya,dhana hiyo pia imekuwaikiungwa mkono na baadhiya viongozi wa makanisa.Jambo la hatari sanaambalo sasa linatudhuru,ni kampeni za serikali zakuwasingizia Waislamumambo mazito yakuhatarisha amani nautulivu nchini ili kuhalalishadhana kuwa Waislamu niwatu hatari. Tunataja hapamifano michache tu kwaniorodha ya uzushi ni ndefu.Januari 2001, WaziriMkuu wa wakati huo,Mheshimiwa Frederick Sumaye aliita waandishi wahabari kuwataarifu kuwaserikali inazo taarifa kuwamagaidi waliopata mafunzonje ya nchi wamerejea nchinina kwamba wamepangakuilipua Hospitali yaTaifa ya Muhimbili, nakwamba vyombo vyadola vitawatia nguvuni. Na kweli mara baada yakauli hiyo Waislamu watatuwafanyakazi wa Muhimbiliakiwemo Profesa Jahazi, bingwa wa Bio-Chemistry,wakatiwa mbaroni kwatuhuma za kupanga kuilipuahospitali. Wote waliachiwa baada ya siku chache, lakinitayari sumu ya propagandahiyo chafu ilikuwaimekwishapenyezwa. Kwakama hiyo kutolewa naWaziri Mkuu hadharani,lau angetokea jasusi yeyoteakailipua hospitali hiyona kuuwa raia wengiwasio na hatia, hivi naniambaye asingeamini kuwauovu huo umefanywa naWaislamu?”Linasema na kuhojitamko la Waislamu kwambakwa nini serikali ipandikizechuki ya aina hiyo kwa raiawake? Na inafanya hivyokwa masilahi ya nani?Mfano wa pili unaotolewakuonyesha jinsi serikaliinavyopandikiza chukina kupalilia fitna nauhasama kati ya Waislamuna Wakristo, ni paleilipodai kuwa Waislamuwakitumiwa na watu wanje walikuwa wamepangakulipua makanisa siku yaJumapili tarehe 2 Septemba2001.Hiyo ilikuwa ni baada yamaandamano ya Waislamuya tarehe 24 Agosti 2001Waislamu wakipingakufungwa Hamisi Dibagulakwa kusema kuwa Yesu siMungu.Tamko linasemakuwa baada ya kaulihiyo ya serikali kuwaWaislamu wana mpangowa kulipua makanisa,askari “walitawanywamakanisani kuwalindaWakristo dhidi ya Waislamuwanaotaka kuwadhuru kwamabomu.”“Je, baada ya kaulihizo, akitokea jasusiyeyote akatega bomu nakuuwa watu kanisani, ninani atakayeshutumiwakwa mauwaji hayo kamasi Waislamu?” Tamkolinahoji.Pamoja na shutuma hizokwa serikali, vinashutumiwa pia baadhi ya vyombo vyahabari ambavyo vimekuwavikizua urongo dhidi yaWaislamu na hakuna hatuazozote zinazochukuliwa.Umetajwa mfano wayale madai kuwa Waislamuwalikuwa wameandaa jeshina silaha za kuulia Wakristona kwamba alipokuwa Rais,Alhaj Ally Hassan Mwinyialikuwa amewagawiaWaislamu majambia yakuwachinjia Wakristo wotenchini.Ukiacha matukio hayoya miaka ya nyuma, tamkolinagusia pia jinsi matukioya hivi karibuni ya sakatala kuchinja Wakristo na lilela kuuliwa Padri Zanzibar,yanavyovishwa gamba laugaidi na watuhumiwawakiwa ni Waislamu. Na katika jitihada hizoza kuwachafua Waislamu,inatajwa kuwa ndio sababuserikali imekimbiliakuwaita FBI bila kujalikuwa kufanya hivyo nikujidhalilisha.Tamko linasema kuwamabeberu wenye kiu narasilimali zetu, wanatumiamwanya huo kujipenyezakikachero na kijeshi hukusisi tukidhani na kufurahiakuwa tunashirikiana na taifakubwa kumbe tumejitiawenyewe kitanzi chaukibaraka.“Hakuwezi kuwa naushirikiano wa kweli bainaya nchi yenye nguvu na nchidhaifu. Katika ushirikianowa nchi kama hizo ukwelini kwamba nchi dhaifuinakuwa ni kibaraka tu wanchi yenye nguvu.”Tamko la Waislamulilisema hayo likinukuusehemu ya hotuba mashuhurisana ya kuwaaga wananchiwa Marekani iliyotolewa naRais George Washington 19Septemba, 1796.Tamko likasisitizakuwa “kwa waliosomana kulielewa Azimio laArusha, yote aliyosemaGeorge Washington,aliyasema Mwalimu Nyerere katika jitihada zakeza kulinusuru taifa letu.(Lakini) leo kwa paparayetu ya kujipendekezakwa Wamarekani imefikiahadi kuwakaribisha ndaniya kambi zetu za jeshikana kwamba na wao niWatanzani wenzetu!” Ni kutokana na ukwelihuo alioeleza aliyekuwaRais wa MarekaniGeorge Washington,tamko limeonyesha jinsi hao washirika wetuwanavyotumia udhaifuwetu mpaka kukamatavijana wetu na kuwapachikaugaidi huku serikali yetuikishindwa kuwatetea.“Baada ya serikali yetu
Inaendelea Uk. 4

Activity (6)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 thousand reads
1 hundred reads

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->