Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword
Like this
8Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1063

ANNUUR 1063

Ratings: (0)|Views: 3,954 |Likes:
Published by Hassan Mussa Khamis
Annur
Annur

More info:

Published by: Hassan Mussa Khamis on Mar 22, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

11/13/2013

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1063
JAMADUL AWWAL
1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
www.annuurpapers.co.tz
Maaskofu wanadaiKanisa lipo katika mateso.Lakini wakumbuke kuwawalishawasha moto kutokaLongido hadi Kyela, nakutoka Ngara hadiMikindani.
Sasa kwa hatua ya kuwekakila kitu mezani kijadiliweupya, yale madai ambayokwa miaka mingi serikaliimeyafunika na kuyapiga
Maaskofu wamepanda
upepo wanavuna tufani
Hakuna mateso, bali ‘mfumo’ umetikiswaHakuna anayejua muungano utaponaMbeleko inayowabeba inazidi kuchakaa
Mtume(saw) amesema,“Anaporudi mtu Hijja anarudishwana ujira mkubwa na zawadi nyingi”. Na akasema(saw),“Husamehewa mwenye kuhiji naanaowaombea”. Hivyo manufaaya HIjja yanawaenea wengi wasiokwenda. Karibuni AhluSunna wal Jamaa. Gharama zoteni Dola 4,300.Tafadhaliwasiliananasi ifuatavyo: Tanzania Bara:0717224437; 0777462022;Unguja:0777458075;Pemba: 0776357117.
(6) SIFA ZA MANUFAA YA HIJJA
chenga, yanakuwa sehemu yamadai ya Katiba Mpya.Hakuna ajuaye kamaMuungano utapona, na iliuvunjike harakati zitainuliwa,na Kanisa haliwezi kupangaziweje.Wanasema “panda upepo,uvune tufani”. Na hiyo ndiyomantiki ya kinachotokeasasa.
(Soma Uk. 7)
Nani atalipa dhulma hiiRais Shein, DPP au Jaji?
UPO usemi wakimasikhara, lakiniwenye maana nzito.Wanasema, hiyo Sikuya Hukumu (Kiama),Mungu awahi maanakesi zitakuwa nyingi.
Wiki iliyopita kesiya viongozi wakuu waJumuiya ya Uamsho naMihadhara ya Kiislamu(JUMIKI) iliingia katikahatua mpya baada yaMahakama Kuu kufutamaamuzi yote ya Mrajiswa Mahakama hiyo.
Soma Uk. 2
BAKWATA wamefanya
 
dhambi kubwa-
Waikela
Ni kwa kuuza mali za Waqfu, Mahakama yaombwa kuzirejesha
Nyerere alimfunga Waikela kwa kuipinga Bakwata 1963
Sheikh Ponda akamilisha ushahidi
Walioandamana kwenda kwa DPP jela mwaka mmoja
NECTA isafishwe kwanza
Kufeli wanafunzi kidato cha nne:
Wakuu Shule za Kiislam wafichua mazitoWashuku kuwa inachakachua matokeoWawasilisha hoja zao kwa Waziri Mkuu
 MZEE Bilal Waikela (mwenye bakora) akitoka nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya Sheikh Ponda.
 
2
 AN-NUUR
JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
Tahariri/Habari/Tangazo
Uongozi wa Masjid Tungi,Temeke jijini Dar es Salaamunawaarifu Waislamu wotekuwa, kutakuwa na Ibadamaalum ya Itqaf msikitinihapo.
Siku:
Jumamosi ijayo tarehe
23/03/2013
msikitini hapo baada ya swala ya Isha.
WOTE MNAKARIBISHWA 
WABILLAH TAWFIIQ
Itqaf Masjid Tungi
UPO usemi wa kimasikhara,lakini wenye maana nzito.Wanasema, hiyo Siku yaHukumu (Kiama), Munguawahi maana kesi zitakuwanyingi.
Wiki iliyopita kesi yaviongozi wakuu wa Jumuiyaya Uamsho na Mihadhara yaKiislamu (JUMIKI) iliingiakatika hatua mpya baadaya Mahakama Kuu kufutamaamuzi yote ya Mrajis waMahakama hiyo.“Maamuzi ya Mrajis yoteyanafutwa kwani hayakuwasahihi kwa vile Mrajishana mamlaka ya kisheriaya kupokea, kusikiliza nakutoa uamuzi kuhusu kesiiliyofunguliwa MahakamaKuu.”Hivyo ndivyoalivyonukuliwa Jaji AbrahamMwampashi wa MahakamaKuu Vuga, akisema.Moja ya mambo makuuyaliyofutwa ikaelezwa kuwani zuio la dhamana ambaloMrajis alilikubali kamalilivyokuwa limetolewa naMkurugenzi wa MashitakaZanzibar (DPP).Jaji Mwampashi alitoleamaamuzi baada ya pandembili katika kesi hiyo zaupande wa serikali na utetezikubishana juu ya uwezo waMrajis katika kutoa maamuziya dhmana kwa washitakiwahao.Mawakili wa uteteziwalidai kuwa Mrajis hanamamlaka hayo na upandewa waendesha mashitakawalidai kwamba anao uwezohuo.Jaji Mwampashi alisemaDPP anao uwezo wa kuzuiaPolisi tu kumpa dhamanamtuhumiwa, lakini sioMahakama kama ilivyotokeakatika suala hili.Jaji Mwampashi alisemaDPP alitakiwa aeleze sababuza washitakiwa kutopewadhamana na ni athari zipi zausalama wa taifa zitatokeaiwapo watakuwa nje, halafundio Mahakama iamue kwakuzingatia uzito wa hoja
Nani atalipa dhulma hiiRais Shein, DPP au Jaji?
zilizotolewa.Alisema kama sheriaingekuwa hivyo kungekuwahakuna haja ya kuwepo kwaMahakama kama mtu mmojaanakuwa na haki hiyo nakusingeifanya Mahakamakuwa kimbilio la wanaoonawanapoteza haki zao.Sisi tunasema swadaktaJaji Mwamapashe. Hakunahaja ya kuwa na Mahakamakama mtu mmoja anakuwana mamlaka ya kuamuakumweka ndani mtuapendavyo.Swali ni je, mpaka mtuanapewa cheo cha kuwaDPP au Mrajis, hajui sheriana kanuni hiyo? Kwa niniMahakama Kuu haikutumiahoja hii anayoitoa JajiMwampashe hivi sasa tokaawali kuhakikisha kuwahaki inatendeka na sheriahusika inafuatwa?Kama anavyosema Jajini kweli kwa mujibu washeria zilizopo, ni kuwawatuhumiwa ambao hivisasa wamekaa rumandemwaka mzima pungufuya nusu yake, watakuwawamedhulumiwa. Nani atalipa dhulma hii?Je, ni viongozi wa serikali,wa mahakama au wote kwa pamoja?Kuna kila dalili kwambakuna vumbi la kisiasalimegubika kesi hii namjadala unaoendelea. Ndiomaana tunapewa hekayahizi za mamlaka ya DPP naMrajis Vs Mahakama.Lakini ni ukweli piakuwa waliodhulumiwakwa kuwekwa ndani bilaya dhamana, hakuna namnaya kulipwa haki yao katikadunia hii.Ila ikumbukwe kuwaipo Siku ya Hakumu. Sikuambayo Mfalme na Hakimuatakuwa ni Allah (S.WT)Pekee. Na Qur’an inauliza, je, hakuwa Mola wako niHakimu wa Mahakimu?Siku hiyo hakutakuwana DPP, Mrajis wala JajiMwampashe na kesi zakisiasa.
WAKUU wa Shuleza Kiislamu nchiniwamewasilisha hojazao kwa Waziri Mkuu,Mheshimiwa MizengoPinda wakihoji uadilifundani ya Baraza laMitihani Tanzani(NECTA), wakionyeshamianya inayowezakutumika kutoa matokeoyasiyo sahihi.
Katika barua yao kwaWaziri Mkuu wamesemakuwa, pamoja na mambomengine, kuna matatizomakubwa ndani ya NECTA ambapo kunauwezekano mkubwa kuwamajibu yanayotolewa naBaraza hilo, sio sahihiwala yanayoakisi uwezowa mwanafunzi kamaulivyooneshwa na matokeoya mitihani aliyofanya. Ni kutokana na wasiwasihuo, wameomba kuwakatika jumla ya mamboyatakayofanywa naTume iliyoteuliwa naMheshimiwa Waziri Mkuu, basi moja liwe ni pamojana kutaka kuwekwa wazialama za kila mwanafunzikama alivyopewa nawasahihishaji wa mitihanikisha ilinganishwe namayokeo ya NECTA.“Mheshimiwa WaziriMkuu kwa kuzingatiayote tuliyosema hapo juundio maana tunasematatizo lililopo linawezakutatuliwa ikiwa utaamuakuwataka viongoziwaandamizi wa NECTA nawale wa Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundikuweka hadharani alamaza mitihani walizopatawanafunzi wa kidato channe baada ya zoezi lausahihishaji kukamilikakama zilivyo katika listone. Aidha viongozi haowa NECTA na WEMUwaweke wazi kanuniiliyotumika kubadilishamatokeo ya wanafunzikutoka list one kupata gredikama zilivyotangazwa na NECTA.”Hoja hii ya Wakuuwa Shule za Kiislamu,wameijenga wakitanguliakuonyesha kuwakumekuwa na ushahidimwingi wa kimazingirana wazi kutokana na
tafiti
Na Mwandishi Wetu
mbalimbali kwamba inakuwavigumu kwa sasa matokeo ya NECTA kuaminika.Wanasema, kumekuwa nausiri usio na sababu na kanunizisizo kubalika kitaalamu zakutoa madaraja ya mwishoambayo mara nyingi yanazuamaswali yasiyo na majibu.“Mheshimiwa WaziriMkuu ni ukweli usiopingikakuwa wadau wote wa Barazala Mitihani tukiwemo sisiwenyewe tunakabiliwa nachangamoto ya usiri mkubwawa uendeshaji wa shughuliza NECTA. Hatujui mchangowa mazoezi ya kila siku (CA)katika alama ya mwishoapewayo mwanafunzi, hatujui pass mark wala hatufahamugrade ranges zinazotumiwana Baraza la Mitihani kwasasa. Baya zaidi ni kwambaBaraza la Mitihani halikotayari kufanya mambo hayakuwa wazi kwa wadau wakelicha ya utafiti wa serikalina ule wa Kamati ya Mlamakudaiwa kuitaka NECTAkufanya hivyo.”“Mheshimiwa WaziriMkuu Sisi Baraza la Wakuuwa Shule za Kiislamutunaamini kuwa kufeli kwawanafunzi wa kidato channe 2012 kumechangiwakwa kiasi kikubwa na usirihuo ulioko NECTA ambaohuwapa fursa ya kuamuakupandisha viwango vyaufaulu (passmark), kushushamchango wa CA na kubadiligrade ranges bila kuwaarifuwadau wala kuwapa muda wakujiandaa.”Kutokana na usiri huona kutokufahamika kwa pass mark na grade ranges,inatuhumiwa kuwa NECTAhutumia mwanya huo katikakipindi inapokaa na matokeo baada ya kusahihishwakuweka viwango inavyotaka.Katika hali hiyo,unapatikana mwanya wakumfelisha au kumfaulishamwanafunzi kinyume na alamaalizopewa na wasahihishajikama ilivyorekodiwa katikalist one.Wakimalizia barua yao,Wakuu wa Shule za Kiislamuwamesema kuwa ni matarajioyao kuwa NECTA itawaelewana kuweka wazi taarifa hizo.Lakini end
apo NECTAitapuuza, wamesemawatakuwa tayari kutafutahaki yao, “ikibidi, kupitiamamlaka na vyombo vyakisheria ili kuviombaviiamuru NECTAitekekeleze wajibu wakewa kutoa taarifa hizo kwaumma.”
NECTA isafishwe kwanza
 
3
 AN-NUUR
JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013
Habari
BAKWATA wamefanya dhambi kubwa-Waikela
MZEE Bilali Rehan Waikela(87), ameiambia Mahakamaya Hakim Mkazi Kisutu,Jijini Dar es Salaam kuwa,kuuzwa ardhi ya Waqfu,Markazi Chang’ombe niaibu na dhulma kubwa dhidiya Waislamu nchini.
Mzee Waikela, amesemahayo Jumatano wiki hiimbele ya Hakim Mkazi waMahakama hiyo Bi. Victoria Nongwa, wakati akitoaushahidi wake katika kesiya jinai namba 245/2012,inayomkabili Sheikh PondaIssa Ponda na wenzake.Akiongozwa na mawakiliwa upande wa utetezi Bw.Juma Nassoro na Yahya Njama, Mzee Waikelaaliiomba Mahakama hiyokuirudisha ardhi hiyo kwaWaislamu, kwani BAKWATAwamefanya dhambi kubwakwa hatua yao ya kuiuza hukuwakijua mali ya waqfu nainahitaji kufanyiwa uadilifu.“Naiambia Mahakamakuwa aibu iliyofanyikani kubwa kwa mujibu waDini yetu, labda wapaganindiyo wanaweza kufanyahivyo. Naiambia Mahakamawairudishe ardhi hiyo kwaWaislamu, kwani hatuawaliyoichukuwa si sahihi.”Alisema Mzee Waikela.Mzee Waikela ambayeni mmoja wa waasisi waChama cha siasa cha TAA,kisha TANU, na kiongoziwa iliyokuwa Jumuiya yaWaislamu ya Afrika Mashariki(EAMWS), aliiambiaMahakama kuwa mali yaWaqfu kamwe haiwezi kuuzwahata kama imerithiwa.Akielezea ufahamu wake juu ya kiwanja cha MarkaziChang’ombe, Mzee Waikelaambaye alikuwa ni Katibu waEast Africa muslim WalfareSociety (EAMWS) mkoawa Tabora, alisema kiwanjahicho kilipatikana kipindi chauongozi wa Jumuiya hiyo yaWaislamu, chini ya uongoziwa Agakhan na Rais wa Misriwakati huo Gamar Abdul Nasser.Alisema kupitia Jumuiyahiyo, zilifanyika juhudikupata kiwanja hicho lengona madhumuni likiwa nikujengwa Chuo Kikuu ChaWaislamu kwa awamu tatu,kwa msaada wa Rais wa Misriwa wakati huo Gamar Abdul Nasser.Alipoulizwa ni kitu ganikilikwamisha adhima hiyo,Mzee Waikela aliwatajaaliowaita ‘mafatani’wakishirikiana na watu
Na Bakari Mwakangwale
wabaya, ambao walipangamikakati ya kuiuwa EAMWSna kuwaundia WaislamuBAKWATA.Alisema njama za kuiuwaEAMWS, zilifanywa naMwalimu Nyerere akimtumiaMzee Abeid Karume, kwakuwalaghai Waislamu ambaoaliwataja baadhi yao kuwa niAdam Nassib, Saleh Masasina Qassim Bin Jumaa.Mzee Waikela alisema, watuhao walizunguka katika mikoaishirini nchini wakati huona kuwashawishi Waislamukuikataa na kutengana naEAMWS. Hata hivyo alidaifitna yao ilifanikiwa katikamikoa nane na mikoa 12waliwakatalia.“Mimi binafsi nilikuwampinzani wa kuitenga nakuiuwa EAMWS, katiya mwaka 1968/9, kwaniwalifika akina Adam Nasibuna watu wake na kunishawishikwa kunipa Shilingi 40/=,nilizikataa wakaondoka.”Alisema Mzee Waikela.Alisema baada ya juhudihizo za kuwalazimishaWaislamu kuikataa Jumuiyayao, ilitumika Serikalikupitia Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo, Bw. SaidiMasanywa, kwa kusimamiakufungwa ofisi zote na malizote za Jumuiya zilizokuwanchi nzima kukabidhiwaBakwata.Aliongeza kuwa katikakuonyesha kwake upinzanikatika kuiuwa EAMWS,alijikuta kati ya mwaka 1963na 1964, akiwekwa kizuizina Mwalimu Julius Nyerere,wakati huo akiwa Rais waJamhuri ya Muungano.“Naiambia Mahakanakwamba, kiwanja chaMarkaz si mali ya Bakwata,wakati tunapewa kiwanjahicho Bakwata haipo,imekuja baadae kwa hilana inda pasi ya ridhaa yaWaislamu na kuhodhi maliza waislamu zikiwemo zaWaqfu.” Alisema Mzee Bilali, baada ya kuulizwa na wakili Nassoro kuwa anaiambia niniMahakama kuhusu madai yaumiliki wa Bakwata katikaeneo hilo.Aidha alifafanua kuwa waokama Jumuiya ya Waislamu,walisimamia mali za Waislamukikiwemo kiwanja hicho kwaajili ya maendeleo yao, lakinialidai baada ya mali hizokuhodhiwa na Serikali nakuikabidhi Bakwata, malinyingi za Waislamu zimeuzwakwa bei chee, si Dar es Salaamtu bali hata zile zilizokokatika mikoa mingine na malinyingine walikimilikisha watuwa Bakwata.“Mfano wa karibu ni hichokiwanja cha Chang’ombe,tulikabidhiwa likuwa nieneo kubwa sana tofauti nasasa, nasikia kimemegwa nakuuziwa watu. Lakini iwemtu kapewa ama kauziwa,aelewe kabisa kuwa mbeleya Mwenyezi Mungu si maliyake, ni mali ya Waislamu,mali ya waqfu haiuzwi,hagaiwi mtu.” Alisema MzeeWaikela.Akijibu maswali ya wakiliwa Serikali Bw. TumainiKweka, Mzee Waikela alisemaBakwata haipo kwa haki,ukifuatwa msingi wa kuundachombo kwa kuzingatiademokrasia, kwani katika juhudi za Bw. Nassibu nakundi lake mikoani, ni mikoanane tu ndio iliunga mkonokuvunjwa kwa EAMWS katiya mikoa 20.Alipoulizwa kamaanaikubali Bakwata, alisemahaikubali, si sasa tu balialiikataa tangu kuanza kwamchakato wake na baadaya kuundwa kwawe mkoaniIringa na mpaka sasa badohaikubali.“Mimi Bakwata siitambui,niliikata tokea wakati huochini ya Sawaya (Waziri waMambo ya Ndani wakatihuo), nikawekwa kizuizinina Nyerere, Bakwataimemilikishwa mali zaWaislamu kinguvu, kimsingimali hizo si za Bakwata ni zaWaislamu.” Alisema MzeeWaikela, ambaye pia alikuwakiongozi wa Baraza la MisikitiTanganyika.Akijibu hoja ya wakiliwa serikali Tumaini Kweka,kuwa waliounda Bakwatamkoani Iringa walikuwani Waislamu, Mzee Bilalialisema wale walikuwa niviongozi wa matawi ya Chama,na hawakuwawakilishaWaislamu kwani alidai halihalisi ilishaonyesha kuwakati ya mikoa 20 ni mikoanane tu iliyokubali. Alisisitizakwamba shughuli za dinihaziendeshwi na viongoziwa siasa bali ni viongozi wadini.Ama alipoelezwa kuwahakuikubali Bakwata kwakuwa alikosa donge, alisemawakati huo hakuwa na dhikiya pesa bali alikuwa ni mtumwenye mali zake na hatawakati anaingia katika siasa pia hakuwa na dhiki.“Sikuikataa Bakwata kwachuki, mimi nilikuwa na pesazangu hata wakati napambanana kupata Uhuru, nilikuwanatoa motokaa (gari) yangukwa Nyerere (Rais) akijaTabora atumie, lengo lilikuwani Waislamu kutendewa haki,nimeikataa kwa sababu yakupindishwa haki.” AlisemaMzee huyo.Kwa ujumla Mzee Waikela,aliianishia Mahakama yaHakim Mkazi Kisutu kwamba, Waislamu nchini wanatenzwanguvu ndani ya Bakwata,kwani alidai kuwa iwapoikitokea Waislamu kupigakura kama wanaikubaliau hawaitaki Bakwata,itaanguka.Hata hivyo Mzee Waikela,alisema hadhani kamainaweza kutokea fursa hiyokwa Waislamu kwani anajuakuwa maslahi ya walioundachombo hicho yataharibika.Katika hatua nyingine kwamara ya kwanza, jana SheikhPonda Issa Ponda, alisimamakatika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mbele yaHakimu Mkazi wa Mahakamahiyo Victoria Nongwa nakutoa ushahidi wake.Akianza kutoa ushahidiMahakani hapo, SheikhPonda alisema kuwa, ni kwelikiwanja hicho kina mgogoro,ambapo Waislamu wanapingaeneo lao kupewa kampuniya Agritanza, ambayo inadaikumiliki kiwanja hicho kwakubadilishana na Bakwata,ambao nao walipewa kiwanjakingine huko Kisarawe.Sheikh Ponda, alisemamigogoro ya viwanja eneola Markaz Chang’ombe ni yamuda mrefu, ambapo kunawakati sehemu nyingineya eneo hilo la MarkazChang’ombe, lilimegwa nakuuziwa mfanyabiasharamaarufu Yusuf Manji, kinyumena matakwa ya Waislamuambao ndio wenye mali.Alisema katika sakata hiloWaislamu walipinga ambapo baadhi yao walikwendaMahakamani, na wenginekwenda Serikalini kupingakuuzwa eneo hilo.Alisema eneo hilo laMarkaz awali lilikuwa kubwa,lakini sasa limebaki dogosana kutokana na tabia yakumegwa kinyemela bilaWaislamu kujulishwa.Kuhusu kiwanja chenyemzozo kwa sasa, ambachomfanyabiashara Hafidh,anayemiliki Kampuni yaAgritanza inayodai kumilikikiwanja hicho, Sheikh Pondaaliieleza Mahakama kuwamara baada ya kupata taarifaza eneo hilo la Markazkumegwa tena, walimfuatiliamtu aliyedaiwa kulimega ilikujua kulikoni.Sheikh Ponda alisemaWaislamu kupitia baadhi yaMasheikh, akiwemo yeye naSheikh Lwambo, walikutanana Hafidh ambapo walipangasiku ya kukutana kujadilitatizo hilo.Alisema baada ya kukutana,walimweleza Bw. Hafidh kuwakiwanja anachodai kupewa niwaqfu, kwa maana kuwa nimali ya Waislam ambayohairuhusiwi mtu kuuza,kuuziwa wala kujimilikishaisipokuwa ni kwa ajili yamatumizi ya dini, kwa maanaya matumizi ya masuala yaWaislamu.Akiendelea kutoa ushahidiwake Sheikh Ponda alisemakufuatia kikao hicho,walikubaliana na Bw. Hafidhkuwa asitishe kujihusisha nakiwanja hicho na kwamba,atatafutiwa kiwanja kingine.Sheikh Ponda, aliwasilishamuhtasari wa kikao kati yaona Bw. Hafidh Mahakamanihapo, waliyokubaliana kuwaBw. Hafidh, hatojihusisha nakiwanja hicho cha Markazkama walivyokubaliana.Hata hivyo, Sheikh Pondaaliieleza Mahakama kuwa, baada ya makubalianokufanyika kupitia kikaowalichokaa, walishangaakuona Bw. Hafidh, akipelekavifaa katika kiwanja hichona kuanza ujenzi tofauti nawalivyokubaliana.Alisema, baada ya kuonahivyo, walimtafuta Bw.Hafidh na kumuuliza kulikoniakiuke makubaliano ya kikaochao cha awali, ya kukiachakiwanja hicho cha Waislamuna kukubaliana kutafutiwakingine.Alisema, kufuatia haliiliyojitokeza Waislamuwalikubaliana na kuamuakujenga Msikiti wa mudakatika eneo hilo, ili kuhakikishakwamba eneo hilo, haliingiliwina mtu mwingine.Hata hivyo, Sheikh Ponda,alisema siku ya Ijumaa yaOktoba 12, 2012 Waislamuwalipokuwa wakijengaMsikiti wa muda, Bw. Hafidhaliamua kulipeleka suala hilo polisi. Ndipo baadae alisemaSheikh Ponda, kwambawalifika Polisi na kuwavamiaWaislamu na kuwaswekandani.Aidha Sheikh Ponda, aliitakaBakwata kurejesha eneo lotela Waislamu Chang’ombe,kama walivyolikuta wakatilikiwa chini ya East AfrcaMuslim Walfare Society.Alisema, kitendo chaBwakata kukiri kuwa eneolimebaki dogo lakini lilikuwakubwa, ni wazi kwambakwa njia moja au nyinginekuna watu wameuziwa hukuwakijua kuwa ni eneo lawaqfu.Hivyo Sheikh Ponda,alihitimisha ushahidi wakekwa kuitaka Bakwata kwahali yoyote, kurejesha eneolote la Waislamu.Kesi hiyo imeahirishwa,ambapo April 4, Wakiliupande wa utetezi atawasilishaMahakamani majumuisho yaushahidi uliotolewa ambapoAprili 18 mwaka huu, kesiitatajwa Mahakamani hapokwa ajili ya hukumu.Taarifa tulizozipata wakatitunakwenda mitamboni,zimefahamisha kuwa baadhiya Waislamu waliokuwawameandamana Februari 15,kuelekea ofisi za Mkurugenziwa Mashtaka (DPP), kwalengo la kutaka kujua sababuza kunyimwa dhamana SheikhPonda, wamehukumiwakwenda jela mwaka mmoja.Hukumu hiyo imetolewa jana katika Mahakama yaKisutu jijini Dar es Salaam.

Activity (8)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 thousand reads
1 hundred reads
Shemahonge Khalifa added this note
ALHAMDULILLAH! NILIKUWA NIMELIMISS ANNUR. NIKO MKOA AMBAPO HALIFIKI. ALLAH AWALIPE KWA KULIWEKA MTANDAONI
Salim Ahnmed liked this
Salim Ahnmed liked this

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->