You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Mahakama yaahirisha hukumu ya Sheikh Ponda

Nkamia apasua jipu la udini UDOM


Mwandosya, Rage wathibitisha udini serikalini Mawaziri, Makatibu wote Ikulu Wakristo Hali ingekuwaje wangekuwa Waislamu?
Na Mwandishi Wetu
HOJA zilizotolewa juzi na jana Bungeni kutetea Serikali kuwa haina udini, kwa upande mwingine hoja na takwimu hizo zimethibitisha madai ya Waislamu kuwa kuna udini. Wakichangia Bungeni kwa nyakati tofauti, waheshimiwa Mark Mwandosya, Aden Range na Munde Tambwe Abdallah wamesema kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete binafsi na Serikali yake, hana udini kwa sababu katika watu anaoteuwa, wengi Inaendelea Uk. 3

ISSN 0856 - 3861 Na. 1067 JAMADUL THAN 1434, IJUMAA -APRILI 19 - 25, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Unaki huu Pambaneni na nafsi msi s i n gi z i e v i m i n i mpaka lini?


MHE. Aden Rage Prof. Mark Mwandosya Mbunge wa Kondoa Kusini Juma Nkamia,

Hata Zanzibar wanawakilishwa na Mbunge Mkristo

MARA tu baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2 0 1 0 , Wa h e s h i m i w a Wa b u n g e w a l i f a n y a uchaguzi kuchagua Mhe Spika, Mhe Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge (Presiding Ofcers) Watatu. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, kati ya Wenyeviti Watatu wa Bunge, mmoja lazima atoke Zanzibar. Matokeo ya uchaguzi huo ni kuwa viongozi WOTE walikuwa Wakristo! Uongozi ulikuwa kama ifuatavyo: Spika Anna Makinda Mkristo, Naibu Spika Job Ndugai, Mkristo, Mwenyekiti Jenister Mhagama Mkristo, Mwenyekiti G e o r g e Simbachawenye, Mkristo

(baadae Mhe Zungu), Mwenyekiti Sylvester Massale Mabumba (Dole, Zanzibar) Mkristo. La kushangaza ni kuwa hata pale alipotakiwa Mbunge kutoka Zanzibar ili awe Mwenyekiti wa Bunge, basi nafasi hiyo pia akapewa Mkristo! Ikumbukwe kuwa Mhe Mabumba ndio Mbunge PEKEE kutoka Zanzibar ambaye ni Mkristo! Kwa upande wa Menejimenti, Katibu wa Bunge (Dr. Thomas Kashilila) na Wakuu wa Idara WOTE ni Wakristo! Je, Mhe Joseph Selasini analionaje hili? A u w a k i w a Wa k r i s t o hakuna tatizo? Unafiki huu wa Mhe Selasini na watu wa aina yake mpaka lini? (Soma Uk. 6, 7)

Waislamu wapumzike Ijumaa, Jumapili kazini


Marufuku nguruwe Chuo Kikuu SUA Pesa ya Pombe isiingie Ikulu, Hazina Ruzuku kwa Kanisa ikome mara moja

Washughulikieni kwanza mashoga Msisahau wateja wa Changudoa Uk. 5 Uk.8 Mzee Mwinyi kasema kweli:

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Habari
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


tulivyosema, Muislamu huwekwa kuondoa muhali. Kwa bahati mbaya, hali hii ya kudunishwa Waislamu imekuwa ya muda mrefu sana mpaka sasa tumekuwa na wanasiasa kama Mheshimiwa Rage ambao wenyewe hawajiamini, hawaoni kuwa nao wana haki ya kuwa Wakuu wa Mikoa/Wilaya, ndio unaona hoja kama hizi za kuitetea Serikali kwamba haina udini kwa vile imeweka Waislamu wachache kila mahali kama Wakristo wanavyotaka. Udini wa namna hii na mawazo kama haya kwa hakika yasipopigwa vita na kufutwa kabisa katika kra na vichwa vya Watanzania, hatutakuwa na salama huko tuendako. Hoja yenyewe ni nyepesi tu kueleweka: kwamba hizi ni kra za kuendeleza dhulma. Na dhulma haidumu. Itaka mahali watu watasimama kwa nguvu zao zote kusema, basi, tunakata haki. Ikitokea na wale waliokuwa wakifaidi katika utaratibu huu wa dhulma nao wakisema hatutaki, hapo ndio itakuwa balaa. Sasa tuna hiyari, ama tuepushe balaa mapema kwa kutenda haki au tusubiri balaa lije.

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


MAONI YETU

Hata Zanzibar ni Mbunge Mkristo


HALI ya uongozi Bungeni hivi sasa ipo kama ifuatavyo: Spika Anna Makinda, Mkristo, Naibu Spika Job Ndugai, Mkristo, Mwenyekiti Jenister Mhagama Mkristo, Mwenyekiti G e o r g e Simbachawenye (baadae Mhe Zungu) Mkristo, Mwenyekiti Sylvester Massale Mabumba (Dole, Zanzibar) Mkristo. Kama ilivyoandikwa katika makala moja katika gazeti hili ni kuwa hata pale alipotakiwa Mbunge kutoka Zanzibar ili awe Mwenyekiti wa Bunge, basi nafasi hiyo pia akapewa Mkristo! Kwa upande wa Menejimenti, Katibu wa Bunge (Dr. Thomas Kashilila) na Wakuu wa Idara WOTE ni Wakristo! Katika hali kama hii, Watanzania (Waislamu) wanachotakiwa kuamini ni kuwa maadhali uongozi wa Bunge umeshikwa na Wakristo watupu, hakuna udini! Kungekuwa tu na udini iwapo japo robo ya viongozi hao wangekuwa Waislamu! Hivi ndivyo wanavyokiri Wakristo na kwa bahati mbaya ndivyo walivyoaminishwa na kukubali baadhi ya Waislamu. Na haya ndiyo tulimshuhudia Mbunge wa Tabora Mjini, Mheshimiwa Aden Range akizungumza Bungeni juzi, Jumatano. Mheshimiwa Rage akimtetea Mheshimiwa Rais Kikwete kuwa yeye binafsi na Serikali yake kuwa haina udini, aliorodhesha watendaji na viongozi muhimu Serikalini wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa/Wilaya n.k, ambapo kwa zaidi ya asilimia

Mr. Aden Rage huu ndio Udini Hoja kama yako itatuangamiza

Waislamu na Wakristo au ikaweka idadi kubwa ya Waislamu ikilinganishwa na Wakristo (kutokana na sifa sio upendeleo); itakumbana na hasira kali za Wakristo. Kwa hiyo hujihami na mapema kwa kuhakikisha kuwa hakuna taasisi inayokuwa na Waislamu wengi. Au kama si hivyo, inawezekana kuwa mfumo uliojengeka Serikalini ni ule ambao wengine huuita Mfumokristo ambao mara zote kwa makusudi, hata kama kusingekuwa na kelele za Maaskofu, huhakikisha kuwa Wakristo wanashika nafasi zote nyeti na kama

70, walikuwa Wakristo. Jamani udini upo wapi hapa? Mheshimiwa Rage alikuwa akiuliza swali hilo mara kwa mara kila alipotoa takwimu na kuonyesha wingi wa Wakristo ikilinganishwa na Waislamu kama ni ushahidi kuwa Mheshimiwa Kikwete/ Serikali haina udini. Sisi tunasema huu ndio udini wenyewe na mawazo/hoja kama hiyo ya Mheshimiwa Aden Rage ni potofu na ndiyo itakayoliangamiza taifa hili. Anachosema Mheshimiwa Rage na akina Joseph na kila wenye mawazo kama yao ni kuwa, inapotokea Serikali ikajaza Wakristo watupu katika timu ya Wakuu wa Mikoa/Wilaya, Makatibu Wa k u u , Wa k u r u g e n z i , Baraza la Mitihani, Wakuu wa Vyuo/Shule, Maofisa Elimu n.k; hakuna udini. Wanachotuambia kwa lugha nyepesi ni kuwa Wakristo ndio wenye haki ya kushika nafasi zote muhimu za uongozi katika nchi hii, kama walivyoshika Bunge na kama ni kupewa Waislamu, basi wasipewe ila wachache tu wa kuondoa lawama! Haya ndio sisi tunasema kuwa ni mawazo potofu kwa sababu yanaendeleza dhulma na ubaguzi katika nchi hii na muda wa kuwa dhulma inadumishwa, basi nchi hii haitakuwa na salama mbeleni. Ta k w i m u a l i z o t o a Mheshimiwa Rage Bungeni ni ushahidi tosha kuwa kuna udini na udini wenyewe ni wa kuwapendelea Wakristo. Kila serikali inapofanya uteuzi, basi inakuwa kana kwamba inaongozwa na kelele kama za akina Selasini, Wachungaji na Maaskofu, kwamba kama ikiweka japo uwiano wa

Kamati Huru ya Makanisa kukishwa mahakamani


Na Bakari Mwakangwale

MAALIM Ally Bassaleh, a m e s e m a Wa i s l a m u wanakusudia kuishitaki Mahakamani Kamati Huru ya Umoja wa Makanisa Tanzania, kwa kuwazushia uongo Waislamu kuwa wana vituo vya Kigaidi. Maalim Bassaleh ameyasema hayo akiongea na Waislamu mara baada ya swala ya Ijumaa, katika Msikiti wa Idrisa, Kariakoo Jijini Dar es Salaam, akiongelea waraka (Barua) ya kamati hiyo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi. Akavisihi vyombo vya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi nchini kutopuuza madai hayo ya Umoja huo wa Makanisa, chini ya Mchungaji Chritopher Mtikila, kwa kuwahoji na kuthibitisha madai hayo. Maalim Bassaleh, alitanabahisha kwamba, endapo vyombo hivyo vya dola vitanyamazia shutuma na madai hayo mazito kwa Uislamu na Waislamu nchini, na tishio kwa Usalama wa Taifa, basi Waislamu watachukua hatua. Tunavitaka vyombo vya usalama wawatafute hao waliosema hayo na wakawaoneshe vituo hivyo vya Kiislamu vinavyotoa mafunzo ya ugaidi nchini kwa Waislamu na wathibitishe, kama si hivyo tunakwena Mahakamani, kwa kuwazushia uongo Wa i s l a m u k w a n i h a t a Uislamu haukubaliani na

vitendo vya kigaidi, hii ni kashfa nzito kwa Waislamu, lakini pia ni tishio kwa Uslama wa Taifa. Alisema Maalim Bassaleh. Maalim Bassaleh, alisema, waraka huo unadai kuwa kuna Waislamu nchini wameandaliwa nje na ndani ya nchi, kwa ajili ya ugaidi ili kuja kuangamiza Ukristo nchini, jambo ambalo alidai ni uzushi mkubwa. Maalim Bassaleh, aliendelea kuuchambua waraka huo aliodai kuwa umejaa fitna, na wenye malengo ya kuwagawa Watanzania, umedai kwamba kuna Waislamu waliokwenda Somalia kufunzwa na AlShabab na Al-Qaida jinsi ya kuangamiza Makafir (Wakristo), na kwamba eti sasa wamerejea nchini kwa ajili ya vita. Alisema, waraka huo umefafanua hayo kwa kusema kuwa huu ni udini wa Rais Kikwete na ugaidi wa Kiislamu (Uk.7), jambo ambalo Maalim Bassaleh, alidai kuwa kauli hiyo ni ya kizushi na kashfa. Hii ni shutima nzito dhidi ya kiongozi wa nchi lakini hilo tunamwachia mwenyewe (Rais), kwa sababu aliyetajwa hapo ni yeye na watendaji wake, kuwashughulikia hiyo ni hiyari yake. Sisi kwa upande wetu tutafuata taratibu za kisheria wakathibitishe Mahakamani. Alisema Maalim Bassaleh. Maalim Bassaleh alisema, kwa mwenendo huo ni wazi kwamba umoja huo wa

Makanisa wamedhamiria kuligawa Taifa. Alisema, viongozi wa Makanisa, wamekuwa hawakosi kasumba na kuzua mambo ili mradi tu, wanapenda kuona Waislamu katika nchi hii wanakuwa ni watu wa kupata misukosuko tu. Kutokana na mihadhara ya Kiislamu kuingiza Wakristo wengi katika Uislamu, ndipo mashinikizo yakaanza kutoka kwa Maaskofu kuitaka Serikali kuwashughulikia Waislamu kwa kwa madai wanaendesha mihadhara ya kashfa. Alisema maalim bassaleh. Maalim Bassaleh, aliwakumbusha Waislamu sakata la Mwembechai, a m b a p o Wa i s l a m u waliuwawa kwa risasi za moto, sambamba na sakata la Ustadhi Dibagula, aliyehukumiwa kwenda jela, yote hayo alisema ni kwa ajili ya Waislamu kusema Yesu si Mungu huku anayesema Yesu ni Mungu yupo sawa kwa Serikali inayodaia haina dini. Rais Mkapa leo anathubutu kusema katika utawala wake hakuwa na udini wakati mimi binafsi katika utawala wake nilipigwa, kwa kulaani Muislamu kufungwa na Serikali yake kwa kusema Yesu si Mungu. Alisema Maalim bassaleh. Machi 31, 2013, inayojiita Kamati Huru ya Umoja wa Makanisa Tanzania, ilimuandikia barua Mh. Dr. Emannuel Nchimbi, aliye Waziri wa Mambo ya Ndani, ikiwashitaki Rais Kikwete pamoja na Waislamu.

3
Na Shaban Rajab
MBUNGE wa Kondoa Kusini Juma Selemani Nkamia, amesema kuwa kuna watu wanaona tabu kuona baadhi ya Watanzania w e n z a o ( Wa i s l a m u ) wakishika nyadhifa za juu katika taasisi za umma na ndio hao wanaopiga kelele za udini. Nkamia amesema hayo wakati akichangia hoja ya Osi ya Waziri Mkuu, ambapo alianza kwa kuzungumzia yale aliyoyaeleza Mh. Selasini akituhumu uongozi wa Chuo Kikuu Dodoma kuwa una udini. Awali akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Rombo (CHADEMA) Joseph Selasini, alisema kuwa kuna tatizo la udini katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kuongeza kuwa, tatizo la udini limepandikizwa na baadhi ya viongozi wa serikali. Hata hivyo, akizungumzia tuhuma hizo, Mheshimiwa Juma Nkamia alisema kuwa tuhuma nyingi za udini chuoni hapo zinatokana na itikadi za watendaji wakuu wa chuo hicho Prof. Idris Kikula na Prof. Shaaban Mlacha. Mhe. Spika, kama tatizo ni (Profesa Idris) Kikula na (Profesa Shaban) Mlacha kwa sababu za itikadi zao, basi tusiingize mambo haya udini chuoni pale. Mimi ninasoma pale, sijawahi kuona tatizo la udini alilolieleza Mheshimiwa Selasini. Lau kama anayeoongoza chuo angekuwa ni Lyimo fulani pale, yasingezungumzwa maneno haya! Chuo kinaendelea vizuri tu na hakuna matatizo pale. Alisema Bw. Nkamia. Itakumbukwa kuwa katika siku za nyuma kidogo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Idris Kikula na Naibu Makamu wa Chuo hicho Prof. Shaban Mlacha, waliwahi kutuhumiwa kuwa wametafuna fedha za mradi wa ujenzi wa chuo hicho. Licha ya watuhumiwa kukanusha mara kwa mara tuhuma hizo, bado zilipamba moto na kuendelea kuchapishwa kwenye vyombo vya mbalimbali vya habari nchini, kiasi cha serikali kulazimika kufanya uchunguzi kwa kupitia osi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili kubaini ukweli wa tuhuma za kisadi katika mradi wa ujenzi wa chuo zilizokuwa zikitolewa dhidi ya viongozi hao wa chuo. Baada ya kukamilika uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, matokeo yalionyesha kuwa hakukuwa na ufisadi wowote uliofanywa katika

mradi huo na kwamba, matumizi ya fedha za mradi yalifanyika vizuri. Tuhuma zikaishia hapo. Haukupita muda, mwezi Juni kuelekea Septemba mwaka jana, zikatolewa tuhuma nyingine kwamba kumekuwa na usadi mwingine uliokuwa ukifanyika chuoni hapo, safari hii zikiwahusisha viongozi wa chuo kutafuna ada za wanafunzi kwa kushirikiana na benki moja mjini Dodoma. Uongozi wa UDOM, ulikanusha kutafuna fedha hizo za ada za wanafunzi chuoni hapo. Katika taarifa ya ufafanuzi ya chuo hicho iliyotiwa saini na Osa Uhusiano wake, Bi. Beatrice Baltazary, ilieleza kuwa habari hiyo iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku ilikuwa na upotoshaji. Katika ufafanuzi wa chuo, ilielezwa kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kulipa gharama zote zinazoambatana na kupata elimu chuoni hapo mara wanapoanza mwaka wa masomo. Kwa mujibu wa ufafanuzi huo, kulingana na utaratibu uliotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa ada kulipwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, inamlazimu mwanafunzi kusaini ili kuthibitisha fedha kupokelewa chuoni na wale wasiosaini, fedha hurejeshwa bodi na deni hubakia kwa mwanafunzi. Hili nalo lilipita. Haukupita muda, zikazagaa habari za kashfa za ngono UDOM. Kwamba baadhi ya wanafunzi wa kike wanajihusisha na biashara ya kuuza miili yao kwa lengo la kujikimu kimaisha. Tuhuma hizo zilitolewa wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM mwaka jana wakati wahitimu takribani 6,392 walitunukiwa vyeti, stashahada , s h a h a d a z a kwanza, uzamili na shahada za uzamivu. Hata hivyo tuhuma za ngono kwa baadhi ya wanafunzi zilidaiwa kusababishwa na ukata uliokuwa ukiwakabili wanafunzi hao, kiasi cha kuwalazimu kutoroka chuoni nyakati za usiku na kujiunga na baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwa uchangudoa kwa lengo la kujiuza. Tatizo hili kwa uhalisia wake limekuwa ni tatizo la vyuo karibu vyote vikuu. Ilishawahi kuripotiwa namna wanafunzi wanaoishi katika hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam za Mabibo namna wanavyojiuza.

Nkamia apasua jipu la udini UDOM


Aidha adha hiyo ya ufuska ilishawahi kuvikumba vyuo vya CBE na IFM vya jijini Dar es Salaam. Hata hivyo uongozi wa vyuo hivyo haukusakamwa mithili ya ule wa UDOM. Hata hivyo watu mbalimbali wenye kukifahamu barabara Chuo Kikuu cha Dodoma, wamekuwa wakishangazwa na kusikitishwa na tuhuma hizi dhidi ya UDOM. Wengi wanaona kuwa kuna agenda ya siri dhidi ya chuo hicho. Ifuatato ni sehemu ya ushuhuda uliotolewa na baadhi ya wananchi wenye uchungu na Taifa lao, ambao waliamua kulifanyia kazi suala la tuhuma za udini UDOM kwasababu zilizotajwa kuwa ni chuki. Kwamba kama ni suala la udini, basi linaweza kujieleza lenyewe kupitia mtiririko mzima wa uwiano wa kiutawala na kiuongozi katika chuo hicho. Uongozi wa UDOM Chancellor: H. E. Benjamin W. Mkapa (Catholic), Vice Chancellor: Prof. Idris Kikula (Muslim), Chairman of Council: Hon. Dr. M. G. Bilal (Muslim), Deputy Vice Chancellor (Academic): Prof. L. Kinabo (Catholic), Deputy Vice Chancellor (Administration) Prof. S. Mlacha ( Muslim).

Habari

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


watu hao na wapambe wao hawalitakii mema Taifa. Hata hivyo, kutokana na chuki iliyoenezwa kwa muda mrefu juu ya jambo hili hapo UDOM, kuna haja ya kufanyika utati zaidi kuhusu muundo wa uongozi katika vyuo na taasisi nyingine za umma kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mzumbe University, Muhimbili Medical Institute na vinginevyo na kuwekwa wazi matokeo kwa madhumuni ya kufuta madai haya ya chuki za kiimani. Kulingana na mtiririko huo wa utawala wa UDOM, inafahamika kwamba viongozi wa wake hawakuteuliwa kwa sababu ya dini zao, bali uwezo wao ambao kwa kiasi kikubwa unajidhihirisha kwa jinsi walivyofaulu kubadilisha mandhari ya vilima vya Chimwaga na vitongoji vyake, pamoja na ramani ya nchi yetu katika dunia ya elimu ya juu. Ujenzi wa UDOM umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua kiwango cha elimu kwa vijana wanaomaliza k i d a t o c h a s i t a . Vi j a n a wa wakulima na masikini wengine wa Tanzania ambao sasa wanasoma UDOM leo wangebakia kuwa machinga au wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwa kukosa sehemu za kujiendeleza. Wanaosoma UDOM ni Wa t a n z a n i a Wa k r i s t o , Waislamu au wanachama wa CHADEMA, CCM, CUF au NCCR.

AN-NUUR

Inatoka Uk. 1

Mwandosya, Rage wathibitisha udini serikalini

Viongozi wengine wa ngazi za juu UDOM: Principal College of Education: Prof. K.M. Osaki (Catholic), Deans of Schools in the College are all Christians. Principal - College of Humanities: Prof. C. M. Rubagumya (Christian), 2 Deans of Schools in the College are all Christians, Principal- College of Informatics: Prof. N. Mvungi (Christian - Protestant), Dean of Students (Christian). Dean, School of Natural Science (Christian), Dean, School of Medicine (Christian), Dean, School of Nursing ( Christian). Source: (UDOM Prospectus and Website) Wafanyakazi - Wanataaluma - Christians 96% - Muslim 4% Wafanyakazi Waendeshaji - Christians 86% - Muslim 14% Wanafunzi - Christians 92% - Muslim 8% (Source UDOM Website, announcements of student admission) Katika mazingira haya inashangaza kuona watu kuzusha kwamba UDOM ni Chuo cha Waislamu kwa kuwa tu, kuna viongozi watatu Waislamu bila kuyafanyia kazi madai yao. Bila shaka

wao ni Wakristo. Akianza Mheshimiwa Aden Rage ambaye alitoa takwimu ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa n.k, ambapo alisema kuwa kote huko Wakristo ndio wengi. Udini upo wapi hapa, alikuwa akiuliza Rage akimaanisha kuwa maadhali Rais kachagua kwa kiwango kikubwa Wakristo katika Serikali yake, udini upo wapi. Akiunga hoja ya Rage, Waziri wa Nchi katika Osi ya Rais asiye na Wizara Maalum, Mheshimiwa Mark Mwandosya alisema kuwa wapo Mawazi wa Nchi 4 wanaomsaidia Rais Ikulu, wote ni Wakristo. Akitoa takwimu zaidi akasema kuwa Makatibu wote Ikulu pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi na Wakurugenzi wote, ni Wakristo. Naye kama Mheshimiwa Aden Rage, Mheshimiwa Waziri Mwandosya akahoji udini upo wapi hapo. Anachosema Mheshimiwa Mwandosya ni kuwa hapawezi kuwa na udini mahali ambapo Rais ameteuwa watendaji

Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Munde Tamwe wote kuwa Wakristo! Kwa maana nyingine ni kuwa, kungekuwa tu kuna udini iwapo katika orodha na takwimu hizo alizotoa Mheshimiwa Mwandosya, kungekuwa na Waislamu. Hili ndilo alilolisema pia Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Munde Tamwe Abdallah ambaye alisema kuwa haoni kuwa Rais Kikwete ana udini kwa sababu aliteuwa Wakuu wa Wilaya 5 wanawake, na wanne kati yao wakawa ni Wakristo na Muislamu mmoja tu! Ambalo Munde hakulisema ni kuwa hali ingekuwaje kama ingekuwa kinyume chake. Kwamba Waislamu wakawa wanne na Mkristo mmoja. Je, bado angesimama na kutoa hoja kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hana udini? Na je, Wakristo wangeweza kuvumilia hali hiyo ya kuona Rais anateuwa Wakuu wa Wilaya ambapo Waislamu ni asilimia 80?

4
Na Omar Msangi A K I C H A N G I A Bungeni mapema wiki hii Mheshimiwa John Chiligati alisema kuwa haitakuwa kumtendea haki Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete iwapo watu watashutumu tu Serikali yake na kufumbia kabisa macho maendeleo makubwa aliyoleta hasa katika sekta ya elimu. Akitumia msemo wa mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, akatoa takwimu kuonyesha jinsi Serikali ilivyopiga hatua katika kupanua elimu ambapo hivi sasa takribani kila mtoto wa shule ya msingi anayefaulu mtihani wa darasa la saba, basi hupata nafasi ya kuingia sekondari. Akifafanua akasema kuwa Mheshimiwa alichukua nchi tukiwa na Sekondari zisizofika 2000, ambapo ni asilimia ndogo sana ya watoto waliokuwa wakimaliza darasa la saba na kufaulu mtihani walikuwa wakipata nafasi ya kuingia sekondari. Kasema hivi sasa kuna jumla ya shule za sekondari zaidi ya 4000. Je, hili utaita ni janga la kitaifa? Alihoji Chiligati. Kama alivyosema Mheshimiwa John Chiligati, changamoto kubwa iliyopo sasa ni kuziboresha shule hizo ikiwa na kuhakikisha kuwa zina walimu, vitabu na vifaa vingine muhimu. Sio kubeza na kuponda juhudi hizo na kupaka picha kuwa hakuna kilichofanyika ila kuharibu. Lakini hata tukiangalia hoja zinazotolewa kuwa kiwango cha elimu kimeshuka, lazima tujiulize, kiwango hicho kimeshuka toka wapi hadi wapi? Lini kilikuwa juu na nini kigezo tunachotumia. Ukiacha lugha za kisiasa, ambayo tumeyarithi kutoka kwa awamu ya kwanza ni kuporomoka kwa viwanda na mashirika ya umma hadi kufa. Akifafanua hali aliyotuachia Mwalimu Nyerere wakati anangatuka Dr. John Sivalon anasema kuwa nchi ilikuwa haina kitu kuanzia chakula, nguo na mahitaji yote muhimu. Anasema, muda mfupi kabla ya Mwalimu Nyerere kuamua kungatuka, hali ya uchumi hapa Tanzania ilididimia sana. Hali hiyo iliitwa hali ngumu ya

Kwa Kikwete imekuwa janga

Makala

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


unaendesha tu udini chuoni hapo. Aliposimama Mbunge Juma Selemani Nkamia aligusia mchango wa Selasini ambapo alionyesha kuwa pengine kinachomsumbua mbunge huyo ni majina ya Prof. Idrisa Kikula na Prof. Shabani Mlacha. Kwamba alichozoea Mbunge huyo ni kusikia akina Peter, John na Nicholus, wakishika nafasi zote za juu katika taasisi za umma. Hii kwamba akina Prof. Idrisa nao wanaweza, hajazoea. Pengine niseme kuwa hili ndio tatizo kubwa la nchi na hili ndio litakalovuruga amani ya nchi hii wala sio haya ya kuchinja au kinachoitwa mihadhara ya kashfa. Alichokizungumzia Mheshimiwa Juma Selemani Nkamia ndio wengine wanakiita Mfumokristo, kwamba umejengeka mtizamo kwamba Wakristo ndio wenye haki ya kuhodhi nafasi zote muhimu za uongozi na utendaji. Akiingia Muislamu anaonekana hafai na atapigwa vita. Viko Vyuo Vikuu vya Umma nchini vipo 19, Dodoma kikiwa kimoja wapo, ambapo wakuu 17 ni Wakristo na Vyuo vitatu tu ndio vyenye wakuu Waislamu. Lakini hutasikia hali hii ikilalamikiwa au hata kama kutafanyika jambo baya katika moja ya vyuo vinavyoongozwa na Wakristo, hutasikia, dini za viongozi hao zikihusishwa na tatizo hilo. Nimewahi kuandika mara kadhaa na narudia tena na sitaona vibaya kurudia siku nyingine, kwamba watoto wengi wa Kiislamu hawakuwa wakipata elimu ya juu sio kuwa walikuwa hawataki au hawana uwezo wa kusoma. Lakini walibaguliwa na kuporwa nafasi zao. Tume na vikao vilivyokuwa vikikaa kuchagua wanafunzi wa kwenda sekondari walikuwa Wakristo watupu na wakati mwingine wenyeviti wakiwa ni mapadiri. Kama alivyowahi kusema Mzee Mwalongo na Almarhum Bori Lilla ambao tuseme pengine kwa bahati mbaya waliwahi kubahatika kuingia katika moja ya majopo hayo, watoto wa Kiislamu waliokuwa wamefaulu vizuri majina yao yaliachwa na nafasi zao kupewa Wakristo waliokuwa na alama za chini. Hali ni hiyo hiyo katika Inaendelea Uk. 5

AN-NUUR

RAIS Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na Jaji Mkuu Chande. uchumi, na kwa kweli ilifanya maisha ya watu kuwa magumu. Bidhaa za kawaida na muhimu zilitoweka kabisa. Vilevile, huduma za lazima zilipotea, isipokuwa kama mtu alikuwa na uwezo wa kuzungumza vizuri. Ili watu wapate dawa ilibidi wapite mlango wa nyuma. Rushwa na hongo vilizidi na mafaili ya kesi na ya maombi ya leseni ya aina mbalimbali yalipotea kiajabu. Mwishowe, manneo haya mnyonge hana haki yalizidi kusikika. Labda tuulize, haya ndiyo mafanikio na maendeleo yanayotarajiwa kupatikana katika nchi yenye elimu bora na wasomi makini? Hivi sasa wanaharakati, vyama vya upinzani na hata wabunge wa Chama tawala, CCM, na wananchi kwa ujumla, wanapiga kelele juu ya mikataba mibovu katika sekta ya madini ambapo nchi inaambulia kwato na mifupa wakati makampuni ya nje yakifaidi maini, steki na nundu (madini). Tunalalamikia pia mikataba kama ile ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ambapo nchi inapoteza mabilioni ya shilingi kila mwaka huku wageni wakifaidi. Tusisahau pia ule ubinafsishaji ambapo wengine wanauita ugenishaji. Pengine tujiulize, elimu iliyotupa wataalamu butu kama hawa waliotuletea madudu mengi kama haya pamoja na yale ya kuagiza wageni kutoka Afrika ya Kusini eti ndio watuendeshee Shirika letu la umeme TANESCO, ndio tunaita elimu bora? Je, hizo zama zilizotufikisha hapo, ndio tunazisifia kuwa zilikuwa zama zilizokuwa na kiwango kizuri cha elimu? Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipokea nchi hii ikiwa haina hata mafuta ya kuanzia kazi akalazimika kuomba mafuta Iran. Aliingia madarakani nchi ikiwa na njaa, watu wakiwa hawana chakula wala nguo za kuvaa. Hizo zilikuwa zama ambapo sabuni ya kuogea na dawa ya mswaki ilikuwa anasa isiyo kubalika. Ukikutwa na kilo mbili za unga wa sembe unakamatwa. Unaulizwa umepata wapi, maana mtindo ulikuwa wa kupewa nusu kilo tu katika duka la kaya na sharti ukapige foleni toka alfajiri, pengine ushinde kutwa mpaka jioni ndio uambulie hiyo nusu kilo! Haukupita muda mrefu, nchi ikajaa neema ya vyakula, nguo na vitu vyote muhimu kwa maisha. Kama alivyojisemea mwenyewe Mzee Mwinyi, watu wakala mpaka wakavimbiwa. Aliyasema hayo Mwinyi baada ya kutukanwa sana akidaiwa kutokufanya lolote la maendeleo katika nchi. Ufupi wa maneno, baada ya watu kushiba, Mzee Mwinyi alipakwa matope na kuonekana hana lolote alilofanya kama ambavyo hivi sasa juhudi zote za kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami hazionekani wala hizi juhudi za kutaka kuhakikisha elimu ya sekondari inakuwa ndiyo elimu ya msingi na kwamba wanaomaliza kidato cha sita wote wanapata nafasi ya kupata elimu ya Chuo Kikuu, haionekani. Kazi ni moja tu: Kuponda, kubeza na kutukana! Siku hiyo hiyo aliyozungumza Mheshimiwa John Chiligati juu ya mafanikio ya Serikali katika kupanua elimu ya sekondari, kabla yake alisimama Mbunge wa Rombo kupitia CHADEMA, Mheshimiwa Joseph Roman Selasini Shao ambapo yeye mada yake kuu ilikuwa suala la udini. Katika jumla ya mazungumzo yake, alishutumu uongozi katika Chuo Kikuu cha Dodoma kwamba hauna maana yoyote kwa kile alichodai kuwa

5
Na Mwandishi Wetu WA Z A N Z I B A R I wametakiwa kupambana na nas zao kwanza kuepukana na maovu, kabla ya kuwalani wanawake wanaovaa hovyo (vimini). Akiongea katika Baraza la Wawakilishi hivi karibuni, Waziri wa Afya, Mheshimiwa Juma Duni Haji amesema kuwa, haioni kuwa tatizo kubwa linalochangia kuongezeka kwa ukimwi ni wasichana wanaovaa vimini; bali Wazanzibari wenyewe kushindwa kupambana na nafsi zao. Alisema, suala la mavazi aina ya vimini sio sababu kuu ya msingi inayochangia kuongezeka kwa maradhi ya ukimwi ila kumekuwa na tatizo kubwa la watu kushindwa kupambana na nafsi zao kuacha kufanya ngono. Katika kukazia hoja yake akasema kuwa, baadhi ya mataifa duniani, wavazi ya vimini ni sehemu ya utamaduni wao, lakini bado wamekuwa na kiwango kidogo cha maradhi hayo kwa vile watu wao wamekuwa wakipambana binafsi na ugonjwa huo. Sababu kubwa na ngumu ni vita vya nafsi, ambavyo viko katika uhuru wa binadamu kwa kutokatana na kufanya vitendo vya ngono na sio vimini peke yake hivi hata wakivaa kama hawafanyi ngono hatapata ukimwi ila tatizo tunashindwa kupambana na nafsi hili ni jambo zito sana. Alisema Waziri huyo. Waziri Duni, amesema kuwa tatizo la kuongezeka kwa maradhi ya ukimwi Zanzibar halitokani na uvaaji wa vimini tu kwa Wanawake bali jamii inashindwa kupambana na vita vya nafsi jambo ambalo linahitaji elimu zaidi kwa umma. Akitoa majibu ya nyongeza ya suali la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma alietaka kujua serikali ina mpango gani wa kurekebisha uvaaji wa nguo zisizostahiki na kupelekea vishawishi vinavyoweza kuongeza ongezeko la mambukizi ya VVU hapa Zanzibar, Waziri Juma Duni Haji alisema kuna mambo makubwa zaidi ya kupigia kelele sio vimini. Akifafanua akasema kiwango cha maambukizi hivi sasa kimeonekana kuongezeka zaidi kwa watu wanaotumia dawa za kulevya ambao hutumia shindano kujidunga ambapo maambukizi yao yapo kwa asilimia 16, huku wanaojiuza miili yao ni kwa asilimia 10.2 na wale

Habari

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


Kwa kuzingatia hilo, Wiraza ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Wizara ya Katiba imeahidi kukaa pamoja kuhakikisha sheria inayokataza watu kuvaa vimini inatekelezwa kwa kuwa tayari sheria hiyo ipo lakini utekelezaji wake ndio bado haujafanyika. Kauli hiyo imetolewa na Waziri Fatma Abduhabib Fereji wakati akijibu suali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma. Mheshimiwa Saleh alitaka kuona Serikali inapiga marufuku uvaaji wa nguo zisizostahiki kama njia moja wapo ya kuzuiya ongezeko la mambukizi ya VVU hapa Zanzibar.

AN-NUUR

Kwa Kikwete imekuwa janga


Inatoka Uk. 4 vyuo vikuu ambapo ushahidi upo kuonyesha jinsi vijana wa Kiislamu waliokuwa wakifanya vizuri walikuwa wakiachwa na kuchukuliwa walio na alama za chini wakibebwa na Ukristo wao kubaki chuoni kama walimu. Sasa pengine ni kutokana

wanafanya vitendo vya kujamiana kwa kuingiliana wanaume kwa wanaume ni asilimia 12.3. Suala la madawa ya kulevya limekuwa ni tatizo kubwa kwa Zanzibar ambapo hivi sasa mtu akipita mtaani, ushahidi wa vijana wengi kutumia madawa hayo, unaonekana wazi. Kwa upande mwingine, masuala la matendo ya kihabithi yaliyosababisha watu wa Kaumu Lut kuangamizwa, yamekuwa yakizungumzwa na watu mitaani na kufanyiwa masihara hata na watu wazima na heshma zao kiasi cha

Pambaneni na nafsi msisingizie vimini


kuonekana kuwa ni jambo la kawaida na pengine zuri. Haya ndiyo mambo Mheshimiwa Juma Duni Haji anataka Wazanzibari wajitizame na kuyashughulikia kabla ya kuwarukia wavaa vimini. Ukiacha hilo, lipo lile la changudoa (wasichana wanaojiuza) ambapo Mheshimiwa Duni anasema kuwa huchangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa ukimwi. Katika eneo hili pamekuwa na mtindo wa kulaumu wasichana kutoka Tanzania Bara kuwa ndio wanaosababisha umalaya

Zanzibar. Hata hivyo, kama alivyosema Mheshimiwa Duni, kinachotakiwa kufanyika ni Wazanzibari wenyewe kujitathmini. Maana kama kusingekuwa na wateja wa kununua biashara ya changudoa hao, bila shaka wasingefurika Zanzibar, kama ni kweli kuwa wanawake wote wanaojiuza wanatoka Bara. Wakati huo huo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema mpango wa kuweka sheria ya kupiga marufuku vimini (viguo vya nusu uchi), unahitaki kuwa na umakini na sio kukurupuka.

na rekodi hii, ambapo Wa k r i s t o w a l i o k u w a katika taasisi za umma waliwabagua Waislamu, ndio akina Selasini wadhani kuwa Muislamu hastahili kuwepo kwa sababu hii sera ya kuwabagua na kuwakwamisha Waislamu itakwama. Mzee Lilla alipohoji mbona majina ya vijana wa Kiislamu waliopata daraja la kwanza na pili hawajapangwa kwenda kidato cha tano, mwenyekiti wa jopo aliyekuwa Padiri alimuuliza, wewe mgeni humu? Mzee Lilla akajibu, Mimi Muislamu. Mwaka jana Baraza la Mitihani Tanzania liliingia katika kashfa kubwa sana. Lilitangaza matokeo yasiyo sahihi ambapo liliwafelisha watoto wa Kiislamu na baadae kulazimika kuyabadili. Lakini wakati huo huo, Baraza hilo linashutumiwa kwa kufanya ubaguzi na upendeleo katika ajira ambapo hivi sasa Baraza hilo linadaiwa kufanya kazi kama Parokia. Wataalamu waliowahi kuingia katika kamati mbalimbali za

kuchunguza Baraza hilo, walipigwa na butwaa kuona jinsi linavyofanya kazi kiholela bila ya kufuata kanuni za kitaalamu za kielimu na mitihani. Moja ikiwa ni katika eneo la kuweka alama za ufaulu na garade range. Lakini maadhali walioshika nafasi zote muhimu katika Baraza h i l o n i Wa k r i s t o , hutasikia wakiguswa wala kashfa zinazowakumba zikizungumzwa au zikihusishwa na dini zao. Tunasema kuwa hii hali ya kudhani kuwa Wakristo ndio wenye haki ya kuongoza nchi hii na taasisi zake muhimu, ndio wengine wanaita Mfumokristo na ndiyo italisambaratisha taifa hili. Na kwa bahati mbaya Serikali yetu inaonekana kulilea na kulipalilia tatizo hili, vinginevyo labda ituambie, ni sababu zipi ni kwa makubaliano gani na Kanisa, na ni kwa sababu gani za msingi ambazo zinaifanya serikali iendelee kujaza Wakristo katika taasisi muhimu wakati Waislamu wenye sifa wapo kuweka uwiano. Mtindo huu wa Serikali ndio umewakisha baadhi ya watu kudhani kuwa wao ndio wenye haki ya kuongoza na kushika madaraka. Wakishika akina Khalfan, hata wakifanya vizuri vipi, yale yao mazuri yataonekana ni janga. Sasa hili ndio Waislamu wanalilalamikia na wasionekane kuwa ni wachochezi.

Wa k a t i n a j i a n d a a kupokea makala hii, nilipokea ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa msomaji mmoja waAn nuur. Ujumbe huo unasema kuwa Machi 13, 1978 zilifanyika sherehe za kusherehekea miaka 25 ya Uaskofu wa Kardinali Rugambwa. Katika sherehe hizo zilizofanyika katika Parishi ya Mwemage, Kata ya Ibwera, Tarafa ya Katerelo, aliyechinja ngmbe 3 alikuwa Marehemu Mzee Mustafa Abdallah, wapishi wakiwa Mzee Zahor Sinani na Mwalimu Said Salum Mutashobya. Hivi kweli ni kuchinja au kuna mkono wa siasa? Alihoji mwandishi na mtuma ujumbe huo. Hoja ya msomaji huyu ni kuwa kama ingekuwa kuna mgogoro kwa upande wa Wakristo kula nyama iliyochinjwa na Muislamu, bila shaka Kadinali Rugambwa asingeruhusu Muislamu kuchinja ngombe wa kuliwa katika sherehe yake. Kwa usomi wake wa Biblia na Ukristo kwa ujumla uliopelekea kupewa Uaskofu na Ukadinali, hatudhani kuwa hakuwa anajua mwongozo wa Kikristo katika kuchinja na kula nyama. Kwa hiyo, ni wazi kuwa kama ni mgogoro, hili ni suala la kutengenezwa na serikali inaweza kulimaliza kama ikitaka. Ni vivyo hivyo suala la mihadhara. Ukiacha wale wanaotukana na

kusema mambo yasiyo katika Biblia, Quran au vitabu vitakatifu, hakuna namna tunaweza kuzuiya Wa i s l a m u k u h u b i r i kuwa Yesu Si Mungu au Wakristo kusema kuwa Yesu Ni Mungu. Kwa hiyo kinachotakiwa hapa, ni kila upande kuheshimu imani ya mwingine. Ila huna namna ya kumfanya mtu anayeamini kuwa anaonewa, akubali kuishi katika hali hiyo ya kubaguliwa na kudhulumiwa maisha yake yote. Atasimama na kupinga. Sasa kama busara itatawala, Serikali na jamii ikachukua hatua za kuona dhulma, tatizo litaondoka. Lakini kwa mtindo huu wa kuwashutumu na kuwatafutia sababu wanaolalamika, mbeleni itakuwa kiza. Lakini tutambue pia kuwa kadiri tunavyochelewa kulitatua tatizo hili, ndivyo wanaofaidika na mfumo huu wanavyopata kiburi na kujiona kuwa wao ndio wenye haki na kila kitu. Matoke yake ni kuwa watakuwa radhi kupambana na wanaotaka kubadili mfumo huu. Ndiyo haya tuliyoyaona Bungeni ambapo mbunge anasimama na kuponda uongozi wa Chuo kwa vile Mkuu na Makamu w a k e n i Wa i s l a m u . Lakini pia ndiyo haya tuliyoyashuhudia ambapo wakati Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea wengine wanamkoromea mpaka akakasirika na kutoa kauli isiyostahiki kutolewa Bungeni.

6
Na Mwandishi Maalum MWEZI Februari 2007, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteuwa Profesa Idris Kikula kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, yaani UDOM na Profesa Shaaban Mlacha kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho kwa upande wa Utawala na Fedha. Aidha Mhe Kikwete alimteuwa Profesa Ludovick Kinabo kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho kwa upande wa Taaluma. Viongozi hawa wakubwa watatu wamekuwa wakifanya kazi chini ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya uteuzi wao, viongozi hao walishughulikia kujenga Chuo cha UDOM ambapo ilipoka mwezi Agosti 2007, wanafunzi wapatao 5,000 walidahiliwa chuoni hapo na masomo yakaanza. Mara tu baada ya chuo kufunguliwa, tuhuma kadhaa zenye hisia kali za kidini zilianza kuelekezwa kwenye uongozi wa Chuo na hasa kwa Profesa Kikula na Profesa Mlacha. Baadhi tu ya shutuhuma hizo ni kuwa Chuo cha UDOM kinafungwa kabisa siku za Ijumaa ili kuwapa nafasi wanafunzi waende kuswali msikitini. Kwa upande wa udahili wa wanafunzi, shutuma kali zimeelekezwa kwa MaProfesa hawa wawili kuwa wanadahili wanafunzi wa Kiislamu tu na kuwanyima Wakristo nafasi ya kusoma hapo chuoni. Shutuma hizo hazikuishia hapo. Wapo watu waliodai kuwa wanafunzi WOTE wa kike wanaosoma Chuoni hapo, bila kujali dini zao, wanalazimishwa kuvaa Hijab, vazi la stara kwa mabinti wa Kiislamu. Tuhumu hizi na nyingine nyingi zimeendelea tokea chuo kianzishwe. Waislamu wamekuwa wakizipuuza tuhuma hizi kwa sababu ni UWONGO MTUPU na walidhani kuwa wanaotoa tuhuma hizi ni watu wasiojua kitu. Jambo la kushangaza na kusitusha sana ni kitendo cha Mhe Joseph Roman Selasini Shao Mbunge wa Rombo (CHADEMA) alipojiunga na kundi hilo na kutoa kauli Bungeni zilizoashiria kuwa UDOM kuna udini kwa maana ya kuwa Waislamu wanawakandamiza Wakristo. Akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri

MAKALA

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


Muislamu 4. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam P r o f . R w e k a z a Mukandala Mkristo 5. Chuo Kikuu cha Sokoine Prof. Gerald C Monela Mkristo 6. Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili Prof. Kaaya Mkristo 7. Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Joseph Kuzilwa Mkristo 8. Chuo Kikuu Huria Prof. Tolly Mbwette Mkristo 9. Chuo Kikuu cha Teknolojia, Mbeya Prof. Joseph Msambichaka Mkristo 10. Chuo Kikuu cha Katavi-Mkristo 11 . C h u o c h a M o s h i MUCCOBS P r o f . Faustine K. Bee Mkristo 12. Chuo cha Elimu DSM (DUCE) Prof. Mfinanga Mkristo 13. Chuo cha Elimu Mkwawa (MUCE)Prof. Amandina Lihamba Mkristo 14. Chuo cha IFM Prof. Godwin Mjema Mkristo 15. Taasisi ya Nelson Mandela Prof. Burton Mwamila Mkristo 16. Taasisi ya Teknolojia DSM (DIT) Prof. Kandoro Mkristo 17. Chuo cha Biashara (CBE)- Prof. Mjema Mkristo 18. Chuo cha Mwalimu Nyerere - D k . M a g o t i Mkristo 19. Chuo cha Uhasibu Arusha P r o f . J o h a n n e s Monyo Mkristo 20. Tume ya Vyuo Vikuu Prof. Sifune Mchome Mkristo Nadhani wengi watakumbuka kuwa mwaka jana wakati Rais Kikwete ameteuwa wajumbe wa Tume ya Katiba, Bwana Edwin Mtei aliandika kwenye jamiiforums kupinga uteuzi ule kwa madai kuwa wajumbe wengi ni Waislamu. Katika kutetea hoja yake, mzee Mtei amedai kuwa katika utendaji wa kazi, si rahisi mtu akaweza kujizuia hisia ya imani (dini) yake isiingilie utendaji wake. Hivyo basi, mzee Mtei alidai kuwa kwa kuwa Tume ya Katiba ina wajumbe wengi Waislamu, itakuwa rahisi kwa imani ya dini hiyo kupenyezwa katika Katiba mpya. Kwa kuzingatia hoja ya mzee Mtei, kama uongozi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu nchini upo katika sura tuliyoionyesha hapo juu, ni dhahiri kuwa si rahisi kwa vijana wa Kiislamu kupata Elimu ya Juu na hasa ukizingatia kuwa Baraza Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR

Nkamia kasema kweli: Waislam Tuzungumze na baba sio mtoto


Mkuu siku ya tarehe 15 Aprili 2013, Mhe. Selasini alitoa shutuma nzito dhidi ya Uongozi wa UDOM kuwa kuna kundi la wanafunzi na waalimu wa Kiislamu wanaofanya vikao vya siri na kupanga njama dhidi ya Wakristo. Kwa mapana yake, kauli ya Mhe. Selasini ina maana ya kuwa ukimya unaoonyeshwa na uongozi wa juu wa UDOM kuhusu suala hili, unathibitisha kuwa uongozi wa Chuo unalijua suala hilo vizuri au unashiriki moja kwa moja katika njama hizo dhidi wa Wakristo hapo chuoni. Kauli hii inawalenga Profesa Idris Kikula na Profesa Shaaban Mlacha kwa sababu wao ndio Waislamu. Shutuma alizozitoa Mhe Selasini ni nzito na hazifai kupuuzwa. Kwa kulijua hilo, Mhe. Juma Selemani Nkamia Mbunge wa Kondoa Kusini alizingatia ushauri wa Wazaramo unaosema kuwa akutukanae kwenye pombe, nawe mjibu kwenye pombe. Akichangia Bajeti hiyo hiyo, siku hiyo hiyo, Mhe. Nkamia alisema kuwa yeye ni mwanafunzi hapo UDOM na hajawahi kusikia ubaguzi ambao Mhe. Selasini anaouzungumzia. Majibu ya Mhe. Nkamia yanazaa maswali kadhaa ambayo ni vyema Waislamu tukajiuliza. Hivi ni kwa nini shutuma nyingi na hasa za udini zimekuwa zikielekezwa kwenye Taasisi kubwa ambazo zinaongozwa na Waislamu? Ni kwa nini Wakristo wamekuwa na tabia ya kuamini na kutaka jamii yote iamini kuwa Muislamu akipewa nafasi ya juu ya uongozi atakuwa amepewa kwa sababu tu ya Uislamu wake na wala si sifa zake? Ni kwa nini akiwepo Muislamu zaidi ya mmoja kwenye uongozi wa juu (kama ilivyo UDOM), Wakristo wanaamini k u w a Wa i s l a m u h a o wamependelewa na kuwepo kwao hapo hawatotenda haki kwa Wakristo? Kwa nini Wakristo wakiwa wengi kwenye uongozi wa juu wa Taasisi yoyote ile wanaamini kuwa hiyo ni haki yao? Ili kupata majibu ya baadhi ya maswali haya, tuangalie Jukwaa ambalo Mhe. Selasini amelitumia kutoa shutuma zake. Jukwaa alilolitumia ni Bunge. Mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, Waheshimiwa Wabunge

MHE Joseph Roman Selasini Shao Mbunge wa Rombo. walifanya uchaguzi kuchagua Mhe Spika, Mhe Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge (Presiding Ofcers) Watatu. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, kati ya Wenyeviti Watatu wa Bunge, mmoja lazima atoke Zanzibar. Matokeo ya uchaguzi huo ni kuwa viongozi WOTE walikuwa Wakristo! Uongozi ulikuwa kama ifuatavyo: Spika Anna Makinda Mkristo, Naibu Spika Job Ndugai, Mkristo, Mwenyekiti Jenister Mhagama Mkristo, Mwenyekiti G e o rg e Simbachawenye (baadae Mhe Zungu) Mkristo, Mwenyekiti Sylvester Massale Mabumba (Dole, Zanzibar) Mkristo. La kushangaza ni kuwa hata pale alipotakiwa Mbunge kutoka Zanzibar ili awe Mwenyekiti wa Bunge, basi nafasi hiyo pia akapewa Mkristo! Ikumbukwe kuwa Mhe Mabumba ndio Mbunge PEKEE kutoka Zanzibar ambaye ni Mkristo! Kwa upande wa Menejimenti, Katibu wa Bunge (Dr. Thomas Kashilila) na Wakuu wa Idara WOTE ni Wakristo! Je, Mhe Joseph Selasini analionaje hili? Pamoja na unyeti wa Taasisi hii, hata mara moja Waislamu hawajalalamika kuwa Bunge linaongozwa na Wakristo watupu. Wao wamekuwa wakiamini kuwa waliochanguliwa wamechaguliwa kwa uwezo

MHE. Juma Selemani Nkamia Mbunge wa Kondoa Kusini. wao (na sio vinginevyo) na kwamba watatekeleza majukumu yao kwa haki na kwa faida ya taifa. Sasa kwa nini mantiki hiyo hiyo haitumiki pale ambapo Waislamu wamechaguliwa au wameteuliwa kuongoza Taasisi yoyote ya Umma? Kwa nini kuwepo na mashaka kuwa wamepata nafasi hizo kwa sababu tu ya dini zao? Kama Mhe Selasini anaona kuwepo kwa Profesa Idris Kikula na Profesa Shaaban Mlacha UDOM ni udini, je ameangalia uongozi wa juu wa Vyuo Vikuu vyote vya Umma hapa nchini? Kwa Mhe Selasini na wale wanaoitakia mema Tanzania, wafahamu kuwa jumla ya Vyuo Vikuu vya Umma na Taasisi za Umma za Elimu ya Juu zinazotoa shahada kwa kiwango cha Digirii hapa nchini ni 19. Ukijumuisha na Tume ya Vyuo Vikuu yaani Tanzania Commission for Universities (TCU) ambaye ndiye Mdhibiti, jumla zinakuwa Taasisi 20. Kati ya Vyuo/Taasisi hizo 20, Wakuu wa Vyuo/Taasisi 17 ni Wakristo na Wakuu 3 tu ndio Waislamu. Kiuwiano hii ni sawa na 85% Wakristo na Waislamu ni 15% tu kama inavyoonekana hapa: 1. Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Idris Kikula Muislamu 2. Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idris Mshoro Muislamu 3. Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dr. Abuu Mvungi

7
Inatoka Uk. 6 la Mitihani limesheheni Wakristo na tokea liundwe halijapata HATA MARA MOJA kuongozwa na Mwislamu. Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kuwa Mhe Rais Kikwete anateuwa Waislamu katika nafasi nyeti za uongozi. Mifano mikubwa ambayo imekuwa ikirudiwa mara kwa mara ni Mkuu wa Polisi Saidi Mwema, Mkurugenzi wa Usalama Othman Rashid, Jaji Mkuu Mohamed Chande na Waziri wa Ulinzi Mhe Shamsi Nahodha. Wakati Wakristo wanalalamikia teuzi hizo mbalimbali ambazo zimezingatia uwezo, ujuzi na uzoefu wa Walioteuliwa, wanasahau kabisa kuwa kwa kipindi kirefu wakati wa utawala wa Awamu ya Tatu Viongozi Waandamizi wa Chama na Serikali walikuwa Wakristo lakini Waislamu hawakuliona kama hilo ni tatizo. Mwaka 1996, mara tu baada ya Serikali ya Awamu ya Tatu ilipoingia madarakani uongozi ulikuwa hivi: Serikali Benjamin William Mkapa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mkristo Fredrick T Sumaye Waziri Mkuu Mkristo Maokola Majogo Waziri wa Ulinzi Mkristo C. Apson Mkurugenzi wa Usalama Mkristo Harun Mahundi Mkuu wa Polisi Mkristo Jenerali Robert Mboma Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mkristo Wakristo wamesahau kuwa katika kipindi hicho Wakuu WOTE wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Waziri wa Ulinzi walikuwa Wakristo WATUPU mpaka baadae alipoteuliwa Omari Mahita. Katika utawala wa Rais Kikwete haijatokea HATA MARA MOJA Wakuu wote wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakawa Waislamu watupu! Aidha ni vyema tukajikumbusha kuwa wakati WOTE wa utawala wa Rais Kikwete Mkuu wa Majeshi amekuwa ni Mkristo. Chama Benjamin William Mkapa Mwenyekiti Mkristo John Samwel Malecela Makamu Mwenyekiti Bara Mkristo Philip Mangula Katibu Mkuu Mkristo Si hivyo tu, Wakristo pamoja na Mhe Selasini wamesahau kuwa katika kipindi CHOTE cha Serikali ya Awamu ya Tatu Mihimili YOTE ya dola ilikuwa inashikwa na Wakristo kama ifuatavyo: Benjamin W Mkapa Rais

Makala

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


kuingiza kontena la majambia nk. Lengo kuu ni kuionyesha jamii kuwa Waislamu ni watu wa shari. Aidha viongozi wa Kiislamu Serikalini wamekuwa wakitupiwa shutuhuma mbalimbali kama ambavyo alivyofanyiwa Profesa Kighoma Malima alipozushiwa uwongo kuwa amejenga msikiti Wizara ya Elimu na mambo mengineyo. La kushangaza ni kuwa wakati haya yote y a n a e n d e l e a , Wa k r i s t o wamekuwa wakifanya vitendo vya kutishia amani waziwazi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yao. Mfano Wakristo wametangaza kuundwa kwa Tume ya Majeshi ya Kivita ya Kikristo (The Commission of Armed Forces). Jambo hili ni la hatari sana na linaacha maswali mengi bila kupata majibu. Je, Tume hii ipo ndani ya Jeshi letu la Ulinzi au nje ya Jeshi? Je, Makamanda wake ni nani na wanaripoti wapi? Je, Amiri Jeshi Mkuu wake ni nani? N.k. Kwenye Gazeti la Mtanzania la tarehe 10 Aprili 2013 kuna mwandishi ameandika makala kuhusu vuguvugu la udini linaloendelea hivi sasa nchini. Kwa mujibu wa jina la mwandishi, inaelekea ni Mkristo. Kubwa katika aliyoyaandika ni kuwa Waislamu wanalalamika hawana uwakilishi wa kutosha kwenye vyombo vya maamuzi na Serikalini. Pamoja ya kuwa huo ndio ukweli, mwandishi anasema kuwa si vyema watu wakapewa dhamana kubwa kwa sababu tu za dini zao na kuwa na haja ya kupata uwiano mzuri wa dini hizi mbili. Kama Waislamu hawapati fursa ya kushika nyadhifa kubwa Serikalini kwa sababu ya upungufu wa sifa na hasa elimu, ni vyema basi Serikali ikaliangalia suala la kuwaendeleza Waislamu kielimu. Pamoja na Ukristo wake, mwandishi amekuwa mkweli na anaona hatari iliyopo mbele yetu ya kuliacha kundi kubwa la raia likiwa nyuma kimaedeleo wakati kundi jingine linapiga hatua. Hawa ndio wazalendo wa kweli na wanaoitakia mema Tanzania ili iwe na amani ya kudumu sio kama Mhe Selasini ambae anaongozwa na jazba na mihemuko. Kwa upande wa Waislamu, nadhani wakati sasa umeka wa kuzungumza na serikali na kuiambia ukweli. Mheshimiwa Juma Selemani Nkamia amekisha ujumbe. Kilichobaki ni wajibu wetu kuufanyia kazi.

AN-NUUR

Nkamia kasema kweli

Dr. Joyce Ndalichako Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani.

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkristo Pius Msekwa Spika wa Bunge Mkristo Francis Nyalali Jaji Mkuu Mkristo Barnabas Samatta Jaji Mkuu Mkristo Aidha hali hiyo hiyo ilijitokeza wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Julius Nyerere wakati yeye alipokuwa Rais, Spika wa Bunge Chifu Erasto Mangenya na Jaji Mkuu Agostino S a i d i / F r a n c i s Nyalali. La kushangaza ni kuwa kila alipokuwa Rais Mkristo, Mihimili yote Mitatu wa Dola imekuwa chini ya Wakristo. Lakini haikuwahi kutokea hata mara moja wakati Rais ni Muislamu (kama ilivyokuwa wakati wa Rais Mwinyi na sasa Rais Kikwete), Mihimili ya Dola kushikwa na Waislamu watupu. Hili halijawahi kutokea hata mara moja! Kwa kuzingatia hoja ya Mhe Selasini na wengine wenye fikra kama zake, uongozi wa UDOM ni mbovu kwani umeshindwa kudhibiti upendeleo na ukandamizaji unaofanywa na Waislamu dhidi ya Wakristo. Swali la kumuuliza Mhe Selasini je, wakati Waislamu walipodhulumiwa waziwazi na Dr. Joyce Ndalichako Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani kwa kufelishwa kwa makusudi kabisa mbona hatukumsikia kusimama Bungeni kuzungumzia dhulma hii? Wakati Getrude Mongella alipokula pesa Dola 200,000 za Bunge la Afrika

na Serikali akakubali kulipa deni lile, mbona Mhe Selasini hakusimama Bungeni kupinga hoja hiyo? Au kwa sababu tu Ndalichako na Mongella ni Wakristo? Wakati Dr. Charles Kimei Mkurugenzi wa Benki ya CRDB anatoa maagizo kwa Mameneja wake wote wa Mikoa kuwa watoe Sadaka Kanisani (fungu la 10) kutokana na faida ambayo Benki imepata, mbona Mhe Selasini hakuhoji Bungeni wizi huu wa sehemu ya fedha za Umma zinazopelekwa Kanisani? Hasa ikizingatiwa kuwa CRDB imesajiliwa kwenye Soko la Mitaji na Hisa. Benki hii ni Kampuni ya Umma (Public Company) ambayo Watanzania wa Dini ZOTE wana Hisa. Au kwa sababu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ni Mkristo na anatoka Moshi kama alivyo Mh Selasini? Unafiki huu wa Mhe Selasini na watu wa aina yake mpaka lini? Mwaka 1992 tumeshuhudia utiaji sahihi wa Makubaliano baina ya Serikali na Makanisa kuhusu Serikali kuwapa fedha Makanisa ili waendeshe huduma za afya katika hospitali zao ambazo zitatumika kwa wananchi pia. Waislamu walilalamikia sana utaratibu ule kwa sababu wajibu wa kutoa huduma ya afya ni wa Serikali. Hivyo basi isingekuwa vyema kwa Serikali kujivua wajibu wake na kuipa Taasisi nyingine. Mantiki ya utaratibu ule ilikuwa ni utaratibu wa muda hadi hapo Serikali itakapopata

uwezo wa kujenga hospitali zake. Cha kushangaza ni kuwa kwa miaka 20 sasa tumeshuhudia namna fedha za Umma zinavyoporwa na kupelekwa Makanisani kwa kisingizio cha kuendesha hospitali teule na kwamba Serikali haina dalili ya kujenga hospitali za Umma. Ikiwa Serikali imeweza kujenga shule za Kata nchi nzima kwa chini ya miaka 2, iweje leo Serikali imeshindwa kujenga zahanati za Kata nchi nzima ili kukomesha uporaji wa mali ya Umma unaofanywa na Makanisa? Kwa kuwa Bunge letu lipo katika kipindi cha kujadili Bajeti ya Serikali tunamwomba Mhe Selasini wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Afya asimame na kuhoji kwa nguvu zote tokea mwaka 1993 hadi leo Serikali imetumia kiasi gani kuhudumia hospitali za Makanisa? Ni kiasi gani zinahitajika kujenga zahanati za Kata nchi nzima? Kwa nini katika kipindi chote cha miaka 20 Serikali haikuona umuhimu wa kujenga hospitali zake na kutimiza wajibu wake kwa raia ambao wanalipa kodi? Iweje Serikali ishindwe kujenga na kuendesha hospitali hali ya kuwa ina vyanzo vingi vya mapato lakini Kanisa liweze kufanya hivyo kwa kutegemea fedha za Serikali na misaada? Ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa hospitali za Umma ili kuachana na utaratibu wa sasa wa kupora fedha za Umma na kupeleka kwenye mahospitali ya Kanisa? HITIMISHO Kwa kuhitimisha tunapenda kumfahamisha Mhe Selasini na wenziwe wenye mawazo kama yake kuwa nchi hii imekuwa na amani kwa muda mrefu kutokana na uvumilivu wa Waislamu. Ni vyema Mhe Selasini akafahamu kuwa amani ya kweli inaenda na HAKI. Amani na haki ni sawa na watoto pacha. Tokea nchi yetu ipate uhuru Waislamu wamefanyiwa madhila makubwa sana na kumekuwa na hila nyingi sana za kuwarudisha nyuma kimaendeleo na pia kuwagombanisha na jamii. Mara kadhaa Waislamu wamekuwa wakihusishwa na vitendo vya uvunjaji wa amani kama vile kusingiziwa

8
Na Omar Msangi TUSIPUUZE kauli ya (Mzee Ali Hassan) Mwinyi (juu ya) kuchinja wanyama. Anasema mwandishi Elizabeth Hombo wa gazeti la Mtanzania katika makala yake iliyochapishwa ukurasa wa 15 wa gazeti hilo toleo la Jumatano, Aprili 17, 2013. Katika makala hiyo, Elizabeth amemsifia Mzee Mwinyi akisema kuwa itakuwa jambo la busara iwapo viongozi wa sasa wa Serikali wanaposhikwa na kigugumizi au kukosa namna ya kutatua matatizo mazito kama haya ya udini, (kwamba) wanapaswa kwenda kuomba ushauri kwa watu wenye busarakama Mzee Mwinyi. Akasema Mzee Mwinyi ameonyesha busara kubwa pale aliposema kuwa haitakiwi kumlazimisha mtu kula nyama iliyochinjwa na mwenziye. Kama unaona aliyochinja mwenzio ni kibudu, basi usile ila chinja yako, kula hata ukitaka kula chura, mjusi, konokono, kula utakacho ruhsa. Hiyo ndiyo kauli ya Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi tunayotakiwa na mwandishi tusiipuuze. Mzee Mwinyi alitoa kauli hiyo hivi karibuni akizungumzia kinachoitwa mgogoro wa kuchinja ambao umesababisha mtu mmoja kuuliwa, watu kujeruhiana na Msikiti kuchomwa moto. Nina imani kwa sasa kupitia tamko hilo la Mwinyi, Wakristo na Waislamu sasa watarudi katika mshikamano kama ulivyokuwa awali na kulinda amani iliyodumu kwa muda mrefu nchini pamoja na ustawi wa Taifa letu. Hii kwamba ni ruhsa Mkristo achinje atakavyo na Muislamu achinje kwa Imani yake, ndiyo itawaunganisha Waislamu na Wakristo na kujenga mshikamano; ndio nauliza: Mwandishi anajua anachokisema? Lakini hili niliache kwanza. Hapana shaka kauli ya Mzee Mwinyi ni ya kujibu na kuunga mkono madai ya Wakristo wanaotaka kuwa nao wawe na haki ya kuchinja na wala isiwe haki ya Waislamu pekee. Na labda niseme kuwa msimamo huu wa Mzee Mwinyi wa kuunga mkono madai ya Wa k r i s t o , k a m a k w e l i ameyatoa kwa dhamira yake ya kutenda haki na sio kwa sababu ya kuwapendezesha/ kuwaogopa, na kuwapendelea Wakristo; basi ruhusa hii isiishie kwenye kuchinja tu. Awasikilize na Waislamu pia. Wakristo wanasema kuwa Jumapili ni siku ya ibada,

Makala
Mzee Mwinyi kasema kweli:

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


atakayekula katika hoteli hizo. Itabidi kila mji na kila mahali kuwe na hoteli na migahawa ya Waislamu (Halal Restaurant). Tunakwenda mbali zaidi, Muislamu akifahamu kuwa ndugu yake/jirani yake Mkristo anakula nyama iliyonunuliwa katika bucha ambayo mchinjaji ni Mkristo, atajua kuwa vyombo vyake vyote vimenajisika. Hatakula wala kunywa kwake na hata kwenda kumtembelea. Swali ni je, hali hii ndiyo itakayoleta umoja na mshikamano kama alivyosema mwandishi Elizabeth? Nimalizie kwa kusema jambo moja. Mzee Mwinyi amesema kuwa wakati akiwa Rais ilipotokea Waislamu wakavunja bucha za nyama ya nguruwe alimaliza mzozo huo kwa kutoa ruhsa kila mtu ale atakacho. Labda niseme kuwa mgogoro katika kadhia ya mabucha ya nguruwe haukuwa Waislamu kuwakataza Wakristo kula nguruwe. Mgogoro ulikuwa Wakristo kuwalisha Waislamu nguruwe na kuwatia najisi ya nguruwe na kila wakilalamika Serikali haichukui hatua hata kwa kufuata sheria zake yenyewe. Tatizo lilikuwa Wakristo kufuga nguruwe ovyo bila kufuata sheria za miji hadi kuacha nguruwe hao kuingia msikitini na kuranda katika nyumba za Waislamu. Tatizo lilikuwa Wakristo kuuza nyama ya nguruwe katika bucha za nyama ya kawaida ambapo inatokea Muislamu kuuziwa nyama hiyo bila ya kujua. Alichofanya Mzee Mwinyi, sio kutatua tatizo. Alichofanya ni kuwaadhibu Waislamu wasio taka kulishwa nguruwe wala nyumba zao kutiwa najisi ya nguruwe. Mwinyi hakuweka mambo sawa kwa kusema anayetaka kula chura na ale. Akina Mbokomu waliacha kuuza nyama ya nguruwe pale Manzese Agentina kwa kuhoa hasira za Waislamu baada ya Waislamu kuvamia bucha yake na kuibomoa baada ya kuona kuwa Serikali inawapuuza. Kama yupo aliyeacha kufuga nguruwe katikati ya maeneo ya Waislamu, aliacha kwa kuhoa hasira za Waislamu. Sio kwa kufuata kauli ya Mwinyi. Wangekuwa wanafuata kauli ya Mwinyi, hadi leo akina Mbokomu wangekuwa bado wanauza nyama ya nguruwe pale Manzese Agentina! Na mtindo huo unaweza kuendelea na kuwa utamaduni wa Waislamu (kuwashughulikia watu wanaowalisha najisi au kuwakwaza kiimani) iwapo Serikali itaendelea kuwapuuza na kwa upande mwingine kuwapendelea na kuwalinda Wakristo. Hii ndiyo hofu yangu kubwa.

AN-NUUR

Waislamu wapumzike Ijumaa, Jumapili kazini

kwa hiyo serikali imefanya Jumapili kuwa siku ya mapumziko. Wasabato nao wakaja juu wakasema, ni haramu kufanya kazi siku ya Sabato, Serikali ikaongeza Jumamosi nayo kuwa siku ya mapumziko. Sasa kama msimamo ni kuwasikiliza watu na kutekeleza madai yao ya kiimani, Waislamu wanasema kuwa ili Ijumaa waweze kujiandaa na kufanya ibada zao vyema na kwa khushui, bila ya wahaka wa kukimbilia kazini, basi Ijumaa iwe siku ya mapumziko kwao. Waislamu watapumzika Ijumaa na kufanya kazi Jumapili. Wakristo nao wapumzike Jumapili, ikika Ijumaa wao waendelee na kazi kama ilivyo sasa. Maana kama hatutaki kuwalazimisha Wakristo kula nyama iliyochinjwa na Muislamu, basi tusiwalazimishe pia Waislamu kupumzika siku ya Wakristo Jumapili. Waislamu wana siku yao Ijumaa. Tunafahamu kuwa nguruwe ni haramu kwa Muislamu na kila kinachotokana na nguruwe. Lakini tunafahamu pia kuwa Serikali hutoa pesa kutoka Hazina ya Taifa inayochangiwa na kodi za Waislamu kununulia madawa na kufanya utafiti juu ya ufugaji wa nguruwe katika Vyuo Vikuu na Vyuo Vya kilimo na Mifugo kama kile cha Sokoine, Morogoro. Sasa kwa mantiki hiyo hiyo ya Mzee Mwinyi, tusiwalazimishe Waislamu kutumia fedha zao kuhudumia mnyama haramu nguruwe.

Kama wapo wanaokula nguruwe, basi wawe na vyuo vyao vya kusomesha wataalamu wao wa ufugaji wa nguruwe ikiwa ni pamoja na kuagiza madawa ya kutibu nguruwe. Serikali isitoe pesa kutoka Wizara husika kufanya kazi hiyo kwa sababu hiyo itakuwa kuwalazimisha Waislamu kutumia pesa zao kumhudumia mnyama ambaye Quran ishasema kuwa nyama yake ni haramu. Lipo pia suala la pombe na riba mambo ambayo ni haramu kwa Waislamu. Kwa kauli hii ya Mzee Mwinyi, basi Serikali itizame namna ambavyo haitawalazimisha Waislamu kunywa pombe au kula riba. Isitumie pesa za taifa kuagiza kondomu wala pombe za kunywewa katika dhifa za kitaifa Ikulu au pesa ya pombe kuingia katika mfuko wa Taifa. Lakini lipo jambo jingine kubwa zaidi. Hivi sasa Waislamu wanalazimishwa kutibiwa chini ya Msalaba na kusikilizishwa kwaya na ibada za Kikristo katika hospitali za mikoa/wilaya na rufaa kwa sababu Serikali imeacha jukumu lake la kutibu wananchi badala yake inachota pesa za Serikali na kulipa Kanisa ndio lifanye kazi hiyo. Swali, ni je, kwa nini Serikali iwalazimishe Waislamu kutibiwa kwa Jina la Yesu? Kwa nini Serikali inakwepa jukumu la kujenga hospitali za Wilaya/Mikoa na za rufaa, badala yake inatumia takribani asilimia

50 ya Bajeti ya Wizara ya Afya kuyapa makanisa ili yawaritadishe Waislamu kupitia matibabu? Hili mbona Mzee wetu Mwinyi halioni? Kama Mzee Alhaj Mwinyi h a t a k i k u o n a Wa k r i s t o wakila nyama iliyochinjwa na Waislamu, kwa nini wakati akiwa Rais aliwalazimisha Waislamu kutibiwa Kwa Jina la Yesu na kuimbiwa kwaya wodini pale aliporuhusu MoU inayochota mabilioni ya kodi za Waislamu na kuyapa Makanisa. Je, hakuona kuwa huku ni sawa na kuwakaanga Waislamu kwa mafuta yao? Nirudi katika ile hoja ya Mwandishi Elizabeth kuwa haya aliyosema Mzee Mwinyi ndiyo yataleta amani na kujenga mshikamano wa Waislamu na Wakristo. Labda tuelewe kuwa wanachopigania Wa k r i s t o , s i o M k r i s t o kuchinja kuku wake au mbuzi nyumbani na kula yeye na familia yake. Wanachotaka ni kuchinja katika machinjio ya umma (public) na nyama ikauzwe buchani kama wanavyofanya Waislamu hivi sasa. Hilo likifanyika ni kuwa machinjio hayo na bucha itakapopelekewa nyama hiyo, zitakuwa najisi kwa Muislamu. Kwa hiyo Waislamu hawatapeleka kuchinja nyama katika machinjio hayo wala kununua nyama katika bucha hizo. Hii maana yake ni kuwa itabidi Waislamu kuwa na machinjio yao na bucha zao. Haitaishia hapo. Kama Wakristo wenye hoteli, migahawa na mama lishe watanunua nyama katika bucha hizi za Wakristo, ni wazi kuwa hakuna Muislamu

9
Na Said Rajab SHAHIDI Omar Mukhtar, Amir wa Mujahidina wa Libya, aliongoza Jihad dhidi ya wavamizi wa Kiitaliano katika miaka ya 1920 - 1930. Omar Mukhtar alikuwa Mwalimu wa Madrasa tu, ambaye amepikwa vyema katika vyungu vya taaluma za Kiislamu. Alikuwa na miaka 70, wakati alipopata jeraha kubwa kwenye mapambano, na akachukuliwa mateka na wavamizi. Leo ningependa kuwaletea kidogo sehemu ya mazungumzo katika Mahakama ya Wavamizi (Waitaliano), kati ya Jaji na Mwanaharakati Omar Mukhtar mwaka 1931, kama yalivyorekodiwa katika DVD inayosimulia mapambano ya Omar Mukhtar, Lions of the Desert (Simba wa Jangwani). Lengo ni kuonyesha na kujifunza msimamo usioyumba wa Kiislamu katika mapambano ya kudai haki: Jaji - Je, Uliipiga vita Dola ya Kiitaliano? Omar: Ndiyo Jaji - Je, Uliwashawishi watu kupambana dhidi ya Italia? Omar: Ndiyo Jaji - Je, Unajua adhabu ya hicho ulichofanya? Omar: Ndiyo Jaji - Kwa miaka mingapi umepigana dhidi ya Italia? Omar: Kwa takriban miaka 20 sasa Jaji - Je, Unajuta kwa

Makala/Tangazo/Habari

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013


kwenda kuishi uhamishoni, iwapo tu angetoa kauli ya maandishi kwa Mujahidina kuacha Jihad. Kisha Omar Mukhtar akasema katika maneno yake mashuhuri: Kidole changu cha Shahada ambacho kila Swala kinakiri kwamba Hakuna Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mjumbe wake hakiwezi kuandika hata neno moja la upotofu. Sisi (Waislamu) hatusalimu amri, tunashinda au tunakufa shahidi! Huyu ndiye mwanaharakati halisi na mpambanaji wa Kiislamu. Hamungunyi maneno katika jambo sahihi. Na yuko tayari kwa lolote katika kupigania haki. Habadili msimamo wake kwa visingizio na vishawishi vya kijinga. Hofu yake kubwa ni kwa Mwenyezi Mungu tu na siyo watawala madhalimu. Wengine wamefungwa kwa dhulma kama tunavyoshuhudia leo, lakini huo ni ushindi kwao. Hakuna walichopoteza. Mwenyezi Mungu mwenyewe anawaeleza vizuri waja wake hawa: Wapo watu miongoni mwa walioamini waliotimiza ahadi waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu: Baadhi yao wamekwishamaliza umri wao (wamekwisha kufa), na baadhi yao wanangoja (siku yao kufika), wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo Qur(33:23)

AN-NUUR

Simba wa Jangwani Shahid Omar Mukhtar

hayo uliyoyafanya? Omar: Hapana Jaji - Unatambua kwamba utanyongwa? Omar: Ndiyo Baada ya kuona msimamo huo madhubuti wa Omar Mukhtar, Jaji yule akasema

kwa mshangao: Jaji - Huo ni mwisho mbaya kwa mtu kama wewe! Baada ya kusikia maneno hayo ya Jaji, Omar Mukhtar alijibu: Omar - Kinyume chake,

hiyo ndiyo njia bora kabisa kumalizia maisha yangu duniani! Jaji yule wa Mahakama ya Wavamizi wa Kiitaliano nchini Libya, alitaka kumuachia huru Omar Mukhtar na kumuondoa nchini Libya

Mahakama yaahirisha hukumu ya Sheikh Ponda


Na Shaaban Rajab

Msaada wa ujenzi wa chekechea Singida vijijini

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, jana iliahirisha kutoa hukumu katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda na

wenzake. Hakimu wa mahakama hiyo aliyefahamika kwa jina la Bw. Katemana, a l i s e m a mahakamani hapo kuwa mahakama imelazimika kuahirisha kusikiliza hukumu hiyo

kwa kuwa hakimu anayeisikiliza kesi hiyo Bi. Victoria Nongwa, bado hajakamilisha kazi ya kuandika hukumu. Hakimu Katema alisema kesi hiyo sasa itatajwa Mei 2 mwaka huu na hukumu kusikilizwa Mei 9.

Waumini wa msikiti wa ISLAMIA MANGIDA wilaya ya Singida vijijini wanaomba msaada ili kufanikisha ujenzi wa Nusery School. Ujenzi wa vyumba viwili na ofisi ya mwalimu unaendelea. Hata hivyo pamoja na jitihada zilizofanywa na Waislamu wa MANGIDA bado kuna upungufu. Ili kufanikisha ujenzi huo tunaomba mchango wa hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ya chekechea hiyo. Yeyote ambaye angependa kuchangia ujenzi huo anaweza kuchangia kupitia Account No. 03120603342 NBC na Mwenyezi Mungu atamlipa. Kwa mawasiliano piga namba 0759 767 742 / 0754 952 008/ 0713 673 216

10
NIMEPOTEZA MDOMO!
Naanza kuwasalimu, kwa salamu ya IMANI Asalam alekhumu, wa Bara na Visiwani Nimekamata kalamu, KUWATANABAISHENI Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Subira jambo ADILI, inadumisha AMANI Itatuweka kwa mbali, na njama zake Shetwani Tupinge tusikubali, kuingia mtegoni Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Ajenda imejicha, wanakusudia nini! Yahitaji kuchekecha, niya yao kubaini Macho ukiyakicha, utayaona ya mbeleni Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Kuzibwa kwangu mdomo, wapo walo furahani Wameibuwa msemo, mchochezi kifungoni Athari zake mfumo, ndiyo hizo tambueni Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Muda wamenitafuta, kuniingiza shimoni Sababu wameipata, sasa nipo hukumuni Kimya kwa miezi sita, sito sikika nchini Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Usiseme BILIKULI, sitorejea hewani Zitupilie kwa mbali, hisia hizo ni duni Kukata ni ujahili, tamaa ni sikizeni Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Mtulie nawaasa, kazini na majumbani Kisa hufata mkasa, ni yao matumaini Kwa hili wakitukosa, watavunjika moyoni Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Kaditama ninafunga, narejea vitabuni Mkutubi si mganga, kutabiri ya mbeleni Bali mimi ni malenga, nayaona ya usoni Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili Isihaka Hemed Mzuzuri Morogoro.

Mashairi/Makala

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013

AN-NUUR

Naanza kwa kulishukuru GAZETI Letu la AN-NUUR kwa kutuwekea ukurasa huu wa kutoa maoni, Mungu atawalipa Inshaalah kwa Kazi kubwa wanayoifanya. Pia nataka kuwasifu Waislamu wa eneo la Mji Mpya hapa Morogoro, kwani wamekua katika hali ya utulivu na kuishi Kiislamu kuliko sehemu nyingine katika mji wetu huu, hivyo inatokana na kuheshimu sana viongozi wetu wa dini na hata Serikali. Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka jana Mji Mpya ilikumbwa na tatizo la mtu kupika nyama kharamu nguruwe. Tatizo hili lilikuwa kubwa mpaka likaleta kufanyika vikao vya hadhara na viongozi wa Serikali likimjumuisha Diwani wa kata hiyo Ngugu Wenslaus Kauogeriz na Mkuu wa Wilaya

Ondoeni kero hii Mji Mpya!!


kipindi hicho Ndugu Said Kalembo. Yote hiyo ilikuja baada ya mwenye Bar hiyo kushindwa kuelewana na Waislamu. Mwishowe Waislamu wa Mji Mpya wakaliacha suala hilo kwa viongozi wa dini na Serikali lakini haijatoka taarifa kamili ya Suluhu ya jambo hilo. Kuna jambo lenye sura kama hilo tena lenyewe lipo Dhahir, kuna nyumba ambazo zinamiliki mifugo lakini wanyama hao wako huru kiasi cha kutishia amani kwa sisi Waislamu wa maeneo haya, tena wanyama hao ni mifugo ya Waislamu wa kata hiyo. Kwa sasa viongozi wetu tunataka kero hii iishe kwa kuonekana. Nyie viongozi wa dini ndio mnaotufundisha kuwa najisi ya nguruwe na mbwa ni moja, Sasa

MUM yakerwa na Fahamu


Ladaiwa kuchonganisha Chuo na Rais Latakiwa kuthibitisha au mahakamani
kuhudhuria. Katika Awamu ya Kwanza ya Urais wake hakuwahi hata kukanyaga chuoni na kila mwaliko aliopelekewa, aliukataa. Rais aliyekataa mialiko ya Chuo Kikuu cha Waislamu ndiye huyo huyo anayekubali na kuhudhuria mialiko anayopelekewa na vyuo vikuu vinavyoendeshwa na upande wa pili wa imani, anahudhuria mahafali yao. Alinukuu Bw. Saad, taarifa sehemu ya taarifa iliyoripotiwa na Gazeti la Fahamu. Bw. Saddy, alisema Chuo kama Taasisi ya Elimu ya Juu, kimesikitishwa na taarifa hizo zenye lengo la kuvuruga uhusiano mzuri baina ya Serikali, hivyo Chuo kimedhamiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti hilo (Fahamu) kwa kuandika taarifa zisizo sahihi dhidi ya chuo hicho. Chuo cha Waislamu Cha Morogoro, kinapenda kuutarifu umma wa Wa t a n z a n i a k u w a kimesikitishwa na taarifa za gazeti la Fahamu la April 9, 2013. Chuo kitalichukulia hatua za kisheria gazeti hilo. Alisema Bw. Saddy. Alisema, katika taarifa hizo, Mhariri/Mwandishi ameonyesha kupata taarifa hizo zinazoelezea

iweje tukalishupalia la nguruwe mpaka ngazi ya juu huku tukijua kuwa kuna nyumba zinafuga mbwa ambao hawana mipaka? Huzurura ovyo. Mbwa hao huingia kwenye magenge mengi yanayouzwa vyakula, nasi tunaona na kunyamazia tuelewe kuwa wenye migahawa hiyo hawajui hatari ya najisi ya mbwa, pia kuwaogopa wafugaji wa mbwa hao ambao hutoka katika nyumba yenye tawi la klabu ya Yanga. Viongozi wadini Mjimpya tunaomba mlifatilie na kuliondoa kero hiyo kwenu Viongozi wa Serikali. Diwani na kamati yako Mpya hata kama si Waislamu lakini kero ya Mbwa mnaijua na hatari yake. Allah Tupe msimamo wa Dini yetu. Msomaji wa gazeti la Annuur. Morogoro.

Na Bakari Mwakangwale

Tangazo la Kazi
MUUGUZI NA OPTOMETRIST WANAHITAJIKA. Muuguzi na Optometrist wanahitajika haraka kuanza kazi katika klinik yetu mpya ya Macho iliyopo Msasani Dar es Salaam. Barua za maombi ya kazi na CV za waombaji zitumwe kupitia. nvmsasani@gmail.com . Maombi ya waliokubaliwa tu ndio zitakazojibiwa. Tafadhali wasiliana nasi, 0757289520, 0713747420 kwa maelezo zaidi. Viwanja Vinauzwa Vimepimwa Kongowe Kibaha Township REGISTERED PLAN NO. 70995 BLOCK H.
Hatua Eneo Mraba Bei (Tsh) 50 x 50 1341 6,705,000 32 x 32 1136 5,680,000 50 x 30 1470 7,350,000 37 x 30 1115 5,575,000 50 x 45 2259 11,295,000 60 x 45 2423 12,115,000 50 x 40 1984 9,920,000 67 x 50 3564 17,820,000 70 x 45 2842 14,210,000 90 x 50 3780 18,900,000 Bei zote ni pamoja na hati miliki Malipo kwa Awamu tatu ( 3) Km. 2 kutoka Barabara ya Morogoro kuelekea Soga Kwa mawasiliano zaidi 0755/ 0715 090754

Plot 1 2 3 4 5 7 8 9 10 11

CHUO Kikuu Cha Waislamu Cha Morogoro, kimesema kitalichukulia hatua za kisheria gazeti la Fahamu, kwa madai ya kuripoti habari zisizo sahihi dhidi ya Chuo hicho. Kwa mujibu wa taarifa ya Asa Habari wa Chuo hicho, Bw. Ally Saddy, amesema katika gazeti hilo toleo la Jumanne April 9 15, 2013, limeripoti habari zenye lengo la kuvuruga uhusiano baina ya Chuo hicho na Serikali. B w. S a d d y, a l i s e m a taarifa hiyo iliyochapishwa katika ukurasa wa nne wa gazeti hilo yenye kicha cha habari Rais Kikwete hakusingiziwa, ndio uhalisi hazina ukweli wowote. Akianisha taarifa hizo Bw. Saad alisema, gazeti hilo limeripoti kuwa tangu kuanzishwa Chuo hicho na tokea, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, awe Rais, ameshaalikwa mara nyingi katika mahafali yao lakini amekataa kuhudhuria. Bw. Saddy, aliendelea kunukuu taarifa ya gazeti hilo zilizodai kunukuliwa kutoka MUM, zikidaia kwamba Rais Kikwete, ndiyo huyo huyo anayekubali mialiko kutoka vyuo vikuu vya upande wa pili wa iman na

baadhi ya mifano (nukuu) inayothibitisha kuwa M h . R a i s D r. J a k a y a Kikwete, analalamikiwa na Waislamu. Baada ya mambo fulani kufanyika yakichangiwa na hali ilivyo sasa nchini ndipo kwa mbinde, Rais Kikwete alikubali kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa majengo ya Kitivyo cha Sayansi Cha Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro, mapema mwezi uliopita, tena baada ya mlolongo mrefu, limenukuliwa gazeti la Fahamu kuhusu taarifa hiyo kuhusu MUM. Asa Uhusianao huyo wa MUM, alisema kuwa Chuo chao hakikuwahi kumualika au kuandika barua yoyote ya mwaliko kwa Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, katika mahafali ya chuo hicho. Kufuatia taarifa hizo, Bw. Saddy, alisema Chuo Kikuu Cha Waislamu Cha Morogoro, kinamtaka Mhariri wa gazeti hilo kuthibitisha taarifa hizo kwa kuonyesha barua za mialiko ya Mahafali ya MUM na kukataliwa na Rais Kikwete. A i d h a , B w. S a d d y, alisema Chuo kinawashauri wahariri wa vyombo vya habari kutafuta na kupata vyanzo halisi vya habari ili kuhakikisha wanaripoti taarifa zilizo sahihi.

UONGOZI BORA - HADITHI YA MUSA NA HARUN


Na Said Rajab.
NENDA kwa Firauni. Bila shaka yeye amepindukia mipaka. (Musa) Akasema: Ewe Mola wangu! Nipanulie (nikunjulie) kifua changu. Na Unifanyie sahali kazi yangu (hii uliyonipa). Na Ufungue fundo lililo katika ulimi wangu. Wapate kufahamu maneno yangu (nitakayowaambia). Na Unifanyie waziri, (msaidizi) katika jamaa zangu-, Ndugu yangu Harun (mfanye awe ndiye waziri wangu). Na umshirikishe katika kazi yangu hii. Ili tukutukuze sana. Na tukutaje kwa wingi. Hakika wewe Unatuona. (Mungu) Akasema: Hakika umepewa maombi yako, ewe Musa! Qur(20:24-36) Quran inahusisha hadithi ya Mitume Musa (AS) na Harun (AS) katika Surah mbalimbali, ikiwemo Surah Ta Ha kuanzia Aya ya 24 mpaka 36. Katika kila tukio, hadithi inabainisha kipengele kimoja au zaidi kuhusu majukumu na vitendo vyao, kulingana na ujumbe unaotakiwa kutolewa na Quran katika eneo husika. Tukileta pamoja elimu hii ya ufunuo kuhusu Mitume hawa wawili, tutagundua hadithi kamili ikiwemo misingi ya Mawasiliano, Kufanyakazi pamoja na Kukasimu madaraka - vyote vikiwa ni vipengele muhimu vya uongozi bora. Amri kwa Mtume Musa AS:Katika Surah Ta Ha, Mwenyezi Mungu anamuamrisha Musa (AS) kumkabili Firauni, mfalme jeuri, mkandamizaji na mwenye nguvu wakati ule, akisema: Nenda kwa Firauni. Bila shaka yeye amepindukia mipaka Qur(20:24). Katika hatua hii, amri ya Mwenyezi Mungu imeelekezwa kwa Musa (AS) peke yake kama Musa. Naye ameitambua hii kuwa ni changamoto kubwa na kazi ngumu kuikamalisha. Majibu yake kwa kazi hii yanatoa mafunzo mengi ya uongozi. Haya yanaweka misingi ya nadharia muhimu kabisa za uongozi, hususan katika vipengele vya kufanyakazi pamoja (teamwork) na ushirikiano (cooperation). Mafunzo ya uongozi katika majibu ya Mussa (AS):- Kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu katika kutimiza amri ya Mwenyezi Mungu. Musa (AS) kwanza anaomba msaada wa Mwenyezi Mungu aimarishe uwezo wake na kumuewezesha kufanikiwa katika kazi aliyopewa. Maombi yake ya msaada yanawakilisha sifa ya kiongozi Muislamu,unyenyekevu na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa kila jambo. Musa Akasema: Ewe Mola wangu! Nipanulie (nikunjulie) kifua changu; Na unifanyie sahali kazi yangu Qur(20:2526). Kupitia Aya hii tunaona kwamba Musa (AS) kama kiongozi alitambua mapungufu yake. Kwanza alifanya uchambuzi wa stadi zinazohitajika kwa kazi aliyopewa, halafu akafanya tathmini ya stadi (skills) zake yeye mwenyewe na kutambua mapungufu yake. Hapa nabii Musa (AS) anatufundisha kwamba ili kazi (mission) ifanikiwe ni muhimu sana kufahamu stadi gani zinahitajika, ikiwa ni pamoja na kutambua uwezo na udhaifu wa kila mtu, katika muktadha wa kile kinachohitajika. Viongozi wanaojiamini hawaoni aibu kukabili mapungufu yao. Kwa haraka sana, Musa (AS) anatambua kwamba stadi zake za Mawasiliano (Communication Skills) hazikuwa nzuri sana. Anamuomba Mwenyezi Mungu amuondolee ugumu alionao katika kuzungumza kwa ufasaha. Katika maombi yake kwa Mwenyezi Mungu, Musa (AS) anaonyesha mtazamo halisia na uwezo wake wa kuona matatizo kwa mbali. Akizongwa na matatizo na mapungufu kadhaa kichwani, anapendekeza ufumbuzi - kuunda timu ya kufanya ile kazi, na mtu ambaye ataongezea kwenye stadi za kiongozi. Kuzingatia Mawasiliano Makini:- Musa (AS) alimuomba Mwenyezi Mungu amuondolee fundo katika ulimi wake kwa sababu ambayo ndiyo msingi mkuu wa Mawasiliano. Sababu yenyewe ni hii: Wapate kufahamu maneno yangu (nitakayowaambia) Qur(20:28). Hakuomba kuondolewa fundo katika ulimi, ili aweze kuzungumza vizuri au kwa kuvutia zaidi. Badala yake, alimuomba Mwenyezi Mungu amuondolee fundo katika ulimi, ili wale watakaomsikiliza waweze kumuelewa. Na huu ndiyo msingi wa Mawasiliano, kwamba mpokeaji wa ujumbe lazima aelewe ujumbe uliotolewa, kama unavyotakiwa kueleweka. Mawasiliano yanatokea, si pale mtumaji anapotuma ujumbe, bali pale mpokeaji wa ujumbe anapoupa maana ujumbe huo. Kupata matokeo mazuri ya Mawasiliano, hatupaswi kuzingatia sana uwezo wa mzungumzaji au muwasilishaji, bali tuzingatie zaidi tafsiri n a u f a h a mu w a ml e n g w a wa ujumbe huo. Tuelekeze mazingatio katika uwezo wa mtu kuwasilisha ujumbe anaotaka kuutoa, na walengwa wakafahamu wazi ujumbe huo kama ulivyokusudiwa. Kanuni hii inaweza kutumika hata katika nyanja nyingine za shughuli za binadamu. Kazi yoyote isipimwe kuwa imefanyika vizuri kiasi gani, bali kwa kiasi gani kazi hiyo imewanufaisha walengwa. Kwa maneno mengine, shughuli zetu zote lazima zilete matokeo (results oriented), na bila shaka matokeo hayo lazima yawe yenye manufaa. Pia tuzingatie tabia ya hadhira tunayoipelekea ujumbe. Mwenyezi Mungu amemuamrisha Musa (AS) kwenda kwa Firauni kwa sababu amepindukia mipaka, lakini wakati huo huo ameonyesha njia maalumu ya kumkishia ujumbe mtawala huyu: Kamwambieni maneno laini huenda atashika mawaidha au ataogopa. Qur(20:44). Funzo linalopatikana hapa ni kwamba maudhui ya Mawasiliano yetu, na njia inayotumika kuwasiliana, lazima vimfae mpokeaji wa ujumbe huo. Zaidi, wakati mwingine njia sahihi ya kumkabili mpokeaji mkali na mkorofi wa ujumbe, siyo kuleta ukali na ubabe, bali kinyume chake. Zungumzeni naye kwa upole kama ilivyoanishwa kwenye Aya. Msingi wa Mawasiliano hasa ni kukisha ujumbe tu na siyo kulipa visasi. Kufanyakazi pamoja kama timu: Nabii Musa (AS) pia alifahamu haja ya kufanyakazi pamoja. Alitambua kwamba alihitaji msaada wa kujazia kwenye uwezo alionao ili aweze kufanikiwa: Na Unifanyie waziri, (msaidizi) katika jamaa zangu. Ndugu yangu Haruni (mfanye awe ndiye waziri wangu) Qur(20:29-30). Viongozi ambao hawajiamini mara nyingi huwachukua wasaidizi walio na sifa za chini kuliko wao, ili kukwepa kupewa changamoto katika maeneo ya udhaifu wao. Lakini viongozi makini, hujiamini na kuelekeza juhudi zao katika kukamilisha kazi waliyopewa. Kwa hiyo wanatafuta watu makini na wenye uwezo wa kuwasaidia katika maeneo ambayo wana udhaifu au upungufu. Musa (AS) alimuomba mtu ambaye alijua ana uwezo, ndugu yake Harun, kwa sababu ambayo tutaijadili baadaye. Nabii Musa (AS) alimtaka ndugu yake Harun kama mshirika, ili kuimarisha zaidi uwezo wake na juhudi zake, ikiwa ni pamoja na kujazia katika stadi zake. Nitie nguvu kwa (ndugu yangu) huyu Qur(20:31). Ili timu ifanye kazi vizuri, Musa (AS) alitarajia mshirika wake kushiriki kikamilifu

11

Makala

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013

AN-NUUR

Mwenyezi Mungu ampe Harun ili amsaidie: Na ndugu yangu Harun ni fasaha zaidi kuliko mimi kwa usemi, basi mtume pamoja nami awe msaidizi, kunisadikisha; hakika mimi naogopa ya kwamba watanikadhibisha Qur(28:34). Timu makini ya uongozi inajumuisha watendaji ambao stadi zao zinaongezea zile za kiongozi, pamoja na za watendaji wengine kwenye timu. Kama tulivyoona awali, Nabii Musa (AS) aliogopa kwamba ufasaha wake wa kuzungumza unaweza usitosheleze mahitaji ya kazi iliyopo; kwa hiyo alimuomba mtu ambaye alidhani ni mzuri zaidi katika eneo hilo. Hii ni alama ya kiongozi bora. Nabii Musa (AS) ameonyesha kwamba lengo l a kuunda timu halikuwa
kupunguza mzigo wa kazi, isipokuwa kupata msaada na nguvu kutoka kwa kila mmoja. Timu hiyo inaelekezwa katika lengo maalumu ili kukabili changamoto fulani, ambayo katika hadithi hii ya Musa, kulikuwa na hatari ya kutuhumiwa kwa kusambaza uongo.

katika kutekeleza kazi na wala siyo kuwa mtazamaji. Na umshirikishe katika kazi yangu hii Qur(20:32). Quran Tukufu inatubainishia moja ya sababu zilizomfanya Nabii Musa (AS) amuombe

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency

Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu. Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika osi zifuatazo:1. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444. 2. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 453838 4. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 444 5. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 786101 6. Dukani kwa Abdala Hadh Mazrui wete pemba 0777 482 665 7. Dukani kwa Mohamed Hadh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456911 8. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 679692 9. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Wahi kulipia. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia ACCOUNT NAMBA 048101000030 NBC Tanbih: Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu. Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu. Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo. Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo. Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi. Nyote mnakaribishwa

AN-NUUR
12
Na Shaaban Rajab RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ametakiwa kubeba mwenyewe jukumu la kuzungumza na viongozi wa dini nchini katika jitihada za kutanzua hali ya uhasama inayolinyemelea Taifa, badala ya kutumia wawakilishi au kukasimu kazi hiyo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwa kuwa suala hilo ni kubwa na linahusu uhai wa Taifa. Aidha serikali imeshutumiwa kuwa imekuwa na udhaifu mkubwa katika kutanzua mizozo ya kidini na kuipatia ufumbuzi wa kudumu nchini kila inapotokea, jambo ambalo limeongeza ufa wa mahusiano kati ya jamii ya Waislamu na Wakristo. Akizungumza na Annuur osini kwake jijini Dar es Salaam katikati ya wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Shirika la Kutoa Elimu kwa raia juu ya Haki za Binadamu, Mazingira, Sera za Taifa na Utawala Bora (MAGEA) Bw. Shaweji Salinyambo, amesema kwamba kwa jinsi hali ilivyo sasa, Rais Kikwete hakupaswa kutuma mwakilishi katika kutafuta suluhu ya tatizo lililopo, bali alitawakiwa kujifunza kwa Rais mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwingi, ambaye enzi ya uongozi wake, aliamua mwenyewe kuchukua dhima ya kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa dini zote mbili na kuzungumza nao juu ya tofauti zilizojitokeza kati ya pande mbili hizo. Mwezi Machi 14, 1993 Mzee Mwinyi aliitisha kikao na kukutana ana kwa ana baina ya Maaskofu na Masheikh kilichofanyika Ikulu, kufuatia malalamiko yaliyotolewa na Maaskofu kuwa wahubiri wa Kiislamu walikuwa wakiukashifu Ukristo katika mahubiri yao. Mkutano huo ulikuja kufuatia tishio lilotolewa na Maaskofu la kumwaga damu, huku upande wa Masheikh nao ukijibu kuwa jaribio lolote la kumwaga damu za Waislamu litajibiwa. Mtafaruku huo ulikuja baada ya Maaskofu kudai k u w a Wa h a d h i r i w a

JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 19 - 25, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa


ya Waislamu. Hivyo alishauri kuwa kama serikali inataka kupata suluhu ya matatizo ya kiimani kwa Wakristo na Waislamu, basi pale inapolazimika kuwakutanisha Maaskofu na Masheikh, ihakikishe kuwa kwa upande wa Masheikh au viongozi wa Kiislamu wawe ni wale wanaokubalika na kuaminiwa na umma wa Kiislamu nchini tofauti na wanavyofanya sasa. B w. S a l i n y a m b o alibainisha udhaifu mwingine wa serikali katika kutatua mizozo ya kidini nchini, kuwa ni mazoea ya kuingilia migogoro inayotokea katika dini moja hususan ya Kiislamu, lakini ikisita kufanya hivyo kwa katika migogoro ya Wakristo. Alitoa mfano wa mzozo wa Dayosisi ya Pare mkoani Kilimanjaro, mzozo wa madhehebu ya Katoliki kati ya Kanisa hilo na Padri Mkwera. Chanzo cha mzozo huo ni kwamba Dayosisi ya Pare inajumuisha Wilaya za Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro. Kabla ya hapo, ilikuweo Wi l a y a M o j a y a S a m e ambayo iligawanywa mwaka 1976 na kuanzishwa wilaya ya Mwanga, na kulikuwa na Dayosisi ya Pare tu. Lakini baadae likatokea kundi linalotaka kuundwa Dayosisi ya Mwanga na kuzua vurugu kiasi cha watu kuuana. Hata hivyo serikali haikuingilia kati mzozo huo ambao kwa sasa umepoa. Aidha kwa upande wa sakata la Padri Mkwera na Kanisa Katoliki, serikali haikuonekana kuingilia mzozo huo wa kiimani hadi ulipomalizwa na wenyewe. L a k i n i Wa i s l a m u wanapoilalamikia Bakwata kuwa haina maslahi na Waislamu na kutaka kufanya mabadiliko, serikali ilitumia kila iwezalo kuilinda, hata ikibidi kutumia vyombo vya dola na kuwadhibiti wale wanaoonekana kuhatarisha uhai wake. Alisema udhaifu huu umechangia kwa sehemu kubwa kuendelea kwa mizozo isiyokoma ya kidini nchini.

Kikwete atakiwa kubeba msalaba wake mwenyewe

RAIS Jakaya Kikwete. Kiislamu walikuwa wakitoa mihadhara ya kuukashifu Ukristo kwamba Nabii Issa (as) yaani Yesu si Mungu na hakuzaa wala hakuzaliwa kwa mujibu wa mafundisho ya Quran. Tishio la Maaskofu na jibu la Masheikh liliiweka nchi katika hali ya wasiwasi. Vyombo vya usalama viliona hatari inayolikabili Taifa kutokanana vita hivyo vya maneno hivyo serikali iliamua kuzikutanisha pande mbili zinahosuka na vilelelezo vyao. Kufuatia agizo hilo la serikali, viongozi wa Kiislamu walikutana na kupendekeza majina ya viongozi walioonekana wanaweza kusimamia kupatikana ufumbuzi wa tatizo lililojitokeza. Baada ya mashauriano walipatikana wawakilishi wa Waislamu ambao walikuwa Sheikh Muhammad Ali AlBukhry, ambaye alikuwa kiongozi wa ujumbe wa Waislamu kwa Rais. Wengine walikuwa ni Sheikh Abubakar Juma Mwilima, Sheikh Aboud Mahmoud Maalim, Sheikh Kassim bin Juma, Sheikh Suleiman Kilemile, Sheikh Othman Matata, Ust. Shaaban Magezi, Ust. Habib Mazinge, Alhaj Said Ricco, Dk. Khamis Saleh na Ust. Suleiman Ngoy. Kwa upande wa viongozi wakuu wa Makanisa alikuwemo Askofu John Ramadhan, Aman Mwenegoha ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Makanisa ya KKKT. Katika kikao hicho kila upande ulitoa maelezo yake hadi ukweli ukapatikana. Hata hivyo tangu amalize muda wake Rais Mwinyi, serikali imekuwa ikishindwa kutumia utaratibu huo kutatua tafaruku za kiimani na badala yake, nguvu za dola zimechukua nafasi katika kutatua mizozo ya kidini nchini, hali ambayo imezidi kuongeza ufa wa mifarakano. Aidha alisema serikali imekosolewa kuwa imekuwa ikikosea kutatua mizozo ya kiimani kwa kutofanya mashauriano na viongozi muafaka wa kidini. K w a m f a n o , B w. Salinyambo anasema kuwa kwa upande wa jamii ya Kiislamu, mara kadhaa serikali imekuwa ikiwatumia viongozi wa taasisi moja ya Bakwata kuwakilisha umma wote wa Kiislamu katika harakati za kutafuta suluhu za kidini. Alisema mara nyingi viongozi wa taasisi hiyo wamekuwa wakikosa utii na uaminifu kwa sehemu kuwa ya Waislamu nchini kwa kuwa viongozi wake wamekuwa wakitetea zaidi maslahi ya serikali na viongozi wake kuliko yale

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like