Welcome to Scribd. Sign in or start your free trial to enjoy unlimited e-books, audiobooks & documents.Find out more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
3Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1068

ANNUUR 1068

Ratings: (0)|Views: 4,243|Likes:
Published by MZALENDO.NET
ANNUUR 1068
ANNUUR 1068

More info:

Published by: MZALENDO.NET on Apr 28, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

10/22/2014

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1068
JAMADUL THAN
1434, IJUMAA -APRILI 26 - MEI 2, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
www.annuurpapers.co.tz
Mtume(saw) ameagiza, “Fanyeniharaka kwenda kuhiji”. Hii maanayake tunahimizwa tuende kuhijji tungalivijana ili tuyafaidi manufaa ya Hijjakikamilifu. Baada ya kupata uwezo,nimakosa kuakhirisha kwenda kuhiji.Masahaba, vijana na wazee, walihijjiHijja nyingi sana. Wewe jee? Karibu Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharamazote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliananasi ifuatavyo: Tanzania Bara:0717224437; 0777462022;Unguja:0777458075;Pemba: 0776357117.
Familia ya Sheikh Ponda
katika wasiwasi mkubwa
Watakiwa kutoa damu, mateNdege yaandaliwa kuwaleta Dar Wasema labda afufuliwe Mzee Issa
Wafungwa 8 wasilimishwa
Ni kazi ya wafungwa wa maandamanoWaislam watakiwa kusaidia familia zao
Unapokuwa Sheikh huna hakiPolisi wajue nao hawapo salamaSi lazima waige ya Pennsylvania Avenue
 Vita dhidi ya Uislamu yapamba moto
Uk. 3
Mwanasheria Mkuu Z’barapasua jipu la Muungano
 Afananisha kero na mtu mwenye ukurutu Akitibiwa pele kumi bado ni mgonjwa sana Asema maridhiano yamekuwa kama togwa Ahimiza ushiriki mchakato wa Katiba Mpya
 MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman
 SHEIKH Issa Ponda SHEIKH Farid Hadd 
Uk. 6
(12) KIJANA, UMESHAHIJI?
 
2
 AN-NUUR
JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 26 - MEI 2, 2013
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
Tahariri/Habari
Mwanasheria Mkuu Z’barapasua jipu la Muungano
MWANASHERIA Mkuu waZanzibar Othman MasoudOthman amesema kuwa mudawa kuwa Muungano utaendeleakuwa wa Serikali mbili,hakuna namna ya kumalizakero zake.
Amesema, chini ya Muunganowa Serikali mbili nchi mojahupoteza Dola na utaifa wake,hiyo ikiwa dosari kubwa sanaambayo lazima izae matatizomengine yasiyotibika.Amesema, ndio maana kila juhudi zikifanyika kuweka vikaona mikakati ya kuondoa kero zaMuungano, haziishi.“Juhudi kadhaa zimefanywakutatua baadhi ya matatizo…lakini ukweli unabaki kuwamwenye ukurutu akitibiwa pele 10 bado ni mgonjwa; tenamgonjwa sana.”Mwanasheria Mkuu Othmanalikuwa akitoa mada ya awalikatika ufunguzi wa kongamanolililoandaliwa na Chama chaWanasheria Zanzibar (Zanzibar Law Society) ikiwa ni moja yakukumbuka na kusherehekeamiaka 49 ya Muungano.Katika kongamano hilolililohudhuriwa na wanachamawa ZLS, Mawakili, Wanasheriana waalikwa wengine,Mwanasheria Mkuu alitumiafursa hiyo kuwakumbushaWanasheria wa “Zanzibar kutimiza wajibu wao kwa jamiikatika mchakato unaoendelea wakuandaa Katiba mpva va Jamhuriva Muungano.”Alisema, anawakumbushawajibu huo kwa sababu mchangona ushiriki wa wanasheria katikahatua zilizopita “ulikuwa hafifuna hauonekani kuimarika hatakatika hatua va sasa.”Kwa upande mwingineamesema kuwa itikadi (zachuki na mifarakano), zinazuiyaushiriki mzuri wa Wazanzibarikatika mchakato wa kuandaaKatiba mpya jambo ambalolitawazuiya kutumia fursa hiyokuondoa matatizo yaliyo katikamuungano.Mwanasheria Mkuuamesisitiza kuwa pamoja na juhudi kubwa iliyochukuliwakuwapatanisha Wazanzibari,lakini itikadi za chuki badozimekuwa kikwazo.“Itikadi yetu ya Zanzibar; miminaifananisha na Togwa. Maanakatika kutengeneza Togwa, juhudi kubwa imechukuliwakuupatanisha mtama na majiuwe kitu kimoja kama vile ilivvokatika uji, lakini imeshindikana.Baada va juhudi vote hivo, Togwalikiwekwa katika chupa, badomtama na maji vinajitenga; maji juu, mtama chini.”Ameyasema hayoakitahadharisha kuwa mivutanoya kiitikadi badala ya kuangaliamasilahi ya nchi na wananchi,
Na Mwandishi Wetu
ilisababisha wasomi na watuweledi kutotoa maoni ya maanawakati wananchi walipotakiwakutoa maoni yao.Akasema, “Katiba mpyalazima iepuke makosa ya sasahivi (katika muungano)”Akaongeza kuwa wajibuwa Wazanzibari hivi sasa nikubainisha misingi inayotakiwakwa muungano kusimama juuyake.Akaitaja baadhi ya misingi hiyokuwa ni pamoja na “Kutambuakuwepo na kuendelea kuwepokwa Washirika wa Muungano.”Kwa maana kuwa kuwe naSerikali ya Zanzibar na ile yaTanganyika ndipo wawili haowakubaliane katika Muungano.Aliutaja msingi mwinginekuwa ni “Kulinda usawa waWashirika wa Muungano katikakuamua, kusimamia na kuendeshamasuala yote ya Muungano.”Huku akisema kuwa ni lazimakatika Muungano huo kuwe nautoaji “fursa sawa na za kutoshakwa Washirika wa Muunganokuendesha Mambo yasiyo yaMuungano kitaifa na kimataifa;na kwamba kuwe na mambomachache na yaliyo bayana yaMuungano.”Awali Mwanasheria Mkuualibainisha matatizo makubwa yaMuungano katika mfumo wa sasaambapo alisema kuwa badalaya matatizo hayo kutatuliwayamepewa hadhi na kuitwa ‘Keroza Muungano’.Amezitaja baadhi ya kasoroza msingi za Muungano kuwani “Misingi ya Muunganokutokuwekwa bayana.”Kwamba washirika waMuungano watambuliwe nahadhi zao kuwekwa bayana.Kasoro nvengine va Msingialiyoitaja “ni kukosekana usawakatika maamuzi vanavohusumambo va Muungano.”“Msingi huu ni mpana.Miongoni mwa mambo muhimuchini ya msingi huu ni kwaWashirika wa Muunganokuwa na usawa katika kufanvamaamuzi ya Muungano. Chinimfumo wa sasa msingi huuhaupo kabisa. Kwa mfano katikauchaguzi wa Rais wa Muungano,upande mmoja tu ndio ambaounaweza kuamua nani awe Raiswa Muungano.”Akasema, kasoro nvenginekubwa ni “kukosekana usawakatika usimamizi wa mambo vaMuungano na katika kuamua serana Sheria za Muungano. Aidha,kwa mfumo wa sasa hakunausawa katika kupanga na kutumiarasilimali za Muungano.”Akiendelea kutaja nakufafanua matatizo ya msingialiyodai kuwa yamepewa hadhikwa kuitwa kero za Muunganoamesema kuwa kero nyingineni “kukosekana uwazi na usawakatika matumizi ya rasilimali zaMuungano.“Rasilimali inajumuishamamlaka va Jamhuri yaMuungano katika mahusianona nchi nvengine au Jumuiya zakimataifa.”Akihitimisha akasemakuwa katika kero kubwainayoteteresha Muungano ni“kutokuwepo ukomo wa mipakaya Muungano.”Akifafanua akasema“Muungano wowote lazimauweke bayana mambo yapihayatoweza kuwa ya Muunganoama kuwa kwake ya Muunganolazima wananchi waamue.”Lakini chini ya “Mfumowa sasa wa Muungano lolotelinaweza kufanywa kuwa laMuungano ilimradi tu theluthimbili za Wabunge wa kila upandewaridhie.”Hili akaliunganisha na lile lakuwa na Muungano wa Serikalimbili.“Kasoro nyengine kubwa yamsingi kabisa ni mfumo wa sasaSerikali mbili.”Katika kulifafanua hiloakasema kuwa wapo watu“wanadhani kuwa mfumo wasasa wa Serikali mbili unawezakufanyiwa marekebisho nakuendelea kutumika.”“Ni imani yangu kuwa mfumohuo una kasoro moja kubwaambayo haiwezi kurekebishwana ndio kiini cha kasoro yake.(kwamba) Mfumo wa Serikalimbili unalazimisha tu mmojakati ya Washirika wa Muunganoapoteze hadhi yake ya utaifa(sovereignty) na kuwa sehemuya Mshirika mwengine (politicalsubdivision).”Hayo ndiyo masaibuyaliyoikumba Zanzibar ambapohivi leo haina Dola wala utaifa.Wakati huo huo, baadhi yawashiriki katika kongamano hilowameitupia lawama Serikali kwakuhusika katika kukwamishautoaji huru wa mawazo yawananchi katika mchakato wakupatikana Katiba mpya.Ilielezwa katika kongamanohilo kuwa baadhi ya Mashehana Wakuu wa Wilaya walihusikakukwamisha mikutano yawananchi ya kutoa maoni.Hata hivyo baadhi ya washirikiwakasema kuwa haiwezekaniMasheha wakawa na ujasiri huokama Serikali haihusiki.Mmoja katika waliotoa maonihayo alikuwa Profesa Shariff ambaye alihoji inakuaje Shehakukwamisha jambo kubwa kamahilo na Serikali isitoe kauli.(Soma hotuba kamili uk.4
HUDUMA ya maji safina salama kwa wananchi,imekuwa kilio kikubwa chawabunge katika vikao vyamkutano wa kumi na moja waBunge la Bajeti vinavyoendeleamjini Dodoma.
Malalamiko ya wabungekuhusu suala la huduma yamaji sehemu mbalimbali nchini,yamekolezwa na makadirioya bajeti ya Wizara ya Maji2013/14 yaliyowasilishwamapema wiki hii na Waziriwa Wizara hiyo Prof. JumanneMaghembe.Wengi walisema kuwa bajetiiliyotengwa na serikali kwaajili ya matumizi na shughuliza Wizara hiyo ni ndogo,ikilinganishwa na umuhimu namahitaji makubwa ya hudumayenyewe.Sote tunafahamu kwambamaji ni uhai. Maji ni maadaambayo inahitajika kwa kila jambo au shughuli inayofanywana mwanadamu katika maishayake ya kila siku.Maji ni huduma muhimuzaidi na inayohitajika zaidikatika kuendesha maisha yamwanadamu kuliko miundombinu mingine yetote.Kutokana na kutokidhi bajetiya maji,wabunge safari hiiwametambua umuhimu wa majina kuamua kuyapa kipaumbelezaidi. Tayari Bunge limeitakaserikali kuongeza fedha katika bajeti ya maji, angalau kupanuahuduma hiyo iwafikie wengizaidi. Hili tunaona kuwa ni jambo zuri.Hata hivyo tunadhani kwambaserikali yenyewe ndio imekuwachanzo cha kukosekana hudumahii muhimu, kwa kushindwakutambua kuwa huduma ya majiinastahili kupewa kipaumbelezaidi kutokana na umuhimuwake uhai wa wananchi.Kwa kifupi ni kwambaserikali imekuwa na matumizimabaya ya fedha za umma,wakati mengine yakiwa hayanalazima, huku ikiweka pembenimambo muhimu ya kutoahuduma kwa umma.Kwa mfano, miongoni mwawabunge inashangaza kwambani wa kuteuliwa au wa vitimaalum, wakilipwa mamilioniya fedha kila mwaka ya vikaovya bunge, wakati huo huowabunge hao wanateuliwakuwa wakuu wa mikoa auwilaya.Hapa tunahoji, kulikuwa nasababu gani, au kulikuwa naumuhimu gani kiongozi wa nchikuamua kumteua mtu kuwambunge na hapo hapo kumteuakuwa mkuu wa mkoa au Wilayahalafu alipwe fedha za ubungena ukuu wa mkoa au wilaya?Malipo na stahili
Kudhibiti matumizi mabayakutasaidia bajeti zetu
wanazolipwa watu hawa kwaubunge wa kuteuliwa na ukuuwa wilaya au mkoa wa kuteuliwakwa kipindi cha miaka mitano,yangeweza kusaidia kujengwavisima kadhaa na kuwasaidiawananchi kuondokana na shidaya maji.Zinaundwa Tume kuchunguzamambo ambayo hayahitajiuchunguzi waTume na kugharimumabilioni ya fedha. Kwa mfano,serikali kuunda Tume yaKuchunguza Matokeo ya Kidatocha Nne ya mwaka jana, hukutayari kukiwa kuna matokeoya Tume zilizokwishaundwakuchunguza jambo hilo hilosiku za nyuma na matokeo yakekutofanyiwa kazi hadi leo.Tuna matumaini kuwa majibuya Tume hii ya sasa kuchunguzamatokeo hayo, licha ya kutumiamamilioni ya fedha bado itakujana majibu yale yale ya Tumeiliyoundwa siku za nyumana majibu yake kufungiwakabatini.Hatuoni kwanini fedha zakuundwa Tume za namna hiizisitumike kupanua huduma zamaji hasa maeneo ya vijijini. Hiini mifano michache.Itoshe tu kusema kwamba,wakati wabunge wakiitakaserikali kutafuta mahali pakupatia fedha za kuongeza bajetiya Wizara ya Maji, ni vyemawakaanza na kupinga matumizihaya mabaya ya fedha za serikali,ili kunusuru fedha zitakazosaidiakugharamia shughuli za msingiza kuhudumia watanzania. Ni vyema ukaachwa huuutaratubu wa kuteua wabungekwa ajili ya kukidhi tu, dhanaya uwiano wa wanaume nawanawake Bungeni. Halafu baada ya hapo miaka mitanoikiisha walipwe mamilioni yafedha kwa kukidhi uwiano. Hayasio matumizi mazuri ya fedha.Wabunge huchaguliwa nawananchi majimboni. Kama niuwiano ukatafutwe majimboniau katika vyama, halafuwakagombee na kupigiwa kurana wananchi.Kwa mtazamo wetu, tunaonakuna haja ya kiongozi wa nchikunusuru fedha za serikalikwa kuacha mazoea ya kuteuawatu kutumikia nyadhifa mbili,Ubunge na Ukuu wa mkoaau Wilaya. Hu sio utaratibuwenye tija kimatumizi, zaidiya kuigharimu serikali tu nakuneemesha watu binafsi.Wabunge watadhibiti kwadhati matumizi haya yasiyokuwaya msingi ya serikali, nafuu yafedha itaonekana katika bajetizetu na angalau zitatusogeza.
 
3
 AN-NUUR
JAMADUL THAN 1434, IJUMAA APRILI 26 - MEI 2, 2013
Habari
Familia ya Sheikh Ponda katika wasiwasi mkubwa
HALI ya wasiwasi imetandakwa ndugu wa SheikhPonda Issa Ponda, baadaya kutakiwa kutolewa damuau mate ili kujiridhisha nauraia wa Sheikh Ponda Issaaliyeko mahabusu.
Habari zilizolifikia An nuur,mapema wiki hii, kutoka kwandugu hao, zinasema, kwambawamekuwa wakisumbuliwana watu wanaojitambulishakwao kuwa ni watu waUhamiaji.Wakiongea kwa nyakatitofauti kwa njia ya simukutoka Mkoani Kigoma naJijini Dar es Salaam, nduguhao wamesema, wamekuwawakitakiwa kutoa damu aumate ili vioanishwe na damuau mate ya Sheikh Ponda.Bi. Tausi Issa Ponda,aliye dada wa SheikhPonda, akiongea na An nuur,Jumatano wiki hii akiwa JijiniDar es Salaam alisema, sualahilo amelisikia akiwa hapaJijini kutoka nyumbani kwaoKigoma.“Baada ya kuelezwa kwakina suala hili sikukubaliananalo kabisa hata mamanimeongea naye mwenyewe pamoja na ndugu wenginewote wa kuzaliwa naPonda kwa ujumla wakawawamekataa, na kushangazwana hatua hiyo.” AlifafanuaBi. Tausi.Lakini, Bi. Tausi, alisema juzi (Jumatano) mjomba wao(Kaka wa mama yake) aliyepoDar es Salaam, alimpigia simuna kwamba watu wa Uhamiajiwamemfuata nyumbanikwake, na kumuhoji kuhusumama yake na kuwaeleza halihalisi ya dada yake.Hata hivyo, alisema, watuhao wa Uhamiaji walimjibukuwa na wao wameshafanyauchunguzi mwingi hadi kwaowamefika, lakini walichokuwawanataka ni kujiridhiashazaidi kupitia njia hiyo yavipimo vya damu ya ShekhPonda, Mama wa Ponda nandugu yake, ili viwekwe pamoja viangaliwe kama nikweli yule ni mama yakealiyemzaa.“Mjomba akawaamenifahamisha hizo habariakaniambia wewe unaonaje,nikamwambia kwakwelihizo habari sikubaliani nazokabisa.” Alisema.Hata hivyo Bi. Tausi,alidai kuwa mjomba wakealimweleza kuwa jamaa haowamemuhakikishia usalamawa dada yake (Mama Ponda),na kwamba katika utoaji huodamu hapatakuwa na tatizololote.Kwa mujibu wa dada
Na Bakari Mwakangwale
huyo wa Sheikh Ponda,alimuuliza mjomba wakekuwa ikiwa Mama yaoatakataa kuchukuliwa matena damu itakuwaje, mjombawake alimjibu kuwa, akikataawatajenga hoja kuwa mwanaesio raia kweli, na kwambakama ana uhakika asingekataakutoa hiyo damu.Bi. Tausi alisema, baadaya kuongea hayo na mjombawake ilimlazimu ampigiesimu kaka yake mkubwaaliyeko Mkoani Kigoma,na baada ya kuongea nayealimuleza hatoweza kuondokana mama yao kutokana nashughuli zake.Bi Tausi, lisema aliwezakuwasiliana na ndugu yakealiyemtaja kwa jina laMayasa Sadala, ambaye nimtoto wa mjomba wake,naye alimweleza wazi kuwahilo suala haliwezekani, nakwamba linahitaji umakini nauangalifu.Bi. Tausi alisema kwataarifa walizo nazo mpakaJumatano wiki hii, ni kuwaSerikali ilishaandaa pesaza ndege pamoja na pesaya kujikimu, kwa ajili yakuwasafirisha kuja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezila kutolewa damu.Awali, Bi. Tausi, alisemamjomba wake alitowa wazokuwa familia ikubalianetu, kwamba Sheikh Pondaakatolewe hiyo damu, ili jamaa hao wajirizishe, kwaniwao hawana shaka na hilo.Hata hivyo Bi Tausi,alisema kuwa hawana imanina waendeshaji wa zoezi hilo,kwani wanaweza wakazuakinyume na ukweli wa vipimokwani familia haina shakahata chembe na uraia wandugu yao bali uadilifu wawatu hao.Bi. Tausi, alisema hayo yoteyanakuja kwa lengo la kutakakujua uraia wa Sheikh Ponda,na kupata uhakika pamoja nakwamba awali walishafanyauchunguzi lakini wanadaihawajajiridhisha.Alisema, kufuatia zoezihilo, familia na ndugu kwaujumla wamekuwa na hofu juu ya zoezi hilo, kwani hivikaribuni uhamiaji wenyewewalifuatilia suala hilo nakuthibitisha uraia wa SheikhPonda.Bi. Tausi, alisema uhamiajiwalifika nyumbani kwaoKigoma na wao kama familiaya Mzee Issa, walifikawakachukua vyeti vyao vyakuzaliwa wakatoa kopi,lakini pia walipewa kitabucha kupigania Uhuru wakati Nyerere anataka kuingia katikautawala ambacho kilikuwa naorodha ya majina ya wazeewaliopigania Uhuru na MzeeIssa Ponda alikuwemo. Naye Bi. Mayasa Sadala,akizungumzia sakata hiloalisema, watu wa Uhamiajiwalifika nyumbani kwa babayake (Mzee Sadallah), nakudai kuwa wameelekezwakuwa yeye ni mjomba wakeSheikh Ponda.Bi. Mayasa alieleza kuwawatu hao walimueleza babayake kuwa wanachotaka niSheikh Ponda na Mama yakewapimwe damu pamoja nakaka yake, na kwamba tiketizao za ndege zipo tayari,kuletwa Jijini Dar es Salaam.Bi. Mayasa,aliyejitambulisha kuwani Katibu wa SadallahFoundation, alisema, baadaya maelezo hayo alimpigiakaka yake Ponda simu,ambapo alimueleza ujio wawatu hao na kufafanua juuya usalama wao katika zoezihilo, jambo ambalo kaka waPonda alikataa, na kuagizwaaambiwe dada yake (Tausi)aliyeko Jijini Dar es Salaam,kwa sasa.“Tausi alipopigiwa simu namjomba wake (Mzee Sadala),naye aligoma akasema yeyehaafiki mama yake kuja walakutolewa damu, hivyo aliwapa jamaa hao namba ya simuya Tausi ili waongee naye.”Alisema Bi. Mayasa.Bi. Mayasa, alisema baadaya hapo, watu hao walimuelezaMzee Sadallah, kuwawanakwenda kukaa kikao naendapo watakubaliana, MamaPonda na wanae wakusanyikeili waenda kutolewa damuhuko huko Kigoma, kishawatakuja kumtoa damu SheikhPonda.Bi. Mayasa, alisema kwataarifa aliyonayo mpakasasa (Jumatano) ni kwambafamilia chini ya Mama Pondawamekutana na wamesemahawatatoa damu wala mateyao.“Mama Ponda kasema hatandege ifike mlangoni kwakehatotoka na wala hiyo sindanohatochomwa, kwa sababuUhamiaji walisha pelelezana wakamfuata mama yakePonda, aliwaeleza kila kituna taarifa walitoa baada yauchunguzi wao.” Alisema Bi.Mayasa, akinukuu maelezo yaMama Ponda.Bi. Mayasa, alisemakujirudia kwa suala hilimuda huu, wakati tayariwalishajiridhisha kuwa Pondani raia, huenda kuna kitukinatafutwa dhidi ya SheikhPonda.Bi. Mayasi alisema, kwamara ya mwisho watu haowalimwambia kaka wa Ponda,kuwa kama wana mashaka nausalama kwa kutolewa damu basi watoe hata mate yao tu.Alisema, familia inaonakuna jambo nyuma ya paziakwani kama ni uhalali wauraia, kwa kawaida damuhuchukuliwa ya baba, sasaakahoji vipi leo walazimishekuchukua damu ya Mamana ndugu zake Ponda, iliwajirishe na uraia wake.“Hata Mzee Sadallah,aliuliza hilo, na kuonyeshahofu yake alidai (Mzee)walishindwa kulitoleaufafanuzi, wamedai eti hatakwa mama inawezekana,sasa tunashindwa kuelewahili zoezi ni kwa lengogani haswa.” Alisema Bi.Mayasa.“Kama ni kujiridhisha uraiawa Sheikh Ponda, wakatafutekaburi la Mzee Issa Ponda,lilipo ndipo wajirizishe, lakinisio kwa mama au kaka na dadazake haya kwetu ni mapya, na pengine ipo namna.” AlisemaBi. Mayasa.Alipoulizwa Mjomba waSheikh Ponda, Bw. Sadala,alikiri kufuatwa na maafisawa uhamiaji lakini hakuelezawalikuwa wakihitaji kitugani.Juhudi za kuwapatamaofisa wa Idara ya Uhamiajikuzungumzia suala hilizinaendelea.
Wafungwa 8 wasilimishwa
WAFUNGWA wanane(8) wa Gereza la Kimbijiwamesilimu.
Wafungwa hao wamesilimu baada ya kukutana nawafungwa Waislamuwalioingia kifungoni baadaya kuhukumiwa kutokana nakesi ya maandamano.Hayo yamefahamikakutokana na taarifa iliyotolewana Amir wa Kamati iliyoundwakuhudumiwa wafungwa hao pamoja na familia zao.Akiongea na An nuur,Amir wa Kamati hiyo Ust.Baiya S. Buiya amesemakuwa, katika ziara yake katikagereza la Bagamoyo alipataushirikiano mzuri kutoka kwaWaislamu wa Mji huo ambaoaliambatanao kufika katikagereza hilo na kuwajulia haliwenzao.Alisema, kwa ujumlaWaislamu hao walioMagerezani wamekuwawakihitaji Misahafu, Juzuuna vitabu vywa swala namaarisho yake na vinginevyenye mafundisho yaUislamu kwa ujumla.Alisema, kwa Waislamuwa gereza la Bagamoyo,wameweza kuanzishautaratibu wa ibada gerezanihumo ambao awali ilikuwangumu, ambapo katika gerezala Kimbiji, Waislamu haowameshasilimisha wafungwaWakristo nane, na wameombawapatiwe vitabu zaidi kwaajili ya Da’awa.Kwa upande mwingine,Waislamu nchini wametakiwakutoa ushiriakiano wa halina mali kwa kamati yakuhudumia Waislamu 52,waliofungwa mwaka mmoja jela pamoja na familia zaowalizozicha.Wito huo umetolewa nauongozi wa Shura ya Maimam(T), baada ya Shura hiyokuunda kamati maalum April14, 2013, ya kuwahudumia
Na Bakari Mwakangwale
wafungwa wa kesi yamaandamano, kufuati kikaokilichowakutanisha Maimamkutoka Misikiti mbalimbali yaJijini Dar es Salaam.Taarifa hiyo iliyosainiwa naAmir wa Shura ya Maimam,Sheikh Mussa Y. Kundecha,ilisema Shura imeunda kamatiya watu sita, ambao watakuwana jukumu la kukusanyamichango Misikitini na kwaWaislamu mbalimbali.“Hivyo naitambulishakwako kamati hii ili muwezekutoa ushirikiano wa hali namali kwa ajili ya kuwahudumiaWaislamu 52 wa maandamanowaliopo magerezani.”Ilisema sehemu ya baruaya kuitambulisha kamati hiyokwa Waislamu.Akiongea na An nuur, Amir wa Kamati hiyo Ust. BaiyaS. Buiya, alisema jukumukubwa la kamati hiyo nikuwatembelea ndugu zaoWaislamu waliohukumiwakifungo cha mwaka mmojahivi karibuni, kujua matatizoyao sambamba na kuwa karibuna familia zao.Buiya alisema Muuminiwa kweli atakaye baki katikaimani yake sawasawa lazimaakutane na mambo matatu,aliyataja mambo hayo kuwani kufungwa kwa ajili ya Allah(s.w), ambapo huyo atakuwahajapata hasara, kwa sababuatakuwa ametekeleza sunnaya Nabii Yusuph.Ust. Buiya, alisema jambola pili ni kufukuzwa katikanchi yake kwa ajili ya Diniyake na huyo naye yakimfikahayo atakuwa hajapatahasara kwake kwani atakuwakatekeleza Hijra MtumeMuhammad (s.a.w).Lakini kubwa lingine Ust.Buiya, alisema Muumini huyo pia ategemee kuuwawa kwaajili ya Allah au Uislamu, nayeatakuwa hana hasara kwaniatakuwa kafa Shaheed.Ust. Buiya, alisema ikiwa
Inaendelea Uk. 4

Activity (3)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 thousand reads
1 hundred reads
Salim Ahnmed liked this

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->