You are on page 1of 3

Tanzania Football Federation

Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA


Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shauri Moyo Road P.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania . Telefax: + 255-22-2861815 E-mail: tanfootball@tff.or.tz . Email: www.tfft.or.tz

TANGAZO
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) 14/08/2013
1. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa TFF utafanyika tarehe 20/10/2013 jijini Dar es salaam. Wale wote wanaopenda kuwania nafasi za uongozi wa TFF wanataarifiwa kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi tarehe 20 Agosti 2013 katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF (Idara ya Fedha), kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha Fomu ni saa 10:00 Alasiri tarehe 20 Agosti 2013. Nafasi zinazotangazwa kugombewa ni: (i) (ii) (iii) 3. Rais wa TFF. Makamu wa Rais wa TFF. Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, nafasi kumi na tatu (13).

2.

Mtu yeyote anayeomba nafasi ya uongozi katika TFF lazima atimize masharti yafuatayo: (i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) (viii) Awe Raia wa Tanzania. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari. Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5). Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini. Awe na umri wa angalau miaka 25. Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza. Awe mwadilifu, mwaminifu na mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu, wajibu na malengo ya TFF kwa weledi. Mtu anayegombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa TFF lazima awe na kiwango cha Elimu kisichopungua Shahada ya Chuo Kikuu na awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

4.

Ada za Fomu za maombi ya uongozi ni hizi zifuatazo: (i) (ii) (iii) Rais wa TFF; Shillingi Laki Tano (Tshs. 500,000/=). Makamu wa Rais wa TFF; Shillingi Laki Tatu (Tshs. 300,000/=). Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Shillingi Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).

5.

Kwa wale ambao walilipia fomu za kugombea katika mchakato uliofutwa na ambao wanakusudia kugombea nafasi zile zile walizozilipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao. Ratiba ya mchakato wa Uchaguzi wa TFF imeainishwa hapa chini: Na. 1. 2. TAREHE 14/08/2013 16/08/2013 20/08/2013 SHUGHULI Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutangaza Uchaguzi wa TFF, nafasi za kugombea na sifa za kugombea uongozi wa TFF. Kuchukua Fomu za maombi ya uongozi wa TFF kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Katibu Mkuu wa TFF). Fomu zitatolewa kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 10.00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha fomu kwa Katibu Mkuu wa TFF ni Jumanne tarehe 20/08/2013 saa 10:00 Alasiri. Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia fomu za waombaji uongozi wa TFF. Kutangaza matokeo ya upitiaji fomu na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo majina ya waombaji uongozi wa TFF (23/08/2013). Kutoa fursa ya pingamizi kwa waombaji uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 26/01/2013 saa 10:00 Alasiri. Pingamizi ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF. Pingamizi zizingatie matakwa ya Ibara ya 11(3) ya Kanuni za Uchaguzi. Wawekaji Pingamizi na waliowekewa Pingamizi kuitwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa utetezi wao kuhusu Pingamizi. Kamati kujadili Pingamizi. Usaili na kutangaza matokeo ya pingamizi na ya usaili / Kuwajulisha kwa maandishi wagombea matokeo ya usaili. Kutangaza orodha ya awali ya wagombea. Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF kuwasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili, kwa kujadiliwa na kutolewa maamuzi na Kamati ya Maadili ya TFF. Kutoa fursa ya kukata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF (TFF Elections Appeal Committee) kwa masuala yasiyo ya Maadili. Rufaa zilizoambatanishwa na ada ya malipo ya Rufaa zitapokelewa na Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 06/09/2013 saa 10:00 Alasiri. Kamati ya Maadili ya TFF kupitia mashauri yote yanayohusu Maadili na kuyatolea uamuzi. Kamati ya Maadili ya TFF kutoa matokeo ya maamuzi ya mashauri ya Maadili kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF na wagombea. Kukata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 19/09/2013 saa 10:00 Alasiri. Kusikiliza Rufaa zilizopelekwa kwenye Kamati ya Rufaa

6.

3.

21-23/08/2013

4.

24-26/08/2013

5. 6. 7.

27/08/2013 29/08/2013 30/08/2013 - 03/09/2013 04 06/09/2013

8.

04 06/09/2013

9. 10. 11.

07-13/09/2013 14- 16/09/2013 17- 19/09/2013

12. 13. 14. 15.

20- 24/09/2013 25-27 /09/2013 28/09/2013- 02/10/2013 03-04/10/2013

16. 17. 18. 7.

05/10/2013 06/10/2013- 19/10/2013 20/10/2013

ya Maadili ya TFF na kutolea uamuzi. Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kuwafahamisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Wagombea matokeo ya Rufaa zilizosikilizwa na Kamati ya Rufaa ya Maadili. Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kusikiliza Rufaa za Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya Maadili. Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kutangaza na kuwapa taarifa za matokeo ya rufaa wagombea waliokata rufaa (zisizohusu mashauri ya Maadili). Aidha Kamati ya Uchaguzi ya TFF nayo kufahamishwa matokeo ya rufaa hizo. Kutoa orodha ya wagombea wote waliopitishwa kugombea uongozi wa TFF na kuwataarifu wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF. Kipindi cha Kampeni kwa wagombea wote. Uchaguzi wa Viongozi wa TFF.

Uchaguzi wa TFF unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF.

Hamidu Mbwezeleni MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF

You might also like