Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword
Like this
4Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
Maazimio Ya Mafunzo Ya Kamati Za Bunge Zinazosimamia Fedha Za Umma Na Bajeti

Maazimio Ya Mafunzo Ya Kamati Za Bunge Zinazosimamia Fedha Za Umma Na Bajeti

Ratings: (0)|Views: 4,804 |Likes:
Published by Zitto Kabwe
MAAZIMIO YA MAFUNZO YA KAMATI ZA BUNGE ZINAZOSIMAMIA FEDHA ZA UMMA NA BAJETI (PAC, LAAC NA BC)
OCEANIC BAY HOTEL BAGAMOYO 17th AUGUST, 2013
MAAZIMIO YA MAFUNZO YA KAMATI ZA BUNGE ZINAZOSIMAMIA FEDHA ZA UMMA NA BAJETI (PAC, LAAC NA BC)
OCEANIC BAY HOTEL BAGAMOYO 17th AUGUST, 2013

More info:

Published by: Zitto Kabwe on Aug 18, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as DOC, PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

10/03/2013

pdf

text

original

 
MAAZIMIO YA MAFUNZO YA KAMATI ZA BUNGE ZINAZOSIMAMIA FEDHAZA UMMA NA BAJETI (PAC, LAAC NA BC)OCEANIC BAY HOTEL BAGAMOYO 17th AUGUST, 2013
1)Kutokana na kutokuwepo na taarifa sahihi kuhusu deni la Taifa kunaumuhimu wa kukutanisha wadau wakuu wanaohusika hususani BOT, HAZINA,Kamati za Bunge na CAG ili kuweza kujua kwa usahihi zaidi ukubwa wa denihilo. Vile vile imeamuliwa kuwa Serikali ishauriwe kuunda chombo hurukitakachosimamia deni la taifa.2)Baada ya kuanzisha mfumo mpya wa bajeti ya Serikali mwaka huu kunaumuhimu wa kuandaa mkutano wa kutathimini mafanikio na changamoto zamfumo huu na kujadili mambo ya kuboresha zaidi mfumo mzuri wa bajeti yaSerikali.3)Kamati za Bunge zinazoshughulikia usimamizi wa fedha na rasilimali za taifazishughulikie zaidi Maafisa Masuuli hatarishi (risk based) ili kuleta thamani yafedha katika utendaji wao. Kamati zishirikiane na CAG katika kuamua ni AfisaMasuuli yupi aitwe kukutana na Kamati.4)Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge na TAMISEMIwaanzishe utaratibu wa kuratibu mikutano na mafunzo ya Wakurugenzi waHalmashauri kwa pamoja kuliko kila Wizara kuwaita watendaji hao katikasehemu mbalimbali kwa muda tofauti na kuwafanya kutokuwepo ofisini kwakipindi kirefu.5)Mfumo wa kutunza kumbukumbu za hesabu na nyaraka mbalimbali katikaSerikali Kuu na Halmashauri uboreshwe ili zinapohitajika zipatikane kwawakati muafaka bila kisingizio cha aina yoyote.6)Kuhusu ukaguzi wa ufanisi CAG asisubiri mpaka asikie malalamiko kutokakwa wananchi au kwenye magazeti bali akague mara kwa mara sehemu zotezenye matatizo.7)Taarifa za mwaka za Kamati za Bunge ziwe na kipengele cha kiwango chautekelezaji wa mapendekezo ya Kamati yaliyotolewa awali. Kamatiziwezeshwe kifedha ili ziweze kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yao.Kanuni za Bunge zieleze utaratibu wa ufuatiliaji wa Maazimio ya Bunge nanamna utekelezaji wake utavyowasilishwa Bungeni. Vile vile Bunge litenge
 
siku ya kujadili Serikali ilivyoshughulikia hoja za Kamati za Bunge. Spikaashauriwe kuhusu umuhimu wa kuunda Kamati ya Bunge ya kufuatilia ahadiza Serikali.8)Mikataba katika ngazi ya Serikali za Mitaa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.9)Serikali inatakiwa kufanya jitihada za ziada kuzalisha wataalam wa fani yamanunuzi. Kuna umuhimu wa PPRA kuongezewa nguvu za ziada za kiutendajiikiwa ni pamoja na fedha na wafanyakazi.10)Bajeti ya Bunge iongezwe kupitia Mfuko wa Bunge na iwasilishwe Bungenina Naibu Spika na sio Ofisi ya Waziri Mkuu.11)Serikali iandae mjadala wa kitaifa wa kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana navitendo vya rushwa na mmomonyoko wa maadili vinavyoongezeka kwa kasihapa nchini. Vilevile viongozi wa umma na watendaji waongoze kwa mfanokwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza majukumu yao.12)Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma haiweki uwazi wa kutangazaumiliki wa mali za viongozi. Hii inapelekea viongozi kutoweka wazi maliwanazomiliki na ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki usio wa ukweli. Ni vyemaSekretarieti wakafanya utafiti wa umiliki wa mali kwa viongozi wa Umma nakuweka taarifa hizo katika tovuti ya Sekretariati ili kuwawezesha wananchikuweza kuona mali zinazomilikiwa na viongozi wao; na pale ambapo kiongozihatakuwa ametoa taarifa ya umiliki huo basi taarifa hiyo itolewe kwa Tume.13)Kwa kuwa leseni za udereva za sasa zinaweza kuweka kumbukumbu zamakosa ya usalama barabarani, basi TRA ikishirikiana na Wizara ya Mamboya Ndani zihakikishe ya kuwa Askari wa Usalama Barabarani wanatumiautaratibu huu wa kisasa wa kutoa “notification” na kutoa risiti za malipo zaelektroniki.14)Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki.Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaanze kutumia risiti zaeletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yanayotokeahivi sasa katika kutumia risiti zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikalizifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine zakielektroniki.
 
15)TRA ihamasishe wananchi na wafanya biashara umuhimu wa matumizi yarisiti za elektroniki, wafanyabiashara waelimishwe umuhimu wa kutoa risitihizo na wananchi waelimishwe umuhimu wa kudai risiti kila wanapofanyamanunuzi. Elimu na uhamasishaji huo unaweza kufanywa kwa kutumia mbinumbalimbali ikiwemo sanaa, timu za michezo, bendi za muziki, redio, TV, mbaoza matangazo n.k.16)Serikali idhibiti makampuni ya uwakala wa kupakia na kupakua mizigo(
clearing and forwarding
) yaliyopo Bandarini ili kudhibiti mapato ya forodha.17)Sheria ya
 Anti Money Laundering
” ya 2006 irekebishwe ili iweke viwangovya fedha ambazo mtu anaweza kuingia au kutoka nazo nchini bila kuzitaja(declare). Kuna umuhimu wa Waziri wa Fedha kutengeneza kanuni zakutekeleza Sheria hiyo.18)Benki Kuu iandae mfumo thabiti wa usimamizi wa Maduka ya Fedha(Foreign Bureau de Change), na kuhakikisha kutungwa kwa sheria inayozuiamatumizi ya fedha za kigeni katika shughuli za kibiashara hapa nchini.19)
The Proceeds of Crime Act, 1991
” ifanyiwe marekebisho na kuwekakifungu kinachomwezesha AG/DPP kuwa na mamlaka ya kuomba mahakamakufungua kesi ya madai (Civil Forfeiture) kwa watu wanaotuhumiwa kwaufisadi.20)Imesisitizwa kwamba CAG akague misamaha ya kodi na kuweka taarifahiyo kwenye taarifa za kila mwaka.21)Serikali iimarishe Taasisi zinazoshughulikia maadili utawala bora nauwajibikaji kama vile Sekretariati ya Maadili ya Viongozi, Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora, Takukuru, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Kamati ya Maadili ya Bunge iliziweze kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizoanzisha Taasisi hizo.22)PCCB na vyombo vingine vinavyohusiana na kushughulikia masuala ya jinai wawe waalikwa kwenye vikao vya Kamati za Bunge ili waweze kutoaushauri kwenye kamati hizo.

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->