Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
2Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
Mtama Press Statement

Mtama Press Statement

Ratings: (0)|Views: 408|Likes:
Published by dewjiblog

More info:

Published by: dewjiblog on Aug 26, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as DOCX, PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

03/04/2014

pdf

text

original

 
 
SEHEMU YA KWANZA
1. UMUHIMU WA CHAKULAChakula ni muhimu kwa maisha ya binadamu, kinamuwezesha kupata nguvuna virutubishi ambavyo husaidia kuujenga mwili na vile vile kuupa mwilikinga inayosaidia kujikinga dhidi ya maradhi mbali mbali.Kuna aina mbali mbali za vyakula ambavyo pia vina kazi tofauti mwilini navina virutubishi tofauti tofauti, hivyo, mtu anatakiwa kula vyakula vya ainambali mbali kwani aina moja ya chakula haiwezi kuwa na virutubishi vyotevinavyohitajika mwilini. Virutubishi vina kazi maalumu mwilini na hiihuwezesha mfumo wa mwili kufanya kazi vizuri.Vyakula vimegawanyika katika makundi mbali mbali kulingana na kazi zavyakula hivyo mwilini. Hata hivyo, vyakula vilivyo katika kundi moja huwezakuwa na aina viwango tofauti vya virutubishi na wakati mwingine hata ainaya virutubishi vilivyomo. Kwa hali hiyo basi, mtu anatakiwa kulamchanganyiko wa vyakula mbali mbali ili kuweza kupata virutubishi vyotevinavyohitajika mwilini.Mlo wenye mchanganyiko wa vyakula vyenye virutubishi vya aina zote,
huitwa “
mlo kamili
”. Mlo kamili ni muhimu sana hasa kwa watoto, ambao
huwasaidia kukua vizuri na kuwa na afya njema. Mlo kamili humwezeshamtu kujikinga na madhara ya maradhi mbali mbali kama vile malaria, surua,kuharisha, shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo na hata ukimwi
.
Mlo kamili na wa kutosha hutoa virutubishi kama vile protini, vitamini,madini na nishati. Vile vile mlo kamili ni muhimu kwa wazee na wagonjwakatika kujenga mwili, na kusaidia uponaji wa majeraha, na kupata nguvubaada ya kukabiliana na maradhi.
 
 
1.1. Mgawanyo wa vyakula
 
Vyakula vyenye wangaHivi ni muhimu katika kuupa nguvu mwili za kufanya kazi mbali mbali.Vyakula vyenye wanga ni pamoja na: nafaka, kama mahindi, mchele, ngano,mtama, ulezi, uwele na kadhalika. Wanga pia hupatikana katika mihogo,viazi vitamu, viazi ulaya, viazi vikuu, magimbi, ndizi, miwa na asali.
 
Vyakula vyenye protini
Protini ni muhimu sana 
katika kujenga mwili na kuwezesha ukuaji wa mwilihasa kwa watoto na pia husaidia kutengeneza kinga ya mwili. Vyakula vyenye
protini ni pamoja na: nyama, (ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata,
samaki, mayai, maziwa na kunde, maharage, soya, dengu, choroko, njegere,mbaazi, na njugu mawe.
 
Vyakula vyenye mafutaVyakula vyenye mafuta huleta joto mwilini, na vile vile huleta nguvu mwilinina kulinda na kulainisha ngozi na pia utando (membrane). Mafuta hutokanana mimea na huwa yanauzwa madukani kama vile, mafuta ya karanga,alizeti, nazi, ufuta, korosho, mawese, mbegu za maboga, mbegu za pamba.
 
Matunda na mboga mbogaMatunda na mboga mboga ni muhimu sana katika mwili, kwa vile vyakulahivi vina vitamini na madini mbali mbali ambayo ni muhimu mwilini.Vitamini na madini huhitajika kwa kiwango kidogo sana lakini ni muhimukwa mwili kuweza kufanya kazi zake vizuri. Upungufu wa vitamini na madinimwilini unaweza kusababisha hitilafu mbali mbali katika mwili na hatakusababisha kasoro zinazoambatana na maradhi mwilini.
 
Vitamini
.
Kuna vitamini mbali mbali ambazo ni Vitamini A, Vitamini B, Vitamini C,Vitamini, D na nyinginezo.
 
 
Vitamini A.
Vitamini A ni muhimu katika ukuaji hasa kwa watoto na utengenezaji wachembe chembe za mwili (cells). Husaidia kuongeza kinga mwilini nakuwezesha macho kufanya kazi vizuri. Vitamini A ni muhimu katika kutunzangozi.Vitamini A, hupatikana katika matunda Na mboga mboga zenye rangi yamachungwa Na manjano, Kama vile karoti, viazi vitamu vya manjano,maembe, na nyanya. Pia hupatikana katika mboga za majani, maini namaziwa.
 
Vitamin
.
Ni za aina mbali mbali, husaidia kuzuia magonjwa mbali mbali Kamapellagra, inayosababisha ngozi kubabuka hasa katika zile sehemuzinazopigwa Na jua, chakula kushindwa kusagika vizuri na hata kusababishakuharisha. Ukosefu wa vitamin B unasababisha beriberi, ugonjwa unaofanyamtu anapungua uzito, moyo unaweza kuwa mkubwa, miguu kuvimba nakujaa maji. Ukosefu wa vitamini B pia unaweza kusababisha midomokupasuka, na dalili nyinginezo mbali mbali.Hupatikana katika mboga za majani kama vile spinach, mchicha, matembelena kadhalika.
 
Vitamini
Vitamini C ni muhimu mwilini, husaidia ukuaji, kuongeza kinga mwilini nakusaidia mwili kutumia madini ya chuma.Hupatikana katika machungwa, limao, machenza, mananasi na mboga zamajani ambazo hazikupikwa mpaka kuiva sana.
 
Vitamini
Ni muhimu katika kuufanya mwili utumie madini ya chokaa ambayohusaidia katika utengenezaji WA mifupa Na meno, pia husaidia kuimarishamoyo na mishipa ya fahamu.
 
Vitamin D hupatikana katika vyakula Kama mafuta ya samaki na maini. Piahutengenezwa katika ngozi kutumia mionzi ya jua.

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->