Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
1Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
Revised Taarifa Kwa Wananchi Kuhusu Uboreshaji Wa Huduma Za Tiba Hospitali Ya Taifa Muhimili Septemba 2 (3)

Revised Taarifa Kwa Wananchi Kuhusu Uboreshaji Wa Huduma Za Tiba Hospitali Ya Taifa Muhimili Septemba 2 (3)

Ratings: (0)|Views: 100|Likes:
Published by dewjiblog

More info:

Published by: dewjiblog on Sep 09, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as DOC, PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

10/16/2014

pdf

text

original

 
HOSPITALI YA TAIFAMUHIMBILI
Cables:
"MUHIMBILI" Postal Address:
Telephones:
+255-22-2151367-9P.O. Box65000
FAX:
+255-22-2150534
DAR ES SALAAMWeb:www.mnh.or.tz
  Tanzania
TAARIFA KWA WANANCHI KUHUSU UBORESHAJI WA HUDUMA MAGONJWA YA MOYOHOSPITALI YA TAIFA MUHIMILI SEPTEMBA 9, 2013
Awali ya yote nashukuru kupata fursa hii ya kukutana na vyombo vya habari ili kuzungumizia baadhi tu yamafanikio ambayo Hospitali ya Taifa Muhimbili imeyapata kupitia Kituo cha Upasuaji Moyo na Mafunzo(Cardiac Surgery Treatment and Training Centre.
Huduma za Upasuaji Moyo:
Kama mnakumbuka tarehe 21 Mei 2008 upasuaji wa moyo ulianza rasmi hapa Muhimbili, ukifanywana madaktari wetu baada ya kupata mafunzo nchini India na Israel. Wagonjwa 105 walifanyiwaupasuaji katika kipindi cha mwaka mmoja na hadi kufikia leo tayari wagonjwa 453 wameshafanyiwaupasuaji. Upasuaji wa moyo unaofanyika ni sawa na upasuaji katika vituo vikubwa vya upasuaji wa moyoduniani kote. Wataalam wetu wamekuwa wakifanya upasuaji wa kuziba matundu kwenye moyo nakubadilisha valvu ambazo zimebana na kushindwa kuruhusu damu kupita kwenye moyo au kulegea nakufanya damu kuvuja kwenda kwenye sehemu isiyohusika katika moyo na kurudisha moyo katika hali yakeya kawaida ya afya ya mgonjwa.Pamoja na kufanya upasuaji huduma nyingine ambazo zimefanyika na zinaendelea kufanyika ni pamoja nakliniki mbalimbali kama vile za magonjwa ya valve, moyo kupanuka, mishipa ya moyo kuziba, mapigo yamoyo kushuka, magonjwa ya moyo ya kuzaliwa ya watoto na upasuaji wa moyo na mishipa ya damu.
Ufungaji wa Vifaa Tiba:
Kituo hiki kina vifaa vya kisasa na vya hali ya juu na mahsusi kwa ajili ya kumudu matibabu ya magonjwamakubwa ya moyo. Hospitali inaendelea kutafuta taasisi zenye uzoefu mkubwa wa matibabu ya moyo ilikuanzisha ushirikiano utakaowezesha kupata wataalamu wao kuja kushirikiana na wataalamu wetu kutibumagonjwa makubwa ya moyo hapa hapa nchini kama njia ya kuongeza uwezo kitaaluma. Tunafurahikuwaambia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi waJamii imetoa fedha kwa ajili ya kununua mtambo mkubwa wa kuchunguza mishipa na shinikizo ndani yamoyo na maradhi makubwa ya moyo ya kuzaliwa
(Catheterization Laboratory).
Huu ndiyo mtamboamboa kwa kipindi kirefu umekuwa ukipelekea Serikali yetu kupeleka wagonjwa wengi wa moyo kufanyiwa
1
 
matibabu nchini India. Mtambo huu umefungwa siku za hivi karibuni, tutaujaribu
(testing)
mapema mweziOktoba mwaka huu. Mtambo huu umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 3.6
Jinsi mtambo wa (Catheterization Laboratory) unavyofanya kazi:
Mtamo huu wa Cath Lab ndio unaotusaidia kuangalia mishipa ya damu inayoenda kwenye moyo, kuangaliamoyo jinsi unavyofanya kazi na pia kama mtu anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo mashine au mtambohuu unatusaidia kuangalia vitu mbalimbali kwenye moyo wa mgonjwa husika ili kujiridhisha kuona kamakuna jinsi yoyote mgonjwa huyu atanufaika na upasuaji huu. Cath Lab inasaidia pia kuweka kifaa saidizikatika moyo wa mtu (pacemaker) ambacho ni kama betri kinachosaidia kuufanya moyo ufanye vizuri sikuzote.
Wafanyakazi wa Kituo hiki:
Kituo hiki kinahitaji wafanyakazi wa kada mbalimbali wapatao 365 lakini kwa sasa kina watalaam 121.Lakini nafurahi kuwambia kuwa katika mwaka uliopita wa fedha tulipata kibali kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100 ili kukidhi mahitaji halisi ya kituo hiki katika kutoa huduma. Pamoja na hayo tunachangamoto ya kupata watalaam waliobobea katika magonjwa ya moyo ambao hawapatikani kwa urahisikatika soko la ajira. Lakini tunajithaidi kuajiri watalaam ambao tutawapeleka kubobea hususani katikaubingwa wa nusu kaputi, upasuaji na mishipa ya damu, upasuaji wa moyo kwa watoto n.k
Gharama za Matibabu:
Kama mnavyojua, huduma za maradhi ya moyo zina gharama kubwa na zinahitaji wataalamu wa hali ya juu. Ili huduma hii iwe endelevu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapitia upya utaratibu wa kulipiamatibabu ikiwa ni na kuzishauri kampuni zote za Bima ya Afya kulipia wateja wao wanaohitaji hudumambalimbali za moyo. Kwa kufanya hivyo Kituo kitaweza kujiingizia kipato kitakachotumika kuboreshahuduma pamoja na kuweka motisha kwa wafanyakazi.Kituo hiki kitakuwa faraja kubwa kwa nchi yetu na kitaipunguzia Serikali mzigo ikizingatiwa kwamba asilimia70 kati ya wagonjwa wote wanaopata rufaa ya Serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi ni wagonjwa wa moyo.Mathalan serikali kwa makisio inatumia kama dola za kimerakani 10,000 kulipia gharama za matibabu yamgojwa mmoja nje ya nchi ukilinganisha na dola za marekani 6,000 mgonjwa akitibiwa katika kituo chetucha Moyo Kwa hiyo, kuanzishwa kwa kituo hiki kutapunguza matumizi ya Serikali kwa kiwango kikubwasana. Hata hivyo Serikali inapitia mchakato wa uboreshaji wa utoaji wa huduma pamoja na upatikanaji wafedha ili kila Mtanzania aweze kupata huduma bora hapa kwetu.
Uwekezaji Uliofanywa hadi sasa 
Ujenzi wa Kituo hiki umejengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Ujenzi pamoja ufungaji wa vifaa hadi hivi sasa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 32 ambapoSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechangia kiais cha shilingi bilioni 16,411,741,367ambapo Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imechangia shilingi bilioni 15,630,769,600. Uwekezaji huuni wa dhati na tuna kila sababu ya kuipoingeza Serikali zote mbili kwa kazi kubwa iliyofanyika hapa.
2

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->