Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
5Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1092

ANNUUR 1092

Ratings: (0)|Views: 3,307|Likes:
Published by MZALENDO.NET
ANNUUR 1092
ANNUUR 1092

More info:

Published by: MZALENDO.NET on Sep 29, 2013
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

02/09/2014

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1092
DHULQADAH 1434, IJUMAA
, SEPT. 27 - OKT. 3, 2013
 
BEI TShs 500/=, Kshs
Sauti ya Waislamu
www.annuurpapers.co.tz
Kenya wachukuetahadhari kubwa
Wachunguze kwa kituo, kuhoji sanaTanzania tusiparamie habari, tujifunzeMwenzako akinyolewa, kichwa chako…
 Vyombo vya habari vinaitisha Tanzania
…Sio Al Qaida wala Al ShababKwa nini? Kwa masilahi ya nani?
Ukumbusho ni Dawa
Dr. Shein akumbushwa ahadi zakeMbatia, Mbowe wasema, “YES Zanzibar”Ni Fitna tu inayowahujumu Masheikh
Walioshambulia Kenya niMujahidina au al Shabab?
Uchochezi wote huu kwa lengo gani?Kasema kweli Waziri wetu Nchimbi…Tuwe makini, watu wengine nuksi
Picha kulia/kushoto, moja ya harakati za kuokoamateka katika shambulio la kigaidi Nairobi, Kenya.
Kesi ya ImamHamza yaanzakusikilizwa
Uk. 12
 
2
AN-NUUR
DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT. 27 - OKT. 3, 2013
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.t
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofsi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Makala/Tangazo
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza program maalum yamaandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2014.Program hii itaanza tarehe 16/09/2013 hadi tarehe 16/12/2013. Jumatatuhadi ijumaa kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 9:00 Alasir.
Masomo yatakayofundishwa ni:-
Elimu ya dini ya Kiislamu, English language, Lugha ya kiarabu, basicMathematics na Computer. ADA: Ni Tshs
60,000/=
 
(Elfu sitini)
tu. Inalipwa yote kabla ya kuanza programu.Fomu za Kujiunga zinapatikana shuleni
BURE baada ya kulipa ada.
Mlete mwanao apate Elimu yenye tija itakayomweze kujiunga na kidato chakwanza.Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba:
0714 888 557/0712 974428
Wabllah tawfq
MKUU WA SHULE
Ubungo Islamic high School
P.o. Box 55105 Tel: 2450069, 0712 974428, fax: 2450822 Dar es salaam.E-mail:ipcubungoislamic@gmail.com
MAANDALIZI YA KUJIUNGA KIDATO CHA I, 2014(PRE- FORM ONE ORIENTATION COURSE)
Serikali yatakiwa kuchukua tahadhari
SERIKALI imetakiwakuacha kuwasakamaMasheikh hukuikiwaacha Wachungajiwakiingia na kufanyawatakavyo nchini,jambo ambalo ni hatarikwa mustakabali waTaifa.
Wito huo umetolewana viongozi wa diniya Kiislamu kwanyakati tofauti katikatiya wiki hii, kufuatiamalalamiko ya Wakristodhidi ya Wachungajiwao kutoka nchi za njewanaojishughulishana mambo ambayo nikinyume na sheria zanchi ikiwemo biasharaharamu ya dawa zakulevya.Akizungumziasuala hilo, MaalimAlly Baswaleh, aliitakaSerikali iwe makini juuya madai ya wauminidhidi ya Wachungaji(Wahubiri) waowanaotoka nchi za nje nakuingia katika Makanisakwa kigezo cha kuhubiri.Maalim Bassaleh,alisema amesomakatika gazeti la HabariLeo, la Septemba 22,2013, ambalo limeelezakwamba hata viongoziwahusika katika idaraza Serikali zinazohusikana masuala ya Mamboya Ndani ya nchi naUhamiaji wamekirikupokea malalamiko yaWakristo hao.“Wamenukuliwawakilalamika kwambakuna baadhi yaWachungaji ambaowanatoka nje ya nchikisha wanasababishamigogoro ndani yaMakanisa. ZaidiWachungaji haokutoka nje ya nchihujishughulisha piana biashara ya dawaza kulevya.” AlisemaMaalim Basaleh.Mbaya zaidi Maalim,alisema kwa mujibuwa malalamiko yaWakristo hao nikwamba, Wachungajihao wanapata vibalivya kuwepo nchinina kujishughulisha nashuhughuli za kihubiripengine mpaka miakamiwili jambo ambalo nihatari kwa maslahi yaTaifa.Alisema, wachungajihao wa Kikristowanapoingia nchiniwamelalamikiwa kuwahupewa vibali namamlaka husika, akadiahali ni tofauti kwaupande wa Masheikhkutoka nchi za Kiarabu.“Kuna Masheikh wetukutoka nchi za Pakistani,India, Arabuni hufikahumu nchini kwa minajilihiyo hiyo ya kuhubiridini, lakini wanapoingiahupata misukosuko sanakutoka katika
idara hizoza Serikalini tofauti na haoWahubiri wa Kikristo.”Alisema Maalim Bassaleh.Alisema, kitendo hiki chakuwasakama Waislamuwaliopo ndani ya nchi auhata wale wanaoingia kwalengo la kuja kufundishadini, na kuwanasibisha namasuala ya kigaidi yanalengo la kuwapaka matopeku
liko uhalisia wake.Alitolea mfanotukio la mlipuko wa bomu Kanisani katikamji wa Arusha, hivikaribuni kwamba baada ya vyombo vyausalama kuwakamataraia wa Kiarabukabla ya uchunguziwakanasibishwa naugaidi.Kwa mujibu wa gazetihilo la Habari Leo,limemnukuu msemaji waIdara ya Uhamiaji nchini,
Na Bakari Mwakangwale
TUNACHUKUA fursahii kuwapa pole jiranizetu Kenya kwa mkasamzito uliowapata wakushambuliwa katikaduka kubwa (ShoppingMall) la Westgate mapemawiki hii.
Aidha tunawapa polewale wote waliopotezandugu zao katika tukio hilona kuwatakia kila la kheriwote waliojeruhiwa katikamkasa huo na MwenyeziMungu awawezeshewapone haraka na kurejeakatika hali ya afya njema.Wakati Kenyaikikumbwa na tukio hilila utekaji na mauaji yawatu wasio na hatia,mataifa mengine yana chakujifunza kupitia mkasahuu, hususan hapa kwetuTanzania.Kwa muda mrefuvyombo vyetu vya usalamavimekuwa vikifanya mzahana matukio ya kigaidi kwakuhusisha ‘vitendo vyauhalifu uchwara’ na ugaidi,huku uhalifu wenyeweukichagizwa na kukuzwana porojo za baadhi yavyombo vya habari.Wakati mwinginevyombo vyetu vya habarihuzusha tuhuma za kigaidinchini kwa sababu tu yachuki za kiimani au kwalengo la kuuza nakalanyingi.Ni jambo lililo wazikuwa mara nyingihabari za ugaidi nchinihuwa zinaripotiwa kwakunasibisha na Uislamu au jamii ya Waislamu.Lugha ugaidi, Al Qaeda,Mujahidina, Siasa kali,Al Shabaab n.k. imekuwaikitumiwa na baadhi yavyombo vya habari navyombo vya dola kamasilaha muhimu yakuituhumu na kuichafua jamii ya Waislamu hapanchini, hata kwa matukioyasiyofanana kabisa navitendo halisi vya kigaidi.Mfano mzuri ni uzushiuliofanywa dhidi yaChuo cha Kiislamu chaAljaazira kule visiwaniUkerewe Mwanza,ambapo zilizushwa na
Poleni wana Kenya
Watanzania bado wanafanya mzaha
kutengenezwa habarikatika gazei moja la kilasiku kwamba chuo hichocha Kiislamu, kinatoamafunzo ya Ugaidi.Aidha gazeti hiloliliongeza kuwa nyakatiza usiku huwa wanaingiawageni wasiofahamikachuoni hapo kwa mitumwiwakiingiza silaha!Mizaha ya mana hiiimekuwa ikifanywamara nyingi na vyombovya habari nchini, nahaishangazi kuona vyombovyetu vya dola, navyo bila hata kuhoji kwa kinawachocheza wa habari hiziza kizushi na kuthibitishahabari zao, navyo huingiakatika mkumbo huo huowa propaganda na wakatimwingine kuwaingizawasiokuwa na hatiamatatani.Pengine hii mizahaya ugaidi imekithirihapa kwetu kwa kuwahatujaonja hasa ladha halisiya ugaidi unaozungumzwaduniani zaidi ya kusikia tukwa wenzetu.Tukio la Westgateni funzo murua kwayeyote mwenye akili naanayejifunza.Kama tutakuwatumejifunza kupitiaWestgate, hatudhanikwamba mchezo huutuliouzoea wa kuzua habariza kupika juu ugaidi hapanchini, utaendelea.Na kama bado wapowenye agenda zao kupitialugha za ugaidi, Al Qaeda,Al Shaabab hapa nchini,hatuwezi kusema, wanahiari ya kuendelea naagenda zao (maana sikio lakufa huwa halisikii dawa).Hatuwezi kusema hivyokwa sababu kila mchuma janga hula na wakwao. Janga likija litatuangamizasote. Kwa hiyo, tutaendeleakufichua na kuzisemeapropaganda za namna hiiili kuinusuru nchi yetu na balaa la kupandikiziwakitisho bandia cha ugaidi.Hatma ya kitisho bandia,ni kuletewa ugaidi halisi.Kamwe hatutachokakutekeleza wajibu huu wa
kuchua propaganda hizi
chafu.
 
3
AN-NUUR
DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT. 27 - OKT. 3, 2013
Habari
 Vyombo vya habari vinaitisha Tanzania
TAARIFA zilizotawalabaadhi ya vyombo vyahabari jana, zilikuwa zile zakitisho cha A-Qaida na AlShabab. Kwamba Tanzaniainakabiliwa na kitisho chaAl Qaida.
“Al-Qaida yatishaTanzania: Watanzaniawapewa mafunzo ya ugaidinje.” Ndivyo lilivyoripotigazeti la Mtanzania.“Hofu Afrika Mashariki:Mtandao wa kigaidi wazidikujitanua, kutawanya‘sumu’.”Lilidai gazeti la Rai nakuongeza kuwa Uhusianowa Uamsho na MombasaRepublican unatia shaka.“Wakati wananchi waAfrika Mashariki wakijawana hofu ya mashambulioyanayopangwa kufanywana vikundi vya ugaidi vyaAl Qaida na Al Shabab,imebainika kuna Watanzaniawaliopewa mafunzo yaugaidi wanaojiandaa kufanyamaovu.” Limesema gazeti laMtanzania jana.Pengine kabla yakuchambua habari hizotuseme yafuatayo. Aprili 5,1986 watu watatu waliuliwana wengine 230 kujeruhiwavibaya katika shambulio la bomu lililofanyika katikaukumbi wa starehe, LaBelle discothèque Berlin,Ujerumani Magharibi.Haraka haraka ililaumiwaLibya na Rais RonaldReagan akaamuru Tripolina Benghazi ipigwe kamanamna ya kulipiza kisasi.Katika shambulio hilo, watu30 waliuliwa wakiwemo wa
familia ya Muammar Gadha.
Masaa mawili mara baada ya shambaulio hilo,Rais Ronald Reagan katikahotuba yake kwa taifa kupitiatelevisheni alisema kuwaaliamuru shambulio hilo kwasababu alikuwa na ushahidiwa uhakika ("direct, preciseand irrefutable" proof),kwamba Libya ilihusika na bomu lililolipuliwa
La Bellediscothèque.
Hata hivyo, mwaka 1998televisheni moja ya Ujerumani,Zweites Deutsches Fernsehen(ZDF television), ilitoa
documentary, iliyochua nani
hasa alihusika na tukio hilolililofanywa kisingizio chakuipiga Libya. ‘Documentary’hiyo iliyorushwa hewani natelevisheni (German publictelevision) Agosti 25, 1998,ilifichua mambo ambayo,haikuwahi kufikirika,na wakati mwinginekuwa vigumu kuaminikakama sio kwa ushahidimadhubuti uliotolewakatika documentary hiyo(msomaji anaweza kuirejeaau kusoma yaliyoripotiwakatika jarida,
Frontal
 ,. kuonakilichokuwepo).Lakini la muhimu zaidikwetu ni kuwa documentaryhiyo ilitolewa wiki tatumara baada ya shambulio lakigaidi Tanzania na Kenyatukio ambalo, lilikuwa mojaya visingizio vya Rais BillClinton kuipiga Afghanistanna Sudan. Ilidaiwa katikashabulio lile kuwa wakatiAfghanistan ilikuwa ikitoamafunzo kwa magaidiwalioshambulia balozi zaMarekani Dar es Salaam naNairobi, Sudan ilikuwa nakiwanda cha silaha za sumu.
Na Omar Msangi
Pamoja na maengiyaliyofichuliwa,kuchambuliwa na kuelezwana Jarida,
Frontal,
muhimu nikuwa huenda waliotuhumiwa
na kukishwa mahakamani
walikuwa watu wasio husika,
lakini waliotumika tu kucha
ukweli na kwamba wahusikahasa ni watu wanaozitumikiataasisi kubwa kubwa zakikachero za nchi fulani.Lakini pia inaelezwakuwa, maadhali Reaganalisema kuwa alikuwa naushahidi madhubuti, wakatihaukuwepo, inatiwa wasiwasipia kuwa hata kinachoitwa nimagaidi waliopo Afghanistanwaliodaiwa kushambulia aukutoa mafunzo kwa watuwalioshambulia Dar naNairobi, inaweza kufuatamkondo huo huo wa kutafutamtu wa kumbebesha lawama.Kama anavyoarifuripota kutoka Ujerumaniakichambua taarifa ya
Frontal
ni kuwa alisubiri sana kwahamu kuona kuwa vyombovikubwa vya habari kamaCBS, NBC, ABC, CNN aumagazeti yao, yatagusiahabari hiyo muhimu ya
Zweites Deutsches Fernsehen
(ZDF television), lakini vyotevilipiga kimya!Katika lile shambulio lakimeta, magazeti yalipigasana zumari yakidai kuwawahusika ni Al-Qaida. Gazetila The Guardian likaripotilikidai kunukuu taarifa zawanasayansi wa Kimarekaniwakisema kuwa kimetahicho kimetoka Iraq. Jaridala Wall St. Journal, nalolikatoa tahariri ndefu likisemakuwa wanaoishambuliaMarekani kwa kimeta ni Al-Qaida na kwamba kimetahicho kimetoka Iraq. Hiyoikafuatiwa na maelezo yammoja wa wabunge namwanasiasa mashuhuriwa Marekani, John McCainakizungumza katika kipindicha televisheni (Late Showwith David Letterman)akisisitiza madai ya kuitiahatiani Al Qaida na Iraq.(Tazama:
 Jump up to: "ANation Challenged: The Inquiry;Experts See F.B.I. MisstepsHampering Anthrax Inquiry".The New York Times. October9, 2001. Retrieved 4 October2011.Jump up ^ "FBI was told toblame Anthrax scare on Al Qaeda
by White House ocials". New
York Daily News. 2 August 2008.Retrieved 26 December 2012. Jump up ^ "Iraq 'behind USanthrax outbreaks'", David Roseand Ed Vulliamy, The Guardian,October 14, 2001 (4) Jump up ^"The Anthrax Source". The WallStreet Journal. October 15, 2001.Retrieved 10 October 2011.Jumpup ^ One Month After 9/11, McCain Said Anthrax 'MayHave Come From Iraq,' WarnedIraq Is 'The Second Phase'",thinkprogress.org, August 1,2008. (6) Jump up ^ "Bentonite".CBS News. August 2, 2008.Retrieved 29 March 2011.Jumpup ^ "Mylroie: Evidence ShowsSaddam Is Behind Anthrax Attacks", Jarret Wollstein, )Newsmax.com, November 9,2001)
Hizo zikawa ndio habarimashuhuri katika vyombovya habari ambazo zilidakwapia na huku kwetu. Sasa rejeakatika taarifa ya FBI kuhusianana uchunguzi waliokujakufanya (FBI: Famous Cases& Criminals, Amerithrax orAnthrax Investigation.) uoneukweli ulivyokuwa.Mwandishi WaseemShehzad akiandika kuhoji, ninani Al Qaida anasema kuwakinachoshangaza ni kuwahawa wanaoitwa Al Qaida, baadhi yao ndio waliotumiwana Marekani katika kumng’oamadarakani kiongozi wa
Libya Muammar Gadha na
sasa wanatumika tena Syria.Akinukuu taarifa ya taasisimashuhuri ya Kimarekani,ambayo ni moja ya taasisimuhimu zinazofanya kazikama
“think-tank”, The Councilon Foreign Relations,
anasemakuwa isingekuwa kuingiana kutumia al-Qaeda katikauasi Syria, waasi (The Syrianrebels) wanaotaka kumng’oaBashar al-Asad, yaani, FreeSyrian Army (FSA) “would be immeasurably weakertoday without al-Qaeda intheir ranks.”Ufupi wa maneno,
Councilon Foreign Relations
(yaMarekani) inasema kuwawaasi wa Syria wanahitajimsaada wa Al Qaida. “FSAneeds al-Qaeda now.”Na ndio maana unaonakuwa Al Qaida hao wanapewakila msaada na Marekani ili tukutimiza lengo la kumng’oaBashar al-Asad.Ni katika mazingira nahali kama hiyo, mwandishiWaseem Shehzad anahoji,“Need one say more about theclose links between the US anal-Qaeda?”Kwamba kunahitajikakusemwa nini zaidi kuonyeshauhusiano uliokuwepo kati yaAl Qaida na Marekani?Desemba 2008 mwandishiGregory F. Fegel aliandikamakala akihoji, nani Al Qaida(What is Al Qaeda?).Fegel anasema hawawanoitwa Al Qaida leo, niwapiganaji na Mujahidinaambao walipigana vitaAfghanistan kuing’oa Urusi yawakati huo, USSR, ilipovamianchi hiyo. Kulingana na siasaza wakati ule za mataifamakubwa mawili duniani(super powers) yaliyokuwayakishindana na kukamiana,Marekani ilisimama upandewa mujahidina kuwasaidiakumpiga Mrusi, ikiwa nipampoja na kutoa mafunzo,silaha na fedha. Nchi za SaudiArabia na Pakistan zilitumikasana katika zoezi hili.Hata hivyo kwa upandemwingine, Marekani ilikuwana tatizo moja, kuwa hawawatu wanaopewa mafunzo nakupigana Jihad ya kumpigaMrusi, wanaweza kuwa hatarihapo baadae kwa masilahi yaMarekani. Kwa hiyo ikawa nilazima kuweka kumbukumbuza kuwafuatilia watu hawa(data-base). Al-Qaida ni nenola Kiarabu lenye maana, “The base”. Kwa hiyo lilitoholewakutoka ile data-base yawapiganaji waliotumiwakumpiga Mrusi. Na hao ndiowanaodaiwa kuwa Al Qaidaambao hivi leo wanaonekanawakitumiwa kule Libya,Syria na hata kuhusika katikamatukio yanayoitwa yakigaidi, iwe kwa mmoja waokuhusika kupiga au kupigwana watu wengine, halafuikadaiwa kuwa ni Al-Qaida.Ni katika mazingira kamahaya mwandishi anasemakuwa,
“Al Qaeda is nothing morethan a bogey man, an invented ghost to frighten children andthe ignorant. Al Qaeda is theinvisible and nonexistent enemythat the US government hasmanufactured to provide anexcuse for its never-ending 'Waron Terrorism', which is in realitya war of US aggression for USdomination of the world and itsresources.”
Huko nyuma vyombo vyahabari viliwahi kusambazahabari za kutisha kuwagaidi Fazul aliyedaiwakushambulia Nairobiameingia Tanzania tayarikwa kufanya mashambulizi.Watu wakatakiwa kuepukamaeneo yenye mikusanyikomikubwa ya watu kamasokoni Kariakoo. Polisi naowakatamba wakisema kuwawamemzingira gaidi huyohatari kwa kusiriba mipaka,hana mahali pa kutokea.Mpaka leo polisi wala vyombovya habari havijatufahamisha,‘hadisi’ ya Fazul imeishiawapi. Aliwezaje kupenyana kuondoka nchini bilakukamatwa?Ni katika kipindi hichohicho baadhi ya magazetiyaliripoti juu ya magaidiwanaohusiana na Fazul,wenye asili ya ‘Kiburushi’walivyoingia nchini kuwindawanyama katika mbuga zetukwa ajili ya kuwapelekeakitoweo magaidi wa Al Qaidawaliopo mafunzoni katikamapango ya Kandahar.Hakuna hata mtu mmojaaliyekamatwa kuhusiana nahabari hizo za kuwatishawananchi, wala haikuelezwaimekuwaje magaidi haowaliweza kuwakwepa
maosa wa uhamiaji, polisi,
wana-usalama na askari wawanyama pori, wakawindana kuondoka na kitoweo bilaya kukamatwa!Leo tena magazetiyanatuambia kuwa Al-Qaidayaitisha Tanzania na kwamba“Watanzania wapewamafunzo ya ugaidi nje”.Na Mkuu wa InterpolTawi la Tanzania, KamishnaMsaidizi wa Polisi (ACP),Gustav Babile akanukuliwaakisema kuwa Polisi inajuakuwa wapo Watanzaniawanaopewa dozi ya ugaidi nakwamba Polisi wapo machokukabiliana nao.Gazeti la Mtanzaniambalo limeipigia ngomasana habari hii ya kitishocha Al Qaida Tanzania,ndio hilo hilo ambalo hivikaribuni liliandika habarindefu kuhusu Chuo chakutoa mafunzo kwa magaidikilichopo katika moja yavisiwa vya Ziwa Victoria kuleMwanza.Katika kutoa picha jinsiwakufunzi wa ugaidi katikachuo hicho walivyo kuwawatu hatari, Mtanzania lilitoamichoro kuonyesha jinsimagaidi hao walivyochaguamahali pa kuweka chuochao mahali ambapo si
rahisi kukwa na watu (hata
Polisi/Usalama wa Taifa)akisahau kuwa Chuo hichokimesajiliwa na baadhi ya
watumishi wa Serikali huka
hapo mara kwa mara kwa
shuguli za kiosi.
Labda kabla ya kuendelezakitisho hiki kipya chaugadi, gazeti la Mtanzanialingetufahamisha kwanza kilechuo cha magaidi, AljazeeraIslamic Centre, kinaendeleajena ile kesi iliyofunguliwa nawahusika wa Chuo hicho
imekia wapi.
Gazeti la Mtanzania katikatoleo lake la 13 Februari,2013 na 20 Februari,2013, lilichapisha habarilikidai kuwa chuo hichokinafadhiliwa na magaidiwa Al Shabab na kwamba
Inaendelea Uk. 4
 MAJERUHI akiokolewa kutoka duka la Westgate, Nairobi, Kenya.

Activity (5)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 thousand reads
1 hundred reads
mgayasudi liked this

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->