You are on page 1of 5

1

TAARIFAYAZITTOZUBERIKABWE(MB)KUHUSUKUVULIWANAFASIZA UONGOZINDANIYACHAMACHANGUCHACHADEMA 1. Utangulizi i. Katika kikaochake cha sikumbilikilichofanyikatarehe 20 22Novemba2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasizangu zoteza uongozi ndaniyachama. Kwa mujibu wataarifa yachama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk KitilaMkumbo ni uhaini nahujumakwachamakutokananawarakaunaojulikana kama mkakati wauchaguzi2013.Ukwelinikwambawaraka uliotajwasisababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha KamatiKuu .Sababuzakufukuzwakwangu kamazilizojadiliwakatikakikaocha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwandaninanjeyavikaovyachama.Hitimisholatuhumahizinikwamba miminimekuwanikikisaliti chama kwakutumikanaCCM naUsalamawaTaifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikaombalimbalivyama.

ii.

Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sanasasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwambamimi ZittoZuberi Kabwesitokuwa chanzocha CHADEMA kuvunjika.Hiki ndicho chama kilichonileana kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiungana siasaaingie CHADEMA.Bado nina imanikubwa na chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana, leonakesho.

2. Kuhusutuhumambalimbalizinazoelekezwakwangu Zipo tuhumanyingiambazozimekuwazikirudiwarudiwakatikavikaovyachamana nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu. Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa

nikizijibukatikavikaombalimbalivyachama.

i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguziwamwaka2010.Ningependakuelezayafuatayokuhusujambohili: MiminilikuwamgombeawaubungekatikaJimbolaKaskazinihukoKigoma. Pamoja na kuwa mgombeawa ubunge,nilifanyakampenikatikamajimbomengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa.Hakunakiongoziyeyotewajuualiyefanyakampenikatikamajimbo mengikamamimi,ukiachamgombeaurais. Kotenilipopitanilimpigiakampeniwagombeawetuwaudiwani,ubungenaRais. Katika MkoawaKigomanilizungukanamgombeauraiskatikakatazotezaKigoma KaskazininamajimboyotemananeyaMkoawaKigoma.

ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli nikwamba niliwapigia sanakampeni wagombea wetu,na hivyondivyo wapiga kurawaKigomawalivyoamua.

iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini. Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama nawatoa tuhumawajenaushahidibayanawajambohili.Si afya kwachamakuendeleakurudiarudiatuhuma hizi kila mara tangu mwaka2010bila uchunguziwowotekufanyikanajambohililifikiemwisho.

iv)Tuhumakwambanimekuwasishirikikatikaopereshenimbalimbalizachama:Ukweli ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwanaopereshenikubwa katika mikoaya Kanda yaNyanda za JuuKusini na nilikwendakatikamikoayotetuliyotembelea.Mwaka2012

baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012 kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi. Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchiniMarekanikufungua matawi kwa mwalikowaWatanzaniawanaoishihuko.

v) TuhumakwambanimekidhalilishachamakwatamkolaPACkwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae. Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja naCCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusujambohilinikamaifuatavyo: Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuoneavyamavingine.Kufanyahivyonikuendelezatabiazilezile ambazotunazipinganaambazotunapiganiakuzibadilisha Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa yakisheria ni kwamba mahesabuyavyamavyasiasa hayajakaguliwanaCAG,nahilinikosalakisheria,bilakujalikosahilinilanani.

vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho zaVikao Mtakumbukakwamba mimi nilikataakuchukua poshotangumwaka 2011kamaishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamowa chama chetu wakupingaposho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 20102015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidikatika mashirikayaumma ambapo mimini mwenyekiti wakamatihusika.Ninapendakuelezayafuatayokuhusujambohili: Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu

mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria.Mtuyeyotemwenyeushahidivinginevyoauwekehadharani. Swalala kukataaposho(sittingallowance)niswalalakiilanikatikachamachetu, na kwangu ni swala la kimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni1900 kati ya wanawake100,000wenyeujauzito. Vifo hivi vinatokana naukosefuwa huduma kwasababuyabajetifinyu.Ndiyomaananilifurahisanakwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidiasanakupatikanafedhaambazozingeokoavifovingivyakinamama. Jambohilisi suala la ugomvi baina yangu naMheshimiwaLema.Nisualala msingikatikachamachetu.

3.UsambazajiwaRipotiyaSirikuhusuZittoKabwe Hivikaribunikulisambazwa warakaunaoitwaripotiyasirikuhusumimiukibebalundola tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA. Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibuyaviongozi wachamailikuwani kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchangowangunililalamikiamambomatatuyafuatayo:

i.

Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwahatuakwamujibuwataratibuzachamachetu.

ii.

Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika nawarakahuu,nitaendeleanataratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile wanachukuliwahatuastahikizakisheria.

4.Hitimisho a) Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania. Natambuapia kwamba, kamailivyokawaidawakatiwamigogorokatikavyamavya

siasa hapaTanzania,kunawatuwalitegemealeoningetangaza'maamuzimagumu'. Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. Napenda wanachama waCHADEMAnawapenda demokrasia nasiasasafiwotenchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwahiari yangu. Nitafuata taratibu zotendaniyachamakatikakuhitimishajambohili.

b) Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenyematarajionaimanikubwakwachamachetu.

c) Kamamwanasiasakijana niliyekaakatika siasa kwa mudasasayapomengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanyakisiasakatikamaishayanguyasiasa.

d) Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia. Kama alivyopata kunena mmoja yawanasiasamaarufu,'kiwangochajuukabisachauzalendokatika nchi nikukubali kutofautianakimawazo', na ninatamani huu ndio uweutamaduniwa chamachetu.

KabweZuberiZitto,Mb DaresSalaam. 24Novemba,2013

You might also like