You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Maoni ya Waislamu yatupwa rasimu Katiba Mpya

ISSN 0856 - 3861 Na. 1106 RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA , JANUARI 3-9, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Somalia wamekwama wanahitaji kusaidiwa


Wameshika bendera ya Uislamu Lakini wapo vitani wanauwana Swali la msingi: Wanasaidiwaje?
Habari Uk. 6

Habari Uk. 3

Jussa, Eddy wataka Masheikh waachiwe


Na Alghaithiyyah Zanzibar

ISMAIL Jussa Landu.

Serikali yakiri kutambua changamoto wanafunzi Waislamu

MWAKILISHI wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar (CUF), Ismail Jussa Landu amesema ikiwa kweli serikali ya umoja ya kitaifa inataka kuonekana kuwa inaheshimu utawala bora na haki za binaadamu, itende haki kwa kuwapa dhamana na kuwaachia Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) waliowekwa ndani zaidi mwaka sasa. Habari kamili Uk. 12

PICHA juu: Wanajeshi wa Al Shabaab wakiwa katika mstari tayari kwa mapambano dhidi ya kikundi cha Ahlu Sunna wal Jamaa (wanaonekana katika picha chini). Wote hawa bendera zao zina Laailha ilallah, lakini wanapigana, wanauwana. Soma uk. 6, 7.

Habari Uk. 3

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Habari
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


ya kuleta ghasia katika nchi ili hatimaye yatokee yale ya Congo (DRC), Afrika ya Kati, Pakistan, Yemen na Somalia. Kwa Rwanda, ilikuwa Wahutu na Watutsi. Kwa Tanzania itakuwa kama Seleka na antibalaka. Hii ndiyo tahadhari tunayoendelea kuitoa na hatutachoka kwa sababu ni wajibu wetu wa Kidini na kama wazalendo wa nchi hii. Hii ni Jihad yetu tuliyoipa kipaumbele kwa sasa na tunaomba na kutaraji Tawfiiq ya Allah katika kulifanya jambo hili. Quran inatuuliza hamfikiri, hamuoni? Katika semina moja wiki iliyopita, lilielezwa tukio moja ambapo walifika watu Bukoba wakajitambulisha kuwa wao ni Al Shabab na wanatafuta vijana wa Kiislamu wa kuwapa mafunzo ili wakashiriki Jihad Somalia. Baadhi ya Waislamu walishtuka wakawaripoti Polisi wakakamatwa. Hata hivyo, inasemekana kuwa watu hao waliachiwa kimya kimya na hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi yao. Katika hali hii, ambayo nchi yetu ipo katika AMISOM na katika hali hii ambayo kila mara vyombo vyetu vya dola vinatoa tahadhari juu y a Al S h a ba b ka m a magaidi: Swali ni je, nini unatarajia kusikia kutoka vyombo vya dola wakikamatwa watu kama hawa. Lakini kwa mujibu wa msimulizi, waliachiwa kimya kimya na akasikia wameibukia Mbeya katika Tabligh! Kilielezwa pia kisa cha mtu mmoja aliyeingia Singida na kudai kuwa yeye ni afisa wa jeshi mstaafu mwenye uchungu na madhila wanayofanyiwa Waislamu Tanzania na duniani. Akasema, anataka kukusanya vijana kuwapa mafunzo ya kijeshi ili kuja kupigania haki za Waislamu. Kweli akapata vijana akaanza kazi ya kupeleka vijana porini kufanya mazoezi. Lakini wakapatikana watu wenye busara wakajiuliza maswali mengi bila kupata majibu. Afsa wa jeshi si mjinga. Anajua nchi zinavyofanya kazi, anajua vyombo vya dola vinavyofanya kazi. Lakini anajua pia hatari ya jambo analofanya kwa nchi kama hii na kwa nchi yoyote dunianikwamba hiyo ni sawa na kuunda kundi la waasi na hivyo anajua fika hatari yake na matokeo yake. Sasa inakuwaje huyu asiwe na wasiwasi kabisa? Wakastuka, wakaingilia kati mtu yule akatoweka, lakini alishakumba vijana. Watu kama hawa, wakati mwingine kupitia kwa watu tunaowafahamu kuwa ni maustadh wetu, wanaharakati, ndio hivi sasa wanafanya harakati kubwa na michakato ya kukusanya vijana kuwatia katika mfumo wa maisha wa kuishi kambini kujiandaa na agenda ambayo haipo wazi hadi sasa. Lakini wanapokamatiwa, ni kujiandaa kwa Jihad. Labda tuseme kwa lugha ya wazi kabisa: Jamani tukikubali kufanyika mambo kama haya, ndio baadae utasikia kuna watu wamelipua mahali, iwe ni Msikiti, Kanisa, kituo cha Polisi, halafu inadaiwa kuwa waliofanya ni magaidi wa Kiislamu. Na utapatikana ushahidi wa vijana kama hawa waliokusanywa wakapewa mafunzo na hawa leo wanaojiita kuwa ni Maafisa jeshi wastaafu wenye uchungu na Uislamu! Hatuna akili? Hatufikiri? Hatufamu mambo? Hatusikii yanayotokea Nigeria, Yemen na Pakistan? Kama tumefikia mahali pa kutokuwa na akili kiasi hicho, tukaona kuwa tuunge mkono mtindo wa vijana kutoweka shuleni, vyuoni na katika shughuli zao za kimaisha wakapewe mafunzo na watu kama hawa walioibuka Bukoba na Singida, basi tumestahiki kuingizwa katika lile kundi linalotajwa katika Quran pale iliposema: Na bila shaka Tumewaumbia Moto wa Jahanamu wengi katika majini na wanadamu (kwa sababu hii): Nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo, na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama; bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (7:179) Sasa kama pamoja na neema ya akili na milango ya fahamu aliyotupa A l l a h , t u m e s h i n dwa kuyatizama mambo haya na kuyapa tafsiri sahihi tukachukua tahadhari, basi tutakapojitia katika jahanamu ya hapa hapa duniani, tusijemlaumu mtu wala kutafuta mchawi. Mchawi ni ujinga wetu wenyewe.

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Tunachopinga ni kutumiwa kujiangamiza sisi wenyewe


KATIKA miaka ya 1980s/90s ilipokuwa imeshamiri minakasha ya Ansaar Sunna na watu walioitwa wa Maulid, baadhi ya Masheikh badala ya kusema hawa wanakataa Maulid, wanasema hawa Ansaar wanapinga kuswaliwa Mtume Muhammad (s.a.w). Katika kukoleza hoja zao wanasema, Quran inasema kuwa Mwenyezi Mungu mwenyewe na Malaika wake wanamswalia Mtume, kisha wanasoma ile aya inayosema: I n n a l l a h a wamalaaika tahuswalun ala n nabii, yaa ayuhal ladhiina aamanu s swalu alaihi wasalim tasliimaa.. Tafsiri na picha waliyokuwa wakitaka kuifikisha kwa Waislamu ni kuwa hawa Ansaar wanapinga Quran, wanapinga amri ya Mungu. Yote hii ili Waislamu wawachukie na wasiwakubali. Wawaone kuwa ni wapotoshaji. Wamekuja na dini mpya inayopinga kuswaliwa Mtume!!! Lakini yupo Ansaar Sunna anayekataa kumswalia Mtume? Jayupo. Ubishi haukuwa katika kumswali Mtume, bali namna ya kumswalia. Kwa matoleo kadhaa ya gazeti hili, tumekuwa tukitoa makala kutoa tahadhari kuwa watu wawe makini, wasije wakaliparamia jambo na kulishabikia, kumbe lina madhara. Na kubwa ikazungumziwa hali inayoendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati, Syria na Somalia. Swali likawa je, hali ya machafuko na vita inayoendelea huko inaweza kuitwa ni Jihad? Kwa Afrika ya Kati jawabu linaweza kuwa jepesi sana kwa anayetaka kujua ukweli. Ukifungua mitandao mbalimbali ya habari utaona picha za askari wa Seleka wanaodaiwa kuwa ni wapiganaji wa Kiislamu-utaona baadhi ya wapiganaji hao wakiwa ni wasichana waliovaa bukuta/pensi

na T-Shirt, matiti nje. Sasa huwezi kusema mpiganaji wa namna hiyo anapigania kusimamisha Uislamu. Anaweza kuwa Muislamu, lakini hapiganii Uislamu. Ndio pale ikasemwa kuwa kinachoendelea Afrika ya Kati ni Civil War, ila imetumbukizwa chuki za kidini, sasa yamekuwa ni mauwaji ya Waislamu na Wakristo. Kwa upande wa Syria na Somalia, hili gumu kidogo kuwa na jibu la wazi kwa tulio wengi. Linahitaji uchambuzi wa kina na akili ya kutizama mambo kwa undani na kwa mapana. Sio kwa uoni finyu. Muhimu tunachosema hapa ni kuwa kamwe hoja haijawa Jihadkwa maana ya kukubali au kukataa. Hoja ni tahadhari. Ukisema nakwenda Jihad, iwe kweli unachofanya ni Jihad. Kama mtu anaamini kuwa Syria/Somalia kuna Jihad na yeye kama Muislamu anawajibika kwenda, na mazingira yana mruhusu kwenda, basi afanye safari aende. Asiache kwenda kwa kutoa kisingizio kuwa kuna watu wanapinga Jihad ndio wamemkwaza. Au kama anaona hawezi kwenda, lakini anaweza kutoa msaada wowote kwa namna yoyote, basi afanye hivyo. Quran inasema: Watasema: Mola wetu! Hakika tumewafuata mabwana wetu na wakubwa wetu, basi wao wametupoteza njia. Mola we tu ! W a pe hawa adhabu maradufu (kubwa zaidi) na uwalaani laana kubwa. (33:67-68) Na katika aya nyingine tunasoma: (Wakumbushe wakati) waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwisha kuiona adhabu, na yatakatika mafungamano yao. Na watasema wale waliofuata, Laiti tungeweza kurudi (duniani) tukawakataa kama

wanavyotukataa. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyowaonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao, wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni. (2:166167) Hoja ya msingi hapa ni kuwa hapatakuwa na utetezi kwamba mimi sikufanya jambo la kheri kwa sababu ya kupotoshwa na fulani. We ukiridhika kuwa jambo hili linafaa, fanya wala usitafute visingizio na kuleta malumbano kama yale ya kusema Ansaara wanapinga kuswaliwa Mtume, wakati wanachosema ni namna ya kumswalia. Ila sisi tutaendelea kutahadharisha kuwa hizi harakati za kuwatoa vijana katika shughuli zao za kimaisha, mashuleni na katika vyuo, eti wakaishi maisha ya kambi kwa ajili ya kujiandaa kusimamisha Uislamu, si sahihi na ni hadaa ya kuja kuwaangamiza Waislamu na kuivuruga nchi. Na harakati kama hizi haziwezi kuwa zimetokana na Waislamu, bali maadui wa Uislamu. Tumewahi kujiuliza vijana kama hao wakiibuka watakuja na agenda gani? Je, wakija na yale yanayotajwa kufanywa na Boko Haram, itakuwa ndio salama kwa Waislamu na Uislamu? Kutakuwa kunakalika? Je, yale yanayodaiwa kufanywa na Boko Haram, tunadhani kuwa kwa namna yoyote yanasaidia Uislamu? Basi tujue kuwa kila atakayekuja na agenda ya kuwakusanya vijana wa Kiislamu kuwapa mafunzo ya mwelekeo wa kimapambano, anacholenga ni kuzalisha watu ki-Boko Haram. Na huyu hawezi kuwa mtu mwema si kwa nchi wala Uislamu. Ni mamluki na wakala wa kuangamiza Waislamu na nchi. Ubaya wa jambo hili ni kuwa mawakala hawa ni watu wanaocheza na saikolojia ya Watu. Wanajua kuwa Waislamu wana malalamiko kinchi na kilimwengu na wanajua kuwa Waislamu ukiwaaminisha kuwa wanapigania Jihad, utawapeleka unavyotaka, hawarudi nyuma wala kuogopa chochote. Hapo ndipo wanapotupata Waislamu kwa wepesi mno na kututumia kwa masilahi yao. Tunaweza kusema kwa uhakika kuwa hawa ni mawakala wanaotumiwa katika kufanikisha ile agenda

Rasimu ya Katiba isipokidhi kukataliwa


Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi-CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama chake kitaendelea kusimamia misingi ya haki na usawa, ili kuhakikisha kuwa kila Mzanzibari anapata haki yake inayostahiki. Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameeleza hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara ya chama hicho uliofanyika viwanja vya Kinyasini, jimbo la Chaani. Amesema Chama hicho kitaendelea kuwa mstari wa mbele kudai mamlaka kamili ya Zanzibar, kwa lengo la kuhakikisha kuwa Zanzibar inaongozwa kwa misingi ya haki na usawa ili wazanzibari waweze kuamua mambo yao wenyewe bila ya kuingiwa na mamlaka nyengine. Hata hivyo amesifia umakini wa Kamati ya Maridhiano, yenye wajumbe sita wakiwemo watatu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watatu kutoka Chama Cha Wananchi-CUF, na kwamba wajumbe wa Kamati hiyo wameonyesha uzalendo wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao. Kwa upa nde wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Mzee Hassan Nassor Moyo, amebainisha kuwa mambo yanayodaiwa kutolewa katika orodha ya Muungano sio mageni, kwani yalikuwemo kwenye mamlaka ya Zanzibar kabla ya kuungana na Tanganyika mwaka 1964. Ameyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na sarafu, mambo ya nje na rasilimali za mafuta na gesi asilia. Aidha Mzee Moyo amewanasihi Wazanzibari kuepuka chuki, fitna na ubaguzi na badala yake waungane kupigania maslahi ya nchi yao. Alipongeza hatua iliyochukuliwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na mwenzake Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, ya kufikia maridhiano ambayo yamewaunganisha Wazanzibari. Naye Mjumbe wa Kamati hiyo ya Maridhiano Mansoor Yussuf Himid (CCM), amesema Zanzibar ni ya Wazanzibari wote na kwamba kila Mzanzibari anastahili kupata haki sawa na mwengine. Amesema kuwa ataendelea kuungana na Wazanzibari kupigania haki ya Zanzibar ndani ya Muungano, ili iweze kuendesha mambo yake yenyewe na kuwashajiisha vijana kutorudi nyuma katika kupigania haki hiyo. Akizungumzia kuhusu rasimu ya pili ya katiba iliyotarajiwa kuwasilishwa Desemba 30, 2013 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Himid alisema ikiwa rasimu hiyo haitokidhi angalau wastani wa matakwa ya Wazanzibari, hawatoikubali na wataikataa kabisa. Watu wa mjini huwa tuna wimbo tunasema supu tayari lakini tunasema ikiwa supu hii ya Jaji Warioba itapungua chumvi au pilipili manga tutaiongeza, lakini kama mbaya hailiki tutamuachia mwenyewe supu yake alidokeza Bw. Himid. Wajumbe wengine wanaounda Kamati hiyo ambao wote walikuwepo mkutanoni na kuzungumza ni Abubakar Khamis Bakar (CUF), Ismail Jussa Ladhu (CUF), Eddy Riyami (CCM) na Salim Bimani (CUF). Katika Mkutano huo Mhe. Maalim Seif alikabidhi kadi 459 kwa wanachama wapya walioamua kujiunga cha chama hicho, sambamba na kuweka mawe ya msingi katika matawi matatu mapya ya CUF ndani ya jimbo la Na Shaban Rajab

Habari/Tangazo

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014

AN-NUUR

Maoni ya Waislamu yatupwa rasimu Katiba Mpya


LICHA ya Waislamu, Jumuia na Taasisi zao kujitokeza kwa wingi kushiriki kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Kuratibu na Kukusanya maoni ya wananchi juu ya rasimu ya Katiba mpya, hakuna mahali ambapo maoni ya jamii hiyo yamezingatiwa na kuingizwa katika rasimu ya katiba hiyo. Hili limefahamika baada ya mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, kuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba na kuikabidhi kwa Rais Jakaya Kikwete, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Jumanne wiki hii. H a l i h i y o imewasikitisha na kuwahuzunisha baadhi ya viongozi wa Waislamu nchini, jambo ambalo

Chaani na kufungua barza ya vijana, iliyoyopewa jina la barza ya Maalim Seif Sharif Hamad, katika kijiji cha Bandamaji Chaani.

limeendeleza tafsiri ya kuendelezwa utamaduni wa kupuuzwa Waislamu katika mambo ya msingi na ya kisera nchini. Tumesikitika sana kuona kwamba maoni yetu hayapo. Maana ya Waislamu kushiriki kutoa maoni yao, ilikuwa ni pamoja na kusukumwa na fikra kwamba sasa mwarobaini wa matitizo yao ya kiimani
Inaendelea Uk. 4

Na Bakari Mwakangwale

Serikali yakiri kutambua changamoto wanafunzi Waislamu


mfumo wa ufaulu wa mitihani usiobadilika au kutofautiana baina ya somo na somo. Aidha Waziri Kawambwa, alisema Serikali imesisitiza matumizi ya alama endelevu Continuous asasment, katika matokeo ya mwisho ya mtihani wa mwanafunzi. Alibainisha kuwa suala hilo lilikuwa halitendeki na kusababisha mkaganyiko mwingi, hata hivyo alidai tatizo hilo halikuwa bayana na halikuwekwa wazi, yaani katika somo moja alama za kufikia daraja B zinakuwa tofauti na alama za daraja B za somo jingine na kwamba, hilo ndilo jambo lililokuwa likileta mfarakano. Kweli mambo haya yalikuwa hayaingii akilini, yaani yalikuwa si ya kitaalamu, palikuwa hakuna mlinganisho wa somo moja na jingine na sidhani kama kuna mahala duniani utaratibu kama huo unatumika, la muhimu zaidi ni uwazi katika tathimini ya mwanafunzi. Alisema Dkt. Kawambwa. Aliongeza kuwa mwanafunzi kama amesoma miaka minne, ukatumika ule mtihani wake wa mwisho tu, bila kutumia alama zake endelevu sio sahihi, kwani ni vigumu kujua siku hiyo ya kufanya mtihani wa mwisho mwanafunzi aliamka vipi, kwa kuwa inawezekana kijana akawa ni mzuri sana lakini asifanye vizuri katika mtihani wa mwisho. Dkt. kawambwa alisema kuwa tathimini ya mwanafunzi kwa miaka minne nyuma kulingana na taratibu zilizopangwa, zitamwezeshe mwanafunzi huyo kuchangia katika mtihani wake wa mwisho. Alisema huo ndio utaratibu ambao Baraza la Mitihani limeuchukua na ndivyo ilivyotangazwa. Alisema pamoja na kwamba kuna changamoto katika utekelezaji wake na baadhi hawajapendezwa na utaratibu huo, lakini Serikali inaendelea kushughulikia suala hilo katika namna ambayo muafaka unaweza kupatikana. Alisema kuwa ni mikakati ya serikali, ikiwezekana utaratibu huo utaanza kutumika NECTA mwaka huu. Utaratibu huo mpya ndio uliokuwapo tangu zamani na mabadiliko hayo yalifanyoka hapo katikati. Waziri alidai hata wakati wanasoma, utaratibu ulikuwa huo uliowekwa sasa. Aidha Dkt. Kawambwa alisema anatambua mchango wa Jumiya za Kidini ikiwemo TAMSYA, katika juhudi zao mashuleni, hususani katika suala la maadili, hasa katika kipindi hiki cha utandawazi. Alisema Utandawazi ni chamgamoto ni kubwa katika mmomonyoko wa maadili kupitia mipango mbalimbali, lakini asasi za dini za wanafunzi zimesaidia kuwafanya vijana kuendelea kulelewa na kubaki katika maadili yanayohitajiwa. Alisema Wizara yake imeshiriki mara kadhaa katika kuhakikisha madai

SERIKALI imebainisha kuachana na utaratibu wa awali wa kupanga alama za ufaulu kwa wanafunzi katika mitihani ya Taifa zilizo kuwa zikitumiwa na Baraza la Mitihani Taifa (NECTA). Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Shukuru Kawambwa, wakati akizungumza na wanafunzi wa Kiislamu katika Mkutano wao Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu (TAMSYA), mjini Bagamoyo. Dkt. Kawambwa, alisema Serikali imeshughulikia na kurekebisha taratibu za Baraza la Mitihani zilizokuwa zinasababisha mashaka mengi kwa wadau. Kuhusu Baraza la Mtihani (NECTA) Waislamu wamekuwa na malalamiko kwa muda mrefu kuhusu Baraza hilo, naomba nitumie fursa hii kwa niaba ya serikali, kwamba taratibu za utunzi na usahihishaji wa mitihani na kupanga matokea sasa umebadilishwa, ile dhana ya ubaguzi wa kidini au ukabila nadhani haitakuwepo. Alibainisha Waziri Kawambwa. Alifafanua kuwa moja ya masuala yaliyolalamikiwa sana na wadau wa elimu, ni utaratibu wa kupanga madaraja ya ufaulu unaobadilika mara kwa mara, yaani flexible grade range. Alisema katika kushughulikia hilo, kuanzia mwaka 2012 serikali iliamua kutumia

ya wanafunzi wa Kiislamu mashuleni yanasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi unaotakiwa. Alibainisha kwamba, Wizara yake imetoa nyaraka mbalimbali zikielekeza mambo muhimu yakiwemo, vipindi vya Dini mashuleni, uendeshaji wake, utaratibu wa mavazi kwa mabinti wa Kiislamu shuleni na nyakati za swala sambamba na mambo mengine yanayohusu Dini. Nikiri tu kama risala ilivyosomwa kwamba, nyaraka nyingine ni za muda mrefu, ni jambo la kibinadamu inawezekana sehemu nyingine zimeanza kusaulika na hazijulikani zipo wapi. Nikiri kwamba wakati wa kuhuisha nyaraka hizo umefika, ili ijuliakane kwamba serikali msimamo wake ni ule ule katika yale mambo ambayo ilikuwa imeelekeza. Alisisitiza. Waziri Kawambwa alisema nyaraka hizo ni juhudi za Serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa Kiislamu wakiwa ni sehemu ya jamii ya Kitanzania, wanapata fursa na stahili sawa katika kupata elimu, huku wakiendelea kuabudu kwa imani zao wakiwa masomoni. Hata hivyo, alisema Wizara yake inatambua kuwepo changamoto kadhaa kwa wanafunzi wa Kiislamu nchini katika vituo vya elimu, ambapo alidai uzoefu unaonyesha migogoro mingi inatokana na kukosekana mawasiliano ya kutosha kati ya walimu au viongozi na Taasisi za dini na wanafunzi mashuleni.

4
AHLU Sunna Waljama'a ni kundi la wapiganaji w a K i i s l a m u linaloundwa na watu wa Twarika (Sufis) ambao wanalipinga kundi la Al-Shabaab. Hawa wameshika silaha wakipigana na Al Shabab kwa madai kuwa hawa Al Shabab wakifanikiwa kushika nchi, wataifanya Somalia kuwa nchi ya Wahhabi. Wakati ule Somalia ikiwa imeshikiliwa na makundi ya wababe wa kivita, hawa ASWJ walikuwa wakishirikiana na mbabe wa kivita Mohamed Farrah Aidid. Hata hivyo wakati huo Ahlu Sunna Waljama'a hawakuwa ni wenye kusikika sana mpaka mwaka 2008 waliposhika silaha kupambana na alShabaab. Inaelezwa kuwa kilicholipua uhasama na vita kati ya Ahlu Sunna Waljamaa, ni kitendo cha Al Shabab kubomoa makaburi ya Masheikh na Makhalifah wakubwa wa-Kisufi katika maeneo wanayoshikilia. Katika mapambano y a o , A S W J , w a m e f a n i k i w a kuwatimua Al Shabab katika maeneo mengi ya katikati ya Somalia na kusini hasa kule Mudug, Gedo, Galgaduud, baadhi ya sehemu za Hiiraan, Shebelle ya kati na Bakool. Machi 15, 2010, Ahlu Sunna Waljama'a walifanya makubaliano na serikali ya Somalia ambapo walipewa wizara tano wachague watu kutoka kundi lao wawe Mawaziri. Walipewa pia nafasi za kidiplomasia na ndani ya vyombo vya usalama. Kwa upande wake wapiganaji wa ASWJ walikubali kuendelea kushirikiana na jeshi la serikali dhidi ya alShabab. Katika jumla ya mapambano ya makundi haya mawili ya Kiislamu yaliyoacha mamia kwa makumi ya askari wa pande zote mbili wakiuwana halikadhalika raia wasio na hatia, ni pamoja na l i l e l i l i lopelekea Ahlu Sunna Waljama'a kutwaa Dhuusamareeb kule Galguduud kutoka mikononi mwa Al Shabab. Hiyo ilikuwa

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


kujielimisha juu ya dini yao halikadhalika mapambano wakiuwana na kutiana vilema Waislamu ambao wote katika uwanja wa mapambanao wanapepea bendera yenye Kalima ya Laa ila hailallah Muhammad Rasuulullah! Kabla ya kuanza mapambano na Al Shabab, Masheikh wa Twarika (Sufis)--Ahlu Sunna wal Jamaa, walifanya mkutano Nairobi, Novemba 2009, ambapo ndipo lilipopitishwa azimio la kushika silaha. Chini ya Uenyekiti wa Sheikh Sheikh Sharif Sheikh Muhieddin, makundi mbalimbali ya Twarika yaliwakilishwa katika mkutano huo, wote wakiwa na mtizamo mmoja wakidai kuwa Al Shabab wanapotosha Uislamu. Sheikh Sharif Sheikh Muhieddin anasema Al Shabaab ni watu waliopotoka ambao wamefahamu vibaya maadili ya Kiislamu. Alisema hayo wakati akiongea na vyombo vya habari mara baada ya mkutano huo. Katika jumla ya madai yanayoletwa dhidi ya Al Shabab, ni kuwa na msimamo unaoweza kusema ni Inaendelea Uk. 8

AN-NUUR

Ahlu Sunna Waljamaa

WAPIGANAJI wa Ahlu Sunna Waljamaa ambao wanapigana na Al Shabab. huo unaoendelea mpaka Shabab, waliuwawa. Aprili 24, 2011. leo? Mapambano mengine Sheikh (Mwenyekiti) L a b d a t u a n g a l i e wa ASWJ wa mkoa wa ni ya Aprili 28, 2011, m a t u k i o m e n g i n e . Gedo, Sheikh Hassan ambapo Ahlu Sunna Mei 3, 2011, yalitokea Sheikh Ahmed (aka Waljama'a wakiwa mapigano makali kwa Qoryoley) alijeruhiwa pamoja na askari wa masaa kadhaa katika na kukimbizwa Nairobi TFG, walipambana na mji wa Garbaharey, Al Shabab katika mji Gedo. Katika mapigano kwa matibabu ambapo wa Luuqin mkoa wa h a y a A h l u S u n n a alifariki siku mbili Gedo. Askari wengi wa Waljama'a walifanikiwa baadae. pande zote waliuwawa. Mapambano ya kuteka eneo hilo Mtu utajiuliza, lililokuwa chini ya Al namna hii yamekuwa katika askari hawa Shabab. Inaelezwa kuwa ya kawaida ambapo waliouwawa au k a t i k a m a p a m b a n o Waislamu wa makundi waliouwana (Waislamu hayo askari 3 wa ASWJ haya mawili, wamekuwa kwa Waisla m u), n i na askari 23 wa Al wakiendesha darsa za wa kutoka kundi lipi watakuwa wamekufa mashahidi? Wote hawa wanadai kupigania Dini isiharibiwe! tukajaribu katika Inatoka Uk. 3 H a w a A S W J rasimu hii ya pili, nako u m e p a t i k a n a . S a s a pia hayakujumuishwa, wanawaona Al Shabab hatuna fursa tena hakuna fursa tena wanaowavunjia alisema kwa masikitiko iliyobaki , alifafanua heshma Masheikh Sheikh Musa Kundecha, Sheikh Kundecha. wao wa Twariqa, ni Amir wa Baraza Kuu la Kufuatia hali hiyo, watu waliopotea njia. Jumuia na Taasisi za Amir Kundecha Wanapotosha Uislamu. Kiislamu nchini. alisema viongozi wa Alisema dhana nzima Kiislamu wamejitahidi Al Shabab nao hivyo ya Waislamu kushiriki kutoa maoni yao kama hivyo. Je, mgogoro wa kikamilifu katika kutoa namna hii, mgogoro wa m a o n i y a o k a t i k a taasisi na kuhamasisha kiitikadi na mtizamo mchakato huo, pamoja u m m a w a K i i s l a m u wa kidini, utatuzi wake na mambo mengine k u s h i r i k i i p a s a v y o utapatikana kwa njia ilikuwa ni kujaribu katika kutoa maoni yao, ya risasi? kutafuta suluhu ya lakini rasimu ya pili Mwaka 1846 Sheikh kudumu kikatiba juu ya imethibitisha kwamba Ali alisema watu wa matatizo yao ya kiimani, maoni ya Waislamu Qadiria katika utawala lakini sasa fursa hiyo hayapo. Geledi waliokufa vitani imepotea kufuatia Nachukua fursa hii wakipigana dhidi yake, maoni yao kuwekwa kuufahamisha umma wanakwenda motoni. kando licha ya ushiriki wa Kiislamu kwamba, Ila maiti wake katika wao. wasifikiri viongozi kundi la Sunna, Tulitoa maoni yetu wao wamewaangusha wanakwenda Peponi. katika rasimu ya kwanza na hawakuwajibika Hatuoni kuwa h a i y a k u j u m u i s h w a , ipasavyo, wamejitahidi mkanganyiko ule ndio

Maoni ya Waislamu yatupwa rasimu Katiba Mpya


k w a k a d i r i walivyoweza, lakini kama ilivyozoeleka, wamepuuzwa Alisema Amir Kundecha. Aidha alisema kwamba pamoja na kwamba Taasisi yao imeshapeleka majina ya wajumbe wake waliopendekezwa kuingia katika Bunge la Katiba, lakini hakuna fursa ya kutosha iliyobaki ya kuwasilisha na kuingizwa maoni ya Waislamu katika rasimu katika chombo hicho. Hata hivyo Sheikh Kundecha, aliahidi kwamba watakutana na viongozi wengine kulizungumzia suala hilo kwa kina zaidi na kulitolea ufafanuzi kwa Waislamu baadae.

Habari za Kimataifa/Tangazo

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014

AN-NUUR

Waislamu 23 wauawa Msikitini Bangui


KWA uchache Waislamu 23 wameuawa Ijumaa mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kushambuliwa wakiwa ndani ya msikiti. Mauaji hayo yamefanywa na kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti Balaka. Sheikh Muhammad Wasil, Imam wa Masjidul Noor mjini Bangui amesema kuwa, Waislamu hao wameuawa baada ya kukimbilia Msikiti humo kujipatia hifadhi. Sheikh Muhammad Wasil, ameongeza kuwa wanamgambo wa Anti Balaka, w a l i w a u w a Waislamu hao kwa kuwakatakata na wengine kuwachinja kama kuku kwa kutumia mundu. Imam wa Masjidul Noor ameongeza kuwa, wanamgambo hao wa Kikristo hawakuwa na huruma hata kwa wanawake na watoto, kwani wote waliokuwa wamejificha Msikitini humo waliuawa kinyama na miili yao ilitelekezwa pembezoni mwa Msikiti huo. Imeelezwa kuwa marehemu hao watazikwa pembeni mwa mwa Msikiti huo, baada ya majeshi ya nchi hiyo kukataa kutoa ruhusa ya kuzikwa kwenye makaburi ya Waislamu yaliyoko nje ya Bangui.

Vita vya kiuchumi Marekani na China kuanza


GAZETI la The Hill, linalochapishwa nchini Marekani limeandika habari za kuanza vita vya kiuchumi baina ya nchi hiyo na China. Gazeti hilo limeandika kuwa, Washington inapanga mikakati ya kutiliana saini na nchi za Umoja wa Ulaya na zile zilizopo pambizoni mwa bahari ya Pasifiki kwa ajili ya kuzuia nguvu za kiuchumi za China. Msemaji wa Ofisi ya mwakilishi wa Marekani katika Shirika la Biashara Duniani, ameliambia gazeti hilo kwamba makubaliano hayo ya pamoja kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya ni hatua ya pamoja ya kukabiliana na wasiwasi wa nchi hizo kuhusiana na masuala ya biashara ulimwenguni. Imeelezwa kuwa, Marekani imeamua kuchukua uamuzi huo kwa hofu kwamba, nguvu na hatua zake za kiuchumi zinazopungua siku hadi siku zitachukuliwa na China. Wakati huo huo, China nayo imeeleza kuwa mikakati ya Marekani ya kuleta mabadiliko kwenye sheria za ndani nchini humo imegonga mwamba. Hii ni katika hali ambay, Congress na Ikulu ya Marekani kwa pamoja, zinafanya juhudi za kufanya miamala mikubwa ya kiuchumi ambayo inahofiwa kuzusha vita vya kiuchumi kati ya nchi hiyo na China katika miaka ijayo.

WANAWAKE Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar, wanakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na maafisa usalama katika vituo vya polisi nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti, maafisa wa usalama nchini Myanmar wamekuwa wakiwateka nyara wanawake na wasichana Waislamu wa kabila hilo na kuwapiga na kuwatukana.

Polisi wabaka wanawake Waislamu Myanmar


Habari zinasema kuwa, baada ya maafisa hao kuwateka huwalazimisha kutumia madawa ya kulevya, huwapeleka katika vituo vya usalama na kuwabaka bila ya wao kujielewa. Hii ni katika hali ambayo jamii ndogo ya Waislamu nchini humo imekuwa ikinyimwa haki zake za kimsingi kutokana na serikali ya Naypyidaw, kupinga kuwapa Waislamu wa

jamii hiyo haki yoyote kwa madai kuwa sio raia wa nchi hiyo. Aidha mara kadhaa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binaadamu, yamekuwa yakiituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia vimavyofanywa na maafisa wa usalama na jeshi, dhidi ya wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo.

AHLUL DAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY


Inawatangazia Waislamu wote kuwa kuimeandaa safari ya Hijja mwaka 2014 sawa na mwaka 1435 Hijria kwa USD 3,600. Kutakuwa na punguzo la asilimia 18 kuanzia muda huu mpaka Machi 22, 2014 Itakuwa dola 952 tu. Kuanzia 23 Machi 2014 kuna punguzo la asilimia 8 mpaka Juni 2014 itakuwa dola 3,312 tu. Mambo yatakayogharamiwa ni semina za Hijja, huduma za afya na kuchanja, airport charge na tiketi za ndege, nyumba Makka na Madina, Ihram na kuchinja kwa ajili ya Tama-Tuu, chakula wakati wote, usafiri na ziara Makka na Madina, Mahema Mina na Arafa. Umra mwezi wa Ramadhani itakuwa ni dola US 1975. Fomu zinapatikana Ofisi ya AHLUL DAAWA Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadininyumba namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tel: 0713 730444 au 0773 804101 au 0785 930444 au 0773 930444. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982 au 0777 413 987. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam Tel: 0784453838. Abdalla Saleh Mazrui (Hoko) Dar es Salaam Tel: 0715 724 444. Dukani kwa Abdalla Hafidh Mazrui Wete Pemba Tel: 0777 482 665. Dukani kwa Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba Tel: 0777 456 911, Sheikh Daud Khamis Sheha Tel: 0777 679 692, Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel: 0777 417 736. Wahi kulipa ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Tel: 0713 730 444 au 0773 804 101 au 0785 930 444. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Salim Tel: 0777 417 736. Sheikh Salim Mohamed Salim Tel: 0774 412 974 au Account No 048101000030 NBC Kariakoo. Atakayemaliza taratibu zote mwanzo ndiye atakayeshughulikiwa mwanzo. Ukilipa kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412 975. Kumbuka kikundi cha AhlulDaawa kwa bei nafuu kuliko wote na huduma bora kuliko wengi Wabillah Tawfiq

6
Na Omar Msangi KUWA Msomali, ni kuwa Muislamu. Huo ni msemo mashuhuri wa Wasomali. Wanachomaanisha ni kuwa Wasomali wote ni Waislamu. Wanasema kuwa kama yupo Msomali anayedai kuwa yeye sio Muislamu, basi atakuwa mamluki tu anayepewa pesa ili akanushe Usomali na Uislamu wake. Msomali anaweza akawa asi, mlevi, haswali, hatoi zakka, lakini hamtaelewana ukimgusa katika Uislamu wake au kumtaka aritadi. Ndio walivyo kwa asili. Kama ni kubadilika, labda wabadilike hawa wanaohamia nchi nyingine wakakulia katika mazingira ambayo si ya Kisomali. Iwapo Uislamu umekuwa kama ndio mila na utambulisho wa Msomali, swali ni je: mbona Uislamu huu tunaoambiwa ni dini ya amani, neno lenyewe Islam ni amani; haujaweza kuwasaidia Wasomali na kuwaepusha na mapigano na mauwaji ya wao kwa wao? Je, hii hali ya kupigana na kuuwana wenyewe kwa wenyewe miaka nenda miaka rudi, haiwi sababu ya kuupaka Uislamu matope na kuonesha kuwa hauna msaada wowote kwa jamii? Why has Islam not kept us from killing each other? (Kwa nini Uislamu haujatusaidia ukatuepusha na kuuwana wenyewe kwa wenyewe?). Wanajiuliza Wasomali na wanauliza baadhi ya watafiti na waandishi wa vitabu. Hivi sasa Somalia ipo katika vita. Jeshi la serikali- Transitional Federal Government (TFG), linapambana na makundi ya Kiislamu ambayo yanapinga serikali yakidai kuwa ni kibaraka wa nchi za kikafiri. TFG inaongozwa na Sharif Sheikh Ahmed. Huyu alikuwa ndiye kiongozi wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu ambao uliweza kusimamisha vurugu, mauwaji na uhalifu ikaanza kujenga serikali ya Kiislamu. Serikali hiyo ya Kiislamu ambayo ndio kwanza ilikuwa ikijengwa, ilivurugwa

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


ndio kikosi cha mapambano katika Umoja wa Mahkama za Kiislamu, wengi wao wakaibuka na kundi jipya la Al Shabab. Kwa hiyo, kimsingi Al Shabab sio kundi la kigaidi kama inavyodaiwa, bali limeibuka kupambana na uvamizi wa Ethiopia na baada ya hapo kupambana na serikali wanayodai ni kibaraka pamoja na askari kutoka nje walioingia Somalia kuilinda TFG. Muhimu la kutaja hapa ni kuwa, ukiacha muda mfupi usiozidi miezi sita ambapo Mahkama za Kiislamu zilileta amani, Somalia imekuwa haina amani kwa miaka 18. Lingine la kutaja hapa ni kuwa hawa walio katika serikali, ndio waliokuwa katika Mahkama za Kiislamu wakidai kusimamisha Uislamu, lakini sasa ndio wanaopambana n a A l S h a ba b. K wa hiyo hapa ni Waislamu ambao awali walikuwa pamoja wakidai kuwa wana lengo moja, lakini sasa ni maadui walio katika majeshi mawili tofauti yakipambana. Jingine ni kuwa haya makundi ya Kiislamu sio moja, sio Al Shabab pekee. Wapo Al-Ahl, Takfir Wal-Hijra, Jamaa Islamiyah, Wahdatul Islamiayat, ambayo imekuja kuwa Al-Ittihad al-Islami (AIAI). Mengine yaliyoibuka katika siku za karibuni ni pamoja na Ahlu Sunnah Wal-jamaa. Hata hivyo, pamoja na kuwa na makundi yote hayo, lakini muhimu zaidi katika vita ya kupinga serikali ya Sharif Sheikh Ahmed, ni al Shabaab. Japo wapo pia na Hezb alIslamiya. Vita hii iliyoanza toka Desemba 2006 inakisiwa kuwa imesababisha kuuliwa watu kwa maelfu. Na katika kukoleza vita zaidi, nchi za Kiafrika zimekuja na The African Union Mission in Somalia (AMISOM) hupeleka maelfu ya askari kupambana na makundi ya Kiislamu yanayopinga serikali. Lakini pengine la kusikitisha zaidi, hawa Hizb al Islamiya na Al Shabab, wamekuwa nao ni maadui wao Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR

Somalia wamekwama wanahitaji kusaidiwa


Wameshika bendera ya Uislamu Lakini wapo vitani wanauwana Swali la msingi: Wanasaidiwaje?

WAFUASI wa Ahlu Sunna wakidhikiri, wakimaliza kudhikiri wanashika bunduki kwenda kupambana na Al Shabab.

na kungolewa baada ya uvamizi uliofanywa na Ethiopia ikisaidiwa na Marekani. Marekani ilidai kuwa Umoja wa Mahakama za Kiislamu ni magaidi wenye

uhusiano na Al Qaidah. Baada ya kungolewa utawala wa Mahkama za Kiislamu, hawa waliokuwa ndio waanzilishi na wapiganaji walioweza

kusimamisha mamlaka iliyoleta amani ya muda Somalia, wakagawika. Baadhi wakaingia katika serikali mpya (TFG), wengine wakapinga na wale vijana waliokuwa

7
Inatoka Uk. 6 kwa wao. Badala ya kupambana na askari wa AMISOM na wale wa serikali, hutokea nao wakashikiana silaha wakauwana na kuuwa raia katika mapigano yao. Inasemekana kumekuwa na harakati katika nchi mbalimbali kuhamasisha vijana wajitolee kwenda Somalia kupigana upande wa Al Shabab. Jaaliya hilo ni kweli na wanapatikana Waislamu wa kwenda huko. Kwa upande mwingine, Sharif Sheikh naye anazidi kupewa msaada wa askari na silaha kupitia AMISOM na sasa jeshi la Kenya lipo ndani ya Somalia likipigana. Picha ya kwanza t u n a y o t a k i w a tuitizame ni hii: Hawa ni Waislamu ambao wote walikuwa katika Umoja wa Mahakama za Kiislamu. Hivi sasa wamegawanyika ni makundi mawili yanayohasimiana. Moja linapata misaada kutoka nchi unaweza kuziita za kikafiri (AMISOM na UN) pamoja na za Waislamu. Kundi jingine linatangaziwa ugaidi. Hakuna nchi inayoweza kujitokeza waziwazi kuwasaidia Al Shabab. Ndio unakuta hii inayoitwa kampeni ya chini kwa chini ya watu binafsi, sio katika ngazi ya kiserikali au nchi, kutafuta vijana kwenda kupigana Somalia. V y o v y o t e utakavyoitafsiri picha hii, kwamba ni Jihad au sio, lakini wanaouwana na kuangamizana ni Wasomali. Ni Waislamu wenyewe kwa wenyewe! Pengine labda turejee nyuma tutizame historia ya Somalia tukitaraji kuwa huenda tukapata jibu la lile swali la msingi: Kwa nini Uislamu haujasaidia kuondoa mauwaji ya Wasomali wenyewe kwa wenyewe? Ukifanya rejea mbalimbali za vitabu, zitakuonesha kuwa makundi ya mwanzo yaliyoingia na kuingiza

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


kuibua na kuimarisha kile kinachoitwa hivi sasa Msimamo mkali wa Kiislamu (Islamicmilitancy.) Tukio la kwanza limetajwa na watafiti wengi kuwa lilitokea katika mji wa Baardheere, kusini mwa Somalia. Na hili lilikuwa na ugomvi kati ya wanadini wa Bardheere (Jamaaca) na watu wa sultani wa Geledi katika Afgoye. Bardheere kama makazi ya watu, inarejea mwaka 1819 mwanzilishi akiwa Sheikh Ibrahim Yabarow, ambaye aliweka taratibu na Shariah za Kiislamu kwa baadhi ya vipengele vya maisha. Kwanza alipiga marufuku matumizi ya tumbaku (sigara) na kucheza muziki. Alipiga pia marufuku biashara ya pembe za ndovu. Kwa upande wa mavazi, ilikuwa ni lazima kwa wanawake kuvaa hijabu. Kufikia miaka ya 1830s, Jamaaca wakaamua kujipanua na kusambaa katika mikoa na miji mingine huo ukiwa ni wakati wa Sharif Abdirahman na Sharif Ibrahim waliotokea Sarmaan, Bakool. 1840 wapiganaji wa Jamaaca walifika Baidoa eneo liitwalo Luuq na hatimaye kuondoa uongozi wa Qadiriyah katika mji wa Baraawe. Hii ilipelekea masheikh wakubwa waliolelewa chini ya Qadiriyah kama Sultan Ahmed Yusuf wa Geledi na Sheikh Maadow wa koo ya Hintire, kupanga namna ya kukabiliana na upanuzi huu wa Uislamu usio katika Twarika zao. Watu wa mji wa Baraawe walilazimika kukubali kufuata kanuni za Kiislamu zilizoletwa na pia kulipa kodi ya Pessa 500 kwa mwaka. Hata hivyo, hii ilizua manunguniko kutoka kwa baadhi ya koo ambazo chini ya uongozi wa Geledi Sultan Yusuf Mohamed, walipatikana wapiganaji kiasi 40,000 ambao walivamia miji hii ya Kiislamu kama Bardheere na kuiangamzia kabisa. Baadhi ya waandishi wa historia ya Somalia, kama Professor Cassanelli, wanalielezea Inaendelea Uk. 9

AN-NUUR

Somalia wamekwama wanahitaji kusaidiwa

WAPIGANAJI wa jeshi la Al Shabaab.

WAPIGANAJI wa kikundi cha Hizbu Islamiyah. Uislamu Somalia katika karne ya 17, 18 na 19, yalikuwa ya Masufi-Twarika (watu wa dhikri). Na hawa walikuwa Qadiriyah, Ahmadiyah na Salihiyah. Masheikh mashuhuri na viongozi wa Twarika hizi wakitajwa kuwa ni Sheikh Madar, Sheikh Abdirahman AlZayli, Sheikh Aweys al-Baraawi, Sheikh Mohamed Guleed, Sayid MohamedAbdulle Hassan, Sheikh Ali Maye, Sheikh Sufi na wengineo walioheshimiwa sana na watu wa Somalia. Inaelezwa kuwa awali Masheikh hawa, Murid hawa, walihubiri kwa amani, hawakuwa wagumu kwa watu na wakati mwingine waliwaacha kufanya mambo waliyozoeya hata kama hayapo katika Uislamu. Kwa namna moja au nyingine, hawakushiriki kabisa katika migogoro au hali iliyoleata umwagikaji damu, bali walikuwa wasuluhishi wakubwa. Hata hivyo inaelezwa kuwa yapo matukio makubwa matatu ambayo, pengine yanaonyesha kuwa toka mwanzo Uislamu haukuwa umepokewa katika ufahamu ulio sahihi na ndio ikawa sababu ya kuanza uhasama miongoni mwa makundi ya Kiislamu na

8
Inatoka Uk. 4 wa Ki-Ansaar Sunna kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine ni kukosa uvumilivu na kuwastahamilia wengine ambapo katika hali hiyo wanadaiwa kupinga na kuwashambulia watu wa Sufi kwamba ni makafiri pamoja na kubomoa makaburi ya Masheikh wao pamoja na sehemu wanazoamini kuwa ni takatifu katika Kismayo kutokana na historia ya Usufi katika Somalia. Usufi, ndio mtizamo mkubwa na ulioenea sehemu kubwa ya Somalia ambapo mara nyingi na mahali pengi, wakuu wa Twarika katika miji ndio hao hao wakuu wa koo. Hofu iliyoingia kwa ma-Sufi hawa ni kuwa iwapo Al Shabab wataachwa washike nchi, basi wataangamiza aqida ya ki-Sufi na badala yake kuweka walichodai kuwa ni Uwahabi (kwa mtizamo wao, sio mtizamo wa mwandishi). Katika historia ya Kiislamu tunasoma juu ya Khawarij (Kharijite) waliouwa Waislamu waliokuwa na mitazamo tofauti na ya kwao. Hawa ASWJ, wanaamini kuwa Al Shabab nao wamekuja kuuwa Wasomali wasio wafuata. Ni Khawarij wa leo. Ni katika kikao cha Nairobi, As Ahlu Sunna wal Jamaa waliunda Baraza la Vita (war council) , na kuanza kuweka mikakati ya kupata silaha na wapiganaji. Kwa upande mwingine, Ahlu Sunna wal Jamaa (ASWJ), wamepiga marufuku baadhi ya vitabu vya dini vinavyochapishwa na kusambazwa na Al Shabab wakidai kuwa vinafundisha vijana kujilipua kwa nia ya kujitoa muhanga (suicide bombers). Madai mengine ni kuwa Al Shaba wanawachukulia Waislamu wasiofuata msimamo wao kuwa ni makafiri. Humkufurisha kila asiyekuwa Salafi

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


Vs unaodaiwa kuwa Uwahabi/misimamo mikali, na hali hii ya kivita iliyodumu kwa muda mrefu sasa, unaloliona kwa haraka ni kuwa Somalia kuna tatizo kubwa la elimu na ufahamu. Sasa ukichukulia kuwa hali ya kivita imedumu kwa muda mrefu, ni kuwa ujinga na kuchanganyikiwa (confusion), itazidi kuongezeka kwa sababu watoto walio wengi hawapati muda wa kwenda kusoma, si shule wala madarsa. Katika hali hii ya kivita, watu watasomaje? Binafsi nadhani kitakachoweza kuwasaidia Wasomali na kikaleta matunda ya kudumu, sio kulisaidia kundi moja kulishinda jingine kwa mtutu wa bunduki. Kama kutapatikana uwezekano wa kuwafanya Wasomali waweke silaha chini na kuwa chini ya serikali yoyote madhubuti, ilimuradi wanabaki na uhuru wao wa kufanya ibada, iwe kwa mtizamo wa ki-Sufi, Ansaar Sunna, Salafi n.k, kisha katika hali hiyo ya amani na utulivu, kazi kubwa ikafanyika kutoa elimu kwa watu. Watu wakapata fursa ya kwenda shule, wakazisoma siasa za ulimwengu zilivyo hivi sasa, wakaisoma dini vizuri na mbinu sahihi za kufikisha na kusimamisha Uislamu, huenda hilo baadae likaleta hata hiyo Dola ya Kiislamu itakayoungwa mkono na Waislamu wote wa Somalia na itakayojengwa katika misingi ambayo si rahisi kubomolewa na maadui wa nje. Al Shabab kwa vile ndio wanaonekana kuwa na nguvu kuliko makundi yote, wanaweza kushinda vita. Lakini katika hali hii ya kuwa katika mgogoro wa kiitikadi na Sufi ambao wana idadi kubwa ya wafuasi katika nchi, na sasa wamejifunza kutumia silaha, watafika wapi?

AN-NUUR

Ahlu Sunna Waljamaa

MPIGANAJI wa kikundi cha Hizbu Islamiyah. Katika zoezi hilo, ASWJ, wamefanikiwa kuondoa Vitabu hivyo katika miji ya Dhusamareb, Adado, Guriel, Harardhere, Hobyo na maeneo mbalimbali wanayomiliki katika Somalia ya kati. Katika zoezi hili, ASWJ, wamepata uungwaji mkono mkubwa na wananchi ambao wamekuwa wakidai kuwa wanahofia kuona watoto wao wakipotoshwa na kupambana na Waislamu wenzao. I am happy that Ahlu Sunna wal Jamaa clerics, who have a deep understanding of the religion, are prohibiting our children from being taught al-Shabaabs wrong ideology about suicide bombing. All praise is due to God for guiding our clerics to prevent such dangers. Alinukuliwa Mama Sadia Mohamed, akisema akimaanisha kuwa anawashukuru Masheikh wa ASWJ, kwa kuondoa hatari hiyo. A child is not born believing in suicide bombing and viewing other Muslims as infidels. This is an idea that is indoctrinated and it will cause many societal problems if it is not combated. Aliongeza Mama huyo, hali inayoonyesha kuwa hata kama Al Shabab watafanikiwa kushinda vita ya silaha na kushika madaraka ya kuongoza nchi, bado kutakuwa na vita ya kiitikadi ambayo itaendelea kusumbua na kuibua vita ya silaha mara kwa mara. Sio ASWJ pekee wapo pia na Hizbul Islam Hizbul Islam iliundwa Januari 2009, Sheikh Omar Iman, akiwa mwenyekiti wake wa kwanza. Msimamo wa Hizbul Islami kama walivyoutangaza hapo tarehe 7 Februari, 2009, ni kupambana na serikali ya Sharif Sheikh Ahmed na majeshi ya African Union (AMISON) yaliyo Mogadishu. Kundi hili limekuwa dhaifu ikilinganishwa na Al Shabab kutokana na migogoro na ugomvi wa kugombea madaraka. Hali hiyo imepelekea kwamba kila wanapopigana na Al Shabab, hupigwa. Baadhi ya wakati migogoro hiyo hupelekea kugawika makundi mawili moja likajiunga na Al Shabab kupigana na jingine. Katika kuzidi kusambaratika, pengine na kutafuta namna ya kujihami, ilifikia kundi zima likatangaza kujiunga na Al Shabab. Hata hivyo mwaka jana (2012) lilijitenga tena kutoka alShabaab na kuanza mapambano. Walifanya hivyo Septemba 2012, baada ya al-Shabab kupigwa sana na majeshi ya serikali/ AMISON na kutimuliwa katika maeneo mbalimbali waliyokuwa wakishikilia. Ndugu waliokuwa wakipigana katika safu moja kupambana na adui, sasa wakashika bunduki kuuwana wenyewe kwa wenyewe wakiacha pembeni adui waliyekuwa wakimpiga kwa pamoja. Ukichukua ugomvi huu wa Al Shabab na Hizbul Islami, unakuta kuwa mgogoro wa Somalia unakuwa katika hali ya utata zaidi maana unazaa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya vita ya wenyewe kwa wenyewe (Civil-warwithin-a-civil-war.) Civil war ya kwanza ni kati ya Majeshi ya Serikali yakiwa pamoja na Ahlu Sunna Wal Jamaa yakipambana na Al Shabab/Hizbul Islam (Islamists vs. TFG) na Civil war ya pili ni al Shabab wakipambana na Hizbul Islam (Al Shabab vs. Hizbul Islam). Swali la msingi hapa ni je, Waislamu hawa, Wasomali hawa, wanasaidiwaje? Ukirejea mkanganyiko wa itikadi za Kisufi

9
Inatoka Uk. 7 tukio hili kama mapambano kati ya nguvu inayoibuka ya kuhuisha Uislamu na Waislamu wahafidhina katika Geledi. Baadhi ya waandishi wanataja kuwa sultani wa Geledi (Geledi Sultanate), alikuwa na mahusiano mazuri na Sultan wa Zanzibar wakati huo, Sultan Sayid Barghash, na hivyo alipata msaada kutoka kwake. Hilo ni tukio la kwanza linaloonesha historia ya mapambano ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe katika Somalia. Tukio la pili linahusishwa na kuingia Sheikh Ali Abdurahman (1787-1952) katika mji wa Merca mwaka 1946 ambapo alizua mapambano na uongozi katika usultani wa Geledi. Huyu Sheikh Ali anatajwa kuzaliwa katika mkoa wa Nugal ulio kati ya Growe na Laas-Aanood katika Puntland ya leo. Kabla ya kufika hapo alikuwa Makka, Saudi Arabia kisha Baghdad, Iraq kwa ajili ya masomo. Akiwa huko anadaiwa kukutana na wafuasi wa Sheikh Mohamed Abdulwahab na aliporejea Somalia akaja na misimamo ya wafuasi hao katika dini na akataka kuilazimisha kwa watu wa Somalia, wengi wakiwa Sufi/ Twarika. Alianza kujenga chuo cha Kiislamu. Hata hivyo akalazimika kuhama baada ya kukataliwa na watu wa mji/koo yake. Alihamia mji mwingine, lakini napo akakataliwa kabla ya kwenda kwa Sultan Nur Osman. Hata hivyo napo aliona hapamfai kwa kuona kuwa Shariah za Kiislamu zinapingwa waziwazi na Sultan Ali. Hapo akaungana na Haji Farah Hirsi, ambaye aliasi familia akitaka kusimamisha usulutani wake. Wakakubaliana kuwa wakishinda, Haji Farah atakuwa kiongozi wa kisiasa wakati Sheikh Ali akisimamia mambo ya dini. Ilikufanikisha lengo hili, Sheikh Ali alitafuta msaada kutoka kwa

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


Zanzibar yalikwama kwa sababu Sultan aliona kuwa kumsaidia ni kuupa nguvu Uwahabi katika eneo hilo. Kwa hiyo Sultan wa Zanzibar akaamua kumsaidia Sultan Geledi kama namna ya kukabiliana na Uwahabi. Waandishi wengi waliochambua historia hii wanakubaliana kuwa msimamo mkali wa Sheikh Ali wa kuwaona wengine sio Waislamu, ni makafiri, ndio uliosababisha akose wafuasi wa kutosha kufikisha elimu aliyokuja nayo. Ilikuwa kila asiye katika mtizamo wake, ni kafiri. Ikawa uhasama mkubwa kati yake na Waislamu walio wengi wa Twariqa na wasoma Maulid. Na hii inadhihirishwa katika vita hii baina yake Sultan wa Geledi ambapo alisema kuwa Waislamu waliokufa wakipigana upande wa Sultan ni watu wa motoni, ila waliokufa wa upande wake ni Mashaheed, wanakwenda Peponi. Hali hiyo ya kutowavumilia Waislamu wengine na kutafuta namna nzuri ya kuwafikia kuwapa elimu, bali kupeana nembo ya ukafiri, iliendelea kushikiliwa na wafuasi wa Sheikh huyu. Hili likawa mbegu iliyozaa hali ya kutokuvumiliana iliyoendelea mpaka leo. Tukio la tatu linamhusu Sayid Mohamed Abdulle Hassan. Huyu aliingia Berbera mwaka 1895 n a a n a t a jwa ka tika vitabu vya historia kuwa pamoja na kuwa mbele katika mapambano ya silaha ya kupambana na mkoloni, lakini pia alikuwa chanzo cha mapambano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi tofauti ya Sufi (Somali Sufi Orders). Alipoingia Berbera, Sayid Mohamed alipinga mamlaka na ufuasi wa Qadiriyah akaja na twarika yake iliyoitwa, Salihiyah (Salihiyah Order). Aliwashambulia hadharani Masheikh wa Qadiriyah, na kutoa Inaendelea Uk. 10

AN-NUUR

Somalia wamekwama wanahitaji kusaidiwa

BENDERA ya chini ni ya Al Shabab na ya juu ni ya Ahlu Sunna Waljamaa. Wote wanapepea bendera ya Laailha ila llahu Muhammadar rasuulullah, lakini wanapigana, wanauwana.

mtawala wa Sharja, Sheikh Saqar al-Qasimi, lakini hakufanikiwa. Baada ya kukosa msaada huo, Sheikh Ali alikwenda Zanzibar a k ita k a m s a a d a wa Sultan Said al-Bu-Saidi. Akiwa na wazo la kusimamisha Falme ya Kiislamu, Sheikh Ali alifika Merca mwaka 1946, miaka mitatu baada ya kushindwa utawala mwingine wa Kiislamu Baardheere na badala yake Usultani wa

Geledi Sultanate kuwa ndio nguvu iliyotawala sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia. Hata hivyo, koo ya Biimal, ambayo ndiyo koo kubwa kabisa katika Merca, iliasi kipindi hicho na Sheikh Ali akaona kuwa hao ndio watu wa kuwatumia katika mipango yake. Mwanzo alijifanya mpatanishi baina ya Sultan Yusuf na watu wa koo ya Biimal. Hata hivyo Sultan Yusuf

akakataa upatanishi wake. Hapo Sheikh Ali akatumia fursa hiyo kutangaza vita dhidi ya Sultan Yusuf akitaraji kuwa watu wa Biimal watamsaidi. Lakini hawakufanya hivyo. Akaingia vitani na watu wachache aliohama nao na ikawa rahisi sana kwake kushindwa. Hiyo ilikuwa mwaka 1846. Kwa upande mwingine, matarajio yake ya kupata msaada kutoka kwa Sultan wa

10
Inatoka Uk. 9 fatwah mbalimbali kupinga mambo yaliyokuwa yakifanyika. H a t a h i v y o , Masheikh wa Qadiriyah walishinda changamoto hii kupitia midahalo na mihadhara iliyoelimisha na kuwaimarisha wafuasi wao. Na kazi hii haikufanywa na Masheikh wa eneo hilo pekee, bali walialikwa Masheikh kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo Sheikh Madar kutoka Hargeysa, aliyekuwa mkuu wa Qadiriyah katika mkoa/Jimbo hilo. Hiyo ilikuwa mwaka 1897 na haukupita muda, Waislamu Qadiriyah wa Berbera wakamtimua Sayid Mohamed. Lakini la kufahamika hapa ni kuwa kabla ya Sayid Mohamed kulazimika kukimbia kutoka Berbera, ilibidi serikali ya kikoloni kuingilia kati kutuliza ghasia baina ya makundi mawili ya Kiislamu, Qadiriyah na wafuasi wa Sayid Mohamed. Ugomvi huu wa Qa d iriy a h n a S ayid Muhamad, ukawa chanzo cha chuki na uhasama wa muda mrefu kati ya Waislamu Qadiriyah na Salihiyah. Na unatajwa kuwa wa kisiasa upande mmoja na kwa upande mwingine dini. Kisiasa kwa sababu Sayid Mohamed alikuwa na lengo la kusimamisha utawala wa Kiislamu kwa mtizamo wa Twariqa yake, lakini hakuchukua muda kuwaelimisha na kupata kuungwa mkono na Masheikh wengine waliokuwa na sauti. Hiyo ikamjengea chuki na kutengwa na Masheikh wenzake pamoja na viongozi wa koo. Kwa upande wa dini, Salihiyah waliwakufurisha Qadiriyah, wakidai kuwa Uislamu sahihi ni ule tu wa Salihiyah. Ugomvi ulikuwa mkubwa kiasi cha Masheikh wa pande mbili kutungiana mashairi ya kutukanana na kukufurishana na kuingizana motoni (Angalia B. G. Martin,

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


makundi haya kuungana na kuwa chini ya uongozi mmoja wenye lengo moja ni mambo mawili. Kwanza ni msimamo mkali wa makundi haya. Kila moja linamwona mwenzake sio sahihi. Je, hatuoni hii ni sawa na ile misimamo ya Salihiyah na Qadiriyah, na hivyo si rahisi kuleta amani na kusimamisha Uislamu, zaidi ya kuleta maafa kwa raia na kwa Wasomali wote? Jambo jingine linalojitokeza ni tamaa ya kila kundi kutaka ndio lishike madaraka ya utawala. J e , h a t u o n i ku wa msimamo huu mkali na kushikiana huku silaha miongoni mwa Al-Shabab, Hizb alIslamiyah, Ahli Sunnah Wal-Jamaa, dhidi ya serikali, itazidi kuongeza maafa na kuteseka kwa Wasomali? Hatuoni kuwa panahitajika wasomi, watafiti, wachambuzi, wanasosholojia, wanasiasa na wasomi wa Kiislamu; wa kuchambua hali hii na kutafuta namna ya kuwaweka kwanza Wasomali katika hali ya maridhiano, kuvumiliana na amani; ndio baadae wakakaa wanaharakati wa Kiislamu kwa kusoma hali halisi ya mazingira ya dunia ya leo; wakizingatia mifano ya Taliban, FIS na juzi kwa Morsi; watatumia Dawah na mbinu gani hadi kufanikiwa kusimamisha Ilamic State katika Somalia? Binafsi naamini kutafuta wanaharakati ama wa kusimama upande wa Al Shabab au Hizb al-Islamiyah, huku AMISOM, Marekani na UN nao wakiongeza majeshi, silaha na msaada wa kifedha n.k, kwa upande wa serikali (TFG), matokeo yatakuwa ni kuzidi kuwaangamiza Wasomali na kuzidi kuivuruga nchi.

AN-NUUR

Somalia wamekwama wanahitaji kusaidiwa

HAWA ni wapiganaji wa kikundi cha Hezb al-Islamiya aluyetafsiri baadhi ya mashairi hayo). Hali hii ilipelekea mapambano ya silaha baina ya Waislamu wa makundi haya mawili ambapo Aprili 14, 1909, wafuasi wa Salihiyah walimuuwa Sheikh Aweys al-Baraawi wa Biyooley. Kwa bahati mbaya au katika kilele cha kuonesha chuki na uhasama uliokuwepo, Sayid Mohamed alipopata habari za kuuliwa Sheikh Aweys, alisikika akiimba kibwagizo cha kujipongeza kwa ushindi. Akasema tizameni, hatimaye, tulipomuuwa mjusi kikongwe, mvua imeanza kunyesha. (Candhagodoble goortaan dilaa roobki noo daaye). Hakuishia hapo na wafuasi wake, lakini wanatajwa pia kuchoma moto madrasa nyingi za makundi yasiyokuwa yakifuata mtizamo wao. Hii ilileta chuki, uhasama, mapambano na mauwaji baina ya Waislamu. Ukiangalia na kuchambua historia na matukio haya matatu, utaona kuwa yalikuwepo mambo matatu ambayo ni tatizo. Moja, ni kushindwa kutambua, kukubali na kuvumilia uwepo wa watu wenye mtizamo tofauti. Pili, kundi moja kujipa Hati Miliki ya Dini (monopoly of religious legitimacy). Kwa maana kuwa wao ndio pekee halali kuwepo. Tatu, utumiaji wa nguvu, vurugu, mapambano (violence) dhidi ya makundi ya Kiislamu yanayotofautiana. Na nne, ni utumiaji wa Shariah, hovyo hovyo (kwa kuchagua). Hali hii ya kimapambano ya sasa, inaanzia kwa kuibuka Al-itihad al-Islami katika miaka ya 1980s ambapo harakati zake za vita vya silaha dhidi ya Waislamu wasio katika mtizamo wa kundi hilo, kuliwaletea maafa makubwa katika mapambano ya Kismayo (1991), Puntland (1992) na Gedo (1996). Pamoja na kuwepo makundi mengi ya Kiislamu kama Al-Ahl, Takfiir Wal-Hijra, Jama Islamiyah, Wahdatul Islamiyat na Al-Ittihad al-Islami (AIAI), lakini makundi makubwa ambayo hivi sasa yameshika silaha ni Al-Shabab na Hizb alIslami. Pamoja na kuwa wote hawa wanapigana dhidi ya serikali ya Sharif Sheikh Ahmed, lakini nao pia ni maadui. Hutokea wakapigana wao kwa wao na kusababisha maafa baina yao na kwa Waislamu wasio na hatia. Wapo pia Ahlu Sunnah Wal-jamaa, ambao nao pia hutwangana na Al Shabab. Swali ni hili: kama kundi moja wapo katika haya yaliyoshika silaha kupigana na serikali litashinda, kuna uwezekano wa makundi mengine kutambua ushindi huo na kuweka silaha chini kuacha kundi hilo litawale? Au baada ya kushinda na kuondoka askari wa AMISOM, wataanza kupigana wenyewe kwa wenyewe? Kama wameshindwa kuwa wamoja katika lengo la kupigana na adui, watakuwa wamoja baada ya adui kuondoka? Hapana shaka kinachokwamisha

11

Habari/Matangazo

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014


Bismillahir Rahmanir Rahiim

AN-NUUR

Inatoka Uk. 12

Masheikh waachiwe
rumande kunawanyima haki zao kikatiba na hakuwatendei haki wao na familia zao. Katika mkutano huo wajumbe wa Kamati ya Maridhiano wakiongozwa na Mzee Moyo waliungana na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwataka Wazanzibari kuungana na kuacha kusikiliza maneno ya chokochoko ambazo mwisho wake ni kuumizana na kujenga hasama miongoni mwao. Maalim Seif alisema ni wakati mwafaka sasa Wazanzibari kukataa kufitinishwa kwani ni muda mrefu wamekuwa katika mifarakano isiyokuwa na maana na sasa wameungana kwa maslahi ya nchi na wananchi wote bila ubaguzi hivyo alitoa wito kuendelea kushikamana ili kufikia lengo la kuitetea Zanzibar na Mamlaka yake.

peke yao, lakini tutizame wale akina mama waliopo majumbani mwao ambayo wana watoto wadogo watakuwa wameathirika kiasi gani kwa waume zao kuwekwa ndani siku zote tokea mwezi wa 10 mwaka jana (juzi) mpaka leo kesi inakwenda na kurudishwa nakuna linalokuwa sasa mimi natoa wito kwa Waziri wa Sheria, Makamo wa kwanza wa Rais ambao mpo hapa katika mkutano nyinyi ni miongoni mwa serikali tunasema suala hili tunaomba mlizingatie suala la kuendelea kuwaweka ndani Masheikh wananchi wamechoka, alisema Eddy. Kauli za kutetewa Masheikh hao zimeonekana kuvuta hisia za wananchi wengi ambapo baadhi yao walikuwa wakisema ni wakati mwafaka sasa Serikali kushughulikia kama ni kuwatia hatiani au kuwapa dhamana lakini kuendelea kuwaweka

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO RIDHWAA SEMINARI-KINONDONI MKWAJUNI KIDATO CHA KWANZA NA CHEKECHEA-2014
UONGOZI WA RIDHWAA SEMINARI UNAPENDA KUWATANGAZIA WAISLAMU WOTE NAFASI ZA MASOMO KWA KIDATO CHA KWANZA NA CHEKECHEA-2014 MASOMO YANAYOFUNDISHWA NI HAYA YAFUATAYO: KOMPYUTA, ARABIC ,ENGLISH ,KISWAHILI , MATHEMATICS, GEOGRAPHY, HISTORY, CHEMISTRY, PHYSICS, BIOLOGY, CIVICS, COMMERCE, BOOKKEEPING NA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU. SIFA ZA SHULE: -SHULE IMESAJILIWA KWA NAMBA S.537 NA S.738 -SHULE INA WAALIMU MAHIRI, WENYE UZOEFU NA NIDHAMU YA HALI YA JUU KAMA VILE SHEIKH RUSAGANYA, ABU BILALI, SOVU N.K -SHULE INA MAKTABA,UKUMBI NA MAABARA ZA KISASA KWA MASOMO YA SAYANSI. -SHULE NI YA KUMI BORA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM MATOKEO YA KIDATO CHA SITA-2013 -SOMO LA QURAAN HUSOMESHWA KILA SIKU ASUBUHI KABLA YA KUANZA VIPINDI. WAHI SASA NAFASI NI CHACHE NA IKUMBUKWE KATIKA KUJALI HALI YA KIPATO CHA WAZAZI WETU ADA NI NAFUU MNO NA INALIPWA KWA AWAMU MBILI TU. KAULI MBIU YETU NI: MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA ILIYOSHEHENI MAADILI NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU KWA MAENDELEO YA KIROHO NA YA KIDUNIA. USAILI HUFANYIKA KILA SIKU YA JUMAMOSI KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU YA MEZANI- 022-2762144 AU SIMU YA MKONONI 0713-215918 AU 0713-400079. WAHI SANA NAFASI NI CHACHE MNO!

Mahitaji ya Vifaa yanayohitajika kufikia hatua ya Zege la Jamvi PLOT No. 152 Block A, Masjid Jumuiyatil Islamia Ubungo Darajani.

Msaada ujenzi wa Msikiti

Na Mahitaji 1 2 3 4 5 6 7 8 9 Nondo 12 MM Nondo 8 MM Binding Wire 20 MAWE 200 CM KOKOTO 70 CM Mchanga 40 CM Cement Mbao Cypruss Misumari JUMLA NDOGO Deni la Mkandarasi (mjenzi) JUMLA KUU

Size Pcs Pcs Kg Lori Lori Lori Mifuko 16 Kg

Idadi 120 60 1 20 7 4 350 120 10

@ 18,000 8000 52000 250000 750000 13500 9000 3000

Tshs 2,160,000.00 480,000.00 52,000.00 5,000,000.00 5,250,000.00 4,725,000.00 1,080,000.00 30,000.00 19,657,000.00

220,000 880,000.00

35,657,000.00

Nb: haya ni Mahitaji kwa ajili ya Zege la Jamvi Kwa mawasiliano zaidi Tupigie Mwenyekiti 0754 462 050 Katibu 0719 760 777 Mwenyekiti Kamati ndogo ya ujenzi ( Goha) 0787 318 116. International Commercial Bank No A/c 00001/01/601059/01 au A/c 0000/01/ 0009/94/02. Au tutembelee katika Msikiti wetu uliopo Ubungo Darajani. Wabillah Taufiq

12

AN-NUUR
MAKALA

12

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014

Soma Gazeti la AN-NUUR kila Ijumaa

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JAN. 3-9, 2014

AN-NUUR

Nahodha sasa naye alilia mamlaka kamili


Na Mwandishi Wetu A L I Y E K U W A Waziri wa Ulinzi na Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe, Shamsi Vuai Nahodha, amesema anaungana na kundi la Wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa Mjini, Nahodha alisema kuwa katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi, suala la mamlaka kamili ni muhimu ili kuimarisha uchumi wa Zanzibar. Aidha Bw. Nahodha, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na baadae kuhamishwa na kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kabla ya kujiuzulu kufuatia sakata la kashfa ya Operesheni Tokomeza Ujangili, alidai kuwa yeye ni mtetezi wa hoja ya kuondolewe suala la mafuta na gesi kwenye muungano. Hata hivyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, wanaodai sarafu ya Zanzibar, Kiti cha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa na Wizara ya Ulinzi, akidai

Jussa, Eddy wataka Masheikh waachiwe


Na Alghaithiyyah Zanzibar
MWAKILISHI wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar (CUF), Ismail Jussa Landu amesema ikiwa kweli serikali ya umoja ya kitaifa inataka kuonekana kuwa inaheshimu utawala bora na haki za binaadamu, itende haki kwa kuwapa dhamana na kuwaachia Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) waliowekwa ndani zaidi mwaka sasa. Masheikh hao waliwekwa ndani tokea mwezi wa 10 mwaka juzi 2012 bila ya kupewa dhamana kwa madai ya kuhatarisha usalama wa taifa ambapo Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP) alitumia kifungu cha sheria ya usalama wa taifa katika kujenga hoja ya kuwanyima dhamana watuhumiwa hayo 10. Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Wananchi (CUF) uliofanyika huko Chaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Jussa alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaini mkataba wa kimataifa wa kuheshimu haki za binaadamu na hivyo inapaswa kuheshimu haki hizo bila ya kubagua. Alisema, katika katiba zote mbili ya Tanzania na ile ya Zanzibar katika kifungu cha 18 cha katiba hizo kinampa mtu uhuru wa kutoa maoni yake na kupokea kwa mujibu wa sheria bila ya kuadhibiwa. Jussa ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa alisema Masheikh wa Uamsho wamewekwa ndani zaidi ya mwaka sasa bila ya kupewa dhamana wakati sheria inaipa mahakama uwezo wa kutoa dhamana kwa watuhumiwa wa makosa yote isipokuwa mauaji na uhaini. Ikiwa Zanzibar inataka ionekane kwamba inaheshimu haki za binaadamu, basi iwape dhamana Masheikh hawa maana hata huko kuwaweka ndani bila kuwapa dhamana ni kinyume na haki za binaadamu muda umeshakuwa mwingi wamewekwa ndani bila ya kuzingatia athari zake katika jamii, alisisitiza Jussa na kuungwa mkono wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo. Katika kitu ambacho kinaonekana kuitia doa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Jussa alisema ni huko kuendelea kuwaweka ndani Masheikh hao na kuwanyima dhamana wakati sheria inasema huwezi kutiwa hatiani mpaka kuwepo na ushahidi uliokamilika hivyo kuendelea kuwaweka ni kwenda kinyume na sheria ambazo Zanzibar wamezipitisha wenyewe. Mjumbe wa Baraza Kuu huyo alisema Masheikh hao wanapaswa kupewa dhamana kwani ikiwa wamefanya kosa wahukumiwe kihaki na haki itendeke kila mmoja aweze kuona na kuridhika na isiwe kwa Masheikh tu bali sheria hiyo iwakamate pia wale wenye kufanya ubadhirifu wa mali ya umma na kujirimbikizia mali ambapo kamati za zilizoundwa na Baraza la Wawakilishi zimeonesha kumekuwepo na wizi mkubwa lakini hakuna aliyetiwa hatiani wala kuwekwa ndani licha ya ushahidi kamili kupatikana. Tunasema wapo watu ambao wanaiba na ushahidi upo, lakini hawakamatwi wala hawawekwi ndani na wala hakuna sheria iliyowagusa wapo nje wanatembea bila ya kuchukuliwa hatua yoyote. Sasa tunasema, mahakimu wa mwisho ni Wazanzibari wenyewe wakiona hakuna haki inayotendeka kwa Masheikh wao basi Wazanzibari wataamua ifikapo 2015, alisema na kushangiriwa na wananchi wengi kwa kupigiwa makofi. Kauli hiyo ya Jussa imeungwa mkono na aliyekuwa Mkereketwa wa Chama Cha Mapinduzi Mohammed Ahmed Sultan (Eddy Riamy)

kuwa masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji. Aidha Bw. Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi, muungano utaendelea kubaki kuwa uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wa Zanzibar. Alisema kwamba licha ya mfumo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo ziko huru badala ya kungangania muungano wa mkataba au serikali tatu ambao alidai haitakuwa salama na Zanzibar.

ALIYEKUWA Waziri wa Ulinzi na Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe, Shamsi Vuai Nahodha.

ambaye ametoa wito kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa kuwapa dhamana Masheikh kwani imekuwa kero kubwa kwa wananchi kila unapopita mitaani. Eddy alisema kuendelea kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana Masheikh hao kunaleta kero kwa wananchi walio wengi ambao wamekuwa wakifuatilia habari za Masheikh hao ambao wana mchango mkubwa kwa jamii hasa ukizingatia Masheikh hao ni walimu wa vyuoni na wengine ni Maimamu wa Misikiti. Mkereketwa huyo ambaye alifuatana na Kamati ya watu sita ya Maridhiano iliyoongozwa na Mzee Hassan Nassor Moyo, alisema kwamba mbali ya kukosekana darsa na kusalisha kwa Masheikh hao lakini pia familia zao zimeathirika kiuchumi na kisaikolojia kutokana na kuwa waume ndio waliokuwa wakitizama familia na sasa kuwekwa ndani kumeathiri familia hizo. Tusiwatizame wao

Inaendelea Uk. 11

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

You might also like