You are on page 1of 8

SIKU YA REDIO DUNIANI 2014 KUTUMIA FURSA YA REDIO KUKUZA USAWA WA KIJINSIA NA KUWAWEZESHA WANAWAKE KATIKA UONGOZI, DODOMA

HOTEL 13 FEBRUARI 2014 Rose Haji Mwalimu, UNESCO

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga, Viongozi na Waandishi kutoka Vyombo nchini, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Habari za asubuhi! Niliyesimama mbele yenu ni Rose Haji Mwalimu, mwanahabari na mtangazaji nguli. Kwa sasa nafanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO), kama mshauri wa masuala ya vyombo vya habari jamii. Maisha yangu na redio jamii yalianza tangu mwaka 2003 nikiwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, (MISA TAN). Miaka ile tulikuwa tukitetea haki ya redio jamii kupunguziwa gharama za leseni, kuanzishwa kwa redio jamii na kupigania vya Habari mbalimbali

mabadiliko ya Sheria ya Utangazaji. Siku hii ya leo inaadhimishwa kwa kuzishirikisha redio jamii ambazo pia zinahudhuria mafunzo ya kuzijengea uwezo wa kuendesha mijadala inayokuza amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mchakato wa mabadiliko ya katiba na kura za maoni, na Uchaguzi Mkuu; mradi ambao unatekelezwa na UNESCO. Nasimama mbele yenu kwa unyenyekevu mkubwa kuwasilisha mada inayohusu Namna ya Kutumia Fursa ya Redio Kukuza Usawa wa Kijinsia na Kuwawezesha Wanawake Katika Uongozi kwenye redio jamii. Utangulizi Mnamo Mwezi Januari mwaka 2013, Baraza la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio la UNESCO la kuadhimisha Siku ya Redio Duniani. Siku hii huadhimishwa tarehe 13 Februari, tarehe ambayo Umoja wa Mataifa ulianzishwa mwaka 1946. Leo hii, Umoja huo unatimiza takribani miaka 58 na nimefurhi

kuungana nanyi

katika ukumbi huu, wanawake kwa wanaume

wote duniani, kuadhimisha Siku ya Redio Duniani kama chombo muhimu hususani katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania. Najivunia nchi yangu ya Tanzania kwani ni kielelezo cha nguvu ya redio hususan redio jamiikwani imeongeza upatikanaji wa habari

kwa makundi wahitaji,na kukuza sauti za watu waliosahaulika katika jamii. Redio ina majukumu na itaendelea kuwa na majukumu makubwa katika upatikanaji wa maendeleo nchini, na kuendeleza usawa wa kijinsia. Redio, Chombo Chenye Nguvu Kukuza Usawa wa Kijinsia Wakati kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani mwaka huu inaadhimisha, Kusherehekea Ushiriki wa Wanawake katika Redio na Wote Wanaowawezesha, ni muhimu kuangalia maendeleo na changamoto zilizopo. Redio ni chombo ambacho kimechangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nchi. Redio jamii kwa upande wake bado ni changa hapa nchini. Ikumbukwe kwamba redio jamii ya kwanza ilianzishwa nchiini mwaka 2002 nayo ni Orkonerei Radio Service, Simanjiro. UNESCO ilianza kutoa msaada kwa redio jamii mwaka 2007, huku kukiwa na redio 2 tu zilizokuwa zimesajiliwa. Tunapozungumzia mwaka 2014, UNESCO inajivunia mafanikio ya imefanikiwa kuanzisha redio jamii 8 nchini. Kutokana na matukio mengi yanayoendelea katika kanda, redio hizi zimejipanga katika mtandao ujulikanao kama Community Media Network of Tanzania kwa kifupi COMNETA. Wakati mitandao kuweza kutoa msaada kwa redio zaidi ya 25 nchi nzima. Vilevile, UNESCO

mingine katika ukanda wa Afrika Mashariki ikifuata nyayo hizo, COMNETA inaendela kuonyesha uwezo wake kama kikundi kinacholenga maendeleo ya kujivunia. COMNETA inavisaidia vituo ambavyo ni wanachama wa mtandao kuwa mfano wa kuigwa katika kushughulikia matatizo yao yanayofanana. Miongoni mwa changamoto hizo, kubwa zaidi ni ile ya kukuza haki na uwakilishi wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume, kuendeleza usawa wa jinsia nje na ndani ya utangazaji. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba redio nyingi za jamii zimepiga hatua mbele katika kuweka uwiano wa kijinsia kwa idadi miongoni mwa wafanyakazi wake. Lakini tukizichambua namba hizi, tunabaini kuwepo kwa pengo kubwa lisilowiana ambalo linaonyesha dhahiri kwamba wanawake bado hawana uwakilishi mkubwa katika viwango vya ufundi na utawala. Pamoja na changamoto zinazochangia mapungufu hayo,

tumeshuhudia pia matokeo ya kuwapa motisha viongozi walioweza kumudu changamoto hizo. Kwa mfano, Adelina Lweramula, ni meneja wa FADECO FM ambae leo hii atazungumza nanyi. Mama huy amesaidia uanzishwaji wa dawati la kwanza Tanzania la Jinsia katika kituo cha redio jamii,maalumu kwa ajili ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia

yanayojitokeza na kutishia maisha ya wananchi wa wilaya ya Karagwe. Khadija Abdallah, aliyekuwa meneja wa ORS, Simanjiro,

ameonyesha umahiri wake katika utayarishaji wa vipindi vya kitamaduni kwa kuishirikisha jamii ya Kimasai wanawake na wanaume kuleta majadiliano yanayolenga kuondoa ubaguzi wa kijinsia na mila potofu zilizopitwa na wakati katika jamii ya Kimasai. Hiyo ni baadhi tu ya mifano ya kujivunia na kuigwa. Changamoto Mabibi na mabwana, wageni waalikwa, hadhara hii inaadhimisha wakati ambapo kuna mambo mengi yanaendelea katika historia ya taifa letu, tunapoelekea kwenye sehemu muhimu ya mchakato wa kupata Katiba mpya ambayo ni Bunge la Katiba na Kura ya Maoni. Vilevile Ttunakaribia kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Wakati mambo hayo yanaendelea ni vema kutafakari na kutambua changamoto ambazo zinaweza kwa namna moja au nyingine kukwamisha mchakato mzima wa kutekeleza demokrasia nchini. Changamoto zetu ni nyingi na zinaogopesha kidogo. Wakati Tanzania imeridhia Protokali ya SADC Habari na Maendeleo(SADC---- na ahadi nyingine, sheria zetu za vyombo vya habari bado

zimekaa kimya kuhusu vyombo vya habari na jinsia, na kuhusu maendeleo ya vyombo vya habari jamii. Redio Jamii kwa upande wake zimeendelea kuchukua hatua za kutayarisha na kutekeleza SERA ZA JINSIA kwa ajili ya vituo vyao. Redio hizo kwa msaada wa UNESCO, na mashirika mengine hususan GEMSAT na TAMWA, zimeweza kuongezeka idadi ya kutumia sera za jinsia kutoka asilimia 20% mwaka 2012, hadi kufikia 60% leo hii. COMNETA inaendelea kushawishi matumizi ya sera moja ya Uhariri na Jinsia, na ni matumaini yetu kwamba idadi itaongezeka na itazidi kuongezeka hapo baadae. Mwaka huu wa 2014 UNESCO inaendesha mafunzo maalumu yatakayowanufaisha waandishi wa redio jamii 250 nchi nzima kwa lengo la kukuza uwezo wa kutayarisha vipindi vya jinsia vinavyohamasisha ushiriki wa wanajamii. Pamoja na juhudi hizi, hatuna budi pia kuzungumzia vikwazo vinavyoendelea katika jamii ambavyo kama havitachukuliwa hatua muafaka vinaweza kurudisha nyuma malengo yaliyowekwa. Pamoja na sababu mbalimbali hususani elimu, imani za mila na tamaduni, kukosekana kwa usawa kiuchumi pamoja na mchakato wa kufanya maamuzi kulikotawaliwa na wanaume; takwimu zinaonyesha kwamba wanawake bado hawana uwezo wa kupata, kutumia na kufaidika na teknolojia mpya (ICT). Wakati tunaainisha vikwazo hivyo, tumeshuhudia ni kwa jinsi gani matumizi ya teknolojia mpya yanavyoweza kuwanufaisha na kuwapa uwezo wanawake kupata

nguvu na kudai haki sawa katika maamuzi, na kupata taarifa inayohitajika ili kufanya maamuzi sahihi sio tu kwa faida yao bali kwa watoto wao, familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa kuelewa hivyo, hatuna budi kuendelea kufanya kazi na waandishi wa habari wa redio jamii ili waweze kueleza mambo muhimu yanayotakiwa kwa wasikilizaji wao ambao ni wanawake na wanaume, huku tukitoa mafunzo kwa vitendo kwa wanawake ili waweze kufikia kiwango cha uongozi katika vyombo vya habari na sekta za kiufundi. Ipo haja ya kuendelea kutumia fursa ya redio kuunganisha vizazi- kwa kuwajengea ujuzi wa kutayarisha vipindi vya redio kwa kuwalenga wasichana kama watangazaji, wasimamizi na maripota ukizingatia kuwa wasikilizaji wengi wa redio jamii ni vijana. Kwa kufanya hivyo, tutawajengea uwezo wa ushiriki wa makundi ambayo yana dhamana na taifa letu la baadae. Hitimisho Nihitimishe kwa kuweka msisitizo kwetu sote tuliopo hapa, ni kwa namna gani tunaweza kuchangia kutimiza wajibu wetu. Wakati vyombo vya habari na redio vinaendeleza na kusisitiza uwiano usiolingana wa usawa wa kijinsia, vinaweza pia kuupiga vita. Redio inaweza kusaidia kukomesha migogoro ya nyumbani. Redio inaweza pia kusaidia wasichana kuendelea na masomo na kupata misaada mashuleni. Redio zinaweza kuwashawishi wanaume kuwa

baba wazuri na mifano ya kuigwa. Redio zinaweza kuwajenga wanawake wajiamini ili waweze kujikwamua na vikwazo mbalimbali vinavyowakabili, kugombea na kushinda nafasi za uongozi katika siasa kwa lengo la kuisaidia jamii inayowazunguka. Redio inaweza kufanya hayo yote, na kwa msaada wetu itafanya hivyo. Kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kutumia fursa ya redio, kuvunja vikwazo vinavyowazunguka wanaume, wanawake, wasichana na vijana ili kila mmoja ajitambue na kuishi kulingana na uwezo alio nao. Hilo ni lengo letu, na hatutasita kuziendeleza ili tuweze kufikia lengo hilo. Ni kwa namna hii tu tunaweza kutumia fursa ya redio ili kukuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kushiriki katika uongozi.

Ahsanteni sana!

You might also like