You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706 FAKSI: 255 22 2460735/2460700 Barua pepe: met@meteo.go.tz Tovuti: www.meteo.go.tz Unapojibu tafadhali nakili: Kumb. Na.: TMA/1622

S.L.P. 3056 DAR ES SALAAM

13 Machi, 2014

Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa.


Taarifa Na. Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Daraja la Taarifa: Kuanzia: Tarehe Mpaka: Tarehe Aina ya Tukio Linalotarajiwa Kiwango cha uhakika: Maeneo yanayotarajiwa kuathirika 201403-02 Saa 9:30 Alasiri Tahadhari 13 Machi, 2014 15 Machi, 2014

Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kila siku vinatarajiwa.
Wastani (60%) Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba, pomoja na mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mara, Mwanza, Simiyu, Geita na Kagera Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua katika maeneo yaliyotajwa hapo juu. Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki. Mvua zinazoendelea na zinazotarajiwa kunyesha ni muendelezo wa mvua za msimu wa masika katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.

Maelezo:

Angalizo:

Maelezo ya Ziada

Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

You might also like