You are on page 1of 8

Bulletin

News
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
Mabadiliko!
nAndilile bosi TPDC nSamaje Mkaguzi migodi
Serikali haitapoteza chochote mkataba wa Statoil -Uk2
NISHATI NA MADINI YAFANYA
Toleo No. 25 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Julai 18-24, 2014
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli
(TPDC) , Bw. James Andilile
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC
anayemaliza muda wake, Bw
Yona Killagane.
Kamishna Msaidizi na
Mkaguzi Mkuu wa Migodi,
Mhandisi Ally Samaje
2 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
NISHATI NA MADINI YAFANYA MABADILIKO
Na Mwandishi Wetu

W
aziri wa Nishati na Madini Prof. Sos-
peter Muhongo amefanya uteuzi na
mabadiliko kwa baadhi ya Watendaji
wa Wizara hiyo kwa kuwateua Bw.
James Andilile kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtend-
aji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
na Mhandisi Ally Samaje anayekuwa Kamishna
Msaidizi na Mkaguzi Mkuu wa Migodi.
Kabla ya Bw. Andilile kushika wadhifa huo ali-
kuwa Kamishna Msaidizi sehemu ya Maendeleo ya
Nishati, wakati Mhandisi Samaje alikuwa Kamish-
na Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki.
Aidha, Bw. Juma Mkobya ameteuliwa kuwa
Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Maendeleo
ya Nishati. Kabla ya wadhifa huo alikuwa Mhandisi
Nishati mwandamizi, Ofisi ya Kamishna wa Nishati
na Petroli Bibi Latifa Mwache Mtoro ameteuliwa
kuwa Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini sehe-
mu ya Uongezaji Thamani Madini (Minerals Ben-
eficiation and Value Addition).
Wengine walioteuliwa ni Mhandisi Hamisi
Komba ambaye amekuwa Kamishna Masadizi wa
Madini, Kanda ya Mashariki Dar es Salaam am-
baokabla alikuwa Kamishna Msaidizi wa Madini
sehemu ya Minerals Beneficiation and value addi-
tion.
Aidha, Bw. Julius Sarota ameteuliwa kuwa
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nya-
sa (Songea), Bw. Juma Sementa Kamishna Msaidizi
wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Mashariki (Mu-
soma), na Bw. Mayigi Makolobela amekuwa Ofisa
Madini Mkazi Nachingwea.
Vilevile, Bw. Nyaisara Mgaya amekuwa Ofisa
Madini Mkazi Bariadi, Bi Fatma Kyando Ofisa Ma-
dini Mkazi Kilimanjaro, Pius Lobe Ofisa Madini
Mkazi Geita na Samwel Ayubu amekuwa Ofisa Ma-
dini Mkazi Njombe.
Uongozi wa Wizara unawatakia wote walioteuli-
wa kila la kheri katika nafasi zao mpya na unaamini
watatekeleza wajibu wao kwa ufanisi na kuzingatia
Uongozi
wa Wizara
unawatakia
wote
walioteuliwa kila
la kheri katika
nafasi zao mpya
na unaamini
watatekeleza
wajibu wao
kwa ufanisi
na kuzingatia
maadili ya kazi
na utawala bora.
Serikali haitapoteza chochote mkataba wa Statoil- Killagane
Na Malik Munis,
Dar es Salaam

Serikali imewataka wananchi kuon-
doa hofu kuhusu habari za kupotosha
kwamba, aitapoteza mapato katika
mkataba wa Ugawanaji wa Mapato
(PSA) kati yake na Statoil kwani hazina
ukweli wowote.
Hayo yamesemwa na Mku-
rugenzi Mtendaji wa Shirika la Maen-
deleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw.
Yona Killagane wakati akizungumza na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.
Kauli ya Killagane imekuja ikiwa
ni siku kadhaa toka baadhi ya magazeti
nchini pamoja na mitandao ya kijamii
kuandika kuwa, Serikali ya Tanzania ita-
poteza takribani shilingi trilioni 1.6 ka-
tika mkataba wa utafiti wa mafuta na gesi
iliyoingia na Kampuni ya Statoil kutoka
Norway.
Kusema kuwa Serikali itapoteza
mapato katika mkataba wa Ugawanaji
wa Mapato (PSA) kati yake na Statoil ni
habari za kupotosha, alisema Killagane.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Bw. Killagane alieleza kuwa, mna-
mo mwaka 2005 Serikali kupitia TPDC
ilitoa ofa ya utafiti wa mafuta katika ki-
talu namba 2 kilichopo bahari kuu am-
bapo mojawapo ya ofa iliyotolewa ni
kwamba, iwapo mafuta yatagundulika
katika gawio la kwanza (first tranche),
kila upande utapata gawio la mgao wa
asilimia 50:50.
Hii ilikuwa ni ofa tu na sio
makubaliano. Kimsingi unatoa ofa
ya kwanza ili kuweza kuanzisha
majadiliano na mwisho mnafikia
makubaliano, alisisitiza Killagane.
Alieleza kuwa, Statoil walipende-
keza gawio liwe kati ya asilimia 95%
kwa Statoil na asilimia 5% kwa Seri-
kali iwapo mafuta yatagundulika, na
kuongeza kuwa, Statoil walikuwa na
sababu za kupendekeza hivyo kuto-
kana na ukweli kuwa, ilikua ni mara ya
kwanza kwa nchi ya Tanzania kufanya
utafiti katika maeneo ya kina kirefu
cha bahari, pia Statoil wangebeba
gharama zote za kutafuta.
Aidha, alieleza kuwa, katika
shughuli za kutafuta mafuta na gesi
kuna kupata au kukosa na kiutara-
tibu serikali hairudishi chochote iwapo
mwekezaji atakosa.
Vilevile, aliongeza kuwa, kutokuwepo kwa miun-
dombinu ya kutoa gesi na mafuta pindi inapogundulika ka-
tika kina kirefu cha bahari na Serikali kutokuchangia katika
kipindi cha utafiti, ni baadhi ya masuala ambayo yalipelekea
Statoil kutaka ofa ya asilimia 95% ya gawio na asilimia 5%
kwa Serikali.
Bw. Killagane alieleza kuwa, hata hivyo majadiliano
yaliyofanywa baina ya Kamati ya Majadiliano ya Serikali
na Statoil yalipelekea kufikia makubaliano ya mgawo wa
asilimia 70% kwa mwekezaji na asilimia 30% kwa Serikali
katika mgao wa kwanza (first tranche).
Aidha, aliongeza kuwa, gawio la asilimia 30 ya Serikali
haijumuishi kodi ya asilimia 30, mrabaha asilimia 5, ushiriki
wa TPDC asilimia 10 participating interest na ushuru wa
huduma asilimia 0.3.
Ikumbukwe kwamba, mwaka 2007 mkataba wa PSA
ulisainiwa kati ya Serikali na Statoil. Hii ilikuwa ni kama
mafuta yatagundulika mgao ungekuwa kama nilivyoeleza
kuwa Serikali kupata gawio la asilimia 30 na mwekezaji asil-
imia 70, alisema Killagane.
Killagane aliongeza kuwa, mwaka 2012 baada ya gesi
kugundulika, kamati ya Majadiliano ya Serikali ilikaa na
Statoil ili kupanga upya kiwango cha mgawanyo wa mapato
na kufikia makubaliano kuwa, Serikali ingepata asilimia 69
na Statoil asilimia 31 hii ikiwa ni baada ya kutoa gharama
za awali za utafiti.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TPDC, Bw. James Andilile aliongeza kuwa, MPSA sio
mkataba wa mwisho na ndio maana mkataba wa ziada wa
kupatikana gesi (Gas Addendum) ulifanyika ili kuruhusu
makubaliano mapya ya kugawana mapato, jambo ambalo
alieleza kuwa ni kawaida kwa makampuni yote katika sekta
ndogo ya gesi na mafuta kufanyika.
Mhandisi. Ally B. Samaje Bw. James Andilile Bw. Juma F. Mkobya
Bw. Julius S. Sarota Mhandisi. Hamisi Komba
Bibi Latifa M. Mtoro
Bw. Juma Sementa
Bw. Mayigi C. Makolobela Bibi Fatuma T. Kyando
Bw. Pius R. Lobe
Nyaisara F. Mgaya Samwel Y. Ayubu
3
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
MAONI
Na Teresia Mhaga-
ma, Canada
K
ampuni ya kimataifa in-
ayotengeneza na kusafiri-
sha malighafi methano ya
nchini Canada Methanex
imeeleza kuwa Tanzania ni moja ya
maeneo muhimu duniani yanayofaa
kwa uwekezaji wa viwanda vya
kutengeneza malighafi hiyo am-
bayo inatumika kuzalisha kemikali
mbalimbali kutokana na uwepo wa
hazina kubwa ya gesi asilia.
Hayo yamesemwa na Makamu
wa Rais wa kampuni ya Methanex
upande wa Amerika Kaskazini Bw.
Kevin Handerson, wakati alipokuwa
akizungumza na Ujumbe wa Tan-
zania ulioongozwa na Naibu Wa-
ziri wa Nishati na Madini, Charles
Kitwanga uliofika katika kiwanda
cha kuzalisha methano kilicho ka-
tika jimbo la Alberta nchini Canada
ikiwa ni sehemu ya ziara ya mafunzo
kuhusu usimamizi na uendelezaji
wa tasnia ya uziduaji.
Bw. Handerson ameeleza kuwa
uzalishaji wa methano utakuwa
na manufaa makubwa kwa Tan-
zania kutokana na malighafi hiyo
kutumika katika masuala mbalim-
bali ikiwemo kutengeneza vifaa vya
plastiki, gesi inayotumika majum-
bani, kutumika kwenye vyombo vya
usafiri, viwanda vya kutengeneza
rangi, viwanda vya mbao, kuzalisha
umeme, kusafishia maji n.k
Pamoja na Tanzania kuwa ni
eneo muhimu kwa uwekezaji wa vi-
wanda hivi vya kuzalisha methano
ni muhimu Serikali ikatenga eneo
maalum kwa ajili ya uwekezaji wa
namna hii, na kuzingatia uwepo wa
sera, sheria, kanuni madhubuti zi-
nazoongoza sekta hii, pia kuwe na
miundombinu imara ya usafirishaji,
maji, umeme wa uhakika pamoja na
uwepo wa rasilimali watu, alisema
Bw. Handerson .
Akieleza kuhusu uwezo wa
kampuni hiyo, Makamu wa Rais wa
Methanex amesema kuwa, kampuni
hiyo ina uwezo wa kuzalisha tani
milioni 8.5 za methano kwa mwaka
na husafirisha malighafi hiyo ka-
tika sehemu mbalimbali duniani
ikiwamo Hongkong, Shanghai, Bei-
jing, Seoul, Tokyo, na Brussels.
Vilevile Bw. Handerson
ameeleza kuwa kampuni hiyo ya
Methanex ipo tayari kuja kuwekeza
nchini Tanzania kwa kuwa wanao
uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika
uwekezaji wa viwanda hivyo, wana
mfumo mzuri wa kutoa mafunzo
kwa wazawa ili kushiriki katika mi-
radi ya methano. Aliongeza kuwa,
wako tayari kushirikiana na serikali
ya Tanzania ili kuendeleza rasilimali
hiyo kwa manufaa ya wananchi.
Naye Naibu Waziri wa Nishati
na Madini anayeshughulikia Nisha-
ti, Charles Kitwanga aliikaribisha
kampuni hiyo kuja kuwekeza nchini
Tanzania kwa kuwa kuna kiasi ki-
kubwa cha gesi asilia cha zaidi ya futi
za ujazo trilioni 50 ambacho pamoja
na kutumika kuzalisha umeme pia
inaweza kutumika kwa shughuli ny-
ingine za kiuchumi ikiwamo kuten-
geneza methano na mbolea.
Alisema kuwa serikali ya Tan-
zania inakaribisha wawekezaji wa
ndani na nje ya nchi kuwekeza ka-
tika sekta za Nishati na Madini ili
kuleta maendeleo endelevu ya sekta
hizo na kwamba zipo sera, sheria
na kanuni nzuri ambazo pamoja na
mambo mengine zinalenga kuvutia
uwekezaji katika tasnia hiyo.
Katika Ziara hiyo ya Mafunzo,
Naibu Waziri Kitwanga ameam-
batana na baadhi ya wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini, Naibu Wa-
ziri katika Ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira,
Ummy Mwalimu na Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, ( TAMI-
SEMI), Kassim Majaliwa.
Tahariri
MEM
Na Badra Masoud
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
H
abari kubwa katika gazeti hili wiki hii ni uteuzi na ma-
badiliko yaliyofanywa na Waziri mwenye dhamana ya
Sekta ya Nishati na Madini nchini naye si mwingine
ni Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kwa watendaji wa
Wizara husika.
Lengo la mabadiliko hayo ni kusogeza huduma za Wizara ka-
ribu na Wananchi ambapo mbali na uteuzi wa Kaimu Mkurugen-
zi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
hatua nyingine ni kufungua ofisi nyingine mpya za madini katika
maeneo mbalimbali nchini.
Maeneo hayo mapya ni pamoja na Kanda mpya ya Ziwa Vic-
toria Mashariki ambayo ofisi yake itakuwa Musoma, Kanda ya
Ziwa Nyasa ambayo ofisi yake itakuwa Songea na ofisi mpya za
madini za mikoa ya Kilimanjaro, Njombe, Nachingwea na Bari-
adi.
Hii ni hatua nzuri ya Wizara yenye lengo la kuboresha hudu-
ma zake kwa wananchi pamoja na kuwa karibu nao ili kupunguza
urasimu unaopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya mtu mmoja
mmoja na hata taifa.
Kwa hakika Wizara ya Nishati na Madini imekuwa katika
mabadiliko katika maeneo mengi hususani katika sekta zake za
Madini na Nishati na ni miongoni mwa Wizara inayotekeleza
majukumu yake kwa vitendo ili kuwahudumia Watanzania.
Kimsingi, Wizara hii ni miongoni mwa Wizara nyeti, am-
bazo zinamgusa kila Mtanzania na ndiyo Wizara inayochochea
maendeleo ya uchumi wa taifa katika sekta zake zote za madini,
nishati ya umeme, mafuta na gesi.
Kutokana na umuhimu huo, Waziri mwenye dhamana ndiye
anayeshika bendera ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ndiyo
maana anatafuta kila njia ya kuondoa urasimu kwenye utendaji
ikiwemo ya kupata leseni za utafutaji madini ambapo hivi kar-
ibuni utazinduliwa utaratibu mpya wa kuomba leseni kupitia njia
ya mtandao popote mwombaji alipo badala ya mwombaji kulazi-
mika kuja Wizarani au katika ofisi za kanda.
Vilevile, mabadiliko hayo yanaendelea katika sekta ya umeme
ili kuondoa ukiritimba wa Shirika la Umeme Tanzania (TANE-
SCO) kufanya kila kitu ambapo Shirika hilo kwa sasa linaan-
daliwa kugawanywa katika Makampuni tofauti ya Uzalishaji
umeme, usafirishaji umeme na usambazaji umeme lengo likiwa
ni kuboresha utendaji wa shirika hilo.
Mabadiliko ndani ya Wizara ya Nishati na Madini yapo men-
gi ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi ikiwemo kufuta leseni za
Watafutaji madini walioomba lakini hawaendelezi utafutaji au
uchimbaji wa madini katika maeneo yao, wakiwemo wachimbaji
wakubwa na hata wadogo .
Pamoja na jitihada zote zinazofanywa na Wizara ni vizuri kila
Mtanzania akatambua kwamba yote hayo yanayofanywa ni kwa
ajili ya kuboresha huduma na hivyo, hatuna budi kuunga mkono
jitihada hizo badala ya kubeza au kulalama pasipo na mafanikio.
Tunapenda kuwaomba wale wote wenye mapenzi mema na
taifa hili kuunga mkono mabadiliko au maboresho katika sekta
zote za nishati na madini na wale ambao wanadhani kuna ma-
hali ambapo wanahitaji kuelimishwa au wana madukuduku au
wangependa kutoa ushauri kwa maslahi ya umma wasisite kufika
katika ofisi zetu za Madini au za nishati ya umeme (Tanesco) zi-
lizopo katika mikoa yote nchini.
Tanzania ni ya wote na kila mtu ana wajibu wa kuijenga kwa
nafasi yake, shime kila mmoja wetu tuwaunge mkono na kush-
irikiana na wote walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali ndani
ya Wizara ama katika taasisi iliyo chini ya Wizara ya Nishati na
Madini.
Tuwape ushirikiano
Watendaji walioteuliwa
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Tanzania yatajwa kuwa eneo
muhimu kuzalisha methano
Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Charles Kitwanga
(wa tatu kutoka kushoto),
Mwenyekiti Kamati ya Kudu-
mu ya Bunge ya Nishati na
Madini, Victor Mwambalas-
wa (wa pili kutoka kushoto)
na Mbunge wa Sumve,
Richard Ndasa (wa kwanza
kushoto) wakimsikiliza Eng.
Ken Paulson, Afisa Mkuu wa
Operesheni katika Kamish-
eni ya Gesi na Mafuta ya
Jimbo la British Columbia
nchini Canada mara walipo-
fika katika Kamisheni hiyo
ikiwa ni sehemu ya ziara ya
mafunzo kwa ujumbe huo
katika sekta ya uziduaji.
4 Bulletin News
http://www.mem.go.tz

Matukio katika picha
http://www.mem.go.tz
Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (wa kwanza
kushoto) akieleza jambo katika mkutano kati ya watendaji wa Kamisheni
ya Gesi na Mafuta ya Jimbo la British Columbia nchini Canada pamoja na
ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini,
Charles Kitwanga (wa tano kutoka kushoto).Wengine katika picha ni
Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa
(wa nne kutoka kushoto) Mbunge wa Ngara, Deogratias Ntukamazina
(wa pili kutoka kushoto), Richard Ndasa (Mb. Sumve), (wa tatu kutoka
kushoto), Raya Ibrahim (Mb.) (wa pili kutoka kulia) pamoja na watendaji
kutoka Wizara ya Nishati . Katikati ni Mhandisi. Ken Paulson, Afisa Mkuu
wa Operesheni katika Kamisheni ya Gesi na Mafuta ya Jimbo la British
Columbia nchini Canada.
Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada kwa ziara ya mafunzo
ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga
(aliyenyoosha mkono), ukiwa katika chumba cha kusimamia mitambo
ya kuzalisha methano (haionekani pichani) katika kiwanda cha kuzalisha
malighafi hiyo kilicho katika jimbo la Alberta nchini Canada.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli (TPDC) , Bw. James
Andilile (kushoto) akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkataba
kati ya serikali na kampuni ya Statoil. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC anayemaliza
muda wake, Bw. Yona Killagane.
5
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Tuzo za madini

Matukio katika picha
Jacqueline Aisaa akitoa maoni yake kuhusu sekta
ya Madini wakati wa maonesho ya 38 ya Biashara
ya Kimataifa Sabasaba 2014. Anayemsikiliza ni
Bw. Issa Mtuwa, Afisa Uhusiano wa STAMICO.
Na Issa Mtuwa STAMICO
W
ananchi wameiomba serikali kuhakikisha
rasilimali za madini zinawanufaisha Watan-
zania wote na sio wachache wenye uwezo,
kauli ambayo imewahi kutolewa siku za hivi
karibuni na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter
Muhongo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati walipotem-
belea katika banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (SABA-
SABA) 2014, wananchi hao wamesema ili azma hiyo iweze
kutimia ni vyema Serikali ikaijengea uwezo STAMICO
kifedha na vitendea kazi ili iweze kutekeleza miradi ya
uchorongaji na uchimbaji madini itakayowanufaisha wa-
nanchi.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake alioambatana
nao katika banda la STAMICO, Mkazi wa mkoa wa Mara,
Bw. Joel M. Changarawe amesema katika kujenga uwezo
wa kifedha wa Shirika hilo, Serikali haina budi kuendeleza
azma yake ya kuikabidhi STAMICO migodi yote mikubwa
ya Madini iweze kumiliki kwa niaba ya Watanzania na ku-
zalisha ili kuongeza tija kwa Taifa.
Nashauri Watanzania tuache ubinafsi na ubepari.
Naishauri serikali Migodi yote ya Madini yenye akiba (re-
serve) kubwa imilikiwe na STAMICO kwa niaba ya Wa-
tanzania badala ya kukabidhi kwa Watanzania wachache
wenye tamaa ya utajiri ambao wanamiliki vitalu vya madini
kupitia migongo ya kampuni za kigeni, alisema Bwana Joel
kwa kuandika kwenye kitabu maalum cha maoni, ushauri na
kero za wananchi.
Naye Jacqueline Aisaa mkazi wa Masama-Moshi, am-
baye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada
ya kwanza katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
alisema serikali iipe meno STAMICO ya usimamizi wa hisa
zote za serikali kwenye migodi yote na usimamizi wa jumla
katika sekta ya Madini ili Wananchi waweze kunufaika na
rasilimali hizo.
WANANCHI
WATAKA
STAMICO
IPEWE NGUVU
KUSIMAMIA
SEKTA YA MADINI
NCHINI
nWaunga mkono kauli ya Waziri wa Nishati na Madini
nWataka wenye uwezo kuacha ubinafsi na ubepari
nWataka rasilimali za madini ziwanufaishe Watanzania wote
Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na
Madini, Charles Kitwanga (wa nne kutoka kushoto, waliosimama), ukiwa katika picha
ya pamoja na watendaji wa kampuni ya kimataifa ya kuzalisha na kusafirisha methano
ya nchini Canada mara baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika kiwanda hicho.
Wengine katika picha ni Naibu Waziri, TAMISEMI, Kassim Majaliwa, (wa nne kutoka kulia,
waliosimama). Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy Mwalimu, (wa
pili kutoka kulia waliosimama) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Na Leonard
Mwakalebela,
STAMICO
S
HIRIKA la Madini
la Taifa (STAMICO)
limefunga upokeaji wa
maombi ya nia (expression
of interest) ya makampuni yanayo-
taka kuingia ubia na shirika hilo ka-
tika uendelezaji wa mradi wa uchim-
baji makaa ya mawe na ufuaji umeme
huko Kiwira.
STAMICO ilitangaza mwezi
uliopita kukaribisha maombi hayo ya-
takayowezesha ubia huo kupata fedha
za kugharamia mradi kwa asilimia 100
na kushiriki kuendesha mradi husika
Makampuni yenye nia ya ku-
wekeza kwa ubia na STAMICO
yalitakiwa kuwasilisha maelezo ya
kutosha kuhusu makampuni hayo
pamoja na uthibitisho wa uzoefu wa
kuendesha migodi ya makaa ya mawe
na ufuaji umeme kwa kutumia makaa
ya mawe.
Makampuni hayo pia yalitakiwa
kuonesha uzoefu wao katika kue-
ndesha miradi kama hiyo sehemu
nyingine Duniani ikiwemo nchi za
Afrika.
Aidha STAMICO iliyataka
makampuni yenye nia kuonesha uw-
ezo wake wa kifedha na kiufundi.
Maombi ya makampuni hayo pia
yalitakiwa kuonesha namna gani ya-
takavyotumia utaalamu na huduma
za ndani kama ilivyoainishwa kwenye
Sheria ya Madini ya mwaka 2010.
Makampuni ambayo maombi
yake yatakubaliwa na STAMICO
yatakaribishwa kuchukua nyaraka za
zabuni na kuwasilisha michanganuo
yao ya kiufundi na kifedha.
Uendelezaji wa mradi Kiwira
umegawanyika katika sehemu nne
ambazo ni upanuzi wa mgodi uliopo
chini ya ardhi, ujenzi wa mgodi wa
wazi, ununuzi na ufungaji wa mitam-
bo ya kufua umeme na ujenzi wa njia
za kusafirisha umeme.
Upanuzi wa mgodi wa chini
utakaoongeza uzalishaji wa makaa
ya mawe kutoka tani 150,000 kwa
mwaka hadi tani 300,000 kwa mwaka
wakati mgodi mpya wa wazi unat-
egemea kuzalisha tani milioni 1.2 za
makaa ya mawe kwa mwaka.
Uendelezaji wa mradi huu pia uta-
husisha ujenzi wa mtambo wa kufua
umeme wa Megawati 200 na ujenzi
wa njia ya kusafirisha yenye urefu wa
km 100 toka eneo la Kiwira Wilayani
Ileje hadi Mbeya mjini.
Ujenzi wa mgodi wa Kiwira ul-
ianza mwaka 1983 na kukamilika
1988 kwa gharama za shilingi bil-
ioni 29, ukiwa ni mkopo wa masharti
nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China.
Mwezi Juni, 2005 mgodi wa Ki-
wira ulibinafsishwa kwa kampuni ya
Tan Power Resources (TPR) kwa asil-
imia 70 na Serikali ilibaki na asilimia
30.
Ubia huu ulilenga zaidi katika
kuzalisha umeme wa MW 200 kwa
kutumia makaa ya mawe ifikapo 2009.
Katika kipindi cha kuanzia Juni,
2005 hadi Julai,2009 zilifanyika kazi
mbalimbali za kuendeleza mgodi huu.
Miongoni mwa kazi hizo ni upem-
buzi yakinifu na usanifu wa mgodi,
upembuzi yakinifu kwa ajili ya kufua
umeme wa MW 200 na kusainiwa
kwa mkataba wa mauzo ya umeme
wa MW 200 na TANESCO mnamo
mwezi Agosti 2006.
Kazi nyingine ni kusainiwa kwa
mikataba ya ujenzi na utengenezaji wa
mitambo, kukamilika kwa tathmini
nne za mazingira na kukamilika kwa
upimaji wa njia ya umeme ya kV 220
kutoka eneo la mgodi kwenda Mbeya.
Mwezi Julai,2009 Serikali ilia-
mua kuurudisha mgodi wa Kiwira
Serikalini kwa asilimia 100 kutokana
na kukwama kwa uendelezaji wa
Mgodi chini ya TPR na kushindwa
kuwalipa wafanyakazi mishahara yao
kwa muda mrefu tangu mwezi Ago-
sti,2008.
Baada ya majadiliano ya muda
mrefu, tarehe 28, Novemba 2011 Seri-
kali na TPR zilifikia muafaka wa Seri-
kali kuuchukua mgodi kwa asilimia
100.
Mtaji unaohitajika kuendeleza
mgodi huu ni takriban Dola za Mare-
kani Milioni 400 ambazo zinaweza
kupatikana kwa njia mbili;kwa
kumtafuta mbia mwenye uwezo wa
fedha au kwa kukopa katika taasisi
mbalimbali za fedha.
Aidha STAMICO inaangalia
uwezekano wa kufanyia ukarabati
mashine ya kufua umeme ya MW 6
iliyopo katika mgodi huu ili umeme
utakaozalishwa uuzwe TANESCO.
Katika mwaka wa fedha 2014/15,
Serikali imeitengea STAMICO shilin-
gi bilioni tano kwa ajili ya usimamizi
na uangalizi wa mgodi katika kipindi
hiki cha mpito.
Stamico yafunga maombi uchimbaji
makaa ya mawe na ufuaji umeme
6 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI
KITWANGA
Serikali yashauriwa kuwabana wawekezaji
Na Teresia Mhagama,
Canada
S
erikali ya Tanzania imeshau-
riwa kuweka sheria mad-
hubuti zitakazohakikisha
wawekezaji wa kigeni wan-
aleta faida nchini badala ya
kunufaisha makampuni yao pekee.
Hayo yamesemwa na Bw. Zee-
shan Syed, Mkurugenzi wa Ma-
husiano ya Kitaifa, Kimataifa na
Serikali katika Taasisi ya Udhibiti
Maendeleo ya Nishati ya Jimbo la
Alberta nchini Canada wakati al-
ipokuwa akizungumza na Ujumbe
wa Tanzania ulioongozwa na Nai-
bu Waziri wa Nishati na Madini,
Charles Kitwanga uliofika katika
Makao Makuu ya Taasisi hiyo iki-
wa ni sehemu ya ziara ya mafunzo
kuhusu sekta ya uziduaji.
Kwa kawaida wananchi huwa
wana matarajio makubwa ya man-
ufaa ya rasilimali zinazowazun-
guka hivyo ni muhimu kwa serikali
kuwa na sheria zitakazowabana
wawekezaji ili wanapomaliza shu-
ghuli zao, pia faida ibaki kwa wa-
nanchi, alisema Bw.Syed.
Mkurugenzi huyo alieleza
kuwa licha ya taasisi hiyo kuwa
mdhibiti wa nishati lakini vilevile
ina jukumu la kudhibiti uhifadhi
wa mazingira ili kuhakikisha kuwa
shughuli za uendelezaji wa nishati
zinafuata sheria za nchi za utunzaji
mazingira.
Naye Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Mhe. Charles Kitwanga
alimweleza Bw. Syed kuwa licha ya
Tanzania kuwa na Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati
na Maji (EWURA), bado nchi ina-
hitaji kujifunza kutoka kwa nchi
nyingine zenye uzoefu ili kubore-
sha shughuli za udhibiti nchini
Tanzania.
Shughuli za udhibiti nishati
katika Taasisi hii zina zaidi ya
miaka 75 na hivyo Tanzania inahi-
taji kupata uzoefu kutoka kwenu ili
kufahamu hatua mlizopitia kufika
hapa mlipo leo, alisema Waziri
Kitwanga.
Wakati huohuo , Naibu Waziri
na Ujumbe wake unaojumuisha
baadhi ya wabunge kutoka Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini walitembelea Chuo Kikuu
cha Calgary ambacho kimebobea
katika kutoa elimu juu ya masu-
ala ya sera za Uchumi, Nishati,
Mazingira na kutoa ushauri katika
utengenezaji sera katika sekta ya
uziduaji.
Katika Chuo hicho Ujumbe
huo ulikutana na Mkurugenzi
anayeshughulikia Sera za Umma,
Bw. Jack Mintz ambaye aliueleza
ujumbe huo kuwa Tanzania ni
moja kati ya nchi sita duniani na
ni pekee kutoka barani Afrika
ambazo zinapewa kipaumbele na
chuo hicho katika masuala ya ush-
irikiano wa kujenga uwezo kwenye
masuala ya sera.
Mkurugenzi huyo alieleza
kuwa, Chuo cha Calgary kita-
shirikiana na Tanzania katika ku-
wajengea uwezo watumishi kwa
kutumia vyuo vingine ambavyo
wana ushirikiano navyo na kwam-
ba mafunzo hayo yanaweza ku-
fanyika ndani na nje ya Tanzania.
Pamoja na suala la kujenga
uwezo kwa watanzania ili ku-
weza kuandaa sera zitakazokuwa
na manufaa kwa nchi, Bw. Mintz
aliueleza Ujumbe huo kuwa ni
muhimu kwa serikali ikawa ndiyo
msimamizi mkuu wa rasilimali
za nchi ili faida zinazotokana na
rasilimali hizo ziwafikie wananchi
wote.
Kwa upande wake, Naibu Wa-
ziri Katika Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mi-
taa (TAMISEMI), Mhe. Kassim
Majaliwa pamoja na kukishukuru
Chuo hicho kwa kuipa Tanzania
kipaumbele katika kujenga uelewa,
alimweleza Mkurugenzi wa Chuo
hicho kuwa hivi sasa nchi ya Tan-
zania inakaribisha wawekezaji
wa ndani na nje kuwekeza nchini
hivyo, suala la kupata elimu na
uzoefu zaidi ili kuendana na kasi
ya uwekezaji ni moja ya masuala
muhimu ambayo yanapewa kip-
aumbele.
Ziarani Canada
Ujumbe kutoka Tanzania
ukiwa katika makao makuu
ya Taasisi ya Udhibiti Nishati
katika jimbo la Alberta nchini
Canada.Katika picha ni,
Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Charles Kitwanga
(wa sita kutoka kulia), Naibu
Waziri TAMISEMI, Kassim
Majaliwa (wa tano kutoka
kulia), Naibu Waziri Ofsi ya
Makamu wa Rais-Mazingira,
Ummy Mwalimu (wa tatu
kushoto). Wabunge, Richard
Ndasa (wa nne kutoka kulia),
Raya Khamisi (wa pili kutoka
kulia). Wengine ni wataalam
kutoka Wizara ya Nishati na
Madini na watendaji kutoka
Mamlaka ya Udhibiti Nishati
ya Alberta wakiongozwa na
Zeeshan Syed, Mkurugenzi
wa Mahusiano ya Kitaifa,
Ujumbe kutoka Tanzania ukiwa Chuo Kikuu cha Calgary katika jimbo la Alberta nchini Canada.Katika picha kutoka kushoto ni,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa saba), Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa (wa tano), Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy Mwalimu (wa sita). Wabunge, Richard Ndasa (wa nne), Deogratias Ntukamazina (wa
tatu), Murtaza Mangungu (wa pili) na Shafin Sumar (wa kwanza kushoto. Wengine (kulia) ni wataalam kutoka Wizara ya Nishati na
Madini na watendaji kutoka Chuo Kikuu cha Calgary, Canada.
7
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
Wachimbaji wadogo waaswa
kuzingatia sheria ya madini
Na Nuru Mwasampeta
K
amishna wa Madini nchi-
ni, Mhandisi Paul Masanja
amewaasa wachimbaji wa-
dogo wa madini wanao-
vunja Sheria kwa kuchim-
ba bila leseni, kuacha mara moja na
kuzingatia Sheria ya Madini ya Mwaka
2010 inayokataza watu kujihusisha na
shughuli za utafutaji, uchimbaji na bi-
ashara ya madini bila leseni.
Aliyasema hayo hivi karibuni al-
ipofanya ziara ya kutatua migogoro ya
madini katika Kanda ya Kati Magharibi
na Kanda ya Ziwa Viktoria.
Kamishna Masanja, aliyeambat-
ana na Kamishna Msaidizi wa Ma-
dini Sehemu ya Leseni, Mhandisi John
Nayopa, alibainisha kuwa migogoro
hiyo imekuwa na athari kubwa katika
maendeleo ya ya sekta ya madini kwa
kuwa imesababisha nchi kuonekana ka-
tika anga za kimataifa kuwa na udhaifu
katika maeneo mbalimbali yanayohusu
usimamizi mzuri katika sekta husika.
Akitoa ufafanuzi, Mhandisi
Masanja alisema nchi inalaumiwa kwa
kuwa na udhaifu katika usimamizi wa
Sheria ya Madini, kutoa upendeleo
kwa wachimbaji wasio rasmi dhidi ya
wamiliki halali wa leseni za utafiti na
kushindwa kuzuia vurugu na maafa ka-
tika maeneo ya madini.
Alibainisha kuwa, wachimbaji
wadogo wanatakiwa kutambua haki
za wamiliki wa leseni na kuwataka
kuachana na tabia ya kuvamia maeneo
mbalimbali yanayomilikiwa kisheria
na kampuni au watu binafsi kwani hali
hiyo inasababisha wamiliki kushindwa
kuendelea na shughuli zao zikiwemo za
utafiti na uchimbaji madini.
Vilevile, alieleza kuwa uchimbaji
haramu unasababisha ajali nyingi na
pia kusababisha madini kuishia mikon-
oni mwa walanguzi, hivyo akasisitiza
kuwa inabidi uchimbaji wa aina hiyo
ukomeshwe mara moja.
Alisisitiza kuwa kwa nafasi yake
ya ukamishna, ana wajibu wa kuwalea
wawekezaji wakubwa na wadogo kwa
kuhakikisha kuwa sheria zinazingati-
wa na kwamba kila upande unapaswa
kuheshimu haki ya mwenzake.
Aidha, Kamishna Masanja aliitu-
mia fursa hiyo kuwaelekeza wachimbaji
hao kuunda vikundi na kuomba leseni
za kuchimba madini hususan wakati
huu ambapo serikali imetenga maeneo
sehemu mbalimbali kwa ajili ya uchim-
baji mdogo, zoezi ambalo alisema lin-
aendelea.
Katika ziara hiyo, Kamishna
Masanja na Ujumbe wake walitembe-
lea maeneo ya Mwanshina-Lusu (Nze-
ga), Shenda na Kanegele (Mbogwe),
Mwime, Nyangalata na Mwabomba
(Kahama) na Ishokelahela (Misungwi).
KITWANGA
Wataalamu mafuta na
gesi Tanzania, kupata
mafunzo Canada
Na Teresia Mhagama, Canada
S
erikali ya Tanzania inatarajia kutuma wataalam kwenda
nchini Canada katika Kamisheni ya Mafuta na Gesi ya
Jimbo la British Columbia (BC Oil& Gas Commission),
kwa lengo la kuwawezesha kupata uelewa zaidi katika
masuala ya udhibiti wa mafuta na gesi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga wakati akizun-
gumza na watendaji wa Kamisheni ya Mafuta na Gesi ya Jimbo
la British Columbia katika Ofisi za Kamisheni hiyo zilizopo ka-
tika mji wa Victoria nchini Canada.
Akiongoza Ujumbe wa Tanzania uliotembelea Kamisheni
hiyo ili kujifunza masuala ya udhibiti wa sekta ndogo ya gesi
asilia na mafuta, Naibu Waziri alisema kuwa lengo la serikali
ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo zinaende-
lezwa na faida yake kuonekana kwa wananchi, hivyo wataalam
watakwenda nchini Canada katika Kamisheni hiyo ili kuongeza
uelewa katika masuala ya udhibiti ambao kwa kiasi kikubwa
utachangia katika kuhakikisha kunakuwa na maendeleo endel-
evu ya rasilimali zilizopo nchini.
Mtazamo wa wananchi wengi ni kuwa makampuni ya ki-
geni yanapokuja nchini hukuchukua rasilimali na kuondoka
nazo bila wananchi hao kufaidika, hivyo, serikali inafanya kila
jitihada ili faida za rasilimali zetu ziwafikie wananchi wote na
moja ya vigezo vya jitihada hizo ni kuwa na mamlaka madhubu-
ti za udhibiti zitakazohakikisha makampuni ya nje na ndani ya
nchi yanafanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria zinazoon-
goza sekta husika, alisema Kitwanga.
Naibu Waziri aliongeza kuwa, Tanzania ikiwa katika mchaka-
to wa kutengeneza sheria na kanuni zitakazoongoza sekta ya gesi
asilia na mafuta, inahitaji kupata maoni na uelewa zaidi kutoka
katika nchi zilizopiga hatua katika uendelezaji wa rasilimali hizo
ikiwemo Jimbo la British Columbia ambalo limegundua gesi asi-
lia kiasi cha zaidi ya futi za ujazo trilioni 2900.
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Operesheni katika Kam-
isheni ya Gesi na Mafuta ya British Columbia, Mhandisi Ken
Paulson alieleza kuwa Kamisheni hiyo ambayo imeanzishwa
zaidi ya miaka 15 iliyopita ina jukumu la kudhibiti shughuli zote
za mafuta na gesi asilia ikihusisha utafiti, uendelezaji na usa-
firishaji wa rasilimali hizo kwa njia ya bomba.
Mhandisi Paulson alieleza kuwa Kamisheni hiyo pia ina ju-
kumu la kukusanya takwimu za kijiolojia zinazotumika katika
shughuli za utafutaji wa gesi asilia na mafuta na kuzitangaza kwa
njia ya tenda ili makampuni yanayohitaji kufanya shughuli za
utafutaji mafuta na gesi katika jimbo hilo yanunue takwimu hizo
kutoka Kamisheni hiyo.
Kuhusu matumizi ya gesi asilia, Afisa Mkuu wa Operesheni
aliueleza ujumbe huo kuwa asilimia 15 ya kiasi cha gesi kilicho-
gunduliwa katika jimbo hilo kinatumika ndani ya jimbo la British
Columbia kwa matumizi mbalimbali na kiasi kinachobaki kina-
safirishwa kwenda Bara la Amerika Kaskazini.
Ingawa tunasafirisha gesi kwenda Amerika Kaskazini,
mahitaji ya soko hilo yanashuka kutokana na kuongezeka kwa
uzalishaji wa gesi nchini Amerika, hata hivyo tumejipanga ku-
kabiliana na hali hiyo kwa kutumia gesi hii kwa masuala men-
gine ikiwemo kuzalisha methano, matumizi ya majumbani na
kutumika katika vivuko ambavyo vitakuwa vinatumia mafuta na
gesi, alisema Mhandisi Paulson.
Kuhusu mfumo wa ugawanaji mapato (PSA) kati ya makam-
puni ya utafutaji na uchimbaji gesi asilia na mafuta, Mhandisi
Paulson alieleza kuwa kampuni ikianza uzalishaji wa gesi au
mafuta, serikali ya jimbo hilo hukusanya mrabaha wa kati ya asil-
imia 10 hadi 20 ya mapato.
Katika ziara hiyo ya mafunzo nchini Canada, Naibu Waziri
wa Nishati na Madini ameambatana na Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalas-
wa pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo,
Murtaza Mangungu (Mb.), Raya Ibrahim (Mb.), Richard Ndasa
(Mb.) wengine ni Deogratias Ntukamazina (Mb.), Shafin Sumar
(Mb.) na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Mpango Mkakati ni muhimu katika
utekelezaji mradi wa usambazaji gesi
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam
W
aziri wa Nishati
na Madini Profesa
Sospeter Muhongo
ameyataka makam-
puni yaliyoungana kwa ajili ya kufani-
kisha ujenzi wa kiwanda cha kuchaka-
ta gesi kuwa na mpango wa utekelezaji
wa mradi huo utakaotoa dira ya
utekelezaji wa mradi, na kuongeza
kuwa, Serikali iko tayari kushirikiana
na makampuni hayo kwa kila hatua ili
kuhakikisha kuwa wanafanikiwa
Profesa Muhongo aliyasema hayo
jijini Dar es Salaam alipokutana na
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya
British Gas (BG) Group Bw. Andrew
Gould aliyeambatana na viongozi
waandamizi kutoka kampuni hiyo.
Kampuni zilizoungana kwa ajili ya
kutekeleza mradi huo ni BG Group,
Statoil, ExxonMobil, Ophir na Pavil-
ion ambazo zitashirikiana na Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
katika kufanikisha ujenzi wa kiwanda
cha kuchakata gesi unaotarajiwa kuan-
za mara baada ya taratibu za tathmini
mbalimbali kukamilika
Mbali na kuwa na Mpango
Mkakati wa Utekelezaji wa Mradi,
Profesa Muhongo aliyataka makam-
puni hayo kushirikiana kwa karibu
zaidi ili kufanikisha malengo yaliyoji-
wekea.
Mpango Mkakati wa utekelezaji
wa mradi ni muhimu mno katika mra-
di mkubwa kama huu, unaweza ku-
fuatwa na kufanyiwa marekebisho pale
inapohitajika lakini kwa kushirikiana.
alisisitiza Profesa Muhongo.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
Bw. Yona Killaghane alisema kuwa
shirika la TPDC lilipewa taarifa kwa
kila hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya
makampuni hayo ya kufungua ofisi ya
mradi.
Naye Mkurugenzi wa BG- Afrika
Mashariki Bw. Derek Hudson akizun-
gumzia mafanikio ya kampuni hiyo
katika kuendeleza wataalamu wake
alisema kuwa kampuni imekuwa
ikipeleka wataalamu wa kitanzania
kwenda kusomea masuala ya mafuta
na gesi katika vyuo vikuu vilivyopo
nchini Uingereza na Australia na
kuongeza kuwa kwa mwaka huu wana
mpango wa kupeleka wataalamu wa-
tano kutoka kampuni hiyo kwenda
kusoma nje ya nchi.
Aidha, Bw. Hudson aliongeza
kuwa wamekuwa wakifadhili wa-
nafunzi kusoma katika Chuo kikuu
cha Dodoma kwa ajili ya kusomea
masuala ya gesi na mafuta.
Alisisitiza kuwa kampuni pia ime-
anza mchakato wa kuwasaidia wakazi
wa Mtwara kupitia michezo kama wal-
ivyoomba awali walipokutana nao.
Naye Profesa Muhongo alisisitiza
kuwa kampuni ya BG Group inataki-
wa kufikiria kuendeleza watumishi ku-
toka TPDC, Wizara ya Nishati na Ma-
dini pamoja na vyuo vya elimu ya juu
ili kuzalisha wataalamu wengi zaidi.
Mwenyekiti Mtendaji na Mku-
rugenzi Mtendaji wa kampuni ya BG
Group Bw. Andrew Gould akielezea
mafanikio ya kampuni hiyo alisema
mpaka sasa imegundua gesi kiasi cha
futi za ujazo trilioni 15 na kuongeza
kuwa BG itahakikisha inatimiza ndoto
zake za kuchangia katika ukuaji wa
uchumi wa Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza na ujumbe kutoka kampuni ya BG Group
ikiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wake Bw. Andrew Gould (wapili kulia) pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati
8 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
HABARI
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA
Na Nuru Mwasam-
peta, Lindi
W
aziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo
amewaagiza wakandar-
asi miradi ya usambazaji
umeme inayotekelezwa chini ya Wakala wa
Nishati Vijijini, awamu ya pili (REA II) ku-
kamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kupun-
guza malalamiko ya wananchi wa Mikoa
ya Kusini wanaodai kutokuwepo kwa dalili
za utekelezaji wa mradi huo ikilinganishwa
na maeneo mengine nchini.
Profesa Muhongo aliyasema hayo al-
ipokuwa akizungumza na wakandarasi wa
kampuni ya kusambaza umeme ya MBH
aliokutana nao Mkoani Lindi hivi karibuni
wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo
ya ujenzi wa bomba la gesi unaoendelea
nchini.
Aidha, Profesa Muhongo aliwataka
wakandarasi wote wanaotekeleza miradi
ya umeme nchini kutokuchukua tenda
pindi watakapobaini kuwa kazi hiyo ha-
wataiweza ili tenda hiyo ikabidhiwe kwa
watu wengine wenye uwezo wa kufanya
kazi hiyo.
Ili kupewa tenda unatakiwa kufanya
kazi kwa bidii, tunataka kazi nzuri ita-
kayokamilika kwa wakati na yenye kuri-
dhisha Alisema Profesa Muhongo
Profesa Muhongo alisisitiza kuwa si
wakandarasi peke yao watakaopoteza kazi
bali hata mameneja wa wilaya na mikoa
wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO)
watakaoshindwa kusimamia utekelezaji wa
miradi na kuikamilisha kwa wakati wata-
poteza kazi zao.
Akizungumzia suala la usimamizi wa
miradi ya REA II Mkurugenzi wa huduma
za ufundi wa REA Mhandisi Bengiel Msofe
alisema watakutana na wakandarasi wote
wanaojenga mitambo ya REA II Jumanne
ya tarehe 22 Julai ili kuwasisitizia juu ya nia
yao ya kutaka miradi hiyo kukamilishwa
kwa wakati waliokubaliana.
Akizungumzia suala la malalamiko
mengi yanayofikishwa wizarani juu ya
ucheleweshwaji wa kuanza utekelezaji wa
mradi huo mikoa ya Kusini, Mhandisi
Msofe alibainisha kwamba, tenda zilipotan-
gazwa kwa ajili ya ujenzi wa njia za umeme
mikoa yote ilipata wakandarasi walioomba
tenda hiyo isipokuwa mikoa ya Lindi na
Mtwara ambayo haikuwa na mkandar-
asi aliyeomba, jambo ambalo lilipelekea
ucheleweshwaji huo ambao umepata ufum-
buzi baada ya kumpata mkandarasi aliyepo
ambaye ameahidi kutekeleza mradi huo
kwa wakati.
Wakandarasi wasio na uwezo
warudishe tenda Muhongo
TUFANYE KAZI KWA UADILIFU, BIDII, WELEDI,
NA USHIRIKIANO BILA KUKATA TAMAA
DAIMA TUSONGE MBELE
KURUDI NYUMA NI MWIKO!!
UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII
Waziri akisalimiana na wajenzi wa bomba la gesi katika eneo la Mto Rufiji.
Asteria Muhozya na Veronica
Simba, Dar es Salaam
W
izara ya Nishati na Madini inatarajia
kufanya warsha kuhusu mabadiliko ya
tabianchi kuanzia tarehe 21 na Julai 24,
2014 mkoani Morogoro itakayohusisha
maafisa wa ngazi mbalimbali kama njia mojawapo
ya kutoa elimu ya utunzaji mazingira. Warsha hiyo
inatarajiwa kufunguliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi
Mwihava.
Akizungumza ofisini kwake hivi karibuni, Afisa
Mazingira Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
Bw. Theodore Silinge alisema kuwa lengo la warsha
hiyo ni kuelimisha na kuhamasisha maafisa wa wizara
ili wawe mstari wa mbele katika kusimamia matumizi
bora ya rasilimali hasa za nishati na madini pamoja na
kuzingatia uhifadhi wa mazingira.
Silinge alisema kuwa mabadiliko ya tabia nchi ya-
nasababishwa na kuongezeka kwa hewa ukaa (Green-
house gases) angani inayosababishwa na matumizi
mabaya ya rasilimali za nishati, ardhi na misitu na
kuongeza kuwa iwapo rasilimali za nishati na madini
zitasimamiwa kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira,
mabadiliko ya tabia nchi hayawezi kujitokeza.
Mabadiliko ya tabia nchi yana athari katika
uchumi wa nchi, kwa mfano ukame uliosababishwa
na mabadiliko hayo umepelekea mabwawa ya maji
kukauka na mitambo ya kuzalisha umeme wa maji
kushindwa kufanya kazi hali ambayo imeathiri uchu-
mi wa nchi kwa kiasi fulani. alisema Silinge.
Bw. Silinge aliendelea kusema kuwa mafunzo
hayo ni mojawapo ya mikakati iliyowekwa na Kitengo
cha Mazingira katika kuelimisha umma na kuongeza
kuwa mafunzo hayo yatatolewa na wataalamu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Akizungumzia mada zitakazowasilishwa ka-
tika warsha hiyo, Silinge alieleza kuwa ni pamoja na
chimbuko la mabadiliko ya tabia - nchi na sayansi zake,
matumizi ya nishati jadidifu na mahusiano yake katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mada nyingine ni pamoja na mikakati ambayo
serikali ya Tanzania imechukua katika kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi, madhara yaletwayo na ma-
badilko ya tabia-nchi katika sekta za nishati, madini,
kilimo, maji na miundombinu, mabadiliko ya tabianchi
na usalama na mabadiliko ya tabianchi na uchumi.
Warsha hii ni mwendelezo wa warsha mbalimbali
za mazingira zinazoendeshwa na Kitengo husika kwa
lengo la kujenga uelewa wa masuala ya mazingira kwa
kada mbalimbali. Warsha nyingine zilizowahi kuanda-
liwa na Kitengo cha mazinira zilihusisha maafisa wak-
aguzi wa mazingira wa Wizara na wa Kanda pamoja
na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Umeme Tanza-
nia (TANESCO).
Warsha Mabadiliko ya Tabia
Nchi kufanyika Morogoro

You might also like