You are on page 1of 2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Baraza la Madiwani la Manispaa yaa Kinondoni katika Kikao chake cha tarehe
22/07/2014 siku ya Jumanne, chini ya Mstahiki Meya Mh.Yusuph Mwenda pamoja
na mambo mengine lilijadili na kutolea maamuzi ya mashauri ya mashtaka ya
nidhamu yaliyofunguliwa kwa Watumishi 11 wa Idara mbalimbali za Manispaa
waliofanya makosa mbalimbali kama Utoro kazini, Matumizi mabaya ya madaraka na
ofsi.
Kati ya Watumishi 11 waliofunguliwa Mashtaka, watumishi 6 ni wa Idara ya Afya, 2 ni
wa Idara ya Elimu ya Sekondari (Walimu wa Leseni) na 3 ni wa Idara ya Utawala na
Utumishi kada ya Maafsa watendaji wa Mitaa ambao ni 2 na polisi msaidizi 1.
Aidha Baraza limefkia uamuzi wa kuwafukuza kazi watumishi 9 na kuwapa karipio
watumishi 2. Kati ya watumishi 9 waliofukuzwa kazi, watumishi 4 ni wa Idara ya
Afya, 3 Idara ya Utawala na Utumishi ambao ni Maafsa watendaji wa Mitaa 2 na
Polisi Msaidizi 1, na 2 kutoka idara ya Elimu ya Sekondari ambao ni walimu wa
Lesseni.
Watumishi 2 waliopewa karipio kutoka Idara ya Afya wametakiwa kujirekebisha,
ambapo watakuwa katika uangalizi kwa muda kuona kama wamejirekebisha
mienendo yao.
Baraza la Madiwani limewataka watumishi wote, kuzingatia sheria, taratibu, kanuni,
miongozo na maelekezo mbalimbali ya Serikali katika kutekeleza majukumu yao ya
kutoa huduma kwa Umma sambamba na kuheshimu maadili ya kazi zao kwa hekima
na busara, ili kuweza kutoa huduma bora kwa wakazi wa Kinondoni.
Aidha, Baraza limesisitiza kuwa halitasita na litaendelea kuchukua hatua za
kinidhamu kwa watumishi wanao fanya makosa mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
SEBASTIAN MHOWERA
AFISA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.

You might also like