You are on page 1of 9

Bulletin

News
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
Toleo No. 27 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Agosti 1-7, 2014
Bomba la gesi laanza kutumika Dar es Salaam-Uk3
Masele angara Masele angara
n Akiwa mafunzoni Marekani
n Awakilisha viongozi vijana kuhutubia Marais duniani
n Obama ampa heko na kusisitiza vijana kupewa nafasi
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kulia) katika picha ya pamoja
na washiriki wa mafunzo kwa viongozi vijana walioonyesha dira kutoka nchi mbalimbali barani
Afrika, mafunzo yaliyofanyika katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida kwa muda wa wiki Sita.
n Akiwa mafunzoni Marekani
n Awakilisha viongozi vijana kuhutubia Marais duniani
n Obama ampa heko na kusisitiza vijana kupewa nafasi
2 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
Na Nuru
Mwasampeta,
Mtwara
W
aziri wa Ni-
shati na Madini
Profesa Sos-
peter Muhongo
amesema upitishwaji wa
bomba la gesi chini ya bahari
umekamilika na kinachosub-
iriwa hivi sasa ni kuungan-
ishwa na mabomba ya nchi
kavu.
Waziri Muhongo amese-
ma hayo mkoani Mtwara
wakati alipofanya ziara ya
kukagua maendeleo ya ujenzi
wa bomba la gesi ambapo,
alisema kuwa, hatua iliyofiki-
wa katika ujenzi huo inari-
dhisha na kuongeza kwamba,
ujenzi huo wa bomba la gesi
kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam utakamilika kwa
wakati uliopangwa au kabla
ya hapo.
Aliongeza kuwa, mara
baada ya kuanza kusafirisha
gesi kila mwananchi atakuwa
katika nafasi ya kuunganishi-
wa huduma hiyo kama ilivyo
katika huduma za kuungan-
ishiwa maji na umeme.
Kwa upande wake Me-
neja wa ujenzi wa bomba hilo
ndani ya bahari Bw. Alex Xu
alieleza kuwa, kazi hiyo ya
kuunganisha mabomba chini
ya bahari imefanyika kitaala-
mu kwa kutumia teknolojia za
hali ya juu ndani ya meli pa-
sipo kutumia rasilimali watu
kuingia chini ya bahari.
Aidha katika ziara hiyo,
Waziri Muhongo alipata fursa
ya kuelezwa kila hatua iliyo-
fanyika katika uunganishaji
wa mabomba hayo.Ujenzi wa
bomba la gesi kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam unatara-
jiwa kukamilika mwishoni
mwa mwaka huu.
MASELE ANGARA MAREKANI
Na Mwandishi Wetu
N
aibu Waziri wa Nishati na Ma-
dini, Stephen Masele anaende-
lea kupeperusha vizuri bendera
ya Tanzania ndani ya Taifa kub-
wa kimaendeleo na kiuchumi la Marekani
kwa kuchaguliwa kutoa hotuba kwa niaba
ya viongozi wa Afrika walioko mafunzoni
nchini humo.
Mhe. Masele aliwakilisha viongozi hao
vijana mbele ya baadhi ya viongozi mbal-
imbali akiwamo Rais wa Marekani Barack
Obama akitoa mada iliyokuwa ikihusu
masuala ya uongozi bora kwa kizazi kija-
cho (Governing For the Next Generation)
na kuombwa kuwasilisha mada hiyo kati-
ka mkutano mwingine wa Marais wa nchi
mbalimbali dunaini utakaofanyika Wash-
ington DC tarehe 6 Agosti mwaka huu.
Ndugu zangu nimekutana na Rais
Barack Obama na Mkutano wetu sisi vi-
jana ulikuwa na manufaa makubwa hu-
susan kwa sisi viongozi vijana wa Afrika
maana ajenda tulizojadili kwenye kikao
hicho zimejumuishwa katika mkutano
mwingine na Wakuu wa nchi malimbali
duniani, alisema Masele
Nina imani kwamba Rais Obama ata-
saidia kushinikiza kuongezwa kwa fursa za
uongozi na ushiriki wa vijana zaidi kwenye
kupanga na kutekeleza maamuzi, alisisiti-
za Masele.
Wakati huohuo Naibu Waziri alieleza
kuwa umefika wakati kwa viongozi wa Af-
rika kuwajibika, kuongoza kwa mfano na
kuwa wawazi kwa wananchi wanaowa-
tumikia kama ilivyo katika nchi ya Mare-
kani.
Naibu Waziri alisema hayo nchini
Marekani wakati alipohudhuria mafunzo
kwa viongozi vijana walioonyesha dira
kutoka nchi mbalimbali barani Afrika,
mafunzo yaliyofanyika katika vyuo vikuu
vya Arkansas na Florida kwa muda wa
wiki Sita.
Akiwa ni miongoni mwa watanzania
wachache waliopata fursa ya kuhudhuria
programu hiyo iliyoanzishwa na Rais wa
Marekani, Barack Obama, Masele amese-
ma kuwa, ametumia nafasi ya masomo
yake nchini Marekani kujifunza jinsi mfu-
mo wa siasa wa nchi hiyo unavyoundwa
na kufanya kazi na kuahidi kutumia baa-
dhi ya kanuni hizo kwa manufaa ya Taifa,
wakati atakaporejea nchini.
Kuhusu suala la ajira, Masele amese-
ma kuwa, Serikali ya Tanzania inajitahidi
kuondoa suala la ukosefu wa ajira kwa
kutengeneza ajira kupitia vyanzo mbalim-
bali lengo likiwa kuwaandaa vijana kuwa
viongozi bora na yeye lengo lake ni kuona
vijana wa Kitanzania wanainuka kiuchu-
mi .
Masele ameeleza kuwa suala la
kutekeleza na kusimamia masuala aliyo-
jifunza nchini Marekani linawezekana
kwa kuwa tayari ana uzoefu katika masu-
ala ya usimamizi na utekelezaji wa masu-
ala mbalimbali ikiwemo sera na sheria ya
madini na wakati huohuo akifanya kazi ya
kuhamasisha wawekezaji wa nje kuja ku-
wekeza nchini.
Nitatekeleza haya kwa faida ya wa-
nanchi, kwa sababu, Mimi si mzungumzaji
sana, lakini linapokuja suala la utekelezaji
wa masuala muhimu, nipo imara na sikati
tamaa, naweza kufanya maamuzi magu-
mu na hii ni asili yangu, ndivyo nilivyo.
Aliongeza Masele.
Akizungumzia faida za mafunzo hayo
Naibu Waziri ameeleza kuwa, mafunzo
hayo yamemuwezesha kuelewa zaidi
masuala mbalimbali yanayotokea katika
serikali na namna ya kutatua migogoro
mbalimbali na kwamba, mafunzo hayo
pia ni fursa muhimu ya kujifunza jinsi ya
kuwa kiongozi wa kimataifa.
Ujenzi wa bomba la
gesi kukamilika kwa
wakati Muhongo
Meli yenye mitambo ya kuzamisha na kuunganisha mabomba chini ya
bahari ikiwa katika bahari ya Hindi nchini Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) na Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano, Badra Masoud wakiwa katika lift maalum
iliyokuwa ikiwavusha toka kwenye boti na kuwapeleka katika meli yenye
mitambo ya kuunganisha na kuzamisha mabomba ya gesi katika iliyotia
nanga katika bahari ya Hindi kwa ajili kazi hiyo ambayo imekamilika.
3
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
MAONI
Na Malik Munisi,
Dar es Salaam,
B
omba la kusafirishia gesi asi-
lia kutoka Ubungo kwenda
mikocheni jijini Dar es Sa-
laam limeanza kufanya
kazi rasmi ikiwa ni mwaka mmoja
toka kukamilika kwake.
Mhandisi kutoka Shirika la
Maendeleo ya Petroli (TPDC) am-
baye ndiye msimamizi wa mradi
huo, Emmanuel Gilbert amesema
kuwa bomba hilo limechukua muda
mrefu kuanza kutumika kutokana
na makubaliano kati ya kampuni ya
Pan Africa Energy na TPDC juu
ya namna ya utekelezaji wa mradi
huo nje ya mkataba wa awali wa
mgawanyo wa mapato (Production
Sharing Agreement-PSA), kufikiwa
mwaka huu.
Alieleza kuwa kuanza kutumika
kwa bomba hilo kunatoa fursa kwa
viwanda na taasisi zilizo maeneo
ya mikocheni kuanza kutumia gesi
asilia katika uendeshaji wa shughuli
zao za uzalishaji. Vilevile, nyumba
70 za Shirika hilo zitapatiwa gesi
hiyo kwa matumizi ya nyumbani.
Bomba hilo lina uwezo wa
kusafirisha gesi kiasi cha futi za ujazo
milioni 7.5 kwa siku (7.5 mmscfd)
na hiki ni kiasi kikubwa ukilingani-
sha na mahitaji ya viwandani na
majumbani,aliongeza Gilbert.
Naye Afisa Masoko kutoka
TPDC, Ayoub Masenza alisema
kuwa, kuanza kutumika kwa bomba
hilo kunamaanisha kubadili mfumo
wa awali wa kutumia gesi iliyokan-
damizwa (Compressed Natural Gas-
CNG) iliyokuwa ikiwekwa kwenye
mitungi midogo kisha kusafirishwa
kwa wateja ikianzia katika kituo kili-
chopo Mikocheni na kusambazwa
katika viwanda vinne pamoja na ny-
umba takribani 57 za TPDC.
Mtaalamu huyo aliongeza,
kubadili kwa mfumo huo ku-
namaanisha kuwa, hivi sasa wateja
wana uhakika wa kupata gesi kila
wakati bila kuchelewa na pia jambo
hilo litapunguza gharama za kusa-
firisha gesi hiyo kwa kutumia magari
makubwa.
Mwanzo ilikua inatupasa kusa-
firisha gesi hii kwa kutumia magari
ambayo kimsingi ilikua inaongeza
gharama, lakini kwa kuanza kutu-
mika bomba hili hivi sasa gharama
za usambazaji zitapungua na pia
wateja watapata gesi kila wakati
kwa uhakika bila kuwa na masha-
ka ya kwamba gari limechelewa
kwenye foleni au mambo mengine
ambayo yangeweza kutokea baraba-
rani kipindi cha usafirishaji, alisema
Maseza.
Bomba limejengwa na Seri-
kali kupitia Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC), Mradi
ambao ulitekelezwa na mkandarasi
mzawa, kampuni ya BQ Contrac-
tors Ltd ambaye ndiye mkandarasi
mkuu.
Tahariri
MEM
Na Badra Masoud
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Hongera Mhe. Masele
umeonyesha njia!!
W
iki hii habari kubwa kwenye gazeti
letu ni kuchaguliwa kwa Naibu Wa-
ziri wa Nishati na Madini anayesima-
mia sekta ya Madini Mhe. Stephen
Masele kuchaguliwa rasmi kama kiongozi kijana
mwenye dira kuhutubia viongozi mbalimbali duni-
ani jijini Washington DC akiwamo Rais wa Mare-
kani Barack Obama.
Masele amepewa nafasi hiyo kupeperusha ben-
dera ya Vijana katika Kikao cha viongozi kilicho-
fanyika tarehe 28 Julai mwaka huu na anatarajiwa
kuwasilisha mada yenye kichwa cha habari Gov-
erning for the next Generation ambapo pia ame-
ombwa kuwasilisha mada hiyo hiyo kwa viongozi
wa nchi mbalimbali duniani utakaofanyika Agosti
6, mwaka huu.
Pamoja na kwamba aliyechaguliwa ni Masele
kupeperusha bendera hiyo kwa niaba ya viongozi
vijana hawana budi kujivunia suala kwani ameit-
angaza Tanzania na Watanzania wa rika zote bila
kujali itikadi.
Tunampongeza sana Naibu Waziri Masele kwa
hatua hiyo na tunamtakia kila la kheri katika kui-
peperusha bendera hiyo ya viongozi vijana na hata
Watanzania kwenye mkutano mwingine wa vion-
gozi wa nchi mbalimbali utakaofanyika hivi kar-
ibuni.
Vile vile Mhe. Masele ametoa changamoto kwa
vijana mbalimbali wa Kitanzania na duniani kwa
ujumla kwamba wasikate tamaa na hakuna lina-
loshindikana kama nia na jitihada zikiwepo.
Shime vijana tumuunge mkono Mhe. Masele na
tufuate nyayo zake za kujituma, kuwa na jitihada
na kutokata tamaa na mwisho kujiamini kwamba
kila kitu kinawezekana na kwamba kila mtu anao
uwezo.
Ni muhimu kwa kila taifa kutambua umuhimu
wa vijana kwamba wana nafasi kubwa katika kujen-
ga nchi hivyo washirikishwe katika kutoa maamuzi
na ikiwemo kupewa uongozi kama ilivyo kwa Mhe.
Masele.
Hongera sana Mhe. Masele Wizara ya Nishati
na Madini tunatambua mchango wako na tunaami-
ni hata Watanzania Wanatambua na kuthamini
mchango wako katika kulijenga taifa letu la Tanza-
nia.
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bomba la Gesi la Dar
laanza kutumika
Bomba hilo lina
uwezo wa kusafirisha
gesi kiasi cha futi za
ujazo milioni 7.5 kwa
siku (7.5 mmscfd) na
hiki ni kiasi kikubwa
ukilinganisha na ma-
hitaji ya viwandani na
majumbani,
4 Bulletin News
http://www.mem.go.tz

Yaliojiri wiki hii Pichani
http://www.mem.go.tz
Balozi wa DRC nchini Tanzania Mhe. Juma Alfani Mpango (wa kwanza kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utaalamu, Tathmini na Vyeti vya Madini ya Thamani
(CEEC-DRC), (wa tatu kutoka kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mvunilwa
Mwarabu, TMAA juu ya namna mashine ya AAS inavyofanya kazi za kupima madini ya aina
mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa pili kulia)
pamoja na Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa (wa kwanza kulia)
wakiwa katika maabara inayotumika kufundishia masomo kuhusu
utafutaji wa mafuta na gesi katika Chuo cha Teknolojia (SAIT) katika
Jimbo la Alberta nchini Canada.
Katibu Mkuu Nishati na Madini Eliakim Maswi akisisitiza
jambo wakati wa kikao na Makamishna wasaidizi wapya
walioteuliwa hivi karibuni.
Bibi Mesret Zemdukun kutoka Shirika la Kimataifa la UNEP
(katikati) akisisitiza jambo baada ya kikao cha maandalizi
ya Kongamano la Jotoardhi linalotarajiwa kufanyika nchini
mwezi Oktoba Jijini, Arusha. Kushoto kwake ni Dr. Peter
Omenda kutoka Shirika la Geothermal Development
Company. Wanaosikiliza wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu,
Eliakim Maswi, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu Mhandisi
Ngosi Mwihava, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia
masuala ya Jotoardhi, Edward Ishengoma na Meneja Mradi
wa Bioenergy, Paul Kiwele.
5
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Tuzo za madini

Yaliojiri wiki hii Pichani
Kutoka kushoto; Mameneja waTANESCO mkoa wa Tabora Mhandisi Monica
Kebara, Mkoa wa Mwanza Mhandisi Stella Hiza, Mkoa wa Morogoro Mhandisi
Macklean Mbonile na Mkoa wa Singida Mhandisi Deogratius Ndamugoba
wakifuatilia mjadala.
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Mhandisi Felchesmi
Mramba akieleza jambo katika kikao kati ya Watendaji wa
TANESCO, REA na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya
umeme vijijini.
Na Mwandishi wetu,
W
aziri wa Nishati na Madini, Profesa
Muhongo ametuma salamu kwa
wakandarasi wanaotekeleza miradi
ya umeme vijijini kuwa hivi karibu-
ni ataanza ukaguzi wa utekelezaji
wa miradi yote ya kupeleka umeme vijijini ili kujio-
nea mwenyewe maendeleo na kasi ya utekelezaji wa
miradi hiyo.
Waziri Muhongo alitoa ujumbe huo kwa njia ya
simu katika kikao kati ya Wakala wa Nishati Vijijini
(REA), Shirika la Umeme nchini (TANESCO)na
Wakandarasi 17 wanaotekeleza miradi ya kupeleka
umeme vijijini kilichofanyika jijini Arusha ili kujadili
maendeleo ya utekelezaji wa mpango kabambe wa
miradi ya kupeleka umeme vijijini na kutathmini
kasi ya wakandarasi hao.
Waziri Muhongo alieleza kuwa mkandarasi yey-
ote ambaye atakuwa nyuma ya muda wa utekelezaji
wa mradi na atakuwa hajapeleka vifaa vya ujenzi ka-
tika eneo la mradi, mkataba wake utasitishwa mara
moja.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa (REA)
Dk.Lutengano Mwakahesya alitoa angalizo kwa
wakandarasi kuepuka masuala ya rushwa wakati wa
utekelezaji wa miradi hiyo na kuhakikisha miradi
yote inakamilika kabla ya Juni 30, 2015 kama seri-
kali ilivyaoahidi kwa wananchi.
Akijibu baadhi ya hoja za wakandarasi hao
kuhusu kuongezeka kwa wigo wa kazi ambazo awali
hazikuwepo kwenye makubaliano ya mkataba, Dk.
Mwakahesya aliwataka wakandarasi hao kutoku-
jiongezea wigo huo wa kazi bila kuwasiliana na Ta-
nesco kwanza.
REA tunapokea mapendekezo ya mabadiliko
ya wigo wa kazi za nyongeza ambazo zipo nje ya
makubaliano ya mikataba yenu kutoka TANESCO
tu, msifanye kazi ambazo zipo nje ya mikataba tu-
liyotiliana saini hamtalipwa alisema Dkt. Mwaka-
hesya.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba alitoa an-
galizo kwa wakandarasi hao kuhakikisha wanafuata
maadili ya kazi kwa kutotumia vifaa vya TANESCO
wakati wa kujenga miradi yao au kutumia vifaa to-
fauti na makubaliano ya mkataba, akitolea mfano
udanganyifu wa kutumia transfoma ya kilovolti 50
wakati mkataba na michoro ikionesha transfoma ya
kilovolti 100.
Pamoja na kutilia mkazo kuwa TANESCO ita-
simamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo,
Mhandisi Mramba alisisitiza suala la ubora wa kazi
na vifaa na kwamba TANESCO itatoa ushirikiano
kwa wakandarasi hao ili kufanikisha kukamilika kwa
miradi hiyo.
Vilevile, Mkurugenzi wa Huduma za Kiufundi
(REA) Mhandisi Bengiel Msoffe alitoa angalizo
kwa wakandarasi hao kuwa makini wakati wote wa
utekelezaji wa miradi kwa kwenda sambamba na
utaratibu ulivyopangwa na kuhakikisha kwamba
wanatuma taarifa ya kila hatua wanayofikia katika
utekelezaji wa miradi hiyo.
Mhandisi Msoffe pia aliwaagiza wakandarasi hao
kuimarisha mawasiliano baina yao na wasimamizi
wa miradi hiyo ambao ni Mameneja wa TANESCO
kwenye mikoa inayotekeleza miradi hiyo.
Kikao hicho kiliandaliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) ambapo wawakilishi wawili kutoka
kila kampuni ya kandarasi walishiriki na kutoa taar-
ifa ya maendeleo ya miradi waliyopewa na kueleza
hatua waliyofikia ambapo kila mkandarasi alipotoa
taarifa ya mkoa anaofanyia kazi, Meneja msimamia
mradi ambaye ni Meneja wa TANESCO kwa mkoa
huo alisimama na kueleza kuridhika au kutoridhika
na kasi ya mkandarasi.
Wakandarasi walioshiriki ni kutoka kampuni
za Shandong Taikai Engineering Group, Angelique
International ltd, Sengerema Engineering Group,
Lucky Exports (Energy division) na Spencon Ser-
vices ltd.
Wengine ni Derm Electric (T) ltd, Namis Corpo-
rate, Chico, LTL Projects (Pvt) ltd, Nakuroi Invest-
ments Co, Urban & Rural Engineering Ltd, State
Grid Electrical JV na STED International Sevices.
Kampuni nyingine ambazo wakandarasi wake
walielekezwa kujiandaa kukutana na uongozi wa
REA jijini Dar es Salaam kwa mjadala zaidi ni OK
Electrical & Electronics Services ltd, MBH Power
ltd, Sinotec Co. ltd na CCC International Engineer-
ing Nigeria.
Miradi ya kupeleka umeme vijijini kwa mikoa
yote nchini imetengewa takribani bilioni 881 kutoka
kwenye bajeti ya serikali ya mwaka 2014/2015 am-
bayo ilipitishwa mwezi Julai mwaka huu mjini Do-
doma.
UPELEKAJI UMEME VIJIJINI:
Miradi ya kupeleka umeme vijijini
kwa mikoa yote nchini imetengewa
takribani bilioni 881 kutoka kwenye
bajeti ya serikali ya mwaka 2014/2015
ambayo ilipitishwa mwezi Julai mwaka
huu mjini Dodoma.
Prof. Muhongo kuanza kukagua wakandarasi
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dk.
Lutengano Mwakahesya akieleza jambo katika kikao kati ya
Wakala huo, Tanesco na wakandarasi wataotekeleza miradi ya
umeme vijijini.
6 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI
KITWANGA
Ni ziara ya mafanikio
Na Teresia Mhagama,
Canada
N
aibu Waziri wa Nishati
na Madini anayeshughu-
likia Nishati, Charles Kit-
wanga ameeleza kuwa,
ziara aliyoifanya nchini
Canada hivi karibuni katika tasnia
ya uziduaji imekuwa ya mafanikio
kwa nchi.
Naibu Waziri alieleza hayo
wakati akitoa taarifa fupi ya ziara
hiyo kwa Balozi wa Tanzania nchini
Canada, Alex Massinda katika Ofisi
za Ubalozi huo zilizopo Ottawa
nchini Canada.
Alieleza kuwa, pamoja na
ujumbe alioambatana nao kujifunza
masuala mbalimbali katika Taasisi
na Kampuni zinazojishughulisha
na sekta za Nishati na Madini, na
kuimarisha ushirikiano kati ya Tan-
zania na Canada, lakini pia ziara
hiyo imeendelea kufungua fursa kwa
watanzania kupata elimu nchini
Canada na nchi ya Canada kufaha-
mu zaidi fursa za uwekezaji zilizopo
Tanzania.
Tukiwa katika jimbo la Alberta
tulitembelea Chuo cha teknolojia cha
jimbo hilo (SAIT) ambacho kime-
bobea katika kutoa wataalam wa
kada ya kati katika masuala ya gesi,
mafuta na madini na tunaendelea
kufanya nao mazungumzo ili chuo
hicho kiweze kushirikiana na Chuo
cha Madini Dodoma katika masu-
ala ya kuandaa mitaala na kuandaa
wataalam watakaotumika katika
shughuli za utafutaji na uchimbaji
wa mafuta na gesi na madini nchini
na watendaji wa Chuo hicho wame-
onesha utayari wa kushirikiana na
Chuo chetu, alisema Kitwanga.
Alieleza kuwa Ujumbe huo wa
Tanzania pia, ulipotembelea chuo
cha Bow Valley katika jimbo la
Alberta, ambapo Rais na Mtend-
aji Mkuu wa Chuo Sharon Carry
alieleza kuwa, chuo hicho kimebo-
bea katika kutoa mafunzo mbalim-
bali yakiwemo ya kubuni na kuende-
leza biashara ndogo ndogo (Business
Incubation), hivyo Naibu Waziri al-
ionesha nia ya kufanya ushirikiano
na chuo hicho, ili kutoa elimu kwa
wachimbaji wadogo itakayowawez-
esha kufanya uchimbaji wenye tija
na kuwapa uwezo wa kusimamia
na kuandaa maombi ya biashara ya-
takayowezesha kupata mikopo kwe-
nye taasisi za kifedha. Rais wa Chuo
cha Bow Valley alisema kuwa yuko
tayari kushirikiana na Tanzania ka-
tika suala hilo la elimu.
Vilevile tulipata fursa ya
kutembelea Mamlaka ya Udhibiti
Nishati ya Jimbo la Alberta (AER)
ambayo ilianzishwa miaka 75 iliyo-
pita ambayo licha ya kudhibiti nisha-
ti lakini pia ina jukumu la kudhibiti
masuala ya uhifadhi wa mazingira
ili kuhakikisha shughuli za uende-
lezaji wa nishati zinafuata sheria za
utunzaji mazingira,alisema Naibu
Waziri.
Aliongeza kuwa, kutokana na
taasisi hiyo kupiga hatua kwenye
shughuli za udhibiti watendaji wake
walieleza kuwa, wapo tayari kutoa
elimu hiyo kwa wataalam kutoka
Tanzania ili Mamlaka ya Udhibiti
Nishati na Maji (EWURA), na
taasisi nyingine kama Wakala wa
Ukaguzi wa Madini (TMAA),
Mamlaka ya Mapato (TRA) n.k
waende kuongeza uelewa kwenye
taasisi hiyo ili kujenga uwezo katika
shughuli za udhibiti na pia kuweza
kutengeneza kanuni bora zinazoon-
goza shughuli za udhibiti. Alisema
Naibu Waziri.
Kuhusu ziara ya ujumbe huo
katika kiwanda cha Methanex kina-
chotengeneza malighafi ya methano,
Naibu Waziri alieleza kuwa, kiwan-
da hicho pia kinatengeneza bidhaa
kama vile ambayo Dimethyl-Ether
(DME) ambayo inaweza kutumika
kwa matumizi mbalimbali ikiwemo
kuwekwa kwenye mitungi ya gesi
kwa ajili ya kupikia, hivyo alieleza
kuwa mbali na bomba kutumika
kupeleka gesi kwa wananchi lakini
pia kutokana na uwepo wa gesi asi-
lia nchini, Tanzania inaweza kuwa
na kiwanda cha methano ambacho
kitakuwa na teknolojia ya kuzalisha
DME ili gesi iwafikie wananchi wen-
gi zaidi kwa njia ya mitungi.
Tukiwa katika kampuni ya Ca-
nadian Solar inayotengeneza na ku-
jenga miradi ya umeme jua, katika
sehemu mbalimbali duniani, uongo-
zi wa kampuni hiyo kubwa ulikuwa
tayari kuja kushirikiana na serikali ya
Tanzania kupitia Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) ili kujenga miradi ya
umeme jua kwa kuwa kampuni hiyo
inaweza kujenga miradi midogo ya
megawati tatu hadi kumi, pia miradi
mikubwa ya kuzalisha megawati 200
hadi 300,alieleza Kitwanga.
Aidha, kutokana na ujumbe
wa Tanzania kuwaeleza watendaji
hao kuwa ipo baadhi ya miradi in-
ayosuasua mfano wa megawati 150
mkoani Shinyanga na ule wa mega-
wati 50 mkoani Kigoma, Watendaji
hao waliahidi kutuma wataalam
baada ya wiki mbili ili kuja nchini
kufanya upembuzi yakinifu ili kuo-
na uwezekano wa kutekeleza miradi
hiyo.
Kuhusu miradi midogo midogo
ya umeme jua, alieleza kuwa, Seri-
kali ya Tanzania itafanya mazun-
gumzo na serikali ya Canada kupitia
Shirika lake la Maendeleo (CIDA)
kuona uwezekano wa kufadhili mi-
radi hiyo.
Naye Balozi wa Tanzania nchini
Canada, Alex Massinda alimweleza
Naibu Waziri Kitwanga kuwa,
iwapo kuna miradi ambayo serikali
ya Tanzania inahitaji ufadhili kupi-
tia CIDA ni vyema ikaandaliwa
mapema kabla ya mwezi Septemba,
kipindi ambacho CIDA huwasilisha
taarifa ya miradi inayotarajiwa ku-
fanyika sehemu mbalimbali duni-
ani katika Wizara ya Maendeleo ya
Canada.
Balozi Massinda pia alieleza
kuwa, pamoja na miradi ya ubia
kuendelea kufanyika kati ya serikali
ya Tanzania na nchi nyingine lakini
miradi inayohusisha ushirikiano wa
serikali na sekta binafsi ni muhimu
na iendelee kupewa kipaumbele
kwani sekta binafsi zina nafasi kub-
wa katika kuinua uchumi wa nchi.
Mbali na Naibu Waziri Kit-
wanga, Ujumbe wa Tanzania nchini
Canada ulijumuisha Naibu Waziri
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-TAM-
ISEMI, Kassim Majaliwa, Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-
Mazingira, Ummy Mwalimu, na
baadhi ya wabunge kutoka Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati
na Madini wakiongozwa na Mwe-
nyekiti wa Kamati, Victor Mwam-
balaswa, Watalam kutoka Wizara
ya Nishati na Madini na Mbunge wa
Ngara, Deogratias Ntukamazina.
Ziarani Canada
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa nne kushoto), ukiwa
katika kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme jua cha Canadian Solar katika jimbo la Ontario nchini Canada.Wengine
katika picha ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Canadian Solar, Brian Lu (wa tano kushoto), Mwenyekiti Kamati ya Bunge,
Nishati na Madini, Mhe.Victor Mwambalaswa(Mb.) (wa tatu kushoto), Mhe.Shafin Sumar (Mb.), (wa pili kulia), Mhe.
Richard Ndasa (Mb.) (wa tatu kulia), Mhe.Murtaza Mangungu (Mb.) (wa nne kulia), Bw.Ronald Drews, Mratibu wa Masuala
ya Biashara kwa Tanzania (wa tano kulia), Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Canada (wa kwanza kushoto) pamoja na
wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Canadian Solar.
nKitwanga aelezea ziara yake nchini Canada
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akiwa amekaa katika mfano
wa mashine inayotumika katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na
gesi (haionekani pichani), wakati Ujumbe kutoka Tanzania, ukijumuisha baadhi
ya Wabunge na Naibu Mawaziri walipotembelea Chuo cha Teknolojia cha Jimbo
la Alberta nchini Canada (SAIT). Wengine katika picha ni Wabunge, Richard Ndasa
(Sumve) (wa kwanza kulia), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) (wa pili kushoto)
na Mjiolojia Ngereja Mgejwa kyutoka Wizara ya Nishati na Madini.
7
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
Simamieni vyema ukusanyaji wa maduhuli
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam
M
akamishna wasaidizi wali-
oteuliwa kusimamia ofisi
mpya za kanda za Wiz-
ara ya Nishati na Madini
katika baadhi ya mikoa
zilizoanzishwa hivi karibuni wametakiwa kusi-
mamia vyema ukusanyaji wa maduhuli pamo-
ja na kusimamia kanuni na sheria za madini.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi
alipokutana nao ofisini kwake kabla ya kuele-
kea katika vituo vyao vya kazi.
Maswi alisema kuwa, sekta ya madini ime-
kuwa na changamoto nyingi katika ukusanyaji
wa maduhuli kwani wapo wamiliki wa leseni
wasio waaminifu wanaokwepa kulipa kodi za
mrabaha na mapato na kuwataka kuwa wasi-
mamizi wazuri ili kuhakikisha kuwa seta ya
madini inachangia kwa kiasi kikubwa katika
ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ninawaagiza kusimamia kwa uadilifu
ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha kuwa
kila mmiliki wa leseni analipa kodi anayosta-
hili huku akifuata kanuni na sheria za madini,
pia hakikisheni mnashughulikia migogoro ita-
kayojitokeza kwa kufuata kanuni na sheria za
madini alisema Bw. Maswi.
Aliongeza kuwa, wawakilishi kutoka
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini
(TMAA) waliopo kwenye migodi wapo kwa
ajili ya kuwawezesha katika kusimamia kodi
itokanayo na uchimbaji wa madini, na kusisiti-
za kuwa ni jukumu la kufuatilia kwa kuhakiki-
sha fedha zinalipwa kwa wakati ni la makam-
ishna wasaidizi.
Vile vile alieleza kuwa, kumekuwepo na
migogoro mingi kwenye umiliki wa leseni za
utafutaji na uchimbaji wa madini na kuwataka
makamishna wasaidizi hao kuhakikisha wa-
nakuwa suluhisho la migogoro hiyo badala ya
kuwa chanzo cha migogoro hiyo.
Aidha, aliwataka makamishna hao kusi-
mamia mikopo na ruzuku inayotolewa kwa
ajili ya wachimbaji wadogo kwa kuhakikisha
kuwa wanapata fedha zao kwa wakati na ku-
wainua kwani wana mchango mkubwa kupitia
sekta ya madini.
Mbali na kuwataka kuwa waadilifu
katika ukusanyaji wa maduhuli na utatuzi
wa migogoro ya madini, Maswi aliwataka
makamishna wasaidizi hao kufanya kazi kwa
kujituma na kudhihirisha kuwa walistahili ku-
pewa nafasi hizo na kuongeza kuwa, atakayes-
hindwa kusimamia nafasi yake hatasita kum-
wondoa na kuweka mtu anayeweza kusimamia
vyema nafasi yake kwa ubunifu zaidi.
Aliwataka kusimamia na kutoa ushirikiano
kwa wafanyakazi walio chini yao katika ofisi
zao mpya na kukwepa makundi na upendeleo.
Lengo la kuwateua ninyi na kuwapeleka
katika ofisi mpya zilizofunguliwa ni moja ya
mikakati ya Wizara katika kusogeza huduma
kwa wananchi na dhamana mliyopewa ni
kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata
huduma zilizo bora na kuepusha malalamiko.
Alisema Maswi.
Alisema kuwa mbali na kuteua makam-
ishna wasaidizi wapya katika ofisi mpya na
kufanya uhamisho, Wizara ina mpango ya
kuwaongezea watumishi wengine kama wa-
hasibu, madereva na wataalam wengine na
kuongeza kuwa pia Wizara ina mpango wa
kuwapatia kompyuta zilizounganishwa na
mfumo maalumu (Mining cadastre services)
kwa ajili ya kushughulikia maombi ya leseni
kwa urahisi zaidi.
Naye Kamishna wa Madini Mhandisi
Paul Masanja alisema kuwa uteuzi uliofanywa
wa makamishna wasaidizi pamoja na kufun-
gua ofisi mpya utaiwezesha sekta ya madini
kukua kwa kasi zaidi na kuchangia zaidi katika
ukuaji wa uchumi.
Tanzania
kushirikiana
na DRC
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Wizara ya Nishati na Madini kupitia Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), imepanga
kuimarisha shughuli za kufuatilia, kuzuia utoroshaji
madini, na ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kush-
irikiana na taasisi za nchi za nje ikiwemo Jamhuri ya
Kidememokrasia ya Kongo (DRC).
Hayo yalibainishwa na Mhandisi Dominic
Rwekaza, Kaimu Mtendaji Mkuu, TMAA wakati wa
mazungumzo kati yake na Ujumbe kutoka Kituo cha
Utaalamu, Tathmini na Vyeti ya Madini ya Thama-
ni (CEEC) cha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
(DRC) ulioongozwa na Mhe. Juma Alfani Mpango,
Balozi wa DRC nchini uliofika katika makao makuu
ya Wakala huo jijini Dar es Salaam.
Ili kutekeleza hilo, Mhandisi Rwekaza aliahidi
kumtumia Mkurugenzi Mtendaji wa CEEC mfano
wa vyeti halisi vinavyotumiwa hapa nchini kusa-
firishia madini nje ya nchi pamoja na majina ya wara-
tibu focal persons wanaohusika na shughuli za utoaji
na usimamizi wa vibali vya kusafirisha madini nje ya
nchi ili kuweza kuwabana wafanyabiashara wanaosa-
firisha madini bila kibali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CEEC, Pascal
Muyumba, alimkabidhi Kaimu Mtendaji Mkuu wa
TMAA, Mhandisi Dominic Rwekaza mfano wa
hati halisi zinazotolewa nchini DRC katika kusafiri-
sha madini nje ya nchi hiyo ili ziweze kusaidia katika
utambuzi wa uhalisia wa vibali vitakavyowasilishwa
na watu wanaosafirisha madini kupitia nchini Tanza-
nia .
Pia, Muyumba alimkabidhi Mhandisi Rwekaza
majina na namba za mawasiliano za waratibu fo-
cal persons wa DRC wanaohusika na usimamizi na
udhibiti wa biashara ya madini nchini DRC ili zitu-
mike kwa ajili ya kuwasiliana pale inapotokea mata-
tizo yoyote kuhusu madini yanayosafirishwa kupitia
nchini Tanzania.
NI UDHIBITI BIASHARA
HARAMU NA UTOROSHAJI
MADINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utaalamu, Tathmini na
Vyeti vya Madini ya Thamani (CEEC) cha DRC, Bw. Pascal
Muyumba ( mwenye suti ya bluu) akimkabidhi Kaimu
Mtendaji Mkuu wa TMAA Eng.Dominic Rwekaza (wa pili
kushoto), mfano wa hati halisi za kusafirishia madini kutoka
DRC .
Katibu Mkuu Nishati na Madini Eliakim Maswi ( katikati mwenye suti nyeusi) akizungumza na
makamishna wasaidizi wapya walioteuliwa .
Vijiji Ruvuma kuneemeka na Umeme
Na Nuru Mwasampeta,
Ruvuma
Vijiji 409 mkoani Ruvuma kuungan-
ishiwa huduma ya umeme ifikapo
mwezi Juni mwaka 2014, idadi hii
inajumuisha vijiji 306 vilivyo chini ya
mradi wa usambazaji umeme vijijini
unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) mkoani humo huku vijiji
103 vikiunganishiwa umeme kutoka
gridi ya Taifa.
Hayo yalisemwa na Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo mbele ya Rais wa Jam-
huri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ali-
kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi
wa miradi ya umeme inayofadhiliwa
na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
katika mkoa wa Ruvuma.
Profesa Muhongo alisema kuwa
mradi huo wa usambazaji umeme
vijijini katika mkoa wa Ruvuma uta-
gharimu kiasi cha shilingi 26.53 bil-
ioni zitakazohusisha ujenzi wa njia
za umeme za msongo wa kilovolti 33
zenye jumla ya urefu wa kilometa 538,
msongo wa kilovolti 11 yenye urefu wa
kilomita 23, msongo wa kilovolti 0.4
yenye urefu wa kilomita 272, ufungaji
wa transfoma 129 za ukubwa mbal-
imbali pamoja na kuunganisha wateja
7,488.
Alieleza kuwa mradi huo
utatekelezwa na kampuni ya Lanka Transfo-
mers Limited, (LTL) ya nchini Srilanka kwa
mkoa wa Ruvuma na kusisitiza kuwa mradi
huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2015
na kunufaisha wakazi wa wilaya za Songea,
Tunduru, Mbinga na Nyasa.
Pamoja na uwepo wa mradi huu, pia
kuna mradi wa kuongeza nguvu ya umeme
kwenye wilaya za Mbinga na Tunduru un-
aotekelezwa na kampuni ya Taikai Co.Ltd
ambapo tayari kampuni hiyo imekamilisha
tathmini ya vituo vyote na kuleta transfoma
katika kituo cha Tunduru Alisisitiza Profesa
Muhongo.
Alieleza kuwa kiasi cha fedha za kitanza-
nia shilingi bilioni 2.27 zitakazohusisha ujenzi
wa vituo viwili vya kuongeza nguvu ya umeme
kutoka kilovolti 11 hadi kufikia kilovolti 33 kwa
ajili ya kufikisha umeme katika vijiji vilivyoko
mbali. Zimetengwa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mbababay
Kapteni John Komba aliishukuru Serikali kwa
kuboresha miundombinu ya kuweka umeme
katika jimbo lake na kupandishwa hadhi kituo
cha afya cha Mbambabay na kuwa hospitali ya
wilaya.
Miradi ya REA awamu ya II ilianza
kutekelezwa rasmi Novemba 2013 na ina-
takiwa kukamilika ifikapo Juni 2015 kwa nchi
nzima.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin (katikati) akisoma maandishi kwenye jiwe
la msingi lililozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete kwenye mradi wa kusambaza umeme vijijini
unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) wilaya ya Nyasa hivi kiaribuni.
8 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
HABARI
TANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA
LAZIMA WATANZANIA TUJIAMINI NA TUAMINIWE NA WENGINE. TANZANIA
IMEINGIA KWENYE UCHUMI WA GESI ASILIA. LAZIMA TUFANYE MAPINDUZI
MAKUBWA YA UCHUMI KWA AJILI YA KUFUTA UMASKINI MIONGONI MWA
WATANZANIA. UCHUMI IMARA UTATOA AJIRA MPYA, AMANI NA USALAMA WA
KUDUMU NA MATUMAINI MAPYA. TUACHANE NA UBINAFSI
HAKUNA KUKATA TAMAA, HAKUNA KUSHINDWA.

UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
YASHAURIWA KUIWEZESHA TANESCO NGUZO ZA ZEGE
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
N
aibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwan-
ga ameitaka Kampuni ya EURO POLES GmbH & Co. KG inayojishughuli-
sha na kutengeneza nguzo za umeme za zege kuileta teknolojia hiyo nchini
ili iweze kuwasaidia watanzania kupata uzoefu wa namna ya kutengeneza
nguzo hizo, jambo ambalo litasaidia pia kupanua wigo wa ajira.
Kitwanga aliyasema hayo wakati alipokutana na kampuni hiyo ambayo imeonesha
nia ya kuingia ubia na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa ajili ya kuten-
geneza nguzo za umeme za zege, ambapo uwakilishi wake uliongozwa na Balozi wa
Ujerumani nchini, Egon Kochanke.
Aliongeza kuwa, Tanzania inahitaji kuhamia katika aina mpya ya utumiaji wa
nguzo za umeme za zege kutokana na kwamba, aina ya nguzo zinazotumika hivi sasa
hazidumu kwa muda mrefu na hasa katika kipindi cha mvua, nguzo hizo zimepelekea
kuwepo na kasoro mbalimbali.
Tumeanza kutumia aina ya nguzo hizi, katika baadhi ya maeneo kama Tanga na
Pangani, lakini lengo letu ni kutumia nguzo hizi katika maeneo mengi zaidi ya nchi yetu,
aliongeza Kitwanga.
Aidha, alieleza kuwa, dhamira ya serikali ya kuhakikisha watanzania wote wanapata
huduma hiyo ya umeme bado ipo pale pale na hivyo, kuitaka kampuni hiyo na TANE-
SCO kuona namna ambayo itafanya kuhakikisha kwamba, teknolojia hiyo inasambaa
katika maeneo mengi nchini.
Hadi sasa ni asililimia 36 tu ya watanzania ambao wameunganishwa na huduma ya
umeme. Bado tunataka asilimia iliyobaki ya watanzania nao wapate umeme, alisisitiza
Kitwanga.
Wakati huo huo, Naibu Waziri alikutana na kampuni Woodside ya Australia, in-
ayojishughulisha na utafutaji mafuta katika ziwa Tanganyika ambapo wawakilishi wa
kampuni hiyo walimweleza, Naibu Waziri Kitwanga uzoefu na utayari wao wa kufanya
kazi katika sekta ya gesi iliyosindikwa, Liqufied Natural Gas. (LNG).
Aidha, kampuni hiyo pia ilimweleza Naibu Waziri kuhusu uwezo wa kampuni hiyo
katika masuala ya teknolojia na namna inavyozingatia suala la uhifadhi wa mazingira
wakati wa kufanya shughuli za utafutaji mafuta na gesi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga, (kulia)
akiongea jambo na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke (kushoto) ofisini kwake
mara baada ya kikao ambapo kampuni ya EURO POLES GmbH & Co. KG imeonyesha nia ya
kushirikiana na Tanesco kujenga nguzo za umeme za zege. Wengine katika picha ni ujumbe
uliofuatana na balozi huyo na Katibu wa Waziri Ngereja Mgejwa (Katikati).
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Woodside ya Australia inayofanya shughuli za
utafutaji Mafuta katika Ziwa Tanganyika, Philip Loader akimweleza jambo Naibu Waziri
Nishati,Charles Kitwanga katika kikao baina ya Wizara na Kampuni hiyo, ambapo
wawakilishi wa Kampuni hiyo walimweleza Mhe. Kitwanga uzoefu wa kampuni hiyo
katika masuala ya Utafiti wa Mafuta na gesi iliyosindikwa Liquefied natural gas (LNG).
Kushoto ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Kamishna Msaidizi, Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
Petroli Mhandisi Stanley Marisa (katikati) akibadilishana mawazo na wawakilishi
wa Kampuni Woodside ya Australia inayofanya kazi ya utafutaji Mafuta katika Ziwa
Tanganyika mara baada ya kikao. Wa kwanza kulia ni Makamu wa Rais wa kampuni
hiyo, Philip Loader, wengine, wa kwanza kushoto ni Makamu wa Rais Mwandamizi
masuala ya teknolojia Saun Gregory, wa pili kushoto ni Afisa Mwandamizi masula ya
mahusiano na ushauri wa utafiti Tim Walster.
9
Bulletin News
http://www.mem.go.tz

You might also like