You are on page 1of 2

National Team Main Sponsor

Release No. 133


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 2, 2014

+258842137852
Maputo

NOOIJ ATARAJIA MECHI YA WAZI DHIDI YA MSUMBIJI
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema anakiamini kikosi chake ambacho
kesho (Agosti 3 mwaka huu) kinacheza mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya
michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas).

Mechi hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji
itakayoingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi
za Fainali itakayofanyika mwakani nchini Morocco.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita
timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye
kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.

Akizungumza hapa Maputo, Nooij amesema anaamini kikosi chake kitacheza
vizuri zaidi kuliko kilivyofanya jijini Dar es Salaam kwa vile hakitakuwa katika
shinikizo la washabiki ambalo mara nyingi hufanya wachezaji wasijiamini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia katika hoteli
ya Pestana Rovuma ikitokea Johannesburg, Afrika Kusini ambapo ilifanya
maandalizi yake mwisho, na itafanya mazoezi leo (Agosti 2 mwaka huu) saa 9
alasiri Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi ya
kesho.

Kikosi hicho cha timu ya Taifa leo imeandaliwa chakula cha jioni na Balozi wa
Tanzania hapa Msumbiji, Shamim Nyanduga.

Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu nao wameungana na timu leo
asubuhi hapa Maputo wakitokea Lubumbashi katika klabu yao ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Tanzania Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA

3
rd
Floor, PPF Tower, Garden Avenue / Ohio Street
P.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania . Telefax: + 255-22-2861815
E-mail: tanfootball@tff.or.tz . Website: www.tff.or.tz


National Team Main Sponsor



Mechi itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda wakiongozwa na Dennis
Batte itaanza saa 9 alasiri kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa
saa 10 jioni.

Wachezaji waliopo katika kiosi cha Taifa Stars hapa Maputo ni Aggrey Morris,
Aishi Manula, Amri Kiemba, Deogratias Munishi, Erasto Nyoni, Haruna Chanongo,
Himid Mao, John Bocco, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mbwana Samata, Mwinyi
Kazimoto, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Ramadhan Singano, Said
Moradi, Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MAPUTO
+258842137852

You might also like