Welcome to Scribd. Sign in or start your free trial to enjoy unlimited e-books, audiobooks & documents.Find out more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
1Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
PRESSS 04AUGOST 2014

PRESSS 04AUGOST 2014

Ratings:
(0)
|Views: 15,422|Likes:
Published by Othman Michuzi

More info:

Published by: Othman Michuzi on Aug 04, 2014
Copyright:Traditional Copyright: All rights reserved

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as DOCX, PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

08/10/2014

pdf

text

original

 
1
 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  WIZARA YA MAMBO YA NDANI  JESHI LA POLISI TANZANIA PRESS RELEASE 04/08/2014
ASKARI POLISI FEKI WA USALAMA BARABARANI ALIYEKUWA ANATAPELI  WANANCHI AKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM
 Jeshi la Polisi
 
Kanda ya Dar es Salaam linamshikilia na kumhoji mtu mmoja aitwaye ROBSON S/O SEIF MWAKYUSA EMMANUEL, miaka 30, Mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya afisa wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani akiendelea na kazi za ukaguzi wa makosa ya usalama barabarani. Mtuhumiwa huyu alikamatwa tarehe 02/08/2014 huko Kata ya Chamazi, Mbagala Majimatitu Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwa amevalia sare za Polisi na cheo cha Stesheni Sajenti. Baada ya kukamatwa alikutwa na gari namba T723 BAK T/Cresta rangi nyeupe analilotumia kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji kutapeli watu akiwadanganya yeye ni askari polisi. Gari hilo lilipopekuliwa lilikutwa na
 
Radio Call 1yenye namba GP380 aina ya Motorola
 
Leseni za udereva zipatazo 40 za watu mbalimbali
 
Stakabadhi 02 za Serikali zenye nambari A0531562 na A1672464
 
Police Loss Report mbalimbali.
 
Nakala 03 za Notification zilizojazwa.
 
Kofia moja ya (Uhuru Cape) ya Usalama barabarani,
 
Beji 01 yenye jina la E.R. MWAKYUSA ya kuweka kifuani.
 
Ratiba ya mabasi yaendayo Mikoani ya SUMATRA Pia mtuhumiwa alipekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vitu vifuatavyo:
 
Pea 04 za sare ya Polisi ya KAKI.
 
Pea 03 za sare ya Polisi ya Usalama Barabarani
 
Koti 01 ya mvua ya Usalama Barabarani
 
Reflector 08 za Usalama Barabarani
 
Kofia 01 (Uhuru Cape) ya Usalama Barabarani
 
2
 
Kofia 02 (Barret) nyeusi za Polisi
 
Mikanda 02 ya Bendera mali ya Jeshi la Polisi
 
Mikanda 02 ya Polisi (Tunic Cross Belt) mweusi.
 
Mikanda 02 ya Filimbi.
 
Cheo 01 cha Sajenti
 
Vyeo 03 vya Stesheni Sajenti.
 
Vifungi 08 vya chuma mali ya Jeshi la Polisi.
 
Cheo 01 cha Stesheni Sajenti cha JWTZ
 
Notification Form zilizojazwa zipatazo 62.
 
PF3 Forms zipatazo 04
 
Notification Forms ambazo hazijajazwa zipatazo 08 Mtuhumiwa huyu aliwahi kuwa askari polisi aliyejiunga na Jeshi hilo Mwaka 2000 akiwa mwenye namba F2460 lakini alifukuzwa kazi kwa fedheha mnamo tarehe 21/03/2014 huko Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha Stesheni Sajenti. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akijitambulisha kuwa ni askari hivyo kufanikiwa kuwatapeli wananchi mbalimbali na kujipatia kiasi kikubwa fedha kwa njia za udanganyifu. Wananchi waliotapeliwa wanatakiwa kuja kutambua leseni zao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake
KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WAWILI, BASTOLA MBILI NA RISASI 14
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
linawashikilia majambazi wawili kwa kutuhuma za kujihusisha na unyang’anyi wa
kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani. Watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 30/07/2014 huko Makumbusho Kijitonyama, kufuatia msako makali unaoendelea wa kuwasaka kisha kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha na makosa mengine. Walipopekuliwa nyumbani kwao walikamatwa na Bastola mbili moja ni GROCK17 yenye namba B019259 iliyotengenezwa nchi ya Jamhuri ya CZECH ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine. Nyingine ni Bastola aina ya CHINESE iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi moja ndani ya magazine. Watuhumiwa waliokamatwa ni hawa wafuato:
 
FREDY S/O STEVEN, Miaka 25, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kiwalani.
 
IRENE D/O NYANGE, Miaka 36, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kijitonyama, uchunguzi unakamilishwa na watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa
 
3
MLEMAVU ATUMIA MGUU WAKE BANDIA KUFANYA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA
 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mlamavu aitwaye SAID S/O TINDWA, MIAKA 36, MKAZI WA VIJIBWENI Wilaya ya Temeke kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya, taarifa za kiintelijensia zilizopatikana kupitia kwa raia wema ziliwafikia makachero wa Polisi kuwa mlemavu huyo ambaye mguu wake wa kulia ni wa bandia amekuwa akiutumia vibaya mguu huo kwa kuficha dawa za kulevya ambazo aliwauzia watumiaji. Aidha kila kete alikuwa akiuza kwa shilingi Tsh.1000. Ilikuwa mnamo tarehe 01/08/2014 katika mtego maalumu uliowekwa na askari wa upelelezi ndipo mlemavu huyo alikamatwa akiuza dawa hizo kwa wateja wake baada ya kuzitoa alikozificha ambapo ni ndani ya mguu huo wa bandia. Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu hiyo kwa muda mrefu kabla ya kukamatwa. Aina ya dawa alizokuwa akiuza ni zile za viwandani kama vile Cocein , Heroin na wakati mwingine bhangi. Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na jalada la kesi yake litapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili sheria iweze kuchukua mkondo wake. Aidha natoa onyo kwa watu wenye ulemavu kwamba wasitumie kigezo cha ulemavu kufanya uhalifu kwa makusudi kwani wanawaharibia walemavu wengine ambao ni raia wema na ambao mara nyingi huonewa huruma na kutotiliwa mashaka.
 WANAWAKE WATATU WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA MTANDAO HARAMU NA NYARA ZA SERIKALI
 Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM linawashikilia wanawake watatu kwa kosa la kujihusisha na mtandao haramu wa nyara za Serikali. Mnamo tarehe 23/07/2014 huko eneo la Mbagala Mission Polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa eneo hilo lina watu wanajihusisha na biashara ya nyara za serikali. Polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata WEMAEL D/O MSHANA na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vipande sita vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola za Kimarekani 30,000 (Dolla elfu thelathini) sawa na shilingi za kitanzania 49,750,000/= (milioni arobaini na tisa mia saba hamsini elfu) ambao ni sawa na tembo wawili waliouawa. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtuhumiwa anashirikiana na watuhumiwa wengine ambao ni UPENDO D/O MSHANA, Miaka 33, na STELLA D/O DANIEL, Miaka 17, Mwanafunzi wa Chuo cha Genessis cha Mtoni kwa Azizi Ali ambao nao wamekamatwa. Uchunguzi zaidi unafanyika kwa kushirikiana na Idara ya wanyama pori ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->