You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA.


RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260,
Fax - +255252503734 MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE TAREHE 27.08.2014.




Mtu Mmoja Mkazi Wa Kijiji Cha Ibungu Ameuawa Na Watu Wasiojulikana Na Mwili
Wake Kutupwa Katika Mto.

Mtu Mmoja Auawa Kwa Kwa Kupigwa Na Kundi La Wananchi Kwa Tuhuma Za Wizi.

Mtoto Wa Miaka 09 Afariki Dunia Katika Ajali Ya Barabarani Wilaya Ya Mbozi


Katika Tukio La Kwanza:

Mtu Mmoja Mkazi Wa Kijiji Cha Ibungu Aliyefahamika Kwa Jina La Daud Paston (22)
Aliuawa Kwa Kukatwa Na Vitu Vyenye Ncha Kali Sehemu Mbalimbali Za Mwili Wake Na
Mtu/Watu Wasiofahamika Na Kisha Mwili Wake Kutupwa Katika Mto Lumbe.

Mwili Wa Marehemu Ulikutwa Na Kutolewa Katika Mto Lumbe Uliopo Katika Kijiji Na
Kata Ya Ikuti, Tarafa Ya Ukukwe, Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya Mnamo Tarehe
26.08.2014 Na Ulikutwa Na Majeraha Sehemu Mbalimbali Ya Kuchomwa/Kukatwa Na Kitu
Chenye Ncha Kali.

Chanzo Cha Mauaji Hayo Bado Hakijafahamika Japo Taarifa Za Awali Zinadai Kuwa
Marehemu Alikuwa Na Tabia Ya Wizi Na Ubakaji. Hakuna Mtu/Watu Waliokamatwa Kuhusiana
Na Tukio Hilo Na Jitihada Za Kuwatafuta Waliohusika Zinaendelea.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi
Ahmed Z. Msangi Anatoa Wito Kwa Yeyote Mwenye Taarifa Za Mtu/Watu Waliohusika Katika
Tukio Hili Azitoe Katika Mamlaka Husika Ili Wakamatwe Na Hatua Za Kisheria Zichukuliwe
Dhidi Yao.


Katika Tukio La Pili:

Mtu Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina La Frank Mwakilalo (25) Mkazi Wa Block T
Alifariki Dunia Akiwa Anapatiwa Matibabu Katika Hospitali Ya Rufaa Mbeya Baada Ya Kupigwa
Na Kundi La Wananchi Walioamua Kujichukulia Sheria Mkononi Kwa Tuhuma Za Kuiba Simu.

Tukio Hilo Limetokea Mnamo Tarehe 26.08.2014 Majira Ya Saa 20:15 Usiku Huko
Katika Maeneo Ya Block T, Jiji Na Mkoa Wa Mbeya. Inadaiwa Kuwa Marehemu Alikamatwa Na
Kuanza Kupigwa Na Wananchi Hao Na Badae Alipelekwa Na Kufungiwa Katika Ofisi Za
Mtendaji Ambapo Alitoroka Na Ndipo Wananchi Hao Walimuona Na Kumkimbiza Na Kuanza
Kumpiga Hali Iliyopelekea Kumvunja Mkono Wake Wa Kushoto Na Kumsababishia Maumivu
Makali Mwilini.

Hakuna Mtu/Watu Waliokamatwa Kuhusiana Na Tukio Hilo. Mwili Wa Marehemu
Umehifadhiwa Katika Hospitali Ya Rufaa Mbeya. Juhudi Za Kuwatafuta Waliohusika Katika
Tukio Hilo Zinaendelea.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi
Ahmed Z. Msangi Anatoa Wito Kwa Wananchi Kuacha Tabia Ya Kujichukulia Sheria Mkononi
Kwani Ni Kinyume Cha Sheria Na Badala Yake Wawafikishe Watuhumiwa Wanaowakamata
Kwa Makosa/Tuhuma Mbalimbali Katika Mamlaka Husika Kwa Hatua Zaidi Za Kisheria.






Katika Tukio La Tatu:

Mtoto Mwenye Umri Wa Miaka 09 Aliyefahamika Kwa Jina La Nelly Alick Mkazi Wa
Mlolo Amefariki Muda Dunia Muda Mfupi Wakati Anapatiwa Matibabu Katika Hospitali Ya
Wilaya Ya Mbozi Baada Ya Kugongwa Na Gari Lenye Namba Za Usajili T.257 Crp Aina Ya
Toyota Noah Lililokuwa Likiendeshwa Na Lameck Madihan (34) Mkazi Wa Mlolo.

Ajali Hiyo Imetokea Mnamo Tarehe 26.08.2014 Majira Ya Saa 15:30 Alasiri Huko
Maeneo Ya Karasha, Kata Na Tarafa Ya Vwawa, Wilaya Ya Mbozi, Mkoa Wa Mbeya Katika
Barabara Ya Mbeya/Tunduma. Chanzo Cha Ajali Hiyo Ni Mwendo Kasi. Mwili Wa Marehemu
Umehifadhiwa Katika Hospitali Ya Wilaya Mbozi. Dereva Amekamatwa Na Gari Lipo Kituoni.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi
Ahmed Z. Msangi Anatoa Wito Kwa Madereva Kuwa Makini Wanapotumia Vyombo Vya Moto
Ili Kuepuka Ajali Zinazoweza Kuepukika. Aidha, Anatoa Wito Kwa Watembea Kwa Miguu Kuwa
Makini Wanapotumia Barabara Ili Kuepuka Madhara Yanayoweza Kuepukika.


Imesainiwa Na:
[Ahmed Z. Msangi Sacp]
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya.

You might also like