You are on page 1of 5

TAARIFA KWA VYOMBO VYA

HABARI
ZIARA YA RAIS MSTAAFU ALHAJJ
DR ALI HASSAN MWINYI KATIKA
JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara
ya siku tatu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ziara hiyo ya Rais
Mstaafu inafuatia mwaliko wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
uliomuomba kuwa mgeni mashuhuri katika sherehe za kuadhimisha
miaka hamsini na mbili (52) ya Afrika. Siku ya Afrika huadhimishwa
tarehe 25 Mei na mataifa ya Afrika pamoja na Mabalozi na
Wawakilishi wa mataifa hayo duniani kote, ikiwa ni sehemu ya
kumbukumbu ya kuasisiwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU)
tarehe 25 Mei 1963.
Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina desturi ya kuungana na
Waafrika pamoja na wadau wengine wanaounga mkono hatua za
ukombozi na kupinga ubeberu katika maadhimisho ya siku hii
muhimu.Katika sherehe hizo, Rais Mstaafu Mwinyi alihutubia hadhira
iliyoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Dkt Muhammad
Javad Zariff na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi waliopo
Iran, Viongozi na Maafisa waandamizi wa Serikali ya Iran, na wadau
wengine muhimu ikiwemo wanataaluma, wawakilishi wa sekta
binafsi na wanahabari.
Aidha, Rais Mstaafu Mwinyi alipata nafasi ya kukutana na Mkuu wa
Kamisheni ya Usuluhishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye pia
ni Rais Mstaafu wa taifa hilo Ayatollah Hashemi Rafsanjani. Ayatollah
Rafsanjani alikuwa Rais wa Iran wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais
wa Tanzania na wawili hao waliimarisha uhusiano wa kidiplomasia
wa mataifa haya mawili ambapo kila mmoja alizuru nchi ya
mwenziwe. Rais Mstaafu Mwinyi aliupokea mwaliko wa taifa hilo kwa
lengo la kuzidi kuimarisha uhusiano wa kidugu baina ya Tanzania na
Iran. Katika ziara hiyo, Rais Mstaafu Mwinyi aliongozana na Mke
wake, Mama Khadija Mwinyi.

RAIS MSTAAFU MWINYI AKILAKIWA


RAFSANJANI IKULU JIJINI TEHRAN

NA

AYATOLLAH

HASHEMI

MAJADILIANO BAINA YA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI NA MKUU


WA BARAZA LA USULUHISHI LA JAMHURI YA IRAN AYATOLLAH
RAFSANJANI JIJINI TEHRAN

RAIS MSTAAFU ALHAJJ ALI HASSAN MWINYI AKIKATA KEKI YA


KUADHIMISHA MIAKA 51 YA SIKU YA AFRIKA. WA KWANZA KULIA NI
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRAN DKT ZARIFF NA WENGINE NI
WAHESHIMIWA MABALOZI WALIOHUDHURIA SHEREHE HIYO.
Taarifa hii imeandaliwa na kusambazwa na Ofisi ya Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

You might also like