Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword or section
Like this
6Activity
P. 1
Mchango wa Dk. Slaa kuhusu bajeti 2010/11

Mchango wa Dk. Slaa kuhusu bajeti 2010/11

Ratings: (0)|Views: 170 |Likes:
Published by Subi
Mchango wa mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa kuhusu bajeti ya Serikali 2010/2011
Mchango wa mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa kuhusu bajeti ya Serikali 2010/2011

More info:

Published by: Subi on Jun 17, 2010
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as RTF, PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

10/27/2011

pdf

text

original

 
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANIDR.WILLIBROD PETER SLAA (MB) KUHUSU MAKADIRIO YAMATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA KWAMWAKA WA FEDHA 2010/2011UTANGULIZI:1: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Kambi yaUpinzani kuwasilisha Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Hotuba ya Mapitio naMwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Matumizi ya Fedha, Ofisi yaWaziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99(3) (7) , Toleo laMwaka 2007.2: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kuwashukuru sana wananchi, nawapiga kura wangu wa Wilaya ya Karatu ambao kama kawaida wameendeleakuniunga mkono wakati wote kwa njia mbalimbali na hasa kwa mshikamano waowa kuijenga wilaya yetu. Nawashukuru sana, na hasa kwa kuionyesha Tanzania nzima kuwa kumbemaendeleo yanawezekana hata bila CCM. Nachukua fursa hii kuwahakikishiakuwa nitaendelea kuwatumika kwa akili, moyo na uwezo wangu wote.3: Mheshimiwa Spika, Nachukua fursa hii pia kuwashukuru Watanzania wotekutoka kona zote za Tanzania wenye mapenzi mema ambao kwa maelfuwamendelea kutuunga mkono na kujifunza kutoka Karatu katika jitihada zaombalimbali za kujiletea maendeleo. Kwa wapenzi wetu wote, Mwenyezi Munguawarudishie mara mia kwa upendo wenu.
1
 
4: Mheshimiwa Spika, nitakuwa nimekosa fadhila iwapo sitatoa shukrani kwaChama changu CHADEMA, chini ya uongozi thabiti wa Mhe. Freeman Mbowe,Mwenyekiti (T). Chadema ndio kimeniwezesha kufika hapa Bungeni. Kwawaliofikiri kuwa ubunge unapatikana kwa njia ya CCM tu, natumaini wameonakuwa Ubunge unapatikana pia kupitia kambi ya Upinzani. Watanzania waache tuhofu na uwoga, Tanzania ni yetu sote. Vyama vyote vya siasa ni “milango namadirisha”tu ya kuwahudumia. Haitoshi kulalamika kila mwaka, mabadilikoyanawezekana kila mmoja akifanya na kutimiza wajibu wake.5: Nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wenzangu wa Kambi ya Upinzaniwakiongozwa na Mhe. Hamad Rashid Mohamed, (Mb) Mbunge wa Wawi naKiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa msaada walionipa wakatiwote katika kipindi chote cha miaka mitano tunayoelekea kumaliza sasa kamaKambi ya Upinzani. 6: Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mhe. Mizengo K.P.Pinda (Mb)Waziri Mkuu, Mhe. Celina O.Kombani (Mb) Mawaziri wa Nchi, na Naibu Wazirina Makatibu Wakuu kwa kuandaa Bajeti hii wakisaidiana na Wataalam wao wote,na kwa ushirikiano walionipa wakati wote katika utekelezaji wa majukumu yangumbalimbali hapa Bungeni na kwa Jimbo langu la Karatu.7: Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa, napenda kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuliongozaBunge letu Tukufu na kuliweka katika medani ya kimataifa kwa ubora, uongozi wakasi na viwango vya juu na kuwa kielelezo cha kweli cha demokrasia katika nchi. Ninamwomba Mwenyezi Mungu awajalie hekima na busara na kuwapatia nguvuna afya mnazohitaji katika kuliendesha vizuri Bunge letu hasa katika kipindi hiki
 
cha lala salama. 
MAJUKUMU YA UPINZANI NA KAMBI YA UPINZANI:
8: Mheshimiwa Spika, hii ni bajeti ya Tano na ya mwisho kwa Serikali ya Awamuya Nne. Kwa kuwa hii ni Hotuba yetu ya mwisho kwa Bajeti hii, tutafuata zaidimfumo wa tathmini ya utendaji wa Serikali kwa kutathmini bajeti hii na Bajetizilizopita za Serikali.9: Mheshimiwa Spika, Kazi ya msingi ya kikatiba ya Kambi ya Upinzani siyokuipigia makofi Serikali ya Chama Tawala bali kuangalia zaidi mapungufu katikamaeneo mbalimbali kwa lengo la kuwaonyesha wananchi kwanini waendeleekuichagua Serikali iliyoko madarakani au kwa nini wasiiondoe kwa njia yaSanduku la kura kama hawajaridhika na utendaji wake.10: Mheshimiwa Spika, Watanzania wanahitaji pia kuonja yale yanayopendekezwakutolewa na vyama vingine. Huu ndio mchezo wa demokrasia japo katikademokrasia “Changa” ukitamka hivyo wengine wanaona huo ni uhaini. Tathminiyetu itafuatiliwa na maoni ya Kambi ya Upinzani.11: Mheshimiwa Spika, Iwapo vyama vya Upinzani vitaipigia makofi Serikali yaChama Tawala, basi vyama hivyo vitakuwa wasindikizaji tu siku zote, wakati nalengo lenyewe la kuvisajili ni kutengeneza ushindani wa sera na utendaji katikakuwaletea matumaini mapya wananchi kwa njia ya uchaguzi wa mara kwa mara na pale Chama Tawala kinaposhindwa kutekeleza matumaini ya Wananchi,wakiondoa kwa njia ya Uchaguzi na kujaribu Chama kingine. Ndio maana yautajiri wa vyama vya siasa.
3

Activity (6)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 thousand reads
1 hundred reads
Nicazius liked this
pkihogo liked this
David Sichizya liked this
John J. Kundi liked this

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->