You are on page 1of 1

4486

Maoni ya Mhariri Karibu kwenye Tovuti yetu na tunaomba maoni yako.


Habari za Kitaifa 26.05.2009 1132 EAT
Habari za Mikoani Serikali yabariki mkataba kuvunjwa
Habari za Zanzibar
Na Nakajumo James,Moshi
Habari za Nyumbani
Wazo Binafsi SERIKALI imebariki maamuzi ya vyama vitatu vya ushirika vya msingi Uswa Mamba, Shari na
Kyeri wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kutaka kuvunja mkataba na kampuni ya uwekezaji ya Fiona
Makala (T) LTD.
Barua
Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro, Kasya Kasya, aliyasema hayo wakati
Mashairi akizungumzia mgogoro baina ya mwekezaji huyo na bodi ya vyama hivyo.
Habari za Bungeni
Alisema mkutano wa vyama hivyo chini ya mwenyekiti wake, Bashiri Shoo, uliofanyika Mei 11
Biashara mwaka huu ulikuwa na baraka zake, baada ya yeye kuwa na majukumu mengine ya kiofisi.
Elimu
Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 300 vyama hivyo vilimtaka wakili wao, Apolo Maruma
Jamii kumuandikia notisi ya siku 30 mwekezaji huyo, Fiona (T) Ltd, awe amekabidhi shamba kwa
Sayansi na Teknolojia vyama hivyo.
Siasa “Wanachama ndiyo wenye uamuzi wa mwisho na mali yao ambayo ni mashamba waliyomkabidhi
Afya mwekezaji, hatua ya kutaka kuvunja mktaba mimi siipingi, ila wafuate taratibu,”alisema Kasya.
Burudani Aidha vyama hivyo viliazimia kutoutambua mkataba wa maridhiano na mwekezaji huyo ambao
pamoja na mambo mengine unaeleza kumsamehe deni la Sh milioni 72.
Michezo
Majarida Yetu Akizungumzia uamuzi wa vyama hivyo, Kasya alivitaka vyama hivyo kutumia utaratibu uliotumika
kuingia mkataba huo ili kuweza kuuvunja kama walivyoazimia.

Alisema vyama hivyo vinamlalamikia mwekezaji huyo kwa madai kwamba baada ya kufanya
vyema katika miaka ya 1999 hadi 2003 kwa kuendeleza zao la kahawa, baada ya hapo alianza
kung’oa kahawa na miti na kuotesha Mahindi na Maharage.

Kwa upande wake, mwekezaji huyo, Benjamin Mengi, alipohojiwa kuhusu hali hiyo alishikilia
msimamo wake kwamba hatambui maamuzi ya mkutano huo.
Rudi Nyuma Songa Mbele

© New Habari (2006)


Ltd. All rights reserved
Hutolewa na New Habari (2006) Ltd. S.L.P. 78235, Dar es Salaam
mtanzania@newhabari.com

You might also like