Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more ➡
Download
Standard view
Full view
of .
Add note
Save to My Library
Sync to mobile
Look up keyword
Like this
2Activity
×
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
Hotuba Ya Raisi Nane Nane 2010

Hotuba Ya Raisi Nane Nane 2010

Ratings: (0)|Views: 871|Likes:
Published by Subi

More info:

Categories:Types, Speeches
Published by: Subi on Aug 10, 2010
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, DOC, TXT or read online from Scribd
See More
See less

10/25/2012

pdf

text

original

 
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHOKIKWETE, KATIKA KILELE CHA SHEREHE ZA SIKUKUU YA WAKULIMA, NANE NANE KWENYEUWANJA WA NZUGUNI - DODOMA, TAREHE 08 AGOSTI, 2010Mhe. Stephen Wassira, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika;Waheshimiwa Mawaziri;Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa;Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa TASO;Mwenyekiti wa TASO Taifa;Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika;Washiriki kwenye Maonesho;Waheshimiwa Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa, Vyama vya Ushirika;Mashirika ya Dini na Asasi nyingine za Wananchi;Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika;Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana:Nakushukuru sana Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Stephen Wassira kwaheshima kubwa uliyonipa ya kunialika katika kilele cha Maadhimisho ya 17 ya Sherehe zaWakulima, maarufu kwa jina la Nane Nane ya mwaka 2010. Nawashukuru na kuwapongezakwa namna ya kipekee Mhe. Eng. James Msekela, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mhe. PasekoOle Kone, Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na viongozi na wananchi wa Mikoa hii kwamaandalizi mazuri ya sherehe za mwaka huu. Hii ni mara ya tatu mfululizo sherehe hizizinafanyika katika kanda ya kati na hapa hapa kwenye Uwanja wa Maonesho wa Nzugunikatika Manispaa ya Dodoma. Sherehe zimefana sana na najiandaa kufaidi zaidinitakapotembelea mabanda ya maonesho.Ndugu zangu,Nawashukuru kwa mapokezi mazuri na burudani. Pia nakushukuru Mwenyekiti wa TASO kwahotuba yako nzuri na wewe Mheshimiwa Waziri kwa maelezo yako ya utangulizi. Lakinishukrani kubwa zaidi nazitoa kwa wale wote walioshiriki maonesho haya kwa kujengamabanda na kutuonesha shughuli mzifanyazo katika kuleta mapinduzi ya kilimo, ufugaji nauvuvi nchini. Nawapongeza sana wale wote walioshinda na kupata zawadi mbalimbali.Hongereni sana! Tuzo mtakazopewa ni uthibitisho wa kiasi gani mmefanikiwa katika kuendeleza kilimo nchini.Ni kitendo cha kutambua kazi nzuri mliyoifanya katika kutumia maarifa ya kisasa na teknolojiazinazosaidia kuongeza tija, uzalishaji na ubora wa mazao ya kilimo na mifugo. Wapo piawanaopata tuzo kwa kutambua mchango wao katika kutoa huduma zinazosaidia kuongeza tija,uzalishaji na ubora wa mazao. Huduma hizo ni pamoja na zile za upatikanaji wa zana za kilimona ufugaji pamoja na pembejeo muhimu kama vile mbolea, mbegu bora, madawa nateknolojia mbalimbali. Wapo wanaotambuliwa kwa huduma za masoko na kwa kuongezathamani mazao ya wakulima na wafugaji. Ni matumaini yangu kwamba tuzo hizo zitakuwakichocheo cha kuongeza juhudi na maarifa zaidi katika kazi zenu. Aidha, ninyi mlioshindamtakuwa darasa la mafunzo kwa wengine.Ndugu Wakulima, Wafugaji na Wanaushirika,Baada ya kumaliza kutoa zawadi nitatembelea baadhi ya mabanda ya maonesho nami nionekwa kiasi gani tunapiga hatua katika safari yetu ya kuleta mapinduzi ya kijani nchini.Nimeambiwa kuwa katika maonesho haya unaoneshwa jinsi utaalamu na teknolojiambalimbali zilizobuniwa na kuanza kutumiwa katika shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvizinavyoweza kuongeza tija. Kwa kweli taarifa hizo zinanifurahisha na kunipa faraja kubwakwamba ipo kazi nzuri inayoendelea kufanywa kuleta mageuzi katika kilimo chetu na ufugajiwetu nchini. Nachukua nafasi hii kuwapongeza wataalam wa kilimo, mifugo na uvuvi kwa kazinzuri ya kubuni, kuandaa na kuifikisha teknolojia na maarifa kwa walengwa. Aidha
 
nawashukuru wenzetu wa sekta binafsi kwa mchango wao mkubwa unaowezesha zana napembejeo za kilimo kupatikana. Pia nawapongeza kwa huduma ya masoko na kuongezathamani mazao yetu.Ni matarajio yangu kwamba mambo yanayooneshwa hapa yatapatikana kwa urahisi mtuanapoyahitaji. Pia yatapatikana kwa bei au gharama nafuu. Ni matumaini yangu pia kwamba,kwa wakulima wenzangu na wafugaji wenzangu tuliobahatika kutembelea maonesho haya aukupata habari zake kupitia vyombo vya habari kwamba tuliyojifunza hapa tutayazingatia nakuyatumia kubadili kilimo chetu na ufugaji wetu. Na njia pekee ya kuthibitisha hayo nikuongeza tija, uzalishaji na ubora wa mazao yetu ya kilimo, mifugo na uvuvi.Ndugu Wananchi, Tukifanya hivyo tutakuwa tumetimiza wajibu wetu kwa mujibu wa kaulimbiu ya mwaka huuisemayo KILIMO KWANZA “Mapinduzi ya Kijani – Uhakika wa Chakula na Kipato”. Kauli mbiu hiini mwendelezo wa ile ya mwaka 2009. Inafanyika hivyo kwa sababu nzuri ya kusisitizaumuhimu wa kilimo kwa mkulima, jamii na taifa. Kwa mkulima kilimo kinamhakikishia chakulana ni chanzo cha mapato yatakayomwezesha kupata mahitaji yake ya msingi ya maisha nahivyo kuinua hali yake ya maisha. Kwa jamii na taifa, licha ya kuhakikisha upatikanaji wachakula, kilimo ni kichocheo kwa sekta nyingine za uchumi kukua na hivyo kukuza pato la taifana watu wake.Ukweli ni kwamba mataifa mengi ambayo sasa ni tajiri yalianzia kwenye kuleta mageuzi yakilimo. Kilimo ndiyo mwanzo wa kila kitu kwa mwanadamu, jamii na mataifa. Bila ya shakamtaelewa kwa nini wadau wa Serikali na sekta binafsi tulikuja na Azimio la Kilimo Kwanzamwaka jana. Kwa sisi, Tanzania asilimia 80 ya watu wetu wanaishi vijijini na wanategemeakilimo kwa maisha yao. Lakini wanategemea kilimo cha kujikimu tu ndiyo maana wengi wao nimaskini na nchi yetu ni maskini.Ndugu Wananchi,Sherehe za mwaka huu ni za tano tangu Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani. Pia ni zamwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010. Vile vile Sherehe hizi zinafanyika mwakammoja tangu nilipozindua Azimio la Kilimo Kwanza katika Uwanja huu huu mwaka jana. Hivyobasi, Maadhimisho ya mwaka huu yanatoa fursa ya pekee kwetu kuangalia tulikotoka, tuliposasa na tunakoelekea katika juhudi zetu za kuendeleza kilimo nchini katika miaka 5 ya Serikaliyetu. Aidha inatupa fursa ya kupima utekelezaji wa Azimio la Kilimo Kwanza.Ndugu Wakulima Wenzangu, Wafugaji Wenzangu, Wana-Ushirika na Wananchi Wenzangu,Leo, naona fahari kusema kuwa tumepata mafanikio ya kutia moyo katika azma yetu yakuendeleza sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Matokeo yake yanaonekana mahali mbalimbali. Tumetekeleza kwa ufanisi malengo ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo yaaniAgricultural Sector Development Programme – ASDP na Azimio la KILIMO KWANZA. Kwa nia yakujenga uwezo zaidi na kuleta mageuzi katika kilimo chetu nchini tarehe 8 Julai, 2010 Serikaliyetu imeridhia Programu Kabambe ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika yaani ComprehensiveAfrica Agriculture Development Programme – CAADP itekelezwe nchini.Utekelezaji wa Programu hii unalenga kutoa msukumo mkubwa zaidi kwa utekelezaji wa dirayetu ya kuendeleza kilimo kama ilivyofafanuliwa katika ASDP na Azimio la Kilimo Kwanza.CAADP inasisitiza mageuzi ya kilimo kama yalivyo malengo ya ASDP, pia inasisitiza ushiriki wasekta binafsi kama ilivyo katika Azimio la Kilimo Kwanza. Kuna mambo matatu mapyayanatiliwa mkazo na CAADP ambayo hatukuyapa mkazo kama huo katika ASDP na KilimoKwanza. Mambo hayo ni matumizi ya matrekta, upatikanaji wa mikopo kwa wakulima na lishe.
 
 Jambo lingine la manufaa kwa Tanzania kujiunga na CAADP ni uwezekano wa kupata misaadaya kuendeleza kilimo kutokana na mfuko maalum ulioanzishwa katika mkutano wa G20 waLaquila, Italia mwaka 2008.Ndugu Wakulima, Wafugaji na Wanaushirika,Ukiacha hayo ya kuwa na dira inayoeleweka kwa mujibu wa ASDP, Kilimo Kwanza na sasaCAADP, tumechukua hatua za makusudi za kuongeza bajeti ya Sekta ya Kilimo kutoka shilingi233.3 bilioni mwaka 2005/06 hadi kufikia shilingi 903.8 bilioni kwa mwaka 2010/2011. Kwaongezeko hilo, bajeti ya kilimo kwa sasa imefikia asilimia 7.8 ya bajeti ya Serikali. Hii ni hatuanzuri kuelekea kwenye lengo la asilimia 10 lililoamuliwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi zaSADC mwaka 1998 katika mkutano uliofanyika Dar es Salaam na Wakuu wa Nchi za Afrika kuleMaputo, Msumbiji, mwaka 2003.Kutokana na ongezeko hili la bajeti malengo ya ASDP na Kilimo Kwanza yamewezakutekelezwa vizuri. Naamini kama uwezo ungekuwa mkubwa zaidi tungefanya makubwa zaidihasa kutokana na ukweli kwamba kazi iliyo mbele yetu ni kubwa zaidi. Kilimo cha umwagiliajikimepanuliwa kutoka hekta 264,388 mwaka 2005/2006 hadi 326,492 Desemba, 2009. Kwakuongeza fedha za ruzuku ya pembejeo kama mbolea, mbegu bora na madawa ya kilimo namifugo kutoka shilingi 7.5 bilioni mwaka 2005/06 hadi shilingi 143.8 bilioni mwaka 2010/11upatikanaji na matumizi ya pembejeo hizo umeongezeka sana sasa.Faida yake imeanza kuonekana kwenye kuongezeka kwa tija na uzalishaji wa mazao yampunga, mahindi na pamba. Tanzania inaweza kujitosheleza kwa chakula kwa wastani waasilimia 95. Lakini mwaka huu tumejitosheleza kwa asilimia 112 kwa maana kuwa tuna ziadaya asilimia 12.Uzalishaji wa pamba na mazao mengine ya biashara nayo kama vile kahawa natumbaku umeongezeka sana. Mpango wa kugawa pembejeo za kilimo kwa kutumia vocha naoumesaidia sana kuwafanya walengwa kunufaika moja kwa moja.Hali kadhalika wafugaji nao wamenufaika. Ng’ombe 11,134,000 wamepatiwa chanjo ya homaya mapafu na chanjo nyingine zinaendelea kutolewa. Majosho mapya 543 yamejengwa nchinzima na Shs.13.5 bilioni zimetumika kwa ajili ya dawa za majosho ya mifugo. Tutaendelea kuongeza fedha za ruzuku ili wakulima wengi zaidi wapate pembejeo za kisasazitakazoongeza uzalishaji na kuwahakikishia wakulima usalama wa chakula na kuwaongezeamapato. Hata hivyo, tunakusudia kuwajengea wakulima mfumo utakaowawezesha kupata kwaurahisi mikopo ya kununua pembejeo na zana za kilimo kama vile, mbolea, mbegu bora,madawa, matrekta n.k.Kwa ajili hiyo kwanza, tumetilia mkazo na kuhimiza wakulima kuanzisha SACCOS ambazondizo zitawarahisishia wakulima kupata mikopo kwa shughuli zao za kilimo, ufugaji na uvuvi.Lakini, SACCOS zinaweza kutoa mikopo midogo midogo tu, hivyo wakulima wanaotakakupanua shughuli zao na kununua zana bora zaidi SACCOS hazitaweza kuwasaidia sana. Kwasababu hiyo, tumeamua kuanzisha Benki ya Kilimo ambayo matayarisho yake yanaendelea.Katika bajeti hii tumetenga shilingi 50 bilioni katika Fungu Maalum kwa ajili hiyo. Tangu mwaka jana tulianzisha utaratibu maalum wa kutoa mikopo ya shughuli za kilimo. Tumeanzisha dirishamaalum la mikopo hiyo kwenye Benki ya TIB. Dirisha hili litakuwa ndiyo kitovu cha kuanzishiaBenki ya Kilimo hapo wabia wetu watakapokuwa tayari.Ndugu wananchi,Kwa kutambua umuhimu wa kuongeza matumizi ya zana bora za kilimo hasa matrektatulianzisha utaratibu wa kuzitaka Halmashauri za Wilaya kuagiza matreka na kuwauziawakulima. Aidha, tumeongeza fedha katika mfuko wa pembejeo kutoka Shs. 4.9 bilioni hadiShs. 30.1 bilioni. Kati ya fedha hizo Shs. 16.3 bilioni zilitumika kuagizia matrekta. Kwa jumla,hatua hizo tulizochukua kati ya mwaka 2006 na 2010 jumla ya matrekta 3,948 yameingizwanchini. Huu ni sawa wa wastani wa matrekta zaidi ya 780 kwa mwaka ambayo ni mafanikio ya

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->