You are on page 1of 9

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA MKUU WA MKOA

MOROGORO

TAARIFA YA MAFUNZO YA MANUNUZI YA UMMA NA USIMAMIZI WA


MIKATABA KWA WAHANDISI WA SERIKALI ZA MITAA YALIYOYOFANYIKA
KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA

EDEMA – MOROGORO

TAREHE 21 - 25 FEBRUARI, 2011.

Februari 2011
YALIYOMO
VIFUPISHO..................................................................................................................................ii
1. UTANGULIZI................................................................................................................................1
2. WARATIBU WA MAFUNZO.......................................................................................................1
3. WAWEZESHAJI WA MAFUNZO..............................................................................................2
4. MADA ZILIZOTOLEWA..............................................................................................................2
5. MAELEZO MAFUPI KWA KILA MADA ILIYOTOLEWA.........................................................3
5.1 Mapitio ya Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya Mwaka 2004 na Kanuni
zake. 3
5.2 Mahitaji ya Mpango wa Manunuzi wa Mwaka.............................................................3
5.3 Tathimini ya Kandarasi.....................................................................................................4
5.4 Kutengeneza Mikataba ....................................................................................................4
5.5 Mapitio ya Usimamizi wa Mikataba, Wajibu wa Wahusika wa Mikataba na
Mawasiliano....................................................................................................................................4
5.6 Hati za Malipo na Upimaji wa Kazi za Ujenzi...............................................................4
5.7 Mabadiliko ya Kazi katika Miradi ya Ujenzi..................................................................5
5.8 Usimamizi wa Madai..........................................................................................................5
5.9 Kukatisha Mkataba............................................................................................................5
5.10 Utunzaji wa Kumbukumbu za Manunuzi......................................................................5
5.11 Kutatua Migogoro..............................................................................................................6
6 MAONI...........................................................................................................................................6

i
VIFUPISHO.
1. PPRA – Public Procurement Regulatory Authority
2. DC – District Council
3. MC – Municipal Council
4. Eng. – Engineer
5. LGTP – Local Government Transport Programme
6. GN - Government Notice

ii
1. UTANGULIZI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa inaratibu Mafunzo ya Manunuzi ya Umma na
Usimamizi wa Mikataba kwa Wahandisi wa Serikali za Mitaa. Mafunzo hayo
yanalenga katika kuwajengea Uwezo Watumishi hao katika swala zima la Manunuzi
na Usimamizi wa Mikataba ili waweze kufanya kazi zao kwa Ufanisi na Tija kwa
manufaa ya Taifa. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema
Manispaa ya Morogoro tarehe 21 – 25 Februari, 2011.

Walengwa mahsusi wa Mafunzo hayo walikuwa ni Wahandisi wa Sekretarieti za


Mikoa na Halmashauri. Wahandisi wa Sekretarieti za Mikoa na baadhi ya
Halmashauri zake kwenye mabano walioalikwa kwenye Mafunzo hayo ni kutoka
Mikoa ifuatayo: Arusha (Karatu DC), Dodoma (Mpwapwa DC na Kongwa DC), Iringa
(Kilolo DC, Ludewa DC na Njombe DC), Kagera (Biharamulo DC na Chato DC),
Kigoma (Kasulu DC na Kigoma MC), Kilimanjaro (Same DC), Lindi (Kilwa DC na
Lindi DC), Manyara (Hanang DC na Simanjiro DC), Mara (Musoma MC na Rorya
DC), Mbeya (Chunya DC, Mbeya DC na Mbozi DC), Morogoro (Kilosa DC na Ulanga
DC), Mtwara (Mtwara DC na Newala DC), Mwanza (Magu DC na Geita DC), Pwani
(Bagamoyo DC na Mkuranga DC), Rukwa (Mpanda DC), Ruvuma (Namtumbo DC),
Shinyanga (Kishapu DC), Singida(Iramba DC), Tabora (Igunga DC, Urambo DC na
Sikonge DC) na Tanga (Lushoto DC, Pangani DC na Mkinga DC).

Katika Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro, Eng. Kishiwa Magembe alihudhuria


Mafunzo hayo.

Aidha Wawezeshaji wa Mafunzo hayo walikuwa ni kutoka Ofisi ya Mamlaka ya


Kuthibiti Manunuzi ya Umma Public Procurement Regulatory Authority (PPRA).

2. WARATIBU WA MAFUNZO.
Maafisa Wafuatao kutoka OWM – TAMISEMI waliratibu mafunzo hayo.

1. Eng. Elina Kayanda – Mkurugenzi LGTP


2. Bw. Richard Lwoga

1
3. WAWEZESHAJI WA MAFUNZO
Katika kufanikisha Mafunzo hayo Wawezeshaji wafuatao kutoka PPRA walishiriki:

1. Eng Dr. Ramadhani S. Mlinga - Chief Executive Officer, PPRA.


2. Eng Raymond – PPRA

4. MADA ZILIZOTOLEWA
Wawezeshaji waliweza kuwasilisha mada mbalimbali katika Mafunzo haya. Pamoja
na mambo mengine, mada zifuatazo zilijadiliwa:

1. Mapitio ya Sheria ya Manunuzi ya Umma No. 21 ya Mwaka 2004 na Kanuni


zake.
2. Mahitaji ya Mpango wa Manunuzi wa Mwaka.
3. Tathimini ya Kandarasi.
4. Kutengeneza Mikataba ya Miradi.
5. Mapitio ya Usimamizi wa Mikataba, Wajibu wa Wahusika wa Mikataba na
Mawasiliano.
6. Hati za Malipo na Upimaji wa Kazi za Ujenzi.
7. Mabadiliko ya Kazi katika Miradi ya Ujenzi.
8. Usimamizi wa Madai.
9. Kukatisha Mkataba.
10. Utunzaji wa Kumbukumbu za Manunuzi
11. Kutatua Migogoro.

2
5. MAELEZO MAFUPI KWA KILA MADA ILIYOTOLEWA
5.1 Mapitio ya Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya Mwaka 2004 na Kanuni
zake.
5.1.1 Sheria ya Manunuzi Na. 21 ya Mwaka 2004 hutumika kwa Taasisi zote za
Umma na Taasisi zisizo za Umma lakini hupokea fedha za Umma kama
inavyosomeka katika Sheria hiyo Sehemu ya 2 (1) (a-b).
5.1.2 Vile vile Sheria hiyo hutumika kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama isipokuwa
kwa vitu ambavyo vimezuiliwa (restricted items) kama inavyosomeka katika
Sheria hiyo Sehemu ya 2 (2) (a-b).
5.1.3 Bodi za Zabuni na Taasisi zake za Manunuzi zihakikishe zinafanya kazi zake
kwa Usawa kwa kuzingatia kuwa zinatoa nafasi sawa kwa wazabuni ili
thamani ya fedha iweze kupatikana kama inavyosomeka katika Sheria
Sehemu ya 43.
5.1.4 Mamlaka ya Kudhibiti Manunuzi ya Umma Public Procurement Regulatory
Authority (PPRA) iliundwa kwa Mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma Na.
21 ya Mwaka 2004 Sehemu ya 5 na Malengo na Kazi zake zimeainishwa
katika Sheria Sehemu za 6 na 7.

5.2 Mahitaji ya Mpango wa Manunuzi wa Mwaka.


5.2.1 Mpango wa Manunuzi wa Mwaka umewekwa kisheria kama Sehemu ya 45 ya
Sheria , Kanuni 40, 46 na 47 za GN 97 na Kanuni 25 na 26 za GN 98
zinavyosomeka.
5.2.2 Idara zote kwenye Taasisi zishiriki katika kuweka inputs kwenye mpango na
Kitengo cha Manunuzi kiratibu mchakato wa Mpango Mzima.
5.2.3 Mpango ni lazima Ujadiliwe kwa kina katika Vikao vya Menejimenti na
muafaka upatikane ikiwa ni pamoja na Mipango kazi ya Mwaka na Mtiririko wa
fedha.
5.2.4 Mpango wa Manunuzi ni lazima uthibitishwe na Afisa Maduhuli Accounting
Officer.
5.2.5 Mpango wa Manunuzi unatakiwa kuwa wa aina tatu: Kwa ajili ya Matumizi ya
Ndani, Kwa ajili ya Matumizi ya Nje na Kwa ajili ya kupeleka PPRA.

3
5.3 Tathimini ya Kandarasi
5.3.1 Malengo ya Kufanya Tathimini na Utaratibu wa jinsi ya Kufanya Tathimini ya
Zanuni ilielezwa.
5.3.2 Mambo ya kuzingatia katika kufanya Tathimini kama inavyosomeka katika
Sheria Sehemu ya 67 na Kanuni ya 90 GN Na. 97.

5.4 Kutengeneza Mikataba .


5.4.1 Maana Kamili ya Mkataba ilielezwa.
5.4.2 Mambo yanayofanya Mkataba ukamilike kisheria yalizungumzwa ambayo ni:
An intention to create a legal relationship, Offer, Acceptance of an Offer,
Consideration, Capacity to Contract na Legality.
5.4.3 Jinsi ya Kumaliza Mkataba Discharge of Contract ililezwa.

5.5 Mapitio ya Usimamizi wa Mikataba, Wajibu wa Wahusika wa Mikataba na


Mawasiliano.
5.5.1 Maana na Umuhimu wa Usimamizi wa Mikataba ulielezwa.
5.5.2 Usimamizi wa Mikataba upo Kisheria kama Kanuni Na. 121, 122 na 123 za
GN Na. 97 za 2005 zinavyoeleza.
5.5.3 Taratibu za Usimamizi wa Miradi ulielezwa
5.5.4 Maana na Umuhimu wa Mawasiliano katika Usimamizi wa Mikataba ulielezwa.
Aidha aina na taratibu za Mawasiliano zilisisitizwa.

5.6 Hati za Malipo na Upimaji wa Kazi za Ujenzi


5.6.1 Taratibu za kufanya Malipo zilielezwa ambazo hutegemea jinsi Makubaliano
Mahsusi ya Mkataba yanavyoeleza.
5.6.2 Aina za Hati za Malipo zilielezwa.
5.6.3 Aina za Malipo zilielezwa pia.
5.6.4 Mwongozo wa Kutoa Hati za Malipo na Kufanya Malipo kwa Mikataba ya
Ujenzi ulielezwa na kusisitizwa.

4
5.7 Mabadiliko ya Kazi katika Miradi ya Ujenzi.
5.7.1 Maana ya Mabadiliko ya Kazi Variations ilielezwa.
5.7.2 Sababu zinazoweza kusababisha Variations zilielezwa.
5.7.3 Taratibu za kufanya Mabadiliko kwenye mikataba zilisisitizwa.

5.8 Usimamizi wa Madai


5.8.1 Maana ya Madai katika Kazi za Ujenzi ilielezwa.
5.8.2 Viashiria vinavyoonyesha kuwa Mkandarazi anaweza kumdai Mwajiri
vilijadiliwa.
5.8.3 Viashiria vinavyoonyesha kuwa Mwajili anaweza kumdai Mkandarasi.
5.8.4 Aina na mambo yanayosababisha Madai yalijadiliwa.
5.8.5 Jinsi ya Kuandaa Madai ilijadiliwa.
5.8.6 Kutatua Madai na Kumbukumbu zinazoweza kuhalalisha Madai zilijadiliwa.

5.9 Kukatisha Mkataba.


5.9.1 Maana ya Kukatisha Mkataba ilielezwa.
5.9.2 Mazingira yanayoweza kusababisha Mkataba kuvukatishwa kwa
kusababishwa na upande wowote wa Mkataba yalielezwa.
5.9.3 Aina za Kukatisha Mkataba zilielezwa na hatua za kuchukua baada ya
kukatisha Mkataba.

5.10 Utunzaji wa Kumbukumbu za Manunuzi


5.10.1 Maana ya Kumbukumbu ilitolewa kama Sheria ya Kumbukumbu Na. 3 ya
Mwaka 2002.
5.10.2 Utunzaji Kumbukumbu za Manunuzi ya Umma umewekwa Kisheria kama
Sehemu ya 56 ya Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya Mwaka 2004
inavyoelekeza.
5.10.3 Kanuni Na. 19 (1) cha GN Na. 97 ya Mwaka 2005 inaonyesha aina ya Taarifa
ambazo Mwajiri anapaswa kuzitunza
5.10.4 Mambo ambayo yanaonyesha mapungufu katika utunzaji wa Kumbukumbu za
Manunuzi yalielezwa.

5
5.11 Kutatua Migogoro
5.11.1 Namna ya Kutatua Migogoro inayoweza kujitokeza wakati wa Utekelezaji wa
Mradi ilielezwa.
5.11.2 Aina za Utatuzi wa Migogoro ambayo ni: Amicable Settlement, Adjudication,
Mediation, Conciliation, Neutral Evaluation, Arbitration na Litigation zilijadiliwa
kwa kina.

6 MAONI
Mafunzo haya yamejenga Uwezo Mkubwa kwa Washiriki katika swala zima la
Manunuzi ya Umma na Usimamizi wa Mikataba ukizingatia kuwa yalitolewa na
Maafisa Waandamizi wa PPRA. Mafunzo haya yatakuwa na tija zaidi endapo
Wahusika wote wa Mchakato wa Manunuzi ya Umma watajengewa uwezo huu. Kwa
mfano Taasisi ya Umma kama Ofisi ya MKuu wa Mkoa – Morogoro, inaweza
kupanga na kuwaita PPRA kwa ajili ya kuendesha Mafunzo haya kwa Wakuu wa
Klasta, PMU, Wajumbe wa Bodi ya Mkoa ya Zabuni na watumishi wote ambao
wataonekana ni Washika dau wa mchakato wa Manunuzi. Taasisi ikishakuwa na
Uelewa wa pamoja wa mambo ya Manunuzi na Usimamizi wa Miradi itaweza
kuendesha mambo yake kwa Ufanisi na kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za
Serikali hivyo Value for Money inaweza kuonekana zaidi.

You might also like