You are on page 1of 109

1

HISTORIA YA PALESTINA

Fawzy Al-Ghadiry

Mfasiri Ibrahim H. Kabuga Islamic Center of Research

2
Haki ya kunakili imehifadhiwa na:

Islamic Centre for Research (ICR) Kimeandikwa na: Fawzy Al-Ghadiry Kimetafsiriwa na: Ibrahimu H. Kabuga Kimehaririwa na: Othman M. Ntalaruka Kimepangwa na kusanifiwa na: Toleo la kwanza: Nakala: Kimetolewa na kuchapishwa na: Islamic Centre for Research (ICR) Dar es Salaam Tanzania Simu: +255 712 566595/+255 763 348213 +255 772 403100/+255 685 590949 Baruapepe: utafititz@gmail.com

3
YALIYOMO Neno la mchapishaji Utangulizi Historia ya eneo la Arabia Udhibiti wa eneo la Arabia na kuibuka kwa makoloni Palestina na ukweli wa Kihistoria Palestina ya zamani Zama za mawe Kuhama kutoka kwenye ukusanyaji mpaka kwenye uzalishaji (8000 17000B.C) Kuibuka kwa jamii za kilimo (4000 8000B.C) Mwisho wa millennia ya nne kabla ya Kristo Wasemiti Wakanani Zama za falme na himaya mbalimbali (Zama za chuma) (550 1200B.C) Waisraeli Himaya ya Wafursi (Waajemi) Himaya ya Wafursi (Waajemi) na zama za Alexander the Great (550B.C. 330 B.C) Himaya ya Warumi (63B.C. 636 A.D).

4
Kuibuka kwa Ukristo Harakati za ufunguzi wa Kiislamu Palestina katika zama za Makhalifa Wanyoofu Zama za Makhalifa wa Bani Umayya Zama za Ukhalifa wa Bani Abbas Himaya ya Watuluni Utawala wa Ikhshidi Fatimiyya Dola la Seljuk Wazungu Vita ya pili ya msalaba (1146 -1149 A.D.) Himaya ya Ayyubi Vita ya tatu ya msalaba Mamaalik Zama za Uthmaniyya Safari ya Napoleon Bonaparte (1798 1801) Kampeni ya Muhammad Ali Makazi ya Wazayuni katika Palestina

5
Mandeti ya Uingereza
Kipindi cha kabla ya mandeti ya Uingereza Mandeti (mandate) ya Uingereza katika Palestina: 1923-1948 Mapinduzi ya Sheikh Eiz Al-Din Al-Qasam Mapinduzi makubwa ya mwaka 1936 na mradi wa kuigawa Palestina Mradi wa kuigawa Palestina Azimio la kuigawa Palestina Wayahudi kuhamia Palestina Kuhamia baada ya uundwaji wa Israeli 1948-1967 Kuwafukuza Wapalestina kutoka majumbani mwao Maazimio muhimu ya kimataifa kuhusu Palestina

6
UTANGULIZI
Tarehe kumi na tano ya mwezi Mei 2006, ilisadifiana na kumbukumbu ya hamsini ya maangamizi makubwa yaliyosababisha msiba mkubwa, ambao haujawahi kulikumba taifa lolote katika historia yote. Maangamizi hayo ni msiba wa kusikitisha wa wananchi wa Palestina. Ni miaka hamsini, ambayo Israeli imetekeleza njama na mikakati yake ili kulazimisha uhalali wa kuwepo kwake katika eneo hilo. Iliweka mkakati kabambe wa kuchomeka taasisi zake na kujenga makazi ya wahamiaji wa Kiyahudi katika ardhi za Waarabu. Ili kufikia lengo hili, Israeli imenyanganya ardhi za Waarabu, kuwafukuza kwa lazima Wapalestina kutoka majumbani mwao na kuwaondoa kwa nguvu katika ardhi yao. Licha ya hayo yote, Mpalestina ameutunza utambulisho wake na kuupandikiza uzalendo katika kina cha nyoyo za watoto wake, akimpasia bendera ya taifa kutoka kwa mzee wake, ambaye maadui walitaka aangamie, kwenda kwa kizazi kipya, ambacho maadui hao hao walitaka kizame na kipotelee katika usahaulifu. Bendera hiyo, pamoja na mapenzi kwa taifa lake vimeendelea kuwa hai, vikitakaswa na kusafishwa na damu ya mashahidi. Siku zote Mpalestina huyu atasimama imara mbele ya shida, mateso, mauaji na njama za kiovu. Siku zote atajitokeza akiwa imara, kwa sababu yeye ni Mpalestina.. Uchunguzi huu wa Historia ya Palestina unatia mkazo juu ya haki ya kila mwanadamu kurudi kwake na kusisitiza kwamba, haki ya kurudi na kumiliki ardhi na makazi ni haki ya milele ya mtu mmoja mmoja na umma kwa ujumla. Hakuna uvamizi, taifa/nchi, mkataba wala makubaliano yoyote yanayoweza kuikaidi, kuikana na kuikiuka haki hii. Kwani kila uvamizi, bila kujali kuwa utadumu muda gani na bila kujali kuwa ni imara kiasi gani, unadhibitiwa na kuhukumiwa na haki hii. Uchunguzi huu unaoelezea historia ya Palestina tangu mapambazuko ya historia mpaka zama zetu hizi, ni sehemu ya kitabu kikubwa kiitwacho Connecting Voices,

7
kilichoandikwa na mwandishi chipukizi wa Kitunisia aitwaye Fawzy Al- Ghadiry. Dhumuni muhimu la kitabu hiki ni kumfahamisha msomaji juu ya mambo mengi kuhusu Mashariki ya Kati, mambo ambayo humfikia yakiwa yamepotoshwa na kugeuzwageuzwa kutokana na ufidhuli na hila za Wazayauni ambao hubadilisha na kuunda matukio. Aidha, lengo la kitabu hiki ni kuwaeleza watu wote ukweli kuhusu yale yanayotokea Mashariki ya Kati, pamoja na kuwafikishia maoni ya Waarabu na Waislamu kwa namna ya moja kwa moja bila ya hila na michezo michafu ya Kizayuni. Kwa msingi huo, kitabu hiki kimegawanywa katika vipengele vipatavyo kumi na moja ambavyo kila kipengele kimoja kinaelezea masuala muhimu ambayo watu wote wanatakiwa kuyajua. Ni jambo la muhimu sana kwa mzawa wa zama hizi kuyajua baadhi ya mambo ambayo hakuwahi kukutana nayo hapo kabla. Mambo ya hakika kuhusu historia ya eneo la Mashariki ya Kati, ambalo ndilo eneo lenye wasiwasi mkubwa zaidi duniani. Hakuna shaka kuwa, mgogoro wa Palestina ndio chanzo kilicho nyuma ya matatizo mengi duniani, kuanzia kwenye kitu ambacho kimekuja kujulikana kama ugaidi, mpaka kwenye uadui, chuki na uhasama dhidi ya Marekani, na wasiwasi na msukosuko katika mahusiano baina ya nchi mbalimbali duniani, yote haya yakiwa ni mlipuko katika mahusiano hayo ambao hakuna awezaye kutabiri athari zake. Hivyo ni lazima kwa watu sasa kwa ujumla kujua kwa nini mgogoro huu wa Mashariki ya Kati ulitokea baina ya kile kinachojulikana kama Israeli kwa upande mmoja na ulimwengu wa Kiarabu, wakiongozwa na Palestina kwa upande mwingine. Mtu hawezi kujua kwa ukamilifu za mgogoro huo mpaka azame ndani katika historia ya eneo hili ili kufichua ukweli kuhusu mwenyeji wa ardhi hii inayogombaniwa. Je, ni Wayahudi wanaoamini kuwa wao ni taifa teule la Mungu na kwamba ndiyo nchi walioahidiwa naye, au ni Wapalestina ambao ardhi hii imepewa jina lao?

8
Kwanza kabisa tuziangazie taarifa ambazo watu wanazo kuhusu historia ya Palestina, kwa kupitia misimamo yao, kisha tutazama katika historia ya eneo hili tokea maelfu ya miaka iliyopita hadi katika zama zetu hizi. Tuanze kuyaangalia maoni ya shahidi wa kwanza, ambaye ni mwanamke wa Kimarekani mwenye umri wa miaka 50, aitwaye Clara: Nijuavyo kuhusu Uislamu: historia ya miaka mingi lakini inayoanzia kwenye miaka ya

1890, ni tofauti na Wamarekani wenzangu wa rika langu ambao hawajui ya wakati wa nyuma zaidi ya wakati Umoja wa Mataifa ulipoianzisha Israeli. Ninajua vema, kwa mfano, juu ya azimio la Balfour na hati ya Theodor Herzl "Judenstadt" na matatizo yote yaliyotokana na hati hiyo.
Ama kuhusu shahidi wa pili ambaye ni mhandisi wa umeme aitwaye George, anasema: Ninajua kwamba kimsingi baada ya vita vya pili vya dunia, Umoja wa mataifa ulilitangaza

eneo la sasa la Israeli kuwa taifa jipya la Waisraeli waliopo duniani kote waliotawanywa na tukio la holocaust. Mauaji hayo ya Kimbari waliotendewa Waisraeli yalikuwa kama nishati ya kisiasa iliyosaidia sana kutekeleza jambo hili. Tangazo hilo la umoja wa mataifa lilifanywa bila kuwajali kabisa wale ambao tayari walikuwa wakiishi katika eneo hilo, yaani Wapalestina. Ninajua kuwa jambo hili lilisababisha matatizo lakini Israeli ilizidisha moto wa matatizo zaidi katika vita vya siku 6 ya mwaka 1969, (au mgogoro kati yake na Misri) kwa kulipanua eneo lao zaidi ya lile lililokuwa limedhaminiwa na Marekani. Ninaamini kuwa, hatua ya awali ya umoja wa mataifa haikuwa halali na kwamba tabia ya Israeli ya kujitanua, huku ikiimarisha ulinzi wao dhidi ya Misri, lilikuwa jaribio la kujipatia ardhi kubwa zaidi. Katika maisha yangu yote nimefundishwa na baba kuwa bila shaka uundwaji wa taifa la Israeli lilikuwa ni kosa la dhahiri kabisa.
Naye shahidi wa tatu Kazy Experimental anasema:

9
Hilo linategemea na jinsi unavyouchukulia ukweli. Kuna waandishi wa historia wanaodai kuwa mawazo yao ndio ukweli. Ninafahamu kuwa kamwe Palestina haijawahi kuwa taifa lenye mamlaka/ utawala (sovereign nation). Wao ni mabaki ya ufalme na himaya ya Uthmaniyya. Ninajua kwamba Uingereza ilikuwa na mkono wake katika uundwaji wa taifa la Israeli baada ya kulitwaa eneo lijulikanalo sasa kama Israeli. Ninajua kwamba kuna matumizi ya nguvu kwa pande zote mbili za mgogoro, hakuna yeyote anayeridhishwa na mwenzake. Kwa kuwa Marekani iliunga mkono na kusaidia uundaji wa Israeli, na kama rafiki, tunalazimika na kuwajibika kuhakikisha kuwa Waisraeli wanaishi na kuendelea kuwa salama. Ninahisi kuwa mgogoro huu unaweza kutatuliwa kwa njia ya kidiplomasia iwapo Yassir na bunge la Israeli wakibadilishwa na wakaja watu ambao wanataka kujadiliana kwa haki na usawa. Kikwazo kimoja ninachokiona kwa Israeli ni kwamba kuna makundi mengi sana yanayotakiwa kujadiliana nayo, kila kundi moja lina matakwa yake binafsi. Kama makubaliano yakifanywa na chama kimoja kunakuwa hakuna ulinzi dhidi ya mashambulizi kutoka kwa makundi mengine
Jibu la shahidi wa nne aitwaye Peter lilikuwa kama ifuatavyo: Nikiwa kama Myahudi ambaye siku zote huenda katika shule ya Kiyahudi, kile

nilichojifunza shuleni kimeyumbishwa sana. Lakini ninachojua kwa hakika ni kwamba Wayahudi na Wapalestina wote waliahidiwa ardhi hiyo na utawala wa Kiingereza na pindi utawala huo ulipokwenda kukabidhi eneo hilo ukatokea mgawanyiko baina ya Wayahudi na Wapalestina. Kisha ni katika vita vya siku sita ambapo kwamba Waisraeli walilitwaa eneo hilo .
Naye shahidi wa tano James akasema: Kuhusu vita vya Waarabu na Waisraeli, ninajua kwamba Waarabu ndio walioanzisha kila

mapambano na jeshi la Kiisraeli lilishinda kila wakati. Ninajua kuwa kila eneo

10
linaloshikiliwa na serikali ya Israeli lilinyakuliwa baada ya kushinda vita vilivyoanzishwa na Waarabu.
Shahidi wa sita Jacob kijana kutoka Canada- ana maoni yafuatayo: Kwa mujibu wa Biblia Wapalestina ndio waliokuwa wa mwanzo kuishi katika eneo hilo na

kisha Waisraeli wakalitwaa kutoka kwa wapagani.


Ama kwa upande wa Lisly, alipoulizwa juu ya anachokifahamu kuhusu historia ya Palestina, jibu lake lilikuwa katika sentensi fupi ambayo inajiosheleza kuliko mamia ya kurasa, pale aliposema: Sijui chochote. Sasa tuigeukie misimamo hiyo ya vijana ambao wametoa maoni yao kwa uhuru mkubwa, na sasa tumuelekee shahidi wa kwanza, Bi. Clara, ambaye amesema kwamba anaijua historia ya Palestina zaidi ya Wamarekani wengine, ambao wanajua tu matukio yaliyotokea wakati wa uanzishwaji wa Umoja wa Mataifa, wakati ambapo ufahamu wake wa matukio unaanzia kwenye mwaka 1890. Kuhusu nukta hiyo, ningependa kuonesha kuwa Bi.Clara amekiri kwamba Wamarekani hawajui chochote kuhusu historia ya eneo la Arabia, kwani Wamarekani wengi hawayajui matukio yaliyotokea katika kipindi cha kabla ya uanzishaji wa Israeli, kana kwamba eneo hili halina historia ya kabla ya kipindi hicho, au kwamba ardhi hii haikuwa na wakazi kabla ya Israeli kusimikwa mahali hapo. Hata Bi. Clara mwenyewe, maarifa yake kuhusu eneo hili ni mafinyu yenye mpaka, kwani Palestina ina mji mkongwe zaidi kujengwa duniani ambao ni Ariha uliojengwa zaidi ya miaka 7000 iliyopita. Kinachovuta hisia zetu ni kwamba, kwa Wamarekani wengi, mwanzo wa historia ya Palestina unadhibitiwa na uwepo wa Israeli!! Kwa hakika hili linaonesha ni kwa kiasi gani uundaji matukio unaofanywa na Israeli ulivyoliathiri taifa la Marekani. Kwani waisraeli hawataki ulimwengu ugeuke nyuma na kuitazama historia ya eneo la Mashariki ya Kati kabla ya uanzishwaji wa

11
taifa la Kizayuni, wanataka watu watosheke na kuiangalia historia ya kipindi cha baada ya tangazo la kusimikwa kwa taifa hilo hadi wakati huu, na kwa hakika wamefanikiwa kufanya hivyo. Historia ya Palestina inatandaa maelfu ya miaka mingi iliyopita, na wala haianzii pale ulipoanzishwa Umoja wa Mataifa au mwaka 1890. Kitabu hiki kimewekwa maalumu kwa ajili ya kuifichua historia hii iliyotiwa giza. Bi.Clara ameelezea hati/azimio la Balfour, lililoipa nguvu Uingereza kuiachia Palestina mikononi kwa Wayahudi, ili kwamba watangaze taifa lao kupitia nguvu hiyo. Tutaizungumzia hati hiyo ili kwamba Wamarekani na ulimwengu mzima wajue namna mgogoro wa Waarabu na Waisraeli ulivyoibuka katika eneo hili la Mashariki ya Kati, na jinsi uvamizi wa Uingereza ulivyoifuja ardhi ya Palestina na kuwapa Wayahudi katika namna ya kikatili na bila kuwafikiria na kuwaangalia wamiliki halali wa ardhi hiyo. Tukihamia kwa shahidi wa pili ambaye ni Bw. George, tunagundua kwamba ameonesha kuifikiria na kuizingatia historia muhimu ya mashariki ya Kati. Ameanza kujibu kwa kusema ninajua, na ameonekana kuwa na uhakika wa kile anachokifahamau na kukielewa, kwani ni kweli kuwa kadhia ya kuitoa sadaka ardhi ya Palestina na kuwakabidhi Wayahudi ilitokea baada ya machafuko ya vita vya 1 vya dunia, na suala la uhamiaji wa Wayahudi kwenda Palestina lilionekana likiongezeka kidogokidogo tangu wakati huo. George anasema kwamba anajua kuwa Wayahudi walikuwa wametapakaa na kutawanyika sehemu mbalimbali za dunia na hawakuwa na utaifa wa kuwaunganisha, jambo ambalo ni la kweli, kisha wakahamia Palestina ili kuanzisha taifa lao, ambapo walipewa baadhi ya vipande vya ardhi ya Palestina walivyovitwaa na kisha kuvipa jina la Israeli. Tukienda mbele zaidi, kutokana na uelewa wake George anakubali kuwa Wapalestina ndio walioanza kuishi katika eneo hilo, kwa kuzingatia kuwa Wayahudi walikuwa ni watu waliotawanyika, na kwamba Palestina ni eneo la Waarabu lililokuwa likikaliwa na Wapalestina.

12
Kisha anaendelea kwa kusema kuwa chanzo cha matatizo yaliyoibuka katika eneo hilo yanatokana na uwepo wa Wayahudi katika eneo hilo la Arabia, pamoja na uanzishwaji wa Israeli kwa gharama ya wenyeji asilia wa ardhi hiyo. Zaidi ya hapo ni kuwa Israeli ilizidisha moto wa matatizo baada ya vita vya siku sita pale ilipozipokonya na kuzitwaa ardhi za Waarabu. Inastahili kutaja hapa kuwa George hakuwa muwazi katika kuainisha tarehe hasa ya kuzuka kwa vita hivi vilivyotokea mwaka 1967 badala ya 1969 kama alivyosema. Bila kuangalia jambo hili, msimamo wa George ni sahihi, licha ya ukweli kwamba hakutoa ufafanuzi wowote. Ni hakika kuwa uwepo wa Israeli katika eneo hili ndio chanzo cha msukosuko na shida zote ambazo zimeendelea kuiumiza Mashariki ya Kati tangu wakati huo, na matatizo hayo hayatokoma hadi pale Palestina itakaporudi katika hali iliyokuwa nayo kabla ya hati ya Balfour. Kwa maana kwamba ardhi hiyo irudishwe kwa wenyeji wake na Wayahudi warudi kule walikotoka. Akiendelea zaidi, amesema kuwa hatua ya Israeli kuzivamia ardhi za Waarabu ndio iliyoifanya itafute dhamana ya uslama wake, jambo ambalo ni kweli, kwa sababu inawezekanaje Israeli izinyakue ardhi za nchi jirani halafu itamani kuishi kwa amani bila ya nchi hizo kujaribu kuzirudisha ardhi zao zilizopokonywa? Kisha Mmarekani huyo anahitimisha jawabu lake kwa kuyataja mawazo ya baba yake aliyekuwa amemwambia kuwa hatua ya uanzishaji wa taifa la Israeli ilifanywa kimakosa. Kwa hakika msimamo huo unaoafikiana na msimamo wa maelfu ya Waislamu na wale wasiokuwa waislamu ulimwenguni kote, unaonesha utambuzi na ufahamu wa baba yake George. Bila shaka utambuzi huo unatokana na yeye kushuhudia usimikwaji huo wa taifa la Kizayuni, na akaona jinsi Wapalestina walivyolazimishwa kuziacha ardhi zao kwa ajili ya wahamiaji waliotoka katika kila upande wa dunia. Unyanganyi huo hakuna Mwarabu anayeweza kuukubali, kwa hiyo Waarabu wanataka kukirejesha kile walichopokonywa, hii ikimaanisha kutokuwepo kwa usalama na amani ambayo watu wengi katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu wanasadiki kuwa abadan haitotengamaa ila pale uwepo wa Israeli utakapowekewa kikomo.

13
Ama shahidi wa tatu, Kazy Experimental, yeye alianza kwa kuibua na kuonesha shaka juu ya ukweli hasa ulivyo, hususan kutokana na kuwepo kwa wanahistoria waovu wanaogeuza ukweli. Ni kweli kuwa shaka hiyo inaweza kuandaa njia ya kuujua ukweli, kwa sababu hajafikiria msimamo maalumu, lakini wakati huo huo bado ametulia tu, kwani haonekani kuhama kutoka kwenye hali ya shaka na kujaribu kuingia ndani zaidi ili kupata maelezo yanayoweza kumfikisha kwenye hatua ya kuujua ukweli. Bila shaka kuna watu ambao wanajaribu kuharibu mambo na kuupotosha ukweli. Watu hao tutawataja katika hiki kitabu. Lakini Kazy na wale wenye mawazo kama yake wanatakiwa kujua kuwa ukweli unaweza kupotoshwa dhidi ya yule asiyeujua, lakini yule anayejua habari zote zinazoanzia nyuma kwenye mamia au maelfu ya miaka iliyopita kamwe hawezi kudanganywa na ukweli uliopotoshwa. Kwa kuwa umma wa Marekani halijui chochote kuhusu historia ya eneo hili zaidi ya historia ya uanzishwaji wa Israeli, hili linaonesha jinsi gani Mmarekani anavyostahili kudanganywa kuhusu jambo hilo, na kuangukia kirahisi kabisa katika mtego wa wanahistoria wadanganyifu. Kwa upande mwingine, umma wa Kiarabu, ambao umeishi katika eneo la Mashariki ya Kati kwa muda wa maelfu ya miaka, kamwe umma huo hauwezi kudanganywa, kwa sababu unaujua ukweli wote kwa kila nukta ndogo ya maelezo, kwa sababu unaishi katika ukweli huu. Kazy anasema kuwa anajua kwamba Palestina haijawahi kushuhudia utulivu na uthabiti katika historia yake yote na kwamba ndipo walipozaliwa WaUthmaniyya. Hakika hizo taarifa sio za kweli hata kidogo. Kwanza, ni kweli kuwa Palestina ilipitia katika vita mbalimbali, lakini kwa upande mwingine ilishuhudia vipindi vingi vya amani na ustawi, kwani muda wote hatupaswi kusimama tu kwenye kipengele hasi, hata kama hali hiyo ilikuwapo. Pili, Palestina sio sehemu ya asili ya WaUthmaniyya, kwa sababu historia ya eneo hili inaanzia nyuma zaidi kwenye maelfu ya miaka kabla ya WaUthmaniyya hao kujulikana. Aidha, Palestina imekuwa ikitawaliwa na nchi mbalimbali ambazo tutazitaja katika kitabu hiki.

14
Akiendelea zaidi, Kazy anakiri na kukubali kuwa Uingereza iliyavamia maeneo ya Palestina, na baadaye kuyakabidhi kwa Wayahudi ili waanzishe taifa lao hapo! Je hii haitoshi kwa Wamarekani kujua kwamba Wapalestina wana haki ya kuitetea ardhi yao na kuirejesha mikononi mwao, baada ya Uingereza kuitoa zawadi kwa Wayahudi, kwa nguvu ya azimio la Balfour ambalo halikuzingatia hisia za kizalendo za wenye ardhi, kuwanyanyapaa na kufumbia macho haki yao ya kuamua mustakbali wao? Kitu kinachoshangaza ni kwamba, baada ya kukiri suala hili, anadai kuwa matumizi ya nguvu huko Palestina yanachukuliwa kuwa yasiyo ya haki kwa pande zote mbili. Inawezekanaje iwe hivyo, hali ya kuwa kuna mnyangganyi na yule ambaye ardhi yake imeporwa na kunyakuliwa? Je, sio haki kwa aliyenyanganywa kuitetea ardhi yake na kuirejesha katika himaya yake? Au hata haki yake imekuwa mali ya yule anayemshambulia, akaipora ardhi yake, akayabomoa makazi yake na kuiangamiza familia yake? Wamarekani wanatakiwa kuzingatia kuwa wenyeji wa ardhi hiyo wanastahili kufanya juhudi ya kuirejesha ardhi yao, na kwamba kila mwenye kuitwaa kimabavu ni dhalimu. Huwenda msimamo wa Kazy ni wa ajabu sana, kwa sababu haukubaliani na mantiki, au tunaweza kuuita kuwa usiokuwa wa haki, kwani amekiri na kukubali nafasi ya Marekani katika kuianzisha Israeli. Aidha, anaona kuwa ni jukumu la Marekani kuhakikisha taifa hilo linaendelea kuwepo ingawa ni taifa la kivamizi lililonyanganya ardhi za Waarabu!! Je hiyo yaweza kuitwa haki? Kama msimamo huu ungefika katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, ungepelekea kwenye mgogoro wenye uhasama mkubwa, kwani Waislamu wangeuona kuwa ni ubaguzi, dhulma, na wenye kudharau hisia zao za kizalendo. Hivyo basi, ninamsihi kila Mmarekani mwenye utashi huru awe na fikra isiyoegemea upande wowote, isiyokuwa ya kibaguzi, na ajibu suali lifuatalo kwa uadilifu pasipo kupendelea upande wowote: je ni haki kwamba nchi kubwa ifanye kazi ya kuwasaidia wageni kuitwaa ardhi ya Wapalestina, kuwafukuza, kuyabomoa makazi yao na kuwaangamiza watoto

15
wao? Na je ni haki kuwapa jina la ugaidi pale wanapoitetea ardhi yao? Je ni haki kuwa Marekani haitakiwi kubakisha chochote katika kutoa dhamana ya uslama wa Wayahudi na uwepo wao katika ardhi isyokuwa yao? Ardhi ambayo wamehamia kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na hivyo kuwatupa nje wakazi wake? Je huo ni uadilifu na haki? Wamarekani wote wanatakiwa kujua kuwa Waarabu wote, Waislamu kwa Wakristo, wanakubaliana juu ya ukweli mmoja, kwamba Israeli ni mvamizi, na kwamba Waarabu wana haki ya kupambana na mvamizi huyo, hivyo kila shari anayoifanya huyo mvamizi haiwezi kuitwa kuwa ni haki yake, na hakuna nchi ya nje yenye haki ya kuunga mkono shari hiyo. Kwa hivyo, hiyo ndio sababu ya makinzano yaliyopo kati ya Waarabu / Waislamu kwa upande mmoja na Marekani ambayo inaona kuwa ni lazima kwa taifa hilo liendelee kusimikwa katika ardhi ya Waarabu. Kazy anaendelea kusema kuwa mgogoro wa Mashariki ya Kati baina ya Wapalestina/ Waarabu kwa upande mmoja na Waisraeli kwa upande wa pili, unaweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia pale tu mamlaka za Palestina na Israeli zitakapobadilishwa kwa kuja mamlaka zenye bidii na azma. Alizungumzia hata suala la kufanyika mazungumzo ya haki na uadilifu ! Hapa ni muhimu niwawekee wazi Wamarekani juu ya nukta kadhaa : Kwanza, kwamba Waarabu wanawaona Wayahudi kama wanyanganyi wa ardhi zao, sasa itakuwaje wafanye mazungumzo na mwizi ? Mpenzi msomaji, jaribu kutafakari pamoja nami, kwamba mtu ameiba gari lako kisha baada ya kupambana naye anakwambia tuzungumze kwa namna ya uadilifu na usawa ili kumaliza vita hivi ambavyo

vimedhoofisha nguvu zetu na kusababisha uhasama na uadui miongoni mwetu. Kisha


mwizi huyo anajitokeza mbele ya watu kama mtu wa amani na mwanaminifu anayefanya juhudi za kutaka majadiliano na amani pamoja nawe, huku katika vipengele vya majadiliano yenu akiwa hajaingiza kipengele kinachohusu kulirejesha gari alilokuibia. Kwa maneno mengine, hana tofauti na mtu mwoga anayetaka kujadiliana nawe ili kumaliza mgogoro uliopo baina yenu kwa kuhofia lile linaloweza kumpata, lakini wakati huo huo

16
hana nia ya kukurudishia gari lako, na hivyo anajivika sura ya mtu asiyekuwa na madhara kwako, mtaka amani, lakini unapozungumzia kuhusu gari lako, anakwambia mimi je, sina haki ya kumiliki gari ? Kwa hakika hivyo ndivyo Wayahudi wanavyofanya. Wanasema sisi je ? Hatuna haki ya kumiliki ardhi na kuanzisha taifa letu mahali hapo ? Wameichagua ardhi ya Wapalestina. Ni uadilifu gani huo anaouzungumzia Kazy ? Kwa sababu Wapalestina na waarabu wanaona kwamba hakuna eneo kwa ajili ya mazungumzo ya haki na Waisraeli, ispokuwa kama mazungumzo hayo yatajumuisha kipengele cha Wayahudi kurejea walikotoka, na kuwarejeshea Wapalestina ardhi zote zilizoibwa. Hiyo ni nukta ya kwanza. Nukta ya pili inahusu njia za kukomesha mgogoro baina ya Waisraeli na Wapalestina. Katika hili, Wamarekani na dunia kwa ujmula- wanatakiwa kutambua kwamba mgogoro huu haitomalizwa kwa kutumia tu njia ya mazungumzo, bali kwa kuzirejesha ardhi husika kwa wenye nazo, na kuwarejesha Wayahudi mahali walipotoka, na hilo linajumuisha uthibitisho wa Waarabu na Waislamu wote. Lakini kinachoonekana sasa ni kwamba vyombo vya habari na wanasiasa wa Kimagharibi wanawasilisha kitu tofauti kabisa, ili kuwashawishi wakazi wa Magharibi kwamba suluhisho linapatikana katika mazungumzo yasiyoligusa suala muhimu la kuzirejesha ardhi kwa wamiliki wake wa halali, kisha wanamuelezea yule anayekataa pendekezo hilo kwamba ni kikwazo katika njia ya kuelekea kwenye amani. Kwa hakika, kama ilivyokuwa katika kesi ya gari lililoibwa, ambapo mtu wa tatu anaingilia kati ya mnyanganyi na aliyenyangnywa, akiwaambia kuwa wanatakiwa kuzungumza ili kusimamisha mapigano, na kwamba suluhisho pekee ni kusimamisha mapigano na sio kurejesha gari, yule anayelikataa pendekezo kama hilo anachukuliwa kuwa ni mtu asiye mwadilifu na kizuizi kwenye njia ya kuelekea kwenye amani. Pendekezo kama hilo linaweza kumpa faida mnyanganyi peke yake, kwani ataepuka kwakutoguswa na madai na vitisho vya aliyenyanganywa. Lakini kwa upande wa aliyenyanganywa, akikubaliana na mazungumzo hayo yasiyokuwa ya

17
haki, amabyo yanaishia tu kusimamisha mapigano, atakuwa ametoa mkono wa kwaheri dhidi ya haki zake na hatothubutu tena kudai gari lake. Kwa hiyo, Wamarekani wanapaswa kuitambua nukta hii ya msingi na yenye mantiki kubwa. Aidha, vyombo vya habari vya Marekani na Magharibi vimekwenda mbali zaidi katika kuwaita Wapalestina kuwa ni waonevu, na kwamba hawataki amani kwa sababu wanakataa mazungumzo yasiyokuwa ya haki ambayo yanawafanya waache kudai haki zao. Kisha Kazy anaendelea kuutetea msiamamo wa Israeli kwa kusema kwamba, mgogoro uliopo katika mchakato wa amani unatokana na kuwepo kwa taasisi nyingi za Kipalestina. Katika hili, Wamarekani wanatakiwa kutambua kuwa Israeli katika macho ya Wapalestina, Waarabu na waislamu wote haina tofauti na mvamizi, ambaye hana haki yoyote anayopaswa kudai katika ardhi hizi. Kwa hiyo, hakuna mtu anayepaswa kuutetea msimamo wa Wayahudi, kwa sababu bila kuangalia jinsi uadilifu unavyoweza kutazamwa na watu wengine, siku zote watu wa eneo hili hawatendewi haki, na mwisho wa yote Wayahudi ni wavamizi na wanyanganyi. Hiyo ni nukta moja. Kwa upande mwingine, makundi mbalimbali ya Kipalestina yanaona kwamba yana haki ya kuhakikisha upatikanaji wa amani ya haki, ambayo itahakikisha haki zao zinarejeshwa. Aidha, Mamlaka ya Kipalestina ndio mwakilishi rasmi wa taifa la Wapalestina, na ndio taasisi pekee inayowawakilisha katika mazungumzo. Kwa kuwa Israeli haizungumzi na na Hamas au Jeshi la Mashahidi wa Al - Aqsa (Al-Aqsa Martyrs Regiments), makundi hayo yanaona kwamba yana haki ya kuhakikisha kuwa mazungumzo yanakuwa ya haki, tukizingatia kuwa yanawakilisha maelfu ya wapalestina. Tumeshasema tangu awali kuwa mazungumzo yasiyohusisha urejeshaji wa haki za wapalestina yanaonekana machoni mwao kuwa mazungumzo yasiyokuwa ya haki, na hivyo hawatoyastahmilia, na huo ndio msimamo wa makundi haya ya ukombozi. Na sasa twende kwa shahidi wa nne Peter, kijana wa Kimarekani mwenye asili ya kiyahudi, ambaye amekiri wazi wazi kuwa alisoma katika shule ya Kiyahudi kwa sababu

18
yeye ni Myahudi na huko alijifunza vitu ambavyo sio haki hata kidogo, jambo ambalo lilitarajiwa kuwa hivyo. Wayahudi wanatumia nguvu kubwa duniani kote kuwaelezea Wapalestina kwa sifa mbaya, jambo linaloamsha chuki za Wayahudi na kuwachochea kufanya maangamizi dhidi ya Wapalestina, na hivyo husafiri mpaka Israeli kwenda kupigana nao. Hakuna shaka kuwa, shule za Kiyahudi ulimwenguni kote zitatumika kupotosha ukweli wa kihistoria kwa lengo la kuwafanya wayahudi kuwa wamiliki wa ardhi hiyo, na kuwahadaa waamini kuwa palestina ilikuwa eneo lisilokuwa na watu / wakazi, na kwamba wao (Wayahudi) ndio taifa lililoteuliwa na Mungu! Na hili ni jawabu kwa Kazy aliyedai kuwa kuna waandishi wa uongo wa historia, jambo ambalo ni kweli, lakini yatakiwa kuongezwa hapa kwamba hao waandishi wa uongo na waumuaji wa mambo hawapo katika upande wa Waarabu ambao wameihifadhi historia ya ardhi yao, bali hao waaandishi wa uongo ni Wayahudi ambao ni wageni katika ardhi hii, na ambao wanataka kuitumia historia kwa namna yoyote ili kuvifanya vizazi vijavyo ulimwenguni viamini kuwa wao wana asili ya ardhi hii tangu zamani. Peter anasema kuwa anajua vema kwamba Uingereza iliwaahidi Wapalestina na Wayahudi kwa pamoja kuwapa ardhi hii (Palestina), jambo ambalo ni kosa kubwa na ni taarifa zisizokuwa na ukweli, ambazo tutaelezea uongo wake katika kurasa za baadaye. Lakini Peter na kila mtu anatakiwa atambue kuwa Uingereza ilikuwa imeahidi kuitoa ardhi hii kwa Wayahudi tu, kama ilivyo katika Azimio maarufu la Balfour ambalo liliitoa sadaka ardhi ya Wapalestina na kuwapa Wayahudi. Ama kuhusu Wapalestina, wamekuwa wakiishi hapo kwa zaidi ya miaka mia tano, lakini walitaka kujikomboa dhidi ya utawala wa KiUthmaniyya uliokuwa umezama katika lidi la uovu na ufisadi katika siku za mwisho za udhibiti wake, na hivyo Uingereza ikaahidi kuwasaidia kujikomboa dhidi ya utawala wa KiUthmaniyya ambao ulikuwa umeungana na Ujerumani katika kuapmbana na Uingereza. Tukichukulia kwamba (Wapalestina) waliwaunga mkono (Waingereza), lakini Uingereza haikutekeleza ahadi yake na badala yake ikawasaliti Wapalestina ambao walipambana katika safu za mbele za

19
majeshi yao, na badala yake wakawalipa fadhila kwa kuitoa sadaka ardhi yao kwa Wayahudi, amabo ni wageni katika eneo hili. Kisha Peter anasema kuwa Uingereza iliigawa ardhi hii na kuwapa Wayahudi eneo lao na Wapalestina nao wakapewa eneo lao, kana kwamba ni kipande cha halua, lakini hili nalo pia halikutokea hata kidogo, kwa sababu Uingereza iliitoa ardhi ya Wapalestina na kuwapa Wayahudi, ardhi ambayo muda wote ilikuwa mali ya Wapalestina, lakini Uiingereza ikaitwaa kwa nguvu na kuitoa sadaka kwa wayahudi, ikalitambua taifa lao na kutolitambua taifa la Kipalestina. Kisha Peter anaendelea kusema kwamba Israeli iliichukua ardhi takatifu ya Wayahudi wakati wa vita vya siku sita!! Kwa kweli sijui ni ipi ardhi takatifu ya Wayahudi anayoizungumzia, kwa sababu hapakuwepo na ardhi hiyo takatifu katika nchi ya Palestina, kwani Nabii Musa (a.s.) hakuwahi hata kuingia Palestina, na alikufa kabla ya kuingia. Inaonekana kwamba Peter ameathiriwa na taarifa alizozipata katika shule ya Kiyahudi, taarifa alizosema tangu mwanzo wa jawabu lake kwamba hazikuwa za haki. Lakini kama alikusudia ukuta wa kiislamu wa Al-Buraaq (Islamic Al-Buraq wall), ambao kwa sasa upo chini ya uvamizi wa Kizayuni na kisha (baada ya uvamizi) wakauita Ukuta wa Maombolezo (Wailing Wall), kitabu hiki kina ushahidi unaothibitisha kwamba mara zote Umoja Wa Mataifa umesisitiza kuwa ukuta wa Al-Buraq ni alama ya Kiislamu (Islamic landmark), na hauhusiani kabisa na maeneo matakatifu ya Kiyahudi. Aidha, Umoja wa mataifa umefanya utafiti wa muda mrefu juu ya suala hili na kufikia hitimisho kuwa ukuta wa Al-Buraq ni alama ya Kiislamu. Hata hivyo, wayahudi waliutwaa kwa nguvu katika kipindi hicho. Lakini ulimwengu umeipuuza ripoti hiyo ya umoja wa mataifa na kuukubali unyanganyi huo wa wazi licha ya kwamba ni uhalifu dhidi ya Waislamu. Tukija kwa shahidi wa tano ambaye ni James, anasema kwamba mara zote Waarabu ndio waliokuwa wa kwanza kuanzisha vita, lakini mara zote Waisraeli ndio waliokuwa washindi. Huu ni uongo mkubwa!! Inaonekana kuwa mtazamo huo ni matokeo ya vyombo

20
vya habari vya Kiisraeli vyenye nguvu kubwa nchini marekani. Vyombo hivyo vya habari vinafanya kazi ya kutia chumvi dhana ya hadithi isiyoonekana ya jeshi la Israeli. Wote tumeshuhudia katika televisheni mwanajeshi wa Kiisraeli mwenye silaha nzito akimkimbia mtoto (wa Kipalestina) mwenye umri wa miaka kumi na moja aliyekuwa akimtupia mawe, jambo lililoishtua Israeli baada ya kutangazwa kwake na ikaelezea hadhari yake kuhusu utoaji wa picha hiyo kwenye uwanda mpana, jambo ambalo lililifanya jeshi la Israeli lidhihakiwe na kuchekwa. Kwa upande mwingine, athari ya propaganda za Kiisraeli zinaonekana katika msimamo wa james, aliyewaita Waarabu kuwa ni waoga, wagomvi, washari na maneno mengine yachukizayo, ambayo Hollywood imeyajaza katika akili za watu. Kwani James anafikiri kwamba siku zote Waarabu ndio wanaoanzisha vita, lakini siku zote majeshi ya Israeli yamekuwa yakishinda, dhana ambayo haina ukweli kabisa. Zaidi ya yote, James na watu wote wa Magharibi wanatakiwa kutambua kwamba Wayahudi ndio walioanzisha uadui. Tutauelezea sifa za uadui huo katika sura ya nne, ambapo taasisi za kigaidi ziliiteka Palestina na kuiharibu. Walifanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina ili kueneza hofu miongoni mwao na kuwalazimisha kuvihama vijiji na mali zao ili kuwaachia wageni. Ni mauaji ya kimbari yaliyotendwa dhidi ya Wapalestina ndiyo yaliyowalazimisha Waarabu kuingilia kati ili kuwalinda Wapalestina baada ya ulimwengu kuwa baridi na kutochukua hatua yoyote na kuonekana kana kwamba ulimwengu huo ulikuwa umekula njama dhidi ya Wapalestina. Inaonekana kuwa kitu pekee anachokikumbuka James ni Waarabu kushindwa katika vita ya siku sita, lakini amejiweka katika kusahau kwamba mwaka 1973 majeshi ya Waarabu yalikaribia kuifuta Israeli katika ardhi ya Palestina lau kama si Marekani kuingilia kati na kulazimisha kufanya mapatano ya amani kwa muda, ambapo Marekani ilikitumia kipindi hicho cha amani ya muda kuwapelekea Waisraeli msaada wa silaha na zana mbalimbali. Sio hilo tu, bali iliwapatia wataalamu, zana na mitambo ya hali ya juu, na kuwapatia taarifa za siri na za maana ambazo zilisaidia sana wakati wa mapambano yao. Hivyo

21
ndivyo Marekani ilivyovunja makubaliano hayo ya amani iliowashurutisha Waarabu na kutuama juu ya uwezo wa nguvu zake. Lakini James hakumbuki lolote katika matukio haya, na simlaumu kwa sababu inaonekana fikra zake zimeelekezwa katika kuyatumikia maslahi ya Kizayuni bila kujitambua. Zaidi ya hayo, ardhi zilizopo chini ya udhibiti wa Israeli hazikutwaliwa kama James anavyovikiria, bali ni ardhi za Wapalestina zilizokuwa chini ya udhibiti wa utawala wa Kiingereza uliodai kuwa ungewasaidia kujikomboa dhidi ya mamlaka ya utawala wa KiUthmaniyya, lakini ilipoingia katika ardhi hizo ilivunja makubaliano yote iliyoyafanya na Wapalestina na kuitoa ardhi hiyo na kuwapatia Wayahudi pamoja na kuwaunga mkono kwa kuwaopa silaha na mafunzo ya kijeshi ili wawe imara kama nilivyotangulia kusema. Tukitoa maoni kuhusu mawazo ya Jacob, ambaye ni mtu pekee aliyeegemeza mawazo yake kwenye ushahidi wa Kihistoria, yaani Biblia. Yafaa tueleze hapa kwamba Quran Tukufu nayo pia imesimulia visa mbalimbali kuhusu Palestina na majaribio ya Wayahudi kutaka kuingia humo, tangu enzi za Nabii Musa (a.s.). Huu ni ushahidi kwamba hii ardhi ni ya Wapalestina, na ushahidi wa Quran na Biblia vinatosha kuwafanya waumini wote waridhike na kukinaika kwamba Palestina ni ya Wapalestina tu. Tuchukulie mathalan kwamba Wayahudi ndio walioanza kuishi eneo hilo, je hiyo itawapa haki ya kulidai tena baada ya miaka mingi kupita, na baada Wapalestina kuishi hapo kwa kipindi chote hicho ambacho Wayahudi walikuwa wametawanyika ulimwenguni kote, hali ya kuwa Wapalestina ndio walioikinga na uvamizi na vita zote na kuilowesha ardhi yake kwa damu zao kwa kipindi cha miaka yote hiyo? Au Wapalestina hao walikuwa tu walinzi wa ardhi hii, wakiilinda kwa damu zao, wakiwatoa muhanga watoto wao kwa ajili yake, wakiwasubiri Wayahudi waje mwishoni na kuichukua kwa mabavu, na kwa nguvu ya ugaidi, silaha na vitisho?

22
Wachache ndio wanaojua ukweli, na wengi hawajui chochote, na ushahidi wa hayo ni binti wa Kimarekani aitwaye Lisly aliyejibu swali letu kwa kusema sijui chochote. Jibu hilo linatosha kutupia mwanga kwenye sehemu ya wananchi wa Marekani ambao hawajui chochote kuhusu historia ya mgogoro unaoendelea nchini Palestina. Sasa ni kwa misingi upi maoni yao ya kisiasa yanaipendelea Israeli au Palestina? Bila kuangalia ni jinsi gani maamuzi ya haki ya eneo hili kuhusu palestina inavyoweza kuwa, bado maoni hayo yataendelea kukosa misingi sahihi ya kihistoria, misingi ambayo tutaifafanua katika kitabu hiki. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alisema: Kundi katika umma wangu litaendelea kuitii

dini na kupata ushindi kwa ajili yake, wakiwashinda maadui wao hawatodhuriwa (hata kidogo) na wale wanaowakimbia, isipokuwa kwa tabu watakayoipata mpaka amri ya Allah (Siku ya Mwisho) itakapokuja nao wakiwa katika hali hiyo Masahaba wakamuuliza: Ewe Mtume wa Allah! Wapo wapi? akasema: Baittul-Maqdis (Jerrusallem) na walio kandokando mwa Baitul-Maqdis...

Historia ya Palestina Ukweli wote kuhusu Historia ya Eneo la Arabia


Wakati Christopher Columbus alipogundua bara jipya lijulikanalo sasa kama Amerika, nchi za Kiarabu zilikuwa chini ya utawala wa dola kubwa la Kiislamu lililojulikana kama Ottoman empire na ambalo lilikuwa limepanua udhibiti wake kwenye ardhi na nchi zote za Kiarabu zinazojulika sasa hivi pamoja na mataifa mengine ya Kiislamu. Utawala huo ndio dola la mwisho la Kiislamu kulitawala eneo la Arabia, na hiyo ni kuanzia mwaka 1516 hadi 1918. Eneo la Arabia na Mashariki ya kati kwa ujumla vimeshuhudia kuibuka kwa serikali na himaya nyingi za Kiislamu zikifuatana moja baada ya nyingine katika ardhi yake kutokana na muda na mahali. Jedwali lifuatalo lililokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali, linaonesha muda wa serikali

23
hizo na maeneo yake ya kijografia tangu kudhihiri kwa Uislamu mpaka kuanzishwa kwa dola ya Othmania (Ottoman empire):

Utawala Mkahalifa Wanyoofu Makhalifa Wa Bani Umayyah Makhalifa Wa Bani Abbasi Utawala wa Idrisi Utawala wa Tuluni Ufalme wa Hamdani Fatimiyyiin

Kipindi cha kutawala 632 - 661 A.D. 611 750 A.D. 750 1259 A.D. 788 974 A.D. 868 905 A.D. 905 1004 A.D. 909 1171 A.D.

Eneo la utawala Peninsula ya Arabia + Bilad Al-Sham1[1] + Misri + Iraq na nchi nyingine kadhaa. Nchi zilizotajwa + kasikazini mwa Afrika+ eneo la Sind + kusini mwa Hispania na nchi nyingine Nchi nyingi zilizotajwa hapo juu ispokuwa Palestina. Morroco. Misri na Syria. Syria na Peninsula ya Arabia Kaskazini mwa Afrika +Misri+ Magharibi mwa Peninsula ya Arabia+ Bilad Al-Sham. Misri+ Palestina + Syria + nchi za Jirani. Katikati mwa Iraq.

Utawala wa 935 969 A.D. Ikhshidi Utawala wa 961 1150 A.D. Mazidyon /ufalme wa Zirid Utawala wa 990 1096 A.D. Aqlyoun Utawala wa 1032 1079 A.D. Mardisi Almoravid 1065 1147 A.D. Almohad 1130 1269 A.D. Ufalme wa 1169 1260 Ayyubi Ufalme wa 1196 1549 A.D. Marinid na Wattasid Ma-Hafsi 1228 1574 A.D.

Iraq + Peninsula + kaskazini mwa Syria. Halab na kaskazini mwa Syria Kaskazini mwa Afrika Kaskazini mwa Afrika Misri+ Yamen + Bilad Al-Sham. Morroco. Tunsia.

24
Utawala wa 1250 1517 A.D. Misri + Bilad Al-Sham + Magharibi mwa Peninsula Mamaalik ya Arabia. Masultani wa Ki- 1281 1924 A.D. Waliziunganisha nchi zote za Kiarabu chini ya Uthmaniyya himaya moja.

Tanbihi: jedwali hili linataja baadhi ya nchi muhimu zaidi zilizotawaliwa na tawala
zilizotajwa na sio zote. Jeduali hili linaonesha wazi uwezo na nguvu za nchi zilizoshirikiana au kushindana katika kulidhibiti eneo la Arabia, Mashariki ya Kati na eneo la Ghuba. Linabainisha wazi juu kutokuwepo kwa nguvu kutoka nje kuja kutawala katika maeneo hayo, hususan kile kijulikancho leo kama Israeli. Hakuna shaka kwamba Mashariki ya Kati imepewa hadhi kubwa kutokana na tunu zake za kiroho na kidini, kwani ndio eneo la asili ya dini na mitume mbalimbali. Aidha, eneo hilo linachukuliwa kuwa ndio njia panda ya kibishara (commercial crossroads), na lilikuwa ndio makutano ya mabara matatu muhimu kwa wakati huo: Uropa, Afrika na Asia. Hivyo eneo hilo lilishuhudia vita vingi vilivyoukumba umma wa Kiarabu kwa karne nyingi kutokana na tamaa na uvamizi kadhaa kutoka nje, pamoja na fitana na magomvi ya ndani yaliyosababisha tawala mbalimbali kudondoka na nyingine kuibuka kutoka kwenye vifusi vya tawala zilizoanguka, kama ilivyooneshwa katika jedwali la hapo juu. Hata hivyo, tamaa ya watu wa nje iliendelea kuwa mwiba mkali, hususan kwa majaribio ya mara kwa mara ya kutaka kuuangamiza utawala wa Kiislamu, kuukamata na kuzihodhi nchi na utajiri wake. Vita vya msalaba ni mojawapo ya uvamizi mbaya sana, ambapo eneo hili liliathiriwa sana na msiba mkubwa wa harakati za kijeshi, ya kwanza ikihamasishwa na Papa Urban II katika Clermont mnamo mwaka 1095. Mwanahistoria maarufu kutoka Ufaransa Foucher de Chartes alilizungumzia tukio hili katika kitabu chake Histoire du plerinage des Francs

Jrusalem, ambapo tunanukuu alichosema katika ukurasa wa 122: Vita hivi sio kwa

25
ajili ya kutwaa mji mmoja, bali kulichukua eneo zima la Asia pamoja na utajiri na hazina zake zote. Hivyo songeni mbele mpaka kwenye kaburi takatifu na muikomboe ardhi takatifu kutoka mikononi mwa wanyanganyi, na itwaeni na muifanye kuwa yenu, kwani kama isemavyo Torati ardhi hii inatoa asali na maziwa.
Miongoni mwa uvamizi mwingine uliowaumiza Waislamu katika kipindi hiki cha historia, ni uvamivi wa kuangamiza uliofanywa na Wamongoli na Watatar ambao waliuangusha utawala wa Bani Abbas mwaka 1258, wakauteketeza mji wa Baghdad, wakawaua zaidi ya watu laki 800 wa mji huo, majeshi yao yakazielekea nchi nyingine za Mashariki ya Kati wakieneza hofu katika ukanda wote ambapo Syria na Palestina ziliangukia mikononi mwao. Kisha kwa ushindani na ukinzani kati ya Ufaransa na Uingereza, ikiwa chini ya uongozi wa Napoleon Bonaparte Ufaransa ilianzisha kampeni dhidi ya Misri na Palestina mnamo 1897, ambapo aliinyakua miji mingi ya Kipalestina, akatekeleza mauaji ya kutisha ya zaidi ya mateka 12000 wa Kiarabu. Vita hivyo vya mwisho vilikuwa vibaya na vya kikatili mno, umwagaji mkubwa wa damu, vita mabavyo vilisababisha msiba na mateso kwa eneo la Arabia, vikitonesha vidonda vyake vilivyotokana na vita vya awali vilivyofanywa na uingereza na Ufaransa ambazo ziliuvunja umoja wa mataifa ya Kiislamu na kuyakalia kwa nguvu, wakawakalifisha wakazi wa maeneo hayo kufuata mifumo tofauti iliyokusudiwa kuharibu na kuvuruga tamaduni na mila za mataifa haya. Ili kujua ukatili uliofanywa na mvamizi huyo ambaye alileta mateso makali zaidi ya yale yaliyofanywa na Watatar chini ya kiongozi wao mvamizi Holako, yatosha kuzikumbusha akili zetu juu ya idadi kubwa ya waathirika wa ukaliaji kimabavu uliofanywa na ufaransa nchini Algeria, idadi iliyofikia mashahidi milioni moja na nusu.

Kulidhibiti Eneo la Arabia Na kuibuka Kwa Makoloni

26
Kutokana na idadi ya vita vilivyoyavunja mataifa ya Kiislamu na umma wa Kiarabu kwa ujumla, utawala wa kikoloni uliweza kuiangusha himaya ya Uthmaniyya na kuzifunga nguvu na ushawishi wake kidogo kidogo. Kisha pakafuatiwa na utiaji saini wa makubaliano ya Sykes-Picot kati ya Ufaransa na Uingereza mwaka 1916. Mataifa hayo yalikubaliana kuligawa eneo la Arabia katika vipande vidogovidogo vinavyoweza kudhibitiwa na kutawaliwa kwa urahisi, hivyo waliziweka Lebanon na Syria chini ya utawala wa kifaransa, Jordan na Iraq zikawa chini ya Mwingereza, huku Palestina ikibaki kuwa taifa dogo. Yote haya yalifanyika bila kujali hata kidogo mawazo ya wakazi wa eneo hili kana kwamba hawakujali mustakbali wa ardhi yao, au kana kwamba wakazi hao walikuwa ni watumwa wa mkoloni ambaye angewafanya atakavyo. Wakikabiliwa na mgawanyiko huu wa mataifa yao pamoja na ukaliaji usio halali dhidi ya nchi za Kiarabu, ilikuwa ni wajibu wa mataifa yaliyokuwa katika eneo hili kupambana ili kuziokoa ardhi za Waarabu kutoka kwa Uingereza na Ufaransa. Jedwali lifuatalo linaonyesha tarehe za uhuru wa mataifa haya kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika mtandao wa Umoja wa nchi za Kiarabu:

Nchi Jordan Oman Emirates Bahrain Comoro Qatar Tunisia Kuwait Algeria Lebanon Djibouti Libya Saudi Arabia Misri Syria Morocco Sudan Mauritania Somalia

Tarehe ya kupata Uhuru 25/5/1946 18/11/1950 2/12/1971 11/8/1971 06/ 07/1975 09/01/1971 20/03/1956 25/02/1961 05/07/1962 22/11/1946 11/08/1971 24/12/1951 23/09/1932 28/02/1922 17/04/1946 02/03/1956 01/01/1956 28/11/1960 01/07/1960

27
Yemen (kaskazini) Yemen (Kusini) Iraq Palestina 26/09/1962 1967 03/01/1932 Bado ipo chini ya utawala wa kizayuni

Jedwli hili linaonesha jinsi nchi za Kiarabu zilivyopata uhuru na kukomesha ukandamizaji na udhalimu wa wavamizi, isipokuwa Palestina inayoendelea kuathiriwa na mauaji na ukatili wa mkoloni ikiwa bado kupata uhuru wake. Wananchi wake walifukuzwa katika ardhi yao, wakaondolewa na kukimbilia katika nchi za jirani, wakati ambapo watu wengine, ambao ni wageni katika eneo hilo na ambao desturi na ada zao zinatofautiana moja kwa moja na watu wa eneo hili walisimikwa katika ardhi za wakazi hao. Waliingizwa na mkoloni wa Kiingereza kwa kutumia nguvu ya mtutu wa bunduki katika kulipa kisasi dhidi ya harakati za kudai uhuru zilizoyaweka huru mataifa ya Kiarabu na kuzinyanyua bendera za ushindi. Hivyo basi, ni muhimu kuelezea kisa kizima cha historia ya Palestina, ili kwamba kila mtu ajue jinsi ulimwengu ulivyofikia hatua hii ya fitna, ugomvi, vita, taharuki na mauaji ya kimbari. Palestina na Ukweli wa Kihistoria Ni rahisi kupata taarifa sahihi kuhusu historia ya Palestina zilizothibitishwa na vyanzo madhubuti, taarifa zinazorudi nyuma kwenye maelfu ya miaka hadi katika zama zetu, na hilo linawezekana kutokana na wingi wa vyanzo na tafiti mbalimbali zinazoambatana na historia hii. Sehemu muhimu zaidi ambayo imetunza taarifa hizo ni Mamlaka ya Palestina ambayo imechukua dhima hiyo ili kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinakuwa huru dhidi ya upotoshaji na uongo wa aina yoyote, na ili kwamba kizazi kijacho, wawe Wapalestina au la, wasije wakaisahau historia hii. Kwa msingi huo, kituo cha kitaifa cha taarifa za Kipalestina kikifanya kazi chini ya Taasisi kuu ya Habari, ambayo nayo ipo chini ya Mamlaka ya Palestina, kituo hicho kinatoa taarifa za kihistoria zinazoambatana na uhakiki na tafiti mbalimbali.

28
Palestina ya zamani Jina la Palestina: Tangu zamani Palestina ilikuwa ikijulikana kama ardhi ya Kanan, ambapo ilitajwa katika ripoti na taarifa za moja wa viongozi wa jeshi kwa Mfalme Mary. Aidha, jina hili limekutwa likiwa limeandikwa kwa ufasaha kabisa kwenye nguzo ya Adrimi, aliyekuwa mfalme wa Alkha (Tal Al-Atshenah) katika kipindi cha katikati mwa karne ya tano kabla ya Kristo. Asili ya neno Palestina, kama lilivyotajwa katika rekodi za Kiassyria wakati wa zama za mfalme wa Assyria (Addizary III) kwenye mwaka wa 800 B.C. linatokana na neno Philsta, ambapo mfalme huyo aliandika kwenye nguzo yake kwamba katika mwaka wa tano wa utawala wake, majeshi yake waliiweka Palastu chini ya udhibiti wake na kuwalazimisha watu wa eneo hilo kulipa kodi. Vilevile neno Palestina lilitajwa na Herodotus kwenye msingi wa Aramea, kama tunavyomkuta akilitumia kwa kuashiria eneo la upande wa kusini mwa Syria au (Syria ya Palestina) jirani na Finithya hadi kwenye mipaka ya Misri. Wakati huo huo, wanahistoria wa Kirumania, kama vile Agathar Chides, Strabo, na Diodoru walilitumia jina hilo. Katika zama za Romania (Romanian Era), jina la Palestina lilitumika kwenye ardhi yote takatifu, kisha likaendelezwa na kuwa jina rasmi la eneo hili tangu enzi za Hadrian, hivyo jina hili likastawi na kutumiwa na kila mtu katika kanisa la Kikristo, ambapo walilitumia sana katika ripoti na taarifa za hija za Kikristo. Kwa upande mwingine, Palestina ilitumika kama sehemu ya Bilad Al-Sham wakati wa enzi za himaya ya Kiislamu. Neema na baraka za ardhi ya palestina, pamoja na daraja yake adhim vimeendelea kuifanya kuwa sehemu ya kukalika tangu zama za kale, ambapo ilikuwa na duru kubwa katika kuunganisha tamadnuni za maeneo mbalimbali ya ulimwengu kutokana na sifa ya daraja yake kuu ambayo imeifanya itambulike kihistoria tangu zama za kale.

29
Zama za mawe Kwa mujibu wa ugunduzi wa taarifa za mambo ya kale, wanasayansi wamekubali kwamba mwanadamu aliishi katika ardhi ya Palestina, mtu huyo anajuliakana kama mtu mwenye kimo kirefu (man of erect stature). Watu hao wa zamani kimsingi walikuwa wawindaji waliosafiri katika kutafuta makundi ya wanyama. Ni muhimu kutaja hapa kuwa katika kipindi hicho binadamu huyo wa zamani alipitia katika awamu mbalimbali za kimaendeleo, ambapo alianza kuendeleza zana zake za uwindaji zilizokuwa zimetengenezwa kwa mawe. Katika awamu ya tatu ya Zama za Mawe, binadamu makini alidhihiri, ambapo kisu chenye ncha kali ndio iliyokuwa zana muhimu katika zama hizo. Mabaki ya binadamu huyo yaligunduliwa ndani ya mapango ya nchini Palestina. Mapango hayo ni kama vile pango la Al-Amira,Al-Ahmar,Al-Wad, Kubarah na maeneo mengine yaliyopo katika jangwa la Negev. Awamu hii inaashiria mwanzo wa mikusanyiko ya bianadamu iliyowakilisha muundo endelevu wa kijami, licha ya ukweli kwamba makundi hayo yaliendelea kuendesha maisha yake kwa uwindaji na kukusanya chakula. Kutoka kwenye mikusanyiko hadi kwenye uzalishaji (17000 8000 B.C) Katika kipindi cha awamu hiyo binadamu alipiga hatua kutoka kwenye hali ya ukusanayaji kwenda kwenye hali ya uzalishaji ambapo alianza kutafuta maeneo ya maji kwa ajili ya kuishi jirani na mahali hapo, akakusanya mbegu za mimea midogomidogo kama vile ngano, shayiri kwa nia ya kuziotesha, ikiwa ni pamoja na kujishughulisha na uwindaji. Hivyo awamu hiyo kutoka kwenye Zama za Mawe ilitofautiana na awamu nyingine kwa kuwa ilikuwa awamu ya uthabiti na maendeleo ya nyenzo za maisha na uzalishaji, hususan baada ya kugundua mahali pa kufinyanga (pottery) na kuitumia katika utengenezaji wa zana mbalimbali. Kudhihiri kwa jamii za wakulima (8000 4000 B.C)

30
Binadamu katika awamu hii alitegemea uvuvi na kilimo cha nafaka, lakini bado alikuwa hajaujua ufugaji wa wanyama. Aidha mbali na kazi hizo, palikuwepo na mawasiliano ya kibiashara kati ya Palestina na Uturuki, kwani zana zilizotengenezwa kwa Obsidi (Obsidian) zilizokuwa zikiagizwa na Uturuki zilikuwa zikipatikana Ariha (Palestina) na katika nchi nyingine. Halikadhalika Ariha nayo ilikuwa ikiagiza mali ghafi kama vile lami na chumvi kutoka bahari ya Dead Sea. Katika awamu zilizofuatia binadamu lijifunza jinsi ya kufuga wanyama. Mwisho wa milenia ya nne kabla ya Kristo (4000 2000 B.C) Kipindi hicho kilishuhudia bmabadiliko ya wazi katika nyanja za kiuchumi, kijamii na ujenzi nchini Palestina. Huwenda kitu kikubwa na cha muhimu zaidi katika kipindi hiki ni kudhihiri kwa idadi kubwa ya makaburi ambayo yamechimbiwa ndani miamba iliyopo Palestina. Katika vipindi vilivyofuata, matumizi ya chuma (metals) yaligunduliwa ambapo binadamu alianza kukitumia katika utengenezaji wa zana na vyombo mbalimbali. Kipindi hiki pia kilishuhudia kuibuka kwa mahekalu, ambapo athari za majengo yake zilionekana katika miji na vijiji vingi vya Palestina. Ama kuhusu maendeleo katika kiwango cha uzalishaji na biashara, ukuaji wa dhahiri ulishuhudiwa, pamoja na kuongozeka kwa viwango vya maisha na maendeleo ya kilimo.

Wasamiti
Kwa mujibu wa ugunduzi wa mambo ya kale uliofanywa katika nchi za Misri na Iraq, Wasemiti ndio jamii za watu wa kale zaidi, ambao waliishi kwenye ardhi ya Palestina tangu milenia ya nne kabla ya Kristo. Walikuwa wakiishi katika pwani ya mashariki ya bahari ya Mediterranean. Ama katika kipengele cha dini, kwa asili watu hawa wanachukuliwa kuwa wanatokana na kizazi cha Shem, mtoto mkubwa wa Nabii Nuhu (a.s.). Kinachothibitishwa ni kwamba wakazi wa asili wa ardhi ya Palestina tangu zamani wote ni Waarabu

31
waliohama kutoka katika Peninsula ya Arabia kufuatia ukame ulilolikumba eneo hilo. Kwa hiyo waliishi katika nchi yao hiyo Canaan kwa zaidi ya miaka elfu mbili kabla ya kudhihiri kwa Nabii Musa (a.s.) na wafuasi wake. Wakanaani Kwa mujibu wa tathmini zilizothibitishwa, tukio maarufu la kuhama kwa Wakanaani kutoka Peninsula ya Arabia lilitokea katika kipindi cha katikati ya milenia ya tatu kabla ya Kristo. Ijapokuwa baadhi ya watafiti wameeleza kuwa Wakanaani waliishi katika nchi hiyo tangu mwanzoni mwa milenia ya tatu, ambapo wanatoa dalili zao kutokana na ugunduzi wa mambo ya kale uliofanywa nchini Misri. Wengine wanaamini kuwa wakanaani walikuwepo katika eneo hilo tangu miaka elfu saba iliyopita, na hayo yanatokana na uchunguzi wa kumbukumbu zinazopatikana katika miji yao ya kale, ukiwemo mji wa kale zaidi ambao ni Ariha uliopo hadi leo, na ambao unachukuliwa kuwa ndio mji wa kale zaidi kuliko yote ulimwenguni. Ingawa tathmini ya mwanzo hasa wa uwepo wa Wakanaani inayumbayumba, kile kinachokubaliwa na watu wote ni kwamba wao ndio walikuwa wa mwanzo kuishi katika eneo hili miongoni mwa jamii za kale zilizokuwepo wakati huo, na ndio waliokuwa wa mwanzo kujenga ustaarabu katika ardhi ya Palestina. Imetajwa katika maandiko ya Kiebrania kwamba Wakanaani ndio wakazi wa asili katika nchi hii, imetajwa pia katika Torati kuwa wao ndio Waamori (Amorite People). Miongoni mwa miji ya kale ambayo bado ipo mpaka sasa ni Ariha, Jericho, Asdoud, Acco, Gaza, Al-Majdal, Jaffa, Askelan na Bisan. Vile vile kuna miji na vijiji vingi ambavyo baadhi yake bado vipo na baadhi vimeshatoweka. Shekeem ndio iliyokuwa mji mkuu wa nchi ya Kanaan. Wakanaani walijulikana kwa kilimo na uzalishaji. Walikuwa hodari katika uchimbaji wa madini, utengenezaji wa vyombo vya udongo, vioo, nguo na vitambaa. Pamoja na hayo pia walikuwa hodari katika sanaa ya ujenzi. Muziki na fasihi viliongoza katika ustaarabu wa Wakanaani, ambapo hakuna jamii nyingine ya Wasemiti iliyotilia maanani sanaa na muziki kama walivyofanya Wakanaani ambao walinukuu aina nyingi za muziki wa jamii mbalimbali

32
zilizolifanya eneo la Mashariki ya Karibu kuwa makazi yao. Kutokana na muziki kuwa katika desturi za kiibada kwa Wakanaani, mahadhi ya muziki na ala zao yalienea na kutangaa katika eneo zima. Hakuna anayeweza kukana kwamba sanaa na fasihi ni mhimili wa ustaarabu. Hivyo sio ajabu tunapofuatilia maandishi ya Waisraeli tukakuta juhudi kubwa iliyofanywa na Waisraeli kuudanganya ulimwengu udhani kwamba wao ndio waliokuwa wajenzi wa ustaarabu huo mkubwa, na kwamba ndio watunzi wa mahadhi, nyimbo na tenzi. Wamefanikiwa katika kuufanya huu uongo uonekane kuwa kweli machoni pa watu wengi. Lakini wanahistoria wakubwa wanaoaminika kama vile Bristed waliyaelezea maendeleo na ustawi wa mji wa Wakanaani pindi Waebrania walipofika hapo. Wameelezea kuwa ni mji uliokuwa umejaa nyumba za kifahari na maridhawa, mji uliosheheni uzalishaji, biashara, maandiko na mahekalu vikionesha kuwa kulikuwepo na ustaarabu ambao wachungaji wa mwanzo wa Kiebrania (Hebrew) walijaribu kuuiga, na hivyo wakayaacha mahema yao na kuwaiga wakazi wa eneo hilo katika kujenga nyumba. Aidha, (waebrania hao) walizivua ngozi walizokuwa wakizivaa majangwani wakaanza kuvaa nguo nzuri za sufu, na kadiri muda ulivyopita ikawa vigumu kutofautisha kati ya Wakanaani na Waebrania (Wayahudi) katika muonekano wa nje. Baada ya ujio wa Wapalestina kutoka upande wa bahari, Waisraeli kutoka Jordan, ardhi ya Kanaan ikagawanyika katika jamii tatu. Kwa hali hiyo Wakanaani hawakuendelea kuwa mabwana pekee wa nchi hiyo. Hata hivyo, lugha yao iliendelea kuwepo. Tangu mapambazuko ya historia iliyonakiliwa, yaani miaka elfu tano iliyopita, hadi wakati wa ujio wa Uingereza mwaka 1920, Palestina imekuwa na lugha tatu pekee: Kikanaani kwa sehemu ya kwanza, kisha Kiaramia (Aramean), ambayo ni lugha Nabii Isa (a.s.), na ya tatu ikiwa ni Kiarabu. Mwanzoni mwa milenia ya pili kabla ya Kristo (B.C.), miji ilikuwa imeanza kushuhudia uchangamfu fulani, na aina mpya za majengo na makaburi zikadhihiri sanjari na utengenezaji wa aina mpya za vyombo na silaha. Aidha awamu hii ilitofautiana na awamu nyingine kutokana na mahusiaono bora ya kibiashara na kisiasa pamoja na maeneo ya kale ya upande wa mashariki, hususan Misri, Bilad Al- Sham, kaskazini mwa Syria na

33
mashariki ya Uturuki. Mbali na hayo, awamu hiyo ilishuhudia maendeleo ya uzalishaji wa vyombo vya udongo na namna ya uainishaji wa udongo na kuuchanganya, kasha kuufinyanga kwa kutumia magurudumu mepesi yaliyowezesha kutengeneza vyombo vizuri na maridhawa. Kwa upande mwingine, awamu hii ilitofautiana na awamu nyingine kwa Misri kulidhibiti moja kwa moja eneo la Bilad Al-Sham katika kipindi cha utawala wa ufalme wa kumi na nane na kumi na tisa, ambao walimshinda mfalme wa mwisho wa himaya ya Hixos mwaka 1567 B.C. Hilo lilitekelezwa kupitia kampeni zilizoanzishwa na Thutmose III dhidi ya Bilad Al-Sham mwaka 1480 B.C. Aidha ilitokana pia na kutokuwepo kwa ngome imara zilizotengenezwa kutokana na tabaka madhubuti la udongo zilizokuwa zimejengwa na Wahixo. Jambo la msingi kulieza hapa ni kwamba, katika kipindi hicho Palestina ilishuhudia hali ya machafuko yaliyoliathiri eneo hili kutoka kasikazini na maeneo ya kati mara baada ya kunza kwa utawala wa ufalme wa kumi na nane, na baada ya kuwaondosha Wahixo na kuwafukuza mpaka Sharohin kaskazini mwa Palestina. Matukio hayo yalirikodiwa kwa upana katika maandiko tangu enzi za Thutmose III, mbapo maelezo hayo yanasimulia vita vya Megiddo vilivyoongozwa na Mfalme wa Megiddo na Mfalme wa Qadish kwa upande wa Syria, ambao waliunda muungano uliojumuisha zaidi ya miji elfu moja na ishirini. Tukio hilo pia lilitajwa katika maalezo yanaonesha ufahamu wa kimaeneo aliokuwa nao Thutmose, pia maandiko hayo yalipatikana katika mojawapo ya nguzo zilizojengwa Karnak na Memphis.

Zama za himaya mbalimbali (Zama za mawe):1200 550 B.C.


Katika kipindi hicho Wapalestina walijihesabu kama warithi halali wa mamlaka ya Misri nchini Palestina, hivyo, kwa hiyo wakaanza kuzitawala sehemu nyingi za nchi hiyo. Kwa kawaida wanaelezewa kuwa ndio wakazi wa pwani ya Palestina, amabapo walianzisha idadi kadhaa ya miji muhimu, kama vile Gaza, Askalan, Asdoud, Aqir, Tal As-Safy na mingineyo. Athari ya Wakanaan ilijidhihirisha wazi kwa Wapalestina. Athari hiyo yaweza

34
kuonekana katika majina ya miungu yao, kama vile Dagon na Ashtartout, halikadhalika maisha ya kidini ya wakazi wa pwani ya Palestina yana asili ya Kikanaan. Aidha, majengo yao ya kidini ambayo mengi yalikuwa ni majengo ya mamlaka katika mji wa Tal Al-Kasilah yalijengwa kwa mtindo wa mahekalu ya Wakanaan na usanifu wa Kimisri. Kwa upande mwingine, kuna madai yaliyotolewa na watafiti wa mamabo ya kale wa Kisraeli kuhusu asili ya baadhi ya uvumbuzi na majengo ya kale, wakiyahusisha na Israeli ya zamani, na ambayo yanajulikana katika vyanzo vya Kimagharibi kama collared-rimjar.

Waisraeli: Neno Israeli linarudi kwa Nabii Yaqoub (a.s.), mtoto wa Ishaaq na mjukuu wa Nabii Ibrahim (a.s.), na ambaye ndiye baba ya jamii hiyo. Nabii Ibrahim (a.s.) alizaliwa katika mji wa Ur ya Chaldee; aliwasili katika ardhi ya Kanaan kwenye karne ya ishirini au ishirini na moja B.C. baada ya kuiacha nchi yake akiwa pamoja na baadhi ya wanafamilia wake kwa lengo la kumuabudu Allah akitekeleza maamrisho ya Mungu yaliyomtaka aihame nchi yake, kwani jamii yake ilikuwa wakiabudu masanamu yeye akiwa akiwa anamuabudu Mungu Mmoja. Kituo chake cha kwanza kilikuwa ni Haran iliyokuwa upande wa kaskazini baina ya mto furati (Euphrates) na Khabour, mahali ambapo baba yake Tarih alifariki dunia. Kisha akaendelea na safari mpaka alipofika Shakim (Nablus). Nabii Ibrahim (A.S.) alimzaa mwanae wa kwanza, Ismail (a.s.) baba wa waarabu, kwa mkewe Hajar (a.s.), na kisha akamzaa mwanae wa pili Ishaaq (a.s.) baba wa Wayahudi kutoka kwa mkewe Sarah (a.s.). Ishaaq aliwazaa Esau na Yaqoub (Israeli), ambaye alizaa watoto 12 ambao ndio baba wa makabila yote ya Wayahudi. Miongoni mwa watoto wa Yaqoub ni Yusufu (a.s.) aliyefanyiwa husda na ndugu zake wakamtupa kisimani huko jangwani na kudai kuwa alikuwa ameuliwa. Wasafiri waliopita mahali hapo wakamkuchukua na kumuuza kwa wafanyabiashara wa Kimisri, na huko Yusufu aliingia katika utumishi wa Farao (Firaun) ambapo alisimamia mamlaka makubwa na hivyo akaweza kumuita baba yake pamoja na

35
ndugu zake. Na hivyo Familia ya Yaqoub ikahamia Misri. Hakuna ajuaye lini Farao wa Misri aliwageuka na kuanza kuwaadhiri na kuwaadhibu mpka pale Nabii Musa (a.s.) alipoanza kufikiria juu ya kuihama nchi hiyo. Huko mlimani, Allah alimfunulia Musa ya kwamba arudi Misri kuiokoa jamii yake na kuwatoa nje ya Misri. Na hivyo Musa na Haroun (a.s.) wakarudi Misri kuwatoa jamaa zao, na hapo safari ya mtawanyiko ikaanza, ambapo ilikuwa ni kwenye mwaka 1227 B.C. Ni katika kipindi hicho kwamba watu wa Musa walibadilika na kumuabudu ndama na kupelekea kuteremshwa kwa Amri Kumi, na kisha Waisraeli waliendelea kuwa katika hali ya kutanga tanga kwa muda wa miaka arobaini.

Nabii musa (a.s.) alituma zaidi ya wapelelezi kadhaa kwenda kuchunguza hali ya ardhi ya Kanaan, ambao walirudi na kumwambia kuwa Kanaani ni ardhi yenye neema, yenye maziwa na asali. Licha ya hilo, watu wa nchi hiyo wana nguvu na Waisraeli hawana nguvu ya kupambana nao. Waisraeli walipoamua kuingia katika nchi ya Kanaan walikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wakazi wa eneo la kaskazini, na hivyo wakalazimika kuelekea upande wa mashariki na kuanza kuvuka mashariki mwa Jordan ambapo Musa (a.s.) alifariki dunia. Kutokan na kifo hicho, Nabii Yousha Bin Noon (Yoshua) alishika uongozi wa msafara na kuendeleza azma ya mapambano. Mji wa kwanza kuingiwa na waisraeli ni Ariha, ambapo waliuzingira mpaka ukaangukia mikononi mwao. Kisha wakaishika sehemu kubwa ya kaskazini mwa Palestina. Wakati wakanaani waliizuia sehemu yake, kwa upande wa Wapalestina waliizuia eneo la magharibi. Tangu wakati wa zama za waamuzi (Makadhi), kipindi kilichofuatia kifo cha Yousha (Yoshua), tawala tatu zilishika hatamu kwa mamia ya miaka. Tawala hizo zilipenyezwa na mlolongo wa vita vya Wakanaan na Waisraeli, na Wapalestina na Waisraeli. Kipindi hicho kiliendelea kwa zaidi ya karne moja na nusu,

36
ambapo waamuzi (Mapilato) 12 walipata kutawla, wa mwisho akiwa ni Samuel. Kisha Waisraeli walikubaliana kumteua Saul kuwa mfalme wao kutokana na mapendekezo ya Samuel mwenyewe, ili apate kuyaunganisha makabila yao chini ya mwamvuli mmoja. Lakini alifariki dunia katika mojawapo ya mapambano dhidi ya Wapalestrina. Kisha alifuatiwa na Nabii na Mfalme Daudi (a.s.) (1010 B.C. 971 B.C.), akifuatiwa na mwanae, Nabii Sulaiman (a.s.) (971 B.C. 931 B.C.) ambaye kipindi chake kilitawaliwa na amani badala ya vita. Aidha alitambulika kwa sifa ya hekima na busara na umahiri katika kazi zake za kibiashara. Mnamo mwaka 724 B.C. himaya ya Waisraeli iliangushwa na Waassyria. Baadaye akaja Nebuchadnezzar aliyewashinda Waassyria na kuanzisha himaya ya Chalde na kuitawala Palestina.

Himaya ya Waajemi: Mwaka 550 B.C. 330 B.C.: Himaya ya Waajemi na zama za Alexander mkuu

Inachukuliwa kuwa ndio mrithi wa Assyria. Ilianzishwa na wafalme wake wa mwanzo: Cyrus, mfalme Cambyses, na Darius I. Eneo la himaya ya Waajemi ilianzia magharibi mwa bahari ya Aeja hadi kwenye mipaka ya India kwa upande wa mashariki, na kutoka kusini mwa Misri mpaka kwneye bahari Nyeusi na eneo la Milima ya Caucasus kwa upande wa Kaskazini. Mfalme Darius alipokalia kiti cha ufalme, aliigawa himaya hiyo katika majimbo 20, na kila jimbo akaliwekea gavana. Kwa sababu hiyo palestina ilikuwa sehemu ya jimbo la tano lililojulikana kwa jina la Kiarami Nabr Nahra, yaani ngambo ya mto. Mto unaozungumziwa hapa ni mto Furati (Euphrates). Jimbo huilo liliundwa na eneo zima liliojulikana wakati huo kama Bilad A-Sham iliyojumuisha Syria, Cyprus, na Phoenicia.

37

Mwaka 330 B.C. 63 B.C. Mnamo mwaka 334 B.C., Alexander Mkuu wa Macedonia alivuka bahari kuelekea Asia Ndogo (Asia Minor), ambapo alipata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Waajemi katika vita vya Granicus, na mwaka huo huo akamshinda mfalme wa Waajemi katika vita vya Issus huko Cilicia. Kisha alisonga mbele kuelekea kusini jirani na pwani za Bilad Al-Sham kwa lengo la kuziharibu manowari za Phoenicia zilizokuwa zikitegemewa na Waajemi katika sehemu ya mashariki mwa bahari ya Mediterranea, na hivyo avika Mlima Taurus ambapo alianzisha mji wa Miriandos ujulikanao leo kama Alexandria. Baadaye alilituma kundi la askari wake kwenda mjini Damascus na kuutwaa, na katika kipindi cha majira ya baridi cha mwaka 332 B.C. alielekea katika pwani za Syria na kuzitwaa. Kufuatia kifo chake, himaya yake ilikumbwa na migogoro na vita vingi vya ndani katika kugombania mamlaka na utawala. Mapambano hayo yalipelekea kuundwa kwa mataifa mawili: taifa la Waseleuc (Seleucid) huko Syria, na jingine la Waptolema (Ptolemaic) katika Misri. Mwaka 175 B.C., vita vilizuka nchini Palestina kati ya Wamacabayo (Macabians) na Waseleuc (Seleucids) vilivyodumu kwa muda wa mika arobaini na kuhitimishwa kwa kuasisiwa ufalme wa Hashmon (Hashmonian) uliongolewa na Pompey mwaka 63 B.C. baada ya kuivamia Jerusalem na kuifanya Palestina kuwa sehemu ya Himaya ya Warumi, kama ilivyokuwa kwa maeneo mengine ya Bilad Al-Sham.

Himaya ya Warumi Mwaka 63 B.C. 636 A.D.

38

Warumi walianza kuinglia masuala ya taifa la Seleucid tangu mwanzoni mwa karne ya pili B.C., kutokana na udhaifu na uduni ulioikumba mamlaka ya Seleuc (Seleucid) kutokana na kuingia katika migogoro na vita vya ndani, na ushindi walioupata Warumi chini ya uongozi wa Domitius Ahenobarbus aliyemshinda Mfalme Antiochus III kwenye vita vya Magnesia mwaka 190 B.C. Aidha, historia inaeleza kuwa mwaka 63 B.C, majeshi ya warumi chini ya uongozi wa Pompey yaliingia Jerusalem baada ya kuuzingira mji kwa muda mrefu na vita vikali vilivyoiacha idadi kubwa ya watu wkiwa wamekufa pamoja na Palestina na eneo la magharibi mwa Syria yalifanywa kuwa sahemu ya mkoa wa himaya ya Rumi. Gavana wa kwanza aliyeteuliwa kuitawala Syria alikuwa ni Crassus, na baadaye mwaka 57 B.C Ghabyonous aliitawala Syria na kuleta mamlaka ya kiungozi mjini Jerusalem. Mwaka 54 B.C. Crassus alirejea kwenye utawala wa Syria. Alikuwa katika kundi linalojulikana kama First Triumvirate (muungano wa Kirumi wa kugawana madaraka) uliosaniwa kati ya Julius Caesar, Pompey Mkuu, na Marcus Crassus, ambapo madaraka yaligawanywa baina yao. Lakini muda mfupi baada ya makubaliano hayo, ugomvi ulizuka baina ya Pompey na Caesar na kufuatiwa na kuuawa kwa Julius Caesar, na kisha mmoja wa wauaji ambaye ni Crassus akawa gavana wa Syria (44 B.C. 42 B.C.). Mnamo mwaka 42 B.C. Mark Antony na Octavian waliwashinda wauaji wa Julius Caesar. Baada ya hapo ulikuja utawala wa Herod aliyelitawala eneo la Jerusalem na Palestina. Utawala wake ulidumu kuanzia mwaka 37 B.C hadi 4 B.C. Kabla ya kifo chake alimteua Antipas kuwa mrithi wake, ambaye alilitawala eneo kubwa la Palestina. Utawala wake ulidumu kuanzia mwaka 4 B.C. hadi 39 B.C. Inaelezwa kwa aliufanya nji wa tiberias kuwa mji wake mkuu. Mwaka 41 A.D. Palestina ikawa taifa la Kiromania (Romanian state).

39
Kuibuka kwa Ukiristo Yesu Kristo (a.s.) alizaliwa Bethelehem mwaka 4 B.C. Kipindi hiki kimegawanyika katika awamu tatu: Awamu ya kwanza ni ile ya baada ya zama za Kristo, ijulikanayo kama enzi za mitume (30 95 A.D.) Awamu ya pili inaendelea kwa muda wa karne nzima kuanzia mwishoni mwa karne ya kwanza hadi mwisho mwa karne ya pili. Kipindi hiki kinahusisha tukio la Constantine Mkuu kuingia katika Ukristo mnamo mwaka 312. Awamu ya tatu inahusisha msukosuko wa mapinduzi ya ndani uliotokea katika kipindi cha nusu ya pili ya karne ya tatu dhidi ya Warumi. Msukosuko huo uliongozwa na mfalme wa tadmuriyah odenathus na baada ya kifo chake ukaongozwa na mjane wake Zenobia. Mwaka 272 A.D., Mfalme Aurelian wa Rumi alifanikiwa kuzuia uasi huo wa Tadmuriyah. Mwaka 395 A.D. himaya ya Romania (Romanian Empire) iligawanyika sehemu mbili: sehemu ya mashariki na shemu ya magharibi, ambapo Theodosius Mkuu alimteua mwanae Arcadius kuwa mtawala wa mashariki, akaamuru kuwa awe mtawala huru. Alitawala eneo hilo kauanzia mwaka 395 hadi 408 A.D. Mfalme huyo vilevile akamteua mwanae wa pili Honorius kuwa mtawala wa magharibi ambapo alitawala kuanzia mwaka 395 A.D. hadi 423 A.D. Kitu kfaacho kutajwa hapa ni kuwa, baada ya utawala wa Constantine na hadi mwaka 527 watawala wapatao 17 walipata kutawala, wanne miongoni mwao wakishika kiti hicho kwa nguvu. Inaelezwa kuwa mfalme justian II alitwaa kiti cha Wabyzantine katika kipindi cha mwaka 565 578 A.D., kisha akamteua Tiberius kuwa mrithi wake (578 582), akafuatiwa na

40
Maurice (582-602 A.D.), akifuatiwa na Phocas (602 610 A.D.), na kisha Heraclius (610 641 A.D.). Vita kati ya Wabyzantine na Wasassani wakati mmoja vilikuwa vikali na wakati mwingine kupoa. Mara nyingi walifanya makubaliano yaa kusimamisha vita, lakini haukupita muda mrefu makubaliano hayo yalivunjwa na vita kulipuka. Kwani mwaka 610 622 A.D. Waajemi walianzisha mashambulizi dhidi ya Warumi na kupata ushindi katika kampeni zao hizo, na hivyo mwaka 614 waliitwaa miji ya Antakya, Damascus, na Jerusalem. Hata hivyo hali ya vita visivyoisha pamoja na mambo mengine yalizidhoofisha himaya hizo mbili, jambo lililowafanya washindwe kukabiliana na Waarabu ambao waliusambaratisha utawala wa wasassani na kuyatwaa maeneo ya Bilad Al- Sham na Misri kutoka mikononi mwa Wabyzantine katika vita vya mwisho vijulikananvyo kama Yarmuk mnamo mwaka (15 A.H./636 A.D.).

Harakati za ukombozi wa kiislamu chini ya Waarabu

Kwa kuingia kwa zama za ushindi, majeshi ya Kiislamu yalielekea Bilad Al-Sham. Mji wa kwanza kufunguliwa na Waislamu ulikuwa basra, na hicho kilikuwa kipindi uongozi wa Abu Bakr As-Siddiq (r.a.). Kisha wakaelekea Palestina, ambapo walikabiliana na Wabyzantine wa Kirumi katika vita vijulikanavyo kama Vita vya Ajnadin vilivyomalizika kwa Waislamu kupata ushindi na majeshi ya Wabyzntine kukimbilia katika mji wa Fahl kwenye ukingo wa mto Jordan jirani na Bysan. Huko Waislamu waliwazunguka na mwishowe watu wa mji wa Fahal wakajisalimisha kwa Waislamu. Mwaka huohuo mwezi wa jumada I Abu Bakr AsSiddiq alifariki dunia. Alirithiwa na Umar bin Al-Khattab (r.a.). Warumi waliendelea kushindwa na Waislamu ambao walipambana nao katika maeneo mengi ya Bilad Al-Sham. Habari za kushindwa kwa Warumi katika vita vya Yarmuk

41
zilipomfikia Heraclius, alihama kutoka Antakya na kuelekea Constantinople. Vita hivyo vilitokea mwaka 636 A.H. Ingawa idadi ya waislamu katika vita hivyo haikufikia hata robo ya idadi ya majeshi ya Kirumi, lakini waliweza kupata ushindi wa ajabu. Vita vya Yarmuk ndivyo vita vya mwisho vya wazi kufanyika katika ardhi ya Bilad Al-Sham, baada yake himaya ya Warumi ilibaki na maeneo mawili tu ambayo ni Jerusalem na Qisarya. Ufunguzi wa Jeruslem ilikuw ni mojawapo ya malengo muhimu ya taifa la Kiislam wakati huo. Hivyo majeshi ya Kiislamu yaliuzingira mji huo, lakini watu wake walikataa kujisalimisha kwa Abu Ubaidah Al-Jarrah (r.a.) ambaye ndiye aliyekuwa kamanda wa majeshi hayo ya Kiislamu. Badala yake walimtaka Umar bin Al-Khattb awe ndiye watkayefanya naye makubaliano ya amani na kuifungua milango ya mji huo. Kwa sababu hiyo, Abu Ubaidah alituma ujumbe kwa Umar, ambaye alikwenda Jerusalem kuwafungulia waislamu milango ya mji huo.

Palestina katika Zama za Makhalifa Wanyoofu

Baada ya waislamu kuifungua Palestina, eneo hilo likawa jimbo lililo chini ya Serikali ya kiislamu, ambapo lilifurahia kila aina ya uthabiti ambao haukuwahi kupatikana hapo kabla. Kabla ya kuwa chini ya utawala huo wa Kiislamu, lilikuwa ni eneo la machafuko yaliyotokana na mapambano ya himaya kuu mbili zenye nguvu (Himaya ya Wabyzantine na himaya ya Waajemi). Baada ya kulifungua, umar bin Al-Khattab mabaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa dola ya kiislamu, alimteua Amr bin Al-As (r.a.) kuwa gavana wake na baadaye akafuatiwa na Abdur-Rahman bin AlKamah Al-Kanany, na baada ya kifo chake uongozi wa eneo hilo ulikwenda kwa Al-Kamah bin Magzr. Hali iliendelea kuwa hivyo hadi pale khalifa Uthman bin Affan (r.a.) alipoiweka Palestina chini ya usimamizi wa Muawiyah bin Abi Sufian, ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa gavana wa Syria.

42

Zama za makhalifa wa Bani Umayyah

Katika kipindi hicho Palestina ilianza awamu mpya katika historia baada ya Muawiyah bin Abi sufian (r.a.) kujitangaza kuwa khalifa na kuuasisi utawala wa ufalme wa bani umayyah uliodumu kwa takriban miaka 90. alianza utawala wake kwa kuelekea Jerusalem mwaka 661 na kutangaza ukhalifa wake na watu wakala kiapo cha utii kwake na kumridhia. Pindi utawala ulipokwenda kwa yazid bin Muawiyah, msukosuko wa ndani ulianza kuibuka. Msukosuko huo ulichochewa na wapinzani wake kama vile Al-Hussain bin Ali (r.a.) Shahidi wa Karbala, na Abdullah bin Az-Zubair (r.a.) aliyedai kuwa na haki ya ukhalifa baada ya kifo cha Al-Hussain, na hivyo watu wa Hijaaz na maeneo kadhaa yaIraq wakamuunga mkono, jambo lililosababisha ufa katika umoja wa umma. Yazid alipofariki dunia, fitna nyingine ilianza kujitokeza baaada ya watu kuzidi kuelekea upande wa Ibn AzZubair, isipokuwa Syria iliyokula kiapo cha utii kwa Muawiyah bin Yazid bin Muawiyah, lakini utawala wake haukudumu kwani aliuawa baada ya siku arobaini za utawala wake. Kutokana na tukio hilo watu wa Syria walielekea upande wa bin Az-zubair, isipokuwa wanajeshi wa Jordan na palestina waliokuwa chini ya uongozi wa Hassan bin Malik bin AlKalby aliyekuwa na mapenzi kwa Muawiyah bin Abi Sufian (Khalifa wa Bani Umayyah). Aliamua kuelekea Jordan ili awe shuhudia wa matukio huku akimuachia Ruh bin Zinbaa Al-Jazamy jukumu la kuliongoza jeshi la palestina. Lakini muda mfupi baadaye, Nathil bin Qayis Al-Jazamy alitangaza kula kiapo cha utii kwa Ibn Az-Zubair na kumhamishia Ruh mjini Jordan, eneo pekee lilillokuwa likiendelea kuunga mkono ukhalifa wa Bani Umayyah. Baada ya vita vya Marj Rahit, mtazamo wa watu wa Syria ulielekea kwa marwan bin Al-

43
Hakam kama Khalifa, na baada yake Khalid bin Yazid bin Muawiyah. Baadaye, ulirudi tena kwa Abdul Malik bin Marwan aliyemrithi baba yake. Katika zama za utawala wa Abdul Malik mpaka ule wa mwanaye Hisham bin Abdul Malik, Palestina ilifurahia uthabiti na ustawi, na hakuna tukio baya lililovuruga utulivu wake. Lakini baada ya kuja kwa utawala wa Hisham, udhaifu ulianza kujitokeza katika dola ya Bani Umayyah, na mgogoro wa ndani ukaanza kupanuka. Mtawala wa mwisho wa Bani Umayyah alikuwa Marwan bin Muhammad, ambaye utawala wake uliashiria kuanguka kwa zama za Bani Umayyah na kuibuka kwa utawala wa bani Abbas.

Zama za Makhalifa wa Bani Abbas Kufuatia kuuawa kwa Marwan bin Muhammad, mazingira yaliwarahisishia bani Abbas kuidhibiti Syria, jambo lililopelekea miji mingi kudondoka moja baada ya mwingine bila kizuizi chochote. Baada ya Abdullah bin Ali kufanikiwa kuileta Syria chini ya mamlaka yake tarehe 16 Aprili 750 A.D., aliingia Palestina kuanzisha zama mpya katika historia ya aradhi hii ya Kiarabu. Bani Abbas walifuata sera kali dhidi ya wafuasi waliobaki wa bani Umayyah nchini Syria, lakini watu wake walikabiliana na sera hizo kwa uasi usiokwisha katika kipindi cvhote cha utawala wa bani Abbas, na hivyo Syria ilikuwa mwiba mchungu kwa utawala huo.

Dola ya Tulun Awamu ya mwisho ya utawala wa bani Abbas ilijawa na matukio mengi yaliyohusisha ukosefu wa uthabiti na msukosuko kutoka upande wa Syria kwenda kwa Bani Abbas. Hali hii iliendelea kuwepo hadi pale mamlaka yalipohamia kwa Ahmad bin Tulun, muasisi wa Dola ya Tulun, iliyoanzishwa Misri mwaka 870 A.D. Mtawala huyu alitaka kuapnua

44
ushawishi wake kwenye maeneo yote ya Bilad Al-Sham kwa hoja ya kuzilinda nchi za Kiislamu dhidi ya shari ya uadui wa Wabyzantine. Kwa hiyo alifanya kazi ya kuziunganisha, na aliendelea kutumia nguvu zake zote katika kuzilinda nchi za Kiislamu hadi alipofariki dunia mwaka 884. Baada ya kifo chake, utawala ulikwenda kwa mwanae Khumarawaih. Dola ya Tulun iliendelea kudumu hadi pale makabila ya Kiarabu kutoka Syria yalipoanza kufanya kinyume na mamlaka hayo. Hata hivyo, Syria iliendelea kuwa chini ya utawala wa Baghdad hadi ulipokuja utawala wa dola ya Ikhshid.

Dola ya Ikhshid Dola hii ilianzishwa na Abu Bakr bin Tughj, na kuwa mwanzo wa utawala wa Ikhshid katika Syria na Misri. Utawala wa Abu Bakr ulidumu hadi alipofariki mwaka 946 A.D. Mwili wake ulipelekwa Jerusalem na kuzikwa huko. Alirithiwa na Abu Al-Qasim Abu Gour.

Fatimiyyiin Zama za Fatimiyyiin zilianza baada ya kuanzisha dola yao huko Misri na kuyaangaza macho yao kwenye eneo la Bilad Al-Sham. Katika kipindi cha utawala wa Al-Muiz liDinillah, wakitumia jeshi lililoongozwa na Jawhar Al-Siqilli, walifanikiwa kupanua eneo la utawala wao hadi Syria. Kipindi hiki kilihanikizwa na misukosuko na vita vilivyotokana na sababu za ndani na nje ya dola hii, hususan kutokana na ukweli kwamba Dola ya Fatimiyyiin iliasisiwa kwenye misingi ya Ushia kinyume na madhehebu iliyokuwepo wakati huo katika Syria. Tofauti hizo za kimadhehebu zilileta msukosuko katika mamlaka na serikalini. Mbali na sababu hiyo, kulikuwa na tamaa iliyojidhihirisha kwa madhehebu mengine kuinyakuwa Bilad Al-Sham na kuitawala. Aidha, mambo mengine ni pamoja na wengine kutamani kuwa huru kwa kujitangaza kuwa majimbo huru.

45

Dola ya Waseljuk Waturuki waliojulikana kama Seljuk walianza kusogea taratibu kuelekea kaskazini mwa Iraq na Syria mwaka 1067 A.D. Hawakuwa na asili ya makabila ya Kiarabu yaliyokuwapo Bilad Al-Sham bali walitokea Turkistan, wakiwa wageni katika Uislamu. Walichanganyika na kuchangamana na watu wa Syria na baada ya muda mfupi wakashika madaraka ya utawala na jeshi, na hivyo wakachukua jukumu la kuilinda nchi dhidi ya Wazungu, na Wamongoli kwa takriban karne nne. Walilazimisha utawala wao katika eneo hilo kwa nguvu za jeshi hadi mwanzoni mwa karne ya ishirini.

Wazungu Kipindi cha vita vya msalaba kilianzia mwaka 1095 hadi 1291, ambapo kulikuwa na hujuma za kijeshi zilizoanzishwa dhidi ya maeneo mengi ya mashariki. Vita vya kwanza vya msalaba vilianza baada ya tangazo lililotolewa na Papa Urban II mjini Clermont mwaka 1095 ambapo aliahamasisha vita vya msalaba kwa kaulimbiu ya Ni Amri ya Kristo. Kwa namna hiyo, vita vya kwanza vya msalaba vilichochewa kwa maneno makavu yaliyotumia kaulimbiu za mafundisho ya kanisa kwa lengo la kuyatwaa maeneo matakatifu katika eneo la mashariki, mahali alipozaliwa Kristo. Papa aliona kwamba iwapo Kanisa Katoliki la magharibi litaongoza vita hivi, litaweza kukamata nafasi za kimamlaka katika eneo la mashariki, iwe katika uwanda wa siasa au dini, kama lilivyofanya huko magharibi. Karne ya kumi na moja ilishuhudia uchipukaji wa kidini katika wigo mpana, hususan miongoni mwa wananchi waliokuwa wamejazwa fikra na mawazo ya vita vya msalaba. Kwani, pindi ulipotolewa wito wa kuanzisha harakati za kijeshi chini ya bendera ya msalaba, wito huo ulipata kuitikiwa na matabaka haya. Karne hiyo pia ilishuhudia nguvu za Mapapa

46
zikiongezeka, hususan katika kipindi cha Papa Gregory VII, na baada yake Papa Urban II aliyeimarisha nguvu ya kanisa na kuona kuwa vita vya msalaba ni njia stahili ya kuimarisha zaidi uwezo na ushawishi wa kanisa, sanjari na kukubali ombi la mfalme wa Byzantine ambaye alituma ujumbe wa kutaka msaada wao baada ya kuhisi hatari ya kuzingirwa kwa mji wake mkuu na kutokuwa na uwezo wa kuepusha hatari ya kuyakosa maeneo matakatifu ambayo yangeangukia mikononi mwa Waarabu. Katika kipindi cha karne hiyo ya kumi na moja, Ulaya ilikuwa imeaandaliwa kiroho na kimwili kuikubali fikra ya vita vya msalaba. Mazingira mabaya ya kijamii, ongezeko la watu, na hali ya kimaumbile ya ardhi za kilimo, majanga ya kiasili na magonjwa ya mlipuko, bila kutaja tamaa na ulafi, yote haya yalisaidia katika kupandikiza vikra za vita vya msalaba.

Vita vya kwanza vya msalaba: vita vya kwanza vya msalaba vilitokea baada ya mtawala wa Byzantine alipoomba msaada wa kijeshi katika namna ya jeshi la kukodi kwa lengo la kuulinda mji wake mkuu. Hivyo jawabu la Ulaya likaja katika namna ya vita vya msalaba, jambo ambalo halikuwa likitarajiwa na mtawala huyo wa Byzantine, ambaye alijikuta ameingia katika hali tete na ya hatari. Mjini Clermont (Ufaransa) katika mwezi wa Novemba 1095, Papa Urban II alitoa hotuba kali iliyoamsha hisia za kidini za idadi kubwa ya waliohudhuria. Mbele ya kundi hilo kubwa la watu, alitoa wito wa kushika silaha kwenda kuwatetea wakristo wa mashariki waliokuwa wakikandamizwa na kwa lengo la kuliokoa kanisa la Al-Qiyamah na wakristo wa mashariki kwa ujumla. Kutokana na maneno hayo, wote walinyanyua sauti na kusema Ni Amri ya Kristo, wakasongamana mbele ya Papa kumuelaza utayari na uungaji mkono wao. Papa huyo aliwaahidi wali ambao wangeshiriki katika vita hivyo kwamba wangekombolewa na kusamehewa dhambi zao, wasingetozwa kodi, na familia zao zingetunzwa kikamilifu katika

47
kipindi chote watakapokuwa vitani. Ama wale waliokataa kushiriki katika vita aliwaonya na kuwakaripia kuwa wangefukuzwa katika kanisa. Hamasa ya kampeni hii ilitangaa kutoka Ufaransa na kuenea katika nchi zote za Ulaya. Dhana ya kuanzisha vita vya msalaba ilikuwa ngeni kwa Wabyzantine wote, iwe viongozi au hata watu wa kawaida, kwani wao walichokuwa wakifikiria ni namna ya kujilinda na hatari ya Waseljuk tu, na wakawatazama wapiganaji wa msalaba kwa jicho la mashaka wakaliona kuwa ni kundi lenye ukatili kama ule ule wa Waseljuk waliokuwa wakilihatarisha eneo la mashariki. Kampeni ya vita vya kwanza vya msalaba ilipokaribia Constantine chini ya uongozi wa Padri Peter, kampeni hiyo ilitanguliwa na sifa mbaya katika safari yake yote ya kutoka Ufaransa hadi Constantine, na hapo mtawala huyo aliyejulikana kwa hila na ujanja aliharakisha kubadilisha njia yake kuelekea pwani ndogo ya Asia, ambapo waliageuka kuwa chambo cha Waseljuk waliowafyekelea mbali. Baada ya kuangamia kwa jeshi la wapiganaji wa msalaba waliokuwa chini ya Padri Peter katika msimu wa joto wa mwaka 1096, ukusanyaji wa majeshi kwa ajili ya vita vya kwanza vya msalaba ulianza katika nchi za Ulaya ya Magharibi. Jeshi hilo lilikuwa kubwa zaidi likiwa chini ya uongozi wa pamoja. Majeshi hayo yalitakiwa kukusanyika mjini Constantine kabla ya kuyavamia maeneo yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Waseljuk. Katika kampeni hii Ufaransa ndio ilitoa askari wengi. Vita dhidi ya Waseljuk vilianza kwa ushiriki dhaifu wa jeshi la Byzantine. Majeshi ya Wanamsalaba yakaanza kuyazingira na kuyatwaa majimbo mbalimbali ambayo yalianguka moja baada ya jingine. Kisha walisonga mbele wakielekea upande wa kaskazini mwa Palestina, ambapo waliikamata Magharat Noman (pango la Noman), na kufanya mauaji ya kutisha, na wakielekea pwani walizitwaa wilaya nyingine. Baada ya kujenga maboma yao huko Sour, Acre walielekea Jerusalem pamoja na maeneo mengine matakatifu. Waliingia katika mji huo mnamo Mei 1099 na kuuzingira kuanzia Mei 7 hadi Julai 15, 1099, na walipoingia ndani ya mji walifanya maangamizi ya kutisha dhidi ya wakazi asilia wa

48
eneo hilo. Baada ya kuanzisha ufalme wa Kilatin wa Jerusalem, viongozi walitoka na kuendeleza mapambano yao ya kijeshi kenye eneo lote la pwani na ndani ya nchi zote za eneo husika. Fatimiyyiin walitanabahi na kukuta wavamizi hao wameshazivamia ardhi zao za Arabia. Walikuwa wamechelewa sana, wakajaribu kukabiliana nao lakini walishindwa katika mapambano makali yaliyotokea karibu na Askalan katika mwezi wa Agosti 1099. Kisha wapambanaji hao wa vita vya msalaba walikwenda kuyatwaa maeneo yaliyobaki katika miji ya pwani, huku Askalan ikibaki kuwa tishio kwa ufalme utawala wa Wakristo (Crusade kingdom) hadi mwaka 1153, kwa kiasi kwamba mji huo ulipokuja kudondoka eneo lote la pwani likawa chini ya udhibiti wa utawala huo wa Kikristo. Kwa zaidi ya miaka 50, mapambano kati ya fatimiyyiin na na utawala wa Kilatin wa Jerusalem (Latin kingdom of Jerusalem) hayakukoma. Vita vya pili vya Msalaba (1146-1149 A.D.)

Katika kipindi hicho, mapambano ya ndani baina ya Wanamsalaba (Crusaders) yalifikia kilele chake isipokuwa mapigano pamoja na mtawala Wa Byzantine Alexius aliyechukua fursa ya kuanguka kwa Bohemond I kuwa dhamana mikononi mwa kiongozi wa Kituruki Amir Malik Ghazi kuipora Antakya kutoka kwake, kwani baada ya kufanyika mazungumzo ya kumlipa fidia Bohemond I, Alexius alikataa kumrejeshea eneo la Antakya. Yote haya yaliwapa Waseljuk fursa ya kuzirejesha ardhi zao walizokuwa wamezipoteza, kwani mwaka 1104, Waseljuk walimuadhibu Bohemond kwa kipigo cha aibu katika eneo la Harran na kumnyanganya maeneo mengi ya Syria yaliyokuwa chini ya udhibiti wake. Kwa upande mwingine, utawala wa kilatin wa Jerusalem ulikuwa ukijitanua katika maeneo yote, jambo lililosababisha hali ya uasi katika mji wa Mosul, ambapo mwaka 1113 liliibuka vuguvugu lililokuwa na lengo la kuyaunganisha majimbo ya Kiislamu ya Iraq na Syria kwa ajili ya

49
kuunganisha nguvu ili kukabiliana na Wazungu. Vuguvugu hilo lilifikia kilele chake wakati wa Imad Al-Din Zinky aliyeibuka mwaka 1127 1146. Aliweza kuzithubutisha nguvu na mamlaka yake kwa magavana wa Iraq na Syria, isipokuwa Damascus. Kwa hiyo Imad AlDin Zinky akaandaa njia ya kuelekea awamu mpya ya makabiliano dhidi ya Wazungu yaliyoendelea mpaka katika kipindi cha mwanaye Nour El-Din Zinky, na baada yao Salah El-Din Al-Ayyubi hadi zama za Mamaaliks waliofanikiwa kuukomesha utawala wa Kilatin wa Jerusalem.

Utawala wa Ayyubi Salah El-Din Yusuf bin Ayyub alizaliwa katika familia ya Kikurd mwaka 1138, Tikrit nchini Iraq. Alihama kwenda Baalbak Lebanon pamoja na baba yake aliyekuwa ameteuliwa kuwa kiongozi wa jeshi katika zama za utawala wa Imad Al-Din Zinky. Kisha mwaka 1164 alihama kwenda Misri pamoja na mjombake Assad Al-Din Shirkuh aliyekuwa ameteuliwa kuwa waziri huko Cairo na baadaye kurithiwa na Salah El-Din. Mwaka 1171 alitangua ukhalifa wa fatimiyyiin na kutangaza kiapo cha utii kwa Khalifa wa bani Abbas, kuanzia hapo ukazuka mgogoro kati yake na Imad Al-Din Zinky, mgogoro uliokwisha baada ya kifo cha Imad Al-Din Zinky. Baadaye, Salah Al-Din alishughulika na kuiunganisha Misri na Syria chini ya uongozi wake ili kwamba aweze kutimiza ndoto yake ya kuwaondosha Wazungu. Mwaka 1187 ulihusisha tukio kubwa la kihistoria, nalo ni vita vya Hattin vilivyoleta mabadiliko katika mahusiano baina ya Mashariki na Magharibi, katika namna iliyowafanya wazungu waliokuwa mashariki waishi katika hali ya kujilinda. Kufuatia vita vya Hattin Salah Al-Din aliitwaa Tiberias, kisha akaelekea upande wa Acre pamoja na Galilee, Nablus, Yafa, Gaza, Ashqelon, Beirut na Sayda, maeneo ambayo yaliangukia mikononi mwake. Baadaye aliyarejesha katika himaya yake maeneo ya Al-Naserya, Qysaryah, Safad, Safoureya, Al-Shaqif na Jabal Al-Tour.

50
Aliendelea na harakati zake hizo mpaka akafika Al-Quds Al-Sharif (Jerusalem), akaizingira na kuwalazimisha wazungu (Crusaders) waondoke katika mji huo kwa makubaliano maalumu na mnamo tarehe 27 Rajab (1187 A.D.) alisali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa. Baadaye Wazungu (Crusaders) walikusanyika katika miji mitatu ya pwani: Antakiya, Tripoli na Soor.

Vita vya Tatu vya Msalaba Vita vya tatu vya msalaba viliongozwa na wafalme wa Ulaya waliokuwa na nguvu sana wakati huo, na vita hivi vilikuja baada ya kuanguka kwa Jerusalem. Licha ya migogoro iliyokuwepo kati ya wafalme hao, jeshi hilo liliweza kufika palestina na kuizingira Acre. Kutokana na hali hiyo, Salah Al-Din alikusanya jeshi lake haraka ili kuwazingira wanamsalaba (Crusaders). Ujio wa majeshi ya Ufaransa na Uingereza yalipelekea kuwepo na mapambano makali kati ya pande hizo mbili yaliyodumu kuanzia mwezi wa Agosti 1189 hadi Juni 1191 na kupelekea kuanguka kwa mji wa Acre. Mnamo Septemba 1192, baada ya majadiliano ya muda mrefu, pande hizo mbili zilifikia makubaliano ya kuacha mapigano kwa kipindi cha miaka mitatu. Kutokana na makabuliano hayo utawala wa Kikristo (crusade kingdom) ulianzishwa na Acre kuwa makao yake makuu huku Wakristo wakipewa haki ya kutembelea maeneo matakatifu yaliyopo Al-Quds Al-Sharif (Jerusalem) na AlNaserya. Baada ya makubaliano hayo ya amani, Salah Al-Din alirejea Damascus baada ya miaka 20 ya mapigano ya mfululizo akafariki mnamo tarehe 3 Machi 1193. Hata hivyo, vita dhidi ya Wazungu (Crusaders) havikusimama hadi wakati wa utawala wa Mamaalik.

51

Mamaaliks Utawala wa Mamaaliks ulikuwa ukijulikana tangu enzi za enzi za ukhalifa wa bani Abbas kutokana na nguvu zake za kijeshi, kwani wengi wao walitoka kwenye wanajeshi waliokuwa msitari wa mbele wa mapambanao na kuja kutwaa madaraka. Baada ya kudondoka kwa utawala wa Ayyub utawala huu ilikamata nafasi muhimu kwa sababu hatima ya Bani Ayyuub ilisababishwa na Mamaaliks ambao walianzisha himaya katika Misri na Bilad Al-Sham, himaya iliyodumu kwa kipindi cha karne mbili na nusu. Mwishoni mamaaliks walifanikiwa kuikomboa Misri, tukio lililotokia baaada ya wanamsalaba (Crusaders) kuweza kuitwaa Damietta na kuanza kuelekea Cairo, huku Al-Salih Ayyub akiwa kwenye kitanda cha mauti na kufa akiacha dola katika hatari hiyo. Kutokana na hali hiyo, mamaaliks walijikusanya na kuamua kupambana na wavamizi hao na kufanikiwa kuwashinda. Katika kipindi hicho alitokea mtu katika historia mtu aitwaye Baybars. Mtu huyu ndiye muasisi hasa wa Dola ya mamaaliks. Mamaaliks walitawala Misri huku Bani Ayyub wakibaki kuwa maliwali wa Syria. Lakini hali hiyo haikudumu, kwani mwaka 1260 Wamongoli, wakiongozwa na Holaco walikuwa wakielekea upande wa mashariki ambapo waliivamia Baghdad na kuukomesha utawala wa Bani Abbas katika eneo hilo, wakaiharibu nchi na kuukanyagakanyaga ustaarabu wake. Baada ya hapo walielekea Damascus na kukumbwa na yale yalioikumba Baghdad. Walimtisha Al-Sultan Qutuz aliyekuwa ameteuliwa kuwa liwali katika Cairo mwaka (1259-1260). Hivyo Qutuz akawaunganisha Waislamu na BayBars akaungana naye. Wote wawili walisonga mbele kwenda kupambana na Wamongoli. Walipita kwenye kambi za majeshi yao zilizokuwa Gaza wakawashinda na kusonga mbele mpaka majeshi yao yalipokutana eneo la Ein Jalout (Marj Ben Amer). Hapo majeshi ya pande mbili yalikabiliana katika mapambano makali ya mwezi Septemba 1260 A.C na Mamaaliks kupata ushindi. Ushindi huu ulileta athari ya kihistoria magharibi mwa Asia. Baada ya hapo, Baybars alichagiza na kusisitiza kwa

52
nguvu zote juu ya kuwaondosha Wazungu katika maeneo hayo. Hivyo, alimuua Qutuz na kushika madaraka na mwaka 1260 1277) alipewa jina la Al-Zahir, yaani mfalme mpambanaji.

Himaya ya Uthmaniyya Mwanzoni mwa kipindi hiki, utawala wa mamaaliks ulifikia kikomo. Nchi nyingi za ulimwengu wa kiarabu zilikuwa zimejiunga na dola ya Uthmaniyya iliyotawala kwa takriban karne nne. Dola ya Uthmaniyya iliyokuwa na makao makuu yake mjini Istanbul Ushawishi na nguvu zake zilitandaa hadi Balqan na Anadul kwa kipindi cha karne mbili za vita na mapambano ya upanuzi. Uwepo wa dola hii kuu na imara katika eneo hili ulisababisha kuzuka kwa mgogoro wa kugombania maeneo ya utawala baina ya dola tatu, ambazo ni: Dola ya Uthmaniyya, Dola ya Safawiya iliyoibuka huko Tabreez, Dola ya Mamaaliks. Mnamo Agosti 1514 A.C. vita vya kwanza vya wazi vilizuka baina ya dola ya Uthmaniyya ikiongozwa na Saleem wa kwanza (Saleem the First) na Dola ya Safawiya ikiongozwa na Shah Ismail, vita vilivyopiganwa katika eneo la Jaldiran jirani na Tabreez. Katika vita hivyo, WaUthmaniyya walipata ushindi kutokana na umahiri wao katika kutumia bunduki za moto. Miaka miwili baadaye, WaUthmaniyya waliwashinda Wamamaalik katika vita vya wazi vilivyopiganwa katika eneo la Marj Dabeq karibu na Aleppo mnamo tarehe 23, Agosti, 1516. Huo ndio ulikuwa mwisho wa utawala wa Mamaalik baada ya WaUthmaniyya kuitwaa Misri.

53

Saleem wa kwanza (Saleem the First): Mwaka huohuo Saleem aliitwaa Syria bila upinzani wowote kwa sababu wakati huo Wasyria kwa upande mmoja walikuwa wakiwachukia Wamamaalik na kwa upande mwingine walikuwa wakiwahofia Waottoma. Baada ya kifo cha Saleem, mwanaye Sulaiman aliingia madarakani (1520 1566) ambaye kutokana na kutumia sheria nyingi katika kuendesha mambo ya Dola alipewa jina la mwanasheria au mtaalam wa sheria au mwanazuoni wa sheria. Katika enzi za Sulaiman, Himaya ya Uthmaniyya ilistawi sana, kupanuka na kutandaa na hata kujumuisha mabara matatu. Vile vile waliyachukua maeneo yote yaliyokuwa yakitawaliwa na ukhalifa wa Bani Abbas na Himaya ya Byzantine na hivyo, Istanbul ikawa makao makuu ya ulimwengu wa Kiislamu na ustaarabu wa kislaamu ukahuishwa. Lakini baada ya kuvumbuliwa kwa Amerika na Cape of Green Hope sambamba na kufufuka kwa elemu na maarifa huko Ulaya, ushawishi na nguvu vikaanza kuhamia Magharibi.

Zaher Al-Omar Al-Zidany: alizaliwa mwishoni mwa muongo wa mwisho wa karne ya kumi na saba. Kufuatia kifo cha baba yake, alichukua utawala wa vijiji viwili vya Arbah na Al-Damon vilivyopo Palestina. Baadaye alianza kupanua ushawishi wake kwa kuungana na Makabila ya Kibedui kwa upande mmoja. Aliingia katika migogoro ya mpakani alipokuwa akijizatiti kuliimarisha jeshi lake na kuweka ngome kwenye maeneo yaliyokuwa chini ya utawala wake akitumia fursa ya Waturuki kushughulishwa na vita dhidi ya Warusi. Alianzisha jeshi kubwa la kutisha nchini Palestina, akaitwaa miji ya Haifa, Yafa, Alid na Nablus. Baada ya kipindi kifupi cha utawala wake uliokuwa umezungukwa na migogoro na mapiganao, nguvu zake zilianza kudhoofika na akazungukwa na manowari za WaUthmaniyya, jeshi

54
kubwa likaenda kumteketeza na kumpiga kwa dhoruba kubwa. Utawala wake ulifikia kikomo kwa kifo chake, na kwa kuwa watoto wake hawakuwa na sifa za kutawala baada ya kifo chake jambo lililomfunguliaa Ahmad Al-Jazar (Agha) njia ya kutwaa madaraka.

Ahmad Pasha Al-Jazar: Agha Ahmad (maarufu kama Al-Jazar) alitokea kwenye ushuhuda wa matukio mjini Acre, alikuwa Mmamaalik mwenye asili ya Bosnia. Alitwaa madaraka ya Serikali ya Sayda na Damascus kwa vipindi tofautitofauti kati ya mwaka 1775 mpaka alipofariki dunia mwaka 1804. Utawala wake ulisifika kwa udhibiti wa majeshi ya ndani ya Palestina, na milima ya Lebanon. Aliwakaidi WaUthmaniyya na kuilijumuisha jimbo la Damascus kwenye utawala wake.

Safari ya Napoleon Bonaparte (1798 1801): Safari ya kijeshi iliyochagizwa na Napoleon dhidi ya Misri na Bilad Al-Sham inaweza kuashiria mwanzo wa ukoloni wa Kizungu dhidi ya eneo la Arabia uliofuatia mapinduzi ya kiviwanda yaliyoshuhudiwa na Ulaya. Baada ya ushindi alioupata dhidi ya Mamaalik na kuingia Cairo Juni 1798, Napoleon Bonaparte aliongoza msafara wa jeshi lake kwenda Bilad Al-Sham. Msafara huo haukwenda nje ya Palestina na maeneo yake ya pwani, isipokuwa kwenda Al-Naserya na Tabarya, ambapo jeshi hilo lililishinda jeshi la Uthmaniyya. Harakati hiyo ilianza kwa kuitwaa Katyah ya Sinai na kuelekea kwenye Kasri la Arish (arish Castle). Miezi mitatu baadaye jeshi hilo lilianza kurudi nyuma kuelekea upande wa Misri baada ya kushindwa vibaya huko Acre katika mwezi wa Mei mwaka 1799. Mnamo Februari 28, 1800, jeshi la Kifaransa likiongozwa na Kleber lilisonga mbele kuelekea Asdoud, kisha kijiji cha Bayneh, Al-Ramlah na Yafa. Aidha waliitwaa Hifa baada

55
ya mapigano makali. Walielekea Acre, mji ambao ulisifika kwa milango yake madhubuti na ngome zake imara zilizozuia mashambulizi na hujuma za maadui. Mapambano makali yalitokea mahali hapo na wakazi wa Acre wakisaidiwa na majeshi ya kiingereza na baadhi ya majeshi ya WaUthmaniyya walilishambulia vikali jeshi la Wafaransa. Napoleon alijaribu zaidi ya mara saba kuingia katika ngome za Acre bila mafanikio. Hata hivyo muda mfupi baadaye Kifo Cheusi kilionesha uso wake wa kuogofya kikizitaka roho za majeshi ya wafaransa. Katika mwezi wa Mei 1800, Napoleon aliiandikia serikali kuu mjini Paris akiwataarifu kuwa kuitwaa Acre ni jambo lililokuwa na hasara kubwa na kwa hiyo aliamua kuyaondoa majeshi yake na kurudi Misri kuendeleza harakati zake huko. Ni katika kipindi hicho ambapo ujumbe kutoka Paris ulimfikia Napoleon na kumweleza kuwa analazimika kurudi Ufaransa. Alisalimu amri mwezi wa Mei 1800 baada ya mzingiro wa vita uliodumu kwa muda wa siku 64.

Kampeni na harakati za Muhammad Ali

Baada ya Napoleon kuyaondoa majeshi yake, Al-Jazar alirejea na kulazimisha uhalali wa mamlaka yake juu ya nchi husika. Alirejea akiandamana na udhalimu uliozidi baada ya kuwakalifisha watu kwa mizigo mikubwa wa kodi aliyoitoza ili kufidia hasara aliyoipata katika vita. Hata hivyo muda mfupi baada ya kukalia kiti cha utawala alifariki dunia mwaka 1804. Kufuatia kifo chake, madaraka yake yalirithiwa na mfuasi wake (Mmamaalik) Soliman Pasha aliyejulikana kwa jina la Al-Adil (mwadilifu) ikiwa ni kinyume na jina la AlJazar (mchinjaji). Utawala wake ulipatana na ule wa Muhammad Ali wa Misri na ule wa Mahmoud II wa Istanbul. Utawala wa Soliman Pasha ulisifika kwa uthabiti na ujenzi mpya wa miundombinu ya nchi. Hali hio iliendelea kuwa hivyo hadi alipokuja Ibrahim Pasha mwaka 1819 1831, ambaye alifuata sera za Al-Jazar zilizoamsha na kuchochea hasira za

56
viongozi wa kijamii walioibua maasi mengi. Mnamo tarehe moja ya mwezi wa Oktoba 1831, Muhammad Ali aliandaa jeshi kwenda Palestina. Jeshi hilo lilikuwa chini ya uongozi wa mwanaye Ibrahim Pasha ambaye aliitwaa miji ya Gaza, Jaffa (Yafa), Jerusalem na Galilee bila upinzani wowote, na baada ya miezi sita ya kuizingira Acre hatimaye mji huo uliangukia mikononi mwake. Kisha alielekea Damascus na kuingia hapo mnamo tarehe 14 Juni 1832, ambapo yalitokea mapambano karibu na eneo la Homs. Mapambano hayo yalikuwa baina yake na jeshi la WaUthmaniyya ambapo aliwashinda na kuitwaa miji ya Halab, Hamah, na Antakya. Kufuatia vita vya Billan Juni 30, 1832, aliingia ndani zaidi ya Asia Ndogo (Anatolia), akwashinda WaUthmaniyya kwenye mji wa Konieh tarehe 21 Disemba 1832 ambapo alifanikiwa kumteka waziri mkuu. Kutokana na mfululizo wa ushindi huo, nchi za Ulaya ziliingilia kati kwa lengo la kuweka maridhiano, ambayo yalipelekea kusainiwa kwa mkataba baina ya pande mbili hasimu. Mkataba huo ulijulikana kama Makubaliano ya Kutaya (makubaliano ya Mei 1833). Makubaliano hayo yalipelekea Sultan Mahmooud II kuutambua utawala wa Muhammad Ali wa kuirithi nchi ya Misri na Bilad Al-Sham. Hata hivyo, utawala huo wa misri haukudumu muda mrefu (miaka tisa tu). Kwani baada ya Wamisri kuondoka kutoka eneo la Bilad Al-Sham, eneo hilo likarudi chini ya mamlaka ya WaUthmaniyya baada ya uingiliaji kati wa mataifa ya Ulaya yakiongozwa na Uingereza. Kitendo hicho kilipanua uwepo wa Ulaya katika eneo hilo na baadaye mataifa hayo yakazidi kujichomeka ndani zaidi kutokana na udhaifu mkubwa ulioikumba serikali. Sababu ya nchi za Ulaya kujaribu kuingilia mambo ya ndani ya eneo hili, hususan Bilad AlSham, ilitokana na masalahi ya kiuchumi na kimkakati waliyokuwa nayo katika eneo la Mashariki ikiwa ni pamoja na kuchukulia waumini wa dini zenye wafuasi wachache na haki zao za kiraia kama hoja ya kuingilia mambo ya ndani ya serikali ya WaUthmaniyya. Aidha, idadi ya mabalozi wan chi hizo katika mamlaka za kisultani iliongezeka, na nguvu zao zikapanuka baada ya uingiliaji wao kufika katika serikali, uongozi mbali mbali, uchumi, mahakama, na masuala ya raia. Balozi maarufu miongoni mwao ni Balozi wa Uingereza

57
Woods aliyekuwa akifanya kazi kama gavana halisi wa nchi hizo ndani ya joho la usimamizi wa mabadiliko. Aidha, nchi za Ulaya zilisonga mbele katika kuchochea makundi ya kijami, kidini na kitaifa dhidi ya serikali kuu na kuongeza wasiwasi na maasi dhidi yake katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuidhoofisha serikali na kushirikiana nayo katika maeneo yenye ushawishi. Kwa upande mwingine, mabalozi hao waliyashikilia masuala ya Wakristo wachache na kupanua ulinzi wao kwa makundi ya kiyahudi ya mjini Jerusalem na maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na kuyatunza makazi ya wahamiaji wa mwanzo wa Kiyahudi. Mbali na hilo, harakati hizi za kimishionari zilishuhudia ongezeko kubwa, ambapo walizielekeza juhudi zao katika mji wa Jerusalem. Hadi mwishoni mwa karne ya kumi na tisa, idadi ya Wamishionari katika mji wa Jerusalem ikilinganishwa na wakazi wengine ilikuwa kubwa sana kuliko eneo lolote lile duniani. Ilipodhihirika kuwa Himaya ya WaUthmaniyya ilikuwa ikielekea ukingoni, kila mtu alifanya haraka kuandaa mahali pa kuweka mguu wake na kuithibitisha nguvu yake kwenye sehemu ya ardhi yake baada ya kuigawa. Sasa tutakichunguza kipindi kilichokuja baada ya utawala wa kiislamu nchini Palestina na mwanzo wa ujio wa wazayuni katika eneo hili la Arabia. Uchunguzi wetu utatokana na chanzo zhetu kile kile, yaani kituo cha Kitaifa cha Habari za palestina kilichopo chini ya mamlaka ya Palestina. Kituo hiki cha Kipalestina kina uhusiano na vyanzo vingi vinavyothibitisha hatua hii ya Historia ya Palestina ambayo tuatainukuu katika ahatua za mwisho. Hivyo,Wazayuni walianza kupenya lini katika eneo hili la Kiislamu la Palestina?

Makazi ya wazayuni nchini Palestina Ni jambo la muhimu kueleza kuwa katika kipindi hicho cha karne ya kumi na tisa, katika Bilad Al-Sham na Palestina, palitokea kile kijulikanacho kama mwamko wa kitaifa pamoja na dhana yake mpya ambayo nguzo zake zilidhihirika huko Ulaya kutokana na maendeleo

58
ya ubepari. Kutokana na uibukaji wa utambuzi huu wa kitaifa, sanjari na mwamko wa kifikra na kiutamaduni ulioibuka katika umma huu wa Kiarabu uliokuwa ukipigania kuwa na umoja, uhuru na udhibiti wa rasilimali zake za kiuchumi, iliibuka hali ya maasi ya umma wote dhidi ya majeshi yote ya kigeni yaliyojiingiza katika umma huu wa Kiarabu. Kwa hiyo tangu mwanzo pakawepo na mwamko wa kizalendo kupinga na kuzuia uwepo wa makazi ya Wazayuni nchini Palestina. Hata hivyo, juhudi hizo hazikuwekwa katika muundo wa pamoja wenye misingi ya kimkakati kwa lengo la kufuatilia programu maalum, kinyume na harakati za Wazayuni ambazo, muda mfupi baada ya kongamano la wazayuni lililofanyika mjini Basel Switzerland mwaka 1897, waliunda vyama na oganaizesheni zao kwa ajili ya kufikia malengo yao. Inaelazwa kuwa wakati wa utawala wa WaUthmaniyya, serikali haikupinga Wayahudi kuishi katika maeneo yake, bali ilikataa wao kuhama kutoka katika nchi nyingine na kuja kuanzisha majimbo yao na kuelekea katika namana ya pekee katika eneo la Palestina. Tangu wakati huo, Baraza Kuu (Sublime Porte) likatoa muongozo kwa mabalozi wake wawaambie Wayahudi wanaotaka kuhamia Palestina kwamba hawakuruhusiwa kuishi Palestina kama wageni na kwamba wanatakiwa kupata uraia wa WaUthmaniyya huku wakisubiri mabadiliko ya lazima ambayo yangelazimishwa kuwpo katika majimbo na maeneo wanayotaka kuishi. Licha ya msimamo rasmi wa serikali ya WaUthmaniyya, kulikuwepo na ongezeko la dhahiri katika harakati za makazi ya Wazayuni nchini Palestina lililotokea kwa njia potofu, na kutokana na uungwaji mkono kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje, na kwa kuwapa hongo wafanyakazi wa serikali ya WaUthmaniyya ambao walishindwa katika baadhi ya mazingira kutokana na mbinyo na msisitizo usiokoma. Mbali na hilo, juhudi za Wayahudi kunua ardhi na kujenga makazi hazikusimama hata kidogo. Historia yatwambia kuwa kutokana na ongezeko la harakati za ujenzi wa makazi ya Wazayuni pamoja na majaribio ya kutwaa ardhi kwa njia yoyote ile, kwa halali au kwa namna isiyokuwa ya halali, vuguvugu la upinzani wa Waarabu liliongezeka, hususan

59
miongoni mwa Wakulima na watu wa mashambani waliopambana kupinga makazi hayo kujengwa katika ardhi zao jambo ambalo lingepelekea wao kufukuzwa. Upinzani huo uliongezeka na kuenea katika vijiji na miji mingi, na upinzani huu wa wananchi hawa dhidi ya harakati hizo (za makazi ya Wayahudi) ulifikishwa kwenye bunge la Uturuki kupitia kwa viongozi wa Kipalestina. Aidha kulikuwa na shambulio kali kutoka chama cha upinzani kikiilaumu serikali kwa kutokomesha vitendo hivyo. Hata hivyo, nguvu za kisiasa za Wazayuni ziliendelea kuongezeka, na makazi ya Wazayuni yakaungwa mkono katika awamu ya pili ya uhamiaji mwaka 1904-1919. Yote haya yalitokana na ufisadi wa uongozi wa Waottoam wa wakati huo pamoja na baadhi ya WaUthmaniyya waliokuwa wanachama wa chama cha free mason kuwa na ushirika na Wayahudi wa Donma waliokuwa wakitekeleza malengo ya Kizayuni, sambamba na mabalozi wa nchi za nje kuunga mkono vitendo hivyo.

Mandeti ya Uingereza Kipindi cha kabla ya Mandeti ya Uingereza Vuguvugu la Kizayuni lililokuwa limeshamiri miongoni mwa Wayahudi wa Ulaya liliibuka mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Neno Zayuni (Zionism) linatokana na neno la Kihebrew (Kiebrania)   Tziyyon, ambalo ni jina la mlima uliopo kusini-magharibi  , mwa Jerusalem na kujulikana kwa Wayahudi kwa jina la Zayuni Zion. Wayahudi huenda kuhiji katika eneo hili kwa kile wanachoamini kuwa Mfalme Daudi (a.s.) alizikwa mahali hapo. Inatambulika kuwa katika kipindi hicho na kabla ya kipindi hicho Wayahudi walikuwa katika makundi makundi tu yaliyotawanyika ulimwenguni, wakiwa hawana muungano wa kisiasa, kiuchumi, kijamii au wa urithi, isipokuwa kamba ya dini pekee ndiyo iliyowafunga

60
pamoja. Jambo hili lilitokana na makundi haya kunywea na kufifia katika jamii walizoishi. Aidha, madai ya Wazayuni ya kuwepo kwa taifa la Kiyahudi ni madai ya uwongo, kwa sababu makundi hayo yalikosa sifa na nguzo zinazounda taifa, ambazo ni uwepo wa taifa moja, eneo moja wanaloishi, lugha moja, tabia na desturi zinazowaunganisha wote. Fikra ya Uzayuni iliibuka ndani ya Ulaya tangu karne ya kumi na sita na kusatawi katika mazingira ya kisiasa yaliyokuwepo huko katika karne ya kumi na tisa (mazingira ya majaribio na kubahatisha), na hususan mwaka 1870. fikra ya Uzayuni iliasisiwa kwenye misingi ya uanzishaji wa makao ya taifa la wayahudi nchini Palestina. Hayo yalitokana na mapatano yaliyofikiwa kati ya vuguvugu la Kizayuni na himaya ya Uingereza kwa msingi wa azimio la Balfour la mwaka 1917. Majeshi ya Kingereza yalipofanikiwa kuingia katika nchi hizo kwa ghiliba na hila, walipokelewa kwa moyo na ukunjufu kama watu waliokusudia kulita uhuru sio kama majeshi ya uvamizi, lakini baada ya kuwasili kwa Kamati ya Kizayuni, Waarabu wakatambua hatari iliyokuwa imejificha, ambapo serikali ya Waingereza iliruhusu kutumwa kwa kamati hiyo nchini Palestina ili ikamilishe hatua za muhimu za utekelezaji wa azimio la serikali kuhusu uanzishaji wa taifa la Wayahudi nchini Palestina chini ya mamlaka ya Jenerali wa Kiingreza (Britishi General), na wakati huo huo iondoshe shaka ya Waarabu kuhusu uhalisia wa nia ya wazayuni. Aidha, uongozi jeshi la wavamizi ulitekeleza mpango wa kuiandaa kidogo kidogo Palestina kuwa makao ya taifa ya Wazayuni kwa njia na mbinu zozote zile. Ni vigumu kuamini kile kilichotokea kufuatia ujio wa Kamati ya Kizayuni, ambacho ni uanzishwaji wa nchi ya Wayahudi ndani ya nchi ambayo asilimia 92 ya wakazi wake ni Waarabu wa Kipalestina.

Mandeti ya Uingereza nchini Palestina: 1923-1948

61
Mwanzoni mwa kipindi hiki Uingereza ulichukua ahadi (mandate) ya kuiongoza Palestina kwa mujibu wa agano la Ushirika wa Mataifa (League of Nations Covenant) japokuwa Uingereza haikuhitaji kuanza kutekeleza vipengele vya makubaliano hayo kwa sababu tayari ilikuwa ikiitawala Palestina miaka mingi kabla ya kutolewa kwa mandeti hiyo, na hilo lilitokana na sera ya ukoloni wake wenye mrengo wa Kizayuni uliyokuwa umeegemea kwenye misingi ya ukandamizaji na matumizi ya nguvu za jeshi mpaka kufikia mwaka 1948. Katika kipindi hicho makundi vyombo na taasisi husika za ndani ya nchi hazikuonesha maendeleo yoyote, hivyo Waarabu hawakuwa na kimbilio jingine isipokuwa kuwasilisha malalamiko yao kwenye kamati ya kudumu ya Mandeti mjini Geneva. Lakini kamati hii haikuwa na mamlaka yoyote ya kufanya uchunguzi na kufuatilia mambo ynayoendelea katika nchi zilizowekewa Mandeti. Kwa hiyo katika kipindi chote cha mandeti ya Uingereza Wananchi Waarabu wakawa hawana kimbilio jingine zaidi ya kufanya migomo, upinzani, maandamano pamoja na ukaidi na uasi wa kiraia, mambo yaliyosababisha mapambano makali na askari wa Kiingereza na walowezi wa Kiyahudi kwa upande mmoja na kwa uapande wa pili Wananchi wa Kipalestina. Mwaka 1924, Kamishna Mkuu Herbert Samuel aliandaa mradi mpya wa kifedha kwa Palestina na mnamo Februari 1927 sheria ya sarafu ya Kipalestina ilitolewa, lakini watu waliituhumu serikali kwamba isingeweza kubuni kila ilichokitaka pasipo udhibiti kwani kufanya hivyo kungeuathiri uchumi wa Waarabu. Sambamba na hilo, juhudi za Kamishna Mkuu zilizaa matunda kwa kuweka sheria ya uraia wa Kipalestina. Kwa mujibu wa sheria hiyo, Wayahudi waliokwisha kuwa na makazi walipewa uraia halali wa Palestina. Wakati wa vikao viwili vilivyofuatana vya Ushirika wa Mataifa (1924-1925), serikali ya Waingereza ilieleza wazi kuwa haikuridhia uanzishwaji wa bunge la kutunga sheria nchini palestina ambalo lingeundwa kwenye msingi wa uwakilishi unaolingana (proportional repsentation), ambapo Waarabu wangekuwa na wingi uliozidi, kwa sababu ingekuwa kikwazo dhidi ya mpango wa serikali wa maandalizi ya makao ya taifa la Wayahudi. Baada ya kipindi cha utawala wa Kamishna Mkuu Herbert Samuel kufikia kikomo, Lord Herbert Charles Blumer aliteuliwa kuwa

62
Kamishna Mkuu nchini Palestina. Uteuzi huo ulifanyika mnamo August 1924, na kudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mwezi Machi 1925, Balfour alifanya ziara mjini Jerusalem kushiriki uzinduzi wa chuo kikuu cha Wayahudi kilichokuwa kimejengwa kwenye ardhi ya waarabu kwenye eneo la mlima Al-Zaytouun, eneo ambalo serikali ya Waingereza ililitwaa kwa nguvu kutoka mikononi mwa wamiliki wake na mwaka 1918 wakawapa Wazayuni. Kutokana na ziara hiyo, yalifanyika maandamano makubwa na Palestina ikatangaza mgomo mkubwa kupinga ziara ya Balfour, jambo lililozilazimu mamlaka za Kingereza kumsafirisha Balfour hadi Beirut na kupanda meli moja kwa moja kuelekea nchini mwake. Imethibitishwa kuwa katika kipindi cha miaka kumi ya mwanzo ya mandeti ya Uingereza, Wahamiaji wa Kiyahudi wapatao 76400 waliinga Palestina, wengi wao wakitoka katika nchi za mashariki mwa Ulaya. Kutokana na ongezeko la kuendelea kwa vitendo vya uhamiaji, Waarabu walihisi kuwa kuna ulazima wa kupinga vitando hivyo vya Wazayuni sambamba na kupinga kitendo cha mamlaka husika kuwa na upendeleo wa wazi kwa vitendo hivyo. Hivyo mapinduzi yakalipuka. Mapinduzi hayo yalichochewa na tukio laAl-Buraq la mwezi Septemba 1928 baada ya Wayahudi kujaribu kuutwaa ukuta wa magharibi wa msikiti wa Al-Aqsa ambao ni mali ya Waislamu. Kitendo hicho kilipelekea Waarabu wa eneo la Arabia kuliunga mkono suala la Wapalestina, na huo ukawa mwanzo wa kile kilichokuja kujulikana kama Mapinduzi ya Buraq yaliyoshuhudia matukio ya umwagikaji wa damu ambapo Waarabu walianza kuzishambulia wilaya za Wayahudi za Al-Khalil (Hebron), Nablus, Bysan na Safad. Kutokana na hali hiyo, majeshi ya waingereza yaliibuka kuwaunga mkono Wayahudi wakitumia jeshi la anga, jeshi la ardhini na silaha nzito nzito na kufanya kila aina ya uonevu na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wa Kiarabu ambao waliwageukia wanajeshi wa Kimisri ili kupata msaada. Majsehi hayo (ya Uingereza) yaliviaharibu vibaya sana vijiji vingi kama vile Deir Yassin, Lifta na vingine vingi. Zaidi ya

63
watu elfu moja walipelekwa mahakamani, wengi wao wakiwa ni Waarabu, na watu 26 walihukumiwa adhabu ya kifo, ambao ni waarabu 25 na Myahudi mmoja tu. Mwaka 1930, idadi ya wahamiaji wa kiyahudi ilifikia 104.750, na katika miaka sita iliyofuata idadi hii ilifikia watu 284.645, ikiwa na maana ya ongezeko la 164%. Idadi hii haijumuishi wale walioingia nchini kwa njia za haramu. Kwenye kilele cha kumbukumbu za Al-Isra (Safari ya Usiku)
(1)

na Al-Miraj (kupaa kwenda mbinguni)

za Disemba 1931,

lilifanyika kongamano Kiislamu lililohudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi ishirini na tatu za Kiislamu sambamba na viongozi mbalimbali wa kitaifa katika ulimwengu wa Kiarabu. Wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mufti Muhammad Amin Al-Hussainy, alisisitiza juu ya nafasi na umuhimu wa Palestina na msikiti wa Al-Aqsa katika ulimwengu wa Kiisalmu.

(1) Safari ya kimiujiza ambayo Mtume (s.a.w.) alichukuliwa usiku kutoka Al- Masjid AlHaram (Makkah) kwenda msikiti wa mbali (Jerusalem). (2) Tukio la Kimiujiza la Mtume (s.a.w.) kupaa kutoka Jerusalem kwenda Mbinguni kukutana na Mola Wake.

Pamoja na hayo, kongamano lilishutumu na kulaani vikali Uzayuni, sera za Kiingereza nchini Palestina na suala la Wayahudi kuhamia nchini humo. Kongamano lilitoka na maamuzi ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Jerusalem, kugomea bidhaa zote za Wayahudi katika maeneo yote ya Kiislamu, na uanzishaji wa kampuni ya kilimo nchini humo kwa lengo la kuzikomboa ardhi za Waislamu. Mwezi Julai 1931, taarifa rasmi ilitolewa kumteua Jenerali Arthur Grenfell Wauchope kama Kamishna Mkuu nchini Palestina. Wauchope aliwasili Palestina Palestina akiwa na muongozo wa kutia nguvu suala la uanzishaji wa makao ya taifa la Wayahudi. Muongozo huo ulitoa maelekezo ya kutumia mbinu za kuchelewesha na kusimamisha utekelezaji wa matakwa ya Waarabu sanjari na kuongeza idadi ya raia wa Kiyauhudi kuwa kubwa nchini Palestina huku wakipendekeza miradi ya urongo na batili kwa lengo la kuwashughulisha Waarabu na kuwapoteza njia. Mwezi Agosti 1932, azimio la kuanzisha Chama cha kudai Uhuru lilitolewa. Chama hicho kilikuwa na dhamana ya kufanya jitihada dhidi ya ukoloni, kupiga vita suala la uhamiaji wa Wayahudi, na kufanya juhudi za kufikia umoja na muungano wa Waarabu. Wapigania uhuru hao walirejea mara kwa mara upinzani wao dhidi ya Hati ya Balfour na Mandeti ya Kiingereza. Aidha, walifichua kuwa robo moja ya bajeti ya nchi ili kuwa imetengwa kwa

64
ajili ya masuala ya ulinzi na usalama kwa sababu serikali ilikuwa ikifanya juhudi za kujenga makao ya nchi ya wageni kinyume na utashi wa Wapalestina. Mwanzoni mwa mwaka 1932, lilifanyika kongamano la vijana wa Kipalestina mjini Yafah kwa lengo la kuzungumzia azma ya kujiandikisha katika huduma ya Vuguvugu la Kitaifa. Mwishoni mwa mwaka 1934, kwa mujibu wa Kamati ya Bill, idadi ya wahamiaji wa Kiyahudi ilifikia 42.359 ikilinganishwa na 30327 ya mwaka 1933, na idadiya wahamiaji 9553 ya mwaka 1932. Na mpaka mwishoni mwa mwaka 1935 idadi ya Wahamiaji wa Kiyahudi ilifikia 61854 waliokuja Palestina kutoka maeneo yote ya Ulaya. Aidha, takwimu rasmi zinaonesha kuwa mpaka mwanzoni mwa mwaka 1935, idadi ya wayahudi nchini Palestina ilikuwa mara mbili ya ile ya mwaka 1929, na hivyo Wayahudi wakawakilisha robo moja ya idadi ya wananchi wote. Mapinduzi ya Sheikh Eiz Al-Din Al-Qasam Mandeti ya Uingereza ilitambua hali tete iliyokuwepo Palestina baada ya nchi kushuhudia mapinduzi ya Sheikh Eiz Al-Din Al-Qasam, ambaye yeye pamoja na kundi la Mujahideen walijitolea nafsi zao kutetea ardhi ya Palestina. Aliuawa kishahidi mjini Jenin baada ya mapambano makali dhdi ya Wanajeshi wa Mandeti ya Kiingereza. Punde tu baada ya tukio hili, Uingereza ilimuamuru Kamishna Mkuu kuweka mradi wa Baraza la kutunga sheria mbele ya Waarabu na Wayahudi kama jawabu la maombi yaliyowasilishwa na bodi ya Vyama Vya kisiasa vya Wapalestina katika mwezi wa Novemba. Mradi huo ulieleza yafuatayo: 1. Pendekezo lililotolewa na serikali mwezi wa Disemba mwaka 1935 kuhusu mswada wa katiba mpya liliwakilisha hatua ya utekelezaji kuelekea kwenye utawala wa kidomokrasia, pindi ilipopendekeza Baraza la kutunga sheria (bunge) kwa wingi mkubwa usiokuwa rasmi. 2. Kuhusu uuzaji wa ardhi, serikali iliamua kupitisha sheria inayopiga marufuku uuzaji wa ardhi, isipokuwa kama mmiliki wa Kiarabu atakapojiwekeakipande cha ardhi kinachomtosheleza yeye na familia yake. 3. Kiwango cha wahamiaji wa kiyahudi kilihesabiwa kwa kina kulingana na ukubwa wa nchi, ofisi mpya ya takwimu ilianzishwa kutathimini kiwango hiki. Mapinduzi Makuu ya mwaka 1936 Na Mradi wa Kuigawa Palestina Mnamo Februari 1936, mapinduzi yaliibuka kufuatia tukio dogo, ambalo ni cheche iliyolipua hisia za Waarabu wa Palestina walioelezea kwamba hawawezi kuvumilia tena.

65
Mapinduzi hayo yalianza baada ya mhandisi (contractor) mmoja wa Kiyahudi kukataa kumuajiri kibarua mfanyakazi au kibarua yeyote Mwarabu katika ujenzi wa shule tatu mjini Yafah alizokuwa amekubaliana na serikali kuzijenga. Kufuatia hali hiyo, wafanyakazi wa Kiarabu walikusanyika eneo la shule hiyo na kuwazuia vibarua wa Kiyahudi wasifike eneo la ujenzi. Tarehe 15 Aprili, Myahudi mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya, ambapo Wayahudi walilipiza kisasi kwa kuwachinja wakulima wa Kiarabu ndani ya majumba yao. Hiyo ndiyo cheche iliyowasha moto, kwani matumizi ya nguvu yasambaa, na wasiwasi ukaongezeka nchi nzima, watu wengi wakapoteza maisha na kusababisha hasara kubwa kwa pande zote mbili. Kwa upande mwingine, uingiliaji wa jeshi la Waingereza kuzima maandamano ya Waarabu, ulisababisha hasara na vifo vingi vya Waarabu. Mgomo mkubwa ulitangazwa nchi nzima, na vuguvugu la upinzani wa kitaifa likaongezeka. Vuguvugu hilo lilikuwa katika mfumo wa makundi na kuwa na ngome kuu katika maeneo ya milimani. Kisha watu wengi kutoka mashariki mwa Jordan, Syria, Lebanon na Iraq walijitolea kuungana na wakazi hao. Kutokana na hali hiyo, makundi ya hayo ya upinzani yakageuka kuwa mapinduzi ya kitaifa yenye silaha na kuungwa mkono na matabaka yote ya watu. Wanamapinduzi walitumia njia mbalimbali za mapambano kama vile kuvunja madaraja, kubomoa reli na mabomba ya mafuta sanjari na kuzishambulia kambi za jeshi, kutupa makumbora katika maeneo yaliyokuwa na majeshi ya Uingereza. Kwa upande wa pili, majeshi ya Waingereza yalitumia ndege za kivita, deraya, mizinga kwa lengo la kuzima na kukomesha mapinduzi hayo, jambo lililoongeza zaidi maasi ya wananchi. Wakati huo huo, kulikuwa na juhudi kwa upande wan chi za Kiarabu za kufanya usuluhishi. Juhudi hizo zilikuwa baina ya Kamati Kuu ya Waarabu na serikali ya Uingereza, ambapo tarehe kumi Oktoba wito wa pamoja ulitolewa kwa upande wa mfalme Bin Saaud, mfalme Ghazi, na mwanamfalme Abdullah kwenda kwa Mkuu wa Kamati ya Waarabu na kwa Waarabu wa Palestina, ambapo walieleza yafuatayo: Sisi tumeumizwa sana na hali ya sasa nchini Palestina, na Sisi pamoja na Wafalme wa

nchi za Kiarabu na mwanamfalme Abdullah, tunakuiteni kwenye hali ya amani na kusimamisha umwagaji damu, kutegemeana na nia nzuri ya wenzetu, serikali ya Uingereza, ambayo imetangaza tamaa yake ya kutenda haki, tukiwa na imani kwamba tutaendelea kuongeza juhudi katika kukusaidieni.

Kufuatia maelezo hayo, Kamati Kuu ya Waarabu (Supreme Arab Committee) ilitangaza kumaliza mgomo na ikawataka watu kusali kwa ajili ya roho za waliokufa shahidi ambao idadi yao ilifikia Waarabu elfu mbili. Mradi wa kuigawa Palestina Tarehe 7 Juni 1937, Kamati ya Kifalme (Royal Committee) ikiongozwa na Lord Bill ilitoa ripoti iliyoshughulikia maoni na mtazamo wa viongozi wa Kiarabu na Kiyahudi. Kamati ilishauri kuwa suala la Palestina lisingeweza kutatuliwa isipokuwa kwa msingi wa maoni ya kuigawa Palestina. Vipengele vikuu vya mradi huo vilikuwa kama ifauatvyo:

66
1. Kuanzisha taifa la Kiyahudi linalogawanya eneo la kaskazini na magharibi mwa Palestina. Taifa hilo litatambaa pwani yote kuanzia mipaka ya Lebanon mpaka kusini mwa Jaffa, likijumuisha Acre, Haifa, Safad, Typerias, Nazareti na Tel Aviv. Taifa hilo litafungamanishwa na Uingereza kwa mkataba wa urafiki na udugu. 2. Maeneo Matakatifu yatakuwa chini ya hifadhi (Mandate) ya Uingereza ikiwemo Jerusalem na Bathelehem. Maeneo hayo yataunganishwa na Jaffa kwa njia maalumu inayohusisha maeneo ya Ramla na pia Nazareti, na hifadhi (Mandate) hiyo itakuwa na jukumu la kuyalinda maeneo hayo. 3. Ardhi za Wapalestina zitajumuisha maeneo ya kusini na mashariki mwa Palestina, ikiwemo mji wa Jaffa mpaka kusini mwa Jordan. Itafungamanishwa na Uingereza kwa mkataba wa urafiki na udugu. 4. Taifa la Wayahudi litatakiwa kutoa msaada wa kifedha kwa taifa la Kiarabu, ambapo Uingereza itatoa pauni (sterling) milioni moja kwa taifa la Kiarabu. 5. Kitu kinachoitwa kubadilishana watu kati ya taifa la Kiyahudi na lile la Kiarabu kitafanyika, ambapo Waarabu ambao idadi yao ni elfu 325 watahamishwa kidogokidogo kutoka katika taifa la Kiyahudi kwenda katika taifa la Kiarabu, na ardhi itaandaliwa kwa ajili yao katika eneo la Beersheba baada ya kukamilisha miradi ya umwagiliaji. 6. Mkataba wa ushuru utasainiwa baina ya hayo mataifa mawili mapema iwezekanavyo ili kuwa na ushuru wa pamoja kwa bidhaa nyingi za kutoka nje. Ama kuhusu makazi ya Wayahudi, maeneo ya ardhi yaliyochukuliwa na taasisi za Kizayuni na watu binafsi kwa mwaka 1936 yalifikia mita za mraba 1.200.000 (1.200.000 sq.m), na idadi ya makzi ikaongezeka mara dufu, ambapo idadi yake ilikadiriwa kufikia makazi 203, na hivyo idadi ya wahamiaji ikaongezeka kutoka wahamiaji elfu 30 mwaka 1927 na kufikia elfu 98 mwaka 1936. Radiamali ya Wapalestina kuhusu mradi wa kuigawa nchi yao ilidhihirika katika uasi usiokuwa na kikomo. Uasi huo ulipelekea ucheleweshaji wa kupitisha mradi huo. Mapinduzi yaliendelea kulipuka hadi vilipowaka vita vya pili vya dunia. Mnamo Novemba 23A38A.C. Malcom Macdonaid Waziri wa makoloni wa uingereza alitoa hotuba muhimu kwenye Bunge la wawakilishi (council of commons) akifafanua kuhusu hali halisi ya Palestina. Maelezo yake yalionyesha ufahamu aliokuwa nao juu ya msimamo wa Waarabu na maoni yao pale aliposema: Tatizo

la wakimbizi katika Ulaya ya kati kamwe halitosawazishwa kwa gharama ya Wapalestina bali linatakiwa kutatuliwa kwa uwanda mpana zaidi Aliendelea kusema : Waarabu wamekuwa wakiishi katika nchi hizo kwa karne nyingi zilizopita, lakini mawazo yao hayakutiliwa maanane wakati wa mkataba wa Balfour na hata wakati wa kubuni mandeti. Katika kipindi cha miaka ishirini ya vita vya mfululizo, Waarabuni wamekuwa wakitazama uingiliaji na uvamizi huo wa kimya kimya unaendeshwa na watu kutoka nje, na muda wote wamekuwa wakionyesha imani yao kwa upinzani wa wazi. Wametishwa na kuogopa kuwa mustakbali wao

67
katika uwanda wa uchumi siasa na biashara katika nchi yao utakabizishwa kwa watu hawa wapya (wageni ). Kama ningekuwaMwarabu nami ningeogopa na kutishika pia. Baada ya haya maelezo wafugwa waliachiwa huru mnamo tarehe

27 Desemba 1938 A.C. ilikuiruhusu Palestina na waarabu kushiriki katika kongomano lijalo la londoni. Wakati huohuo baadhi ya wajumbe wa Kiarabu kutoka Misri Iraq Saudi Arabia Yemen na Jordan ya mashariki walikwenda kwenye Mkutano huo. Mnamo tarehe 7 Februari 1939 kongomano la meza ya duara (Round table conference ) lilifunguliwa na bilamafanikio na mnamo tarehe 17 Mei1939 A.C serekali ya waingereza iltoa kile kilichojulikana kama The white book (kityabu cheupe) kikikusanya yafuatayo: 1. Katiba: Kipengele cha kumi kilieleza kuwa Ndani ya miaka kumi

Serekali ya kifalme inalenga kuunda serekali huru ya Palestina itakayofungamana na Uingereza kwa mkataba maalum
2. Uhamiaji: Serekali ya kifalme itawajibika kuruhusu upanuzi wa ardhi ya makao ya taifa la kiyahudi kwa njia ya uhamiaji kwa sharti kwamba uhamiaji huo uidhinishwe na waarabu. 3. Maeneo: Kifungu cha 16 ndani ya White Book kilieleza kwamba, Nchi hiyo itagawanywa katika maeneo mbalimbali. Kwa upande mmoja, uhamishaji wa ardhi kutoka kwa Waarabu kwenda kwa Wayahudi umepigwa marufuku. Kwa upande mwingine suala hilo limepambanuliwa huku katika upande wa tatu likiwa limeachwa wazi. Baada ya vita kuu ya pili, ulimwengu wa Kizayuni uligundua kuwa vita hivyo viliifanya Uingereza kuwa dhaifu, lakini ikiwa na nafasi muhimu machoni mwa Marekani ambayo iliendelelea kuwa na nguvu na kwamba Marekani ilikuwa na maslahi mbalimbali katika eneo la Mashariki ya Kati. Hivyo, ulimwengu wa Kazayuni uliongeza mara dufu harakati zake za kisiasa kupitia nafasi ya juu iliyokuwa nayo Marekani ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ndiyo taifa pekee lililokuwa na uwezo wa kuisukuma na kuishinikiza serikali ya Uingereza kutekeleza matakwa ya wazayuni. (Katika kufikia matakwa yao Wazayuni) walitumia njia mbalimbali, njia kuu ikiwa ni ya kidiplomasia kwani walitegemea nguvu na mkazo uliokuwa ukifanywa na wakala wa Uzayuni nchini Uingereza. Njia ya pili ilikuwa ni kutekeleza mikakati iliyowekwa kulingana na msukumo na shinikizo la Marekanai kwa serikali ya Uingereza. Njia ya tatu waliweka shinikizo kwa mbinu za vitisho na ukatili zilizotokana na undelezaji wa vitendo vya kigaidi na kufanya hujuma kali dhidi ya uongozi wa Mandeti. Mfumo wa Uzayuni na Wakala wa Wayahudi vyote kwa pamoja viliendelea kutekeleza kila walichotaka. Hivyo wakajaribu kuushawishi utawala wa Marekani, akiwemo Rais wa nchi hiyo Harry Truman ambaye muda mfupi tu baada ya kuingia Ikulu alituma ujumbe maalum kwenda kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Churchil. Hiyo ilikuwa tafrehe 24, Julai 1945. Vile vile, Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Atly katika ujumbe uliotumwa kwake tarehe 31 Agosti, 1945, aliombwa kuwaacha Wayahudi 100,000 waingie Palestina.

68
Katika kujibu ujumbe wa Marekani, mnamo tarehe 19 Oktoba, 1945A.C. Uingereza ilipendekeza kwamba Marekani ishirikiane nayo katika jukumu la kupangilia sera ya Palestina kwa kuunda kamati ya uchunguzi ya pamoja baina ya Marekani na Uingereza (Angola-American Inquiry Commiree) kudurusu na kulitafiti suala la Palestina. Mradi wa kuigawa Palestin: Mnamo Septemba 1947. A.C., Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa iliundwa kufuatia ombi la serikali ya Uingereza. Kamati hiyo ilijulikana kama UNSCOP UNITED NATIONS COMMITTEE ON PALESTINE (kamati maluum ya umoja wa mataifa kwa ajili ya Palestine). Kamati hiyo iliundwa na wanachama kumi na moja pasipo kujumuisha mataifa matano makuu ambayo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama. Hawakujumuishwa kwa madai kuwa ushiriki wao ungepelekea kuundwa kwa ripoti yenye upendeleo maalum. Wajumbe hao kumi na moja walichaguliwa kutoka mataifa ya Australia, Sweden, Canada, India, Czechoslovakia, Iran, Uholanzi, Guetemala, Peru, Uruguay na Yugoslavia. Jaji wa Kisweden ndiye aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo. Alitakiwa kuwasilisha ripoti ya kueleweka, mwezi wa Septemba, kutatua tatizo hilo kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati. Waarabu walipinga juu ya utumwaji wa kamati nyingine kwenda Palesstina, na hivyo wakapiga kura dhidi ya huo mradi. Mfumo na muundo wa hiyo kamati ulikuwa wa ubaguzi na upendeleo dhidi ya Warabu kwa sababu baadhi ya wajumbe wake ima walikuwa wakiunga mkono Uzayuni au walikuwa chini ya ushawishi wa Marekanai. Kamati ilikamilisha ripoti yake tarehe 31 Agosti, 1947 A.S., na kuituma kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo ilikuwa na mmapendekezo kumi na moja. Mradi wa kuigawa palestina ulikuwa na wito wa: Kuigawa palestina katika mataifa mawili, moja la Waarabu na jingine la Wayahudi. Sehemu ya eneo hilo itakuwa chini ya uangalizi (Mandate) wa kimataifa kwa usimamizi wa umoja wa mataifa. Asilimia ipatayo 56 ya nchi hiyo itakwenda kwa Wayahudi. Mataifa hayo mawili yatakuwa huru baada ya kipindi cha miaka miwili, kuanzia tarehe mosi Septemba, 1947 A.C., kipindi kinachowekwa kwa kila moja kupitisha katiba yake, kusaini makubaliano ya kiuchumi, kuanzisha umoja wa kiuchumi, kuunganisha ushuru wa forodha na sarafu. Vile vile, mradi huo unasisitiza na kukubali uwepo wa taasisi ya kuratibu uhamiaji wa Wayahudi. Baada ya mapendekezo hayo kuwekwa wazi, Bodi kuu ya Waarabu tayari ilikuwa imetangaza waziwazi kupinga mipango hiyo. Siku moja baada ya ripoti hiyo kuchapishwa, Golda Mayrson, Mwakilishi wa Ofisi ya Wazayuni alieleza moja kwa moja kukubaliana na vipendengele vingi muhimu vya mradi huo. -Waarabu kwa ujumla na Wapalestina kwa namna maalum walielezea kuudhika sana na mradi huo. Waarabu wote walionyesha kuudhika kwao kwa kufanya maandamano nchini Iraq, Syria, Lebanon na katika nchi nyingine nyingi za Arabia.

69
-Kwa hali hiyo mnamo tarehe 6 Septemba Kamati ya Siasa ya Muungano wa nchi za Kiarabu ilikutana mjini Soufar, Lebanon ili kudurusu yake yaliyokuwa katika ripoti ya kamati hiyo, ili waweze kuchukua hatua ya kisiasa ya pamoja Matokeko ya Mkutano huo ilikuwa ni kuchukuliwa kwa maamuzi yafuatayo: 1. Kamati ya siasa ina msimamo kwamba utekelezaji wa mapendekezo ya kamati husika ulikuwa na hatari kubwa ambayo inatishia usalama na amani ya Palestina nchi zote za Kiarabu. Hivyo, imeamua kupinga, kwa nguvu zote, ili kuzuia utekelezaji wa mapendekezo hayo. 2. Kamati imechukua msimamo wa kuwaweka wazi Waarabu wote juu ya hatari inayolikabili suala la Palestina. Hivyo, inatoa wito kwa kila mwarabu kutoa msaada na mhanga wowote anaoweza kuutoa 3. Kamati imeamua kuzijulisha serikali za Marekani na Uingereza, kwamba uamuzi wowote utakaochukuliwa kuhusu suala la Palestina pasipo kuelezea uundwaji wa taifa huru la Waarabu, uamuzi huo utasababisha vurugu na fujo ya hatari katika Mashariki ya Kati. 4. Kamati imeamua kuyaomba mataifa wanachama (wa muungano wa nchi za Kiarabu) kutoa msaada wa haraka sana kwa Wapalestina, kama vile fedha, silaha na wanajeshi. Kutokana na mradi wa kuigawa Palestina, Waarabu wa Kipalestina walianza kuleta upinzani dhidi ya harakati za ujenzi wa makazi ya Wazayuni, upinzani ulioungwa mkono na Waarabu wote. Upinzani huo ulienea maeneo yote ya nchi, vita vikali vikaripuka na kila aina ya silaha ikatumika, hali iliyopelekea kupoteza maisha ya watu wengi. Kutokana na msukosuko huo wa hatari, tarehe 19 Machi Baraza la Uslama la kimataifa lilikutana kwa lengo la kuidurusu hali tete ya Palestina. Ikadhihirika wazi kuwa mpango wa kuigawa nchi hiyo kamwe usingeweza kutekelezeka kwa amani. Hivyo, Wayahudi wakaamua kuzuia jaribio lolote litakalofanywa na Baraza la Usalama kutangua azimio la kuigawa palestina. Ili kuishinikiza Umoja wa Mataifa kupitisha sera hiyo (ya kuigawa Palestina), Wayahudi walifanya shambulio katika maeneo ya Nakhshoun lililowawezesha kukikamaa kijiji cha Waarabu cha Qastal katika jimbo la Jerusalem. Mnamo tarehe 9 Aprili, katika vita vikali Abdel QaderAl Husaini alifanikiwa kuwaondosha wayahudi katika kijiji hicho cha Qastal. Aliuawa kishahidi huko, lakini masaa kadhaa baadaye wakazi wa kijiji hicho wakiwa wanashughulikia mazishi ya kiongozi wao Wayahudi waliitumia nafasi hiyo na kurudi na kulitwaa tena eneo hilo. Katika hujuma zao hizo walikiharibu vibaya kijiji cha Qastal. Kwa sera hiyo ya shambulio la kukata kiu ya damu, Wazayuni walitekeleza mauaji ya kutisha ya Deir Yasin kwenye viunga vya mji wa Jerusalem. Waliingia katika kiiji hicho wakiwa na silaha nzito nzito, wakawachinja na kuwakatakata wakazi wake. Waliwaua Waarabu 250, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Mwandishi wa Kiyahudi aitwaye John Kimy aliyaelezea mauaji haya kama ukatili wa

70
kufedhehesha zaidi katika historia ya Wayahudi. Hakujua kwamba hapo baadaye Wayahudi wangetekeleza mauaji ya kutisha na yenye ukatili wa kupindukia zaidi kuliko huo. Waingereza walikuwa msaada mkubwa kwa Wayahudi katika kuyatambua na kutimiza malengo na shabaha zao. Katika kipindi chote cha mandeti waliwapa mafunzo ya kijeshi na kuwapatia silaha. Zaidi ya hayo, pindi Waingereza walipokuwa wakijiondoa katika eneo lolote walikuwa wakilikabidhi eneo hilo kwa Wayahudi. Kipindi hiki cha mwaka 1948 kilihitimishwa na hata kupewa jina la Msiba mkuu wa mwaka 1948, ambao ulisadifiana na Wayahudi kuzitwaa kimabavu ardhi nyingi za Palestina na kuwafukuza wananchi na wakazi wake, isipokuwa katika maeneo ya Gaza, Ukanda wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalem. Wakati huo huo, Ikulu ya Marekani White House ilikuwa tayari imemwita mwakilishi wa ofisi ya Wayahudi mjini Washington Ilyaho Eishtein na kumfahamisha kuwa Marekani imeazimu kwa dhati kuutambua uhuru wa Israeli ikiwa Washington itapokea ombi maalum la kutaka kuitambua. Mnamo Mei 14, saa kumi na mbili kamili kwa majira ya Washington, mandeti ya Uingereza nchini Palestina ilitangazwa kufikia kikomo. Saa kumi na mbili na dakika kumi na moja, Marekani ikatangaza kulitambua taifa la Israeli. Leo Palestina inapata tabu chini ya ukaliaji kimabavu unaofanywa na Wazayuni ambao waliuhadaa ulimwengu kwamba wana uhalali wa kuishi katika ardhi ya Waarabu wa Kipalestina, na baadhi ya nchi za kidemokrasia zikahadaika na udanganyifu huu kwa kushiriki kwa katika kongamano lililojulikana kama Kongamano la San Remo. Kongamano hilo lilifanyika mwaka 1920, ambapo nchi hizo ziliamua kuiweka Palestina chini ya Mandeti ya Uingereza, maamuzi ambayo ndani ya miaka miwili yalipelekea Palestina kuwa chini ya mamlaka ya Uingereza. Uingereza ilimtuma Herbert Samuel, ambaye ni kiongozi wa Kizayuni, kuwa mwakilishi wake wa kwanza nchini Palestina. Kwa hiyo, Kamishna huyu akawa mwakilishi wa Uingereza nchini Palestina na wakati huo huo akiwa kama mwakilishi wa Wayahudi. Mwaka 1922 Ushirikia wa mataifa (League of Nations) ulitoa agizo (Mandate) la Uingereza kuitawala Palestina, ambapo kutokana na agizo hili Uingereza ilianza kujenga makao ya taifa la Wayahudi nchini Palestina. Jambo hilo lilifanyika bila kuwatilia maanani wakazi asilia wa ardhi hii. Lilitokea bila kuwashaurisha, na lilifanyika kinyume na matakwa yao. Kwa hakika hiyo ni demokrasia ya uwongo ambayo wakoloni wanajivunia. Ukweli wa mambo (ironically), mhamasishaji wa fikra ya uanzishaji wa taifa la Wayahudi, Theodo Herzel, ambaye ni Muastria, mwaka 1896 aliandika kitabu kwa jina la The Jewish State (taifa la Wayahudi). Katika kitabu hicho alipendekeza kuanzisha taifa hilo katika moja wapo ya maeneo mawili: ima Argentina au Palestina! Kisha baadaye akaiweka Uganda, ambalo ni taifa la Kiafrika, kuwapendekezo jingine katika orodha ya nchi kadhaa zilizopendekezwa kama vile Pakistani!! Sio hayo tu, kwani hata kabla ya Herzl, viongozi wa Kiyahudi walikuwa wakifanya mikutano yao huko ambapo ramani ya Uganda ilichorwa.

71
Pamoja na nchi hii ya Kiafrika kutokuwa na chochote cha maana kwa Wayahudi, lakini ilikuwa miongoni mwa malengo ya mikakati ya Wazayuni. Mkondo ufuatao wa matukio unaonesha baadhi ya mambo ya hakika yasiyoweza kukanushwa na yeyote, yanayotoa siri ya Wazayuni kusitasita katika kuchagua nchi moja wapo kati ya Argentina na Palestina. Taarifa hizi zinapatikana kwa mtu yeyote anayetafiti historia ya vuguvugu la Kizayuni na mikutano yao iliyofanyika katika nyakati mbalimbali: Mwaka 1896 na baada ya kudhihiri kwa fikra zinazopinga Usemiti (anti-Semitism notions) huko Ulaya, Theodor Herzl katika kitabu chake kiitwacho The JewishState, alipendekeza suluhisho la tatizo hili kuwa ni kuanzisha makao ya taifa la Wayahudi katika nchi za Argentina au Palestine. Mwaka 1897, mkutano wa kwanza wa chama cha Wazayuni ulifanyika nchini Switzerland na kutangaza azimio lake lililojulikana kama Programu ya Basel (Basel program) kwa lengo la kuitwaa Palestina na kuanzisha chama cha kimataifa cha Wazayuni (International Zionist Movement). Mwaka 1904, mkutano wa nne wa chama cha Wazayuni ulifanyika, ambapo iliamuliwa kuanzisha makao ya taifa la Wayahudi nchini Argentina. Mwaka 1906, bunge la chama cha Kizayuni liliamua kuifanya Palestina kuwa makao ya taifa la Wayahudi. Mwaka 1914, baada ya kuanza kwa vita kuu ya kwanza ya dunia, Uingereza iliwaahidi Waarabu kuwasaidia kupata huru kutoka kwa utawala wa WaUthmaniyya kama wangeiunga mkono Uingereza katika vita vyake dhidi ya himaya ya Uthmaniyya. Kwa hali hiyo Uingereza iliingia Palestina kama jeshi la ukombozi, lakini huo ukawa udanganyifu mkubwa uliowapata Wapalestina katika historia yao kwani ulibadilisha moja kwa moja mustakbali wao. Mwaka 1916, makubaliano ya Sykes Picot (Sykes-Picot Agreement) yalisainiwa kati ya ufaransa na Uingereza, ambapo nchi hizo mbili zilikubaliana kuligawa eneo la Arabia maeneo madogo madogo yanayoweza kudhibitiwa na kutawaliwa kwa urahisi. Kwa namna hiyo, wakaamua kuiweka Lebanon na Syria chini ya udhibiti wa Ufaransa, huku Jordan na Iraq zikiwekwa chini ya udhibiti wa uingereza, isipokuwa Palestina iliyobaki kuwa nchi ndogo. Katika mwezi wa Novemba 1917, serikali ya Uingereza ilitoa hati ya Balfour (Balfour Declaration) katika namna ya barua maalumu kutoka kwa waziri wake wa mambo ya nje James Arthur balfour kwenda kwa kiongozi wa chama cha kizayuni. Katika barua hiyo, waziri huyo wa mambo ya nje aliahidi kuwa Serikali ya kifalme ingefanya kila juhudi katika uanzishaji wa makao ya taifa la Wayahudi nchini Palestina. Yafuatayo ni maandiko ya barua hiyo: Hati ya Balfour (The Balfour Declaration)

Mpedwa Bwana Rithchild, Kwa niaba ya Serikali ya Mfalme, nina furaha kubwa kukufikishia hati hii ya kuunga mkono juhudi za Wayahudi, hati ambayo imewasilishwa na kupitishwa na baraza la mawaziri.

72
Serikali ya Mfalme inalitzama kwa kulikubali suala la uanzishaji wa makao ya taifa la wayahudi nchini palestina, na itatumia juhudi zake katika kuwezesha kufikiwa kwa malengo haya. Ieleweke wazi kuwa hakuna jambo litakalofanyika ambalo litaathiri haki za kiraia na za kidini za jamii zisizokuwa za kiyahudi katika palestina, au haki na hadhi ya kisiasa wanayoipata wayahudi katika nchi nyingine yoyote. Nitashukuru iwapo utaifikisha hati hii kwenye shirikisho la Wazayuni. Imesainiwa na :Arthur james Balfour
Hii ni barua iliyotumwa na waziri wa mashauri ya nje wa uingereza kwenda kwa kiongozi wa chma cha Kizayuni. Kitu kinachovuta hisia katika maandiko ya barua hii ni sentensi inayoonesha dhahiri kuwa waziri huyu anakiri wazi kwamba ardhi hii ni ya Wapalestina tu. Sentensi hiyo ni hii ifuatayo: " His Majesty's Government view with favor the establishment in Palestine of a national home for the Jewish people" (Serikali ya Mfalme inalitzama kwa kulikubali suala la uanzishaji wa makao ya taifa la wayahudi nchini palestina). Katika sentensi hii Waziri anaahidi kuwanzisha taifa jipya nchini Palestina!!! Kitu gain zaidi kinachoweza kusemwa ili Kuthibitisha kuwa wakati huo Israeli haikuwepo, na kwamba ardhi ya Waarabu amabyo sasa hivi ndio kiini cha mgogoro, ni mali ya Wapalestina na sio waisraeli ambao ni wavamizi wa wazi waliovamia eneo hili, na ambao hawana cha kuwafungamanisha na ardhi hii tukufu zaidi ya ulafi wao. Kuna uthibitisho mwingi unaowafanya wale wale wanaojaribu kuuficha waonekane kuwa kichekesho. Miongoni mwa uthibitisho huo wa wazi na wenye kuondosha shaka, unaoonyesha udhaifu wa visingizio vinavyotolewa kuhusu taifa la kizayuni, na kufichua uwongo wa kwamba palestina ni ardhi ya Kiyahudi, uthibitisho huo ni watawala wa taifa hili lenyewe. Kwa yakini, maraisi wa taifa hili la kivamizi ni ushaihidi tosha kuwa Palestina ni ardhi ya Waarabu, na kwamba Waisraeli ni wageni na wakoloni waliokuja kunyanganya ardhi hii takatifu. Tangu kuanzishwa kwa Israeli tarehe 14 Mei 1948 hadi nmwaka 1996, ilitawaliwa na serikali 26 zenye maraisi 8, waliokuwa wakongwe zaidi na wa mwanzo kuitawala Israeli. Jeduwali lifuatalo, ambalo taarifa zake zimekusanywa kutoka vyanzo mbali mbali vinavyohusu wasifu wa viongozi hao, linaonesha majina halisi, tarehe na mahali walipozaliwa, sanjari na kutaja umri waliokuwa nao walipoingia kwa mara ya kwanza katika ardhi ya palestina: Waziri mkuu Tarehe ya kuzaliwa Mahali alipozaliwa Poland Urusi ya Mwaka alioingia Palestina 1906 1905 Umri wake wakati wa kuingia Palestina Miaka 20 Miaka 12

David 1886 Ben_Gurion M. Sharett 1854

73
Levi Eshkol Golda Meir Yitzhak Rabin Menachem Begin Yitzhak Shamir Shimon Peres 1895 1898 1922 1913 1915 1923 Kusini Ukraine Kyiv Ukraine Jerusalem Urusi Poland Poland 1914 1921 1942 1942 1934 Miaka 19 Miaka 23 Miaka 29 Miaka 20 Miaka 11

Jeduali hili laonyesha jinsi taifa la Kizayuni lilivyojengwa kwenye uwongo wa kwamba ardhi ya Palestina ni ya Wayahudi. Kabla ya kuanzisha taifa la Israeli, taasisi za kizayuni zilieneza msemo mashuhuri wa kibaguzi usemao: land with no people, to people with no land (Ardhi isyokuwa na watu, kwa watu wasiokuwa na ardhi). Kwa hiyo walikiri bayana kwamba hawana ardhi kwa kusema people with no land (watu wasiokuwa na ardhi), lakini waliongopa waliposema kwamba Palestine is a land with no people (Palestina ni ardhi isiyokuwa na watu), kwa sababu ilikuwa na imeendelea kuwa ardhi ya mapigano, na ni ardhi iliyojaa manukato ya historian a ustaarabu, ni ardhi ya Wapalestina tu. (Wapalestina) hawakuwahi kuiacha ardhi yao hii. Historia inaweka wazi kuwa waliilinda ardhi hii kwa damu zao katika kupambana na wavamizi mbali mbali kama vile, Wazungu (Crusaders), Wamongoli, Watatari, na wakoloni wengine. Jeduali lililotangulia laonyesha umri waliokuwa nao viongozi wa Israeli walipoingia kwa mara ya kwanza nchini Palestina. Aliyekuwa na umri mdogo kuliko wote ni simon Peres aliyekuwa na umri wa miaka 11, ambaye aliingia nchini Palestina kwa mara ya kwanza mwaka 1934 akitokea nchini Poland alikoishi kwa miaka 11 na kuzoe zaidi ada na desturi za mfumo wa maisha ya Ulaya kuliko ule wa Waarabu wa Palestina. Ama kuhusu Menachem Begin, kwa mara ya kwanza aliingia Palestina akiwa na umri wa miaka 29, na hivyo alikuja na mfumo wa maisha tofauti na ule wa Wapalestina. Alikuja Palestina akitokea nchini Urusi kama mhamiaji wa kiyahudi kama ilivyokuwa kwa maelfu ya watu wa aina yake waliokuja kutoka maeneo mbali mbali ya ulimwengu. Lakini suali linalojitokeza hapa kwa nguvu ni kwamba: Wazayuni walifanikiwaje kuficha ukweli na kuwajaza Wayahudi nchini Palestina? Wayahudi waliwasili vipi Palestina kutoka ulimwenguni kote kwa urahisi hivyo, licha ya upinzani mkubwa wa Waarabu? Umiliki wa ardhi uliwezaje kuhama kutoka kwa wamiliki wake wa kweli kwenda kwa wageni waliopanua kidogokidogo udhibiti wao juu ya Palestina yote na kuanzisha taifa jipya la kigeni linalotofautiana na wakazi wa asili ya eneo hilo katika kila kipengele?

74
Hapa ndipo panapojitokeza mchezo wa mkubwa na wa hatari uliotekelezwa na wahamiaji wa Kiyahudi katika kuhodhi mambo ya Wapalestina na kuwafukuza kuoka kaika nchi yao, na wao kuikalia kimabavu hadi leo. Kwani uhamiaji huu ndio iliyokuwa silaha kali ya kwanza iliyotumiwa na Wayahudi dhidi ya wamiliki halisi wa ardhi hii, baada ya kumiminika kwa wingi mkubwa wa wahamiaji nchini Palestina ambao baadaye uliwawezesha kuitawala nchi. Mbali na fikra hii, wapinzani wengi wa Kipalestina wanachukulia kwamba hakuna kitu kinachoitwa raia wa Israeli, bali wote ni askari wanapaswa kupambana nao kwa kuzingatia kwamba silaha ya kwanza iliyotumiwa na wayahudi ni silaha ya hila na hadaa iliyowezesha Wayahudi wengi kuingia palestina. Wayahudi Kuhamia Palestina Kuhamia kabla ya uundwaji wa Israeli Ardhi takatifu na adhimu ya Palestina inaheshimika kwa umuhimu na hadhi iliyo nayo machoni pa Waislamu kutokana na Msikiti wa Al-Aqsa kuwa katika ardhi hii. Msikiti huu ndio Qibla cha kwanza cha Waislamu ambapo kabla ya Kaabah iliyopo Makkah kufanywa kuwa Qibla chao walikuwa wakielekea huko (Masjid Al-Aqsa) wakati wa sala zao. Hakuna Mwislamu wa mahali popote atakayekubali au kuridhia Wayahudi kuyadhibiti maeneo matakatifu ya Waislamu na kuikalia ardhi hiyo tukufu, itakuwaje kama adui fulani ataingizwa kwa nguvu na kwa ujanja ndani ya ardhi ya Palestina ya Waarabu? Jambo hili litaamsha ghadhabu na hasira ambazo hakuna Mwislamu yeyote atakayebaki kimya na kuridhia uadui huo. Leo hii tunashuhudia namna makundi ya kishabiki ya Kiyahudi yanavyotishia kuuvunja Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa, jambo litakaloleta msiba na janga kubwa. Makundi ya wahamiaji wa Kiyahudi yaliyotoka maeneo mbalimbali ya dunia kuja Palestina yalikuwa ndiyo yalikuwa nguzo kuu ya mafanikio ya mpango wa Kizayuni nchini Palestina, kwani taasisi na vyma vya Kizayuni vilivyoundwa baada ya Kongamano kuu la Wazayuni, vilitumia uwezo wake wote kufadhili uingiaji kinyemela wa Wayahudi katika ardhi za Palestina. Vyama hivyo vilitumia uwezo wake kwa kuandaa mazingira na kupanga mipango ya kuwatoa Wayahudi katika nchi zao za asili ulimwenguni kote na kuwavuta kwenda Palestina ambayo ardhi yake iliandaliwa kuwa kituo cha usimikaji wa taifa la Kiyahudi. Mwaka 1869, kufuatia shinikizo lililotolewa na nchi za Ulaya kwa dola ya Uthmaniyya, shinikizo lililotokana na dola hiyo kuwa na madeni mengi na udhaifu uliokuwa umeikumba, Dola hiyo ilitunga sheria iliyowaruhusu wageni binafsi, taasisi au makampuni kumiliki ardhi katika eneo lolote, mijini na hata nje ya miji. Ruhusa hiyo ya wageni kumiliki ardhi kikawa chanzo cha wakulima na wananchi kwa ujumla kuwa na wasiwasi, kwa sababu ilikuwa sawa na kuwaruhusu Wayahudi wajae nchini na kununua ardhi chini ya ulinzi na mamlaka ya wageni. Tama na ulafi wa Wazayuni katika kununua ardhi ukaanza, ambapo walianza kuwasahwishi wakulima na wageni waliokuwa wakimiliki mashamba makubwa wayauze mashamba yao. Wakulima wakaanza kuwa na mashaka juu ya mustakbali wa mashamba na maisha yao. Kituo cha Kitaifa cha Habari za Kipalestina kinaeleza kuwa, mwaka 1837

75
makazi ya kwanza ya Kiyahudi yalijengwa nchini Palestina kwa msaada wa tajiri wa kiingereza mwenye asili ya Kiyahudi Montfort, ambapo idadi ya wakazi (inhabitants) wakati huo ilikuwa ni Wayahudi 1500, kisha idadi ya wahamiaji ikaongezeka na kufikia elfu 10 katika mwaka wa 1840, na baadaye ikapanda mpaka elfu 15 mwaka 1860, na hadi kufikia mwaka 1881 idadi ya Wayahudi ilifikia elfu 22. Katika mwaka wa 1882, msongamano wa wahamiaji wa Kiyahudi wenye asili ya Urusi walianza kumiminika nchini Palestina, licha ya Serikali ya WaUthmaniyya kuweka sheria iliyopiga marufuku uhamiaji. Kundi la kwanza la wayahudi lililowasili Palestina lilikuwa na wahamiaji 2000, kisha idadi hii ikaongezeka na kufikia Wayahudi elfu 25 mwaka 1903. Makazi ya Wayahudi nchini Palestina ndiyo yaliyokuwa mhimili wa uingiaji wa Wazayuni katika nchi, na hilo liliwezekana kupitia mpango wa wageni na Wapalestina wasiokuwa Waarabu kuuza ardhi zao kwa wahamiaji wa Kiyahudi. Kwa hiyo, idadi ya miji mipya ya wayahudi iliyojengwa katika kipindi cha utawala wa WaUthmaniyya, kinachoanzia mwaka 1882 hadi 1913, idadi hiyo ilifikia miji mipya 24, ambayo imetajwa na Dokta Mustafa Al Dabbagh katika kitabu chake Biladuna Falastin (Nchi yetu palestina) juzuu ya kwanza, sehemu ya kwanza ya chapa ya Al-taliaa, Beirut, 1965. Katika kitabu hicho amelishughulikia suala hili kwa kina na kutaja tarehe ya ujenzi wa kila mji na idadi ya wakazi wake. Ama kuhusu kipindi cha Mandate ya Uingereza, utawala huo uliaanzisha makazi (miji mipya) ipatayo 253 kati ya mwaka 1920 hadi mwaka 1958. Vile vile Dokta hind Amin AlBadiry katika utafiti wake uitwao Palestine lands (Ardhi za Palestina), chapa ya Arab League ya mwaka 1981, ametoa maelezo kamili kuhusu tarehe ya ujenzi wa kila mji na idadi ya wakazi wake. Katika utafiti huohuo ameweka bayana namna wayahudi, hadi mwaka 1947, walivyozikama ardhi za Palestina, na kupitia jeduali lifuatalo: The way of possession Its percentage from the total Area of Palestine %5099 (Land area seized by the Jews) in Dunnum

Uthmaniyya period and the outset of the British Military Regime Palestine Government rented it to the Jews Government granted it to the Jewish Agency Sold by big non-

864044

%40:8 %5064 %6075

5;90444 7690444

:690444

76
Palestinian Absent owners Sold by big Palestinian owners Total

%40.: %:0:

6:50844 ;0444

Jeduali hili laonyesha asilimia ndogo sana ya ardhi iliyokuwa imechukuliwa na wahamiaji wa Kiyahudi tangu walipoingia palestina hadi mwaka 1947, ikilinganishwa na ardhi ambazo bado zilikuwa katika umiliki wa Wapalestina. Hii inatokan na ukweli kwamb Wayahudi walikuwa ni wageni katika nchi ya Palestina, na hivyo walikuwa na ardhi ndogo. Kutokana na hali hiyo hawakuweza kuchukua zaidi ya asilimia 6.6 za ardhi. Baada ya vita vya kwanza vya Dunia, na kushindwa kwa Dola ya WaUthmaniyya kulikoashiria muanguko wa himaya iliyojipanua kwa karne nyingi, Palestina iliangukia chini ya Mandate ya Uingereza ambayo nayo ilimteua Kamishna wake Mkuu na kumuagiza huko kwa ajili ya kuendesha mamabo ya Palestina. Dokta Hind Amin Al-Badiry, - mtafiti maarufu na mwanachama wa Chama cha waandishi na wanahabari wa Kipalestina, mwenye shahada ya Sanaa (B.A) kitengo cha Historia kutoka chuo kikuu cha Damascus Syria, na mwenye Digrii ya sanaa (M.A) na Falsafa (Ph.D) kutoka chuo Kikuu cha Shams Cairoanathibitisha ndani ya jarida maarufu linalohusu masuala ya Kihistoria Al-Fustat kwamba katika kipindi cha utawala wa Kamishina Mkuu wa Uingereza (British High Commissioner) Herbert Samuel, ambaye alikuwa Myahudi, sheria mpya zilitungwa huku sheria nyingine zilizowekwa na utawala wa WaUthmaniyya zikibadilishwa kwa lengo la kuhalalisha suala la ubadilishaji wa umiliki wa ardhi kwenda kwa Wayahudi. Daktari huyo analithibitisha hili kwa kusema: In the year 1920, the administration of Samuel worked persistently and actively to carry

out the plans of the Zionist Committee, thus the first step it took was to inaugurate departments to record lands, and appointed the Zionist Norman Bentwich in charge of them. In the same year the dangerous area law was passed, which Bentwich worked on immediately putting it into practice, in order to confiscate lands. As a consequence to this, the Uthmaniyya Bank closed its doors (which was the sole bank that lent the peasants at small interests). He then imposed high taxes on people, to the extent that even the peasants, whose revenues were lower than any other class, used to pay the highest tax rates. In addition to this, authorities changed laws, in a way that turned things upside down, all this with the aim of cloaking the process of usurping lands under the pretenses of legitimacy and in the name of law, thus many unjust laws were passed to serve this aim. When the authorities imported products similar to what the people cultivate, they faced a deadlock, and many of them were ruined, owing to their continuous bankruptcy and the piling up of debts,

77
the percentage of inability to pay taxes among them reached 75%, not to mention the harassment, persecution, imprisonment, public fees, and the collective punishment that were practiced against them. Moreover the Jewish Usurers (the only lending body that remained after the closing of the Uthmaniyya bank) played a role in driving the peasants to bankruptcy, where the rate of interests over the debts reached 200%, which led to the forfeiture of the mortgaged lands in payment of the debts, as they were sold in a public auctions. These lands in specific are what Zionism exploited to propagate that the Arabs sold their lands, in addition to lands sold by the big Arab landlords, which is extremely small, and doesnt exceed 1%). All the succeeding High Commissioners followed in the footsteps of Herbert Samuel. Yediot Ahronot press had published in its issue dated 14/7/1972 an article entitled Blunder, Naivety, and Coloring written by the ex-Knesset member Yashyho Ben-Fort, where he justified this racial and vicious way of stealing lands from its owners by saying: The truth is that there can never be Zionism without settlement, and there can never be a Zionist state without expelling the Arabs, confiscating their lands, and fencing it.
Maana yake: Mwaka 1920, utawala wa Samuel ulifanya juhudi bila kusita na kwa haraka zaidi

kutekeleza mipango ya Kamati ya Kizayuni, na hivyo hatua ya kwanza aliyoifanya ni kuanzisha idara maalumu za kusajili na kurikodi ardhi na kumteua Mzayuni Norman Bentwich kuwa msimamizi wa idara hizo. Mwaka huo huo sehemu hatari ya sheria ilipitishwa na kwa haraka kabisa, Bentwich alianza kuzitekeleza kwa vitendo ili kupokonya ardhi. Kufuatia hatua hii, Benki ya Waottoma ilifunga milango yake- (ndiyo benki pekee iliyowakopesha wakulima kwa riba ndogo). Kisha aliwakalifisha wananchi kutoa kodi kubwa, kwa kiasi kwamba hata wakulima ambao pato lao lilikuwa chini kuliko matabaka mengine ya jamii walilipa viwango vikubwa vya kodi. Aidha, watawala walibadilisha sheria katika namna iliyoyabadilisha na kuayavuruga mambo, yote haya yakifanywa kwa lengo la kuuvika joho mchakato wa unyanganyi wa ardhi chini ya kivuli cha uhalali na kwa jina la sheria, na hivyo sheria nyingi za kidhalimu zilipitishwa kwa ajili ya kulitumikia lengo hili. Watawala walipoingiza bidhaa sawa na zile zilizokuwa zikizalishwa na wanachi, raia walikabiliwa nangogoro, na wengi wao waliharibikiwa kutokana na kuendelea kufiliska na mizigo mikubwa ya madeni. Kiwango cha kushindwa kulipa kodi miongoni mwao kilifikia hadi asilimia 75, sambamba na usumbufu, mateso, vifungo, kodi za umma, na adhabu za pamoja zilitekelezwa dhidi yao. Wafanyabishara ya riba wa Kiyahudi (watu pekee waliokuwa wakitoa mikopo baada ya kufungwa kwa Benki ya Waottoma) walikuwa na nafasi kubwa katika kuwapeleka wakulima kwenye hali ya kufilisika, ambapo viwango vya riba ya madeni vilifikia silimia 200, jambo lililopelekea kutwaliwa kwa ardhi zilizowekwa rehani kama njia ya kulipa madeni hayo, kwani ziliishia kuuzwa katika minada ya hadhara. Ardhi hizi ndizo hasa zilizotumiwa na mpango wa Wazayuni kutangaza kwa mba Waarabu

78
waliuza ardhi zao kwa kujumuisha ardhi zilizouzwa na Waarabu waliokuwa wakimiliki mashamba, ambayo ni madogo sana yasiyozidi asilimia 1). Makamishna wote waliokuja baadaye walifuata nyayo za Herbert Samuel. Gazeti la yediot Ahronot katika toleo lake la tarehe 14/7/1972 lilichapisha makala yenye kichwa cha habari fFujo, Ujinga, na kupiga chuku iliyoandikwa na Yashyho Ben-Fort, ambapo anahalalisha mfumo huu ubaguzi na uovu katika kuiba ardhi kutoka kwa wamiliki wake kwa kusema: Ukweli ni kwamba hapawezi kuwa na Uzayuni bila makazi, na hapawezi kuwa na taifa la Kizayuni bila kuwafukuza Waarabu, kuzipokonya ardhi zao, na kuzijengea uzio
Matokeo ya mazingira na hali hii, ni kwamba mpango wa wahamiaji wa Kiyahudi kumiliki ardhi za Wapalestina uliandaliwa, na idadi yao ikaongezeka kutokana na wahamiaji kuendelea kumiminika kuanzia mwaka 1850, hasa mwishoni mwa kipindi cha utawala wa himaya ya Uthmaniyya, kama inavyoonekana katika jeduali lifuatalo: Jumla ya wahamiaji wa Kiyahudi katika maelfu 25 25 20 14 83 Wastani wa kila mwaka wa wahamiaji wa Kiyahudi katika maelfu 0.8 1 2.9 3.5 1.3

Mwaka 1850-1880 1881-1903 1904-1910 1911-1914 Jumla

Jeduali hili laonyesha wazi jinsi wahamiaji walivyoendelea kumiminika bila uingiliaji kati wa aina yoyote, jambo linaloonesha kuwa uhamiaji huo ulikuwa umepangwa na ulikuwa na lengo maalum. Leo hii tunayajua na kuyaona matokeo yake yanayojidhihirisha katika udhibiti wa ardhi ya Palestina na kuanzishwa kwa taifa la kigeni lijulikanalo kama Israeli. Kituo cha Habari cha Kipalestina (Palestinian National Information Center) kimeweka jeduali hili linalopatikana katika tovuti yake, kikieleza kuwa Palestina ilikabiliana na mikondo mitano mfululizo ya mawimbi ya wahamiaji wa Kiyahudi, kufuatia matatizo ya mfululizo yaliyoyakumba maeneo waliyokuwa wakiishi wayahudi hapo awali. Matatizo hayo yalianza mwishoni mwa karne ya 19 hadi vita vya pili vya Dunia. Kituo hicho kimezigawa hatua za uhamiaji huo katika awamu zifuatazo: 1. Awamu ya kwanza1882 1903: uhamiaji huu ulitokea katika makundi mawili, ambapo Wayahudi wapatao elfu 25 waliingia Palestina, wengi wao wakitokea katika nchi za Romania na Urusi. Uhamiaji huu ulifadhiliwa na vyama vya Wapenzi wa Uzayuni (Lovers of Zion), chama cha BILU, pamoja na baadhi ya viongozi wa kikoloni na taasisi za Kiingereza.

79
2. Awamu ya Pili 1904 1918: Uhamiaji huu ulitokea kufautia kuanzishwa kwa chama cha Kizayuni. Idadi ya wahamiaji ilifikia watu elfu 40, wengi wao wakitokea katika nchi za Urusi na Romania. Kwa kaisi kikubwa kundi hili lilitokana na vijana hodari waliokuwa wamepewa mafunzo ya kijeshi na vyama vya Kizayuni na vile vya wakoloni. Mpka mwishoni mwa awamu ya pili ya huu uhamiaji, na kufuatia kulipuka kwa vita vya kwanza vya Dunia, idadi ya wahamiaji ilifikia Wayahudi elfu 85, huku idadi ya ardhi zilizochukuliwa ikifikia dunnum elfu 418 na mashamba (agricatural settlements) ya kilimo yapatayo 44. 3. Awamu ya Tatu 1919 1923: Katika awamu hii idadi ya wahamiaji ilifikia Wayahudi elfu 35, kwa kiwango cha wahamiaji 8 kila mwaka, wengi wao wakitokea Urusi, Romania, Poland, pamoja na idadi ndogo ya wahamiaji waliotoka Ujerumani na Amerika. 4. Awamu ya Nne 1924 1932: awamu hii ilianza katika kipindi ambacho uingereza ilikuwa ikiitawala Palestina, ambapo wahamiaji elfu 80 waliingia, wengi wao wakitokea katika matabaka ya kati, hususan kutoka Poland. Walitumia kiasi kidogo cha fedha waliyokuja nayo katika kutengeneza miradi yao midogo midogo. Wimbi la uhamiaji wa Kizayuni lilifikia kilele chake mwaka 1924, ambapo Wayahudi wapatao elfu 33 waliwasili nchini Palestina ikilinganishwa na wahamiaji elfu 13 wa mwaka 1924. Baada ya hapo idadi yao ilianza kupungua tena na kufikia wahamiaji elfu 13 katika mwaka 1926. Idadi ya wahamiaji iliendelea kushuka katika mwaka wa 1927, kutokana na matatizo ya kiuchumi yaliyokuwa yakiikabili nchi hiyo, na hivyo idadi yao ikapungua hadi kufikia wahamiaji elfu 3 na katika mwaka uliofuata wa 1928 idadi yao ikashuka zaidi na kufikia elfu 2 tu. Kwa hiyo, hadi kumalizika kwa awamu hii, idadi jumla ya Wayahudi waliofika Palestina ilifikia watu 175,000, ambao watu 136,000 miongoni mwao waliishi katika makazi ya raia, na waliobaki walitawanyika katika mashamba (Agricultural Settlements) 110 ya kilimo. 5. Awamu ya Tano1933 1939: Katika awamu hii, idadi ya wahamiaji waliomwagika nchini Palestina ilifikia watu 215,000, wengi wao wakitokea katika eneo la Ulaya ya Kati lililokuwa limeathiriwa na utawala wa Nazi na kufanya idadi ya Wayahudi waliotoka Ulaya ya Kati pekee kufikia wahamiaji elfu 45. Katika mwaka wa 1928 asilimia ya wahamiaji wa Kiyahudi waliotoka Ujerumani kuja Palestina ilifikia 52% ya wahamiaji wote wa Kiyahudi. Mwaka 1933 The White Book (Kitabu Cheupe) kilitolewa, ambapo Uingereza iliweka kikomo cha wahamiaji kuwa watu elfu 75 ndani ya miaka mitano mbele; na hivyo ikapunguza sana idadi kubwa ya wahamiaji waliokuwa wakisafiri kwa njia rasmi, huku ikifungua milango kwa uhamiaji usio halali wala rasmi na kufanya idadi ya wahamiaji kufikia kilele chake mwaka 1935 ambapo idadi yao ilifikia watu elfu 62. Baadaye kiwango hicho kilianza kuporomoka kutokana na msukosuko wa wapinduzi uliokuwa umepamba moto nchini Palestina katika mwaka wa 1936 baada ya Wapalestina kushindwa kuvumilia

80
na kukaa kimya mbele ya mawimbi ya wakimbizi yaliyokuwa yakimiminika katika ardhi zao. Dokta Muhammad Salamah Al-Nahal, anabainisha hali hii katika kitabu chake kiitwacho The Policy of British Mandate in The Arabic Palestinian Lands chapa ya Palestina, toleo la pili Beiruti ukurasa 74, 75, 76, ambapo kupitia majeduali yafuatayo anaweka wazi idadi ya wahamiaji wa Kiyahudi walioingia Palestina. Jeduali lifautalo lina maelezo kuhsu uhamiaji huo uliotokea katika kipindi cha mwaka 1920 hadi 1936: Jeduali 1 Mwaka 1920 1921 1922 1923 1924 1925 1926 1927 1928 1929 1930 1931 1932 1933 1934 1935 1936 Jumla Idadi ya Wahamiaji 5514 9149 7844 7421 12856 33801 13081 2713 2178 5249 4944 4075 9553 30327 42359 61854 29727 282.645 Asilimia 1.95 3.24 2.77 2.63 4.55 11.96 4.63 0.96 0.77 1.86 1.75 1.44 3.38 10.73 14.98 21.88 10.52 100%

Dokta Riyad Al-Aylah katika utafiti wake uitwao The Development of the Palestinian Issue (Historically, socially, and politically) {maendeleo ya kadhia ya Palestina, Kihistoria, kijamii, na kisiasa} toleo la pili la Mei 1998, ameeleza kwamba wakati wa vita vya pili vya dunia, Wayahudi wapatao elfu 55 waliingia Palestina kwa njia ziszokuwa za halali, ambapo manowari ya Kiingereza ilipewa jukumu la kuziongoza meli zilizokuwa zimewabeba wahamiaji wa Kiyahudi pamoja na kuwapa huduma ya maji, chakula, na mafuta mpaka walipofika katika pwani za Palestina. Aidha, kati ya mwaka 1940 hadi 1948 Wayahudi wapatao elfu 20 waliingia nchini, na kipindi cha Mandate ya Uingereza kilipomalizika idadi ya Wayahudi ilifikia watu 625,000. Kwa maneno mengine idadi yao ilikuwa sawa na theluthi moja ya raia wa nchi hiyo.

81
Jeduali lifuatalo, ambalo limenukuliwa kutoka chanzo hicho hicho cha jeduali lililotangulia, linaonesha asilimia ya raia wa Kiarabu na Kiyahudi waliokuwapo nchini Palestina katika kipindi cha mwaka 1918 hadi 1948. Jeduali 2 Asilimia ya Wayahudi 7.20% 14.67 16.90 20.90 27.15 30.1 31.40 31.48 Asilimia ya raia wa Kiarabu 92.80% 85.33 83.10 79.41 72.85 69.99 68.60 68.52 Mwaka 1918 1925 1931 1933 1935 1940 1946 1948

Jeduali hili linaonesha wazi ongezeko la idadi ya Wayahudi kutoka 7, 20% katika mwaka 1918 hadi 31,48% mwaka 1948. Bila shak ongezeko hilo kubwa la idadi ya Wayahudi waliomiminika Palestina kutoka ulimwenguni kote katika kipindi cha miaka 30 pekee, lingepelekea kubadilika hatua kwa hatua kwa uwiano wa nguvu na mamlaka kwenda kwa hao wadukizi, ambao walikuwa wageni katika eneo hili, waliokuja kutoka sehemu mbali mbali za dunia, baada ya kusita na kuchelewa kuchagua nchi ambayo wangejenga taifa lao la kigeni na la kivamizi, kwani Argentina lilikuwa chaguo lao jingine ambapo awali walikuwa wameyaelekeza malengo yao ya kilafi kwenye taifa hilo, lakini mwishowe wakaichagua Palestina. Watu wa Palestina ambao walikuwa wamedhoofishwa na vita nyingi, walikuwa wakitamani kupata uhuru, amani na usalama lakini badala yake wakakumbana na ukandamizaji, vitisho, maumivu na machafuko ambayo Waarabu kwa ujumla wanaendelea kukumbana nayo hadi sasa. Jeduali lifuatalo linaainisha nchi walizotoka hao wageni, kuanzia mwaka 1919 hadi 1936: Jeduali 3 Nchi Poland Urusi Ujerumani Romania Lithuania Idadi ya Wahamiaji 124.010 30.429 28.629 14.754 9.305 Asilimia 42.80 10.50 9.89 5.10 3.22

82
Yemen na Eden Marekani Ugiriki Iraq Latvia Uturuki Czechoslovakia Austria Iran Nchi nyingine Jumla 8.529 7.674 6.516 6.122 4.546 4.016 3.748 3.690 3.047 34.583 289.616 2.95 2.65 2.25 2.11 1.57 1.39 1.29 1.27 1.05 11.96 100%

Kuhamia baada ya uundwaji wa Israeli 1948-1967: Kwa kuinyanganya Palestina na kutangaza uundwaji wa taifa la Israeli mwaka 1948 na kuwafukuza Waarabu wa Kipalestina kutoka katika ardhi na nchi yao, Wazayuni walianza kutumia nguvu kubwa katika kuhimiza na kurahisisha uhamiaji wa Wayahudi kuja Palestina na wakatoa kile kilichokuwa kikijulikana kama sheria ya Ujio (law of Return) iliyoidhinishwa mwaka 1950 na kuamuru kwamba kila Myahudi ana haki ya kuingia nchini kama Myahudi anayerejea nyumbani. Uhamiaji uliendeshwa kupitia viza maalum ya wahamiaji. Aidha sheria ya utaifa wa Israeli mwaka 1952 ambapo kila mwananchi wa Kiyahudi aliyehamia Israeli alikuwa na haki ya kupata kitambulisho cha uraia wa Israeli mara tu anapoingia nchini. Zaidi ya hayo, uhamiaji uliboreshwa, kuandaliwa na kusimamiwa na wakala wa Wayahudi na kutoa uangalizi maalum kwa masuala ya wahamiaji pale walipoingia nchini, jambo ambalo lilipelekea kuwepo kwa ongezeko la wahamiaji. Jeduali lifuatalo lililopatikana kutoka katika chanzo cha majeduali mawili yaliyotangulia, yaani uchunguzi uliofanywa na Muhammad Salamah Al-Nahal, linaelezea uhamiaji wa Wayahudi nchini Palestina katika kipindi cha mwaka 1948 1967: Jeduali 4 Mwaka 1948 1949 1950 1951 1952 1953 1954 1955 Idadi ya Wahamiaji 101.828 239.576 170.249 175.095 24.369 11.326 18.370 37.478

83
1956 1957 1958 1959 1960 1961 1962 1963 1964 1965 1966 1967 56.234 71.224 27.082 23.895 24.510 47.638 61.328 64.364 54.716 30.736 15.730 14.327

Tukiliangalia jeduali lililotangulia tunabaini mambo yafuatayo: Kwanza: ongezeko la idadi ya wahamiaji wa Kiyahudi walioingia Palestina katika kipindi cha miaka minne ya mwanzo baada ya uanzishwaji wa taifa la Kizayuni. Katika kipindi hicho wahamiaji wapatao 700,000 waliingia, wakati ambapo idadi ya Wayahudi waliokuwapo nchini Palestina mwaka 1948 ilifikia watu 650,000. Sababu zilizopelekea ongezeko la wahamiaji wa Kiyahudi ni hizi zifuatazo: 1-Taasisi na mashirika ya Kizayuni kuwasafirisha Wayahudi waliobaki katika makambi ya wakimbizi ya Magharibi mwa Ulaya baada ya vita vya pili vya dunia kuja Palestina. 2- Mazungumzo yaliyofanywa kati ya serikali ya Israeli na ile ya Romania mwaka 1948 na kupelekea kuwasili kwa wahamiaji wa Kiromania wapatao 118,000 katika kipindi cha mwaka 1948 1951. 3- Wazayuni walitumia mbinu za kiovu na za kigaidi ili kufikia malengo yao ya uhamiaji hususan na katika nchi za Mashariki ya Kati, hasa nchini Yemen, Iraq na Libya ambapo Wayahudi walitekeleza matukio ya ulipuaji wa mabomu katika miji walioishi wayahudi ili kuibua hofu na hivyo kuwataka wahamie Palestina ili kujikomboa dhidi ya ugaidi. Matukio haya yanatoa mwanga wa mizizi ya ugaidi wa Wazayuni ulioshamiri tangu mwanzoni mwa karne iliyopita ambapo waliwaua Wayahudi wenzao ili kuwalazimisha wahamie Palestina. Pili: kupungua kwa idadi ya wahamiaji katika kipindi cha miaka mitatu iliyofuata ya kuanzia mwaka1952-1955 kwa sababu ya mgogoro wa kiuchumi uliolipuka nchini kutokana na ongezeko la wahamiaji na mlipuko wa ukosefu wa ajira. Tatu: kuendelea kwa uhamiaji maradufu katika kipindi cha mika mitatu ya 1955-1957, ikilinganishwa na kipindi cha nyuma na hali hiyom kuwa na mahusiano na matukio ya Hungary na hali ya kiuchumi katika nchi iliyotokana na mashambulio ya pande tatu kwenye ardhi ya Misri na katika eneo la Ukanda wa Gaza.

84
Nne: anguko la wazi la idadi ya wahamiaji baada ya mwaka 1957, hali iliyotokana na wahamiaji kutoka Kaskazini mwa Afrika kusimamisha safari za uhamiaji baada ya serikali za Kiarabu nchini Morocco, Tunisia na Misri kuwahamasisha Wayahudi kubaki katika nchi hizo kwa kuwapatia hali na mazingira mazuri ya maisha na usalama, hususan baada ya shambulio la Uingereza na Ufaransa kwenye Mfereji wa Suez lililokomesha harakati na vitendo vya kigaidi vilivyokuwa vikitekelezwa na mawakala wa Kizayuni. Tano: ongezeko la idadi ya wahamiaji kuanzia mwaka 1961 mpaka kufikia kiwango cha wahamiaji 50,000 kwa mwaka, ikiwa ni katika kipindi cha kuanzia mwaka 1961 hadi 1965. Kutokana na chanzo cha Kiisraeli, ambacho ni muhtasari wa kitakwimu wa Israeli (Statistical Absract of Israel), No.45(1994),ukurasa.43, jeduali lifuatalo linaweka bayana idadi na asilimia ya wahamiaji walioingia Palestina kuanzia mwaka 1882 1993 (kwa asilimia), ikiwa ni pamoja na mabara waliyozaliwa: Kipindi Idadi ya Kutoka Asia Kutoka Ulaya % walichohama wahamiaji na Afrika na Amerika 1882-1914 55.000-70.000 100 1919-1948 482.857 100 10.4 89.6 15\Mei 19482.363.481 100 35.3 64.7 1993 15\Mei 1948687.624 100 49.9 50.1 1951 1952-1954 54.676 100 76.4 23.6 1955-1957 166.492 100 68.3 31.7 1958-1960 75.970 100 36.0 64.0 1961-1964 228.793 100 59.4 40.6 1965-1968 82.244 100 49.7 50.3 1969-1971 116.791 100 27.3 72.7 1972-1974 142.755 100 9.2 90.8 1975-1979 124.827 100 14.3 85.7 1980-1984 83.637 100 27.1 72.9 1985-1989 70.196 100 20.4 79.6 1990 199.516 100 2.7 97.3 1991 176.100 100 11.9 88.1 1992 77.057 100 6.5 93.5 1993 76.805 100 4.1 95.9 Jeduali hili linatoa picha ya mawimbi ya wahamiaji wa Kiyahudi kutoka katika mabara mbali mbali na kuonyesha ongezeko la hatua kwa hatua la idadi ya wahamiaji tangu mwanzoni mwa karne ya ishirini, ambapo idadi ya wahamiaji hao haikuwa zaidi ya watu

85
55000 kisha tunaona idadi hii ikiongezeka katika mwaka 1955 na kufikia watu 166000, na baadaye katika mwaka 1990 inafikia watu 199000. Ongezeko hili la wimbi la wahamiaji waliomiminika nchini Palestina lilifanya uwiano wa nguvu kutetereka na kuongeza hitilafu na tofauti kati ya wageni na wamiliki halisi wa ardhi, jambo lilolazimisha kushamiri kwa Wayahudi na baadaye kuitawala palestina. Jeduali lifuatalo, mabalo limechukuliwa kutoka katika kitabu cha mwongozo mkuu wa masuala ya Israeli (General Israeli Guide) kilichoandikwa na Mahmoud Miaary wa taasisi ya masuala ya Kipalestina, katika mlango unaohusu muundo na mchanganyiko wa raia (population composition), ukurasa 37-89 inaonesha kwamba hadi miaka ya sabini Israeli iliundwa na Wayahudi wengi waliozaliwa nje ya Palestina. Kisha asilimia ya Wayahudi waliozaliwa Israeli au Palestina kabla ya mwaka 1948 ilianza kuongezeka na kuunda raia wengi wa Israeli wenye asili ya kiyahudi waliofikia asilimia 60.9 mwaka 1993. Wakazi wa Israeli kutokana na nchi zao za asili Nchi ya asili Na. Ya Jumla Jumla -Asia Uturuki Iraq Yemen Iran Nchi nyingine (ikiwemo India na Pakistan) Africa - Jumla Morocco Algeria na Tunisia Libya Misri Nchi nyingine (ikiwemo Ethiopia) Ulaya, Amerika na Ukraine Jumla Muungano wa Kisovieti Poland Romania Na. Kamili 4.335.2 736.300 86.300 256.500 158.00 134.7 100.2 837.6 502.8 126.5 74.7 63.0 70.6 1.730.5 712.1 262.5 258.0 % 100.0 17.0 2.0 5.9 3.6 3.1 2.3 19.3 11.6 2.9 1.7 1.4 1.6 39.9 16.4 6.0 5.9

86
Bulgaria na Ugiriki Ujerumani na Austria Czechoslovakia (ya zamani) Hungary na nchi nyingine za Ulaya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini na visiwa vya Oceania Palestine\Israel-born, father also 59.9 85.0 191.8 1.4 2.0 4.4

161.2 1.030.8

3.7 23.8

Katika uchunguzi huu utokanao na chanzo kilichotajwa hapo juu, inadhihirika wazi kwamba jamii ya Kiisraeli ni jamii ya wahamiaji au walowezi, ambapo 39.1% ya wakazi hao wa Kiyahudi wanaendelea kuzaliwa katika maeneo ya nje ya nchi na 37.1% wanazaliwa wanazaliwa ndani ya nchi (Palestina au Israeli) lakini wazazi wao wanazaliwa nje ya nchi. Na kwamba ni 23.8% pekee ya wakazi wa Kiyahudi na wazazi wao ndio wanaozaliwa ndani ya nchi. Raia wa Kiyahudi wameongezeka haraka, na tangu kuanzishwa kwa Israeli tarehe 15 Mei 1948 hadi mwishoni mwa mwaka 1993 wameongezeka na kuwa zaidi ya mara sita. Ukubwa wa uhamiaji, kwa ujumla, umechangia nusu ya ongezeko la idadi ya watu na nusu nyingine imechangiwa na ongezeko la kiasili. Wapalestina nchini Israeli, bila kujumuisha wa kazi wa Al-Quds, ni 15.4% ya wakazi wote. Kupitia ongezeko la kiasili la watu (natural population growth), wananchi wa Kiarabu wamefanikiwa kulinda na kuhifadhi mizania yao licha ya ongezeko kubwa la wahamiaji wa Kiyahudi, ongezeko ambalo kiwango chake ni karibu mara mbili ya ongezeko la kiasili la Wayahudi. Kulingana na suala la nchi ya asili, linalobainishwa na takwimu za serikali ya Israeli, yaani takwimu inayoangalia mahali mtu alipozaliwa au alipozaliwa baba yake, wakazi wa Kiyahudi katika Israeli wamegawanyika katika makundi matatu ya asili: 1-Wayahudi wa kimagharibi (au wenye asili ya magharibi), waliozaliwa Ulaya na Marekani {Western Jews (or from western origins), born in Europe America}. 2- Wayahudi wa kuzaliwa, ambao wazazi wao walizaliwa katika nchi za kigeni Ulaya na Marekani {Native-born Jews, of foreign-born fathers in Europe America}. 3- Wayahudi kutoka Mashariki (au wenye asili ya mashariki): waliozaliwa Asia na Afrika na wayahudi wa kuzaliwa, wanaotokana na wazazi waliozaliwa Asia Afrika {Eastern Jews (or from eastern origins): born in Asia Africa and native-born Jews, descendants of foreign-born fathers in Asia Africa}. Kwa kuongezea kwenye taarifa hizo zote zinazohusiana na wahamiaji walioingia Palestina, suala la uhamiaji wa Wayahudi wenye asili ya Urusi waliohama kutoka muungano wa

87
iliyokuwa usoviet linaonekana dhahiri, kwani wahamiaji hawa walioingia katika maeneo ya Palestina wanaunda 10% ya wakazi wote waliopo hapo, na ushawishi na nguvu zao katika maisha ya kisiasa yameongezeka sana tangu wakati wa uhamiaji mkubwa uliowaingiza wengi wao katika Israeli kwenye miaka ya themanini na tisini. Katika kipindi cha miaka minne (1990 1993), zaidi ya watu nusu milioni walihama kutoka Muungano wa zamani wa Soviet kuja Israeli, jambo lililopelekea kuwepo kwa ongezeko la 10% ya wakazi wake. Wengi wa watu wazima katika wahamaiji hao walikuwa ni wahitimu wa Chuo Kikuu au kutoka vyuo vya Teknolojia vya Kisoviet. Aidha tabaka kubwa miongoni mwao walikuwa ni wahandisi na wajenzi. Vyanzo mbalimbali vimethibitisha tukio hili la uhamiaji. Vyanzo hivyo ni kama vile, shirika la kimarekani la Sephardi (American Sephardi Federation), wakala wa Wayahudi katika Israeli (Jewish Agency for Israel) na Ofisi ya kituo cha Takwimu (Centre Bureau of Statistics). Vyanzo vingine ni kitabu cha Ahmad Khalifa kiitwacho The Russian immigrants in Israel, Jarida la utafiti kuhusu palestina, toleo namba 38, lililotoka wakati wa majira ya kuchipua (spring) ya mwaka 1999, ukurasa 80 & 124. Jeduali lifuatalo linajumuisha maelezo yaliyothibitishwa na vyanzo hivyo: Wahamiaji kutoka Muungano wa zamani wa Usoviet Wahamiaji kutoka katika Umoja wa iliyokuwa Jumla ya Wahamiaji Soviet 9505 12.965 13.034 24.000 199.516 176.100 77.057 76.805 79.844 76.361 70.605 65.962 56.700 938.454 Katika Maelfu 202 2096 2283 12.932 185.227 147.839 65.093 66.196 67.771 64.489 58.447 54.521 45.400 772.496

Mwaka 1986 1987 1988 1989 1990 1991 1992 1993 1994 1995 1996 1997 1998 Jumla

88
Baada ya kuziona taarifa, takwimu na ukweli wote huo, bila shaka ni wazi sasa kwamba kamwe Waisraeli hawakuwa wamiliki halali wa ardhi ya Palestina, bali wao ni wakoloni tu walioungwa mkono na majeshi ya kidhalimu kuidhibiti safari ya wananchi wa Palestina na kuyabadilisha maisha yao katika shida tuishuhudiayo hii leo. Ni muhimu kueleweka kuwa kumbukumbu ya wananchi wa Kiarabu haihitaji taarifa au data zozote katika data hizo kutambua kuwa Wazayuni ni wageni, kwa sababu historia ya nchi zote za Kiarabu inaeleweka vyema tangu enzi na enzi. Jambo linalosikitisha ni kwamba wamiliki halisi wa ardhi hii wanaishi chini ya mbinyo na ukandamizaji wa mamlaka yenye mabavu sana ulimwenguni, kwa kiasi kwamba yeyote anayeitetea nchi yake Palestina anaitwa Gaidi. Wanayachukulia matendo ya kinyama ya kila siku ya kuwachinja Wapalestina kuwa Isareli inafanya hivyo katika kujilinda wakati kiukweli ni matumizi na ukandamizaji wa kibeberu. Tunu na maadili yamebadilishwa sana kiasi kwamba baadhi ya watu Ulimwenguni wanawatetea wakoloni na wavamizi hao dhidi ya wahanga ambao ardhi zao zimenyanganywa kwa mabavu kwa mkono wa chuma. Tukio hili kubwa zaidi la uhamiaji katika historia ya binadamu limeonesha wazi kabisa kuwa wakazi wa kile kijulukanacho leo kama Israeli ni wageni (aliens) katika ardhi hii ya Palestina ya Arabia. Idadi kubwa ya Wayahudi wamekalia ardhi ndogo za Palestina, je Wapalestina waliobaki walikwenda wapi baada ya tukio hili kubwa la wageni kuhamia katika ardhi yao? Wamiliki wa kweli wa ardhi hizi walikimbilia wapi baada ya wanyanganyi kutoka nje kuzipora ardhi zao? Kuwafukuza Wapalestina kutoka majumbani mwao Imeshaelezwa hapo awali kwamba Palestina ipo magharibi mwa Asia; kwenye eneo la kusini mwa pwani ya mashariki ya Bahari ya Mediterranean na hivyo kuwa katikati mwa eneo la ulimwengu wa kihistoria/ wa kale ulioifanya kuwa daraja linalounganisha mabara ya Asia na Afrika, na kuwa kiunganishi kati ya Bahari ya Mediterranean na Bahari nyekundu. Vile vile niliashiria kwamba Palestina inajumuisha eneo la 27.009 km pekee, ikiwa ni pamoja na Ziwa Tiberias (Lake Tiberias) na jimbo la Hawla na nusu ya eneo la Bahari ya Chumvi (Dead Sea). Eneo hili kwa ujumla wake linafaa kwa makazi kutokana na uwepo wa Ziwa Tiberias na nusu ya eneo la Bahari ya Chumvi (Dead Sea). Eneo hili la Palestina ni dogo sana linaloweza kuwa sawa na asilimia 4 tu ya jimbo la Texas, hii ikiwa na maana kwamba ni dogo zaidi kuliko jimbo hilo kwa mara 25. Kadhalika ni sawa na asilimia 15.3 ya eneo la Washington na sawa na karibu asilimia 21 ya eneo la mji wa New York. Udogo huu waonekana wazi kuwa hautoshelezi hata kidogo mahitaji ya Wapalestina, sasa ikiwa ni hivyo, hali inakuwaje pale makundi haya makubwa ya umati wa watu kutoka duniani kote wanapohamia katika eneo hili lenye udogo kama huu? Viongozi wa Kizayuni walioongoza zoezi la kuwahamishia wayahudi nchini Palestina waliujua vema ukweli huu, na walijua vema kwamba Palestina haikuwa ikiwatosha hata watu wake wenyewe, achilia mbali umati wa Wayahudi waliomwagikia ndani yake. Hivyo, viongozi hawa wa Kizayuni waliamua kuiondoa Palestina kutoka kwa wakazi wake wa asili ili itwaliwe na wageni wanaotoka sehemu mbalimbali za dunia. Fikra hii iliwahi kuwekwa

89
katika makala iliyoandikwa na aliyewahi kuwa mbunge wa bunge la Israeli (Knesset) katika gazeti la Kiisraeli Yediot Ahronot la 14/7/1972. Ukweli ni kwamba uwepo wa Mpalestina nchini palestina ni wa kale sana na yupo mahali hapo tangu binadamu alipotokea kwa mara ya kwanza katika eneo la Arabia. Uthibitisho wa hilo ni mji wa Kipalestina wa Ariha (Jericho), ambao ndio mji mkongwe zaidi katika historia, ukiwa na umri wa zaidi ya miaka 7000. Lakini uwepo wa Israeli ni wa hivi karibuni tu na maelezo yaliyotolewa kuhusu uhamiaji yanafichua na kubainisha ukweli huu. Kama ambavyo Wazayuni walivyotekeleza matendo ya kigaidi dhidi ya Wayahudi wenzao (nchini Iraq, Libya na Yemen) kwa lengo la kuwahamasisha kwenda Israeli wakati wakiyapenda maisha yao katika nchi hizo zilizotunza utu na heshima yao, vivyo hivyo ndivyo walivyotekeleza ugaidi huo dhidi ya Wapalestina kuwalazimisha kuzihama ardhi zao na kuwaachia wageni waliokuja kusababisha masaibu na vita vinavyoendelea kushuhudiwa hadi leo. Vitendo hivi vya kigaidi dhidi ya Wapalestina vilivyoanza mwanzoni mwa karne iliyopita vilianzisha na kuchochea wimbi la mauaji ya kutisha. Mbunge wa bunge la Kiyahudi alikiri juu ya ukweli huu katika makala yake yaliyochapishwa katika gazeti la Kiisraeli la Yediot Ahronot, ambapo alilichukulia suala la kuiondoa Palestina mikononi mwa wakazi wake kuwa ni dharura isiyoepukika ili kujenga taifa lao la kigeni na la kivamizi kwenye ardhi ya eneo hili. Ulimwengu wote unapaswa kujua jinsi Wayahudi walivyoingia Palestina na kuitawala, na jinsi Israeli ilivyoingia katika eneo hili la Arabia na kuzusha vita na masaibu ya kikatili yanayowasibu watu wa eneo hili na kufanya mambo haya yajulikane kwa watu wachache tu wa dnia hii kutokana na kubezwa na vyama vya kisiasa na mfumo wa vyombo vya habari vyenye mahusiano na Ulimwengu wa Kizayuni. Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Kikoloni, Malcolm MacDonald, tarehe 23 Novemba 1938 alitoa ushuhuda muhimu katika bunge la wawakilishi (House of Commons) ambapo alifafanua hali halisi ya Palestina. Chini ya kichwa cha habari cha Mradi wa Kuigawa Palestina (Division Project), Ushuhuda huo unachukuliwa kuwa uthibitisho wa maana juu ya ukweli wa hali ya Palestina katika wakati huo. Maelezo hayo yalibainisha ufahamu wake juu ya nafasi ya Arabia na usahihi wa mawazo ya Waarabu. Ushuhuda huu uliotolewa na Waziri huyo wa Uingereza unaweka wazi hali tete ya Kisaikolojia ambayo Wapalestina waliishi pindi Wayahudi walipoivamia nchi yao, ambapo hapo mwanzo waliukubali uingiaji wa wayahudi kwa namna ya amani na wakaamiliana nao vizuri kwa sababu waliwaamini, na kwa sababu ya urahisi na ujinga wa kutojua njama iliyokuwa nyuma ya muonekano wa hawa wavamizi. Leo hii ulimwengu wote unajua kilichokuwa kimefichwa na wayahudi baada ya kuwaona raia wa Palestina sasa wakiwa hawana makazi na watoto wao wakichinjwa na kuuawa kila siku. Wayahudi waliusaliti uaminifu waliopewa na Wapalestina, ambao siku moja waliwakaribisha na kukubali wakae katika ardhi yao. Lakini kwa masikitiko makubwa wakajikuta chini ya mtutu wa bunduki za hawa wageni waliogeuka na kuzishikilia mali na milki za Wapalestina, wengi wao wakijikuta wamekuwa wakimbizi katika nchi za jirani.

90
Wakili Wakim Wakim, Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kutetea haki za watu walioondoshwa Israeli (National Committee for the Defense of the Rights of the Uprooted in Israel), katika makala yaliyochapishwa kwenye tovuti ya kamati ya Wanawake ya Kutetea haki ya Wapalestina ya kurudi nchini kwao (Womens Committee for Supporting the Palestinians Right of Return) katika makala hayo anaeleza yafuatayo: Wakati wa kutangaza azimio la kuigawa Palestina, namba 181 la tarehe 29/11/1947, zaidi ya Waarabu 243000 walikuwa wakiishi katika mikoa iliyokuwa chini ya Dola la Kiyahudi kwa mujibu wa azimio hilo. Waarabu hao waliishi katika vijiji 219 na miji minne ya Haifa, Tiberias, safad na Baysan. Katika kipindi cha kati ya azimio hilo hadi mwezi Juni 1948, zaidi ya Waarabu 239000 walifukuzwa katika eneo hili na vijiji 180 vya Waarabu viliondoshwa na kuharibiwa kabisa. Kadhalika wakazi wote wa miji mikubwa mitatu: Safad, tiberias na Baysan walifukuzwa, ambapo Wapalestina 1950 ndio waliobaki mjini Haifa. Wakati huo huo taasisi za jeshi la Kizayuni ziliwafukuza Waarabu wapatao 122000 kutoka katika mikoa iliyokuwa chini ya udhibiti wa Dola ya Palestina na vijiji 70 viliondoshwa na kuharibiwa kabisa. Wakazi wa Yafa na Akka takriban wote waliondoshwa. Aidha, sehemu kubwa sana ya wakazi wa AlLadd na ar-Ramlah walifukuzwa. Watu wengi hudhani kuwa tukio la kuwafukuza Wapalestina katika ardhi yao lilitokea sanjari na kulipuka kwa harakati za jeshi la Kizayuni za mwaka 1948. Lakini tukizama katika kurasa za historia ambayo vyombo vya habari na itikadi za Kizayuni viliiiweka gizani katika namna ambayo haikuwahi kutokea hapo kabla, historia hiyo yathibitisha kwamba ufukuzaji ulianza taratibu kinadharia pale Herzl alipozindua kitabu chake The Jewish State (Dola la Kiyahudi), kinachotambulika kama Torati ya Wazayuni. Msingi wa uanzishaji wa taifa la Kiyahudi katika nchi yetu ya Palestina ulikusudiwa kuwafukuza watu wetu wote, au angalau wengi wao, kama taasisi za jeshi la Kizayuni zilivyofanya na baadaye dola la Israeli. Kwa kweli tukio la kwanza la kuwafukuza Wapalestina lilitokea mwaka 1905, pale walowezi wa Kizayuni walipokula njama na baadhi ya makabaila kutoka Lebanon kununua ardhi kutoka kwenye kijiji kinachotazamana na Al-Jalil Al-Ala (Upper Galilee) na kuwaondosha wakulima waliokijenga na kuustawisha udongo wake kwa jasho na damu yao. Mmojawapo wa walowezi wa Kiyahudi aliwahi kuandika katika kipindi hicho juu ya mapenzi makubwa waliyokuwa nayo wakulima kwa ardhi zao akisema, hata wanyama wao walilia pindi walipolazimishwa kuondoka. Kadhalika uthibitisho wa kihistoria unaonesha kwamba kabla ya mlipuko wa vita Janga la mwaka 1948 - wakulima wa Kipalestina wapatao 70,000 walifukuzwa na vijiji vyao vikabomolewa hata kabla Umoja wa Mataifa haujaidhinisha jinai iliyolihalalisha azimio la kuigawa Palestina sawa kwa sawa baina ya Wapalestina na walowezi wa Kiyahudi. Jumla ya Wapalestina waliofukuzwa nchini mwao ilikuwa ni zaidi ya wananchi 726000, na waliobaki Palestina ni Wapalestina wapatao 156000 pekee, ambapo watu 40000 miongoni mwao wamehamishwa nchini Palestina na kukimbilia kwenye vijiji na nchi za jirani, idadi yao kwa sasa ni zaidi ya watu 200000 waliohamshwa kabisa kutoka makwao. Katika vijiji walivyokimbilia wanaunda asilimia 50 ya wakazi wa maeneo hayo au hata kuwa zaidi. Idadi kubwa ya watu hao waliohamishwa na wasiokuwa na makazi ndani na nje, inathibitisha dhahiri uwongo wa madai ya Wazayuni wanaodai kuwa wakimbizi hao

91
walihamishwa makwao kufuatana na matakwa ya viongozi wao, ikizingatiwa kuwa kipindi cha kati ya 1/12/1947 na tarehe mosi ya Juni ambapo taasisi za kijeshi za kizayuni ziliongeza vitendo vya kigaidi dhidi ya wakazi wa Palestina, kipindi hicho ni kifupi mno. Harakati iliyokubaliwa iliokubaliwa mapema na wanahistoria wa kijeshi wa Kiisraeli wakiongozwa na Benny Maurice, inathibitisha ukweli wa maelezo ya Wapalestina yanayothibitisha kwamba operesheni ya kuwafukuza Wapalestina kwa lazima ilifanyika kwa kupangwa na kuratibiwa kwa mbinu maalumu kwa mfumo wa Kuitakasa kimila Palestina dhidi ya wakazi wake wa Kiarabu. Kwani operesheni hiyo ya kuwafukuza Wapalestina kwa lazima iliambatana na mashambulizi makubwa ya dhuluma, ugaidi, vitisho na mauaji yaliyokuwa kama sababu kuu zilizosimama nyuma ya pazia la kuondolewa Waarabu katika ardhi ya Palestina. Mwanahistoria wa kijeshi wa Israeli Prof. Ytzhak, mhadhiri katika chuo kikuu cha Bar-llan, alikadiria kwamba mauaji ya maangamizi ya kupangwa (organized bloodbaths) yaliyofanywa na makundi ya Kiisraeli yalifikia zaidi ya mauaji tisa ya maangamizi ya kinyama. Operesheni hizi za kijeshi zilisuhubiana na sera ya vita vya kisaikolojia kwa kutoa habari kwa watu wa ndani kuhusu mauaji yaliyokuwa yakiendelea ili kwamba ukatili huo wa kimbari, ubakaji, na uharibifu ziwafikie wakazi hasa wahafidhina wa vijijini kwa lengo la kupandikiza ndani ya nyoyo za wakazi hao hali ya kitisho hofu kubwa itakayowafanya wavihame na kuvikimbia vijiji vyao kwa ajili ya kuokoa roho, heshima na mali zao. Vile vile kuna ushuhuda mwingi unaothibitisha kwamba vijiji vingi vya mpakani mwa Palestina vilizungukwa kutoka katika pande tatu na kupigwa mabomu kuwalazimisha watu kukimbilia upande wa nne ambao katika matukio mengi eneo hili la nne lilikuwa upande wa kuelekea Lebanon, Syria au Jordan. Madai ya uwongo ya Wazayuni kwamba mwaka 1948 Wapalestina waliziacha ardhi zao kufuatia amri ya viongozi wao, madai hayo ni miongoni mwa propaganda za uwongo za Wazayuni zenye lengo la kupunguza wasiwasi ulioenea dunia nzima kuhusu wananci wa Palestina, hususan wakimbizi. Mwandishi, Tzvi, anasema: Leo kila mzawa anajua kwamba lau kama isingekuwa matukio ya mwaka 1948

ya Wapalestina kuzikimbia kwa wingi ardhi zao, Dola la Israeli lisingeundwa, hali ni zaidi katika kipindi cha usimamishaji wa mapigano ambapo dola hilo lilipanua mipaka iliyoainishwa wakati vita vya ukombozi vilipofikia kikomo .

Ama kuhusu Count Folke Bernadotte, Msuluhishi wa Umoja wa Mataifa, aliielezea hali ya vijiji viwili vilivyoelekezewa mashambulizi ya kidhalimu ya makundi ya kizayuni na jinsi wakazi walivyolazimishwa kuvihama vijiji vyao na kisha vijiji hivyo vikaharibiwa na kuteketezwa, kama ilivyoelezewa katika ripoti yake aliyoiwasilisha kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa. Aidha, katika utafiti uliofanywa na Prof. Israel Shahak kuhusu vijiji hivyo vilivyokimbiwa, anasema: Ukweli kuhusu vijiji vya Waarabu vilivyokuwepo kabla ya

mwaka 1948, ambavyo ni miongoni mwa ardhi zilizotumika kuanzisha dola la Israeli, ukweli huo ni mojawapo ya siri kubwa zinazofichwa sana katika uhai wa Israeli, kwani ni vigumu kupata ripoti, kitabu au kijarida kinachozungumzia idadi au mahali vilipokuwa vijiji hivyo, jambo lililofanywa kwa makusudi ili kwamba iweze kukubaliwa kama ngano/uwongo rasmi unaozungumzia nchi ambayo haikuwa na watu, ukifundishwa katika shule za Israeli

92
na kusimuliwa kwa wageni na watalii. Prof. Israel Shahak amewasilisha orodha
inayojumuisha majina ya vijiji 385 ambavyo viliharibiwa naWaisraeli na kufutwa kabisa vikiwa ni miongoni mwa vijiji 475 vilivyokuwepo kabla ya mwaka 1948. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni hali halisi na nyaraka nyingi kutoka katika hifadhi ya nyaraka za jeshi la Israeli zilianza kufichuliwa ili kuthibitisha kwama mamia ya mauaji ya kutisha yalitendeka na Wapalestina wasio na hatia waliuawa katika mauaji baridi (cold blood). Prof. Ytzhak, mhadhiri katika Chuo Kikuu Cha Barllan na Mtaalamu wa Historia za Kijeshi, amechapisha uthibitisho na uchunguzi wake kuhusu zaidi ya mauaji tisini ya kinyama yaliyotekelezwa ndani ya vijiji vya Wapalestina, miongoni mwake ni: Kijiji cha Sasa nyumba 20 zilibomolewa na kuwadondokea wakazi wake na watu 60 wakauawa. Kijiji Hawsan watu 12 walichinjwa bila sababu au kufanya uasi wowote; Kijiji cha Al-Dawayima watu 80 waliuawa na kuchinjwa (Mlima wa Al-Khalil (Hebron); kijiji cha Ailbon vijana 12 walipigwa risasi mbele ya macho ya kundi la wakazi waliozungukwa (katika eneo la AlJalil) na vijana wengine 17 wa Kibedui na wakazi wengine wa kijiji hicho wakiwa wametawanywa maeneo mbalimbali, inaonekana kana kwamba walikuwa wakitoa upinzani kwa wauaji; Kijiji cha Majd Al-kurum vijana 5 walipigwa risasi (katika eneo la Al-jalil); vijiji vya Banah Na Deir Al-Asad wakazi wa vijiji hivyo walikusanywa na vijana wanne kati yao wakachukuliwa na kupigwa risasi mbele ya hadhira ya watu; Kijiji cha Safsaf- watu 56 waliuawa baada ya kufungwa kamba na kutumbukizwa kisimani, wanawake wanne na binti mdogo mwenye umri wa miaka 14 walibakwa; Kijiji cha Saliha watu 94 waliuliwa kwa kuzidonndosha kuta za nyumba zao juu ya ya vichwa vyao; Kijiji cha Ayn Al-Zaytun watu 32 waliuawa na kisha saa walizokuwa wamezivaa mikononi mwao zikachukuliwa; Kijiji cha Qisarya kila aliyeshindwa kukimbia aliuawa; Kijiji cha Al-Kabri kijiji hicho kilivamiwa, vijana 7 wakauawa na waliobaki wakakimbia. Hakuna shaka hata kidogo kwamba mauaji na ukatili huu uliofanywa na vikundi vya kizayuni ulitekelezwa kwa mpango maalum ulioandaliwa kwa lengo la kuwafukuza Wapalestina. Muda mfupi uliopita (Shortly ago) katika mwezi wa Juni 1948 shirika la upelelezi la jeshi la Israeli lilichapisha waraka unaochambua sababu za kuwafukuza Waarabu nchini Palestina, waraka ambao unazikanusha kabisa propaganda za Kizayuni na kueleza baadhi ya sababu zilizokuwa nyuma ya mpango wa kuwafukuza Waarabu nchini Palestina kama zifuatazo: 1-Vitendo vya uadui na uhasama wa Wayahudi vilivyoelekezwa moja kwa moja kwenye vijiji, miji ya Waarabu na kuvidondosha vijiji na mijiji mikuu ya Waarabu, vitendo hivyo vinaunda 55% ya sababu zilizopelekea kuondoka kwa wananchi hao. 2-Operesheni zilizotekelezwa na makundi ya kigaidi ya Kiyahudi, kama vile Etzel na Lehi, yaliyohusika na vitendo vya kigaidi katika miji ya Yafa na Al-Jalili (Galilee), mji mkuu (city centre) na eneo la Al-Quds na kutekeleza mauaji ya kinyama ya Deir-Yassin (Deir-Yassin Massacre). Athari iliyosababishwa matukio hayo ni 15%. 3-Vita vya maneno ya vijembe na kisaikolojia vilikuwa na athari ya 2%.

93
4-Maamrisho na maonyo yaliyotlewa kwa wakazi waviache na kuvihama vijiji vyao ili kuyawezesha majeshi ya kiarabu kuwaokoa. Athari yake ni 5%. 5- Hofu kubwa na mashaka kuhusu uwezo wa majeshi ya Waarabu. Athari yake ni 11%. Kuhusu vurugu, hamisha hamisha na bomoa bomoa iliyofanywa dhidi ya vijiji vya Wapalestina katika Vita vya Siku Sita na baada ya vita hivyo, ni lazima kufahamu kuwa AlJalil na eneo la kaskazini ziliathirika na kupata pigo kubwa zaidi katika mpango huu, ambapo mwandishi maarufu Charles Caiman anasisitizia ukweli ufuatao katika makala yake yaitwayo, After the Disaster the Arabs in the Israeli State 1948 1950 (Baada ya Janga la vita vya siku sita Waarabu ndani ya Dola ya Israeli 1948 1950): 1. Vijiji 68 katika vijiji 73 vya wilaya ya Safad viliharibiwa. 2. Vijiji 21 katika vijiji 51 vya wilaya ya Akka viliharibiwa. 3. Vijiji 20 katika vijiji 23 vya wilaya ya Tiberias viliharibiwa. 4. Vijiji 17 katika vijiji 19 vya wilaya ya Baysan viliharibiwa. 5. Vijiji 32 katika vijiji 40 vya wilaya ya Haifa viliharibiwa. 6. Vijiji 4 katika vijiji 23 vya wilaya ya Nazareth viliharibiwa. Kwa sababu hiyo, matokeo yake ni kwamba vijiji 162 (na miji mitatu) ya Waarabu kutoka katika vijiji 229 vya mamlaka za kisheria zilizotajwa hapo juu viliharibiwa vibaya kabisa. Israeli ilianzisha upya sera ya kuwafukuza Waarabu hata baada ya kuanzishwa kwake na hata baada ya makundi ya Kizayuni kuvidhibiti vijiji na jamii za Waarabu.kadhia ya Birim, ambayo inaendelea kuingiliana na mahojiano ya wabunge wa bunge la Israeli (Knesset), ni shutuma za wazi kuhusu njia zilizotumiwa na viongozi wa Kiisraeli dhidi ya wakazi wa Kiarabu. Sera hiyo pia inashirikisha tamaa kubwa ya Wazayuni hao kuitakasa kimila ardhi hiyo kutoka kwa wakazi wake wa Kiarabu. Utafiti unaonesha kuwa operesheni za kuwafukuza kwa nguvu Wapalestina ziliendelea hata baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusimamisha ugumvi kwa muda yaliyofanyika mwaka 1949 baina Israeli na nchi za Kiarabu zinazopakana nayo. Kwa sababu mwaka 1950 wakazi wa Al-Ghabisiyya walifukuzwa na Israeli ikalitangaza eno hilo kuwa Kanda inayodhibitiwa na jeshi. Hali kama hiyo ilitokea pia katika maeneo ya Amqa, Kafr Inan na Saffuriyya ambapo mwaka 1953 wakazi wa maeneo hayo walifukuzwa. Kadhalika, wakazi wa vijiji vya Kirad Al-Baqqara na Kirad Al-Ghannama katika uwanda wa Hawla walifukuzwa mara kadhaa katika kipindi cha miaka ya 1948,1951 na 1956. Mwaka 1957, wakazi wa An-Naqb walifukuzwa na kukusanywa katika eneo la sayaj. Mwaka 1974, Isareli iliwafukuza wakazi wa Al Mafraj kutoka katika jiji chao kilichokuwa jirani na eneo la Khadirah na kuanzisha mahali hapo kinu cha kuzalisha umeme. Mwaka 1981, na baada ya kukamilishwa kwa muafaka wa Camp David baina ya Isareli na utawala wa Kimisri, maelfu ya Waarabu walitimuliwa kutoka eneo la Tall Al-Malh katika mji wa An-Naqb (Negev) mpaka katikati ya mji (city centre): maeneo ya Al-Ladd, Ar-Ramlah na Al-Muthalth kwa lengo la kujenga viwanja vya ndege vya kijeshi badala ya viwanja vilivyoachwa katika eneo la Sinai. Mwaka 1987, serikali ya Israeli iliunda kamati kwa lengo la kuchunguza majengo yasiyokuwa na leseni katika maeneo ya Wapalestina. Kamati

94
hiyo ilijulikana kama kamati ya Marcovitch, ambapo mwaka 1989 ilipendekeza kuwa inalazimika kubomoa makazi 11000 zinazomilikiwa na Waarabu kwa hoja ya majengo yasiyokuwa na leseni. Makazi haya yamegawanywa katika jamii 100 za Waarabu zisizotambuliwa na mamlaka za Israeli kwa lengo la kuwaondosha wakazi wa makazi hayo. Mwaka 1995, waziri wa Israeli wa ujenzi na makazi alitoa amri ya kuwaondosha na kuwafukuza wakazi wa kijiji cha Al-Hawashlah katika mkoa wa An-Naqb pamoja na eneo la Waarabu la Al-Jahileen. Mwisho wa makala ya wakili Wakim Wakim, Katibu Wa Kamati ya Kitaifa ya kutetea haki za watu waliohamishwa kutoka Israeli (National Committee for

the Defense of the Rights of the Uprooted in Israel).

Wazayuni pia walikimbilia kutekeleza mchakato wa kisheria na kiraia dhidi ya walioondolewa pamoja na vijiji vyao; hivyo hata baada ya uthabiti wa hali ya kijeshi mamlaka hizo ziliendelea kutumia taratibu zote za kiutekelezaji kisheria na kiraia kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa ardhi na vijiji walivyovichukua kwa mabavu kutoka kwa Waarabu, kwa sababu ya hofu ya kwamba Waarabu waliofukuzwa wangerejea katika vijiji vyao. Kwa sababu hii, mamlaka za Israeli ziliweka sheria na kanuni ambazo zilishuwaghulikia - kwa namna isiyokuwa ya moja kwa moja - watu walioondoshwa na kwa njia ya moja kwa moja zikishughulikia ardhi na vijiji vilivyoachwa. Kadhalika sheria hizo, zilianzisha mifumo ya ulazima wa hali ya dharura, kama vile kuyafunga maeneo hayo kijeshi. Kwa upande mwingine, mamlaka za Israeli ziliendesha mikakati ya kiraia na kuanzisha maelfu ya makazi ya Wayahudi kwenye ardhi za Waarabu, jambo lililopelekea kuongezeka kwa mchakato wa kuviharibu vijiji vya Waarabu ikiwa ni jaribio la wazi la kuwaondosha katika historia na kuwafuta katika akili za watoto wao waliokimbilia katika vijiji vya jirani vilivyokuwa vikimilikiwa na Waarabu. Umoja wa Mataifa unawaelezea wakimbizi hawa katika nyaraka zake kama ifuatavyo: Kila mtu aliyekuwa na nyumba ya kawaida nchini Palestina miaka miwili kabla ya mgogoro wa mwaka 1948 na kwa sababu ya mgogoro huo alipoteza nyumba yake pamoja na nyenzo zake za maisha na kukimbilia katika mojawapo ya nchi zilikopatikana huduma za Wakala wa Umoja wa Mataifa wa misaada na ustawi kwa wakimbizi wa Palestina katika mashariki ya mbali (UNRWA =United Nations Relief and Works Agency for the Palestinian refugees in the Far East). Kwa kipindi chote cha karne ya ishirini, raia wa Kipalestina walikumbwa na mawimbi makubwa ya kufukuzwa na kuondoshwa kwa wingi katika makazi yao, tukio kubwa zaidi likiwa ni lile la mwaka 1948-49 wakati wa vita vya Waarabu na Wazayuni, ambapo watu wapatao 800.000 waliondoshwa kabisa katika makazi yao. Wakati wa vita vya mwaka 1967 baina ya Waarabu na Wazayuni, watu wapatao 400000 waliondoshwa katika makazi yao, na mwaka 1991 wakati wa vita vya pili vya Ghuba watu wapatao 35000 waliondoshwa. Aidha, ziada ya udhibiti na sera za kimabavu ziliwekwa kwa nguvu kwenye maeneo ya Wapalestina yaliyonyakuliwa mwaka 1948 na 1967 (kwani upokonyaji wa ardhi, kubomoa nyumba, kunyanganywa haki za utaifa, upelekwa uhamishoni, pamoja na

95
sera za serikali na migogoro ya matumizi ya silaha katika jamii za kipalestina zilizotawanyika, yote hayo yalisababisha kuondoka kwa maelfu ya Wapalestina. Kwa sababu wakimbizi wengi wa Kipalestina ni wale waliohamishwa kabisa katika makazi yao mwaka 1948 sambamba na wajukuu zao (zaidi ya milioni tano) na wanawakilisha karibu theluthi moja ya idadi yote ya Wapalestina. Tukijumuisha idadi ya wakimbizi walioondoshwa katika makazi yao kwa mara ya kwanza mwaka 1967 pamoja na hawa waliopo katika Msitari wa Kijani (Green Line), yaani walipo ndani ya Israeli, tunakuta kwamba karibu robo tatu ya Wapalestina walifukuzwa katika makazi yao kwa katika kipindi cha nusu karne. Kwa msingi huu, wakimbizi wa Kipalestina ndio makundi makubwa na ya kale zaidi ulimwenguni. Wengi wa wakimbizi hawa wanaishi katika maeneo yanayokaliwa kimabavu ya Ukingo wa Magharibi, ikiwemo Al Quds (Jerusalem), na Ukanda wa Gaza umbali mabao ni karibu maili 100 kutoka kwenye makazi yao ya asili ambayo sasa yapo ndani ya Israeli, na wamepigwa marufuku kutekeleza haki yao ya kurudi kwenye maeneo hayo. Serikali zilizokuja baadaye nazo zilipinga suala la wakimbizi wa Kipalestina kurudi kwenye makazi yao, kwa sababu ya tamaa ya dola hilo kuihifadhi na kuilinda Israeli kama dola la Kiyahudi lenye eneo-ardhi la Kiyahudi pamoja na Wayahudi kuzishikilia na kuzitawala kikamilifu ardhi hizo. Tangu mwaka 1948 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa umetoa zaidi ya maazimio hamsini kukabiliana na Tatizo la wakimbizi wa Kipalestina, azimio muhimu zaidi likiwa ni azimio namba 194 lililotolewa 11-12-1948, ambalo lilikuwa likiwekwa wazi mara kwa mara katika maazimio yaliyofuatia. Azimio hili linasema: The Palestinian refugees problem, the most important among them was resolution 194 issued in 11-12-1948, that was repeatedly indicated in the succeeding resolutions. This resolution says: The refugees who wish to return to their country must be allowed to

return, and to peacefully live with their neighbors on the nearest date possible. As for those who do not wish to return they must be compensated for their belongings and the destruction and wreckage that befell them, and this is according to the international law or the principles of justice, and responsible governments or authorities should be bound to do this. Yaani: Wakimbizi wanaotaka kurudi nchini kwao wanapswa kuruhusiwa na
waishi kwa amani na majirani zao haraka iwezekanavyo. Ama wale wasiotaka kurudi wanapaswa kufidiwa mali, ubomoaji na uharibifu uliowapata, na hili linapaswa kufanywa kwa mujibu wa sheria za kimataifa au kwa misingi ya haki, na serikali na mamlaka husika zinatakiwa kulitekeleza hili. Kwa msingi wa azimio hili, iliundwa tume ya Kimataifa ya Haki na Maridhiano (International Conciliation Commission) kwa lengo la kuwezesha mchakato wa kuwarejesha makwao wakimbizi, kuwathubutisha kwa amani na kuwalipa fidia. Azimio namba 194 linachukuliwa kuwa msingi wa maazimio yote ya Umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi. Ni muhimu kuelewa kuwa Umoja wa Mataifa utaitambua Israeli kama taifa pale tu itakapolitekeleza kwa vitendo azimio hili. Lakini Israeli imejifunza kutoheshimu azimio

96
lolote linalotolewa na vyombo vya Kimataifa ila pale ambapo azimio hilo litakapokuwa linakwenda sambamba na maslahi na ulafi wake. Tunapozungumzia janga lililoikumba palestina (Vita vya siku sita) na mkakati wa kufukuza asilimia 80 ya Wapalestina kutoka katika maeneo yaliyoshikiliwa mwaka 1948, tunazungumzia janga na msiba mbaya zaidi kuwahi kuwakumba watu dunia katika kipindi cha nusu ya pili ya karne iliyopita. Kwani ukaliaji na ufukuzaji huu ni matokeo ya harakati ya uhasama wa ubaguzi wa kiitikadi, lakini ni watu wahache tu ndio wanaojali na kulitilia manaani. Ili kuyafahamu maazimio ya kimataifa yaliyotolewa kuhusu Palestina, ambayo Israeli haikuthubutu kuyaheshimu, Kituo cha Habari cha Kipalestina (Palestinian National Information Center) kilichopo chini ya mamlaka ya Palestina (Palestinian National Authority) kinatoa jeduali lifuatalo linaloonesha maazimio ya kimataifa, mazingira yake na tarehe ya kutolewa kwake: Maazimio Muhimu Ya Kimataifa Kuhusu Palestina

tarakimu 1.

namba ya azimio 181 kifungu 2

tarehe 29/11/1947

wahusika Mkutano Mkuu la Umoja wa Mataifa Baraza La Usalama la Umoja wa Mataifa

2.

42

5/3/1948

3.

43

1/4/1948

Baraza la

maudhui ya azimio Kuigawa Palestina katika mataifa mawili ya Waarabu na Wayahudi Kiapo cha serikali zote na wananchi, ikiwemo wale walio Palestina na maeneo ya jirani, kufanya juhudi zote zinazowezekana kuzuia au kupunguza hali ya ghasia na wasiwasi inayoendelea nchini Palestina. Wito wa

97
Usalama kuandaa makubaliano ya usimamishaji vita kwa muda kati ya jamii za Waarabu na Waisraeli na kusimamisha machafuko. Wito wa kikao cha dharura cha Mkutano Mkuu kudurusu upya kadhia ya utawala nchini Palaestina. wito kwa wote walio nchini Palestina kusimamisha harakati za kijeshi na vitendo vya ghasia, vitisho, ugaiadi na hujuma. Kuunda kamati ya amani ya Palestina. ombi kwa Baraza la Walinzi (Guardians Council) kudurusu njia za kuilinda Al-Quds (Jerusalem) na watu wake. Kupendekeza uteuzi wa ujumbe maalum

4.

44

1/4/1948

Baraza la Usalama

5.

46

17/4/1948

Baraza la usalama

6. 7.

48 23/4/1948 185 26/4/1948

Baraza la Usalama Mkutano Mkuu

8.

187

6/5/1948

Mkutano Mkuu

98
wa Manispaa ya Al-Quds (Jerusalem). Kuitambua kazi ya Kamati ya Palestina na kumteua Conte Barnadot kama msuluhishi na mpatanishi wa kimataifa. Uteuzi wa msuluhishi na mpatanishi wa Kimataifa. Kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina. Kuunda tume ya upatanishi, usuluhishi, haki na maridhiano yenye kazi ya kuripoti hali ya Jerusalem katika mfumo wa kudumu wa kimataifa. Kuwarejesha wakimbizi makwao na kuwalipa fidia. Azimio linaainisha uundwaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ustawi kwa

9.

189

14/5/1948

Mkutano Mkuu

10.

186

14/5/1948

Mkutano Mkuu Mkutano Mkuu

12

212

29/11/1948

12.

194

11/12/1948

Mkutano Mkuu

13.

302

8/12/1949

Mkutano Mkuu

99
Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Mbali. (UNRWA= United Nations Relief and Works Agency for the Palestinian refugees in the Far East). Kulaani shambulio la Isareli katika eneo la Gaza kwa kuliona shambulizi hilo kama uvunjifu wa makubaliano ya usimamishaji vita na uwajibikaji kwenye muafaka wa amani. Wito kwa Israeli kusimamisha harakati zinazohatarisha hali ya mji wa Al- Quds (Jerusalem). Kuonesha masikitiko juu ya hatua zilizofanywa na Israeli kubadilisha hali ya mambo katika mji wa

14.

106

29/3/1955

Baraza la Usalama

15.

2253

4/7/1967

Mkutano Mkuu

16.

2254

14/7/1967

Mkutano Mkuu

100
Al-Quds (Jerusalem). Kuamua na kuchanganua misingi ya amani ya haki na ya kudumu katika Mashariki ya kati. Kuunda kamati maalumu kuchunguza vitendo vya Israeli vya uvunjifu wa Haki za Binadamu katika meneo iliyoyakalia kimabavu. Kulaani uvunjifu wa Haki za Binadamu katika maeneo yaliyokaliwa kimabavu na kuitaka Israeli kuacha vitendo vyake vya ukandamizaji. Kuitaka Israeli kwa mara nyingine kusimamisha hatua zote zinazohataraisha hali ya mji wa Al-Quds (Jerusalem). Kuilaani Israeli kwa kuunajisi

17.

242

22/11/1967

Baraza la Usalama.

18.

2443 (Kifungu 19\12\1968 23)

Mkutano Mkuu

19.

2546(Kifungu 24)

11\12\1969

Mkutano Mkuu

20.

267

3\7\1969

Baraza la usalama

21.

271

15\9\1969

Baraza la Uslama

101
Msikiti wa AlAqsa na kuitaka kusimamisha hatua zote zinazohatarisha hali ya mji wa Al-Quds (Jerusalem). Kutambua haki ya Wapalestina ya kujiamulia mambo yao wenyewe na kuitaka Israeli kwa mara nyingine kuchukua hatua za haraka za kuwarejesha nyumbani wale waliofukuzwa. Kuisisitiza Israeli kusimamisha hatua zote za kunyanganya ardhi au kupanua ujenzi wa makazi katika maeneo yaliyochukuliwa kimabavu na kuitaka kamati maalumu kuendelea na kazi zake. Kuialika PLO, kama mwakilishi wa Wapalestina kushiriki katika mazungumzo ya Mkutano Mkuu

22.

2672 ( Kifungu 25)A,B,C,D

8\12\1970

Mkutano Mkuu

23.

2851(Term26) 20\12\1971

Mkutano Mkuu

24.

3210

14\10\1974

Mkutano Mkuu

102
wa Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la Palestina katika vikao vyake vikuu. Kuipa PLO hadhi ya kuwa shuhuda kwenye Mkutano Mkuu wa UN. Masikitik dhidi ya hali ya Israeli ya kutoheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayohusu harakati zake za kubadilisha hali ya mji wa AlQuds (Jerusalem). Hali ya mambo katika Mashariki ya Kati. Harakati haramu za Israeli katika maeneo yaliyotwaliwa kimabavu. Kulaani kitendo cha Israeli kuendelea kuyakalia maeneo ya Waarabu yaliyochukuliwa kimabavu

25.

3237

22\11\1974

Mkutano Mkuu

26.

298

25\9\1971

Baraza la Usalama

27. 28.

3414(Kifungu 30) 32\5

5\12\1975 28\10\1977

Mkutano Mkuu Mkutano Mkuu

29.

32\20

25\11\1977

Mkutano Mkuu

103
30. 33\29 7\12\1978 Mkutano Mkuu mwaka 1967. Kulaani kitendo cha Israeli kuyavamia maeneo ya Waarabu na kutoa wito wa suluhu ya kina. Kulaani hatua ya Isaraeli ya kuendelea kuvunja haki za Binadamu katika maeneo inayoyakalia kimabavu. Haki ya Waarabu ya kuwa na taifa /nchi huru na kuwa na haki ya kutumia maliasili zilizopo katika ardhi zao. Ujenzi wa makazi ya walowezi katika maeneo ya Wapalestina ni kitendo kisichokubalika. Wito kwa Israeli kuanza kuondoka kabla ya 15/ 11/ 1980 kutoka katika maeneo yote ya Waarabu iliyoyatwaa kwa mabavu tangu mwezi wa Juni

31.

34\90 A,B,C

12\12\1979

Mkutano Mkuu

32.

34\136

14\12\1979

Mkutano Mkuu

33.

446

22\3\1979

Baraza la Usalama

34.

7\2 the seventh urgent exceptional Term

29\7\1980

Mkutano Mkuu

104
35 35\110 5\12\1980 Mkutano Mkuu 1967. kutetea na kusisitiza haki ya mataifa ya Kiarabu na watu wate ambao maeneo yao yamekaliwa kimabavu na Israeli, kuwa na mamlaka kamili ya kutumia maliasili zao. Kulaani vikali dhulma za Isareli dhidi ya Lebanon na wananchi wa Palestina na kusisitiza kwa mara nyingine pingamizi kamili dhidi ya Uamuzi wa Israeli wa kuichukua kwa nguvu Jerusalem. Kuitaka Israeli kubomoa makazi ya walowezi wa Kiyahudi yaliyopo na kuachana na mpango wa ujenzi wa makazi ya walowezi katika maeneo inayoyakalia ikiwemo mji wa

36.

35\207

16\12\1980

Mkutano Mkuu

37.

465

1\3\1980

Baraza la Usalama

105
Al-Quds (Jerusalem). Kutangaza ubatili wa hatua zilizochukuliwa na isareli kubadili muundo wa mji wa AlQuds (Jerusalem). Kueleza kuwa sheria kuu (principal law) kuhusu Jerusalem haitambuliwi. Vitendo vya Israeli vya kunyonya maliasili zilizopo katika maeneo ya Wapalestina na Waarabu ni vitendo vilivyo kinyume na sheria. Kuilaani Isareli kwa sera yake katika maeneo inayoyakalia na kuzitaka nchi mbalimbali kutoipa misaada Israeli. Kulitambua na kulizingatia tatizo la palestina. Kuthibitisha kwa mara nyingine haki ya

38.

476

30\6\1980

Baraza la Usalama

39.

478

20\8\1980

Baraza la Usalama

40.

36\173

17\12\1981

Mkutano Mkuu

41.

4\7-E

28\4\1982

Mkutano Mkuu

42.

37\86 A,B,C,D,E 39\17

10\12\1982

Mkutano Mkuu Mkutano Mkuu

43.

23\11\1984

106
Wapalestina kujiamulia mambo yao na kuwa huru. Hali ya mambo katika Mashariki ya Kati. Hali ya mambo katika Mashariki ya Kati.

44 45.

39\136 A,B,C 39\146

14\12\1984 1984

Mkutano Mkuu Mkutano Mkuu

Jeduali hili lenye mkusanyiko wa maazimio ya Umoja wa Mataifa linaonesha wazi ukaidi na dharau isiyokifani iliyoonyeshwa na majeshi ya kivamizi ya Wazayuni kuhusu maazimio haya na kuendelea kuwavamia Wapalestina kwenye ardhi zao na kuyanajisi maeneo yao matakatifu. Azimio namba 2253 la tarehe 4/7/67, azimio namba 267 la tarehe 3/7/69, na azimio namba 476 la tarehe 30/7/1980, maazimio yote haya yanafichua azma ya Israeli kuibadilisha hali halisi ya mji wa Al-Quds (Jerusalem) na kuufanya kuwa mji wa Kiyahudi kutoka kwenye hali na sifa ya kuwa mji wa Kiislamu ili baadaye wapate kuwadanganya walimwengu, hasa katika zama zetu hizi, na kuwafanya waamini kwamba Al-Quds ni mji wa kiyahudi na hatimaye kuuvunja msikiti wa Al-Aqsa na kujenga Hekalu mahali pake, hekalu ambalo ni mojawapo ya ngano za uwongo na uzushi wao wa kidini. Katika kusisitiza juu ya maazimio haya yaliyoendelea kupuuzwa na Israeli, Umoja wa Mataifa ulitoa maazimio mapya yaliyoshutumu na kulaani ukaidi na uasi uliokuwa ukifanywa na Israeli dhidi ya maagizo ya taasisi za kimataifa pamoja na hatua yake ya kuendelea kubadilisha alama na mambo muhimu ya mji wa Al-Quds. Maazimio hayo yanayoishutumu Israeli ni pamoja na maazimio namba 2254 la tarehe 14/7/67, azimio namba 271 la tarehe 15/9/69 na azimio namba 298 la tarehe 25/9/1971, maazimio ambayo kwa masikitiko makubwa yalizuiwa na Israeli kutoyatilia umuhimu maazimio ya Umoja wa Mataifa. Aidha, azimio namba 478 la tarehe 20/8/1980 lilitangaza kutoitambua sheria kuu inayohusu mabadikliko yaliyotekelezwa na Israeli katika mji wa Al-Quds. Sio hayo tu, bali pia kuna maazimio mengine yanayolaani na kushutumu vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na ukandamizaji wa kidhalimu unaofanywa na Israeli. Maazimio haya ni namba 2546, 271, 2851, 32/20, 34/90 na 207/35. maazimio haya imam yanalaani uvunjifu wa haki za binadamu jambo ambalo ni mazoea ya Israeli, na kulaani mashambulizi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia au upanuzi unaofanywa na Israeli na kuyapora maeneo ya ardhi za Wapalestina. Aidha maazimio hayo yanalaani na kushutumu kitendo cha kuunajisi Msikiti Mtukufu wa AlAqsa, ambao ni nyumba ya ibada kwa Waislamu na ambalo Wayahudi hawana haki hata kidogo ya kuingia mahali hapo.

107
Taarifa za idara ya Habari ya Kipalestina inaeleza kuwa, wakimbizi wa kipalestina wametapakaa kwa wingi kwenye nchi za jirani, ambapo idadi ya Wapalestina ilikadiriwa kufikia watu 7766185 kwa mwaka 1998, asilimia 54 wakiishi nje ya mipaka ya Palestina na kukusanyika kwa wingi katika maeneo mengine ya ulimwengu wa Kiarabu, huku wengi wao wakiishi katika nchi za Jordan, Syria na Lebanon. Kwa maneno mengine wanaishi katika maeneo ya jirani kutokana na kitendo cha kuwafukuza katika makazi yao kilichotokana na Janga la mwaka 1948 lililopelekea wengi wao kukimbilia katika nchi za Kiarabu zinazopakana na Palestina. 1- Jordan: Kiwango cha wakimbizi wa kipalestina ni (31.4%) ya iadadi ya watu wa Jordan na ni zaidi ya (42%) ya wakimbizi wote wa Kipalestina. Sensa ya wakimbizi wa Kipalestina nchini Jordan inaonesha kuwepo kwa takribana wakimbizi milioni moja, asilimia 18 ya watu hao wakiishi katika makambi kumi ambayo yalihifadhi watu wapatao 280,000 kulingana na rekodi ya UNRWA. Idadi ya wakimbizi wanaoishi nchini Jordan iliongezeka tangu lilipotokea janga hilo lililotajwa hapo juu ambapo kwa mwaka 1948 idadi yao ilikadiriwa kufikia watu 100.000. Watu hawa ni wale waliovuka Mto Jordan na kuishi katika makambi mbalimbali. Baada ya Israeli kuyavamia na kuyakalia kimabavu maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza katika mwaka 1967 wimbi jipya la watu waliofukuzwa katika makazi yao lilimiminika na idadi yao kufikia watu wapatao 240.000. 2- Syria: kiwango cha wakimbizi wa Kipalestina nchini Syria ni (10.2%) ya wakimbizi wote waliosajiliwa, ambao wanawakilisha asilimia 2.3 ya wakazi wote wa Syria. Zaidi ya asilimia 30 ya wakimbizi wote wa Kipalestina nchini Syria wanaishi katika haya makambi. Kambi ya Al-Yarmok inayohifadhi zaidi ya Wapalestina 100.000 haimo katika orodha ya makambi rasmi yaliyo chini ya UNRWA, licha ya huduma zake mbali mbali kuenea katika kambi hiyo. Wakimbizi walio nchini Syria wanatoka katika mikoa ya kaskazini mwa Palestina, hususan Safad na Haifa. Wakimbizi hao ni asilimia 62 ya wakimbizi wote. Wengine walitokea katika miji ya Yafa, Tiberias, Akka na miji mingine. Mwaka 1967 zaidi ya watu 100,000 walihama kutoka katika Milima ya Golan (Golan Heights) wakiwemo wakimbizi wa Kipalestina kuelekea maeneo mbalimbali ya Syria. Aidha, maelfu ya Walebanon walikimbilia Syria wakati wa vita vya kiraia vilivyoivuruga Lebanon mwaka 1982. 3- Lebanon: baadhi ya wakimbizi wa Kipalestina walielekea Lebanon baada ya Janga la mwaka 1948. Wakimbizi hao ni asilimia 10 ya wakimbizi wote wa Kipalestina na wanaunda asilimia 10.5 ya watu wote wa Lebanon. Kwa sasa kuna kambi kumi na mbili za wakimbizi wa Kipalestina kwenye ardhi ya Lebanon, ambapo wakimbizi hao wanakabiliwa na matatizo mengi, matatizo muhimu yakiwa yakiwa ni: miundombinu dhaifu ya makambi, msongamano kupita kiasi na ukosefu wa ajira. Nchini Lebanon kuna kiwango kikubwa sana cha wakimbizi wa Kipalestina wanaoishi katika umaskini wa kupindukia na wamesajiliwa katika programu ya kuwa katika dhiki. Vilevile, wakimbizi waliopo Lebanon wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa haki za kijamii na za kiraia sambamba na ukosefu wa huduma za shirika la misaada

108
katika maeneo elimu, afya na huduma za kijamii. Aidha, katika kipindi cha miaka iliyofuatia vita vya kiraia, shirika la umoja wa mataifa la misaada na ustawi kwa Wapalestina (UNRWA) lilisitisha kabisa kutoa dhamana ya elimu ya bure, jambo lililopelekea kuzuka kwa matatizo kadhaa wa kadhaa, kama vile watu kukosa masomo, kukua kwa kiwango cha wasiojua kusoma na kuandika kilichofikia asilimia 48 ya wakazi wa makambini kulingana na takwimu za hivi karibuni, ambapo idadi ya wahitimu wa chuo kikuu ilididimia na kufikia asilimia 4.2. Katika kuhitimisha mjadala wa tatizo la wakimbizi wa Kipalestina tutatoa baadhi ya maelezo yaliyotolewa katika ramani ya kanda ya shughuli na operesheni za shirika la UNRWA. Maelezo na ufafanuzi huo unashughulikia utawanyikaji na ueneaji wa wakimbizi waliosajiliwa na shirika hili kuanzia tarehe 30 Juni 2001. Eneo Jordan Lebanon Syria Ukingo wa Magharibi Ukanda wa Gaza Jumla ya Maeneo Walio kambini 287.951 214.728 109.466 163.139 460.031 1.235.315 Walio nje ya kambi 1.351.767 168.245 282.185 444.631 392.595 2.639.423 Jumla 1.639.718 382.973 391.651 607.770 852.626 3.874.738

Jeduali hili linatoa ushahidi wa jinsi wakimbizi hawa walivyotawanyika sehemu mbalimbali baada ya kufukuzwa katika ardhi ambayo hapo awali ilikuwa imewakusanya pamoja, yaani Palestina. Aidha, linaonyesha kwamba wakimbizi walio nje ya kambi ni mara mbili ya wale walio ndani ya kambi, hii ikiwa na maana kuwepo kwa mateso na shida za hali ya maisha Vitendo vya kigaidi vya Wazayuni havikuanza leo bali vilikuwepo tangu siku ambayo Uzayuni uliingia kwa mara ya kwanza katika eneo la Mashariki ya Kati na ushahidi mkubwa wa hilo ni mauaji ya kinyama na umwagaji damu uliofanywa na unaoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya wamiliki halali wa ardhi kwa lengo la kuwalazimisha kuzikimbia ardhi zao na kuwaachia wageni wapya wa Kiyahudi. Vyanzo vilivyotumiwa na Kituo cha habari cha Kipalestina (Palestinian National Information Center) katika kutoa uthibitisho wa Historia ya Palestina: - Dr. Haitham Al-Kilany: the Arab Islamic Palestinian wars Palestinian encyclopedia, fifth volume, 1990. - Dr. Hindy Al-Bidary the Palestinian lands between Zionist claims and historical facts Cairo, the Arab League Printing House, 1988.

109
- Arab institute for practice and statistical researches. The demographic characteristics of the Palestinian people, Beirut, Anidl publishing house, 1985. - Mustafa Ad-Dabagh, Our Country Palestine first part, At-Taliah publishing house, Beirut, 1965. - Araf Al-Araf, The Disaster, p. 952. - Bayan Nuwayhad Al-Ht, Palestine: the Problem and the People, Al-Istiqlal publishing house, 1991. - Al-Yas Shofany, compendium of Palestine History, Palestinian studies institute 1998. - Dr. Abdul-Wahab Al-Kialy, compendium of Modern Palestine History Beirut, Arab institute, 1975. - Asmaa Abdul-Hady Faur, Palestine and the Jewish claims, Al-Ummah publishing house, 1990. - Publications of the Palestinian studies institute\Lebanon defense ministry. Palestinian problem and Zionist danger Beirut studies series, 1973.

Ufafanuzi wa maelezo: (1) Fatimiyyiin: (2) Mandate: nchi moja kukabidhiwa madaraka ya nchi nyingine.

You might also like