Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Save to My Library
Look up keyword
Like this
3Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUR FEBRUARI 24-MACHI 1, 2012

ANNUR FEBRUARI 24-MACHI 1, 2012

Ratings: (0)|Views: 1,926 |Likes:
Published by MZALENDO.NET

More info:

Published by: MZALENDO.NET on Feb 26, 2012
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

02/26/2012

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1000 RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA FEBRUARI 24-MACHI 1, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
Hatari kubwa Songea
Imam wa Msikiti achinjwa, kisa..Wananchi wapeleka maiti kwa RPCNi baada ya kutoa kauli za maudhi
Mchawi wa ZanzibarSi Joyce Ndalichako
Uk. 8
Tutizame kuna nini paleHamamni, Haile Selassie
Mtoto Aziza awaliza wazazi, walimuAtaka Wizara ya Elimu wawajibike
RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein. AZIZA Mohamed
WAZIRI wa Elimu (SMZ)Ramadhan Abdallah Shaban
 MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit  Mwambungu
 
2
AN-NUUR
RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA FEBRUARI 24 - MACHI 1, 2012
TAHARIRI/UJUMBE
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM.
www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOLMafunzo maalum kwa wanaorudia kufanyamtihani wa Kidato cha Nne, Oktoba 2012
Ubungo Islamic High school inawatangazia wanafunzi Waislamu wote kuwaimeandaa mafunzo maalum kwa wale wanaotarajia kurudia kufanya mtihaniwa kidato cha Nne, Oktoba 2012.Mafunzo hayo yatasimamiwa na waalimu maalum wenye sifa na uwezo wakuhakikisha kuwa mwanao anapata Elimu bora na malezi mema.Masomo yanayofundishwa ni: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Arabic, Civics,Mathematics, English, Kiswahili, History, Geography, Physics, Chemistry,Biology, Commerce na Book-Keeping.Masomo yataanza tarehe 01/03/2012 hadi 31/08/2012. Ni mafunzo maalumkwa muda wa miezi sita.Fika ofisi ya Mkuu wa Shule upate fomu yako kwa bei ya Tsh 10,000/=.Kwa mawasiliano zaidi: 0754 260241
Mlete mwanao! Asipoteze nafasi hii adhimu
MKUU WA SHULE
Polisi wasiwe kamaraia warusha mawe
WALA msilegee, walamsihuzunike, kwani nyinyindio wa juu mkiwa niWaumini (3:139).
Huzuni ikipitilizahumpelekea mtu kukatatamaa na kutoona thamaniya maisha na hata kufikiahatua ya kunywa sumu aukujiua wakati furaha ikizidihumfanya mtu akasahaumajukumu mengine mazitoyaliyo mbele yake.Matokeo ya kidato channe yaliyotangazwa hivikaribuni yamewaachawanafunzi na wazaziwengi kwenye majonzihuku wachache wakiwa nafuraha. Hii ni kutokana naidadi kubwa ya wanafunziwaliomaliza kutofanyavizuri katika mitihani yao.Katika matokeo hayo,kati ya watahiniwa 426,314waliofanya mtihani huoOktoba mwaka jana, niwahitimu 33,577 sawa naasilimia 9.98 waliopatadaraja la kwanza hadi latatu.Wahitimu 146,639sawa na asilimia 43.60walipata daraja la nne na156,089 sawa na asilimia46.41 walifeli kabisa kwa
Muongozo kwa Wahitimu Kidato cha Nne
kuambulia daraja la sifuri.Vyovyote iwavyo,matokeo haya si yakujivunia kwani yanatoafursa finyu kwa vijana wetukuweza kujiendeleza.Pamoja na hilo, kubwani kuangalia namna boraya kusonga mbele kwawale ambao hawakufanyavema wakijipanga upyakuangalia ni yepi yakufanya ili kuweza kusongambele baada ya jitihada zaozilizotangulia kutofanikiwawakati wale waliofauluvizuri wakiweka mipangona mikakati madhubutiitakayowawezeshakuendelea zaidi. Jambo la kwanzaanalopaswa kulitambuamwanafunzi ni kukubalimatokeo aliyoyapata.Kuukana ukweli huuhakutakuwa na msaadakwake. Ni wazi zinawezakuwapo kasoro za hapana pale katika masuala yausahihishaji, lakini mchangowake katika matokeo ya jumla unaweza usiwemkubwa sana. Hata hivyo,endapo itathibitika kuwakuna hujuma za makusudidhidi ya wanafunzi aushule fulani zilizopelekeawanafunzi kufeli aukufutiwa matokeo, ni vemasuala hilo likafuatiliwa kwakina na taasisi husika ilihaki itendeke.Kwa muhtasari, matokeoya kidato cha nne unawezakuyagawa katika makundiya daraja la kwanza, darajala pili, daraja la tatu, darajala nne na daraja sifuri.Aidha unaweza kuyagawakatika makundi manne -walio na sifa za kuendeleana kidato cha tano na vyuovya ufundi; walio na sifaza kujiunga na vyuo vyaualimu lakini hawana sifaza kuendelea na kidato chatano na vyuo vya ufundi;walio na sifa za kujiunga navyuo vingine; na waliofelikabisa ambao wanakosa sifaza kuendelea na masomoya kidato cha tano na vyuokwa vigezo vya ufaulu wakidato cha nne.
Kujiunga kidato cha tanona vyuo vya ufundi
Awali ya yote ifahamikekuwa wanafunziwanaochaguliwa moja kwa
Inaendelea Uk. 4SOTE tunafahamu kwambakazi kubwa ya Jeshi la Polisinchini ni kulinda usalamawa raia pamoja na mali zao.Kuzuia uhalifu na kutoamsaada katika matukiombalimbali ya kibinadamukama kusaidia wagonjwana kutatua baadhi yamizozo ya wananchi paleinapowezekana.
Askari Polisi hakupewaajira kwa ajili ya kuua watu,kutishia watu, kudhulumuwala kusababisha vurugukwasababu tu ya jeuri yawadhifa wake au kwa maslahiyake. Jana vyombo vya habarivimeripoti kwamba watuwanne wameuliwa kwakupigwa risasi na polisimjini Songea MkoaniRuvuma, huku wengine 41wakijeruhiwa. Mauaji hayoyamedaiwa kufanywa naaskari wa jeshi la polisi mkoanihumo, walipokuwa wakizuiamaandamano ya wananchiwaliokuwa wakielekeaOfisi ya Mkuu wa mkoa waRuvuma, Said Mwambungukutoa kilio chao cha kukithirimauaji ya ndugu zao kwasababu ambazo mpaka sasahazijajulikana.Wananchi haowamenukuliwa wakisemampaka sasa watu tisawameuliwa na hakuna mtualiyekamatwa na kutiwahatiani kutokana na mauajihayo.Tunafahamu sote kwambauhai wa mtu ni jambo lamsingi kuliko jambo jinginelolote lile. Kama watu tisawanauliwa na polisi wapolakini hakuna anayetiwahatiani, katika hali ya kawaidamazingira haya ni ya hatarizaidi kuishi watu.Pia kwa kiwango chamauaji kama hicho bila yawauaji kubainika, ni wazikwamba yanajengwa mazoamabaya ya kuua watu zaidikwa imani kwamba hataukiua hutatambulika.Itafika mahali hata ugomvimdogo tu wa kubishanaukasababisha kulipwa kisasicha kuua kwa kuwa muuwajiatakuwa na hakika kwambahakuna atakayemchunguzana kumbaini. Ndio maanawananchi wameandamanakupinga mazingira haya yasijekuzoelekea na kuonekana yakawaida.Hatuhitaji kufika huko,ni mtazamo wetu kwambakatika suala hili, kulikuwahakuna haja ya kuwazuiawatu waliokuwa wakitakakufikisha kilio chao kwakiongozi wao, tena kilio chamsingi kinachohusu maishaya watu kwa njia ya amani.Tunaona kwamba ubavuuliotumika kuwasulubu raiawema hao, waliokuwa nania njema ya kushitakia kwakiongozi wao juu ya jinai yamauaji, huku polisi ambaondio wenye jukumu la kulindausalama wao wakishindwakuchukua hatua stahiki.Hatudhani kwambayangetokea mauaji iwapowananchi hao waliochoshwana vitendo vya mauaji dhidiyao wangeachwa wakamfikiaMwambungu na kutoa kiliochao. Wala hatuamini kwambakama mauaji yanayotokeamara kwa mara mjinihumo yangetendewa hakina Polisi kwa kuchunguzana kuwakamata wahusika,wananchi hao wangepatwana hamu ya kuandamanakwenda kumuona Mkuu waMkoa.Tunaona kwamba shidayote hii, ni matokeoa ya polisiwenyewe kushindwa kutimizawajibu wao kila yanapotokamauji mjini humo. Hali hiyondiyo iliyowafanya wananchikuchoka na kushindwakuendelea kupiga kimya.Yamekuwa ni mazoea kwa jeshi letu la polisi kutumianguvu kupita kiasi dhidi yaraia, hata pale ambapo nguvuhizo hazistahiki.Mara nyingi wanausalamahawa huamini zaidi katikakutumia jazba na njia ya mkatoya risasi za moto kutulizahali. Wanafanya hivyo kwamakusudi wakiamini kuwahata wakiua, kuna kauli nzuriya kujilinda nayo dhidi ya jinai hiyo. Kwamba walikuwawakijihami.Ushauri wetu ni kwamba,kuna haja ya jeshi la polisikufika mahali na kutahayarikwamba sasa kashfa na aibuza mauaji wanayofanya,imetosha. Watumie ujuzizaidi na wawe na dhamira nanguvu ya kudhibiti hasira namunkari wao.Wao wana mabavu,wana marungu na risasi zamoto. Wasiwe wepesi wakutumia zana hizo kamawaandamanaji na wananchiwanaorusha mawe.
 
3
RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA FEBRUARI 24 - MACHI 1, 2012
AN-NUUR
HABARI
VIKOSI vya utawalaharamu wa Israelvimeufunga msikiti waal Aqsa, mashariki mwaQuds tukufu baada yakujiri mapigano makalikati ya walowezi waKizayuni na Wapalestinawaliokuwa wakitekelezaibada zao katika msikitihuo.
Habari zinasema kuwa,mapigano hayo yalianza baada ya makumi yawalowezi wa Kizayunikuingia katika eneo lamsikiti huo mtukufu nakuwashambulia wauminiwaliokuwa wakiendelea naibada zao.Raia kadhaa wa Palestina
 Vikosi vya Israel vyafungamsikiti wa al Aqsa
wamejeruhiwa katikahujuma hiyo.Vikosi vya utawalaghasibu wa Israelvimefunga milango yote yakuingia katika msikiti huona hivyo kuwafungia ndanimakumi ya Waislamu waPalestina waliokuwemondani.Msikiti wa al Aqsa,ambao ni kibla cha kwanzacha Waislamu na moja yamaeneo matukufu sanakwa Waislamu, umekuwauwanja wa mapiganokati ya askari wa jeshi lautawala wa Kizayuni waIsrael na Waislamu waPalestina tangu utawalahuo ulipokalia kwa mabavuardhi ya Wapalestina.
Tutizame kuna nini paleHamamni, Haile Selassie
MWANAFUNZI huyuanauliza, “kwa nini sisitufutiwe matokeo yetu?”
Anasema, “nakuombeniwazee na walimu wetutushikamane tusiogope kufawala nini.”Hata hivyo anawajia juuwazee akisema, “lakini,wazee mnatuponza maanasisi mlituunga mkono wakatiwa kufanya maandamano”.Halafu ikawaje? Anasema“tulipewa kibali na tukafanyamaandamano lakini matokeoyake wazee mlituruka baadaya kuona polisi wamekujakutupiga mabomu ya machozimkatuacha sisi wanafunzipeke yetu tukikamatwa nakupigwa na polisi.”Huyo ni Aziza Mohammedambaye hivi karibunialiwaliza wazazi alipokuwaakizungumzia masaibu yakena wenzake waliofutiwamatokeo ya mtihani wa kidatocha nne.Aziza ambaye nimwanafunzi kutoka skuliya Laureate amesema,wanyonge wanaonekanahawana haki kwani pamojana kusoma katika mazingiramagumu yasiyo rafiki kwausomaji na usomeshaji, sasawameadhibiwa na inaonekanaSerikali ya Mapinduzi haipotayari kuwatetea.Anawashutumu piawazee akisema kuwawameonyesha udhaifumkubwa katika kutetea hakipale walipowaacha wanafunziwakipigwa virungu na polisi
Na Mwandishi Wetu
wao wakatimua mbio.Hiyo ilikuwa ile sikuwanafunzi wa skuli zaZanzibar walipotaka kufanyamaandamano kupingakitendo cha Baraza la Mitihanikuwafutia matokeo.Akiongea katika namnaambayo anawakilisha kiliocha watoto wanyonge kutokakatika familia zenye kipatokidogo, Aziza amesema ndotozao zimeyeyuka na hawajui lakufanya.Kilichomsikitisha zaidianasema ni pale ambapowalipigwa na polisi walipotakakuonyesha masikitiko na hisiazao kwa maandamano.Akifafanua alisema,walipata kibali chamaandamano ila walikamatwana kupigwa kwa kutetea hakizao.Akasema, ndoto zaozimekuwa kama ndegealiyeruka hawana cha kufanya,“ni mambo ya kusikitishasana kwetu na ndugu zetundoto zetu zimekufa.”Mwanafunzi huyoakizungumza hivi karibunikatika kongamano lakujadili kufutiwa matokeo,aliwaliza washiriki kutokanaalivyokuwa akichangia madahiyo ya elimu.Alisema, wamesomakwa taabu huku wazaziwao masikini wakihangaikahuku na huko kupata pesaza ada, sare za shule na vifaavingine, lakini baada ya juhudi zote hizo, hapo ndipowalipoishia.Watoto wengiwaliozungumzia suala hili,wanailaumu serikali kwakutoonyesha dhamira yakweli ya kulifuatilia suala hilihuku ikijua kuwa madharayake ni makubwa kwa watotowa wanyonge.Ikasemwa kuwa huenda nikwa vile watoto wa wakubwaserikalini hawasomi katikaskuli za serikali zisizo nasifa ya kuwa shule katikazama hizi ndio maanahaiwashughulishi.Baadhi ya watu waliotoamaoni wanasema kuwa wengiwa wanafunzi waliofutiwamatokeo wakiwa wanatokanana familia za kimasikini,wamebaki wakilalama hukuwakiwa na huzuni na hivisasa wanahangaika huku nakule bila ya mafanikio.Imekuwa kana kwambawatoto hawa wa kimasikinidunia imewapa mgongo nahuko wanakokwenda ni kizakitupu na hakuna mtu wakuwaashia taa ya kuona kilipousoni.“Inasikitisha, inahuzunishana inatisha kuona viongoziwetu wengi wanaliona sualala kufutwa matokeo yamtihani kama vile ni jambo lakawaida na hawataki kukubalimadhara yake kwa vijanawetu waliofutiwa matokeoya mitihani.” Anasema SalimSaid.“Hivi sasa katika kila pembeya Unguja na Pemba wazazina watoto wao wanasikitikana wengine kulia kutokanana kufutwa kwa matokeo yamithani wa kidato cha nnekwa mamia ya watoto wa
Inaendelea Uk. 7
Hatari kubwa Songea
HALI si shwari tena Songea.Sheikh Jamaldeen, Imamwa Msikiti wa Kitera, nimiongoni mwa watu sitawaliouliwa katika kipindikisichozidi wiki tatu.
Sheikh Jamaldee aliuliwakwa kupigwa panga lashingo na kichwani saa 3usiku tarehe 20 Februari,2012 wakati akitokakufungisha ndoa.Alifanyiwa ukatili huokiasi mita 80 tu kutokanyumbani kwake hukuwauwaji wakiondoka bilaya kuchukua chochote.Aidha, hakuna kiungo chamwili wake kilichokatwakinyume na baadhi ya taarifaambazo zimelihusisha tukiohilo na ushirikina.Kesho yake, kwa maanaya Februari 21, tukio kamahilo lilitokea tena katikaeneo la Matarawe.
Na Mwandishi Wetu
Aliuliwa kijana maarufukwa jina la Bambo akiwadereva wa pikipiki,Bodaboda.Awali kijana huyu alikuwakondakta wa basi la Bambolinalokwenda Mbinga.Kufuatia mauwaji ya kijanahuyo, wananchi waliamuakuchukua maiti yake nakuipeleka kwa Kamandawa Polisi wa Mkoa (RPC)Michael Kamuhanda.Taarifa kutoka eneola tukio zinafahamishakuwa wananchi waliamuakuchukua hatua ya kupelekamwili wa marehemu ofisinikwa RPC Kamuhanda badalaya chumba cha kuhifadhiamaiti hospitali kutokana nakauli zilizokwisha kutolewana Kamanda huyo ambazoziliwaudhi wananchi.Awali, kupitia Redio Jogoo, Mkuu huyo waPolisi alikaririwa akisemakuwa mauwaji yanayotokeaSongea yanatokana na wivuwa kimapenzi.Kwa upande mwingineakasema kuwa hakunamauwaji ya kutisha yamfululizo yanayotokeaSongea, bali ni watutu wanazua na kukuzamambo.Kufuatia madai hayoya RPC, ndio alipouliwakijana ‘Yebo’ wananchiwakaamua wampelekeemaiti akaone kuwa kweliwatu wanauliwa.Hata hivyo, polisiwaliingilia kati kuzuiyamaiti isipelekwe kwa RPCna ndio ikaishia katikamaandamano yaliyopelekeamaafa ya kuuliwa watu nawengine kujeruhiwa.Kauli ya Kamanda waPolisi katika Redio Jogooilikuja baada ya kutokeamauwaji ya mfululizo nawananchi kuanza kushumuPolisi kwamba hawajachukuahatua au bila ya kusikiakwamba kuna watuhumiwawamekamatwa.Pengine katika kujiteteandio RPC akasema kuwa,kwanza hakuna taarifa zamauwaji ya kutisha, balitaarifa za kutiwa chumvina kwamba kama yapomauwaji, basi yanatokanana wivu wa mapenzi.Hata hivyo, wana-Songeawanauliza, inakuwaje wivuhuu wa kuuwana uje mudahuu tena ulete mauwaji yamfululizo ya watu sita katikakipindi cha wiki tatu?Wimbi hili la mauwajililianzia Ruhuwiko, likajaMlete na kufuatia Lizabon.Kote huko aliuliwa mtummoja mmoja na woteama hupigwa mapangaau nondo na hakuna kitukinachochukuliwa.Taarifa zinafahamishakuwa kutoka Lizabonakauliwa mtu mtaa waRuvuma, mjini hapa Songeandipo yakaja haya ya juzi yaSheikh Jamaldeen na kishakijana ‘Yebo’. Jambo ambalo lipo wazini kuwa mauwaji hayahayahusiani na masualaya wizi au ujambazi kwanihakuna mali inayochukuliwakwa kila aliyeuliwa.Wapo wanaodai kuwani masuala ya kishirikina,lakini pia inakuwa vigumukuthibitisha kutokana namazingira ya mauwajikutoacha alama rahisikutafsirika hivyo.Wengine wanaingia ndanizaidi wakihusisha matukiohaya na uingiaji wageniambapo sasa Songea sio ileya zamani.Ukiacha wageni wakutoka humu humu nchinina nchi jirani za Kiafrika,wapo pia Wamarekani naWaisrael.Wapo Waisrael ambaowanadai wamekujakuwekeza katika mashambaya kahawa na wamepewashamba la zamani la Meralilililopo Lipokela, njia yakwenda Mbinga.Kwa upande waWamarekani, hawainaelezwa kuwa wapokatika madini ya Uranium,Namtumbo. Na mudamwingi wengi wanaonekanamjini Songea katika internetna madukani.Kuwepo kwa wageni hawana wafanyakazi wao kutokamikoa mbalimbali na nchimbalimbali ukiacha walewajasiria mali wanaokujakama watu binafsi, ndiohudaiwa kubadili hali yaSongea.Kwamba huenda wagenihawa wamekuja na tabiaambazo hazikuwepo Songeana Ruvuma kwa ujumla.Hata hivyo bado ni jambolinalohitajika kufanyiwauchunguzi kwamba. Swalini je, mauwaji haya kwalengo gani?Ingekuwa yana alamaya ujambazi, basi hililingeeleweka haraka.Lakini inapokuwa kuuwa bila kuchukua chochote,hapa pana utata mkubwawenye kutaka tahadharikubwa.Yalikuwepo pia madaikwamba kuna kikundicha washirikina kutokaMsumbuji ambacho huuawatu na kunyofoa viungona kutoweka navyo.Na wengine wakisemakuwa huenda walewaliokuwa wakifanyamauwaji Mbeya na kunyofoaviungo ndio wamehamiaSongea.Hata hivyo, habarizinaonyesha kuwa katikawatu wote hawa sitawaliouliwa mfululizo,hakuna aliyenyofolewakiungo chochote.Katika hali kama hii,uchunguzi makini na wakina wa polisi unahitajikaili kujua nini hasa kinatokeaSongea hivi sasa.

Activity (3)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 thousand reads
1 hundred reads

You're Reading a Free Preview

Download
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->