Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
1Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
IKIMBIE ZINAA

IKIMBIE ZINAA

Ratings: (0)|Views: 8|Likes:
Published by ngulumi82
IKIMBIE ZINAA
IKIMBIE ZINAA

More info:

Published by: ngulumi82 on Jul 01, 2012
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

02/25/2014

pdf

text

original

 
SOMO: IKIMBIENI ZINAA
 
Wiki ya Kwanza
 
 
Je! Unaamini ya kuwa Mungu anaweza kusema na watu kwa njia ya ndoto? Najua ni rahisikuamini kuwa Mungu alisema na watu zamani kwa njia ya ndoto kama tunavyosoma katikaBiblia; lakini je! Unaamini ya kuwa Mungu anasema na watu kwa njia ya ndoto siku hizi?Najua kuna watu wanaoamini na wengine hawaamini. Sijui wewe uko upande gani.
Lakini nataka nikueleze hivi; Kufuatana na Biblia kuna ndoto za aina tatu;
 (a) Kuna ndoto kutoka kwa Mungu. Soma kitabu cha Hesabu 12:6, na Yoeli 2:28.(b) Kuna ndoto zinakuja kwa sababu ya shughuli nyingi. Soma kitabu cha Mhubiri5:3.(c) Kuna ndoto za uongo zinazotoka kwa shetani aliye baba wa uongo. Soma kitabucha Yeremia 23:52 na Yohana 8:44.Unaweza kutofautisha kwa namna gani tofauti iliyopo kati ya hizi ndoto? Na utajuaje kuwandoto uliyoiota imetoka kwa Mungu? Kila ndoto lazima ipimwe na Neno la Mungu. Ikiwaimetoka kwa Mungu, ni lazima utakuta neno la Mungu ambalo linaeleza maana yake. Maranyingine ndoto toka kwa Mungu huja kama fumbo; lakini Roho Mtakatifu ajuaye kuyafumbuamafumbo ya Mungu (1 Wakorintho 2:10,11), atalifunua fumbo hilo kwa kukuonyesha neno laMungu linalofanana na ndoto hiyo.Si busara kuzikubali ndoto zote unazoota bila ya kuzipima katika Neno la Mungu. Na pia sibusara kuzikataa ndoto zote bila kuzipima katika Neno la Mungu.Nimeona nianze kwa kukueleza haya kwa kuwa chanzo cha kuandika kitabu hiki, ni ujumbewa Mungu ulionijia kwa njia ya ndoto.Ndoto yenyewe ilikuwa hivi: Niliona katika ndoto mtu mmoja mkristo, tena aliyeokokaakifanya mambo ya zinaa bila hata kuogopa. Na wakati nilipokuwa nikimtazama na kusikitika,nikasikia sauti toka juu yangu ikisema;
“ NITACHUKULIANA MPAKA LINI NA MWANADAMU AFANYAYE MAMBOYA JINSI HIYO?”
Baada ya kusikia maneno hayo nikaamka.Wakati huo ulikuwa ni alfajiri, na ndoto hiyo ilinipa maswali na masononeko mengi moyonimwangu. Na niliamua kumshirikisha mke wangu Diana juu ya ndoto hiyo.Mke wangu akaniuliza;
“ Maana yake nini ndoto hiyo?”
 
 
Nilipotaka kufungua kinywa ili nimjibu uchungu mzito ulijaa moyoni mwangu, nikasikiakuugua rohoni, na mara nikaanza kulia!Unaweza ukaniuliza;
“Mwakasege kwa nini ndoto ikulize machozi?”
 Hili ni swali zuri. Hata mimi nilijiuliza kwa nini nitoe machozi kwa ajili ya ndoto. Lakinibaada ya kulifuatilia jambo hili katika maombi na katika neno la Mungu nilielewa sababu yake.Je! Unafahamu matokeo ya Mungu kusema
“Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamuafanyaye mambo ya jinsi hiyo?”
Ukisikia maneno ya jinsi hii ujue Mungu amekasirika na kunamaangamizo mbele.Hebu na tulifuatilie jambo hili katika biblia ili tulione uzito wake.
Nuhu na Gharika.
 Ni vizuri ukumbuke ya kuwa gharika ilitokea wakati wa Nuhu kwa sababu ya zinaa.
“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
wana wa Mungu waliona hao binti za wanadamu
 – 
ni wazuri; WKAJITWALIA WAKEWO WOTE WALIOWACHAGUA. Bwana akasema, ROHO YANGU HAITASHINDANANA MWANADAMU MILELE, kwa kuwa yeye ni nyama; basi siku zake zitakuwa mia naishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile, tena baada ya hayo, wana wa MunguWALIPOINGIA kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watuhodari zamani, watu wenye sifa. BWANA AKAONA YA KUWA MAOVU YAMWANADAMU NI MAKUBWA DUNIANI NA KWAMBA KILA KUSUDIANALOWAZA MOYONI MWAKE NI BAYA TU SIKU ZOTE. BWANA AKAGHAIRIKWA KUWA AMEMFANYA MWANADAMU DUNIANI, AKAHUZUNIKA MOYONI.Bwana akasema, Nitamfutilia usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambulisho nandege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata
neema machoni pa Bwana.”
(Mwanzo 6:1-8)Ukiendelea kufuatilia habari hii katika Biblia utaona ya kuwa baada ya gharika ya majiwalibaki watu nane tu! Wanadamu wengine wote waliangamia kwa sababu ya nini?
 – 
Zinaa!
Sodoma na Gomora
 Wasomaji wa Biblia wanafahamu kabisa ya kuwa miji ya Sodoma na Gomorailiteketezwa kwa moto baada ya Mungu kuihukumu kwa sababu ya uasherati uliokuwaukifanyika ndani yake. Soma Mwanzo 19:4-25.Na pia katika kitabu cha Yuda 1:7 tunasoma hivi: -
“Kama vile Sodoma na Gomara, na miji iliyokuwa kando kando, waliofuata
UASHERATI kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili,imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa mile
le.”
 
 
Ikiwa Mungu aliwatenda hivi watu wa Sodoma na Gomora, ni kitu gani kinamfanyamwanadamu wa siku hizi adhani ya kuwa Mungu amebadilika juu ya kuadhibu wale wotewafanyao uasherati? Katika miji hiyo miwili ni watu watatu tu waliobaki
 – 
Lutu na watoto wakewawili! Wanadamu wengine waliokuwa katika miji hiyo waliteketezwa kwa sababu ya nini
 – 
 Zinaa!
Kuhani Eli na watoto wake.
 
“Basi Eli alikuwa mzee sana, naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe
waliwatenda Waisraeli; na jinsi WALIVYOLALA NA WANAWAKE waliokuwa
wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania.”
(1Samweli 2:22)
Hata baada ya baba yao kuwaonya hawakusikia, na matokeo yake ni:-
 1. Watoto hao wawili, Hofni na Finehasi walikufa wote siku moja;2. Wana wa Israeli walipigwa na adui zao Wafilisti na Sanduku la aganolikatekwa;3. Kuhani Eli alikufa.Yote haya yalitokea katika taifa ambamo watoto wawili wa kiongozi waliuwa wakifanyamambo ya Zinaa bila hata kujali maonyo.Je! Bado unajiuliza kwa nini nilitoa machozi baada ya kusikia sauti ya Mungu katika ndotoikisema
“Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamu afanyaye mambo ya jinsi hiyo?”
 
Siku za Mwisho.
 
“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana
 watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye
kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi…….Kwa
maana katika hao wamo wale WAJIINGIZAYO KATIKA NYUMBA ZA WATU, NAKUCHUKUA MATEKA WANAWAKE WAJINGA WENYE MIZIGO YA DHAMBI,waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi.
(2 Timotheo 3:1,26).Je! Siku hizi wanawake hawatekwi mateka na wanaume ili wafanye mambo ya zinaa?Vishawishi vimekuwa vingi, na wanawake wengi wameanguka katika mitego hiyo ya kupendafedha na anasa, na mwisho wake ni kufanya uzinifu.Kwa nini wanaume wengi wamekosa akili juu ya jambo hili. Ni kitu gani kimewapofushamacho wasione ya kuwa uzinifu ni mbaya? Biblia inasema;
“Mtu aziniye na mwanamke hana
akili kabisa; afanya jambo litaka
lomangamiza nafsi yake.”
(Mithali 6:32)Ni dhahiri ya kwamba palipo na zinaa pana uharibufu, na wengi wanaangamia. Na natakanikuambie ya kuwa Roho Mtakatifu akikuwekea mzigo huo ndani yako na kuliona jambo hili

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->