Professional Documents
Culture Documents
ISSN 0856 - 3861 Na. 1024 SHAABAN 1433, IJUMAA JULAI 6 - 12, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Innalillahi wainna ilayhir rajiuun: Mzee wetu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Mbona wapo kina Paulo, Petro na Luka? Ungemfananisha na Mtume Mwingira Wapo pia Mzee wa Upako, Mch. Rwakatare
Uk. 2
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume amewatoa wasiwasi Wazanzibari akisema kuwa hakuna haja ya kuwahoa Uamsho.
Maamuzi ya kususia sensa yalikuwa ya Shura Kukiuka Shura ni kuvunja maelekezo ya Quran Angelirejesha Suala hilo katika Shura ya awali
Karume amesema, hata wale wanaodhani hawawahitaji Uamsho, watambue pia nao Uamsho ina faida kwao lau watatafakari kidogo. Mheshimiwa Amani Abeid Karume akipiga
Inaendelea Uk. 2
2
Cel: 0784 370 208, 0652 849227, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
TahaririMakala
AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
MAONI YETU
Wahadhiri wanaoyasema haya kama yalivyokuja katika Qur an 5:75), Mwalimu wao ni Mtume Muhammad (s.a.w). Sasa kama Maaskofu na Wakristo kwa ujumla wanasema kuwa Wahadhiri hawa wanakashifu Ukristo, ina maana kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) ndiye Mwalimu Mkuu wa wanaokashifu Ukirsto. Hii maana yake ni kuwa kama Mtume Muhammad (s.a.w) angekuwa hai leo, ilikuwa awe wa kwanza kukamatwa katika ile kadhia ya mauwaji ya Mwembechai ambapo vyombo vya habari vya Bwana Reginald Mengi vilifanya kazi kubwa sana katika kuwabamiza Waislamu. Ni kwa mantiki hii, sisi hatudhani kuwa Mzee Alhaji Ally Hassan Mwinyi atakuwa
AN-NUUR
Inatoka Uk. 1 mfano mwepesi kabisa kumfanya Boraa kufahamu, aliwafananisha Uamsho sawa na waamsha daku. Akasema, kuna Waislamu katika mwezi wa Ramadhani hawahitaji kuamshwa kula daku, wanaamka wenyewe. Lakini wapo wengine, bila kupita kigoma cha kula daku wanaweza wasile daku siku hiyo. Katika hali hiyo akasema kuwa, yule ambaye hana usingizi wa kuhitajia kuamshwa, anaweza kuwaona kula daku kama kero. Lakini akitokea kukurupushwa na kigoma cha kula daku, japo anaweza kukasirika, lakini akitizama saa akiona muda umefika, atafurahi na kula daku yake. Akizungumza katika mkutano uliofanyika Jimbo la Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Dk. Karume alisema kwamba CCM haijalala hivyo wanachama wa CCM hawana sababu ya kuwa na hofu na Uamsho kwani wao hawakulala na wenye kuamshwa ni wale waliolala. Kwani nyie mmelala mpaka muamshwe, nyie mko macho etihao ni kama wale wanaoamsha daku utakasirika, lakini ukiamka unasema ahaa kumbe muda wa kula daku; tena hofu ya nini? Alisema Dk. Karume na kuwachekesha waliohudhuria mkutano huo. Makamu huyo Mwenyekiti alilazimika kutoa maelezo
amemtendea haki Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dr. Reginald Mengi kumfananisha na Mtume wa uwongo kwa mujibu wa imani yake. Hatuamini pia kuwa Dr. Mengi alifurahi kufananishwa na mtu ambaye kwa imani yake na kwa msimamo wa Maaskofu wake ni Mwalimu Mkuu wa Wahadhiri wanaokashifu Ukristo. Japo lengo la Mzee Mwinyi lilikuwa kumsifu Mengi, lakini hatudhani Dr. Reginald Mengi amekia mahali pa kupenda sana sifa kiasi cha kutokujali ni sifa gani anapewa au anafananishwa na nani. Ni kwa sababu hiyo, hatudhani kuwa Mengi atakuwa amefurahi kufananishwa na mtu anayekanusha uungu wa mwokozi wake Yesu Kristu. Sisi tunamjua Dr. Mengi kwamba ni mtu wa dini. Ni
Karume. Akizungumzia suala la maoni kuhusu Muungano, Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM alisema watu wote wanaotoa maoni kimsingi wanatumia haki ya kikatiba na kidemokrasia hivyo wana CCM wanachotakiwa ni kuendelea kusimamia azma ya ujenzi wa chama chao huku wakiendelea kuheshimu misimamo yao bila ya kuyumbishwa. Msipatwe na homa, ondoeni hofu na wasiwasi , waacheni Masheikh wajibishane na Masheikh wenzao na sisi wanasiasa tutafute majibu mujarab yatakayofaa ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha vijana wetu kutambua mahali tulikotoka, tulipo sasa na kule tuendako, alisema. Mkutano huo uliofanyika katika Tawi la Gulioni ambako alizungumza na wanachama wa matawi mawili la Gulioni na Mwembeladu ni wanachama wachache waliohudhuria tofauti na matarajio ya watu wengi ambapo kuliwekwa mabomba nje ya tawi hilo lakini wasikilizaji walikuwa kidogo mno. Viongozi walioambatana na Dk. Karume ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Yussuf Mohammed, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mjini Borafya Silima, Mbunge wa Rahaleo, Abdallah Juma Abdallah (Maabodi), na Mwakilishi wake Salim Nassor (Aljazira),
3
Na Shaaban Rajab
ZIPO taarifa kuwa Waislamu nchini wanapanga kufanya maandamano nchini kupinga kitendo cha kudhalilishwa Sheikh wao Nurdeen Kishki pamoja na Masheikh wengine aliokuwa nao. Habari zinasema kuwa lengo jingine ni pamoja na kumtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani kuomba radhi kwa udhalilishaji huo na serikali kutoa tamko la kukemea kitendo hicho. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana tukienda mitaani, kuna vikao vya ushauri vinaendelea katika Misikiti, Taasisi na Jumuiya mbalimbali za Kiislamu ambapo baadae itafanyika Shura ya pamoja kuamua nini la kufanya juu ya kadhia hii. Shura na vikao hivo vinakuja kufuatia taarifa ya kukamatwa na kudhalilishwa Sheikh Nurdin Kishki. Tukio hilo limeelezwa kuwa ni katika kuendeleza mwitikio wa kile kinachoitwa mapambano dhidi ya ugaidi. Katika tukio hilo, Sheikh Nurdin Kishki na Masheikh wenzake wakiwa wameambatana na ujumbe wa Masheikh kutoka Yemen akiwemo Mufti wa Yemen, juzi Jumatano walifanyiwa udhalili mkubwa na polisi baada ya kukamatwa na kudaiwa kuwa ni majambazi. Wakiwa njiani kutokea Tanga kuja jijini Dar es Salaam, Sheikh Kishki na wenzake walivamiwa na polisi Bagamoyo mkoani Pwani na kuamriwa kulala chini huku wakisukwa sukwa wakishukiwa kuwa ni majambazi. Umati wa watu wakiwemo watoto wadogo walijazana katika eneo la tukio kushuhudia Masheikh hao baada ya taarifa kuzagaa kwamba watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamekamatwa na polisi. Hata hivyo wengi walishangaa na kupigwa na butwaa baada ya kukuta kuwa watu waliokuwa wakishukiwa kuwa ni majambazi, walikuwa ni Masheikh akiwemo Mufti wa Yemen, ambao walikuwa wamelazwa chini huku polisi wakiwazingira chini ya ulinzi mkali. Hata baada ya Masheikh hao kujieleza na kujitambulisha kwamba wao sio majambazi kama taarifa za polisi zinavyosema bali ni Masheikh waliokuwa safarini kuja Dar es Salaam, utetezi huo haukutosha kuwafanya polisi kuacha kuwadhalilisha kwani waliendelea kupigwa
Habari
AN-NUUR
na kugaragazwa sakafuni kama majambazi. Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa taarifa zilipelekwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantum Mahiza ili kuja kuingilia kati tukio hilo kufuatia askari waliowakamata mashekh hao kuendelea kushikilia msimamo wao wa kuwadhalilisha. Shuhuda mmoja wa tukio hilo alieleza kuwa kufuatia Mkuu wa Mkoa kupewa taarifa hiyo, alijibu kuwa tayari amemwagiza OCD wa Wilaya ya Bagamoyo kuchushughulikia mkasa huo hivyo Waislamu wavute subra OCD huyo hadi atakapoka mkuu huyo katika kituo cha polisi Bagamoyo ambako ndiko Sheikh Kishki na wenzake wanashikiliwa. Wakati Mkuu huyo wa Polisi Wilaya akisubiriwa, Waislamu walishamiminika kituoni hapo kujua hatma ya Masheikh hao.
na maosa waliowadhalilisha wachukuliwe hatua mara moja. Alisema udhalilishwaji huo kamwe hautakaliwa kimya. Alisema hata kama maosa hao wa polisi walikuwa wanawashuku, hawakustahili kuwaburuza na kuwalalisha chini kama wahuni. Kama wametushuku na walikuwa wamekusudia kufanya uchunguzi dhidi yetu, wangetuhoji kistaarabu hapo kituoni kwao na kama hawakuridhika, basi wangetuhifadhi kistaarabu kwa kuwa tayari tulikuwa kituoni, naamini kama wangekuwa ni Mapadri udhalilishwaji huu usingefanyika hata kama wangeshukiwa ujambazi. Lakini kwa kuwa Kishki amevaa kanzu ana koa na kilemba, basi hao ndio, wa kulazwa chini, kupigwa, kufanyiwa kejeli, tena tukiwa na wageni wetu kutoka nje ya nchi, hili latosha kuwafanya Waislamu watambue kuwa
4
Na Azza Ally Ahmed
WA I S L A M U a c h e n i kukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufuata mkumbo wa vunja jungu. Ndugu zangu Waislamu, dhana ya vunja jungu inabeba mambo machafu kama uzinzi, unywaji pombe, miziki na mengineyo. Wenye tabia hii ya vunja jungu ni wale wanaokusudia kurudi upya katika maovu baada ya mwezi wa Ramadhani kuisha. Yaani wale wanaoifanyia mzaha Dini ya Allah. Nikinukuu hadithi ya Anas isemayo, walikuwa Waislamu kila ukikaribia kuingia kwa mwezi wa Ramadhani wakisoma sana Quran na wale wenye uwezo kimali wakitoa mali zao kuwapa maskini ili kuwapa nguvu za kuingia katika mfungo hali yakuwa wana uhakika (Kujiandaa na mfungo wa Ramadhani). Mwenyezi Mungu ( s . w. ) a n a t u f a h a m i s h a kwamba: Enyi mlioamini m m e l a z i m i s h w a kufunga (swaumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu. (Qur. 2:183). Maneno haya matukufu yana mafunzo makuu matatu. Kwanza, kufunga ni amri wala si jambo la hiari. Pili, kutokana na maslahi yanayopatikana katika funga, maslahi ambayo ni muafaka kwa maumbile ya binadamu, amri hii pia inawahusu wanadamu waliokuwepo kabla yetu. Tatu, tunafahamishwa kuwa, kwa kuitekeleza amri hii tutalikia lengo la kuumbwa kwetu. Lengo ambalo tusingelifahamu bila ya kuelimishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.) pale alipotuambia kuwa: Sikuwaumba majini na wanaadamu ila wapate kuniabudu (Quran 51:56) Ni vipi Mwenyezi Mungu (s.w) anatutaka tumuabudu katika mwezi wa Ramadhani? Je, hii ina maana kuwa katika miezi mingine ya mwaka mzima hatutakiwi kumuabudu au kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.)? J i b u n i Tu n a t a k i w a kumuabudu au kumcha Mwenyezi Mungu (s.w.) kwa masaa yote 24 ya kila siku na katika kila kipengele cha maisha yetu kwa mwaka mzima. Pili tunatakiwa kumcha Mwenyezi Mungu kwa juhudi zetu zote mpaka
Makala/Tangazo
AN-NUUR
Vunja jungu
mauti yatukute tukiwa Waislamu wa kweli. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife isipokuwa mmekwisha kuwa Waislamu kamili. (3:102) Na katika kumtii Mwenyezi Mungu tunatakiwa tusichague baadhi ya mambo ya kufanya kwa kuwa tu tunayapenda na kuacha mengineyo ambayo hatuna mapenzi nayo, bali, ni kufuata amri zote au kwa maneno mengine ni kutii kila kipengele kilichopo katika maisha yetu. Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, wala msifuate nyayo za shetani; kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri. (2:208) Kama utaratibu wa kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w.) ndio huu, inakuwaje Allah (s.w.) atuamrishe kufunga Ramadhani ili tupate kumuabudu? Kuna hekima gani katika mwezi wa Ramadhani tofauti na miezi mingine? Ni kuwa, katika mwezi wa Ramadhani tunapewa au tumetunukiwa nafasi ya pekee. Nafasi ambayo kama tutaitumia ipasavyo itatusaidia kulikia lengo la kuumbwa kwetu. Kuhusu kheri zinazopatikana ndani ya mwezi wa Ramadhani,
Nabii Muhammad (s.a.w.) anasema: Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Mwenyezi Mungu ambao ameujaza Rehma, Baraka na Msamaha. Na pia ni ukweli usio na shaka kuwa, kwa kutokuzingatia taratibu
Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeandaa safari ya Hijja na Umra mwaka 2012 kwa dola (US) $ 3375 tu. Mambo yatakayogharamiwa. Semina za Hijja, Huduma za Afya, Airport charge na Tiketi za ndege, Nyumba za kulala Makka na Madina, Ihram na Kuchinja kwa ajili ya Tamaa-tuu, Chakula wakati wote, Usari na ziara Makka na Madina, Mahema Mina na Arafa. KUHIJIWA ni DOLA US $ 1450. Fomu zinapatikana. 1 Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam- Magomeni Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba namba 26 Mkabala na Show Room ya Magari Tel: 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930 444 au 0773 930 444. 2. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar RahaLeo Tel: 0777 484982, 0777 413987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar Es salaam Tel: 0784 453838. 4. Abdallah Salehe Mazrui ( Hoko) Dar es salaam Tell. 0715 72 4444. 5. Salim Is-haq Dar es Salaam Tell: 0754 286010, 0774 786101. 6. Dukani kwa Mohamed Hadh Mazrui Wete Pemba Tel: 0777 482665. 7. Sheikh Daudi Khamis Sheha Tel: 07776 79692. 8. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel: 0777 417736. Wahi mapema kulipia ili ushughulikiwe mapema, kama utalipia kwa Account No 048101000030 NBC piga simu kwanza 0774 412975. Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa ni cha Bei nafuu zaidi na huduma zake ni bora zaidi ya vikundi vingine.
za mwezi wa Ramadhani tutakuwa ni wenye kuipoteza tunu adhimu ambayo imetoka kwa Allah s.a.w, kwa wenye hasara kubwa duniani na akhera. Mwezi wa Ramadhani unatupa nafasi ya kuanza maisha mapya na kujiwekea
Kimataifa/Tangazo
AN-NUUR
wanaharakati wanaopinga vita na siasa za kibepari za Marekani. Flanders amesema kuwa harakati ya kuteka Wall Street ni mfano wa yale yanayotendeka mara kwa mara nchini Marekani. Amesema kuwa kutiwa mbaroni kwa wingi watu wasiokuwa na hatia, kutolewa taswira isiyokuwa sahihi kuhusu vyombo vya habari na kuwatambua vijana wanaopigania haki zao kuwa ni wahalifu, ni mifano ya wazi ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Marekani.
Waislamu. Alisema Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ufaransa, Muhammad Bishari. B w. B i s h a r i p i a amezilaumu taasisi nyingine za Kiislamu nchini Ufaransa kwa kunyamazia kitendo hicho na kusema kuwa taasisi muhimu za Kiislamu zinapaswa kutekeleza majukumu yao katika suala hilo.
Habari
AN-NUUR
Na Bakari Mwakangwale kauli ambayo haikuwa na shura kwa kuzishirikisha UMOJA wa Wanazuoni taasisi zingine kama wa Kiislamu Tanzania ilivyokuwa awali. (Hay-Atul-Ulamaa), Kwa upande wake u m e s e m a , M u f t i w a Maalim Ally Baswaleh, Bakwata Sheikh Shaaban akijibu swali nani msemaji S i m b a , a m e k h a l i f u wa Waislamu kutokana Uislamu kwa kubatilisha na matamko kutoka na kauli na msimamo wa msimamo tofauti, alisema pamoja ya Waislamu kwa hali ilivyo ni sawa kutoshiriki Sensa. na vyama vingi vya siasa, Hayo yamebainihwa kila mmoja anamwaga na Umoja huo, Jumatano sera zake hivyo mwenye wiki hii wakiongea na sera yenye mashiko ndie Waislamu katika Hoteli atakayefuatwa. ya Tansoma, Kariakoo Awali akisomo tamko Jijini Dar es Salaam, la Hay-Atul-Ulamaa, juu wakisisitiza msimamo ya ushiriki wa Sensa kwa wa Waislamu kutoshiriki Waislamu alisema, msima Sensa inayotarajia kuanza wao unabaki palepale Agosti 26, mwaka huu. na kuwataka Waislamu Aidha umoja huo pia kutoshiriki zoezi hilo umesema, kuwa msimamo mpaka pale Serikali itakapo kwa Waislamu ni ule tekeleza matakwa yao ulioshirikisha Jumuiya na ya kuingizwa kipengele Taasisi zote za Kiislamu cha dini katika dodoso la baada ya kukaa Shura Mjini Sensa yatakapotimizwa. Dodoma muda mfupi baada Alisema, Hay-at, inataka ya kikao cha viongozi wa ieleweke, si kwamba Dini na Serikali, ambapo Waislamu wanapinga Sensa Serikali ilikataa maombi au hawaelewi umuhimu ya Waislamu na kukubali wake, bali wanalichukulia zoezi hilo katika mambo ya Maaskofu. Kwa hiyo, kama Mufti yanayoendana na Sunnah a l i o n a k u n a h a j a y a ya Mtume (s a w), kwani kubadili msimamo, basi baada ya kuhamia Madina, angelirejesha suala hilo aliagiza ifanywe hesabu katika Shura liangaliwe ya idadi ya wakaazi wote wa mji huo, ili kuweza upya. kuwapatia huduma za Wa k i j i b u m a s w a l i kijamii. kutoka kwa waandishi Kutokana na kuelewa w a h a b a r i w a l i o t a k a vyema umuhimu wa sensa kujua Waislamu wafuate kwa maendeleo ya jamii, msimamo gani baada kamwe hawezi kupinga, ya Mufti kutoa tamko la lakini imebidi waisusie kuwataka kushiriki Sensa, kutokana na kupuuzwa Sheikh Abdallah Bawazir, madai yao ya msingi. amesema kiitikadi Mufti Alisema Maalim Bassaleh S i m b a , a m e k h a l i f u akisoma tamko lao. Alisema, upo umuhimu Uislamu. mkubwa wa kuelewa Akisherehesha nukuu ya idadi ya Watanzania kwa aya Qur an 4:115, alisema mujibu wa dini zao kwani kwa kuzingatia aya hiyo, kama hakuna umhimu Waislamu walishafanya huo, vipi Televisheni ya Shura yao na wakatoa njia Taifa-TBC1, itangaze yao ya kufuata, ambayo takwimu kama hizo kisha ni kutoshiriki katika zoezi ije kuomba radhi. lijalo la sensa, sasa Mufti Kutokana na utata huo, amekengeuka katika njia alisema Maalim Basaleh, hiyo ya Waislamu. ndio maana Waislamu Alisema, tamko la awali watoa rai kwa Serikali yao lilijumuisha Taasisi zote kuwa kipengele cha Dini za Kiislamu ikiwemo kirejeshwe kuonyesha Bakwata, hivyo Waislamu katika kuanzia sensa ya wasiyumbe kutokana na mwaka huu, ili zipatikane
zoezi hili la Sensa Agosti, na hata za miaka ijayo mpaka pale kipengele cha dini kiwekwe katika dodoso la sensa na usimamizi wake uwe wa uwiano baina ya dini zote.
DAKTARI bingwa wa magonjwa ya wanawake Dkt. Muzdalifa Abeid (aliyekaa katikati) akiwa na baadhi ya madaktari wenzake wa MSV)
JUMUIA ya Wataalam wa Afya wa Kiislamu nchini, Muslim Sunshine Volunteers (MSV) imefungua kituo cha afya jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha utabibu kiitwacho SMV Maternity and Child Care kimefunguliwa Ilala mtaa wa Kigoma na Bukoba jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Kituo hicho kimeanza kutoa huduma ya afya kwa wanawake na watoto chini ya miaka mitano. Akizungumza katika
haa ya uzinduzi wa kituo hicho, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake Dkt. Muzdalifa Abeid, alisema kituo hicho kitakuwa kinatoa huduma za matibabu na kuwashauri wanawake na watoto chini ya madaktari bingwa wa kada hiyo. Jumuia hiyo yenye w a j u mb e mad ak tar i 13, ilianzishwa mwaka 2007 nia kubwa ikiwa ni kuufikishia umma huduma ya afya kwa karibu kwa misingi ya Kiislamu. Siku ya ufunguzi wa kituo hicho, madaktari hao waliendesha huduma mbalimbali kwa akina
mama ikiwa ni pamoja na kuwafanyia uchunguzi wa magonjwa ya saratani ya matiti na stula. Aidha wataalam hao walitoa elimu kwa ujumla kwa akina mama juu ya maradhi hayo ambapo walifunzwa namna ya kujichunguza, kutambua dalili, hatua za kuchukua na namna ya kuendea tiba ya maradhi hayo. Kabla ya kufungua kituo hicho, MSV imekuwa ikiendesha huduma mbalimbali za kitabibu katika sehemu mbalimbali nchini, i k i w e m o Wi l a y a n i Ikwiriri, kupima afya za akina mama mkoani Morogoro.
7
Na Omar Msangi
ALIWAHI kusema msemaji mmoja kwamba japo Uislamu na Ukristo zote ni dini, lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya dini hizo. Katika kutoa ufafanuzi akatoa maelezo yafuatayo: Anasema, Yesu amezaliwa mamilioni ya miaka baada ya kuumbwa dunia. Yesu amezaliwa maelfu ya miaka baada ya kuumbwa Adam na Hawa. Na Yesu amezaliwa na mama. Amezaliwa na mama anayejulikana kwa jina. Ni Binti Fulani. Mtoto wa fulani. Na kwamba hata ngariba aliyemtahiri siku ya siku saba baada ya kuzaliwa, anajulikana kwa jina. Lakini Yesu huyo huyo tunaambiwa kuwa ndiye Mungu Mkuu! Anasema, hoja hizi hizi katika Uislamu ni kinyume chake. Zinatumika KU-REASON, kujenga hoja kuonyesha kuwa mtu mwenye sifa hizo hawezi kuwa Mungu. Katika jumla ya mambo ambayo yamepigiwa zumari sana katika nchi hii na kuonekana kana kwamba ndio ukweli wenyewe, ni suala la udini. Kila anayesimama katika jukwaa la kisiasa na kila anayeandika na kuzungumza katika vyombo vya habari, ataimba wimbo huo huo. Kwamba nchi hii haina udini. Kwa nini? (eti) Mwalimu Nyerere alipigania utaifa akaondoa udini na ukabila. Na kwa maana hiyo hiyo, watendaji na viongozi serikalini hufanya kazi kwa kujali masilahi ya taifa. Hawana upendeleo. Huu ndio msingi wa nasaha za Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dr. Alex Malasusa pale alipowaomba Watanzania kujihadhari na tabia ya udini aliyodai kuwa inaanza kuchipua nchini. Kwamba udini huo ukiachwa kuota na kuchanua itakuwa sababu ya kuleta machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini. Askofu Malasusa alitoa nasaha hizo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa Sinodi ya 12 wa kanisa hilo. Hotuba hiyo ilisomwa kwa niaba yake na Askofu Paul Akyoo wa Dayosisi ya Meru, Arusha. Anachosisitiza hapa Askofu Malasusa katika nasaha zake ni kuwa Tanzania kulikuwa hakuna udini, ila sasa ndio kuna watu wanaotaka kupanda mbegu hiyo. Kwa hiyo anataka Watanzania wasiipe nafasi mbegu hiyo kumea. Yupo Mbunge mmoja kutoka Zanzibar Alhamisi iliyopita aliongea maneno mazito sana bungeni, lakini kwa bahati mbaya yamepotea bure. Yeye alishangaa kuona wabunge wengi kusimama kudai nao wapate mgao wa chenji ya rada. Chenji ya rada ni zile fedha za rushwa na usadi zilizorejeshwa na serikali ya Uingereza. Anasema, watu wanagombea fedha hizo utadhani kuna biashara ilifanyika sasa imezaa faida nzuri. Kwamba suala la msingi ilikuwa kujua nani alihusika na usadi ule na kuhakikisha kuwa anachukuliwa hatua. Lakini watu wamengangania kupata mgao wa pesa ya ufisadi iliyorejeshwa. Sasa hawa ni wabunge. Na huko ndani ya serikali kwenyewe kinachosikika ni kupanga namna ya kuzitumia pesa hizo. Kwamba zikanunulie madawati na vitabu shule za msingi naSuala nani alihusika na usadi ule na achukuliwe hatua, hiyo haimo. Sasa inapofikia hali kama hii utajua kuwa tatizo hapa sio Asa au Waziri aliyehusika kutoa tenda ya
Makala
AN-NUUR
Ndalichako asingekua Joyce nchi ingetikisik Kanisa livunje mfumokristo amani itadumu Likitegemea bangi la Nyerere, lisha-expire
kuwa na Baraza la Mitihani bovu lisiloaminika, linalotoa matokeo ya kuchakachua, haionekani. Sasa nashindwa kujua hii ni kutokana na ukweli kwamba tangu hapo misingi ya Imani za dini hizi mbili ni tofauti. Kwamba Waislamu wanatakiwa kuhoji na kujenga hoja katika kuamini au ni kwa sababu gani wengine hawaoni uzito wa tatizo hili. Lakini kwa upande mwingine najaribu kufikiria, kama badala ya Joyce angekuwa Hajat Profesa Fatma na waliolalamika ni Wakuu wa Shule za Kikristo, na madudu yawe ndio haya ya Dr. Ndalichako, hali ingekuwaje! Katika Tamko lao kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu wametoa mifano mbalimbali kuonyesha jinsi ambavyo Baraza la Mitihani na majopo mbalimbali ya uteuzi wa wanafunzi kuendelea na masomo walivyokuwa wakihujumu vijana wa Kiislamu. Mifano imetajwa ikiwa ni pamoja na kutaja majina ya vijana wa Kikristo waliokuwa wamefeli wakapewa majina ya vijana wa Kiislamu waliofaulu. Mkristo aliyefeli akaendelea na masomo, aliyefaulu akarudi mitaani. Leo yeye na kizazi chake wanatukanwa kwamba hawataki kusoma! Jambo hili lilikuwa jepesi sana. Ilikuwa iundwe Tume ichunguze, na kwa bahati vijana walioporwa nafasi zao wapo au rekodi zao zinaweza kupatikana shuleni walikosoma. Lipo pia lile ambapo aliyekuwa Waziri wa Elimu Kighoma Ali Malima alibadili mtindo wa kuchagua wanafunzi kwa majina ikawa kuchagua kwa namba, idadi ya wanafunzi Waislamu waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza ikaongezeka kwa asilimia 40. Wizara ipo, rekodi Wizarani zipo. Lakini badala ya jambo hilo kutizamwa positively inaonekana kwamba wanaoleta madai haya wanaleta udini. Na ndio hao wanatuhumiwa na akina Askofu Malasusa kwamba wanapanda mbegu ya udini. Watu hawa hawaleti udini, wanapinga udini ambao umefanya Baraza la Mitihani kuwa na vitengo vya siri vya kuwachinjia watoto wa Kiislamu. Wanapinga udini ambao umefanya Baraza la Mitihani kuwa kama Parokia badala ya kuwa na sura ya kitaifa. Wanapinga udini ambao umefanya serikali badala ya kutumia
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dr. Alex Malasusa
ununuzi wa rada ile, bali ni tatizo la kimfumo. Mfumo uliopo unaruhusu usadi na kulinda masadi na kwa mtindo huu nchi haiendi kokote. Zipo taarifa kuwa baadhi ya wazazi na wanafunzi wanakusudia kuishitaki serikali kutokana na kufuta matokeo yao ya mitihani ya kidato cha nne ya mwaka jana. Lakini wakati huo huo, bado haujapatikana ufumbuzi juu ya madai ya Wakuu wa Shule za Kiislamu waliotuhumu Baraza la Mitihani Tanzania kuhujumu matokeo ya shule zao. Wakuu hao walitoa mfano wa somo moja tu la Islamic Knowledge ambapo walisema kuwa wana wasiwasi kwamba madaraja yaliyotolewa hayatokani na alama walizopata wanafunzi katika usahihishaji. Bahati nzuri haukupita muda Baraza la Mitihani likakiri kwamba lilifanya makosa. Likasema limesahihisha. Na usahihishaji wenyewe ilikuwa kuzidisha alama zilizotoa madaraja ya awali kwa factor ya 1.5. Hata hivyo mara tu baada ya kutolewa matokeo ya pili, Wakuu hao waliandika tena barua Wizara ya Elimu wakisema kuwa hata matokeo hayo ya pili yamekosewa. Kwamba hakuna mjumuiko wowote wa kihesabu unaoweza kuzaa matokeo ya pili ukitumia factor ya 1.5 katika yale matokeo ya awali kama Baraza lilivyodai. Hii maana yake ni kuwa matokeo ya pili yalikuwa ya kubuni tu au ya kuchakachua kama yalivyokuwa ya kuchakachua yale ya awali. Kwanza tukubaliane kuwa hili ni Baraza la Mitihani. Hiki ni moja ya vyombo nyeti nchini. Lakini tizama jambo hili lilivyochukuliwa mpaka sasa. Maadhali waliolalamika ni Wakuu wa Shule za Kiislamu walioona ubovu huo katika Baraza la Mitihani, limefanywa ni la Waislamu, sio suala la kinchi. Inachukuliwa kama siasa kali fulani wanaleta tu ghasia katika nchi. Ile hatari ya
8
Na Mwandishi Maalum WAPO watu wanasema kuwa kutekwa na kisha kupigwa sana Dr. Steven Ulimboka ilikuwa jambo jema kwake. Kwamba heri ya madhara aliyopata kwa kipigo hicho, kuliko shari iliyokuwa ikimsubiri mbele kama asingepata watu wa kumnusuru kwa njia hiyo ya kipigo. Lakini pengine kabla ya kuchambua kauli na maoni hayo, kwanza niungane na Watanzania wote kulaani kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dr. Steven Ulimboka huku nikitaraji kuwa vyombo vya dola vitafanya kazi yake kwa makini kuhakikisha kuwa wahusika wanapatikana na kupewa stahiki yao kwa mujibu wa sheria. Lipo fundisho katika Uislamu ambapo waumini wanaambiwa kuwa sio kila jambo linaloonekana kwa sura yake ya nje kuwa ni zuri, basi ni jema kwao. Linaweza kuwa ni shari iliyojificha katika uzuri. Kwa upande mwingine wanaambiwa kuwa sio kila jambo baya linalowapata, basi ni shari kwao, inaweza kuwa ni heri iliyoajia kwa sura ya ubaya. Katika namna ya aina yake, ndivyo Mbunge wa Viti Maalum na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya alivyoitizama kadhia ya kupigwa Ulimboka, hapana shaka bila kujua kuwa hiyo ni katika moja ya mafundisho ya Kiislamu. Akizungumza Bungeni Jumatatu wiki hii, Mheshimiwa Stella Manyanya alisema kuwa kipigo alichopata Dr. Ulimboka ni mpango wa Mungu wa kumuokoa asiendelee kuongoza mgomo wa madaktari. Kwamba, lau Dr. Ulimboka asingepata kipigo hicho, basi angeendelea kuwa kinara w akuongoza mgomo wa madaktari jambo ambalo lingesababisha madhara mamkubwa kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na vifo. Sasa kwa kufa watu hao an kwa kuteseka wagonjwa wasio na hatia, hapana shaka Dr. Ulimboka angepata sehemu ya madhambi yanayotokana na mateso
Makala
AN-NUUR
DKT. Steven Ulimboka. ya waja hao wa Mwenyezi Mungu wasio na hatia. Ni kwa mantiki hiyo, Stella Manyanya anaona kuwa bado Mungu anampenda Ulimboka ndio maana akamnusuru kubeba dhambi kama alizobeba Adolf Hitler aliyesababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Ukiacha maoni hayo ya Manyanya, wiki hii kumekuwa na hali ya kurushiana maneno na tuhuma baina ya Wabunge wa CCM na wale wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya nani anahusika. Wapo wabunge waliosema waziwazi bila ya kutafuna maneno kuwa CHADEMA ndio wanaohusika kuchochea mgomo wa madaktari na huenda pia ndio wanaohusika na kupigwa Dr. Ulimboka. Kwa upande mwingine, wapo wabunge wa CHADEMA wanaotuhumu kuwa kupigwa Ulimboka ni mpango uliopangwa na serikali (ya CCM). Labda swali ni je, kama ni serikali (CCM), ilifanya hivyo ili ipate nini? Na kama ni CHADEMA au mtu mwingine yeyote, ikiwa ni pamoja na watu bianfsi au taasisi za kijamii na hata za kidini; ilisuka mpango huyo, lengo nini? Pengine kama kuchangamsha tu bongo zetu, tujaribu kuchambua makundi yote hayo tuone mizani inaelemea wapi. Ila nitahadharishe hapa kuwa huu ni uchambuzi tu wa kuchangamsha bongo, taarifa za uhakika ni zile zitakazotokana na uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola. Akijibu tuhuma, hisia na uvumi kuwa serikali inahusika, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda alisema Bungeni kuwa serikali itakuwa ni ya ajabu sana kama itakuwa imefanya jambo lake. Hoja yake ilikuwa kwamba wamekuwa na Ulimboka kwa muda wote wa mgogoro kati ya serikali na madaktari na iliofanya hivyo huku ikijua kuwa Dr. Steven Ulimboka sio daktari mtumishi wa serikali. Sasa leo wamdhuru ili iwe nini? Kauli kama hiyo ilitolewa pia na Mheshimiwa Rais Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Jumapili wiki iliyopita. Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali. Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana. Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana. Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa. Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya
Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kuka hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Hiyo ndiyo kauli ya serikali. Ukitizama mgomo huu wa sasa utaona unatofauti kubwa sana na ule wa awali. Katika mgomo wa awali, serikali ilikuwa imekaa mahali pabaya sana. Madaktari, wanaharakati na vyombo vya habari, vilifanikiwa kuwateka wananchi kwa kiwango kikubwa wakawa upande wa madaktari, wagonjwa na uhai wao wakakosa mtetezi. Ilie haki yao ya kusihi ikaonekana kuwa ni collateral damage inayostahiki kutolewa ili madaktari wapate mshahara wao wa milioni saba na ushei waliokuwa wakidai. Katika mgogoro wa sasa, kwanza wanaharakati wamesita kujitokeza haraka haraka, kwa uwazi na kwa nguvu kabisa kushabikia mgogoro na kuwaunga mkono madaktari. Hawakuonekana wakitamba katika vyombo vya habari mpaka ile siku baadhi yao walipokuwa ndani ya gari la wagonjwa lililokwenda kumchukua Ulimboka huko alikokuwa ametupwa baada ya kupigwa. Wakaonekana tena pale Uwanja wa Ndege na mabango yao wakisubiri kumpokea na kumsindukiza Ulimboka akipelekwa nje ya nchi kutibiwa. Ni vivyo hivyo kwa upande wa vyombo vya habari. Kwa kiwango kikubwa vilishindwa kushabikia suala hili kama vilivyofanya kjatika mgomo wa awali. Mi nadhani walishaona kuwa saikolojia na msimamo wa wananchi ulikuwa katika kuwalani madaktari. Ni wachache wal;iohojiwa walijitokeza waziwazi, akiunga mkono madaktari. Wengi waliwalani wakiwataka waache mgomo. Wapo waliohoji wakisema, kabala madaktari hawajagoma, wafikirie lau polisi na wanajeshi wao wanagoma Inaendelea Uk. 9
Makala/Tangazo
SHAABAN 1433, IJUMAA JULAI 6 - 7, 2012 Sasa japo haiwi kuwa ni sababu ya kuivua katika tuhuma, lakini hoja ya serikali kuwa, kwa nini sasa na sio wakati ule?, inakuwa na nguvu za kimantiki. Ila kuna jambo moja alilisema Rais Kikwete. Alisema, Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali. Binafsi sioni kwa nini serikali itoe kauli kama hii, labda ituambie kuwa ina wasiwasi kuwa kuna mapandikizi ndani ay serikali. Kuopigwa Ulimboka hivi sasa kumebadili kabisa sura ya mgogoro huu na serikali imejikuta ikiwa ikilazimika kujitetea wakati ilikuwa kazi ni kwa madaktari kutaka kuwashawishi wananchi na wagonjwa wanaokufa na
AN-NUUR
hali itakuwaje. Nakumbuka mwananchi mmoja akitoa maioni yake katika kipindi cha Baragumu (Chanel Ten) alisema kuwa wapo asikari wa JWTZ ambao wapo katika mahandaki na katika mazingira magumu kabisa ya kikazi wakijitoa muhanga kwa ajili ya ulizni
mahali pazuri wakati katika mgomo wa awali ilikuwa katika wakati mgumu sana. Na kama ni kufanya jambo, kwa hakika ingeshawishika kufanya wakati ule ikiwa ni pamoja na kutaka Dr. Steven Ulimboka asiwepo kama kiongozi wa madaktari kwa sababu yeye si Dakitari mtumishi wa serikali.
kuikosa huduma kwamba, hawatetei mishahara minono ila namna nzuri ya kuwatibu. Kwa kitendo hiki cha kupigwa Ulimboka, huruma sasa inahamia kwa madaktari kwa kiasi fulani. Hawezi kufanya jambo hili, ila yule anayetaka kuihujumu serikali. Sasa kama yupo mtu ndani ya serikali kaagiza jambo hili lifanywe, japo Mheshimiwa Rais Kikwete anasema kuwa Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali, lakini hiyo ni ishara pia kuwa ndani ya serikali si salama. Serikali imevamiwa na mapandikizi. Mapandikizi wanaolipwa mishahara na kuhudumiwa na serikali, lakini wakiihujumu serikali ndani kwa ndani, sasa hii ni hatari kubwa zaidi. Mtu unaweza kusema, afadhali hata iwe ni serikali yenyewe ilifanya kuliko kufanywa na watu ndani ya serikali kwa nia ya kuihumu. Ukija kwa watu walio nje ya serikali, iwe ni vyama vya siasa, watu binafsi, taasisi za kijamii na hata za kidini; mi sioni ni kwa sababu gani kwa mfano CHADEMA ipange mpango wa kumdhuru Dr. Steven Ulimboka, labda kama utapatikana ushahidi kwamba bado wana nia na lengo la kutaka serikali ifikie mahali isitawalike kama walivyowahi kusema baadhi ya viongozi wao siku za nyuma. Mara tu baada ya kutangazwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu mbayo CHADEMA walidai kuwa yalichakachuliwa na taarifa zao kupambwa sana katika vyombo vya habari, palitokea kutolewa kauli kwamba na baadhi ya viongozi wa chama hicho wataendesha maandamano nchi nzima na kuhakikisha kuwa nchi haitawaliki. Sasa kama yupo mtu bado ana nia kama hilo, huyo unaweza kumtilia shaka kwamba anaweza kufanya lolote ilimuradi lengo hilo litimie. Vinginevyo, itakuwa ni suala tu la kurushiana madongo ya kisiasa na bora tusubiri vyombo vya usalama vitaibuka na taarifa gani.
10
Makala
AN-NUUR
Mkasa Wangu wa Kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere, Dar es Salaam Mwaka 2006
yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikisoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imeka siku yangu. Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kukiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu. Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila Inaendelea Uk. 13
yako anakuja nyumbani kwako halafu anakunusisha mbwa wake aliokuja nao ili kujihakikishia kuwa ndani mwako hakuna bomu au gaidi na wewe unakubali! Si umwambie tu kwamba kama anahisi nyumbani kwako hakuna usalama asije? Lakini pale Arusha Akina Ernest wetu hawakuweza kumsaidia Rais wetu kwa sababu vichwani mwao washajiaminisha kuwa wenye akili ya kukiri na wanaojua jambo zuri ni FBI, CIA na watu kama hao. Na maelekezo yao hayapingwi. Hawakuweza kumsaidia Mkapa kwa sababu walishakishwa mahali ambapo hata kama wangeambiwa kuwa baba yake aliyemuacha kule nyumbani akija kazini ni gaidi, basi angeamini na angekwenda kumkamata kama angeamriwa kufanya hivyo na FBI. Na hivi ndivyo walivyofanya alipofika nchini hapa kwa mbwembwe George W Bush. Tutakumbuka kuwa kiasi wiki mbili kabla ya Bwana Bush kuingia nchini wapo Watanzania wenzetu walikamatwa wakawekwa ndani. Ndugu
Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO. Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa). Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0557 800999/0683 800999.
VIROBA MURUA
11
Na Rashid Mtagaluka TOKEA ulimwengu ushuhudie mauaji ya kinyama ya Daktari bingwa Alhaji Jumbe Mohammed Maphingo (46), sasa ni mwaka mmoja na mwezi mmoja. Vilevile leo ni siku ya sita tokea ulimwengu huu pia ushuhudie kitendo cha kiharamia kilichofanywa na watu wasiojulikana cha kumteka, kumpiga na kumjeruhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Ta n z a n i a D k S t e v e n Ulimboka. Kimsingi hii yote ni misiba na maafa yasiyoweza kusahaulika katika jamii. Isipokuwa nianze na wa Dk Maphingo Jumbe ambaye siku ya Mei 22, 2011 majira ya kati ya saa 3:30-4:00 za usiku akiwa nyumbani kwake Bulongwa, alivamiwa na wanafunzi wa chuo cha utabibu cha hapo na kumshushia kipigo kilichosababisha kifo chake! Asubuhi yake taarifa za kifo hicho zikasambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya hapa nchini, chini ya kichwa cha habari kilichosomeka Wanafunzi Makete wadaiwa kuua Daktari. Maelezo yaliyomo kwenye habari hiyo ndiyo yaliyonishawishi mimi na wenzangu tufunge safari hadi huko Bulongwa kwa lengo la kuipa jamii taarifa kamili ya kile kilichotokea, badala ya zile zilizoonesha kujaa mapungufu yaliyogubikwa na utata usioelezeka. Kwa mujibu wa Afisa Utawala wa hospitali ya Bulongwa inayomilikiwa chuo hicho ambacho marehemu Dk Maphingo alikuwa mkufunzi wake Bwana Edward Masavella, Dk Jumbe alifikwa na umauti huo baada ya kuvuja damu nyingi zilizotokana na kipigo cha maharamia hao wasio na huruma. Sio lengo langu kuwatonesha ndugu, jamaa na maraki msiba wa mpendwa wetu huyo, la hasha! Bali nataka kuweka kumbukumbu sawa tu kufuatia hili tukio la hivi majuzi. Afisa huyo wa utawala alitueleza mimi na wenzangu wawili tulioongozana hospitalini hapo kwamba, Daktari alikuwa akitarajiwa kupandishwa cheo na kuwa Mganga Mkuu wa hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Kati. Alisema kabla ya
Makala
AN-NUUR
BI. Helen Kijo Bisimba. marehemu kufikwa na kadhia hiyo, mwanafunzi mmoja wa kike aliyemtaja kwa jina alitoka katika mabweni yaliyo jirani na nyumba aliyokuwa akiishi Dk Maphingo na kwenda kumgongea ili akabidhi barua ya kujieleza kwanini usiku uliopita hakulala chumbani kwake. Mbali ya kuwa daktari katika hospitali hiyo, pia marehemu alikuwa akifundisha utabibu katika chuo hicho, na uongozi ukampa cheo cha mkuu wa nidhamu. Hata hivyo cha kushangaza kuwa muda huo sio wa kawaida kwa mwanafunzi yeyote kuwa nje ya bweni na haikujulikana wapi alikopata ruhusa ya kutoka na kwenda kwa Dk Maphingo, alisema Masavella kwa uchungu katika mahojiana hayo. Jambo hilo lililozusha shaka na maswali kibao sio tu kwa uongozi wa hospitali ya Bulongwa, lakini hata kwa ndugu jamaa na maraki wa marehemu, lilipelekea hata sisi kuwa katika taadhari kubwa wakati wote tuliokuwapo kijijini hapo kwa ajili ya kazi hiyo. Taarifa za awali kutoka kwa Afisa utawala huyo ziliendelea kufahamisha kwamba, binti huyo alipoingia tu nyumbani kwa Dk alivua kanga yake aliyokwenda nayo hapo na kuanza kupiga kelele za kubakwa na mara kundi la wanafunzi wa kiume likavamia na kuanza kumsulubu Daktari huyo mpole kwa magongo na mawe mithili ya mtu auavyo nyoka aliyeingia ndani ya nyumba yake hadi walipohakikisha hawezi tena kunyanyuka ndipo nao wakatawanyika. Kinachostaajabisha katika tukio hilo ni kuona vijana hao walivyoka kwa haraka eneo la tukio wakati ambapo liliko bweni lao ni mbali sana ukilinganisha na nyumba ya daktari mwenziwe ambaye hata hivyo hakutokea kutoa msaada. Baada ya hapo tukadhani labda asasi mbalimbali za wanaharakati na zile za kutetea haki za binadamu zingetumia fursa hiyo kulaani na kukemea kitendo hicho cha kinyama kwa daktari bingwa ambaye ni hazina kwa Taifa letu. Aidha, si Jumuiya ya Madaktari kupitia kwa Mwenyekiti wake Dk. Steven Ulimboka, Katibu wake Dk. Edwin Chitage wala chama cha madaktari ambacho kilithubutu angalau kulaani tu mauaji ya daktari mwenzao huyo ambaye alikuwa ni mwanachama hai katika Jumuiya hiyo. Pia si rais wa MAT Namala Nkopi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa wakati ule, Waziri Mkuu Pinda wala Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Bi Hellen Kijo-Bisimba waliojitokeza kupanua midomo yao kulaani tukio hilo. Hatukusoma, kusikia na kutazama tena kwenye vyombo vya habari wakilishupalia suala la mauaji ya Dk. Maphingo kama tunavyoshuhudia hivi sasa kufuatia tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk. Ulimboka kama vile Dk. Jumbe hakustaili kuishi! Kinyume chake Dk. Ulimboka ambaye ni kinara wa kuhamasisha migomo ya madaktari katika hospitali za serikali chini ya mwavuli wa Uenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, aliyekutwa akipata vilevi katika klabu ya viongozi (Leders Club) maeneo ya Kinondoni na kutekwa na watu wasiojulikana ndiye anaonekana mwenye haki ya kutetewa na kuonewa huruma zaidi! Nisieleweke vibaya kwamba huwenda kwa kusema hivi pengine naunga mkono kitendo alichofanyiwa
12
Mashairi
AN-NUUR
NDUGU msomaji, assalaam alaykum. Mnamo tarehe 30 June 2012 imeadhimishwa miaka 35 tangu Jumuia ya Afrika Mashariki ilipouawa kutokana na chuki binafsi aliyokuwa nayo Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania mnamo mwaka 1977. Rais wa Uganda wa wakati huo Idd Amin Dadaa na Mwanasheria Mkuu wa Kenya aliyeitwa Charles Njonjo ambaye alikuwa hana uhusiano mzuri na Mwalimu, na katika kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia hiyo iliyoanzishwa mwaka 1967 ikazaliwa kutokana na East African High Commission nayo ilijikita sana kwenye uchumi na ilikuwa na mashirika yafuatayo: Makao makuu, shirika la reli, shirika la ndege, shirika la Bandari, shirika la Posta, kampuni ya kupakia na kupakua mizigo melini. Nikiwa mmoja wa watumishi wa iliyokuwa Jumuia hiyo kwa upande wa kampuni ya kupakia na kupakua melini na ambayo hadi sasa bado tunapaza sauti za kilio cha kutolipwa mafao yetu kufuatana na sheria zetu za Jumuia hiyo, ila tunashuhudia jinsi serikali inavyozidi kuwa na ubabaishaji wa kukataa kutulipa kwa misingi ya Jumuia hiyo ya mwaka 1967-1977. Tabu hii imetupata sisi Watanzania tuliokuwa watumishi wa mashirika hayo sita. Jambo la kushangaza ni kwamba wenzetu waliokuwa watumishi wa upande wa Uganda walilipwa na serikali yao na wala hawana mgogoro na serikali. Kwa upande wa Kenya kadhalika nao hawana mgogoro wowote na serikali yao kwani nao walishalipwa mapema. Pamoja na kwamba uongozi wetu kwa upande wa Tanzania walituelekeza kuwa tuwaite wakenya kuwa ni manyangau (neno hili ni la Kijaluo, kwa Kiswahili ni masi) na
Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie: Mhariri AN-NUUR, S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
mashirika hayo kabla ya kuvunjwa Jumuia, wameishia kupuuzwa, kudharauliwa na hata kuambulia virungu vya polisi. Watumishi hao jumla yao ni 30,000 pamoja na familia zao, lakini inasikitisha kuona hata pale ilipofunguliwa kesi ya madai namba 95/2003 mwaka 2005 na kushinda chini ya Jaji Urio wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam bado hakuna malipo yaliyofanyika. Pia Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa aliahidi kuwa alitenga shilingi 450,000,000,000,000 kwa ajili ya kuwalipa wastaafu wa Jumuia hiyo na kueleza kuwa hizo ni za kuanzia tu na kwamba Rais ajaye atamalizi kulipa. Pamoja na dhamira ya Rais wa awamu hiyo ya kulipa, tulipatwa na mshangao pale ambapo Waziri wa Fedha wa wakati huo aliposema ametenga bilioni 50., alipoona kakosea aliongeza bilioni Pamoja na hayo, wastaafu hao waliendela kudai court oder kama alivyoagiza Jaji Mkuu Augustino Ramadhani lakini mpaka sasa majaji wawili wameshakutana nao na bado wanaendelea kupokea pingamizi kutoka serikalini kwa maana ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Badala ya kutekeleza agizo la aliyekuwa Jaji Mkuu, na kwa kuwa madai wa wastaafu kwa serikali ni mapunjo ya mafao yanayotokana na utumishi wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki kwa msingi wa sheria zake za mwaka 1977. Pamoja na kufanya maandamano mengi, juhudi zote hizi wadawa walitumia jeshi la polisi kuwaadhibu wanaodai. Ndipo Jaji mstaafu Ramadhani alipoamua kuliitisha jalada la civil case namba 95/2003 ili aweze kujiridhisha. Akaona bora aungane na majaji wanne wa mahakama ya Rufaa. Walipoliona jalada na
13
Makala
AN-NUUR
Inatoka Uk. 10 kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama. Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msarishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya. Nikawauiza, Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli? Wakasema, Ndiyo maana leo tumekukamata. Nikawaambia, Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni Mzungu wa Unga kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya. Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran? Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Amerika na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha. Mbona hamkunikamata wakati ule? Ikawa swali na jibu swali na hivyo. Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislamu sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyanyasa Muislamu? Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa
14
Makala
AN-NUUR
Inatoka Uk. 13 wenyewe Waamerika wapo hapo mkutanoni. Baada ya kuwalani Waamerika sasa nikaigeukia serikali ya Tanzania na kuishutumu vikali kwa kupitisha Sheria ya Ugaidi. Hapa nikaeleza kuwa Waamerika wasione kuwa Tanzania imepitisha sheria hiyo ya ugaidi kwa haraka kwa sababu Tanzania ina tatizo na ugaidi. Nikaeleza kuwa sheria hiyo imepitishwa kwa sababu Bunge la Tanzania limehodhiwa na Kanisa na kupitishwa kwa sheria hiyo hakuna uhusiano wowote na ugaidi ila Wakristo wamepata fursa ya bure ya kupambana na Uislamu wakitumia serikali ya Marekani kama upawa wao wa kuopolea finyango ya moto kwenye chungu kinachotokota. Nikauchekesha mkutano kwa kuwaambia kuwa Wamarekani wamefanywa wajinga na Kanisa kwa kuchonganishwa na Waislamu
cha mwisho niingie kwenye ndege inayoelekea Detroit, Marekani nikachopolewa kutoka kwenye mstari na nikawekwa pembeni peke yangu kwa usaili wa ziada. New York kadi yangu ya benki ilikataa kutoa fedha kwa siku nzima hadi siku ya pili. Nilikujafahamishwa baadae kuwa system ilikuwa inanichunguza kwanza. Ilikuwa siku ya pili baada ya kuonana na maofisa wa benki ndipo kadi yangu ikaanza kutoa fedha. Geneva, Uswisi kadi yangu ilikataa kutoa fedha katika mgahawa. Sikujua kama ni yale yale au haya yalikuwa mengine. Lakini pasi hii asa wa uhamiaji wa Tanzania alipoiingiza kwenye compyuta yake alimwita mwenzake kuja kutazama kisha wakawa wanacheka. Waliona nini kwenye pasi yangu Allah ndiye ajuaye. (25th February 2008)
Inatoka Uk. 11 wanapokwenda kupata matibabu wana makosa gani? Juzi hapa tumeshuhudia jopo la madaktari, taasisi za kutetea haki za Binadamu wakiwemo kina Hellen KijoBisimba na Ananilea Nkya wakiandamana kumsindikiza Ulimboka uwanja wa ndege wakiwa na msururu wa magari yapatayo nane, wenyewe walipoulizwa kulikoni wakasema eti wanaonesha mshikamano! Mbona mshikamano huu hatukuuona alipouawa Dk Maphingo? Kama si unaki na uabalakala kumbe tusemeje?. Vy a m a v y a C U F n a CHADEMA, ni mfano wa sekta hiyo ya kisiasa ambayo vimelaani kitendo cha kutekwa na kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, huku vikiitaka serikali kuunda tume huru ya uchunguzi, kauli ambayo hatukupata kuisikia wakiitoa pale alipouawa Dk Alhaji Maphingo Jumbe. Je, dhambi ya Dk Maphingo iliyofikia hata
(KMA) kwa kushirikiana na mtandao wa kuwajengea uwezo, kinga na matibabu waathirika hao yaliyofanyika Nairobi, Kenya. Cheti cha mafunzo ya namna ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI ambacho alikipatia Kampala, Uganda Februai 2006. Cheti cha utati juu ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI alichokipata mwaka huohuo wa 2006, Chuo Kikuu cha Makerer, Uganda. Novemba 7-Novemba 15,2005 alihudhuria mafunzo juu ya uangalizi na utabibu wa ugonjwa wa UKIMWI kama yalivyoandaliwa na mpango wa kudhibiti Ukimwi Tanzania (NACP) jijini Dar es Salaam, Tanzania. Pamoja na mafunzo mengine mengi ambayo kutokana na ufinyu wa nafasi sikuweza kuyataja. (Mwandishi wa habari hizi anapatikana kwa simu +255 (0) 718 406 242)
15
Inatoka Uk. 16
Makala
AN-NUUR
kwa ujumla hawaamini na hawakubali kuwa Waislamu ni wachache, hivyo anadhani Serikali inashindwa kurejesha kipengele cha Dini ili kuficha ukweli, kwani huenda kutakuja hoja, vipi Waislamu ni wachache Serikalini na sekata zake. Akahoji na kusema kuwa kuna maswali serikali inatakiwa kujibu moja likiwa ni kwa nini nafasi kama za Wakuu wa Wilaya na Mikoa, zimekuwa ni miliki ya Wakristo kwa maana kuwa idadi yao ni kubwa sana ikilinganishwa na Waislamu. Akizungumzia kauli ya Mufti Shaaban Simba, alisema Mufti, amewasemea Bakwata, na sio msimamo wa Waislamu wote. Hili tumelizoea kwa Bakwata kwenda kinyume na maslahi ya Uislamu na Waislamu, hata suala la mwezi wa Ramadhani wametugonganisha sana, tulizuiwa mpaka kuswali kisa Bakwata hawajasema. Lakini imefika mahali Waislamu wameelewa hata wakisema Waislamu wanapima. Alisema Sheikh Barahiyan. Alisema, anasikitishwa na Serikali kila mara kupuuza hoja au ushauri wa Waislamu lakini imekuwa nyepesi kupokea na kuwakubalia Wakristo kwa yale wanayoyataka, akitolea mfano sakata la Maaskofu kuijia juu Serikali baada ya kuondoa misamaha ya kodi kwa asasi za kidini na hatimae Serikali kurejesha misamaha hiyo. Alisema, muda muafaka ukika atautangazia umma, na kwa sasa Mkoani Tanga, wanatumia Misikiti kutoa maelekezo kwa Waislamu kutoshiriki Sensa, ikiwa kipengele cha Dini hakitokuwapo. Wakati huo huo, kufatia taarifa ya Mufti wa Bakwata, kutoa tamko la Taasisi yake, kuwataka Waislamu kushiriki Sensa, imedaiwa kuwagawa wadau wa Taasisi hiyo huku wakimtuhumu Mufti wao kutumiwa na Serikali
lihifadhiwe. Alisema, imeka wakati sasa Bakwata isimamie Waislamu si Serikali ili kuweza kurudisha imani
ya Waislamu nchini, kwani alidai mambo haya ya kuwabadilikia Waislamu ndiyo yanayoondosha imani ya Waislamu kwa Baraza hilo.
kitengo kama hicho lakini misaada yake kwa kiwango kikubwa imekuwa ikitoka kwa masharti ya kufuata itikadi za Kishia badala ya kutizama Uislamu kwa ujumla wake. Ipo haja ya kupiga kelele, vipi watuache tumezungukwa na mabenki yatoayo riba, Saccos zenye mfumo huo. Hali hii inawaacha Waislamu kujiingiza katika dhambi ya riba. Alisema Sheikh Barahiyan. Akaongeza kuwa, misaada inayokuja kutoka nchi za Magharibi (hata
kupitia serikali) hufika na kulenga sehemu zenye Wakristo wengi, akitolea mfano sehemu kama za mkoa wa Tanga kutelekezwa. Alisema, misaada hiyo ingekuwa inafika kutoka nchi za Kiislamu, huenda ingeelekezwa katika mikoa ambayo iko nyuma kimaendeleo, ambayo ni wazi kuwa ni yenye Waislamu wengi. Alisema, Mkoa wa Tanga kuna barabra ya Pangani kuingia Dar es Salaam, njia ambayo ni fupi ukilinganisha na hii iyatumika hivi sasa, lakini
imetelekezwa. Sheikh Barahiyan amesema kuwa lau barabara hiyo ingetengenezwa, ingesaidia kuinua uchumi wa wakazi walio pembezoni mwa njia hiyo ambayo wengi wake ni Waislamu. Kuna Balozi za nchi za Kiislamu, tuzifuate tuwashauri waanzishe vitengo, kama ilivyo kwa Iran. Irani ni Taifa la Kiislamu, lakini linaeneza itikadi za Kishia, sasa hili ni tatizo kumtoa mtu katika itikadi yake kwa ajili ya kumpa msaada tu. Alisema Sheikh Huyo.
KINGDOM OF SAUDI ARABIA COMMITTEE OF DAAWAH IN AFRICA TANGAZO LA MASHINDANDANO YA FAMILIA YA MTUME (S.A.W.)NA MASWAHABA KATIKA QUR-AN NA SUNNAH ZA MTUME (S.A.W.) Kamati ya Da-awah Afrika inawatangazia Waislamu wote kwamba kuna mashindano kuhusu familia ya Mtume (s.a.w.) na Swahaba (r.a. ) kuanzia mwishoni mwa mwezi wa sita hadi tarehe 19/7/2012. Nakala za mashindano hayo zinapatikana sehemu zifuatazo: Tanga: Msikiti wa Alkheir, muone Sheikh Ally M. Kiroboto. Dar es Salaam: ka Msikiti wa Alfurqan, Buguruni Malapa, muone Sheikh Juma O. Poli (0754302082). Unguja: Muone Sheikh Twalib Juma (0777413502), ka osi za Africa Muslims Agency, Mwanakwerekwe. Pemba: Muone Sheikh Yusuph Hamza, Kengeja. Wanaoruhusiwa kuingia katika mashindano hayo ni Waislamu wote; wake kwa waume, kuanzia umri wa miaka 20 ishirini na kuendelea. Mashindano yameandaliwa kwa lugha ya Kiarabu, Kingereza na Kiswahili. Wahi nakala yako mapema kwani muda ni mfupi. Wale watakaokosa nakala halisi (original), wanaruhusiwa kurudufu (kutoa Photocopy). WASHINDI KATIKA MASHINDANO HAYA WATAPATA ZAWADI KAMA IFUATAVYO: -Mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu watazawadiwa safari ya kwenda Hija kwa 2012. -Mshindi wa nne na wa tano watazawadiwa Computer ya mkononi (laptop). -Mshindi wa sita, wa saba na wanane watazawadiwa chombo cha kusomeshea Qur-an tukufu. -Mshindi wa tisa na wa kumi watazawadiwa simu za mkononi. Wabillahi tawq
16
AN-NUUR
16
AN-NUUR
Kiongozi Ansaar asema Waislamu hawashiriki Bakwata wagawanyika, wengine wapinga ya Mufti
Na Bakari Mwakangwale
gani lina Waislamu wengi na wapi ni wachache ili kuweza kupeleka huduma hiyo kulingana na idadi ya mahitaji. Alisema, haoni sababu ya Serikali kutaka kujua idadi ya Misikiti na Makanisa, na kukataa kujua idadi ya watu wake wanaotumia nyumba hizo za ibada. Alisema, hivi sasa Serikali imeruhusu kufungua mabenki ya Kiislamu nchini ambazo hufata Sheria za Kiislamu ikiwa ni pamoja na kuepuka riba, hivyo ni vyema kwa Serikali kuwa na takwimu za idadi ya Waislamu ili kuwasaidia wanaotaka kufungua Benki hizo kujua ni wapi penye Waislamu wengi kwa ajili kupeleka huduma hiyo kwa maana mfanyabiashara makini huangalia ni wapi penye wateja wengi wa biashara yake. Sheikh Barahiyani amesema kuwa, wadau wa afya wameonyesha kuwa sehemu ambayo kuna Waislamu wachache kumekithiri ugonjwa wa macho huku zile sehemu ambazo Waislamu ni wengi, ugonjwa huo haupo. Akasema, ingekuwa bora kwa Serikali kupata takwimu sahihi ili kujiridha na kufanya utati sababu ni ipi inayotoa tofauti hizo kiafya. Alisema, pamoja na kuwa Serikali inadai haina dini lakini wananchi wake wana dini, hivyo kujua idadi yao kiimani katika sehemu husika, itaisaidia Serikali kuona ipeleke huduma zake kulingana na mahitaji ya imani ya watu wake na kuepusha dhana ya upendeleo kwa watu wa dini moja. Sheikh Barahiyan anasema kuwa yeye na jamii ya Waislamu
Inaendelea Uk. 15
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.