Start Reading

Dini ya Fedha

Ratings:
160 pages1 hour

Summary

Dini n muunganiko mzito wa kiumbe kwa Muumba wake. Ni uamuzi thabiti wa mtu kushikamana na kile ambacho kwake ni tunu au thamani iliyo kuu kupita zote. Kwa sababu si rahisi kukutana na Muumba huyo kwa akili peke yake na vipimo vya sayansi, njia pekee ya kukutana na Muumba huyo huwa ni imani ya mtu kwa yule anayempokea kuwa ndiye chimbuko la maisha yake, kiongozi wa maisha yake, marejeo ya chaguzi zake na hatima ya maisha yake.

Baadhi ya watu, Mungu wao ni dunia (Wafilipi 3:19). "Mwisho wao huyahusudu ya dunia na uharibifu. Mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedhea yao, waniao mambo ya duniani"

Mtazame kiumbe binadamu, anavyoweka thamani katika ngazi mbalimbali, utagundua kwamba, wengine tunu zao za mahali pa kwanza ni mali, vyeo, sifa na majina makubwa, kujulikana makabila yao, familia zao na wengine sehemu zao za kuzaliwa.

Read on the Scribd mobile app

Download the free Scribd mobile app to read anytime, anywhere.