You are on page 1of 3

Utangulizi

1. Mpaka hapa tulipofika ni wazi kuwa hakuna mwananchi wa Zanzibar

asiyejua Zanzibar imepita katika historia gani hadi kufika hapa tulipofika hivi sasa. Historia ya Zanzibar imejaa misiguano ya kijamii iliyosababisha dhiki kubwa kuanzia wakati wa kudai uhuru hadi baada ya mapinduzi.
2. Historia ya hivi visiwa vyetu ni historia iliyojaa machungu, machozi na

ukiwa. Sisi vijana ni kizazi cha kwanza baada ya mapinduzi na shida hizo za migongano na shida zilizofuatia zilikuwa kwetu sisi kitu cha kuhadithiwa na wazazi wetu lakini sasa si hivyo tena. Maafa yaliyoikumba Zanzibar enzi hizo sasa kwetu hivi sasa ni dhahir kabisa na tunazishuhudia kwa macho yetu wenyewe.
3. Wazee wetu wametuhadithia kuwa mapinduzi ya mwaka wa 1964

yalifanywa ili kuondoa dhulma na kuweka haki kwa raia wote. Suala ambalo sisi vijana tunajiuliza hivi leo ni hili, Je lengo la mapinduzi limefikiwa katika miaka 48 ya mapinduzi? Iweje leo ikiwa nchi hii ni huru na haki imetamalaki pawepo tena na msuguano katika jamii yetu, msuguano ambao umezua balaa la watu kupigwa na wengine kuuawa na zaidi ya hayo pakawa na vyombo vya dola vinavyotisha wananchi? Haya ni maswali ambayo yanataka tafakuri nzito ili kupembua upi ukweli na upi ni uongo.
4. Ikiwa baada ya miaka hii yote ya uhuru ulioletwa na mapinduzi tena

wakati mwingine huitwa mapinduzi matakatifu iweje tena mwananchi aliyekombolewa na mapinduzi anapigwa mabomu na kwa takriban sasa miongo miwili wananchi wawe wanapambana na askari waliovalia kivita katika mitaa na vichochoro vya Zanzibar. Hii ni fedheha kubwa kwa nchi yetu.
5. Hali ikiwa ni hii ni wazi kuwa kuna jambo kubwa sana halijatengamaa

katika nchi yetu. Sasa ikiwa hali haijatengemaa ni wazi kuwa mapinduzi yetu yameingia walakin na yametekwa, mapinduzi ya kuikomboa Zanzibar kutoka udhalimu hayapo tena mikononi mwa wananchi.
1

Mapinduzi yamehodhiwa na kikundi cha watu wachache walioipa nchi mgongo na kushughulishwa na maslahi yao binafsi.
6. Hii

haiwezi

kuwa

ndiyo

iliyokuwa kuwa

ndoto

yale

wazee

wetu

wanamapinduzi.

Tujaalie

haya

yanayoisibu

Zanzibar

yangelifanywa na watawala wakoloni waliopita. Maana kama ndoto ya Zanzibar huru ilikuwa ni hii Zanzibar ya leo ya vyombo vya dola kuwa adui wa wananchi basi Zanzibar ni kichekesho katika historia ya nchi zilizojikomboa kwa mtutu wa bunduki. Hapa inabidi vijana tujiulize nani anaeteteresha haya mapinduzi yetu na kwa sababu gani na ni watu gani hawa walioteka mapinduzi haya yalitofanywa na wazee wetu?
7. Hali hii imeirudisha historia ya Zanzibar pale ilipokuwapo kabla ya

mapinduzi na unaweza kusema hali ya sasa ni mbaya zaidi kwani watawala wa leo wameonyesha uadui dhidi ya raia wanaowatawala.
8. Katika hali hii ndipo sisi vijana tukasimama na kuchukua haki yetu ya

kuinusuru nchi yetu na ndiyo maana leo tupo hapa kuweka mikakati zaidi ya kuirejeshea Zanzibar hadhi yake, heshima yake iliyopotezwa na kuikabidhi nchi yetu kalamu ili iandike historia mpya itakayosomwa kwa mapenzi na kumbukumbu nzuri miaka mingi baada ya sisi vijana kutoweka. Maazimio Yetu Vijana wa Zanzibar Baada ya kusema hayo hapo juu sisi Vijana wa Zanzibar tunaazimia na kusema haya yafuatayo:
1. Tume ya Katiba lazima izingatie haki na katika hili sisi vijana hatuhitaji

kusisitiza zaidi.
2. Sisi vijana tunadai katiba na sheria za nchi ziheshimiwe kwa maslahi ya

umma kwani bila ya kuzingatia vitu hivyo na wengine kujiona wako juu ya sheria matokeo yake ni vurugu na mambo kama haya na mfano wa
2

haya ni usaliti mkubwa kwa mapinduzi ya mwaka 1964 na heshima ya wazalendo walioikomboa Zanzibar.
3. Sisi vijana tunalaani vitisho na juhudi za kutoa maelekezo kwa wananchi

na kwa baadhi ya vijana wenzetu kukidhi matakwa ya wanasiasa wachache wasioona umuhimu wa ustawi wa nchi yetu na wananchi wake bali matumbo yao.
4. Vijana wote bila kujali itikadi ya vyama tujitokeze kwa wingi katika kila

pembe ya nchi kuelimishana na kuhamasisha vijana wote kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao juu ya katiba mpya kama fikra zao na ukweli wa hali ya nchi ulivyo. Huu si wakati tena wa sisi vijana kusubiri maelekezo ya wanasiasa kwani mustakbal wa nchi yetu upo mikononi mwetu.
5. Mwisho sisi vijana tunasema na kusisitiza kuwa ni haki ya Wazanzibari

kudai muungano ulio na heshima na usawa kwa wanaoungana.


6. Sisi vijana tunaaamini kwa dhati kabisa kuwa njia ya kufikia na

kuirejeshea nchi yetu hadhi na heshima yake ni kuwa na muungano wa mkataba utakaokuwa na serikali mbili kila moja ikiwa na mamlaka kamili.