You are on page 1of 50

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUUTAMISEMI-MHE.AGGREY MWANRI (MB) KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA TAREHE 07 - 15 JANUARY 2013.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, S.L.P 128, Sumbawanga, RUKWA. Simu. Na. 025 - 2802137/2802138 Nukushi: 2802117/2802318 Baruapepe: rasrukwa@yahoo.com January, 2013

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMIMHE. AGREY MWANRI (MB) KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA TAREHE 07 - 15 JANUARY, 2013. 1.0. UTANGULIZI. Mheshimiwa Naibu Waziri, Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha wewe na ujumbe wako hapa Mkoani Rukwa. Ni matumaini ya Uongozi wa Mkoa wa Rukwa na wananchi wake kuwa, ziara hii itakuwa ya manufaa makubwa kwa maendeleo ya Mkoa wetu na Ukanda wote wa Ziwa Tanganyika, kwani tunajua wazi kwamba tutapata ushauri, maelekezo na maagizo kwa ajili ya kuboresha utendaji wetu wa kazi. Aidha, nichukue nafasi hii kutoa shukrani zetu kwa Serikali kwa kuwateua miongoni mwa viongozi wa Mkoa wa Rukwa kuanzisha Mkoa mpya wa Katavi, uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dr. Rajabu Rutengwe kuwa Mkuu wa kwanza wa Mkoa mpya wa Katavi na Eng. Emmanuel Kalobelo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa ni faraja kubwa kwetu. Mheshimiwa Naibu Waziri, Taarifa hii ya Mkoa wa Rukwa inaeleza na kuainisha hali ya Ki-jiografia, Ki-utawala, Maendeleo katika Sekta za Ki-uchumi, Ki-jamii na ki-siasa. Aidha, taarifa hii pia itagusia fursa za maendeleo, mafanikio na changamoto zilizomo katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Ushirika, Uvuvi, Ardhi, Maendeleo ya Jamii, Biashara, Viwanda, Miundombinu, Mawasiliano, Masuala Mtambuka, Haki za Binadamu pamoja na Utawala Bora. 2.0 HALI YA KI-JIOGRAFIA Mgawanyo wa Mkoa niliouelezea hapo juu unaonyesha kuwa, kwa sasa Mkoa wa Rukwa una eneo la kilometa za mraba 27,713 wakati kilometa za mraba 22,792 ni la ardhi na kilometa za mraba 4,921 ni eneo la maji. Mipaka ya sasa ya Mkoa wa Rukwa upande wa Kusini - Magharibi Mkoa unapakana na nchi ya Zambia, upande wa Kaskazini - Mashariki Mkoa wa Katavi, upande wa Kusini Mashariki Mkoa wa Mbeya, na upande Magharibi nchi ya
2

Kidemokrasi ya Kongo (DRC). Mkoa wa Rukwa uko KusiniMagharibi mwa Tanzania kwenye Latitudo 050 na 090 Kusini na Longitudo 30 - 330 Mashariki. 3.0 HALI YA ULINZI NA USALAMA Mhe. Naibu Waziri, Kwa ujumla hali ya Ulinzi na Usalama katika Mkoa ni shwari na ya kuridhisha kwa kiasi kikubwa. Matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza yameendelea kushughulikiwa na kudhibitiwa na Kamati za Ulinzi na Usalama za kila Wilaya kwa kushirikiana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. Kwa upande wa Kisiasa viko vyama tisa (9) vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2010 wa Rais, Wabunge na Madiwani. Chama Cha Mapinduzi, ndicho chama chenye nguvu kisiasa katika Mkoa wa Rukwa. Kati ya Waheshimiwa Wabunge 7, wote wanatoka Chama Cha Mapinduzi na kati ya Wahe. Madiwani 86 wa kuchaguliwa, 78 wanatoka Chama Cha Mapinduzi, 6 kutoka CHADEMA, 1 kutoka CUF na 1 kutoka TLP. 4.0. KI-UTAWALA. Mhe. Naibu Waziri, Katika maeneo ya utawala, Mkoa wa Rukwa unazo Halmashauri za Wilaya tatu (3) ambazo ni Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri za Wilaya za Sumbawanga na Nkasi. Halmashauri ya nne ni ya wilaya mpya ya Kalambo ambayo bado haijaanza rasmi. Pia mkoa una jumla ya Wilaya tatu (3), Tarafa 14, Kata 64, Vijiji 313, mitaa 125 na Vitongoji 1,638 kwa mchanganuo ufuatao:HALMASHAU RI Sumbawanga MC Sumbawanga DC Kalambo DC Nkasi DC TOTAL ENEO KM. ZA MRABA 1,003 8,203 4,211 9,375 22,792 TARAF A 2 4 5 5 16 KATA IDADI YA WATU 2012 PROJECTI 2003 ON 152,939 214,979 167,260 216,883 752,06 1 221,033 296,327 220,423 299,413 1,037,19 6

WILAYA SUMBAWAN GA KALAMBO NKASI

VIJIJI 24 101 101 87 313

15 15 17 17 64

4.2

Maeneo Mapya ya Utawala


3

Mkoa umepokea Wakuu wapya wa Wilaya zote tatu ambao ni Mhe. Mathew S. Sedoyeka - Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Moshi Musa Changa - Mkuu wa Wilaya ya Kalambo na Mhe. Iddi Hassan Kimanta - Mkuu wa Wilaya ya Nkasi. Mkoa Rukwa unajivunia kupokea Wilaya mpya ya Kalambo ambayo tayari imeshapatiwa baadhi ya viongozi na watumishi ngazi ya wilaya kama vile, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Polisi wa Wilaya, Afisa Usalama wa Wilaya, Afisa Tawala wa Wilaya. Mkoa ulishaainisha maeneo ya ofisi na makazi ya Viongozi wa ngazi ya wilaya pamoja na watumishi watakao kwenda kuanzisha eneo hilo jipya la utawala. 4.3 Changamoto Kuna upungufu wa vitendea kazi; magari, samani za ofisi, nyumba na ofisi zitakapoanzia wilaya yetu mpya kwani ofisi na makazi yaliyopo kwa sasa ni ya kukodisha toka kwa watu binafsi. Utaratibu uliotumika kutoa fedha kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa mipya ungesaidia sana kama ungetumika kwa uanzishaji wa wilaya pia. 5.0 ELIMU 5.1. ELIMU YA AWALI Mhe. Naibu Waziri, Mkoa wa Rukwa kwa mwaka wa 2012 una wanafunzi wa elimu ya awali 19,315 wakiwemo wavulana 9,894 na wasichana 9,421 wote wakiwa na umri wa kati ya miaka 5 na 6. 5.2 ELIMU YA MSINGI Mhe. Naibu Waziri, Mkoa wa Rukwa umeweza kuandikisha wanafunzi 37,525 sawa na asilimia 109.11 kuanza darasa la kwanza 2012 wakiwemo wavulana 18,800 na wasichana 18,725 kutoka katika lengo la kuandikisha wanafunzi 34,392 hata hivyo zoezi la uandikishaji kwa wanafunzi wa mwaka 2013 lilianza mwezi Disemba na hivyo bado linaendelea. 5.2.1 MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2011 NA 2012 Jumla ya watahiniwa 28,551; ambao ni wavulana 13,781 na wasichana 14,770 walifanya mtihani kati ya watahiniwa 30,070 waliosajiliwa ikiwa ni asilimia 94.69. Kati ya wanafunzi waliofanya
4

mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2011, vijana 14,612 walifaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka 2012 kati yao 8,221 ni wavulana na 6391 ni wasichana. Ufaulu huu ni sawa na asilimia 51.07 ya watoto waliofanya mtihani. Mwaka 2012 jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba ni 18,683, waliofanya ni 17,518 na waliofaulu ni 10,219 kati yao wavulana ni 5,574 na wasichana ni 4,645 sawa na asilimia 58. Jumla ya wanafunzi waliochaguliwa ni 8,068 kati yao wavulana ni 4,430 na wasichana ni 3,638 sawa na asilimia 78. Asilimia 22 ni waliofutiwa matokeo, wasiojua kusoma na kuandika na wachache wamekosa nafasi. 5.3. ELIMU YA SEKONDARI. Mhe. Naibu Waziri, Mkoa una jumla ya shule za Sekondari 80 zikiwemo 68 za Serikali na 12 zikiwa ni za watu binafsi na mashirika ya dini. Shule zenye kidato cha V-VI zipo 10 ambapo sita (6) za Serikali na nne (4) sio za Serikali. Mwaka 2012 jumla ya wanafunzi 5,820 wakiwemo wavulana 3,694 na wasichana 2,126 walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne. Aidha, jumla ya wanafunzi 6,487 wa kidato cha pili wakiwemo wavulana 3,881 na wasichana 2,606 walifanya mtihani mwaka 2012. Matokeo ya mitihani ya Kidato cha pili na cha nne bado hayajatoka. 5.4. ELIMU YA UALIMU. Mhe. Naibu Waziri, Mkoa una chuo kimoja cha Ualimu cha Serikali kiitwacho Sumbawanga kinachotoa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti daraja la IIIA na mafunzo ya cheti cha Sayansi Kimu. Pia, Mkoa una vyuo viwili binafsi vya Ualimu vinavyotoa mafunzo ya ualimu daraja la IIIA vyote vikiwa vimepata usajili na hivyo Mkoa kuwa na vyuo vitatu vya mafunzo ya ualimu. Vyuo hivi vimesajiliwa kwa majina ya Rukwa Chuo cha Ualimu na St. Aggrey Chanji. 5.5. ELIMU YA UFUNDI Mhe. Naibu Waziri, Mkoa hauna Chuo cha VETA mbali na vituo vya ufundi stadi vinne (4) katika fani za Useremala, Uashi na
5

Sayansi Kimu. Aidha, vipo vyuo vya ufundi viwili (2) katika fani za Ufundi Magari, Uchomeleaji na Kompyuta. Ni vema sasa Mkoa wa Rukwa ukawa na Chuo chake cha VETA kama ilivyo mikoa mingine nchini. Eneo kwa ajili ya ujenzi wa chuo hiki limeainishwa. 5.6. UKAGUZI WA SHULE Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri za Wilaya zimekuwa zikisaidia ili Wakaguzi wa shule waweze kukagua shule za Msingi. Katika kipindi cha Julai 2011 - Juni 2012 shule za msingi 42 zilikaguliwa. 5.8. ELIMU YA JUU Mhe. Naibu Waziri, Mkoa unacho Kituo cha Chuo Kikuu Huria chenye jumla ya wanachuo 150 katika kozi mbalimbali. Katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2012 jumla ya wanachuo 57 wamefuzu na kutunukiwa vyeti katika fani mbalimbali. 5.9 CHANGAMOTO Mhe. Naibu Waziri, Zipo changamoto ambazo zinaikabili sekta ya Elimu mkoani Rukwa nazo ni: Upungufu wa hosteli/daharia katika shule za sekondari Mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Ushiriki hafifu wa wananchi katika kuchangia utekelezaji wa MMEM na MMES 5.10 MATARAJIO YA BAADAYE: Matarajio ya Mkoa ni kuboresha taaluma kuanzia shule za awali, msingi, sekondari na vyuo ili kukidhi ushindani wa kielimu katika soko la kitaifa, Afrika mashariki na kimataifa. 6.0 SEKTA YA AFYA Sekta ya afya kwa mwaka 2011 iliendelea na jukumu lake la kutoa huduma kwa wagonjwa mbali mbali wanje na wa ndani (waliolazwa). Katika kutoa huduma jumla ya wagonjwa 149,580 walitibiwa kama wagonjwa wanje kati yao 67,145 walikuwa watoto chini ya miaka mitano. Kwa wagonjwa wanje magonjwa kumi sugu yalioongoza ni kama yanavyoonekana katika jedwali Na 1.
JEDWALI NA. 1: 6

IDADI YA WAGONJWA KWA MWAKA 2012 MKOA WA RUKWA MAGONJWA 10 YALIYOONGOZA KWA WAGONJWA WA NJE. WATOTO CHINI YA MIAKA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA MITANO (5) MITANO(5+) Aina ya Ugonjwa IDADI Aina ya ugonjwa IDADI 1 Diarrhoeal diseases 1,167 Malaria 3,475 2 Malaria 2,684 Congestive Cardiac 127 Failure 3 ARI 255 Diarrhoeal diseases 564 4 Pneumonia 1,055 Pneumonia 491 5 Non infections 129 Anaemia 422 Gastrointestinal Disease 6 Burns 110 Acute Respiratory 324 Diseases 7 Urinary Tract 87 Fractures 270 Infections 8 Other nutritional 65 Hypertension 245 Disorders 9 Severe protein 37 Urinary Tract Infections 181 energy malnutrition 10 Anaemia 265 Tuberculosis 162
Source of Data: DHMIS Reports 2011

Sekta pia ilitoa huduma kwa wagonja waliolazwa kwa magonjwa mbalimbali. Katika mwaka 2011 Jumla ya wagonjwa 27,716 walilazwa katika vituo vya kutolea huduma. Kati yao 14,117 walikuwa watoto chini ya miaka 5. Magonjwa kumi sugu yaliyoongoza kwa wagonjwa waliolazwa ni kama yaliyoonekana katika Jedwali Na 2.
JEDWALI NA 2: MAGONJWA 10 YALIYOONGOZA KWA WAGONJWA WALIOLAZWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO UMRI WA ZAIDI YA MIAKA (5) MITANO (5+) Aina ya Ugonjwa IDADI Aina ya ugonjwa IDADI 1 Malaria 5,663 Malaria 4,748 2 Intestinal worms 2,007 ARI 822 3 Pneumonia 1,721 Diarrhoeal diseases 685 4 Anaemia 689 Pneumonia 660 5 ARI 847 Intestinal worms 648 6 Urinary Tract Infections 349 Urinary Tract Infections 422 7 Non Gastrointestinal 199 Genital Discharge 335 Diseases syndrome 7

8 9 10

Burn Severe Protein Energy Malnutritions(PEM) Other Nutritional Disorders

173 Pelvic Inlammatory Diseases 76 Minor surgical conditions 65 Skin infections

328 327 264

Kitengo cha kinga katika sekta ya afya kilitoa chanjo kwa ajili ya kukinga maradhii mbalimbali kwa kufuata miongozo na taratibu za kitaifa na kimataifa.Kwa mwaka 2011 chanjo ilitolewa kama inavvyoonekana katika Jedwali Na 3.
JEDWALI NA 3: CHANJO ILIYOTOLEWA 2011 KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO
N o Distri ct Total BCG Vacci nated % DPT3 Polio 3 Vaccin % Vacci a na ted ted Measles % Vacci na ted % Vit A Vacci na ted %

1 2 3

SBA MC SBA DC NKAS I TOTA L

9243 4092 7 1397 6 6414 6

1433 2158 1 1545 0 3846 4

16 53 11 60

8469 21660 13844 43973

9 2 5 3 9 9 6 9

8469 2065 1 1355 1 4267 1

9 2 5 0 9 7 6 7

9262 2209 0 1488 8 4624 0

10 0 54 10 7 72

9662 10 5 2233 55 1 1488 10 8 7 4688 73 1

6.1 UPATIKANAJI WA DAWA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA Katika mwaka 2011 vituo vya kutolea huduma vilitoa huduma kwa wagonjwa kama kawaida pamoja na upungufu wa vifaa na dawa. Jedwali Na. 4 hapa chini linaelezaea idadi ya siku ambazo vituo havikuwa na dawa/vifaa kiwilaya. Idadi hii imekokotolewa kwa kujumlisha idadi ya siku za kukosa dawa kwa kila kituo.
JEDWALI NA.4.
WILAYA AINA YA DAWA JUMLA

SBA MC 301

SBA DC 3,064

NKAS I DC 1,729 5,094

WASTANI WA SIKU AMBAZO KITUO KILIKOSA DAWA

AMOXYCILLINE TABS

26

B.BEMULSION BENZYLPENILLIN INJ. COTRIMOXAZOLE SUSPENSION COTRIMOXAZOLE TABLETS DOXYCLINE TAB ERGOMETRINE INJECTION FOLIC ACID TABS LIDOCAINE INJ MEBENDAZOLE TABS METRONIDAZOLE TABS ORS OXYTETRACYCLINE EYE OINT. PARACETAMOL TABS P.P.F VAIL WATER FOR INJECTION EXAM. GLOVES POVIDONE IODINE SOLN SILK SUTURE SURGICAL GLOVES SYRINGE REUSABLE

335 7 695 362 220 845 751 843 215 158 598 1,565 307 1,298 550 358 663 248 388 2,050

9,306 3,053 0 0 0 5,348 3,558 3,018 8,843 7,446 10,198 7,113 5,164 13,187 12,329 3,035 11,968 2,101 4,588 3,939

3,264 1,155 0 0 0 2,344 931 790 3,610 3,344 3,423 2,001 3,416 3,440 4,516 1,492 5,148 1,217 1,292 2,791

12,905 4,215 695 362 220 8,537 5,240 4,651 12,668 10,948 14,219 10,679 8,887 17,925 17,395 4,885 17,779 3,566 6,268 8,780

65 13 4 2 1 43 26 23 64 55 71 54 45 90 87 24 89 18 31 44

6.2. CHANGAMOTO Sekta ya Afya mkoani inakabiliwa na changamoto zifuatazo: Uhaba wa watumishi kutokana na watumishi wanaopangiwa kuja mkoa wa Rukwa kutoripoti katika vituo vyao vya kazi. Upatikanaji wa madawa na vifaa kwa wakati kutoka bohari kuu ya madawa (MSD). Bado kuna maeneo magumu kufikika hasa mwambao wa Ziwa Tanganyika
7.0. SEKTA YA MAJI

Mhe. Naibu Waziri, Kiwango cha usambazaji maji safi na salama katika Mkoa wa Rukwa ni asilimia 43 tu. Jitihada zinafanyika kuhakikisha kuwa usambazaji unakidhi mahitaji ya watumiaji ifikapo 2025 kulingana na dira ya maendeleo. Upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ni kama unavyoonekana kwenye jedwali ambapo Manispaa ya Sumbawanga (Mjini) inaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa (54%) na mji wa Namanyere kuwa na kiwango kidogo (16 %) kama inavyoonekana kwenye jedwali.
9

JEDWALI NA.5: UPATIKANAJI WA MAJI MKOANI Mahali Manispaa ya Sumbawanga (Vijijini) Manispaa ya Sumbawanga (Mjini) Sumbawanga vijijini Namanyere Nkasi vijijini Upatikanaji wa maji (%) 41.8 54 45 16 42

Mhe. Naibu Waziri, Vipo vyanzo vikuu viwili vya maji ambavyo vinatumika kusambaza huduma ya maji kwa wananchi, vyanzo hivyo ni maji yaliyopo chini ya ardhi (Ground water) na yaliyopo juu ya ardhi (Surface water). Teknolojia zinazotumika kusambaza maji kutoka katika vyanzo vinavyofanya kazi ni, pampu za mkono za visima virefu zipatazo 384 na visima vifupi 194, pampu za umeme za visima virefu zipatazo 7, miradi ya kutiririsha maji kwa mserereko (Gravity) 38 mradi wa maji ya kusukuma kwa mashine (pumped scheme) 1. Pia kuna maji ya chemichemi zilizohifadhiwa (protected spring) 2. Jedwali Namba 6 hapa chini linaonesha mgawanyo wa vyanzo vya maji.

JEDWALI NA. 6: VYANZO VYA MAJI. Halmashauri / Mamlaka Nkasi DC Aina ya mradi wa maji Miradi ya mserereko Miradi ya kupampu Visima virefu vyenye pampu ya mkono Visima virefu vyenye pampu ya dizeli Visima vifupi vyenye pampu ya Hali ya mradi Unafanya Haufany kazi i kazi 6 1 1 6 145 47 82 1 57 10

Sumbawanga DC

Sumbawanga MC

Mamlaka ya Maji Sumbawanga

Mamlaka ya Maji Namanyere

mkono Chemchem zilizohifadhiwa Miradi ya mserereko Visima virefu vyenye pampu ya mkono Visima vifupi vyenye pampu ya mkono Chemchem zilizohifadhiwa Miradi ya mserereko Visima virefu vyenye pampu ya mkono Visima vifupi vyenye pampu ya mkono Chemchem zilizohifadhiwa Miradi ya mserereko Visima virefu vyenye pampu ya mkono Visima virefu vyenye pampu ya umeme Chemchem zilizohifadhiwa Visima virefu vyenye pampu ya mkono Visima virefu vyenye pampu ya umeme

2 21 181 111 8 5 33 1 9 6 14 3 2 11 4

7 38 76 3 2 5 2 -

7.1 MAJI VIJIJINI Mhe. Naibu Waziri, Mipango ya Maendeleo ya Uboreshaji wa upatikanaji na usambazaji wa majisafi na salama ili kuhakikisha kiwango cha huduma ya maji kinapanda kwa kila Halmashauri inafanywa kupitia program ndogo ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kupitia mradi unaojulikana kama Quick win na Mradi wa Vijiji Kumi pia kupitia vyanzo vingine vya fedha. 7.1.1 Quick win Mhe. Naibu Waziri, Kupitia Quick win ambayo ilitekelezwa mwaka 2007-2010 visima virefu vyenye pampu ya mkono 15 vilichimbwa na 6 vilikarabatiwa, visima vifupi vyenye pampu ya mkono 5 vilichimbwa pia miradi ya maji ya mserereko 3 ilikarabatiwa wakati miradi mipya 4 ilijengwa na uhifadhi wa chemichemi 2 ulifanyika. Miradi hii iligharimu kiasi cha Shilingi mia sita kumi na nane milioni mia moja arobaini na mbili elfu mia nne sitini na sita na senti tisini na tano (618,142,466.95).
11

7.1.2 Vyanzo vingine vya fedha Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zimekuwa zikitumia fedha za Wahisani na za ndani katika utekeleaji wa miradi ya Maji. kiasi cha shilingi mia saba arobaini na tatu milioni mianane sabini na nane elfu mia nane ishirini na tatu na senti tisini na tatu (743,878,823.93) zimetumika kujenga visima virefu 41 vyenye pampu ya mkono na kukarabati visima virefu 11. Miradi hii ilitekelezwa kati ya mwaka 2007 na mwaka 2012. Fedha hizo ni za Mfuko wa TASAF, Fedha za miradi ya maendeleo (LGCDG) na fedha za wahisani (Tanzania Rural Revival). 7.1.3 Mradi wa Vijiji 10 Mhe. Naibu Waziri, Utekelezaji wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2010-2013 chini ya programu ya maendeleo ya sekta ya maji unaojulikana kama mradi wa vijiji kumi unaendelea ambapo usanifu wa miradi umekamilika na uchimbaji wa visima vya majaribio umekamilika na jumla ya visima 11 vimechimbwa, kati ya hivyo visima tisa vina maji ya kutosha . Vijiji 37 vimependekezwa kutekeleza miradi ya maji chini ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira vijijini kama jedwali namba 7 hapa chini linavyoonyesha:

12

Jedwali Na.7: VIJIJI VITAKAVYOTEKELEZA PROGRAMU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI. Halmashau Na Jimbo la Idadi ya ri uchaguzi Walengw Kijiji a 1 Luwa 4773 2 Kanondo 3850 Sumbawang Sumbawanga 3 Mponda 2054 a MC 4 Malonje 3000 5 Mawenzusi 6000 6 Katumba Azimio 4140 7 Milanzi 4374 8 Nambogo 2372 9 Mlanda 6494 10 Matanga 2395 11 Kisumba 2884 12 Chelenganya 1914 13 Kasense 2467 14 Chipu 3306 15 Pito 2642 16 Tamasenga 4756 17 Malagano 4160 1 Kisumba-Kasote 6073 Sumbawang 2 Matai 8601 a DC Kalambo 3 Kamawe 1130 4 Mwimbi 5285 5 Mwazye 4172 6 Mpui 5939 7 Ikozi 6066 Kwela 8 Laela 12132 9 Kilyamatundu 4805 10 Nankaga 6037 1 Tambaruka 1933 2 Isale 3029 Nkasi DC Nkasi 3 Matala 2439 Kaskazini 4 Chala B 3005 5 Kabwe 10135 6 Kamwenda 9011 7 Kisula 1757 Nkasi Kusini 8 Mpasa 6841 9 Kingombe 1632 10 Mkinga 11380

13

Mhe. Naibu Waziri, Utekelezaji wa miradi ya vijiji kumi utaanza kwa kutekeleza miradi 7 katika vijiji vya Nankanga, Matai, Kanondo, Kisumba, Chelenganya, Chala na Kamwanda (Kirando) ambayo itaanza wakati wowote baada ya Halmashauri kupewa vibali (No-objection) vya Wataalam Washauri (Consultants) na ujenzi wa miundombinu. Tunaomba zoezi la utoaji wa vibali hivyo liharakishwe ili tuweze kuendelea na awamu ya pili ya utekelezaji wa miradi kwani ni muda mrefu sasa wananchi wamesubiri kupata huduma bora ya Maji safi na salama. Kiasi cha Shilingi bilioni nne miatano sitini na moja milioni miambili ishirini elfu mia saba arobaini na mbili (4,561,220,742) kimetengwa kutumika kwa ajili ya Wataalam Washauri, Wachimbaji wa visima vya majaribio na Makandarasi wa ujenzi wa miundi mbinu ya maji katika miradi 7 itayotekelezwa kama inavyoonekana kwenye jedwali Namba 8 hapo chini.
Jedwali Na.8: GHARAMA ZA MIRADI SABA (7). JINA LA HALMASHAUR I Sumbawanga MC KIASI CHA FEDHA KAZI

463,124,141 Uchimbaji wa visima 2 vya majaribio 73,000,000 Usimamizi wa miradi (phase1) 696,350,672 Ujenzi wa Miundombinu ya Maji 213,421,631 Usimamizi wa miradi (phase1) 273,237,000 Uchimbaji wa visima 4 vya 98,366,238 1,423,092,000 225,855,500 110,514,000 majaribio Usimamizi wa miradi (phase2) Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Usimamizi wa miradi (phase1) Uchimbaji wa visima 12 vya

Sumbawanga DC

Nkasi DC

majaribio 24,591,560 Usimamizi wa miradi (phase2) 959,668,000 Ujenzi wa Miundombinu ya Maji

7.2. MAJI MJINI Mhe. Naibu Waziri, Serikali imeanza kushughulikia tatizo la maji katika Mji wa Sumbawanga kwa kutekeleza Miradi miwili yenye kuleta mafanikio ya haraka. Miradi hiyo ni Uchimbaji wa visima virefu 13 katika bonde la mto Lwiche na ukarabati wa mabomba ya zamani ikiwa ni pamoja na ufungaji wa bomba mpya za kutoa
14

Maji kwenye visima hadi Mjini. Hadi sasa visima 13 vimechimbwa ambapo visima nane vina maji na vinaweza kutoa jumla ya lita 4,000,000 kwa siku. Ukarabati wa mabomba maeneo ya mjini umekamilika km. 46. Usanifu wa bomba za kutoa maji kwenye visima hadi Mjini umekamilika pia ujenzi wa tanki la maji ya visima eneo la Mto Lwiche umefikia asilimia 80%. Kazi zilizosalia ni kufunga pampu za umeme katika visima na kulaza bomba za kutoa maji katika visima hadi mjini. Mhe. Naibu Waziri, Gharama za mradi wa visima ni Sh. 393,640,200.00 na gharama za mradi wa kulaza mabomba mapya na kukarabati bomba za zamani ni Sh. 4,944,594,450.00. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Dunia. Mradi huu utakapoanza kufanya kazi uzalishaji maji wakati wa kiangazi unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 30% ya sasa na kufikia asilimia 80% ya mahitaji ya maji ya mji ambayo ni lita 9,000,000 kwa siku. Wakati wa msimu wa Mvua, huduma ya maji kutoka katika visima na vyanzo vya sasa vya mito, itatosheleza mahitaji ya maji ya sasa. Mradi ulitarajiwa kukamilika Mwezi Octoba, 2012, lakini kumekuwa na changamoto za kiutendaji. 7.2.2: MAJI MJI WA NAMANYERE. Mhe. Naibu Waziri, Huduma ya Maji katika Mji wa Namanyere si ya uhakika kwani maji ya visima vya kupampu yanapatikana kulingana na upatikanaji wa umeme ambao si wa uhakika, Pia maji kutoka bwawa la Mfili si ya uhakika kutokana na gharama za uendeshaji wa mradi kuwa juu kulingana na bei ya dizeli. Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi iliandaa mpango kabambe wa Maji katika Mji wa Namanyere, mpango huu uliwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. 7.2.3 MRADI WA SEVEN (7) TOWN URBAN UPPER PROGRAM. Mhe. Naibu Waziri, Mradi wa Seven (7) Town Urban Upgrading Programme unalenga kukidhi mahitaji ya maji ya muda wa kati na muda mrefu kwa miji saba ya Lindi, Mtwara Musoma, Sumbawanga, Kigoma, Babati na Bukoba. Kazi ya Usanifu na uandaaji vitabu vya zabuni za ujenzi wa miundo mbinu ya maji safi na usafi wa mazingira katika mji wetu umekamilika. Taratibu za
15

kuwapata Wakandarasi wa ujenzi zinaendelea na ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi Januari 2013 kupitia ufadhili wa umoja wa Ulaya na Serikali ya Ujerumani. 7.3. CHANGAMOTO Mhe. Naibu Waziri, Sekta ya maji inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kudumisha Huduma ya Maji katika Mkoa wetu. Changamoto hizi ni: Uharibifu wa mazingira hasa kuchoma moto misitu kunakosababisha kukauka kwa vyanzo vya maji, Wizi wa miundombinu ya maji,bomba na mifuniko ya chemba za maji, Ucheleweshwaji wa kupatiwa msamaha wa kodi ya mapato (VAT) kwa miradi, Utekelezaji wa miradi inayoendelea umekuwa hauendi kama ilivyopangwa kutokana na fedha kutopatikana kwa wakati pia ucheleweshwaji wa vibali vya Wataalam Washauri. 8.0. MAENDELEO YA JAMII. Mhe. Naibu Waziri, Sekta ya Maendeleo ya Jamii inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996, 8.1. HALI HALISI YA MKOA KIJINSIA: Mhe.NaibuWaziri, Katika Mkoa wa Rukwa hali ya ujinsia bado hairidhishi, kwa kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vinaendelea miongoni mwa wanandoa wakiwemo wanawake na wanaume na ukatili dhidi ya watoto. Jumla ya wanawake 7,463 wamepatiwa mafunzo ya Sheria kuhusu masuala ya Sheria ya Mikataba, Sheria za Kazi, Sheria za Ndoa, Sheria za Mirathi, Sheria za Ardhi na Sheria ya Mtoto. Lengo mafunzo lilikuwa kuwajengea uwezo wanawake kuzitambua haki zao za msingi katika maisha yao ya kila siku. 8.2. WEZESHAJI WA KIUCHUMI. Mhe. Naibu Waziri, Mkoa unawezesha jamii kiuchumi katika juhudi za kuondokana na umaskini wa kipato kwa kutoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake kupitia Mfuko
16

wa Maendeleo ya Wanawake (WDF). Mafunzo ya ujasiriamali yametolewa kwa vikundi 806 na jumla ya vikundi vya Akinamama vipatavyo 117 ambavyo vimepatiwa mikopo yenye thamani ya Shilingi. 91,000,400 kati ya hizo fedha zilizorudishwa ni Shilingi 45,469,800. Deni lilobaki ni Shilingi millioni 45,930,200 ufuatiliaji bado unaendelea. 8.5. HUDUMA KWA MAKUNDI YENYE UHITAJI. Mhe.NaibuWaziri, Mkoa umetoa misaada yenye thamani ya Shilingi. 28,689,100 kupitia NMSF Grant kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji kama Watoto Yatima, wajane, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wapatao 899. Mkoa umewatambua walemavu wa ngozi (Albino) wanawake 448 nawanaume 349, jumla797. Vilevile, Mkoa una vituo sita (6) vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi: Manispaa ya Sumbawanga vituo vinne (4), Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga kituo kimoja (1) na Nkasi kituo kimoja (1): 8.6. MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI: Mhe.NaibuWaziri, Mkoa unafanya ufuatiliaji na utaratibu wa mapambano dhidi ya UKIMWI. Jumla ya watu 83,000 wamejitokeza kupima VVU/ UKIMWI kwa mwaka 2012 ikiwa wanaume ni 41,519 na wanawake ni 42,481. Waliokutwa wameambukizwa jumla ni 27,196 ikiwa wanaume ni 10,525, wanawake ni 16,671 na watoto wenye maambukizi ni 1,754 kwa mwaka 2012. Mkoa umeendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa njia ya hamasa kwa kutumia gari la sinema (cinema van) na pia kutoa misaada ya kibinadamu kwa makundi yenye uhitaji katika kata 27,WAVIU 313 wamepatiwa misaada,watoto yatima 2,747 wamelipiwa ada shule za sekondari na msingi. 8.7 UFUATILIAJI WA ASASI ZA KIRAIA. Mhe.NaibuWaziri, Mkoa umefanya ufuatiliaji na kuzijengea uwezo jumla ya Asasi za Kiraia 115 zilizo hai. Pia Mkoa unawezesha usajili wa Asasi mbalimbali zinazoomba usajili . wadau hao wanatambuliwa na Mkoa wanatoa huduma za kijamii kama utoaji wa huduma za kibinadamu kwa WAVIU, watoto yatima, wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi,pia hutoa hamasa dhidi ya mapambano dhidi ya UKIMWI,
17

hamasa ya kilimo cha kisasa, hamasa ya afya ya uzazi, na kuwajengea uwezo wavuvi kwa kuwapatia elimu ya UKIMWI, uvuvi na utunzaji wa rasilimali maji na mazingira yanayowazunguka kwa ujumla. 9.0. KILIMO: Mhe.NaibuWaziri, Hali ya maendeleo ya kilimo kwa msimu wa 2011/2012 ni ya kuridhisha. Kulikuwa na athari za mwenendo wa unyeshaji mvua ambapo mwanzoni (Desemba Januari 2012) zilinyesha kwa wingi kiasi cha kuathiri kalenda za upandaji na ukuaji wa mimea. Baadaye mwezi Machi kulitokea ukame wa karibu majuma matatu hali iliyoathiri uwekaji mbolea ya kukuzia mashambani na ubebaji wa mazao hasa mahindi. Mkoa wa Rukwa ulilenga kulima jumla ya hekta 395,141 za mazao ya chakula kwa matarajio ya kupata tani 1,409,869.5. katika utekelezaji zimelimwa jumla ya hekta 380,671 sawa na 96% na kutupatia mavuno ya tani 1,000,349.2 sawa na 71% ya malengo. Katika msimu wa kilimo wa 2012/2013 Mkoa umelenga kulima jumla ya hekta 401,837.0 za mazao ya chakula na hekta 93,103.0 za mazao ya biashara ambazo tunatarajia kupata tani 1,357,836.0 za mazao ya chakula na tani 184,731.4 za mazao ya biashara. 9.1 Hali ya chakula Mhe.NaibuWaziri, Mahitaji ya chakula kwa wakazi wa Mkoa wa Rukwa wapatao 1,037,196 (projection 2012) ni sawa na tani 280,043, hivyo tulikuwa na ziada ya tani 820,306, kati ya hizo ziada ya mahindi ni tani 239,766. Kulingana na hali mbaya ya chakula nchini hususan mikoa ya kanda ya kati, kanda ya ziwa na Kaskazini, na kwa kuwa Mkoa wetu umekuwa kimbilio la wengi kwa mahitaji ya chakula, kiasi kikubwa cha ziada hiyo kimenunuliwa na kusafirishwa nje ya Mkoa. 9.1. Matumizi ya Pembejeo Mhe.NaibuWaziri, Mkoa wa Rukwa tulipatiwa jumla ya vocha za pembejeo zenye ruzuku 316, 779 zinazotosheleza jumla ya ekari 105,593 kwa idadi hiyo hiyo ya kaya za wakulima. Vocha hizo zina
18

thamani ya Shilingi bilioni 7.6. Mgawanyo na matumizi yake kwa Halmashauri ni kama ilivyo katika jedwali Namba 9 hapa chini.
Jedwali Na.9: MGAWANYO WA VOCHA ZA PEMBEJEO KIHALMASHAURI. HALMASHAURI Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga Halmashauri ya Wilaya Nkasi JUMLA MAPOKE ZI 140,157 55,401 121,221 316,779 MATUMIZI 139,296 53,924 121,116 314,336 BAKI 861 1,477 105 2,443

Changamoto Mkoa ulikabiliana na changamoto zifuatazo katika kutekeleza Mfumo wa usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa kutumia vocha: Bei za mbolea ya kupandia kuwa juu tofauti na ilivyotegemewa na kufanya baadhi ya wakulima walengwa kushindwa kuchangia tofauti ya bei. Uwezo mdogo wa wakulima kuchangia gharama za package nzima zinazofikia Sh. 124,000 hadi 133,000/=, hivyo kuchagua aina moja ya pembejeo mfano, mbegu tu au mbolea ya kukuzia tu. Hali hii imefanya malengo ya uzalishaji (tija) yasifikiwe. Baadhi ya mawakala kutokuwa na elimu ya uhifadhi na utunzaji wa pembejeo za kilimo. Mwitikio mdogo wa wakulima katika kutumia mbolea ya Minjigu kutokana na sababu mbalimbali. Kukosa mawakala wakutosha wenye mitaji ya kusambaza pembejeo vijijini kabla ya malipo Uadilifu mdogo kwa baadhi ya mawakala na watendaji kusimamia zoezi zima la ruzuku. Kutoeleweka vizuri mfumo wa kutumia hati za kukiri kupokea pembejeo kwa mkulima badala ya vocha kabla ya kuleta vocha. Kuchelewa kwa malipo kwa mawakala kulishusha morali wa kuhudumia wakulima.
19

9.2. Ununuzi wa mahindi Mhe.NaibuWaziri, Wakala wa hifadhi ya chakula cha Taifa kituo cha Sumbawanga walikadiria kununua kiasi cha tani 60,000 za mahindi katika msimu wa 2011/2012 kwa kutumia vituo 13 vya Mazwi, Bohari, Matai, Mwimbi, Katazi, Legezamwendo, Laela, na Mtawisa katika wilaya ya Sumbawanga na Namanyere, Mtenga, Kasu, Swaila na Ntalamila katika wilaya ya Nkasi. Ununuzi ulianza mwezi Agosti 2012, hadi kufikia mwezi Desemba 2012, tani zipatazo 7,346.42 zilinunuliwa sawa na asilimia 12.24. Hali hii ilitokana na mahindi mengi kuuzwa mapema na kwa bei ya juu kwa wafanya biashara kutoka mikoa iliyokuwa na upungufu wa chakula. 9.3. KILIMO CHA UMWAGILIAJI. Mhe. Naibu Waziri, Mpango kabambe wa Umwagiliaji Taifa wa mwaka 2002, ulibaini kuwa Mkoa wa Rukwa una jumla ya Hekta 527,721 zenye uwezo wa kumwagiliwa. Kati ya eneo hilo kekta 14,310 zina uwezo wa juu, hekta 42,294 zina uwezo wa kati na hekta 471,117 uwezo wake ni wa chini. Kwa sasa eneo linalomwagiliwa ni hekta 14,382.08 sawa na 25.41% ya eneo lenye uwezo wa juu na kati wa kumwagiliwa. Mkoa una jumla ya Miradi ya Umwagiliaji 10 ambayo inaendelezwa kwa njia ya kisasa na Miradi ya Umwagiliaji 16 ambayo haijaendelezwa inamwagilia kwa kutumia njia za asili (Traditional Irrigation). Kwa mwaka 2011/2012 Mkoa ulipangiwa jumla ya Sh.1,322,000,000/=kutoka Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya (DIDF). Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:- Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Sh.1,072, 000,000/= na Wilaya ya Nkasi Sh.250, 000,000/= . Aidha kwa mwaka 2012/2013 Mkoa umepangiwa jumla ya Sh.1,031,250,000/= kutoka Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya (DIDF). Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:- Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Sh.515,625,000/= na Wilaya ya Nkasi Sh.515,625,000/=.
20

9.4.1. CHANGAMOTO ZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI: Mhe.NaibuWaziri, Katika utekelezaji wa shughuli za Umwagiliaji mkoa unakabiliwa na changamoto zifuatazo. Upungufu wa wataalamu na vitendea kazi, katika ngazi ya Halmashauri za Wilaya. Kutokuwepo na wakandarasi wa ndani (Private Sector) wa kutosha mkoani wenye uwezo wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji. Kutokuwepo na wawekezaji(Investors involved in Irrigation Agriculture) toka sekta binafsi (Private Sector) kwenye Kilimo cha umwagiliaji. Elimu ndogo kwa wakulima juu ya kuzingatia matumizi bora ya maji utunzaji bora wa mimea na matumizi bora ya zana za kilimo katika skimu za umwagiliaji. Elimu ndogo kwa wakulima kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira. Hii inasababisha athari za mazingira, mfano kukata miti na kulima kwenye vyanzo vya mito au kando kando ya mito. Elimu ndogo Kwa Wakulima juu ya umuhimu wa uibuaji wa miradi ya umwagiliaji katika ngazi ya vijiji. Mkoa umejipanga kutatua changamoto kama ifuatavyo: Halmashauri za Wilaya zimeelekezwa kuajiri wataalam wa umwagiliaji angalau mhandisi mmoja wa umwagiliaji, mpimaji mmoja na fundi mchundo wa umwagiliaji watatu. Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakandarasi wa ndani (Private Sector) waliopo mkoani wenye uwezo wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji wafanye kazi hizo. Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa ili sekta binafsi (Private Sector) wawekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji (Investing in Irrigation Agriculture). Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuzingatia matumizi bora ya maji, utunzaji bora wa mimea na matumizi bora ya zana za kilimo katika skimu za umwagiliaji. Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira.

21

Halmashauri zimeelekezwa kuweka sheria ndogo ndogo kuzuia ukataji wa miti na kulima kwenye vyanzo vya mito au kando kando ya mito. Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa uibuaji wa miradi ya umwagiliaji katika ngazi ya vijiji . Mkoa umetoa maagizo kwa kila Halmashauri kuwa na Mpango wa matumizi bora ya ardhi. 9.4.3 MATUMIZI YA ZANA ZA KILIMO: Mhe.NaibuWaziri, Matumizi ya wanyamakazi (maksai) kwa mwaka 2011/2012 ni asilimia 80% ya nguvu kazi iliyotumia wanyamakazi katika kulima hekta 405,016 za mazao ambalo ni sawa na 324,012.8 hekta ya eneo lililolimwa kwa wanyamakazi kwenye msimu wa kilimo. Mkoa wa Rukwa una jumla ya trekta kubwa 60 na matrekta madogo 199 Mwaka 2011/2012 hekta 40,501.6 zimelimwa kwa kutumia trekta kubwa na hekta 32,401.0 kwa kutumia matrekta madogo na hekta 8,100.32 kwa wanaolima kwa mikono. 9.4.4 Miradi ya Sekta ya Kilimo. Mhe.NaibuWaziri, Katika mwaka 2011/2012 Mkoa umepangiwa jumla ya Sh. 2.659 bilioni za miradi ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo. Pamoja na kupangiwa fedha hizo mwisho wa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Mkoa ulivuka na kiasi cha Sh. 2.665 bilioni. (Sumbawanga Sh.1.77 bilioni na Nkasi Sh. 0.885 bilioni). Miradi iliyolengwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa masoko, ujenzi wa maghara, ujenzi wa skimu za umwagiliaji, ukarabati wa nyumba za maafisa ugani, ujenzi wa vituo vya rasilimali za kilimo, ujenzi wa majosho, marambo ya Kilyamatundu na Mtenga, ujenzi wa machinjio, ujenzi wa machinjio,ujenzi wa minada ya mifugo na Majosho. Pamoja na Serikali kuendelea kuzipatia Halmashauri fedha kwa ajili ya Miradi ya ASDP kumekuwepo na changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa miradi hiyo zifuatazo: Kasi ndogo ya wakandarasi katika kutekeleza miradi ya DADPS iliyopo Wilayani.
22

Uchangiaji mdogo wa wananchi katika Miradi ya maendeleo ya kilimo (DADPS) Baadhi ya Miradi kutekelezwa chini ya viwango. Uhaba wa wahandisi wa Umwagiliaji katika wilaya za Mkoa wetu. Uhaba wa wakandarasi wenye uzoefu katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji Umakini mdogo wa watendaji wa Halmashauri katika kusimamia miradi ya maendeleo ya kilimo. Halmashauri kutumia fedha za miradi kwa shughuli zisizoendana na utekelezaji wa miradi. Ushirikiano hafifu kati ya idara na idara katika Halmashauri. Ucheleweshwaji wa fedha za Miradi ya Sekta ya Kilimo toka Serikali kuu. 10.0 MIFUGO 10.1 Rasilimali za Ufugaji.

Mhe.NaibuWaziri, Kulingana na Sensa ya Kilimo ya 2003, asilimia 34 ya wananchi wa vijijini katika Mkoa wa Rukwa hujishughulisha na ufugaji. Hivyo ufugaji ni shughuli ya pili kwa umuhimu kiuchumi baada ya kilimo cha mazao. Mifugo ni rasilimali (asset) muhimu inayomilikiwa na wananchi wa vijijini baada ya ardhi. Mbali na kutumika kama benki hai mifugo hii pia hutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa njia ya nguvukazi na samadi. Zaidi ya asilimia 70 ya wakulima wa Mkoa wa Rukwa hutumia nguvukazi ya wanyama katika shughuli mbalimbali. Maeneo yanayotumika katika malisho Mkoani ni hekta 1,136,218 na malisho yasiyotumika kutokana na mbungo ni hekta 18,952. Mkoa mpya wa Rukwa unakadiriwa sasa kuwa na ngombe 438,953, mbuzi 152,899, kondoo 22,686, nguruwe 49,989, kuku 470,595 na punda 6,171. Utekelezaji katika eneo la ufugaji ulihusisha yafuatayo:10.2 Shughuli zilizofanyika katika kipindi kilichopita ni kama ifuatavyo
23

(i)

Kuratibu usambazaji na matumizi ya dawa ya kuogesha mifugo yenye ruzuku. Mwezi Juni, 2012 mkoa ulipokea jumla ya lita 5,600.5 za dawa ya kuogesha mifugo yenye ruzuku ya Serikali kwa 40%. Jumla ya lita 2,400.5 za dawa zilipelekwa mkoa wa Katavi. Kutokana na matumizi hafifu ya dawa hii katika baadhi ya maeneo, wasambazaji waliopangiwa na serikali kuleta dawa hii mikoa ya Rukwa na Katavi bado wanayo dawa ya mwaka uliopita lita 14,437.6 ambayo inaendelea kusambazwa. Kati ya majosho 62 yaliyopo, yanayofanya kazi ni 35 (56%).

(ii)

Kufuatilia matukio na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko. Ugonjwa wa Homa ya Mapafu (CBPP) umeendelea kuenea katika maeneo mengi ya Mkoa. Wilaya ya Nkasi imeendesha chanjo dhidi ya ugonjwa huu kwa ufanisi mkubwa ambapo jumla ya ngombe 111,381 (82%) walichanjwa mwezi Juni/Julai baada ya wafugaji kuchangia gharama ya Sh. 200/= kwa ngombe. Aidha kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na kondoo katika baadhi ya mikoa, chanjo dhidi ya ugonjwa huu inaendelea kutolewa katika wilaya za Sumbawanga na Nkasi ambapo hadi sasa wanyama 6,000 wamechanjwa katika wilaya ya Sumbawanga. Mashindano ya wafugaji kitaifa Mfugaji kutoka Wilaya ya Nkasi aliwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika mashindano ya wafugaji kitaifa mjini Dodoma na kuibuka mshidi wa kwanza katika kundi la wafugaji wadogo wa ngombe wa nyama. Ushindi huu unaendelea kutangaza fursa zilizopo katika Mkoa wa Rukwa.

(iii)

10.3 MIKAKATI YA SEKTA Mhe.NaibuWaziri, Mkoa wa Rukwa unazo fursa nyingi za ufugaji ikiwa ni pamoja na ardhi ya kutosha, mvua za kuaminika, rasilimali ya mifugo ya kutosha na soko zuri la ndani na nchi jirani ambazo hazina rasilimali ya kutosha ya mifugo. Mkoa unayo machinjio ya
24

kisasa yenye uwezo wa kuchinja kwa wakati mmoja Ngombe 200 na Mbuzi zaidi ya Hamsini.

10.4 CHANGAMOTO ZA SEKTA Mhe.NaibuWaziri, Mkoa unakabiliana na changamoto mbalimbali katika kuendeleza sekta ya ufugaji. Baadhi ya changamoto zinazoathiri ufugaji katika Mkoa wa Rukwa ni pamoja na zifuatazo: Baadhi ya changamoto muhimu zinazoathiri ufugaji katika Mkoa wa Rukwa ni pamoja na zifuatazo: Ukosefu wa mipango ya matumizi bora ya ardhi; pale ilipo mipango hii haizingatiwi. Uhamiaji holela wa mifugo kutoka mikoa jirani. Mbali na kusababisha migogoro ya ardhi hali hii huchangia sana kuenea kwa magonjwa ya mifugo. Msongamano wa mifugo katika baadhi ya maeneo, hasa yale yenye vyanzo vya maji vya uhakika. Huduma duni za ugani kutokana na uhaba wa wataalam na wachache waliopo kutotumika ipasavyo. Sekta binafsi dhaifu na ukosefu wa asasi za wafugaji. Uhaba wa miundombinu ya huduma za mifugo

12.0 UVUVI. Mhe.NaibuWaziri, Kutokana na sensa ya mwaka 1999 uzalishaji wa samaki toka Ziwa Rukwa unakadiriwa kuwa ni tani 7,000 na Ziwa Tanganyika linakadiriwa kuzalisha samaki kiasi cha tani 165,000 hadi tani 200,000 kwa mwaka wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 80 hadi milioni 100. Kuna aina mbali mbali ya samaki wanaopatikana katika maziwa na mito iliyopo katika Mkoa wetu. Ziwa Tanganyika linatupatia samaki aina ya dagaa, migebuka, sangara, kuhe, kambale na samaki wa mapambo. Ziwa Rukwa linatupatia kambale, gege na mamba. Dagaa na migebuka wanaopatikana ziwa Tanganyina na gege toka ziwa Rukwa mara nyingi hukaushwa na kupelekwa kuuzwa
25

kweye masoko makubwa ndani na nje ya nchi mfano Zambia, Kongo na Burundi. 12.1. CHANGAMOTO. Ukosefu wa nishati ya umeme kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika . Ukosefu wa zana bora za uvuvi kwa wavuvi. 13.0. USHIRIKA. Mhe.NaibuWaziri, Hadi kufikia mwezi 31 Disemba, 2012 Mkoa una jumla ya Vyama vya Ushirika 93 zikiwemo SACCOS 80 zenye jumla ya Wanachama 10,938 na Hisa za jumla ya Sh.286,600,000/= akiba za Sh.1,581,083,000/= na amana zenye thamani ya Sh.27,999,000/= hivyo kufanya jumla ya mtaji wenye thamani ya Sh.1,872,682,000/=. Jumla ya Sh.5,732,891,000/= zimetolewa kama mkopo kwa wanachama na kiasi cha Sh.4,085,820,000/= kimerejeshwa sawa na asilimia 71.3 ya kiasi cha fedha zilizokopeshwa. 13.1: CHANGAMOTO. Mhe.NaibuWaziri, Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kuendeleza sekta ya Ushirika Mkoani Rukwa unakabiliwa na changamoto zifuatazo: Upungufu wa Maafisa ushirika katika Halmashauri. Upungufu wa vitendea kazi kwa maafisa ushirika ikiwemo vyombo vya usafiri. Baadhi ya Halmashauri kuchelewesha makato (deductions) ya SACCOS za wafanyakazi. Baadhi ya wanachama wa Vyama vya Akiba na Mikopo kuchelewesha ama kutorejesha kabisa mikopo. 14.0 SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA Mhe. Naibu Waziri, Katika sekta hii kuna viwanda vidogo na vya kati vinavyoendeshwa, Viwanda hivyo vinajihusisha na shughuli za usindikaji wa nafaka, samaki, nyama utengenezaji wa sabuni. Hadi sasa Mkoa una Viwanda saba ambavyo ni:- SAAFI Co.LTD, Tropical grain Co.LTD, Fantashiru Milling, Ikuwo Enterprises, Energy Milling.Co.Ltd, Migebuka Premium (Premji).
26

14.1. BIASHARA Mhe.NaibuWaziri, Mkoa unaendelea kuhakikisha kuwa unawakwamua wananchi wake kiuchumi. Katika jitihada hizo maafisa biashara wamekuwa wakitoa elimu na ushauri kwa wajasiriamali juu ya kuendesha biashara zao kwa mafanikio na uboreshaji wa vifungashio kwa wasindikaji ili kuwavutia wateja. Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO) imekuwa mstari wa mbele katika kuiendeleza sekta ya biashara. 14.2. BEI ZA VYAKULA NA BIDHAA MBALIMBALI Mhe. Naibu Waziri, Tokea tupate agizo la kuangalia mwenendo wa bei hapa Mkoani, hali ya upatikanaji wa bidhaa mbalimbali imekuwa ya kuridhisha na bei ya baadhi ya bidhaa imekuwa ya kupanda na kushuka kama ifuatavyo; Vyakula: Bei ya rejareja kwa kilo moja ya Sukari ni kati ya Sh. 2,000 hadi 2300. Mafuta ya kula lita 10 ni Sh. 30,000 sawa na Sh. 3,000 kwa lita Unga wa Sembe kilo moja inauzwa kwa Sh. 700/-1,000 Mchele unauzwa Sh. 1,400 hadi Sh. 1,700 kwa kilo. Bidhaa nyingine bei zake ni kama ifuatavyo:- Petrol lita moja Sh. 2,262 /=, Diesel lita moja Sh. 2,300/=, Mafuta ya taa, lita moja Sh. 2,221/=, Gesi kilo 15 ni Sh. 57,000/= na Saruji mfuko wa kilo 50 unauzwa kwa shilingi 21,000/=. 14.3. CHANGAMOTO ZILIZOPO: Ubovu wa miundombinu Ukosefu wa nishati kwa baadhi ya maeneo Ukosefu wa masoko ya baadhi ya mazao 15.0 MALIASILI NA MAZINGIRA Mhe. Naibu Waziri, Mkoa wa Rukwa una fursa nyingi za maliasili (utalii, misitu na ardhi) ambazo bado hazijatumiwa kikamilifu kama Maporomoko ya mto Kalambo yenye mita 235, wanyama waliopo katika mapori tengefu ya Lwafi, mbega wekundu waliopo katika msitu wa hifadhi wa Mbizi. Uwepo wa makaa ya mawe, uwepo wa ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa pamoja na mito midogo midogo
27

mingi. Katika kutekeleza sera ya Taifa na sheria ya Mazingira, Mkoa umeendelea kuhamasisha wananchi katika kuhifadhi Mazingira kwa njia mbalimbali zikiwemo za upandaji miti na utoaji elimu ya utunzaji wa mazingira. 15.1. HIFADHI YA MAZINGIRA (i) UPANDAJI MITI; Jumla ya miti 2,468,052 ilioteshwa na kupandwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Rukwa mwaka 2011/2012. (ii) MATUMIZI BORA ARDHI Jumla ya vijiji 13 vimeshatekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi (Land Use Plan) kati ya vijiji 259 vilivyopimwa. ELIMU YA MAZINGIRA; Elimu hii inatolewa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya ziwa Tanganyika, mradi uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Divisheni ya Mazingira, Taasisi ya kuhifadhi wanyama iliyopo Mbeya (WCS - Wildlife Conservation Society), REYO - Rukwa Environment Youth Organization, KAESO, ADAP - Association for Development for Areas Protected, REDESO, GMU n.k,

(iii)

15.2. MRADI WA HIFADHI YA ZIWA TANGANYIKA Mhe.NaibuWaziri, Katika Mkoa wa Rukwa, Programu hii inatekeleza miradi miwili kama ifuatayo: Mradi wa usimamizi wa Bonde (Catchments Management) Mradi wa uendelezaji wa Uvuvi na Hifadhi ya Mazingira ya ziwa Tanganyika. Mambo ambayo yanapelekea kuandaa mkakati wa kuhifadhi ziwa Tanganyika yanatokana na mambo yafuatayo;- Uchafuzi wa ziwa (environmental pollusion) - Kuongezeka kwa tabaka la udongo (sedmentation) - Uharibifu wa makazi ya viumbe ( destruction of breeding site) - Uvuvi usio endelevu ( unsustainable fisheries) 15.3. MISITU NA NYUKI
28

Mhe.NaibuWaziri, Katika kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya Misitu na nyuki kazi zifuatazo zimetekelezwa kwa mwaka 2011/2012 Mkoa umekusanya Shs.201,559,099/= kutokana na ushuru utokanao na mazao ya misitu na ukataji wa leseni za biashara ya mzao ya misitu. Jumla ya mita za ujazo 3000 zimetolewa kwa ajili ya ukusanyaji wa kuni Tani 420 za asali zimepatikana kutokana na urinaji wa asali Kamati 15 za wafuga nyuki zimeanzishwa katika vijiji 15 na vikundi 77 vimenufaika na elimu ya ufugaji nyuki. Jumla ya mizinga 684 ya kisasa imewekwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri zetu za Mkoa wa Rukwa. Jumla ya miti 2,468,052 imeoteshwa maeneo mbalimbali katika Mkoa wa Rukwa kwa mwaka 2011/2012. 15.4. WANYAMAPORI Mhe.NaibuWaziri, Katika kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya wanyamapori kazi zifuatazo zimetekelezwa kwa mwaka 2011/2012. Jumla ya watu 2800 waliondolewa kwenye Mapori ya Akiba, ambapo walikuwa wakiendesha shughuli za kibinadamu (kilimo, ufugaji na uvuvi), ambapo wawaliokuwa wanaendesha shughuli za uvuvi wamepewa muda wa kuondoka (mwisho mwezi wa kumi) wafugaji walioachia mifugo 17 walitozwa faini na mmoja alifungwa na wawili wanatafutwa. Aidha zoezi hilo la kuwaondoa wavamizi litaendelea katika msitu wa hifadhi wa Kalambo na misitu mingine ya hifadhi. Jumla ya doria 2 kubwa na doria 4 ndogo zimefanyika katika maeneo misitu ya asili na Mapori ya Akiba. 15.5. CHANGAMOTO: Uelewa mdogo wa wananchi dhidi ya hifadhi ya mazingira. Ukataji wa miti holela kwa ajili ya nishati ya kuni, mkaa, ujenzi na upanuzi wa mashamba. Uchungaji holela wa mifugo na wa kuhamahama, na Uchomaji moto ovyo.
29

15.6. MIKAKATI: Kuwashirikisha wananchi katika uibuaji wa miradi ya maendeleo inayohusisha masuala ya mazingira, mfano mradi wa utengenezaji wa sabuni. Kuendelea kuzijengea uwezo kamati za mazingira za vijiji ( VNRC) 16.0. 16.0. MIUNDOMBINU SEKTA YA BARABARA

16.1. MATENGENEZO YA BARABARA KUU Mhe. Naibu Waziri, Hadi kufikia tarehe 31, Novemba 2012, kazi za matengenezo ya barabara kuu na za Mkoa zilizopangwa kufanyika katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 zilikuwa zimekamilika ambapo km 447, madaraja 25 yalijengwa ama kutengenezwa kwa gharama ya Shilingi. 1,452,759,000. Matengenezo ya barabara kwa bajeti ya 2012/13 yanaendelea kufanyika na yapo katika hatua tofauti za utekelezaji. 16.1.1 UKARABATI NA UJENZI WA BARABARA KUU NA ZA MKOA. Katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 ukarabati/ujenzi kwa kutumia fedha za ndani (bajeti ya maendeleo) tulitarajia kutengeneza km 101, barabara hizi zimekamilika kwa kutumia Sh. millioni 3,014,797. MIRADI YA MAENDELEO YA BARABARA 16.2.1 UKARABATI NA MATENGENEZO KUPITIA MPANGO WA PMMR (PerformanceBased Management and Maintenance of Roads).
16.2

Mhe. Naibu Waziri, Mradi wa PMMR kwa sasa unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 ambayo mikataba iliyopo ni ya Miaka Mitano. Katika kipindi cha 2010/2011 hadi 2011/2012 kiasi cha km 111.59 za barabara zimekarabatiwa ambapo zimeigharimu Serikali Sh.5,763,432,621.72.

30

16.3. UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI (SUMBAWANGA -LAELA- TUNDUMA (228.40 KM) 16.3.1. SEHEMU YA SUMBAWANGA - LAELA (95.31 KM) Eneo hili linajegwa na Kampuni ya Aarsleff-BAM International Joint Venture V.O.F kutoka Denmark na Uholanzi kwa gharama ya USD 97 Milioni chini ya mhandisi mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufaransa. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia tarehe Novemba, 2012 yalikuwa yamefikia 49.9% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri. 16.3.2. SEHEMU YA LAELA - IKANA (64.2 KM) Eneo hili linajegwa na Kampuni ya China New Era International Engineering Corporation kutoka China kwa gharama ya Sh. bilioni 76.1 chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufaransa. Maendeleo ya jumla ya mradi Desemba, 2012 yalikuwa yamefikia 65.51% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri. 16.3.3. SEHEMU YA IKANA - TUNDUMA (63.7 KM) Eneo hili linajegwa na Kampuni ya Consolidated Contractors Group S.A (offshore) (CCC) kutoka Ugiriki chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufaransa kwa gharama ya Sh. billion 82.5. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi Desemba 2012, yamefikia 44% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri. 16.3.4 SUMBAWANGA-NAMANYERE-MPANDA/KIZI-KIBAONI (274 KM) 16.3.5 SEHEMU YA SUMBAWANGA-KANAZI (75 KM) Eneo hili linajegwa na Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas ODwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikana na
31

Apex Engineering Ltd kutoka Tanzania kwa gharama ya Sh. bilioni 78.8. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia Desemba, 2012 yalikuwa 25.1% ya kazi zote zilizopangwa. Kuchelewa kwa malipo ya Mkandarasi kumeathiri kasi ya utekelezaji wa mradi, ambapo mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba, 2012. 16.3.6 SEHEMU YA KANAZI-KIZI-KIBAONI (76.6 KM) Eneo hili linajegwa na Kampuni ya China Hunan Construction Engineering Group Corporation kutoka China, chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas ODwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd kutoka Tanzania, kwa gharama ya Sh.82.84 bilioni. Maendeleo ya jumla ya mradi Desemba, 2012 yalikuwa 30.12% ya kazi zote zilizopangwa. Mkandarasi anaendelea vizuri ingawa kuchelewa kwa malipo ya Mkandarasi kumeathiri kasi ya utekelezaji wa mradi ambapo mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba,2012.
16.3.7 SUMBAWANGA-MATAI-KASANGA PORT (112KM)

Eneo hili linajegwa na Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G)/ Newcentry Company Ltd chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas ODwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd kutoka Tanzania. Gharama ya Mradi ni Sh.133.3 billion. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia Desemba, 2012 yalikuwa 30.29% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu unatekelezwa kwa mkataba wa Usanifu na Ujenzi (Design and Build Contract). Usanifu wa kina wa kilometa 70 za kwanza umekamilika na Mkandarasi ameruhusiwa kuanza kazi katika kilometa 60 za kwanza. Usanifu wa kilometa 42 zilizobaki unaendelea. 16.3.8 MIRADI YA UPEMBUZI YAKINIFU NA USANIFU WA KINA Miradi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Mkoa ni:32

i).

Barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda: Sehemu ya Kizi-Sitalike -Mpanda (123 km) Barabara ya Matai-Kasesya (47 km)

ii).

16.4 CHANGAMOTO Mhe.Naibu Waziri, Tunakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo: (i) Uhaba wa mitambo ya matengenezo na ujenzi wa barabara pamoja na Magari kwa Wakandarasi na hata Wakala (TANROAD) (ii) Ugumu wa makandarasi kupata dhamana (bonds/guarantees) kutoka katika vyombo vya fedha na hivyo kuchelewa kuanza kazi. 17.0. KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA NA ENEO JIPYA LA KISUMBA 17.1. HISTORIA FUPI YA KIWANJA Mhe.NaibuWaziri, Kiwanja hiki kipo katika daraja la 3C ambapo miundombinu yake huruhusu kutua na kuruka kwa ndege za uzito usiozidi tani 20. Barabara ya kutua na kuruka kwa ndege (runway) katika kiwanja hiki ni changarawe na ina urefu wa km. 1.6 tu. Kiwanja kina hudumia ndege za ndani ya nchi (charter flights) za kukodi, ndege za abiria, ndege za serikali na nyakati nyingine nchi za jirani kama vile Zambia kwa ajili ya huduma za jamii za kuangamiza wadudu waharibifu. 17.2.UENDESHAJI KIWANJA Miundombinu: Katika majukumu yetu ya uendeshaji kiwanja tunawajibika kuhakikisha kuwa wakati wote miundombinu ya kiwanja hususani barabara ya kutua na kuruka ndege ziko katika hali salama kwa ndege kutua na kuruka. 17.3. HUDUMA ZA ZIMAMOTO NA UOKOAJI. Kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kiko katika daraja la sifuri (0) la viwango vya zimamoto (fire service category zero). Hii kutokana na kutokuwepo kabisa kwa gari la kutoa huduma ya zimamoto na uokoaji.
33

17.4. MAPATO NA MATUMIZI YA KIWANJA Kiwanja hiki ni moja ya viwanja vingi vinavyoendeshwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ambavyo havina mapato ya kutosha kujiendesha chenyewe. Hivyo matumizi ya kiwanja ni makubwa mara 36 ya mapato, kuanzia mwaka 2005 hadi 2011 kiwanja kimepata jumla ya Sh.8,437,900.00 na kutumia jumla ya Sh. 398,800,282.00 kwa kujiendesha, kama inavyoonyesha hapo chini katika jedwali namba 10.
Jedwali Na.10: MAPATO YA KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA SN Mwaka Mapato (Tsh.) Matumizi (Tsh.) 1 2010/2011 5,640,022 109,042,143 2 2009/2010 4,785,000 8,749,6974 3 2008/2009 1,163,500 86,465,786 4 2007/2008 1,918,200 86,966,658 5 2006/2007 285,600 75,601,685 6 2005/2006 285,600 62,269,179 Jumla 8,437,900 398,800,282

17.5. CHANGAMOTO ZINAZOKABILI KIWANJA Mhe.NaibuWaziri, Kiwanja cha ndege cha sumbawanga kinakabiliwa na changamoto zifuatazo: Kiwanja chetu hakina jengo la Watu Mashuhuri (VIP). Hivyo hupelekea tunapopata ugeni wa kitaifa inatulazimu kuchanganyika na abiria wa kawaida. Kiwanja hakina mitambo ya ukaguzi wa kiusalama kama mashine za kukagulia mizigo ya abiria (X-ray machine), mashine za kubaini vifaa vya chuma(walk through metal detectors). Hali hii huwalazimu maafisa wa usalama wa kiwanja kufungua mizigo ya abiria kwa ajili ya ukaguzi(Physical search) na kasha kutumia Hand held metal detectors kwa ajili ya ukaguzi wa abiria kabla ya kupanda ndege. Hali ya kukosekana kwa mitambo hiyo hupelekea ugumu wa kazi na kusababisha usumbufu na kero kwa abiria wanadai kuwa hali hiyo inawadhalilisha. Ukosefu wa gari la zimamoto; kituo hiki hakina kabisa gari la zimamoto.
34

Migogoro ya ukatishaji watu kiwanjani. Kutokana na ukosefu wa uzio wa usalama kuna tatizo la ukatishaji watu kiwanjani la mara kwa mara. 17.6. MIPANGO YA MAENDELEO Kiwanja cha sumbawanga ni mojawapo ya viwanja saba vilivyofanyiwa usanifu wa kina (feasibility study and Detailed Engineering Design) kwa ufadhili wa benki ya Dunia katika mwaka 2007/08. Baada ya usanifu wa kina serikali imekuwa ikitafuta fedha kutoka kwa vyanzo mbalimbali ili kuweza kukarabati miundombinu ya kiwanja. Na kwa sasa serikali imeshafanikiwa kupata mkopo wa Euro million 50 kutoka European Investment Bank (EIB) kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vitano ikiwemo Sumbawanga. Serikali ya Mkoa wa Rukwa imeshatenga eneo jipya la kujenga kiwanja kikubwa cha ndege katika eneo la Kisumba umbali wa km 20 toka Sumbawanga mjini. Serikali ya Mkoa kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ilipendekeza ianze kujenga kiwanja katika eneo la Kisumba badala ya kuendeleza kiwanja cha sumbawanga mjini kwa kutumia mkopo wa fedha kutoka EIB uliokusudiwa kukiendeleza kiwanja cha Sumbawanga mjini. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imetenga Shilingi milioni 20 katika mwaka wa fedha 2012/13 kwa ajiri ya kufanya tathmini ya eneo la kisumba kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja kipya. 18.0. BANDARI YA KASANGA Mhe.NaibuWaziri, Bandari ya Kasanga huendesha shughuli zake kwa kusimamiwa na Kampuni ya Agro Truck Investment Ltd. Kampuni hii inakarabati ghati kwa kuongeza eneo la kuegesha meli pamoja na ujenzi wa ghala ili kukidhi mahitaji ya abiria na mizigo. Fedha za ukarabati zilipatikana kwa msaada wa Serikali ya Norway kupitia ushirikiano wa Rukwa Association of Non Governmental Organization (RANGO). Ujenzi wa Bandari ya Kasanga unatarajiwa kugharimu kiasi cha Dola Laki Mbili za Kimarekani ($ 200,000).
35

18.1. MAFANIKIO: Mhe.Naibu Waziri, Bandari inatazamiwa kupanuliwa kwa kujenga Maghala na majengo mengine ili kukidhi mahitaji ya bandari. Kwa hivi sasa tayari Maghala 2 yamejengwa na yanatumika kikamilifu. Maghala hayo yanauwezo wa kuhifadhi takriban tani 3,000 kila moja na yamegharimu Shilingi bilioni 1.1 fedha toka Mamlaka ya Bandari ya Tanzania. 18.2. CHANGAMOTO: Mhe.Naibu Waziri, Bandari ya Kasanga inakabiliwa na changamoto nyingi katika uendeshaji wake. Changamoto hizo ni pamoja na: Ukosefu wa fensi kuzunguka eneo la bandari Ukosefu wa nyenzo za kufanyia kazi ikiwepo focal lifts, winchi na safari chache za meli zinazofanywa kwa mwezi, na

Ukosefu wa huduma ya umeme wa uhakika.

19.0. SEKTA YA ARDHI. Mhe. Naibu Waziri, Mkoa hutegemea ardhi yake kwa ajili shughuli za Kilimo na kiuchumi katika kuleta maendeleo endelevu na kupunguza umaskini, mchango wa Sekta ya Ardhi katika maendeleo ya Mkoa ni pamoja na uhakika wa kupata chakula na kipato. Mkoa wa Rukwa una jumla ya vijiji 288, vijiji 201 kutoka Wilaya ya Sumbawanga na Vijiji 87 kutoka Wilaya ya Nkasi. Kati ya vijiji 237 (82.3%) tayari vimepimwa mipaka yake indaendelea katika Halmshauri zote husika. Aidha Mkoa wa Rukwa una mpango wakuhakikisha matumizi bora ya ardhi katika miji, vitongoji na vijiji vyake inaendelea kutayarishwa kulingana na upatikanaji wa fedha kwenye bajeti. Hadi kufikia Oktoba 2012 vijiji 19 vilikuwa tayari vimeandaliwa matumizi bora ya ardhi ambapo ni asilimia (6.6%) ya vijiji vya Mkoa wa Rukwa. Taratibu zinaendelea ili kuhakikisha kwamba vijiji vyote vinaandaliwa matumizi bora ya ardhi. Mkoa una mpango pia unaolenga kuhakikisha miji yetu inakuwa safi na salama kwa wakazi wa mijini. Mipango inayoelekezwa ni pamoja na: Kuhakikisha ardhi yote iliyoko mijini inapangwa na kupimwa.
36

Kuboresha endelevu.

Miundombinu,

huduma

za

jamii

na

makazi

Kuibua fursa na ajira na kuweka mikakati ya kuondoa umaskini uliokithiri mijini. Kuhakikisha wadau wote wa maendeleo mijini wakiwepo NGOs, CBOs, Cooperatives wanahusishwa kwenye mipango ya kuendeleza miji yetu Kuhakikisha wakati wote wa kuendeleza miji yetu mazingira yanalindwa. Kuhakikisha kwamba wakati wote wa kushughulia masuala yote ya ardhi sheria, kanuni na miogozo inafuatwa na kuzingatiwa ili kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.

Mafanikio:- Katika kipindi kilichoishia Octoba, 2012 Mkoa umeweza kufanya kazi mbalimbali kama inavyoonyesha katika jedwali namba 11 hapa chini.
Jedwali Na.11: UPIMAJI WA VIWANJA.
H/Mashauri Viwanja vilivyopang wa Viwanja vilivyopim wa Viwanja Vilivyoan daliwa Masham ba yaliyopi mwa Vijiji Vilivyopim wa mipaka Vijiji Vilivyoandal iwa matumizi bora ya ardhi Viwanja vilivyopim wa kwa uwekezaji

S wanga DC Swanga MC Nkasi Jumla

397 5500 2327 8224

436 1500 587 2523

4 1237 30 1271

19 32 3 54

155 82 237

15 4 19

13 10 23

19.1. CHANGAMOTO: Mkoa unakabiliwa na changamoto zifuatazo:(i) Mipango ya matumizi bora ya ardhi; Halmashauri hazijafanya kazi ya kutosha ya kubainisha matumizi bora ya ardhi kutokana na kinachoelezwa kuwa ni ufinyu wa bajeti. Kazi hii ikifanyika kikamilifu itasaidia kuepusha migogoro ya
37

Wakulima na Wafugaji katika Mkoa wetu pamoja na maliasili zilizopo.

20.0 MKONGO WA TAIFA Mhe. Naibu Waziri, Shughuli za kutandaza Mkongo wa Taifa zimekamilika katika Mkoa wetu na hadi sasa hakuna tukio lolote la hujuma dhidi ya Mkongo lililolipotiwa kutokea Mkoani kwetu. Hata hivyo Mkongo huu haukupitia katika Mji wa Namanyere ambapo ndio makao makuu ya Wilaya ya Nkasi. 21.0 SEKTA YA NISHATI 21.1. MITAMBO YA KUFUA UMEME Mhe. Naibu Waziri, Mji wa Sumbawanga unategemea umeme kutoka nchi jirani ya Zambia. Katika mwaka wa 2010, Serikali ilinunua na kufunga Generator nne zenye uwezo wa kuzalisha megawati tano (5). Kazi ya kusimika Mitambo ya kufua Umeme ilianza mwanzoni mwa mwezi April, 2011 na kumalizika mwanzoni mwa mwezi Juni, 2011. Mitambo ilianza kufua Umeme kuanzia tarehe 02.08.2011 japokuwa kwa vipindi tofauti tofauti umeme huu umekuwa haupatikani kwa sababu ya kukosekana kwa mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo. 21.2. MRADI WA UMEME NAMANYERE Mhe.NaibuWaziri, Awali mradi huu ulitarajiwa kukamilika mnamo mwezi wa Disemba 2011. Kazi ya kuweka nguzo na kutandaza nyaya kutoka mjini Sumbawanga hadi Namanyere wilayani Nkasi imekamilika. Ni matumaini ya mkoa kuwa umeme utawaka katika mji mdogo wa Namanyere vikiwemo vijiji 12. Mkoa unahitaji msukumo kutoka ngazi ya juu katika kuhakikisha kuwa umeme unapatikana Katika makao makuu ya wilaya zake zote na hasa wiliya mpya ya kalambo Mjini Matai na Namanyere. 22.0. MFUKO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA WATUMISHI MKOA WA RUKWA (RCSFF)
38

Mhe.NaibuWaziri, Mfuko wa kuboresha mazingira ya Watumishi Mkoa wa Rukwa (Zamani ukijulikana kama Mfuko wa Mwalimu Nyerere) tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2007 umewezesha upatikanaji wa jumla ya walimu wa sekondari 380 pamoja na watumishi wa idara ya afya 36 ( katika kada za Madaktari na Wauguzi). 22.1. HALI YA KIFEDHA YA MFUKO Mhe.NaibuWaziri, Hadi kufikia Desemba 2012, mfuko una jumla ya shilingi milioni moja. Kwenye akaunti zake mbili zilizo katika benki za CRDB na NMB. Aidha, Mfuko umewekeza fedha sehemu mbili tofauti kama ifuatavyo: UTT zimewekezwa Sh.200,000,000/= ambazo zimeishatoa faida ya Sh.57,000,000/=. Benki ya CRDB zimewekezwa Sh.35,000,000/= ambazo zimetoa faida ya Sh.4,500,000/= . 22.2. CHANGAMOTO NYINGINE ZINAZOUKABILI MFUKO. (i) Halmashauri hazichangii Mfuko wa kuboresha Mazingira kwa Watumishi (ii) Wananchi wengi bado hawajafahamu umuhimu wa kuchangia mfuko huu kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi za mfuko. (iii) Usimamizi usioridhisha wa mfuko wenyewe. 23.0. KONGAMANO LA UWEKEZAJI. Mhe. Naibu Waziri, Mkoa Umeweza kuandaa kwa mafanikio makubwa Kongamano la uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika lililofanyika Wilayani Mpanda kuanzia tarehe 15-18/10/2011 na kufunguliwa rasmi na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 17/10/2011. Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuzinadi fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika Ukanda huu. Jumla ya washiriki zaidi ya 300 walishiriki kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo mabalozi 34 kutoka nchi mbalimbali. Aidha tathimini ya kongamano hilo ilifanyika tarehe 25/11/2012 ambapo Mkoa ulikuwa umepokea maombi toka kwa wawekezaji kumi na moja (11) walioonesha nia ya kuwekeza katika shughuli za Uvuvi, Hotel za kitalii, usafili wa Anga. Kati ya wawekezaji hao, tayari wapo waliokwisha kamilisha taratibu za uwekezaji na
39

wanaendelea na kazi, mfano yapo makampuni mawili ya Auric Air Na Mission Aviation Fellowship (MAF) wanaotoa huduma ya usafiri wa Anga mara tano kwa wiki, ujenzi wa Hotel mbili za kisasa za New Holland na Kalambo Falls lodge. Aidha kwa upande wa uwekezaji katika kilimo wapo wakulima nane(8) ambao wameingia mkataba na kampuni ya bia ya TBL kwa ajili ya uzalishali wa shairi ambapo jumla ya Ekari 2,050 zitalimwa. 24.0. MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA Mhe. Naibu Waziri, Mkoa umefanikiwa kutoa kitabu maalumu kinachoelezea wapi tulipokuwa wapi tulipo na wapi tuendako, kitabu hicho kinaitwa Taarifa ya Mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa Desemba 1961 - Desemba, 2011 Mkoa umeweza kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya maonesho Viwanja vya Sabasaba vya Mwalimu J.K. Nyerere vilivyopo Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 1 - 12 Desemba, 2011. Katika ngazi ya Mkoa maadhimisho yalifanyika Mjini Namanyere, kwa kuambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za idara za serikali na mashirika ya Umma zikiwemo Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wajasiriamali na Wadau wengine wa Maendeleo. 25.0 UTAWALA BORA. 25.1. TAARIFA YA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA. 25.1.1 MAPATO YA HALMASHAURI Mhe. Naibu Waziri, Katika mwaka wa fedha wa 2012/2013, hadi kufikia Novemba 2012, Halmashauri zetu zililkuwa zimekusanya jumla ya Sh.941,795,132.5 ikiwa ni makusanyo yake ya ndani sawa na asilimia 20.5 ya lengo la mwaka. Mchanganuo wa Mapato kwa kila Halmashauri ni kama inavyoonekena katika Jedwali namba 12 hapa chini.
Jedwali Na.12: MAPATO YA HALMASHAURI MKOANI RUKWA. HALMASHAURI MANISPAA YA SUMBAWANGA HALMASHAURI YA SUMBAWANGA MAKISIO 1,651,147,2 10 1,902,858,0 00 MAKUSANY O 433,166,507 350,779,748. 50 40 ASILIM IA 26 18

HALMASHAURI YA NKASI JUMLA

1,027,078,0 00 4,581,083, 210

157,828,877 941,775,13 2.5

15 20.5

25.1.2 UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO. Mhe.Naibu Waziri, Katika mwaka wa fedha 2011/2012 Halmashauri zilitengewa jumla ya Sh.27,969,707,000/= ambapo hadi Juni 2012 fedha zilizopokelewa ni Sh.24,049,435,915.86/= sawa na asilimia 86 tu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Aidha kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Halmashauri zilitengewa jumla ya Sh.14,276,905,000/= ambapo hadi Novemba 2012, fedha zilizopokele- wa ni Sh.6,637,374,275/= sawa na asilimia 46 ya lengo la mwaka. Mchanganuo wa utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo itapatikana katika Halmashauri husika wakati wa ziara. 25.1.3 Changamoto katika utekelezaji wa miradi Mhe.Naibu Waziri, Miradi ya maendeleo imekuwa ikitekelezwa kulingana na fedha zinavyopokelewa. Aidha, Halmashauri zinakabiliwa na changamoto zifuatazo; Kuchelewa kupata fedha kutoka Serikali Kuu. Ukosefu wa vipaumbele madhubuti katika bajeti zao. Uwepo wa miradi viporo mingi. Kukopwa kwa fedha za miradi ya maendeleo kwenda matumizi mengineyo. Usimamizi usio wa viwango wa miradi. Fedha kutoletwa kulingana na bajeti iliyoidhinishwa. Wakandarasi wengi kutokuwa waminifu katika kutekeleza miradi kwa viwango. 25.1.3. VIKAO VYA KISHERIA. Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zimeendelea kuendesha vikao vyao vya Kisheria kama kawaida japo kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 baadhi ya Halmashauri hazikufanya vikao vya kisheria kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha. 25.1.4. HALI YA WATUMISHI.
41

Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zote tatu za Mkoa wa Rukwa zinao Wakurugenzi. Aidha, kutokana na muundo mpya wa Vitengo na Idara za halmashauri ulivyo kwa sasa, nafasi nyingi za Wakuu wa Idara na Vitengo bado zinakaimiwa na ni jukumu la halmashauri husika kupendekeza na/ama kujaza nafasi zilizowazi kwa kutumia watumishi wenye sifa waliopo katika halmashauri ama kuomba kwa wizara husika. Kwa mfano jedwali Namba 13 hapo chini linaainisha mahitaji ya wakuu wa idara na vitengo:
Jedwali Na 13: MAHITAJI YA WAKUU WA IDARA KATIKA HALMASHAURI N o. 1. Jina La Nafasi Halmashau Zilizojazwa ri Manispaa ya Idara nane (8) Sumbawang za zamani na a kitengo kimoja cha ukaguzi wa ndani Halmashauri ya Sumbawang a Nafasi saba (7) idara za zamani zimejazwa. Nafasi Zinazokaimiwa Nafasi 5 (tano) vitengo vipya. Nafasi 2 (mbili) za idara mpya na nafasi 3 (tatu) idara za zamani Nafasi 4 (nne) vitengo vopya na idara mpya 2 (mbili) Nafasi 4 (nne) idara za zamani. Vitengo vitano (5) vipya Idara mpya mbili (2) na idara nne (4) za zamani Hatua zilizochuku liwa. Mchakato wa kuteua watumishi kukaimu nafasi mpya unaendelea. Wameteuwa watumishi wenye sifa kukaimu nafasi mpya unaendelea. Mchakato wa kuteua watumishi wenye sifa kukaimu nafasi mpya unaendelea

2.

3.

Halmashauri Idara tisa (9) ya Nkasi na kitengo kimoja cha ukaguzi wa ndani.

Aidha kwa upande wa watumishi, halmashauri zinakabiliwa na uhaba wa watumishi ambapo uhaba mkubwa unaonekena katika katika Sekta ya Afya na Elimu kama Jedwali Namba 14 linavyoonyesha hapa chini.
Jedwali Na 14: MAHITAJI YA WATUMISHI. No . 1. Jina La Halmashauri Manispaa ya Sumbawanga 42 Watumishi waliopo Mahitaji Upungufu ya wa watumishi watumishi 1,876 2,550 713

2. 3.

Halmashauri ya Sumbawanga Halmashauri ya Nkasi

3,663 491

6,114 701

2,451 210

26.0 HOJA ZA UKAGUZI. Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zimeendelea kujibu hoja za ukaguzi za ndani na nje za mwaka 2009/2010 hadi 2010/2011 hii inalenga pia kuboresha hali ya usimamizi wa matumizi ya fedha. Kwa mwaka wa fedha 2010/2011 Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga zilipata hati safi na Hati ya mashaka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Kutokana na ripoti hiyo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa umekwisha chukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha hoja hazijitokezi, mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika Dodoma, pia Katibu Tawala Mkoa pamoja na wataalam wake kuzitembelea Halmashauri zote tatu (3) na kufanya nao vikao kwa ajili ya kuhakikisha hoja zinajibiwa kwa wakati na kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia Mkaguzi Mkazi aliyepo Rukwa.
26.1. AINA YA HATI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU (2008/09 -

2010/2011 Jedwali Na 15: HATI ZA UKAGUZI KATIKA HALMASHAURI. Na


HALMASHAURI 2008/2009 2009/1010 2010/20 11

1. Manispaa Sumbawanga 2. Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga 3. Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Hati ya mashaka Hati safi Hati safi

Hati ya mashaka Hati ya mashaka Hati ya mashaka

Hati safi Hati safi Hati ya mashak a.

26.2

MUHTASARI WA HOJA KATIKA HALMASHAURI KWA MIAKA 2008/09 43

2010/2011.

Jedwali Na 16: MUHTASARI WA HOJA.


S/ N HOJA SWANG A MC SWANG A DC NKASI DC

1. 2. 3. 4. 5.

CAG Audit Queries 2010/2011 Current year Management Queries Management previous ordinary queries Management previous project queries Maelekezo ya LAAC JUMLA

6 27 26 5 10 74

7 21 15 3 23 69

3 24 1 8 11 47

Katika hoja zilizohojiwa kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zilisababishwa na mambo yafuatayo (mapungufu): Kutopatikana fedha kwa wakati (fedha za miradi ya maendeleo).

Kutokamilika kwa miradi ya maendeleo. Kutokuwa na tathmini halisi ya fedha inayotakiwa katika gharama za miradi.

Suala la kazi na thamani halisi (value for money) kwa shughuli nyingi zilizofanyika. Udhaifu katika utekelezaji/usimamizi. Katibu Tawala Mkoa ameweka mikakati ya kuhakikisha hoja hizo hazijitokezi tena na hasa kwa kudhibiti visababishi ambavyo vimeainishwa hapo juu kwa kufanya yafuatayo: Kukamilisha miradi yote viporo (Mkoa na Halmashauri zake zote). Kuomba Serikali ilete fedha kwa wakati (kabla ya kuisha mwaka wa fedha)
44

Kila Halmashauri kutokuanza miradi mipya. Kutoa Elimu kwa wanasiasa wanaozuia wananchi kushiriki katika utekelezaji/kuchangia miradi ya maendeleo. Kuimarisha miundombinu ya barabara ili kufikisha vifaa katika maeneo ya miradi. Kuwa na wataalam wa kutosha na wenye weledi katika fani za IT, ukaguzi na manunuzi.

Kuandaa na kufuatilia miongozo ya fedha inayotolewa na Wizara mama, Wizara ya fedha na uchumi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.

Aidha Halmashauri wamejibu hoja zote za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa hoja hizi hazijitokezi tena. Majibu ya hoja hizo yamekabidhiwa kwa Mkaguzi Mkazi wa Rukwa kwa ajili ya hatua zaidi za utekelezaji. 27.0. MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA Mhe.Naibu Waziri, Elimu imetolewa kupitia vipindi vya redio mara tatu, machapisho (1325), Semina kumi na mbili (12), mikutano ya hadhara thelathini (30) na vilabu vya wapinga rushwa Mashuleni sitini na mbili (62). Aidha, TAKUKURU pia imeendelea kuchunguza makosa ya rushwa hasa katika pembejeo za kilimo ambapo kati ya Julai 2011 hadi Januari 2012 kesi za pembejeo zipatazo (12) zimefunguliwa mahakamani ambapo washitakiwa wapatao thelathini (30) wakiwemo mawakala na watendaji wa Serikali wamefikishwa mahakamani. 28.0. HALI YA MAGEREZA MKOANI Mkoa wa Rukwa una magereza matatu ambayo ni Gereza Mollo, Mahabusu Sumbawanga, na Kitete.
(i)

Magereza ya Kilimo na Mifugo:


45

Kilimo kina fanyika katika magereza ya Mollo, na Kitete yenye ukubwa wa ekari 37790.5, kati ya hizo ekari 16,365 zinafaa kwa kilimo, ekari 21,425.5 zinafaa kwa malisho. Eneo linalolimwa na magereza yetu yana ukubwa wa hekta 371.2 na jumla ya mifugo inayofugwa ni 350 ikihusisha Ngombe, Mbuzi na Nguruwe. (ii) Magereza ya Mahabusu Mkoa una gereza moja la Mahabusu la Sumbawanga lenye uwezo wa kuhifadhi wahalifu 108. Kwa sasa linahifadhi wahalifu/wafungwa mpaka 368.

28.0. CHANGAMOTO: Ukosefu wa jengo la Ofisi ya Gereza la Mkoa kwani inayotumika sasa ni nyumba ya mtumishi na mabanda yaliyoongezwa kwa muda. Ukosefu wa gereza la mahabusu wilaya ya Nkasi. 29.0. USALAMA WA RAIA: Kumekuwepo na ongezeko la makosa na uhalifu kama vile mauaji kwa imani za ushirikina, unyanganyi wa kutumia nguvu, kuchoma nyumba moto na uvunjaji kuongezeka. 29.1. MAFANIKIO: Juhudi za Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu tumefanikiwa kupunguza mauaji ya vikongwe wanaotuhumiwa kwa imani za kishirikina, jakapokuwa katika takwimu zetu zinaonesha kuwa mauaji yamezidi, sio kwa vikongwe ni kwa rika mbali mbali hasa umri wa kati ya miaka 40 hadi 50. 29.2.
a) TATIZO

CHANGAMOTO:

LA ARDHI: wananchi wengi vijijini wanauana kugombea mashamba. b) MIFUGO: Ongezeko la mifugo vijijini imekuwa ni chanzo cha migogoro kati ya wakulima na wafugaji. c) MATUKIO YA KUCHOMA NA KUBOMOLEANA NYUMBA:

46

Baada ya mavuno wananchi huchomeana nyumba kwa kisingizio cha imani za kishirikina.

na

kuboleana

30.0. MASUALA YA UHAMIAJI: Mkoa ulibaini kuwa na wahamiaji haramu elfu kumi na nne mia nne thelathini na tatu (14,433) kutoka Congo DRC, Burundi, Zambia na Rwanda. 30.1. MAFANIKIO: Wahamiaji haramu 255 wamekamatwa kwa mwaka 2011, wengine walipelekwa Mahakamani wengine walifungwa na wengine 172 walipewa hati ya kufukuzwa nchini (PI. NOTICE). 30.2. CHANGAMOTO: Vituo vya mipakani ukiondoa kituo cha Kasesya havina majengo ya Ofisi. Suala la usafiri ni tatizo kwa vituo vyote. 31.0. ULINZI WA MGAMBO: Mkoa huendesha mafunzo ya Mgambo kila mwaka, lengo la mwaka uliopita lilikuwa ni kutoa mafunzo ya Mgambo kwa wanamgambo 600, mafunzo yalianza Julai, 2011. Mafunzo yalitolewa katika vituo vinne (4) ambapo washiriki 596 walianza mafunzo na waliohitimu ni 420 na kufanya Mkoa wetu kuwa na jumla ya wanamgambo 15,155. 32.0. SENSA YA WATU NA MAKAZI, PAMOJA NA KATIBA. Mhe. Naibu Waziri, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya watu na makazi nchi nzima ifikapo tarehe 26/8/2012, ambapo maandalizi ya zoezi hili yapo katika hatua mbali mbali, ikiwemo: Kutenga maeneo madogo madogo (EA) ya kuhesabia watu, mafunzo ngazi ya Taifa (TOT) mafunzo ya ngazi ya Mkoa, mafunzo ngazi ya Tarafa, nyaraka mbali mbali za Sensa pamoja na fedha kwa ajili ya kuendesha zoezi la Sensa. Viongozi wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya na viongozi wa dini wameendelea kuhamasisha shughuli za Sensa na Katiba katika ngazi zote.
32.1.

Maeneo ya Kuhesabia.
47

Jumla ya maeneo madogo madogo 2986 kwa mkoa mzima wa Rukwa yametengwa kwa mchanganuo ufuatao: Nkasi 855, Manispaa ya Sumbawanga 210, Halmashauri ya Sumbawanga 800 na Kalambo 621. Kama sehemu ya maandalizi ya Sensa mkoa uliendesha mafunzo ngazi ya mkoa kuanzia tarehe 17/07/2012 hadi tarehe 28/07/2012, ambapo waliofunzwa ngazi hii ya mkoa wamekwenda kuwafunza wasimamizi na makarani ngazi ya tarafa, mafunzo haya yalihusisha makundi yafuatayo: 1. Maafisa Elimu Kata zote 64 za mkoa wa Rukwa 2. Maafisa maendeleo ya jamii, Halmashauri zote 3. Maafisa Afya toka kila Halmashauri 4. Maafisa ardhi toka kila Halmashauri 5. Maafisa Kilimo toka kila Halmashauri 6. Maafisa Elimu toka kila Halmashauri 7. Maafisa toka Wizara ya Mambo ya ndani 8. Maafisa toka Ofsi ya Mkuu wa Mkoa 9. Wawakilishi wa walemavu. Baada ya kukamilika mafunzo ngazi ya Mkoa yalifuatia mafunzo mengine ngazi ya Tarafa kuanzia tarehe 09/8/2012 hadi 19/8/2012, ambapo katika ngazi hii makarani na wasimamizi wa Sensa waliweza kufunzwa namna ya kwenda kukusanya taarifa hizi za sensa kwenye maeneo yaliyopangiwa. Makarani/wasimamizi walipatikana kupitia taratibu zote zilizoelekezwa na Serikali, ambapo walimu na watu wengine wasio walimu waliweza kupata nafasi za kuwa makarani wa Sensa. 32.2. VIFAA NA NYARAKA ZINGINE ZA SENSA Vifaa na nyaraka zingine za Sensa toka Kituo cha Vifaa kilichopoo Kibaha - Pwani zililetwa mikoani kwetu japo baadhi ya vifaa vililetwa kwa kuchelewa katika hatua ya mafunzo. 32.3. FEDHA: Fedha kwa ajili ya mafunzo ngazi zote mbili (2) Mkoa na Wilaya/Tarafa pamoja na mafunzo ya madiwani zililetwa kupitia Hazina ndogo Rukwa na kuzigawa kwenye Halmashauri husika kwa kuzingatia mgawanyo wa bajeti.
48

32.4. CHANGAMOTO: Pamoja na kuwa Sensa ilifanyika vizuri, lakini kulikuwa na changamoto nyingi zifuatazo; Kuchelewa kupata fedha za kujikimu na mambo mengine siku za mwanzo za mafunzo katika hatua zote mbili za (Mkoa na Tarafa). Baadhi ya vifaa vya mafunzo kuchelewa kuletwa mkoani ikiwemo Ramani na bags za kutunzia vifaa na nyaraka zingine. Upungufu wa vyumba vya kulala (ngazi ya Tarafa) na hivyo wengine kulazimika kulala madarasani. Kutopata maeneo ya kuaminika (usalama wa chakula) kwenye baadhi ya maeneo/vituo vya mafunzo ngazi ya Tarafa. Upungufu wa madawati kwenye baadhi ya vituo vya kufundishia (ngazi ya Tarafa). Halmashauri zetu kutokuwa na fedha za kutosha kukabiliana na maagizo toka HQ Dar es Salaam ya kugharamia/kuwapa fedha za kuendesha zoezi la Sensa jambo ambalo halikuwa jukumu letu. Uhaba wa magari Mkoani/Wilayani. Baadhi ya vifaa kutoletwa kabisa (Calculators, Sale za kuvaa n.k.) 32.5 Namna zilivyotatuliwa baadhi ya changamoto: Washiriki waliamua kununua magodoro/mikeka ya kulalia na hivyo kulazimika kulala madarasani. Madawati yalibebwa kwa gharama nafuu kutoka maeneo ya karibu kwenda vituo vya mafunzo. 33.0. HITIMISHO Mhe. Naibu Waziri, Napenda kuchukua fursa hii kwa mara nyingine tena kukukaribisha Mkoani kwetu wewe na ujumbe wako nawatakia afya njema na kila la kheri katika kipindi chote cha ziara yako Mkoani Rukwa. Tupo tayari kutekeleza yote utakayotuagiza na kutuelekeza katika kipindi chote utakachokuwa pamoja nasi.
49

KARIBU SANA

50

You might also like