MAFISADI WA MUZIKI Walio wengi wamezoea kusikia ufisidi katika siasi, viongozi waliokua na uuzo wa tabia na kujilimbikizia mali

chungu nzima. Ufisadi hauishii kwenye siasa tu bali kuna ufisadi kila sehemu, kwenye kazi, mashirika binafsi, michezo na hata katika tasnia ya muziki. Ufisidi katika tasnia ya muziki upo, tena mkumbwa na si rahisi kuusikia wala kuuona hata ukiwa msaani. Swala hili la ufisadi katika muziki tumekuwa tukilifatilia kwa muda sasa kama wadau wamuziki na tumefanya uchanguzi wa kina sana kwa kuongea na watu tafauti tafauti katika mziki, wasanii, maproducer, ma presenters, ma dj na wadau wa mziki. Tumekua tukisikia malalamiko mengi sana ya wasanii hivi karibuni kwanini nyimbo hazipingwi? Kwanini hawapati show? Na maudhi mengine mengi. Hivi sababu nini hasa ? Nyimbo zao ni mbaya? Hawana vipaji au? wasanii kama chidi benz, lady jd, ali kiba, bushoke, prof jay, matonya, makamua, qchief, TID, na wengine wengi. Kuna jambo hapa japo kua wengi hawataki kulizungumzia kwa kuogopa au labda kwa ufahamu mdogo. Nyuma ya yote haya kuna mafisadi, hawa ni watu ambao wanaupeleka mziki wanavyotaka wao kwa kujifanya kama wao ndio wamiliki wa huo mziki na kutumia nafasi zao za kazi vibaya kwa manufaa yao binafisi bila kujali mustakabali wa tasnia ya muziki. Kuna kijikampuni kinaitwa OSATA ambacho kazi yake kubwa ni promotion, publishing na usimamizi wa wasanii tafauti tafauti kwa njia ya mikataba mifupi mifupi. Wamiliki wa kampuni hiyo ni Babu tale, said fela na suka othumani suka, OSATA ni ufupisho wa majina haya matatu. Herufi O katika OSATA ni Othuman suka ambaye ni mfanyakazi wa cloudfm kwenye upande wa kusikiliza /kuhakiki nyimbo za wasanii na kuzipitisha kabla ya kupigwa.

Na herufi SA katika OSATA ni said fela ambaya ni meneja wa kundi la Tmk Wanaume family ,

Herufi za mwisho TA katika OSATA ni Tale ambaye pia ni manage wa kundi la Tip Top connection.

Kazi kubwa ya kampuni hii ni kusambaza muziki kwenye redio, television, mitandao ya jamii na sehemu nyingine nyingi. Kampuni hiyo haiishi kwenye kusambaza tu bali inafanya promotion ya hizo kazi walizosambaza kwa kutumia pesa au lugha nyingine fasaha rushwa. Rushwa kwa maana kuwapa mapresenter na madj wa redio tafauti tafauti pesa kupiga hizi nyimbo wanazozipromote. Katika uchunguzi wetu kampuni hiyo inamtoza msanii kiasi cha shilling mil 3 kusambaza na kufanya promotion ya nyimbo. Kwa haraka haraka unaweza kusema hakuna tatizo, OSATA inafanya biashara tu na hakuna ofisadi wowote ule unaendelea. Katika shughuli hizi za promotion ya nyimbo katika redio na television, OSATA huwalipa madj na wafanyakazi wa media kupiga kazi zao na pia kuwashawishi kutokupiga kazi za watu wengine ili wapate wateja wengi katika kampuni yao.

OSATA inamtandao wa wanahabari nchi nzima, wafanya kazi hawa wa redio na television hulipwa ilikupiga video na nyimbo zaidi ya kawaida. Tatizo linakuja pale ambapo nyimbo mbaya inapewa nafasi na nyimbo bora haipigwi kabisa kwasababu OSATA imelipia promotion kabambe. Kibaya zaidi ni pale mfanyakazi wa redio anapokua ni mmoja wa miliki wa kampuni ya usambazaji ambae ni Suka Othumani suka, unafikiri kutakua na haki kweli kwenye upangiliji wa nyimbo kwenye ratiba ya redio? Unafikiri nyimbo yako itapita kweli kama hujalipa kwa OSATA ili ufanyiwe promotion? Sanaa inakuwa vipi kwa hali hii? Lazima msanii alalamike kwa hali hii kwababu huwezi kupata show bila muziki wako kusikika. Huwezi kuendesha maisha kama hupati angalau show moja katika mwezi, unaposikia msanii kaingia katika madawa ya kulevya msimcheke tu bali kuna mambo mengi katika muziki yanachangia kumpoteza msanii na hili ni moja wapo. Operesheni za OSATA zinaendeshwe kisiri siri sana na wamiliki wanaotambulika ni babu tale na saidi fella, huku wakimtaje othumani wakijuafika jina hilo halitambuliki kwenye umma. Angalia interview hii kwenye youtube ya kipindi cha sporah babu tale akimtaja othumani na saidi fella

http://www.youtube.com/watch?v=uTgt_lRNQBE dakika 17 sekunde 40. Katika interview hiyo babu tale anaizungumzia OSATA jinsi invyofanya kazi na redio/TV.

Jina hili la othumani limetumika ili isijulikane kuwa huyo mtu ni suka othumani suka ambaye ni huyu hapa katika facebook account http://www.facebook.com/suka99

Osata inatumia nyundombinu za clouds FM na Television kufanya promotion hizo za mziki kupitia mgongo wa suka . Mikutano ya OSATA hufanyika THT (Tanzania House of Talent) na office za cloudfm, ukifatilia kwa karibu unaweza ukadhani OSATA ni operesheni ya redio hiyo, mameneja hao hujichanganya kama wafanyakazi ukiwaona unaweza usiwatafautishe na wafanya kazi cloudsfm.

Sisi kama wadau wa muziki baada ya kufanya uchunguzi wa kina tunaamini kabisa hii ni kazi ya ruge mutahaba baada ya kuona Tanzania fleva Unit imefeli na kujiondoa katika picha mbaya katika

tasnia ya muziki. Osata nikama chombo ambacho kinatumika tu na THT/Ruge Mutahaba kucontrol muziki na media nyingine kwa ajili ya manufaa yake binafsi. Kila show utakayoenda lazima umkute, mwasiti, linah, barnaba, chege, made, tundaman, n.k – haimanishi kua hawa ni wasanii bora Tanzania bali ndio wanaosambaziwa kazi zao na hili kundi la mafisadi. Akitokea mtu mwingine anayejifanya anasambaza na kufanya promotion anazimwa haraka sana kwa fitna na mipango ya osata. Osata imefika mpaka mmalaka ya kuwaambia ma presenter wasipinge nyimbo ya baadhi ya wasaanii hapa nchini kwa lengo la kuwapoteza ili waende kulipia promo. Kila mtu analia kivyake ila hamna mtu anayetaka kuongelea ukweli kwa kuuogopa ,Osata, ruge, THT and Cloudfm. Hii media house ilipata stress kubwa sana kipindi cha Bwana Sugu na Anti-virus, kulikua hamna amani mjengoni hata mahudhurio ya matamasha hayakua mazuri. Kwa kutumia njia zake za kifisadi ruge mutahaba akaweza kuuzima moto- akaihusisha serikali kwa kumpeleka sugu bungeni ili wapate suluhisho, kumbumbukeni mnachezea maisha ya watu, mnaharibu kazi za watu, kujifanya nyie ndio wamiliki wa muziki mtakuja kuumbuka vibaya sana mbele ya haki. Hii tahadhari kwa vituo vya redio, television, magezeti na vyombo vya habari vyote kuwa kuna ofisadi unaendelea, hili hundi na washiriki wake wanatumia pesa kuendesha vyombo vyenu. Fanya uchunguzi wako binafsi utaona mwenyewe, kabla ya matamasha makubwa utaona video na nyimbo flani za wasanii flani zinapigwa kweli na ndio hao hao utawakuta kwenye matamasha. Osata, ruge, cloudsfm na tht nia yao ni kuucontrol muziki. Sisi kama wadau wa muziki tunasema haiwekani kabisa. Huu ni ufunio wa kwanza tu tunaendelea na uchunguzi, kuna nyaraka nyingi zinakuja na tutaziwakilisha kwa jamii zikiwe zimeambatana na interviews. Joseph Kusaga moto unaanza tena huu usije ukatoa lawama tena, hakuna atakayekusikiliza mara hii sababu unawaachia vijana wanafanya ufisadi kwenye ufalme wako. Kama ulikua hujui basi natumia umeujua ukweli. Shukrani.

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful