In The Name of Allah, the Magnificent, the Merciful Tanzania Muslim Professionals Association Magomeni Adjacent Kinondoni Municipal

Plot 169 Block R Morogoro Road, Kinondoni Dar es Salaam Email: amir@tampro.org tampro1997@yahoo.co.uk Web: www.tampro.org
7th July, 2013.

Press Statement
Ndugu wanahabari, Umoja wa Wataaluma wa Kiislamu Tanzania (Tanzania Muslim Professionals Association) Kila Mwaka unatumia nafasi ya kuukaribisha Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani kuwakutanisha wanataaluma mbali mbali kutoka Taasisi Mbali Mbali ili kujadili masuala ya Kitaifa na Kimataifa pamoja na kujifunza Miongozo ya Kiislamu (Quran & Hadith) juu ya jambo maalumu linalojadiliwa kwa Muongozo wa wanazuoni wa Kiislam pamoja na kuona mbinu mbali mbali za taaluma za fani zao mbali mbali zinawezaje kusaidia kuleta maendeleo katika taifa na Waislamu kwa ujumla. Ni lengo la Kongamano hili la kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani la Mwaka 2013 kuhamasisha udugu na Ushirikiano Miongoni mwa Wanataalum wa Kiislamu na pia kuwa sehemu ya msaada kwa wanazuoni wetu katika kusaidia kuangalia Masuala Mbali mbali ya Kijamii na Kiuchumi yanayoikabili jamii ya Watanzania hasa Waislam na jinsi gani Dini ya Kiislam inaelekeza juu ya kuleta suluhu na Maendeleo kwa jambo husika kupitia misingi Mikuu ya Uislam ambayo ni Quran na Sunnah za Mtume Muhammad (SAW). “Mwanamke ni Nguzo Kuu katika Mafanikio ya Jamii” au kwa Kiingereza “A WOMAN, the power behind Community Prosperity” ndio kauli mbiu ya WELCOMING RAMADHAN CONFERENCE ya Mwaka huu 2013. Hii imetokana na historia ya Uislam kwa Miaka Mingi kwa kupitia muongozo wa Mwenyezi Mungu (Qur’an) pamoja na Jinsi gani Mtume Muhammad (SAW) na Mitume yote iliyotangulia kabla yake wamekuwa wakisimamia haki na maendeleo kwa mwanawake wakiamini kuwa kumuendeleza mwanamke ni sawa kabisa na kuendeleza kizazi chote kwani bado mafundisho ya dini na maumbile ya Mwanamke aliyopewa na Muumba Wetu Kiasili yanamfanya awe mtu mwenye usimamizi wa karibu sana wa Maendeleo ya familia hususani vijana kuliko Mwanamume Kongamano hili limekubaliana na kuona kuwa wanawake waislam hasa wanataaluma wana majukumu makubwa sana katika jamii ya leo. Kwa hiyo bila ya kuwahamasisha na kuwafanya watambue umuhimu wao katika kujenga jamii bora yenye maadili na imani, Taifa linaweza kufika mahali ambapo linaongozwa na watu ambao wanajali maslahi binafsi, wasio na Imani na maadili mema ambayo yanaathiri mfumo mzima wa maendeleo ya Jamii, Kisiasa na Kiuchumi. Inawezekana kabisa mporomoko unaotokea sasa wa maadili ni athari za

In The Name of Allah, the Magnificent, the Merciful

kutomuhusisha vyema mwanamke katika sera na mipango ya kimaendeleo au kusahau majukumu makuu ya Mwanamke katika kujenga Jamii Imara na yenye taaluma na Maadili mema kama dini yetu ya Kiislam inavyotufundisha.Uislamu unaelekeza kuwa Mwanamume ndio Kiongozi mkuu wa Familia, lakini kiongozi lazima awe kuna nguzo zinazoshikilia uongozi wake, na moja ya nguzo kubwa katika kuleta jamii bora basi mwanamke amepewa jukumu la kuiangalia familia kwa karibu zaidi na hili hasa ndio linamfanya awe kinara na nguzo kuu ya mafanikio ndani ya jamii hasa akilelewa katika maadili bora ya kiislam. Pia Kongamano limeona kuwa Katika jamii zetu zinazotuzunguka kumekuwa na mambo mengi ya Kimila na Desturi hasa vijijini ambayo bado yanamkandamiza mwanamke. Jambo hili katika jamii za Kiislam zilizopo vijijini na hata hizi za mijini limekuwa kubwa na limechangiwa sana na uelewa mdogo wa dini ya Kiislamu ambayo kihistoria imekuwa ikimuweka mwanamke katika daraja la juu sana kama ilivyoelezwa katika Qur’an na Matendo ya Mtume Muhammad (SAW). Kwa hiyo Kongamano hili pia linawataka wanawake wanataaluma wa Kiislam kujiingiza kusoma zaidi dini na kuelewa haki na majukumu yao ndani ya Jamii na pindi wapatapo nafasi wawaelimishe wanawake wanzao ambao hawajapata nafasi ambazo Allah amewaruzuku wao. Kongamano hili la Ramadhani pia linawaomba wanaharakati mbali mbali ambao wamekuwa na mtazamo potofu juu ya Msimamo wa Uislam na nafasi ya Mwanamke ndani ya Jamii, kuanza kusoma dini ya Kiislamu kwa undani na kuelewa kabla hawaja toa matamko ambayo mengi yamekuwa ya kupotosha Mafundisho halisi ya Uislam na mara nyingi yamepelekea kuiangamiza jamii katika vitendo viovu zaidi kuliko mitazamo yao finyu ya kibinaadamu ambayo kamwe haiwezi kushinda mipango ya Mungu aliyetuumba. Ukitaka kutofautisha Uislam na Muislam lazima usome Uislam kwanza ambao unapatikana katika Qur’an na Hadith halafu ndio unaweza kuzungumza vizuri juu ya nafasi ya mwanamke katika nyanja mbali mbali za kijamii na si kuanza kuchanganya Uislam na mila na tamaduni za maeneo ambayo wakazi wake wengi ni waislam. Ni vyema wanaharakati wakasoma Uislam unafundisha nini juu ya Mirathi, Ndoa na Umiliki mali na kuona jinsi gani na nafasi gani Mwanamke Uislam unamuweka katika kusimamia mambo haya ambayo mara nyingi tumesikia ndio wimbo mkubwa wa wanaharakati juu ya Uislam. Kongomano la Kukaribisha Ramadhani limekuwa likifanyika Kila Mwaka Katika Jumapili ya Mwisho ya Mwezi wa Shaaban na kwa kipindi cha Miaka Mitano mfululizo kongamano limefanikiwa kujadili na kupata majawabu ya masuala mbali mbali yaliyokuwa kama Kauli Mbiu ya kila Mwaka kama vile “Kufuta Umasikini kupitia Zakah na Sadaqah”, “Nafasi ya Elimu katika Kuleta Maendeleo ya Jamii”, “Athari za Vyombo vya habari katika Jamii pamoja” na “Mifumo ya Benki za Kiislam” Kwa hiyo Kongamano la Kukaribisha Ramadhani la Mwaka 2013, limefanikiwa kuonyesha jinsi gani Mwanamke wa Kiislam amepewa majukumu makubwa

In The Name of Allah, the Magnificent, the Merciful

kusukuma jamii katika nyanja mbali mbali kiimani, Kimaadili pamoja na Kiuchumi na kuyumba au kutomuhusisha Mwanamke katika Mikakati ya Kimaendeleo na athari katika nyanja mbali mbali za kijamii na kiuchumi. Kongamano hili limekuwa likifanyika kwa kipindi chote hicho kwa Udhamini mkubwa wa Banki ya Kiislamu ya Amana (AMANA BANKI) ikishirikiana na INOCH LTD, ,ID PRESS, Nestle NIDO na PROSMS. Kongamano hili linategemea kuwa kama ukumbusho kwa Wataaluma wote wa kiislamu juu ya kuendelea kumthamini Mwanamke na Kumuendeleza ili kujenga jamii bora ya Kiislamu inayofuata maadili bora na sahihi ambayo italeta athari kwa maendeleo ya Taifa pia litakuwa ni chachu kuwakumbusha kutosahau kutekeleza majukumu yao ya Kiimani katika kipindi chao chote cha maisha na kushirikiana na wanazuoni wetu ambao muda mwingi wanakuwa katika wakati mgumu kuendeleza jamii kiroho. Wanataaluma wa Kiislam pamoja na Wanazuoni wa Kiislam kwa pamoja tunawatakia waislamu wote na Watanzania kwa Ujumla Mfungo Mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1434H. Napenda kuwashukuru wanahabari wote kwa kuhudhuria na uhusiano ambao mmekuwa mkionyesha siku zote na pia kuwahusia kuendelea kuelezea picha nzuri juu ya Uislam na waislam ili kudumisha mshikamano na Umoja wa Taifa. Inshaallah Mwenyezi awafanyie wepezi katika kusukuma Mbele Nchi yetu Tanzania. Ahsanteni kwa kunisikiliza na tuwasiliane kwa anuani ziizotajwa. Karibuni tena

Mussa Mziya Mwenyekiti Umoja wa Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania – Tanzania Muslim Professionals Association (TAMPRO) +255 754 261 600

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful