Professional Documents
Culture Documents
Makala Maalum
Mimi ni Mansoor Yussuf Himd
JAMVI LA BARAKA
>
>
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walitaja upotevu wa fedha kutokana na usajili wa meli za kigeni ambapo mapato yanayotokana na uwakala wa kampuni ya Philtex ya Dubai, inayosajili meli za kimataifa, hayakuwa wazi.
> Yaliomo
04 08 10 12 17
2
Ufisadi waila SUK Ili Zanzibar iendelee itilie mkazo ICT Kutoka Magazetini Makala Maalum Ngurumo la Mkama Ndume Matusi ya Komba Wapya wa CCM Jamvi la Baraka Bado Mansoor anao uhai wa kisiasa Kauli ya Mwinyi Mkuu Mkeka wa Mwana wa Mwana Wanafacebook wasemavyo Uhafidhina wa Kisiwandui, Ukoloni wa Dodoma Ladha ya Beti Tufungue kitabu Hivi ndivyo Kriketi ichezavyo
08
10
19 24 28 32 44
Tartiiib, CCM bye bye
16
36 38 40 48 50 53
58
60
Mhariri
Ahmed Rajab
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
Kulindana
Kwingi
N A M AUA M O H A M M E D
anzibar ina safari ndefu ya kwenda kabla ya kuwa nchi iliyostawi kiuchumi kwa vile mfumo wake wa kiutendaji umebomoka kabisa, licha ya kuongozwa na serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa. Uchunguzi uliofanywa na Zanzibar Daima Online katika taasisi mbalimbali za serikali pamoja na mitaani, umegundua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoundwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) inakabiliwa na ufisadi wa kutupwa. Ubaya zaidi ni kuwa kunakosekana hatua zozote za kinidhamu dhidi ya wanaohusika ambao baadhi ya wakati wakiwa wanajulikana hata na watu walio nje ya taasisi hizo. Miongoni mwa taasisi zilizotajwa kuoza kwa ufisadi ni zile zinazotegemewa kuendesha uchumi kama vile bandari, viwanja vya ndege na utalii. Baraza la Wawakilishi lililoahirisha vikao vyake mwezi uliopita lilimalizika kwa shutuma za wazi za ufisadi serikalini uliobuliwa na Wawakilishi kadhaa. Lakini Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, analaumiwa kuwa alihitimisha hotuba yake ya kuliahirisha Baraza hilo kwa kukemea kufichuliwa huko kwa ubadhir-
ifu wa fedha za umma, akitishia kutumia sheria inayolinda siri za Serikali dhidi ya utolewaji wa taarifa kama hizo. Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa, Balozi Iddi alihoji kwamba ni kosa la jinai kutumia hoja za siri za Serikali kuibua maovu Serikalini. Ni mtu huyu huyu juzi tu aliliambia Baraza kwamba eti yeye anachukia rushwa na wizi Serikalini na kwamba hawezi kuvimilia vitendo hivyo. Leo anakuja na vitisho kwa wale wanaofichua uovu huo, alisema Jussa akiongeza kwamba ikiwa walioko Serikalini hawapendi kufichuliwa uovu, wizi na ufisadi unaofanyika basi waache uovu, wizi na ufisadi huo. Zanzibar Daima Online imefahamishwa na vyanzo kadhaa vya habari ndani na nje ya Serikali kwamba kiwango cha kulindana bado ni kikubwa ndani ya mamlaka zinazohusika na usimamizi na uendeshaji Serikali, kiasi ya kwamba uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa haujabadilisha kabisa utamaduni wa kula na kusaza. Lakini Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Rashid Seif, amemuambia mwandishi wetu kwamba tuhuma za ufisadi zinazotajwa kuiandama Serikali yake ni mambo ya kikawaida ya
Mtandao wa E Government unashukiwa kula fedha nying kuliko kazi iliofanywa. Mradi wa wa uwanja wa Ndege Zanzibar umefeli baada ya zaidi ya dola 60 za mkopo kuingizwa humo. Mradi wa mkonga wa taifa umegharimu dola milioni 19 na Wawakilishi wanataka tume iundwe.
Miongoni mwa taasisi zilizotajwa kuoza kwa ufisadi ni zile zinazotegemewa kuendesha uchumi kama vile bandari, viwanja vya ndege na utalii
kikazi ambayo yamekuwa yakishughulikiwa ipasavyo. Hakuna pahala pasipokuwa na mapungufu. Sio sahihi kusema hakuna ushughulikiaji. Mambo yanatekelezwa kama ilivyo kawaida, alisema Waziri huyo anayetokea CUF, chama ambacho kimekuwa kikipingana na ufisadi tangu kilipokuwa kwenye upinzani. Rashid alisema si jukumu la wizara kudhibiti ubadhirifu kama upo, bali kwa mujibu wa taratibu za nchi kuna chombo maalum kinaitwa CAG (Chief Auditor Gen-
eral, mdhibiti mkuu na mkaguzi wa mali za Serikali). Hicho ndicho chombo kinachoshughulikia udhibiti wa mali za Serikali. Kama wao (Wawakilishi) wameona kuna ripoti iliyosema (pametokea ubadhirifu) halafu wizara haikuchukua hatua, ndio ilikuwa waseme. Lakini tuliwaambia haya mambo hayako tena. Kama yalifanyika, ilikuwa hapo nyuma. Tokea mamlaka iundwe, kila kitu kiko kwenye order (sawasawa). Hata hivyo, uchunguzi wa Zanzibar DaiWWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
>
ma Online umegundua kwamba ubadhirifu na ufisadi Serikalini unachochewa sana na watendaji wakuu, wakiwemo makatibu na wakurugenzi, na hasa kwa misingi ya siasa. Ali Nassor Ali, mfanyabiashara kisiwani Unguja, aliliambia jarida hili kwamba kuna mifano mingi ambapo makatibu wanakosa kuwajibika kwa mawaziri wao kwa kuwa hawakuteuliwa na mawaziri hao bali (wameteuliwa na) Rais. Kwa vile katibu mkuu huyo na mkurugenzi haoni sababu yoyote ya kuwajibika kwa waziri kwani hana uwezo wa kumfuta kazi, hasa kwa kuwa waziri anayehusika hayuko mrengo mmoja (wa kisiasa) na Rais inakuwa vigumu kwa katibu mkuu au mkurugenzi kusikiliza amri ya waziri huyo.
Mapinduzi iliyokuwa ikiongozwa na Dk Mwinyihaji Makame Mwadini; na Wizara ya nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora iliyokuwa chini ya Haji Omar Kheri. Dk Mwinyihaji sasa anaongoza wizara mpya ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora, na Haji Omar Kheri amepewa jukumu la kuongoza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum (vikosi). Wizara nyengine zilizopata mtikisiko ni Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais - Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo iliyokuwa ikiongozwa na Omar Yussuf Mzee; na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika chini ya Haroun Ali Suleiman.
Hii ni dhahir kuna ubababaishaji, hakuna utaratibu wa mapato hayo... imekuwa hayaeleweki na ripoti za fedha zinaashiria kuna upotevu mkubwa wa fedha, na meli zinaposajiliwa makubaliano, kwa mujibu wa maelekezo ya Shirika la Kimataifa la Usafiri katika Maji - International Maritime Organization (IMO), kila meli iliyosajiliwa inatakiwa itoe nafasi tano za ajira za ubaharia kwa nchi husika, je, hili linafanyika? alihoji Hamza Hassan Juma, Mwakilishi wa Kwamtipura (CCM).
zotumika ni fedha za mkopo zaidi ya dola za Marekani milioni 60. Mradi wa mkonga ambao haujakamilika umegharimu dola milioni 19 za Marekani (sawa na zaidi shilingi bilioni 31), wajumbe walitaka tume iundwe kuchunguza sakata hilo, lakini Spika wa Baraza na Serikali hawakuridhia.
Katika muundo mpya, Omar Yussuf Mzee Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, Zan- sasa ni Waziri wa Fedha; na Haroun Ali zibar haitapigahatua za maendeleo kwa Suleiman ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais kuwa siasa imewekwa mbele kuliko masla- Kazi na Utumishi wa Umma. hi ya nchi. Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Hivi karibuni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mo- Vijana, Wanawake, na Watoto, waziri wake hammed Shein alifanya mageuzi katika akiwa Zainab Mohammed Omar pia ilifumubaadhi ya wizara zake. Alizifumua wizara liwa na kuundwa upya. Baada ya kuundwa upya Mama Zainab sasa anaongoza wizara tano nyeti na kuziunda upya. mpya, kubwa, ya Ustawi wa Jamii, UwezesShein alifanya mabadiliko katika wizara haji wa Wananchi Kiuchumi, Maendeleo ya hizo, siku chache baada ya wajumbe wa Vijana, Wanawake, na Watoto. Baraza la Wawakilishi kutoa tuhuma kadhaa nzito za ufisadi katika wizara hizo, huku Ufisadi ulitajwa katika wizara na taasiwakitaka Serikali ichukue hatua za haraka si nyingi za serikali, lakini ufisadi mkubwa na kali dhidi ya watumishi wanaotuhumiwa umebainika katika Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, hasa Mamlaka ya Usafiri kufanya ufisadi. wa Baharini (Zanzibar Maritime Authority Baadhi ya watu wanasema kuwa Shein - ZMA), na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege amefanya mabadiliko ili kupunguza mianya (Zanzibar Airports Authority - ZAA). ya ufisadi, japo baadhi ya wengine wana mtizamo kuwa hakuna mabadiliko ya ku- Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walitaja shtua yaliyotokea kwa sababu mawaziri ni upotevu wa fedha kutokana na usajili wa meli za kigeni ambapo mapato yanayotowalewale, na watendaji ni walewale. kana na uwakala wa kampuni ya Philtex ya Wizara zilizofumuliwa ni Wizara ya Nchi Dubai, inayosajili meli za kimataifa, hayakuOfisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la wa wazi.
> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03
Spika alishauri tuhuma hizo zichunguzwe na Serikali, na Balozi Seif Ali Iddi ameahidi kufanya uchunguzi kubaini kama tuhuma ZMA, kupitia wakala wake Philtex, imeku- za ufisadi katika mradi wa mkonga ni za wa ikisajili meli tangu mwaka 2009, laki- kweli. ni nafasi za ubaharia hazionekani, wakati Katika mfululizo wa malalamiko ya ufisaZanzibar inakabiliwa na tatizo kubwa la di katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, waukosefu wa ajira kwa vijana. wakilishi pia walionyesha wasiwasi wao Hija Hassan Hija, Mwakilishi wa Kiwani kuhusu matumizi ya fedha katika miradi ya (CUF) pia alilalamika kuwepo kwa ukwe- ujenzi wa barabara, Unguja na Pemba. paji mkubwa wa ulipaji wa ushuru katika bandari ya Zanzibar akitoa mfano wa tuhuma kuwa makontena mia tatu hayalipiwi kila mwezi. Inatakiwa kwa kila kontena moja, ada ya Bandari ni [shilingi] elfu sitini (60), lakini ada hiyo imekuwa haionekani. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pia waliibua ufisadi katika mradi wa mkonga wa taifa ambao baada ya kukamilika, utawezesha taasisi za Serikali kuwa na mtandao wa mawasiliano. Mtandao wa kwanza unaolengwa ni kuziunganisha taasisi za serikali, E-Government, halafu baadaye itafuatiwa na mtandao wa afya E-Health, na mengineo, lakini Wawakilishi wametilia shaka kubwa kuwa fedha zilizotumika ni nyingi kuliko kazi iliyofanywa. Mradi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, umefeli na kukera wajumbe wengi wa Baraza la Wawakilishi ambao wamehoji kwa nini hali hiyo ikatokea na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali, wakati fedha ziliUkiangalia barabara nyingi visiwani humu zimesita, mfano ujenzi wa barabara za: Amani/Mtoni, na Wete-Gando-Wete-Chake, umesita bila sababu zinazoridhisha, alisema Mwakilishi mmoja. Pia matumizi ya pesa kwa ajili ya barabara sita za kusini Pemba yanatia shaka kwani, barabara hizo zimekosa viwango ambapo tokea zifunguliwe sasa ni mwaka mmoja tu lakini zimeshaanza kuharibika, kwa mujibu wa kumbukumbu za Baraza la Wawakilishi. Barabara hizo zilizinduliwa kwa sherehe za Mapinduzi lakini haijafika sherehe ya Mapinduzi nyingine barabara hizo tayari zimeshaanza kuchimbika hii ni kukosa viwango va ubora vya barabara. Na licha ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya ufisadi unaotokea Serikalini, wasiwasi mkubwa ni kwamba utamaduni wa kulindana na kudharauliana utaendelea kuitafuna sekta ya umma na ya binafsi visiwani Zanzibar kwa siku kadhaa zijazo.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
>
ARA nyingi, kama si zote, tunapokuwa tunazungumzia mustakbali wa nchi yetu, tunakuwa tunasisitiza sana juu ya vigezo vya maendeleo vinavyojikita kwenye siasa au uchumi. Ni nadra kuitupia macho elimu na hasa elimu ya mambo ya ufundi na hasa zaidi ile inayohusu teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT). Elimu hii imekuwa muhimu sana katika miaka ya hivi karibuni kote duniani na ushahidi unaonyesha kwamba zile nchi zilizoipa kipaumbele elimu hiyo zimepata mafanikio makubwa katika maendeleo yao ya kiuchumi na ya kijamii katika muda usio mrefu. Kwa kutoitia sana maanani elimu ya teknolojia ya mawasiliano tunakuwa tunajipunja wenyewe kwani elimu hiyo siku hizi ndiyo yenye kusakwa kote duniani kwa vile ni muhimu kwa maendeleo ya mataifa makubwa na madogo. Nchi kama yetu ina nafasi nzuri ya kunufanika kutokana na elimu aina hiyo. Tunaipata nafasi hiyo nzuri kwa sababu hatunayo elimu hiyo. Hatuwezi, kwa hivyo, kufanya makosa kama yanayofanywa na nchi zilizo na uzoefu wa elimu ya aina hiyo na zenye kutaka kujiendeleza katika nyanja hiyo.
zetu na fikra zetu ili tuwe na namna mpya ya kufikiri. Pili, itatubidi tuwe tayari kuyatumia maarifa tutayoyapata kwa ubia kwa manufaa yetu sote, bila ya kubaguana. Katika hili Serikali, bila ya shaka, ina dhima kubwa. Ninavyosikia ni kwamba Wizara ya Elimu inajitahidi kuwa na mfumo wa aina mpya wa elimu utaoweza kukuza uwezo wake wenyewe na wa walimu pamoja na wanafunzi wa kuitumia hiyo teknolojia ya mawasiliano. Pa kuanzia kwanza ni katika klasi, darasani. Wizara ya elimu inapaswa iwe na mkakati wa kuzifanya skuli ziwe na jukumu la kuwafanya Wazanzibari wawe na uwezo wa kuitumia teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT).
yetu. Hakuna asiyejua kwamba ikilinganishwa na nchi nyingine duniani hata baadhi ya zilizo barani Afrika Zanzibar imetupwa nyuma katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa kiwango kikubwa wa kulaumiwa ni sisi wenyewe.
Zamani tulijitupa wenyewe nyuma kwa Elimu ya watoto haihusiki na kusoma tu kutoipa elimu umuhimu unaostahiki. na kupata maksi nzuri klasini tu. Elimu Haitukhalis kukaa na kushika tama ni njia ya kuvumbua vitu vipya tusivyovi- huku tukilalamika na kuwahusudu wenzetu walioendelea. Tunaweza, tukitaka, jua na pia njia ya kuongeza maarifa
kuwafukuzia na kuwapata. Lakini tutahitaji kwanza tuwe na moyo, ari na dhamira ya kukubali kwamba hatuna njia ya kuwafikia wenzetu ila kukamia kuipata elimu Haitoshelezi kwamba wenye kujifunza hiyo ya teknolojia ya mawasiliano. kuhusu matumizi ya ICT wawe na uwezo Ni rahisi bila ya shaka kukaa na kusema wa kujua namna ya kuitumia tu teknolojia tunataka hiki na tunataka kile. Ni vigumu hiyo. Watahitaji pia wawe na uwezo wa kuandaa mkakati utaobadili namna tukujua namna ya kuisarif hiyo teknolojia na livyozoea kufikiri na tukazibirua fikra zetu. pia waidhibiti vilivyo lugha ya teknolojia hiyo. Itatubidi kwanza tuwe na mpango wa kuitumia elimu hiyo kwa kuzipindua akili Hiyo si kazi ndogo kwa sababu kila uchao
Inaendelea Uk.27
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
KUTOKA MAGAZETINI
gazeti la Mwananchi siku ya Jumatano (tarehe 4 Septemba) Sheikh Khalid amefikishwa hospitalini hapo kufuatia kuugua ghafla na ugonjwa ambao hadi sasa haujabainishwa wazi na madaktari wanaomshughulikia. Kamishna wa Magereza Zanzibar, Khalifa Hassan, alibainisha kuwa huko nyuma Sheikh Khalid Azzan alishawahi kuumwa wakati akiendelea kusota katika gereza la Kiinua Miguu, lililopo kando kidogo ya kitovu cha Unguja Mjini. Wakili wa viongozi hao wanaokabiliwa na
>
dege ya Shirika la Ndege la Oman (Omanair) iliigonga ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) iliyokuwa imeegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aman Abeid Karume mjini Zanzibar siku ya Jumatatu (tarehe 2 Septemba) wakati ndege hiyo ilipokuwa inaanza safari yake kuelekea Dae es Salaam, liliripoti gazeti la Mwananchi siku ya Jumanne. Ndege hiyo ya Omanair iliyokuwa na abiria 150 iliigonga sehemu ya bawa la ndege ya Ethiopian Airlines, jambo am-
kesi ya uharibifu wa mali na kuhatarisha amani ya nchi, Abdalla Juma, alisema kuwa Sheikh Khalid Azzan anaugua ugonjwa wa kibofu cha mkojo ugonjwa ambao unampasa mteja wake apelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi. Hata hivyo Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Omar Abdalla Ali, amesema kwa sasa hawajajua ni maradhi gani aliyonayo mtuhumiwa huyo, ila walishaanza kumfanyia vipimo na kusisitiza kuwa wanaendelea kumfanyia matibabu.
10
ahakama ya Wilaya ya Chake Chake, Pemba, imemuhukumu Abubakar Mkulu Bakar (28) kifungo cha miaka 60 gerezani kwa kosa la kuwabaka watoto mapacha, liliripoti gazeti la Zanzibar Leo siku ya Jumatano (tarehe 4 Septemba). Kikao cha Mahakama hiyo kilichoogozwa na Hakimu Khamis Ramadhan kiliridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka dhidi ya mshitakiwa huyo mkaazi wa Wambaa na kuamua kwamba anapaswa kutumikia
11
amati ya maridhiano Zanzibar imetoa pendekezo la kufanyiwa marekebisho jina la Jamhuri ya muungao wa Tanzania na badala yake iwe jamhuri za muungano wa Tanzania, kwa lengo la kuleta usawa wa kutambulika kwa nchi mbili hizo ambazo ziliungana tangia mwaka 1964, liliripoti gazeti la Sura ya Mtanzania la tarehe 5 Septemba 2013. Pendekezo hilo lilitolewa na mmoja ya mjumbe wa Kamati hiyo, Ismail Jussa Ladhu, wakati wa mkutano wa kujadili rasimu ya katiba huko Bwawani mjini Zanzibar, Agosti 31 mwaka huu. Sambamba na pendekezo hilo la kufanyiwa marekebisho jina la Jamhuri ya muungano, kamati hiyo pia iliitaka tume ya marekebisho ya katiba
kuyaondoa mambo yote ambayo si ya muungano na ambayo yamo kwenye rasimu ya katiba, kwa madai kuwa hayakustahili kuwekwa kwenye rasimu hiyo. Aidha wametaaka pawepo na usawa kwenye Taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na Mahakama, Bunge, pamoja na Barazala mawaziri, sambamba na kubadilishana nafasi ya uraisi kwa washirika wa muungano. Hata hivyo wameitaka tume ya mabadiliko ya katiba kuyaondoa mambo matatukati ya yale saba ambayo yameanishwa na rasimu ya katiba na badala yake yabakie mnne kati ya hayo ikiwa ni pamoja na Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya nje, usajili wa vyama vya siasa, Uraia na uhamiaji.
Azzan Hamdan, amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja tangu Septemba 1 huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa dhidi yake, liliripoti
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
MAKALA MAALUM
>
12
13
TANBIHI: Jumamosi ya tarehe 31 Agosti 2013, Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar iliitisha kongamano kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani Zanzibar, kutoa msimamo wake kuhusu Rasimu ya Katiba mpya, lakini pia mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Mansoor Yussuf Himid, ambaye alifukuzwa kutoka Chama cha Mapinduzi hivi karibuni, alitoa hotuba ya kwanza hadharani tangu afukuzwe. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba hiyo.
mengi ya kuyasema, lakini ninayo ya kuyasema. Na nitasema wa udhati wa moyo wangu. Siogopi. Mapinduzi Daima. Ndio maana siogopi. Mapinduzi. Siogopi. Kwa maana, maana sahihi ya mapinduzi naielewa. Ni freedom. Uhuru. And I am a free man (mimi ni mtu huru). Mimi na nyinyi, sote ni watu tulio huru. Free. Ninawaombeni pia munistahmilie. Pengine mliyoyatarajia kutoka kwangu hamtayasikia. Inaweza kuwa hivyo, lakini nakuombeni mlihishimu hilo na mnistahmilie na nikikosea mnisamehe, maana tangu ninatoka nyumbani kwangu ninamuomba Mwenyezi Mungu anijaalie kauli thabiti. Na anijaalie niwe na kauli ya ukweli, na anijaalie nisiwe na kauli za fitna, wala uchochezi, wala ubaya. Kwa hivyo, nawaombeni mnistahmilie na pia ikiwa yale mliyotarajia hayakuwa, basi
muendelee kuwa wavumilivu. Ninaanza kwa kuwashukuru sana sana wananchi wa jimbo la Kiembesamaki kwa heshima kubwa na imani kubwa waliyonipa kuwa Mwakilishi wao tangu mwaka 2005. Ninawashukuru sana sana. Hishima haikuwa ndogo, ni hishima kubwa. Imani haikuwa ndogo, ni imani kubwa. Nawashukuru sana na kuwatakia maisha yenye salama na mafanikio pamoja na familia zao. Na namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuyafanya maisha yao kuwa mepesi na kuyafanya kila la kheri. Hakuna binaadamu aliyekamilika. Ninawaomba sana, kwa unyenyekevu mkubwa, wanisamehe pale nilipowakosea. Mimi hawajanikosea, ila nawashukuru kwa mema waliyonifanyia.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
wenyezi Mungu amlaze pema Marehemu Abeid Karume, yeye na wenziwe, Awasamehe kwa makosa yao, na sisi atupe kauli thabiti. Tufuate nyoyo na misingi yao iliyolenga katika mustakabali wa Zanzibar na kizazi chake. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhana Wataala, Mwingi wa
Ujuzi na Mwenye kuelewa kipi kipo ndani ya kila nafsi ya kiumbe alichokiumba, kilicho hai leo na kinachokuja. Atujaalie hikma na busara na atuepushe na fitna. Aujaalie mkusanyiko wetu huu uwe wa manufaa na tija kwa Wazanzibari wenzetu na kizazi chetu. Atujaalie pia tumalize kwa salama na kuelekea kwetu kwa salama. Mengi yameshasemwa. Mimi leo sina
>
MAKALA MAALUM
mapenzi na hishima kubwa na wananchi wa Kiembesamaki, sitaki kuwa Mwakilishi wa mahakama. Sitaki. Pili, sina pesa ya kuchezea na mshahara ndio ushakatika hivyo. Kisha, ya nini malumbano? Hakuna haja. Waungwana hawalumbani hata kidogo. Nimeulizwa na waandishi wa habari, uchaguzi mdogo nitagombea? Sigombei. Ya nini kuendeleza machungu ya wananchi wa jimbo la Kiembesamaki? Ya nini tuendeleza malumbano na siasa za matusi? Hapana. Mwaka 2015 nikiwa hai, nikiwa mzima na bado nikiwa nina dhamira na moyo wa kuwatumikia watu, ninaweza nikafikiria vyenginevyo. Naulizwa umechukizwa na kufukuzwa? Una ugomvi na CCM? Sina. Na nitakwambieni kwa nini. Binaadamu daima mwenye ukweli wa nafsi yake, muungwana hatizami moja. Hili si dogo. Kwangu mimi ni kubwa, tena sana, na ndio maana tulipokuwa tunaimba Sisi Sote, miye nililia, kwa sababu si dogo hili. Miye naitwa Mansoor Yussuf Himid. Nilitaka mwenyewe kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Sikulazimishwa na mtu. Na kinyume inavyosemwa nilikwenda mwenyewe kuitafuta hiyo kadi yangu ya mwanzo mwaka 1987. Lakini madhali Mwenyezi Mungu amewapa wanadamu midomo, wana haki ya kusema, basi waache waseme. Ukweli wa nafsi na ukweli wa hali halisi naujuwa mimi. Kwa hivyo mimi sina ugomvi na Chama cha Mapinduzi. Nimejenga historia ya udugu na kifamilia ndani ya Chama cha Mapinduzi. Nina wenzangu mle ambao tumeishi kwa hisani kubwa na mapenzi makubwa. Na mikono ya pole mingi sana iliyonifika mimi kwa watu kunitafuta imetoka humo humo ndani ya CCM. Kwa hivyo, yale kwangu mimi hayatafutika. Nitaendelea kuwaenzi wenzangu na nitaendelea kuwaheshimu. Maamuzi ya kisiasa ndio maamuzi ya kisiasa kama tulivyosema Sitaki Basi. Wenzangu wamenipa, wameniona sifai kuwa miongoni mwao. Ni haki yao kwa sababu ni chao. Ni chao. Miye simo tena. I am a free agent (ni wakala huru). Wapo washaanza kunitafuta: Tutakufanya mwenyekiti wa chama chetu weye! Lakini kama nilivyosema, mimi mtu huru. Wala wasidhani wala wasidhani kama nikiamua kufanya maamuzi yoyote yale yaliyokuwa ndani ya misingi ya katiba na sheria, kwamba nitakhofia. Nitafanya. Kama kutukana tena hapo, haya tu. Kila mmoja atajijuwa mwenyewe. Nikaulizwa utakata rufaa? Mimi sikati rufaa. Sikati rufaa. Ya nini? Tunarudi pale pale, sitaki mwenziwe basi. Wenzio washakupima, hawakutaki tena, namkatia rufaa nani? Hapakaliki tena eti pale. Miye siye. Miye si mwenziwao. Kwa hivyo, hapana. Nilimsikia mmoja wao akisema Sisi na yule yashatuishia (huku akikunguta mikono). Na mimi yashaniishiya. Ninazo hisia zangu kama binadamu, zinaungana na historia yangu na historia ya wazee wangu. Lakini sasa si pahala pake, si wakati wake. Pengine miezi ya mbele,
>
Ninawashukuru pia wote nilioshirikiana nao katika maisha yangu ya kisiasa ndani ya Serikali katika wizara zote nilizozitumikia, ndani ya Baraza la Wawakilishi nawashukuru wawakilishi wenzangu wote. Namshukuru Mheshimwa Spika na watumishi wa Baraza kwa namna tulivyoishi kwa wema. Mwenyezi Mungu awajaalie na wao wote kila la kheri. Nimekuwa nikiulizwa maswali mengi sana na waandishi wa habari kutoka kila pembe ya dunia Marekani, Ulaya, Uchina, yaani nchi nyengine ambazo ndio kwanza nimezisikia kipindi hiki, mpaka simu inakataa mwisho wake inaganda, inanibidi kutafuta mafundi kuja kuiweka sawa. Nataka niyajibu baadhi ya yale ambayo ninayakumbuka, ili yaishe hapa. Sioni sababu ya kuendeleza jambo. Nikaulizwa sababu za kufukuzwa. Sizijui. Mtawauliza wenyewe walionifukuza. Lakini nilisikia kwa mbali, kwamba walisema kwenye kikao kwamba huyu ndiye aliyesema juu ya suala la mafuta na gesi asilia, Muungano huu ni wizi wa mchana. Mwenziwe Sitaki? Basi (Inajibu hadhira). Nimeulizwa, je nitakwenda mahakamani? Siendi. Sababu kubwa ni kuwa nilichaguliwa kwa
miaka ya mbele, tukiwa tumetulizana, kama nitakuwa nalo la kusema, nitalisema. Sitokhofia kusema. Lakini kwa sasa niseme tu, kwamba nawashukuru sana wenzangu. Mimi naendelea kuenzi historia ya udugu na matumaini niliyojenga kule. Ninawashukuru wenzangu wengi sana. Tena mtashangaa, mikoa mingi sana ya Bara, viongozi wengi wamenipigia simu, wengine wakiwa wameshangaa, wengine wakiwa na huzuni kubwa, lakini wote lengo lilikuwa ni kunipa pole, kunitaka nitulizane na kumshukuru Mungu. Na Alhamdulillah, nishamshukuru Mwenyezi Mungu, na ninaendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu Ndiye wa kutegemewa na Ndiye wa kushukuriwa. Riziki itatoka kwengine kama ipo. Kama haipo, ndiyo mipango ya Mungu. Nikaulizwa na waandishi wengi, je uko salama kwa maana hakuna aliyenitisha? Alhamdulillah. Lazima niseme ukweli. Mbali ya kupata faraja na kuungwa mkono kwa wingi, hakuna aliyenitukana, hakuna aliyenibughudhi. Niko salama kama raia wanavyopaswa kuwa salama. Alhamdulillah, namshukuru Mwenyezi Mungu. Kusema vyenginevyo, nitakuwa nasema uongo na miye sitaki kusema uongo. Bonyeza hapa uisikilize hotuba kamili:
15
14
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
16
17
azanzibari na Watanganyika wana malezi tafauti kuhusiana na sura ya Muungano. Ambapo Watanganyika wanauangalia huu kuwa ni Muungano wa Serikali Moja, Wazanzibari wanauangalia kuwa ni wa Shirikisho la Serikali Tatu. Hata kama si Serikali Moja wala Tatu iliyoandikwa popote katika sheria kuu zinazoongoza nchi hizi mbili, bado tabia, matendo na maono ya watu wa pande hizi yanasomeka hivyo. Ndiyo maana, si rahisi kwa Mtanganyika kumkuta anajiita kwa jina hilo, maana kwa wengi wao Tanganyika imeshapo-
tea, lakini kila mara utamkuta Mzanzibari akijiita na akijinasibisha kwa Uzanzibari wake. Huu ni uamuzi wa kimapinduzi kwa pande zote mbili za Muungano. Kwa Tanganyika ni wa kimapinduzi kwa kuwa umeweza kupindua fikra za takriban vichwa milioni 40 na kuvifanya viamini kitu kimoja. Kwa Zanzibar ni wa kimapinduzi kwa kuwa vichwa milioni moja tu, ambavyo ni chini ya asilimia 3 tu ya Watanzania wote na vinavyokaa katika chini ya asilimia moja tu ya ardhi yote ya Tanzania, vimeweza kuhimili hisia za kutokuridhika
kwa miaka 50 ya Muungano huu. Lazima tukiri kwamba ni ujasiri tu ndio unaomwezesha mwanadamu kuweza kukaa na fundo la moyo kwa miaka mingi kama hii. Kubwa zaidi kwetu ni kukiri kwamba kuna kutokuridhika huko kwa upande wa Zanzibar, ndipo tuweze kusaidiana kuyageuza mateso yetu kuwa faraja. Kukubali huko kutayaendeleza Mapinduzi ya kweli ya Zanzibar kwa kuyapa maana katika maisha ya kila siku na ya kila mmoja wetu.
Mapinduzi hasa ni matokeo ya kutokuridhika, ambako husababishwa na mgogoro kati ya njia ambazo watu wanaouona ukweli na njia ambazo wangelipenda ukweli huo Zanzibar inauona ukweli kuwa Muungano huu, katika hali uliyo, ni tatizo kwake na, sasa, ingelitaka kuuona kuwa ni sehemu ya utatuzi wa tatizo hilo. Huko hakuwezekani ila kwa Mapinduzi; na hayo si mapinduzi ya mapanga na marungu, wala bunduki na mizinga, bali ya fikra na mkakati. Haya ni Mapinduzi ambayo yanatakiwa yapitie hatua tano za matayarisho kwa ajili ya mapinduzi ya kuporomoka kwa mfumo mkongwe, ya kuharibika kwa mahusiano makonWWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
>
gwe, ya kujenga mahusiano mapya; na ya kuuimarisha mfumo mpya. Ama kwa kujijua au kutojijua, tayari tumeshapita kipindi cha kwanza cha matayarisho kwa ajili ya Mapinduzi, kipindi ambacho kilitawaliwa na woga wa wananchi na mateso ya watawala. Kilikuwa ni kipindi ambacho, ingawa palikuwa na kiwango kikubwa cha kutokuridhika na jinsi Muungano huu unavyoikandamiza Zanzibar, si Wazanzibari wengi waliothubutu kueleza kutokuridhika huko. Bali hata wale wachache waliothubutu, walisemea vibuyuni ambako ama walichokisema kilimalizwa huko huko au wenyewe walimalizwa kwa njia zao za kumalizana. Sasa tulipo, kwa maoni yangu, ni katika hatua ya pili ya Mapinduzi, ambapo mfumo mkongwe wa Muungano usio na maslahi kwa Zanzibar unaelekea kuporomoka. Kawaida kipindi hichi ni matokeo ya kupotea kwa uongozi ndani ya kundi la watawala, ambapo mgawanyiko wa makundi humfanya kila mmoja kutenda vyake. Mara nyingi hatua hii haifikiwi mpaka ajitokeze kiongozi anayejiona kuwa mwanamageuzi kutaka kuunusuru mfumo
> WWW.YOURDOMAIN.COM ISSUE 03 - WINTER 2012
mkongwe; na akafeli. Mwanasiasa wa Kifaransa na mtaalam wa uchumi Anne-Robert-Jacques Turgot na mwanasiasa na waziri mwenzake Jacques Necker walijaribu kuunusuru ufalme wa Ufaransa kabla ya mwaka 1798 na Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi Pyotr Arkadyevich Stolpyin alifanya jaribio kama hilo nchini Urusi kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, lakini wote walishindwa. Huo huwa ni wakati ambapo, kutokana na mtikisiko wake, mfumo mkongwe huwa kama tayari umeshakufa kitambo, lakini kwa kuwa watu wanaothubutu kuyathibitisha mauti yake hawajatokea, basi huendelea kuwepo tu ukiendea upepo na kudura ya Mungu. Nabii Suleiman (A.S) alikuwa amefariki siku nyingi, lakini watumishi wake waliendelea kutumika wakidhani bosi wao amekaa kitini akiwasimamia, hadi mchwa alipokuja kuila fimbo yake. Kuna watu waliojua kuwa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Ufaransa imeshakufa tangu mwaka 1934, lakini maziko yake yalifanywa mwaka 1940. Wazo ninalojaribu kuliwasilisha hapa ni kwamba, sasa umefika wakati wa yale
Na viashiria vya utabiri huo vimeanza kujengeka sasa. Changamoto iliyo mbele yetu kwa sasa ni ukweli kwamba hatua za tatu, nne na tano zinakuja kwa kasi na, yumkini, hatuna matayarisho mazuri kuzikabili. Kwa mfano, hatua ya tatu, ambayo ni ya kuharibika kwa mahusiano makongwe, kwa mintarafu ya kuharibika kwa muundo wa sasa wa Muungano, ina matatizo yake. Mojawapo ni kwamba, wenye maslahi na mahusiano haya hivi sasa, wameanza kutumia nguvu zao za ziada kuzuia yasiharibike. Na ingawa, kutokana na matakwa ya kiwakati hawatafanikiwa, lakini kama ilivyo kawaida ya mti mkubwa unapoanguka, husababisha maafa kwa pale unapongokea (panaweza kuchimbika shimo kubwa) na kule unakoangukia (unaweza kuelemea nyumba au wapita njia na kuwajeruhi kama si kuwatoa roho zao). Lakini mara tu kipindi hiki kinapoanza, hutanguliwa haraka sana na kipindi cha ujenzi wa mahusiano mapya. Huu ni mfano wa ujenzi wa nyumba mpya juu ya kongwe, ambapo mwenye nyumba huendelea kujenga nyumba mpya, huku yeye akiwemo ndani.
Huvunja kiambaza kimoja kwanza na kusimamisha kipya mahala pa kilichovunjwa, kabla hajakwenda katika kiambaza chengine. Ingawa huweza kuchukua muda mrefu kwa nyumba kukamilika, kutegemea na uwezo wa kifedha, kiufundi na mazingira ya ujenzi. Lakini ni staili ya yenye faida moja kubwa: hakuna wakati ambapo mwenye nyumba analazimika kulala nje, hata kama katika kipindi cha ujenzi huwa hakai katika makazi mazuri sana. Hapo ndipo, kwa maoni yangu, nchi hii inapoelekea. Muungano huu utaanza kuvunjika na mpya kuundika kwa wakati mmoja. Ninachoeleza ni kwamba tunakwenda katika kipindi ambacho hatutasema kuwa hatuna Muungano moja kwa moja, lakini pia hatutakuwa na Muungano huu. Mwisho tutaingia kwenye kuimarisha mahusiano mapya tutakayoyajenga. Ukweli ni kwamba Zanzibar na Tanganyika, bali pamoja na mataifa mengine yaliyo jirani, yataendelea kuwa na mahusiano dumu daima. Lakini tafauti na sasa, mahusiano yajayo kwa sababu ya Mapinduzi haya, yatakuwa na sura nyengine na matakwa mengine. Hata hivyo, tuzinduke Wazanzibari, kwamba jambo pekee linaloweza kutufikisha hapo ni moja tu. Nalo ni mkono mmoja kuyashikilia Mapinduzi yetu na mwengine kuishikilia Zanzibar yetu. Yaani isiwe tu Mapinduzi Daima, lakini iwe pia Zanzibar Daima; maana Mapinduzi Daima hayana maana ikiwa hatuna Zanzibar.
18
19
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
LA KUSEMWA LISEMWE
>
NA SALIM S SALIM
ukua kwa kasi kwa vuguvugu la watu wa Zanzibar la kutaka mamlaka kamili ndani ya Muungano kunaonekana kukitia kiwewe chama cha CCM. Hivi sasa viongozi wake, badala ya kujibu hoja zinazotolewa juu ya suala hilo, wameamua kuropokwa matusi ya nguoni na kujipapatua kama anavyofanya farasi anapokuwa katika sakaratil maut ( anapokuwa anakata roho). Hali hii ya kusikitisha na inayochefua roho na ambayo ni kinyume na ustaarabu wa Wazanzibari uliojengeka tokea dahari na enzi kutokana na misingi ya dini, utamaduni, silka na khulka ilionekana katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Unguja. Baadhi ya viongozi wa CCM waliopanda jukwaani ka-
tika uwanja unaoitwa Kombawapya uliweza kuwalinganisha na komba waliolewa kwa kutamka maneno ya kashfa ambayo ni nadra kuyasikia hadharani kutoka katika mdomo wa Mzanzibari, awe nyumbani au nje. Waliokuwa hasa wakiongoza katika matusi ya nguoni ni viongozi wenye nyadhifa za juu katika CCM na Jumuiya yake ya Vijana (UVCM), hasa Mwenyekiti mpya wa taifa wa UVCM Sadifa Juma Khamis na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini, Borafya
20
21
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
LA KUSEMWA LISEMWE
Askari polisi waliopelekwa hapo kuhakikisha mkutano unafanyika kwa mujibu wa sheria na hapatolewi kauli za kuhatarisha amani au kuchochea fujo walikaa kimya na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, wakati wa mkutano wala baada ya mkutano, dhidi ya hao waliokuwa wakibwabwaja matusi. Habari za uhakika zimeeleza kwamba siku iliofanyika mkutano ule viongozi wa juu wa CCM/Zanzibar na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, walikuwepo Zanzibar. Kinana ambaye huelezwa kama muungwana aliyetimia aliondoka Zanzibar siku ya pili yake bila ya kutoa tamko la kulaani au kukemea uhuni ule. Hii imetoa tafsiri kwa baadhi ya watu kwamba walichofanya wahuni wale kimepata baraka ya viongozi wa juu wa chama chao. Baadhi ya wakuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar wamekuwa na kigugumizi na wengine wamejifanya mabubu wanapoulizwa kwa nini wanaruhusu uhuni wa aina ile na kitu gani kinachowazuia kuhakikisha sheria zilizopo zinachukua mkondo wake katika kuwawajibisha kisheria watu wanaotukana watu hadharani. Baadhi ya wazee wa Zanzibar ambao walishuhudia mikutano ya chama kilichojulikana kama cha Haki za Binaadamu kilichokuwepo Zanzibar kabla ya Mapinduzi na kilichopata umaarufu kwa lugha yake ya matusi wanasema matusi yaliokuwa yakisikika kwenye mikutano ya Haki za Binaadamu ni kichuguu tu kwa matusi yaliosikika hivi karibuni. Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanauliza : Je, Polisi ingelikaa kimya na kufunga pingu zake kama matusi yale yalielekezwa kwa viongozi wa CCM? Watu wengi waliohojiwa wanasema usiku ule ule yangefunguliwa mashitaka dhidi ya walioyatamka matusi, wale waliowakaribisha juu ya jukwaa na walioomba kibali cha kufanyika mkutano.
>
Silima. Wawili hao waliugeuza mkutano huo kuwa darasa la masuala ya kaumu Lut na bila ya kuona haya wala vibaya waliwahusisha baadhi ya viongozi na wanasiasa maarufu wa chama cha CUF, wakiwemo waliokuwemo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na vitendo vya liwat. Matusi hayo mazito yaliojaa uhuni pia yaliporomoshwa kwa ahli na marafiki wa viongozi hao wa CUF, kama vile waliokuwa wakitamka uchafu huo hawakuzaliwa na mwanamke. Baya zaidi na ambalo linakwenda kinyume na maadili na uwajibikaji katika taaluma ya tasnia ya habari matusi haya hayakukatishwa na yaliendelea kutangazwa moja kwa moja na baadhi vituo vya televisheni na radio.
22
hawa au chama hicho kina ilani mpya ya uchaguzi ambayo inashajiisha makada wake kutukana watu? Kwa sasa kiwewe hiki cha kutaka watu wasishindane kwa hoja bali kwa matusi na kuvifanya viwanja vya mikutano ya kisiasa viwe maeneo ya kufanya utafiti wa kuandika kamusi la matusi la lugha ya Kiswahili kinaipeleka Zanzibar pabaya.
Watu wengi waliokuwa wakifuatilia matangazo haya majumbani na hata sehemu zenye watu wa rika tafauti walilazimika kuzima radio na televisheni zao. Mmtu mmoja aliyehudhuria mkutano huo ambaye naye alilazimika kuondoka baada ya muda alisema: Siku hii itaingia katika kurasa chafu za historia ya Zanzibar. Ilikuwa aibu , fedheha na ushenzi uliokithiri kipimo chochote kile cha unyama. Kinachoshangaza walipokuwa watu hawa wakitukana viongozi wenzao waliopo wenye hiyo sehemu ya wageni wa heshima walitulia kama kunguru waliotiwa maji na hakuna aliyethubutu kuwkemea: Hivyo sivyo. Wengine waliokuwepo hapo wakiwa na watoto na wajukuu zao nao walishangaza watu kwa uamuzi wao wa kufurahia na kushangilia matusi.
Uchunguzi wa jarida hili umebaini kuwa mmoja wa waliofurutu ada ya kutoa matusi siku ile amekuwa akitibiwa baada ya kila kipindi kwa matatizo ya akili katika Wapo pia wanaouliza je, CCM imebadihospitali ya wagonjwa wa akili iliopo Zan- li jina kutoka Chama cha Mapinduzi na kuwa Chama cha Matusi au hayo matusi zibar. ndio mapinduzi yanayokusudiwa? Nini kilichotokea hata akaweza kukabidhiwa nafasi ya juu ya uongozi wa UVCM hivi Historia haitawasahau wahuni hawa karibuni ni swali ambalo labda viongozi wanaoshabikia kutukana watu ovyo matusi ya nguoni na wale wote wenye uwewa CCM wenyewe watalijibu. zo wa kuwadhibiti na walioamua kuwaLakini jibu linalosubiriwa kwa hamu ni lile nyamazia. la swali linaloulizwa kwa shauku kubwa, nalo ni: Je, CCM itawachukulia hatua watu
23
Natoa pongezi zangu kwako binafsi pamoja na waandishi wenzio mliojitolea kulisimamisha Zanzibar Daima OnLine. Matumaini yetu, Wazanzibari, ya siku nyingi yametimia. Nimepata fursa ya kuyapitia majarida yote mliyotoa. Naamini kwa dhati kabisa Wazanzibari watalikaribisha kwa moyo mkunjufu. Mchangayiko wa mada katika toleo la pili ni mfano mzuri wa kuliendeleza. Nilifurahi kuyasoma makala ya mwandishi wenu wa michezo. Alinikumbusha wakati wa utoto wetu pale Abdul Majham akin'gara katika timu ya Taifa na Vikokotoni. Naam yeye na Marhemu Shioni Mzee walikuwa wakicheza kama roho zao "zimeunganishwa" pamoja. Akiwa na mpira mmoja anajua wa pili atampasia vipi. Wakati huo mabeki ndio akina Mtumwa Mwenda (Police), Chifu (Miembeni), Abdulla Azan (Police) nk. Tunatarajia kusoma mengi ili vijana wetu wafahamu tunakotoka na sisi wazee kukumbushana yaliyopita. Kwa pamoja tutaweza kuendelea kuijenga Zanzibar ya wote. A. Abdalla - Denmark Kopenhagen, Denmark
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
JAMVI LA BARAKA
>
Zimbabwe
Gabriel Mugabe aliibuka mshindi akipata asilimia 61 ya kura na chama chake cha ZANU-PF kikashinda theluthi mbili ya viti vya bunge. Ushindi huo uliwashangaza wengi ndani na nje ya Zimbabwe. Wengi wanaamini kulipita mizengwe iliyoendeshwa kitaalamu. Uchaguzi wa Zimbabwe umezusha swali: wengine wanajifunza nini ? Katika nchi nyingi migogoro ya kisiasa inayoibuka baada ya kufanywa chaguzi husababishwa kwa sehemu kubwa na Tume ya Uchaguzi kutokuwa huru. Tatizo hili lilikuwa donda ndugu katika chaguzi zote za Zanzibar tangu ulipoanza mfumo wa demokrasia ya vyama vingi 1992. Katika chaguzi zote zilizofanywa Zanzibar chini ya mfumo huo wa vyama vingi Tume ya Uchaguzi (ZEC) ilikuwa ikikosa uwiano kati ya wadau wahusika na ilikuwa mateka
Ingawa Wazanzibari tumekubaliana kuwa na maridhiano na tumeona haja ya kuondoa uhasama wa kisiasa, bado vizingiti vipo
U
24
chaguzi mkuu uliofanywa Zimbabwe mwishoni mwa Julai ulihitimisha mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ulioko Zanzibar,ingawa huo si wa mpito kama wa Zimbabwe kwa vile umo ndani ya Katiba. Uchaguzi huo wa Zimbabwe una somo kwa Zanzibar. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zimbabwe ,iliyoundwa baada ya mzozano wa uchaguzi wa 2008, ilidumu kwa miaka mitano hadi uchaguzi wa Julai licha ya misukosuko mingi. Katika uchaguzi wa Julai Robert
wa chama kinachotawala cha CCM. Kuna dhana kwamba kwa vile mwenyekiti wa Tume huteuliwa na Rais basi daima huwa mtiifu kwa Rais aliyemchagua na hawi mtiifu kwa sheria na kiapo alichoapa cha kuiheshimu na kuitii sheria hiyo. wamekuwa na tabia ya kushindwa kueIngawa Wazanzibari tumekubaliana lezana ukweli na kuendelea kulindana, kuwa na Maridhiano na tumeona haja ya kuuondoa uhasama wa kisiasa, bado kukubaliana na matokeo. vizingiti vipo: Haya Zanzibar ina uzoefu nayo tangu 1995 . - Mizengwe na wizi wa kura; Ni takriban miaka mitatu sasa tangu - Tume kuwa ndiyo yenye kauli ya mwisho na uamuzi wake kutoweza kup- uchaguzi uliopita. Mbali na kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) baina ingwa; ya CCM na CUF, hakuna hatua kubwa ili- Wanaoshindwa kutoweza kupinga yochukuliwa na Rais Ali Mohamed Shein matokeo ya uchaguzi wa Urais mahaka- kuonyesha kuwa kweli amenuia kuiona mani; Zanzibar inafungua ukurasa mpya. - Na hata Jumuiya za kikanda na bara la Ahadi alizotoa wakati alipozungumza Hoteli ya Bwawani siku yalipotangwa Afrika kama Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Muungano matokeoya uchaguzi uliopita,kuhusu dosari ziliopo hakuzitekeleza. Alitamka, wa Afrika (AU) ambazo viongozi wake
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
25
TOLEO 03 >
>
>
JAMVI LA BARAKA
nikimnukuu vyema: Nimeyasikia na kwa kweli ni mazito.Nitazungumza na wenzangu ili kuyarekebisha. Hatuna uhakika ikiwa alizungumza na wenzake lakini hadi sasa ni wazi kuwa hakuyarekebisha. Kwa sehemu kubwa mazingira yaliosababisha utata miaka ya nyuma bado hayajabadilishwa. Uteuzi wa wakuu wa mikoa, wa wilaya na wa nyadhifa mbalimbali Serikalini hadi leo bado unazingatia u-CCM. Zaidi ya yote Tume ya Uchaguzi bado inateuliwa pasina kuwepo uwiano na hali ya kuwaridhisha wadau wote wanaokhusika CCM na CUF na hata vyama visivyo na uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi lakini vilivyosajiliwa rasmi kuwa ni vyama vya kisiasa.
26
Inatoka Uk. 09
huko Pemba mwezi mmoja uliopita, katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamadi aliionya Tume mpya dhidi ya fununu zilizozagaa kwamba ina mpango wa kuyapunguza majimbo ya uchaguzi Pemba hadi kufikia 14. Pindi hilo likiwa na ukweli bila shaka litatafsiriwa kuwasehemu ya mizengwe ya mapema kabla yauchaguzi wa 2015. Yote hayo hayayafanyi mazingira yawe mazuri na ni kikwazo cha maendeleo, haki za binaadamu na demokrasia .Madosari kama hayo ndiyo yaliyoisibu demokrasia nchini Zimbabwe. Alau wajumbe wawili wa Tume ya Uchaguzi Zimbabwe walijiuzulu baada ya kutangazwa matokeo. Hatua yao ilikuwa na ujumbe mzito. Hapana shaka wahafidhina wa Zanzibar, wapinga mageuzi, wapinga maendeleo na wasioitakia mema wamo mbioni. Mizengwe na hila za aina zote ndio nguzo zao za kuhakikisha wanaendelea kuwepo kwenye madaraka . Ni matarajio ya Wazanzibari kwamba uchaguzi wa 2015 hautaandamwa na jinamizi la Zimbabwe na kina Mugabe. Maridhiano ndiyo dira lakini dira hiyo itatimia tu pindi hitilafu zilizokuwa kikwazo miaka mingi zitaondolewa. Hayo yanapaswa kuanza kufanyiwa kazi sasa. Ikiwa wanasiasa na watunga sheria (Wawakilishi) wamelewa madaraka na wamelala fofofo, umma ambao ndiyo uliowaweka madarakani una jukumu la kuyapigania kwa nguvu zote, ili 2015 Zanzibar ipige hatua nyingine mbele baada ya Maridhiano yalioidhinishwa na asilimia 66 ya umma wa Wazanzibari.
Aidha wale wasio wana CCM wanaendelea kunyimwa vitambulisho kuanzia vya ukaazi , vya Uzanzibari hadi vya kupigia kura. Si hasha wakati wa kukaribia uchaguzi ujao litaongezeka na la daftari la kupigia kura. Rais Shein ameunda Tume mpya hivi karibuni kuchukua nafasi ya ile iliomaliza muda wake mwezi Januari mwaka huu na iliyoundwa namtanguliziwake Amani Karume 2008. Kazi nzuri kubwa iliofanywa na Tume hiyo ilikuwa ni kusimamia kura ya kwanza ya maoni katika historia ya visiwa hivi kuhusu uundwaji wa Serikali ya Umoja wa kitaifa. Lakini katika ripoti yake ya kutathmini utendaji wake katika kipindi cha miaka mitano, Tume hiyo ilieleza kwamba ilishindwa kukamilisha kazi ya kupitia upya mipaka ya majimbo ya uchaguzi. Katika mkutano mmoja wa chama chake
27
Nimegusia juu ya dhima ya Wizara ya Elimu katika kunyanyua somo la teknolojia ya habari na mawasiliano visiwani Inasikitisha zaidi kusikia kwamba ni skuli Zanzibar. Lakini ninajua kwamba tuna 13 tu, kama asilimia 5 ya skuli zote, zinaz- magwiji wa fani hii walio ughaibuni na owafunza wanafunzi masomo ya teknolo- wengine waliostaafu na waliorudi nyumbani. Nadhani kuna haja ya kuzingatia jia ya mawasiliano na kasoro ya asilimia jinsi gani watavyoweza kuchangia ili ku3 ya walimu wanatumia teknolojia ya ICT saidia elimu hii muhimu iweze kupenya kufundishia. kwa urahisi katika skuli zetu za Unguja na Takwimu zinazidi kusikitisha ukisikia Pemba. kwamba miongoni mwa walimu 7,534, ni 268 tu, kasoro ya asilimia 5 walio-
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
NA MOHAMED ABDULRAHMAN
28
wa Muungano wa serikali mbili, ambapo yeye Mansoor anataka Muungano wa serikali tatu, Zanzibar ikiwa na mamlaka kamili. Mansoor ni muumini wa Muungano, lakini ulio chini ya msingi wa kuheshimiana, usawa na haki. Wako wanasiasa kadhaa ndani ya CCM huko Tanganyika na Zanzibar wenye mawazo sawa na ya Mansoor, lakini hawajapewa kadi nyekundu au hata ya manjano. Makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, amekwenda mbali zaidi na kusema yeye ni muumini wa serikali MOJA ya Muungano. Tamko hilo lilinyamaziwa kimya ndani ya CCM, mshipa watu haujawapiga. Lakini sababu hasa ninayoiona mimi ni kwamba Mansoor ana bashasha ya kimaumbile, anamiliki haiba ya baba yake. Kwake yeye Mapinduzi Daima
29
ni karata ya kutaka kuyapindua daima mawazo ya Wazanzibari wasikubali fikra mgando. Chama cha Wananchi (CUF) siku hizi nacho pia kinalipiga baragumu linalonadi Mapinduzi Daima. Hoja ya Mapinduzi Daima yaonyesha sasa imewaunganisha Wazanzibari na kuwa vuguvugu linalogeuka kuwa wimbi lisilozuilika kutaka nchi yao iwe na mamlaka kamili. Pia Mansoor yaonyesha ana ule moyo wa kujiamini, sifa aliyokuwa nayo Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid
Karume, kwamba Wazanzibari wanataka na wana uwezo wa kujiamulia wenyewe mambo yenye maslahi nao, tena bila ya kuwajali watu wengine, ikiwa ni wa madola makuu au madogo. Hofu ya CCM ni kwamba lau Mansoor angeachiliwa ndani ya chama hicho aendelee kutetea anachokiamini angeweza kuzidi kuwaambukiza kifikra baadhi ya viongozi wengine chamani. CCM hivi sasa iko mashakani huko Tan-
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
ganyika kutokana na upinzani unaopata nguvu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kwa hivyo, CCM haiko tayari kuachia safu zake Visiwani zikiwa zinadhoofika zaidi. Kumfukuza mwanasiasa huyo ni jaribio la chama kutaka kujinusuru. Hiyo ni haki ya chama chochote, hata cha mpira, seuze tena chama kikubwa cha kisiasa. Hilo, kwa bahati nzuri, Mansoor amelitambua, na ndio maana amewataka Wazanzibari wote waheshimu mawazo ya watu wanaotafautiana nao. Malumbano hayafai, tena hasa katika wakati huu muhimu utakaoamua mustakbali na hatima ya Zanzibar. Kuna wenye kufikiri kwamba ingekuwa vizuri Mansoor angejiengua mwenyewe kwanza kutoka CCM kabla ya kungojea afukuzwe. Yaonyesha hajataka kulipa fadhila nyingi alizofanyiwa na chama hicho kwa kujigeuza kuwa msaliti wa chama hicho na kuwafungulia njia wazi wale watu wasiokubaliana naye wazidi kumsakama kisiasa. Mwishowe ilidhihirika wazi, na kama alivyoungama mwenyewe, kwamba kwake yeye Zanzibar ni muhimu zaidi. Zanzibar KWANZA na chama baadaye, ndio kauli mbiu yake. Ninahisi kwamba chama kumtema kabla ya yeye kukitema kumemjengea sifa zaidi. Ni taabu sasa yeye kutuhumiwa kwamba amekisaliti chama.
30
Dondoo kutoka kitabu Mzanzibari Asimlia Hadithi Yake kilichoandikwa na Sheikh Shaaban Saleh Farsy.
Unaweza kutangaza biashara yako kupitia Zanzibar Daima Online, jarida la kila wiki mbili lenye wasomaji wengi wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili duniani kote.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
hiano inayoongozwa na Mzee Hassan Nassor Moyo, ilianzishwa 2009. Miaka mitano hivi imeshapita tangu ianzishwe kamati hii yenye wajumbe sita mchanganyiko kutoka CCM na kutoka Chama cha Wananchi (CUF).
NA JABIR IDRISSA
32
HAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinapita katika kipindi kigumu sana. Wengi wa viongozi wake wana uchovu wa kiwango cha juu. Kadiri ninavyopima staili zao za kutenda, nataasaf kwamba wamechoka kufikiri na hawatendi tena kwa muala. Hawatendi baada ya kuwa wamefikiri. Wanatenda pasina kutafakari. Tatizo zaidi hutokea inapoonyesha kuwa siku hizi viongozi wakubwa wa chama hichi wanatenda bila ya kufikiria athari za wanachokitenda. CCM imekuwa ni chama tafauti na asili yake. Zamani ukiona viongozi wake wamefanya jambo au wameamua jambo fulani, basi huwa waliifikia hatua hiyo baada ya kuangalia kila hali. Wananchi walizoea kuwaona viongozi wa chama hichi wakituliza akili
33
TOLEO 03 >
>
>
wanatangaza leo kuwa hawaitambui Kamati ya Maridhiano. Ofisi Kuu ya CCM/ Zanzibar hapo Kisiwandui, inathubutu leo, miaka mitano baada ya kuundwa kwa Kamati ya Maridhiano, kuhoji ni lini chama hicho kilitoa baraka zake kuianzisha kamati.
34
Sasa basi, tamko la Waride linawahenyesha Moyo na wenzake kuwa hawajatumwa kwa vyovyote vile kushiriki katika Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Kamati ya Maridhiano na ieleweke kuwa (NEC), Itikadi na Uenezi, Waride Bakari wajumbe wamejipeleka wenyewe ili kuJabu anaandika tamko lisemalo kitendo chochote cha kamati hiyo kulihusisha jina potosha na kuwahadaa wananchi kwa manufaa yao. la CCM (katika mambo yake) kihesabiwe na wananchi kuwa ni utapitapi, chokoMoyo ni mtu wa umri. Isitoshe, umri choko na ukorofi wa kisiasa. wake ni tafauti kabisa na alionao Waride, mtoaji wa tamko la CCM, chama ambacho Eti wana-CCM waliokuwa wajumbe wa Moyo kakitolea jasho lisilo kiasi. Chama NEC, wajumbe wa Baraza la Mapinduzi leo ni watapitapi na wakorofi wanaotia ambacho Eddi Riyami kakihenyea na chama ambacho Mansoor hakijitoa kukichokochoko. jenga. Waride anasema katika tamko lake hilo, Waride, katika tamko hilo ambalo amelikuwa CCM ina utaratibu na kanuni zake toa kwa niaba ya uongozi wa juu wa za kuunda kamati na si kuundiwa au kusemewa na kundi lolote. Anasema in- CCM/Zanzibar, hawezi kusimama kwa kigezo chochote kile sambamba na Moyo apotokea haja ya kuunda kamati yoyote wakapanga siasa na namna ya kuzicheile, wajumbe wake hutokana na maaziza. Kisiasa, kiumri, kihadhi, kiungwana na mio ya vikao halali vya kikatiba na si kukizalendo Moyo na Waride ni kama lila na kurupuka kama ifanyavyo inayojiita Kafila hazitengamani. mati ya Maridhiano. Kwa CCM, Moyo sasa anakurupuka na anaongoza kamati isiyotambuliwa na Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Kwa CCM, Moyo pamoja na Mohamed (Eddi) Ahmed Riyami na Mansoor Yussuf Himid ambao ni wajumbe wa kamati yake, ni wavurugaji wenye malengo ya kukidhi tamaa zao. Anavyofikiri Moyo hawezi kufikiri Waride. Vile anavyoyaona mambo Moyo sivyo anavyoyaona Waride pamoja na wengi wa hao waliomtuma aipinge Kamati ya Maridhiano. Ni watu wasiofanana kwa namna yoyote ile. Wakati Waride ni wa leo, Moyo ni mtu wa taarikh.
35
Badala ya kuwa Moyo na wenzake ndio waliokurupuka, ukweli ni kwamba Waride na wenzake katika CCM ndio wenye upungufu wa kuyajua mambo. HawajiViongozi wa CCM wametokwa na haya tambui wapi wametoka, wapi wapo na siku hizi. Wanatupa tu buu kama vile wa- wapi wanakwenda. navyopiga ndege gizani. Wanabahatisha.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
NA RIZIKI OMAR
36
Jambo hili linakwenda sambamba na utatanishi wa makusudi unaofanywa na Serikali ya Muungano. Utatanishi wenyewe ni kwamba, kwa upande wa Serikali ya unapozungumzia Muungano wetu, Muungano, imefanya mara nyingi huko kuna mambo mawili ambayo ndiyo nyuma, kumpa Mzanzibari kuongoza uhalisia wake: kwanza, huu ni wizara ambayo si ya Muungano; ikijua Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, fika kwamba kufanya hivyo ni kinyume nchi mbili zilizokuwa na mamlaka kamili cha mantiki ya Muungano wenyewe na na ambazo zilisalimisha baadhi ya mam- kwamba kunachochea malalamiko ya laka yake hayo kwenye chombo kimoja, haki kutoka kwa Watanzania wa Bara. huku kila upande ukibakia na sehemu Si jambo la haki hata kidogo, kwa mfano, nyingine ya mamlaka yake. kwa Mzanzibari kuwa Waziri wa Habari, Huu si Muungano baina ya mkubwa na Utamaduni na Michezo, au Maliasili na mdogo panapohusika hadhi ya nchi ziliNishati, maana hayo si mambo ya Muunzoungana, maana eneo la kijiografia wala gano. Wako Watanzania wa Bara wenye idadi ya watu havikuwa vitu vilivyoamua uwezo mkubwa kuongoza wizara hizo. kuwepo na kutokuwepo kwa Muungano, kwa hivyo haviwezi leo kuamua uendes- Na hata Bungeni, si haki kwa wabunge kutoka Zanzibar kujadili na kuamua hwaji wa Muungano wenyewe. mambo ya Tanzania Bara ambayo si ya Pili, ni ukweli kwamba huu Muungano ni Muungano. Si haki pia kwa Serikali ya kitu kikubwa na muhimu sana kwa pande Muungano kuunda wizara ambazo zizote mbili za Muungano. nachanganya mambo yaliyo na yasiyo ya Wakati huo ndio uhalisia kuhusu Muun- Muungano katika kapu moja, kama ilivyo, kwa mfano, katika suala la elimu ya juu, gano, siasa za Serikali ya Muungano zinaonyesha vyengine. Angalia, kwa mfano, sayansi na teknolojia.
mjengeko wa Serikali hii katika uwiano Utatanishi wa kwanza unazalisha malwa nafasi zinazoshikiliwa na watu kutoka alamiko kwamba Wazanzibari wanafaipande hizi mbili kwenye wizara za Muun- dika na kudekezwa sana na Muungano
> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03
utawala ya Tanganyika kama kulivyo na mamlaka ya utawala ya Zanzibar, tutaen- la kimantiki kwa wakati mmoja: kwamba katika mjengeko wa utawala serikalini, delea kuwa mbali kabisa na uhalisia wa majina ya vyeo vya wakuu wa vitengo
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
>
hunasibiana na vitengo vyao, kwa mfano mkuu wa kurugenzi ni mkurugenzi na mkuu wa wizara ni waziri.
njaa na kiu). La kujiuliza ni ikiwa hivi kweli Muungano huu uliumbwa na roho ya kushiba na kukinai au uliKutokana na kupuuzwa na kudharauli- umbwa na uroho wa kufakamia na wa kwa makusudi kwa matatizo ya Mu- kusaza kila kitu? Ikiwa hivyo ndivyo, ungano huu, hakujawahi kupita muongo kuna siku kutakuwa na cha Zanzibar ambapo Muungano hautikiswi na kutena na, au, cha Tanzania Bara peke tikisika. Kwa bahati mbaya ni kwamba, yake?
kila Muungano unapotikisika, machoni mwa wakubwa huonekana kama kwamba unatikisika kwa kuwa hauna mambo ya kutosha.
38
Na, hivyo, kama vile Mfalme Jeta wa Shaaban Robert alivyokuwa akila na kunywa kila kilichopo, basi nao wakubwa huzidi kuumiminia Muungano kila cha Zanzibar na kila cha Tanzania Bara tumboni mwake. Hilo ni kosa kubwa katika sayansi ya utatuzi wa migogoro. Wapemba husema: Ganga shina, matawi hayagangika! kwa maana ya kuwa, kutibu maradhi ni kukitibu chanzo chake na sio dalili zake. Ni kosa kutokujiuliza kwa nini Muungano huu unatikisika (haushibi) na kujiuliza tu vipi unatikisika (unalilia
Baadhi ya wakati Wazanzibari hukumbushwa na wenzao wa Bara ule msemo wa Kiingereza usemao: You cannot eat your cake and have it! kwa maana ya kuwa mtu hawezi kuila keki yake na bado akaendelea kuwa nayo. Ni ama aile imalizike na asiwe nayo au asiile kabisa ikiwa anataka kubakia nayo. Lakini kuna upande mwengine wa ukweli katika suala hili la keki: nao ni kuwa kuna mtu asiyeila keki yake na bado asiwe nayo na mwengine anayeila keki yake na akaendelea kuwa nayo. Ndivyo siasa za Muungano kuelekea Zanzibar zilivyothibitisha kwa nusu karne hii ya kuwepo kwake.
Abdul Hamid Zanzibar na Tanganyika ziliungana kama nchi mbili huru bila ya kuzingatia ukubwa na wingi wa watu wake, hivyo ni vyema kama kweli viongozi wanataka kuuenzi Muungano huu ni lazima waondoshe fikira za udogo wa Zanzibar na watu wake katika maamuzi na migao ya fedha kama mshirika sawa wa muungano. Akili Idd Tuliza Nadhani huo utakuwa ndio mwisho wa CCM kutawala Zanzibar. Abdul Hamid Huu ni udhaifu wa kisiasa ulioneshwa na viongozi wa CCM/Zanzibar baada ya kushindwa kujibu hoja za Mh.Mansoor na badala yake kuanza kutoa maneno machafu na matusi ya nguoni. Jambo muhimu ni kumuomba Mh.Mansoor kupuuza matusi yao ili kutowapa mwanya wahafidhina kuendeleza siasa zao za chuki na husda katika Zanzibar yetu. Ustaadh Harith naam jina la ccm bado linaendelea kuwa baya zanzibar katika vichwa vya wasomi na wenye akili maana huwezi kusikiliza mkutano wa ccm wewe na familia yako. mi nawaomba wajirekebishe kinyume chake watakimbiwa na wanachama kila siku. Rajab Juma Othman Hii ni mbegu walioipanda wenyewe walipata nafac ya utawala na wakashindwa kuitetea nchi walikua wanadili na cuf tu hebu ikumbuke kauli ya kiungwana iliotolewa na maalim Seif NITAKUA NANYINYI NIKIWA NDANI YA CCM NA NJE YA CCM Abdul Hamid Huu ni udhalilishwaji kwa viongozi wetu wa Zanzibar kwani wakiukaji wa sera ya Muungano wapo wengi sana akiwemo yeye Naibu Spika wa Bunge la Muungano, aliyerikodiwa akipigia debe muundo wa serikali tatu lakini ccm dodoma hawakumfukuza na wala hawakumletea maneno yasio na maana. Inaendelea Uk. 47
39
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete [kushoto] na Makamo Mwenyeki wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
40
N A M U S TA FA S H A R I F
.
adhia ya kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansoor Yussuf Himid, imewagusa Wazanzibari wengi. Wapo waliofurahishwa na kufukuzwa kwake na walioona kuwa wamepata ushindi. Hawa ni wale tunaowaita siku hizi kuwa ni wahafidhina, waliokuwa wakikerwa na kukereketwa kwa kazi aliyokuwaakiifanya. Wako waliosikitishwa na kuvunjwa moyo na uamuzi huu wakilalamika wakiiona CCM kama
ni adui wa Zanzibar na maslahi yake. Hawa wanaamini kuwa kilichomfukuzisha Mansoor ni kusimama kwake kidete kuitetea nchi yake ya Zanzibar na maslahi yake ndani ya Muungano. Wanavyoona ni kwamba Mansoor ameponzwa na juhudi zake za kuleta maridhiano, umoja na heshima miongoni mwa Wazanzibari na za kuhakikisha kuwa wanaungana katika kusimamia mambo yenye maslahi na taifa lao la Zanzibar na vizazi vyake vya baadaye. Lakini kuna kundi maalum la Wazanzibari
ambalo limeathirika zaidi na moja kwa moja kutokana na sakata hili. Nalo ni la wananchi wa jimbo la Kiembesamaki ambalo mwakilishi wake alikuwa Mansoor. Ijapokuwa CCM ndiyo iliyomdhamini Mansoor kubeba bendera yake na kusimama kama mgombea wa nafasi ya uwakilishi katika jimbo hilo, lakini ni juhudi za wanajimbo ndizo zilizompeleka mwakilishi wao huyo katika Baraza la Wawakilishi, na si CCM kama CCM. Ni wananchi ndio waliohimizana, wakapigana kampeni na hatimaye wakasimama
misusuru kwa misururu kupiga kura zao na kuhakikisha wanamchagua mwakilishi wanayemtaka. Hawakujali mvua wala jua, njaa wala kiu, lakini walichokuwa wakikitaka ni kumuona Mansoor anakuwa mwakilishi wao. Na haya hayakutokea mara moja. Mara zaidi ya moja, wananchi wa jimbo hilo, tokea pale alipoingia katika ulimwengu wa siasa, walimridhia na
41
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
kumpa imani na kura zao ili awe kiongozi wao wa jimbo. Hata katika uchaguzi wa 2010 na uliofanywa baada ya Mansoor na wenzake kufanikiwa kuleta Maridhiano ya Wazanzibari jambo ambalo liliwakera sana wanaCCM wahafidhina na pengine ikawa miongoni mwa vyanzo vya kumfika yaliyomfika wananchi hawakusita kumpa kura zao na kukubali kuongozwa naye. Vyereje leo wakatoke watu wachache na sababu zao tu, wakaseme wanamfukuza mwakilishi wa watu eti kwa sababu amekwenda kinyume na sera ya chama (kama kweli amekwenda kinyume), bali si matakwa ya wananchi waliomchagua na anaowaongoza? Kwa imani yangu, si kila aliyempigia kura Mansoor alikuwa mwanaCCM, bali wanachama wa vyama vyengine na wale wasiokuwa na vyama pia walimtilia voti zao. Kwa hali hii, watu wa Kiembesamaki wamenyanganywa haki yao waliyoipata kidemokrasia, wamepotezewa kiongozi mpenda watu wote wa jimbo lake, vijana, wazee, kike kwa kiume. Watu hawa wameondolewa mwenzao anayependa maendeleo yao na aliyekuwa na msaada mkubwa wa hali na mali kwao.
lichokifanikisha, lakini hawakujua kuwa ukiujuwa huu, huu huwiji. Ni dhahiri kwamba viongozi wa CCM Kisiwandui Zanzibar ndio waliokuwa wakishadidia na kuisukuma CCM Makao Makuu Dodoma kumfukuza Mansoor kwa sababu wakati wote wao wenyewe wamekuwa wakilisema hili. Ni wao waliolianza na walihakikisha kwamba watafanikiwa. Wahafidhina wa Zanzibar wamekuwa na chuki dhidi ya Mansoor na kutokana na kufanikiwa kwake katika mengi. Nasema kufanikiwa, maana tafsiri ya jina Mansoor niliyoipata kwenye mtandao wenye majina ya watoto wa Kiislamu ni mshindi. Na, naam, Mansoor amewashinda kwa mengi. Miongoni mwao ni hili la kusimama pamoja na Kamati ya Maridhiano ya Mzee Hassan Nassor Moyo kuhakikisha Wazanzibari wanazika tafauti zao ili waweze kusimamia mambo yao na kujifunza kukubaliana pale wanapotafautiana. Jambo hili kwa kiasi kikubwa limefinikiwa, Alhamdulillah.
matakwa haya ya wahafidhina awali, lakini ukweli ni kwamba ilikuwa inafurahia. Mzanzibari yeyote anayesimama dhidi ya Muungano, kichwa chake ni halali ya Chimwaga.
Tanganyika ndiko inakosalitiwa zaidi kuanzia kwenye maagizo yake, sera zake mpaka mali zake lakini hujasikia kufukuzwa mtu.
42
Lakini la ushindi wa Mansoor na wenzake limekuwa mwiba mkali kwa wahafidhina na wasioitakia mema Zanzibar, ambao siku zote wanataka kuiona ikiwa nyuma tu kwa hali yoyote. Ndipo wakaamua Kwa kukurupuka huku walikokurupukumuwekea kisasi cha kumuadhibu, na ka CCM bila ya kuwasikiliza wananchi kama wasemavyo wenyewe, hata bado, wa Kiembesamaki, naona kwa maneno kwa maana ya kwamba hawataishia ya vijana wa kileo itakula kwao, kwani wana wa Kiembesamaki wanamjua nani hapo. Uvumi ni kwamba sasa wanamMansoor na wako tayari kumsikiliza ata- pikia jungu Rais Mstaafu Amani Karume ili naye wamuadhirishe kama alivyowaakachokisema na kumfuata popote pale dhirisha wao, kwa kuwaletea Maridhiano atakapokwenda, kwani yeye ndiye kiongozi wao waliyemchagua na kumridhia. na Serikali ya Umoja wa Kitaifa wasiyoitaka. Nasema itakula kwao wahafidhina wa CCM Zanzibar, ambao kwa kusaidiana na Dodoma, kwa upande wake, licha ya kuriwakoloni wa Dodoma wamefanikisha wa- potiwa kwamba ilikuwa inapingana na
> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03
Lakini kwa sababu mshtakiwa alikuwa Si siri kwamba Mansoor amekuwa mstari Mzanzibari, tena aliyeshtakiwa na mawakala wa ukoloni, kwa kosa la kupingawa mbele katika kusimama na kutetea na na ukoloni basi mkoloni hakuona uzito Mfumo wa Muungano utakaoirejeshea wa kushusha hukumu yake. Hukumu heshima yake Zanzibar. Hivyo, ni wazi kwamba kwa kujitangaza alivyojitangaza, hii, hata hivyo, haitashushwa kwa akina Phillip Mangula anayetaka Serikali Moja, mbele ya CCM Dodoma Mansoor alishawala Job Ndugai na wenziwe wanaotaka saini hati yake ya kifo, nao wakawa wapia Serikali Tatu kama Mansoor. Hawa ni nasubiri apelekwe tu wamnyonge. wenyewe. Sababu ni kwamba alitishia maslahi ya Tanganyika ambayo inajiona kama mko- Nimalizie kwa kujumuisha nukta zangu loni ambaye ametawalishwa na Zanzibar mbili: moja, uhafidhina ndani ya CCM Kisiwandui ulilipika jungu la Mansoor na milele. utayapika na ya wengine, maana hauKama historia inavyotuonyesha, kudai taki mabadiliko. Lakini na ukoloni ndani maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano ya White House Dodoma nao umetumia ni kugombana na mkoloni. Na madhafursa hiyo kumpoteza mmoja wa wale li Mansoor amethubutu kulifanya hilo, wanaopingana na ukoloni. ameingia kwenye ugomvi na mkoloni. Na madhali wahafidhina, vibaraka wa Imani yangu kubwa ni kuwa mkoloni ukoloni wapo na wakoloni wenyewe bado naye yumo katika kupika jungu hili au wana nguvu, basi tutaona mengi sana kama hajapika japo kwenye kulila hatoki mwaka huu. Sababu ni kuwa sisi Wazankwani nnachokiamini mimi migogoro zibari tumeamua kuvunja mahusiano ndani ya CCM haipo Zanzibar tu, na kama makongwe na mtawala. kusalitiwa CCM haisalitiwi Zanzibar tu.
43
Unaweza kutangaza biashara yako kupitia Zanzibar Daima Online, jarida la kila wiki mbili lenye wasomaji wengi wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili duniani kote.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
>
Zanzibar sifa mbele ya wenziwe. Lakini kwa wenye akili ndiyo pia ishara ya kuonyesha kuwa sasa CCM si imara tena, maana uimara wa chama haupo kwenye matusi hata kidogo.
44
N A S A LU M A B D A L L A H
dugu wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, tupatieni mgombea atakayekidhi matarajio ya wananchi na sio matarajio yako wewe mpigakura. Tupatieni mgombea atakayekidhi matarajio ya Watanzania. Watanzania wanahitaji mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Hii ilikuwa ni kauli ya Mwalimu Julius Nyerere, wakati huo akimpigia debe mgombea wake wa urais abebe bendera ya CCM katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, mwaka 1995. Nyerere aliuacha wasia huo na kila siku wanaCCM hujidai kuukariri, lakini ukweli ni kuwa wameisahau maana yake. Na ni kuusahau ama kuupuuza kwao ndiko kunakowafanya warudi nyuma badala ya kwenda mbele.
Ukweli ni kuwa Tanzania inaenda mbele na CCM inarudi nyuma. Binafsi nilidhani yale ya 1984 ya kuangushwa Aboud Jumbe, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania na juu ya yote Makamu Mwenyekiti wa CCM, na baada ya kufukuzwa chamani Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake sita miaka minne baadaye, yalitokea kipindi kile cha nyuma kwa sababu tulikuwa kwenye kiza Lakini leo tupo kwenye mwangaza na yanatokea yale yale. Kufukuzwa kwa Mansoor Yussuf Himid ni ishara inayotosha kuwa CCM inarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Na baada ya kumwangusha Mansoor Dodoma, sasa wanaonekana wamechanganyikiwa na uamuzi walioufanya wao
CCM imekuwa haina adabu hata kwa Rais wa Zanzibar ambaye anatokea CCM, Dk. Ali Mohamed Shein. Hivi karibuni tulishuhudia bango kubwa kwenye mkutano CCM imeyaandika maandishi haya ukuta- wa Kibanda Maiti, ambao ulihutubiwa na ni na kuyaacha hapo hapo kama sanamu mwenyewe Dk. Shein, limeandikwa Walisilo na maana kwao. Hawayaheshimu. naotaka Nkataba wende kwao. Hilo neno Hawajifunzi kwayo. Nkataba liliandikwa hivyo wakimaanisha wanaotaka hivyo ni Wapemba na hivyo Matokeo yake? CCM imekuwa si imara wao ndio waende kwao Pemba. Rais wa tena na sasa ndio maana Tanzania imenchi hii ni Mpemba. Ni ufedhuli mkubwa anza kuyumba. Lau ingelitambua kuwa huu. wakati unabadilika visiwani Zanzibar na ingekubali kuibeba dhana ya Mamlaka Kuelekea shinikizo la kumfukuza ManKamili kwa visiwa hivyo, basi leo CCM in- soor, mmoja wa wanaCCM hao alisema gejizolea wanachama wengi zaidi, ingeiwazi wazi mbele ya Rais Shein kwamba marika zaidi na pingine huo ungekuwa ati tuuvunje muungano wa Unguja na mwisho wa vyama vya CHADEMA, CUF na Pemba, Pemba wawe na nchi yao na sisi vyengine humu Visiwani. Unguja tubakie kwenye Muungano wetu Walichobaki nacho CCM ni nini? Nguvu za vyombo vya dola na matusi ya majukwaani. Leo ili uonekane mwanaCCM kindakindaki ni lazima uwe unatukana vyama vyengine hata viongozi wakuu wa nchi, bora tu wawe hawatokei kwenye kundi la kihafidhina la chama chako. Kumtukana Maalim Seif, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, hadharani na viongozi wengine ni ishara inayotosha kumpa mwanaCCM wa na Tanganyika, huku akidai aonyeshwe hati ya Muungano wa Unguja na Pemba.
45
Huu ni uhaini. WanaCCM wameishiwa na hoja. Wanasema wazi wazi tuwatoe Wapemba wakaunde serikali yao. Basi na wamtoe sio tu Maalim Seif, bali pia Rais Shein, Waziri Muhammed Aboud na wenzao wengine wakaunde serikali yao Pemba na Unguja iwe wilaya ya Dar es Salaam. Leo CCM imeacha kupigana na ufisadi na
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
>
Kutoka Uk.39
imekuwa inapigana na wasema kweli, wanaotaka mabadiliko na demokrasia isimame. Kosa kubwa la hao wanaopigwa vita ni kusema kweli kwamba Wazanzibari sasa wanataka Muungano wenye haki, usawa na heshima kati ya nchi yao na Tanganyika. Mara kadhaa CCM Dodoma imekuwa ukiichagulia Zanzibar hata Rais, kiongozi mkuu wa nchi ambaye hakidhi matarajio ya nchi. Chini chini CCM/Zanzibar hukwambia kuwa hawaipendi Dodoma. Ukiwauliza kwa nini, watakwambia kuwa huwa inawaletea viongozi wasiowataka. Lakini maajabu ni kwamba wanaCCM hao hao wa Zanzibar, wakitaka kumgeuka mwenzao, hukimbilia huko huko Dodoma wasipokupenda kwenda kumchinjia na kurudi na damu mikononi mwao, wakasherehekea Kisiwandui. Tunaotaka mabadiliko ambayo kwenye CCM hatujayapata tunaisubiri kwa hamu tuizike CCM 2015, maana tayari tumeshajuwa wapi tutakapoyapata mabadiliko. CCM isahau kuwa itayazima maamuzi ya wananchi walio wengi. Umma umewakataa. Kwenye akili zao wana fikra zile zile zilopitwa na wakati kuwa Chama kinawekwa madarakani na dola. Wamesahau kuwa Chama huwekwa madarakani na wananchi, ndio maana leo wanakimbilia polisi na jeshi.
Nassor Shaame Kwa maoni yangu kufukuzwa kwa wanachama wa CCM kwa kupigania maslahi ya Zanzibar si jambo geni wapo walio makundi mengi alianza na Mzee jumbe na dhana yake moja na moja tatu akawajibishwa, wakafuatia kundi la Wasomi vijana ndani ya CCM na leo tunashuhudia kijana mansoor naye akiingia katika hishoria ya kupigania maslahi ya Zanzibar. Wazanzibari wako nyuma yake kamwe hatutakodisha nyumba kwa kupata kilo ya mchele. Rashid Mohammed Wazanzibari ccm sio chama chetu wabunge wametoa maoni yao ya serikali tatu lakini wao ni Watanganyika hawavunji ilani ya chama. Omar Hussein Zanzibar imekua ikisifika kama ni visiwa vya watu wastaarabu kwa karne nyingi, na ustaarabu wa watu wa Zanzibar ndio umepelekea sehemu za Bara pia kustaarabika kutokana na mchanganyiko baina yao na Wanzibari, kwa muda sasa tumeona ustaarabu huu umeanza kupotea kwa njia moja au nyengine. CCM ni chama chenye uzoefu wa kuongoza kuliko chama chochote cha siasa, mambo wanayoyafanya isingeingia akilini kwa mtu kusikia kwamba CCM ndio kinara wa mambo hayo,kejeli kashfa, matusi tena ya nguoni ambayo ni aibu jamii kukaa na kuyasikiliza ndio imegeuka kua ilani na sera ya CCM zanzibar tena watu hushangiria pale muhubiri aliye jukwaani akiporomosha mvua ya matusi na wengine humpa pesa kama ni tunza kwa ujinga anaoufanya, kwa kweli inasikitisha, CCM/UVCCM Zanzibar hawawezi kufanya mkutano bila kumwaga shehena ya matusi,kupandikiza chuki na uhasama baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kwa kisingizio cha U-Pemba na U-Unguja kwa kutaka watu warudi kule walikotoka, kweli hii inaashiria kushindwa kisera na kuamua kugeuza viwanja vya siasa kua ni viwanja vya matusi, wengi wetu tungetegemea kwa kipindi hichi kigumu katika upinzani wa nyama vingi na mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya CCM wangekuja na sera zenye mvuto na ushawishi wa hali ya juu ili kurejesha na kujenga imani kwa wananchi waliowaweka madarakani kwa kuwaeleza kwa nini wao wanapigania sera ya serikali mbili na kwa nini wanapinga sera ya serikali tatu,lakini haikua hivyo. Mimi hujiuliza hivi ni kwa sababu viongozi wengi wa CCM/UVCCM Zanzibar hawajasoma? Lakini mbona kuna wengine wana elimu zao kwa nini hawa wasiwe wakosoaji na wakatazaji kwa wale ambao hawakubahatika kupita skuli wakafuta angalau ujinga? au hawa watoaji wa matusi na uchochezi ni wahamiaji na sio miongoni mwa Wazanzibari ambao wanasifika duniani kwa ustaarabu wao? Kwa kweli sipati jibu, kwa kweli kama wameona kufanya hivi ndio kujenga vguvu zaidi kwa wanachama wao kuelekea ushindi mwaka 2015 na ndiko kutakakozima harakati za Wazanzibari kupigania mamlaka kamili ya nchi yao kwa kweli wamegonga mbuyu, Wazanzibari walisha amshwa, wako macho na wamesha elimika na wameshachoka na siasa za chuki na uhasama na sasa wanataka amani upendo na mshikamano katika jamii, CCM/UVCCM Zanzibar wameshapoteza dira na wanaelekea kugonga mwamba.
46
47
Hoja wanazozitoa ndio njia mwafaka kwao kuelekea Mamlaka Kamili. Basi bye Tayari CCM Zanzibar ishaleta mapandikizi bye CCM. Nyerere alishatuusia kuwa mabadiliko tutayapata kwengine, madhali watakaopiga kura katika Kura ya Maoni na katika Uchaguzi Mkuu. Lengo ni kuta- tumeyakosa kwako. Na kama alivyosema ka Mamlaka Kamili Zanzibar yasisimame Mansoor majuzi pale Bwawani, hayo na CUF isishinde kwenye Uchaguzi Mkuu. yanakuja tartiib.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
LADHA YA BETI
>
Mcheza Kwao
Kucheza tucheze kwetu, kwetu tulikozaliwa Kunako wazazi wetu, wazazi waheshimiwa Heshima asili yetu, tuiombe tutapewa Vijana tucheze shime, hima tutaaminiwa Tucheze kike kiume, hamna kubaguliwa Tucheze tusisimame, mchezo hautakuwa Tucheze tufanye ari, tukijua tutapewa Tuzipandishe na mori, na kwa nguvu tulizopewa Wazee wakitukiri, zawadi tutachukuwa Hili halina ubishi, kwetu tukikuchaguwa Kwazidisha ushawishi, mchezo tukanogewa Kwetu michezo haishi, kila tutapoamua Nasisitiza kwa leo, na maneno kufungiwa Hajuti mcheza kwao, hata akikosolewa Anayo mapendeleo, kila mchezo ukiwa Said O. Shoka Chake Chake Pemba
Kulikumba Jini
Utumwa naliopewa, nende kwa jini nifike Hamshike sawasawa, nimfunge afungike Ashindwe jipapatuwa, chupani nimfundike Kisha nende panganikwe, silisili kumtia Na vifaa nikapewa, na nyenzo za uhakika Makombe hazinguliwa, ya kunywa na ya kupaka Na kafara hasomewa, na hirizi hajivika Alipo nikamfika, lengo kwenda mchukuwa Halikuta kubwa jini, lisilo mfano wake Tangu juu hadi chini, sioni khatima yake Katikati msituni, meketi kitini pake Bali nisitetemeke, nili nikijiamini Havitoa viapio, sauti ya kushituka Hamwamba Hima njoo, na maguuni anguka! Ela sijesema nyoo, mdomo sijefumbuka! Naye wala hekanuka, hekaidi ninenayo! Hali kapinda magoti, na u chini uso wake Kwayo nyepesi sauti, na nzuri ladha yake Kanamba: Sikaze nati, nitume nikatumike! Nusura chozi litoke, kwa huruma na laiti Nikawa swahibu yake, hajikuta aniteka Kama mtu na mwenzake, tulozoeana myaka Yalokuwa dhidi yake, yote yakanitoweka Naye kwangu kadhalika, nikawa ni mwenza wake Kwetu watu wakangoja, majibu niyapeleke Nirudi nivikwe koja, shujaa nieleweke Zenda saa siku zaja, neno langu sisikike Lotumwa nikamshike, mekuwa wangu mbeja!
Mohammed Ghassani Bonn Ujerumani
48
49
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
NA MOHAMMED GHASSANI
[Sehemu ya Mwisho]
zuia kudra. (uk. 91) Wasemavyo wamalenga: Muda na kudura hazina zisubirio, ndivyo ambavyo wakati ulivyolazimisha kuja kwa vyama vingi hata kama wakubwa walikuwa hawavitaki. Kwa hivyo, nyoka (siasa za vyama vingi) hakuweza kuzuilika kuingia katika chumba cha Bwan Tajir (nchini). Watawala na mawakala wao katika vyombo vya habari, vyombo vya dola, taasisi za kijamii na kwengineko, hawakuwa na uwezo wa kuvizuia vyama vingi visirudi, kwa kuwa hayo yalikuwa ni matakwa ya wakati. yao, kama vile Bwan Tajir anavyoogopa kuwa nyoka angelimfichulia aibu zake za woga na ugoigoi. Kupitia mdomo wa Bwan Tajir, serikali ya chama tawala inamkaripia mtu inayedhani kuwa amechangia kurudi kwa vyama vingi: Usiniambie mie habari ya (nyoka) kutoka wapimie nilikwambia naogopa nyoka. Nilikukabidhi kazi ya kuhakikisha nyoka sio tu hawaonekani, lakini pia wasikaribie nilipo. (Uk. 91) Ukweli ni kuwa, laiti serikali ya chama tawala ingelikuwa na uwezo wa kuzuia vyama vingi visije, ingelifanya hivyo. Lakini kilichotokea ni kuwa wakati ulikuwa umeshafika, na hakuna ambaye angelikinzana na matakwa ya wakati, kama Ya Zanzibar na Jumba Maro ni mama mmoja, baba mmoja. vile anavyosema Nokoa Mkuu, ambaye alituhumiwa na kuhukumiwa kwa kumruhusu nyoka kupita hadi chumbani kwa Bwan Tajir, kwamba: Sina uwezo wa kuLakini ikiwa walishindwa na hicho, kuna chengine ambacho waliweza kukifanya: nacho ni kuandaa mikakati na mbinu za kuvizuia vyama hivi kuwaondoa wao madarakani. Na karamu (chaguzi) za magube na varange ndiyo ikawa njia ya wao kujihalalishia kuendelea kubakia madarakani huku wakiudanganya ulimwengu kuwa na wao wana demokrasia ya vyama vingi. Ndivyo karamu ilivyoandaliwa katika Jumba Maro. Bwan Tajir alimtafuta Shawishi Mkuu kuwa muandaaji na mpishi wake. Shawishi huyu akawa na jukumu moja tu: kwa upande mmoja, kuhakikisha kuwa
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
Karamu ya maro
TUFUNGUE KITABU
>
N
50
ilitangulia kusema kuwa dhima ya mchambuzi/mhakiki wa kazi ya fasihi ni kuirejesha kazi watuni, yaani kuisaidia jamii kujisoma baina ya mistari ya msanii. Na hili ndilo nitalolifanya sasa kwa kuwasaidia wenzangu kujiona walivyo kupitia mistari hii michache ya Ally Saleh katika Karamu. Natokea Zanzibar kama alivyo mwandishi wa Jumba Maro. Ni maoni yangu kwamba Karamu hii aliyoiwasilisha Ally Saleh inaakisi moja kwa moja chaguzi zetu katika mfumo wa vyama vingi. Ninaamini pana mfanano mkubwa baina ya maandalizi, uendeshaji na matokeo ya chaguzi zetu ndani ya mfumo huu wa vyama vingi na karamu hii ya Bwan Tajir (ambaye kwa tafsiri yangu ni serikali ya chama tawala). Ule mkasa wa kuingia kwa nyoka katika chumba cha Bwan Tajir naufananisha na kuja kwa siasa za vyama vingi katika nchi, ambazo zilijipenyeza bila ya ridhaa ya dhati ya watawala. Siku zote watawala wamekuwa wakiogopa kuwa upinzani utahatarisha maslahi
51
>
>
watu wengi zaidi wenye haki ya kula karamu hiyo hawapati fursa na, kwa upande mwingine, wale wasio na haki hiyo, lakini ambao kula kwao kutakuwa kwa faida ya Bwan Tajir, wanaila kwa matonge na kwa kufuta sinia mbili mbili. Kwa ufupi, Shawishi Mkuu alikuwa na dhima ya kuifuja karamu. Ndivyo ilivyo katika uhalisia. Kwamba katika kuandaa mazingira ya kuendelea kubakia madarakani, watawala wanawatafuta akina mashawishi wakuu na kuwafanya wawe na mamlaka ya kuandaa na kusimamia chaguzi ziitwazo za vyama vingi. Kwa maana nyengine ni kuwa watawala wanajiundia mitandao inayohawakikishia kuwepo kwao madarakani dumu daima, hata pale umma (watu wazima wa mji) utakapokuwa umeshawakataa. Hiki ndicho kinafanyika hadi leo Zanzibar, ambako mtandao madhubuti wa masheha, vyombo vya dola na Tume ya Uchaguzi, unahakikisha kuwa Wazanzibari wengi wenye haki ya kupiga kura hawaandikishwi kuwa wapiga kura, kwa upande mmoja na, kwa upande mwingine, wale wasiokuwa na sifa, lakini ambao wanatumiwa kukipigia kura chama tawala wanaandikishwa ikibidi hata zaidi ya mara moja. (Rejea ripoti ya TEMCO/REDET: The Politics of the PVR, 2005) Mkasa wa Karamu ya Jumba Maro kuliwa na watoto wadogo huku watu wazima wakitazama macho tu, ndio mkasa wa kura za majimbo kadhaa ya Zanzibar ambako kura zinazoambiwa zimemchagua mgombea fulani hupigwa na watu wasiotimia umri huku washaotimia wakilia machozi. Mkasa wa watu wachache kula sahani mbili mbili za biriani huku wengine wakienda miayo kwa njaa, ndiyo mkasa wa upigaji kura zaidi ya mara moja katika
> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03
52
53
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
MICHEZO
>
NA BABU JIMBE
akuna ajuaye wapi na lini mchezo wa kriketi (cricket) ulipoanza. Lakini inadhaniwa kuwa mchezo huu ulianzia katika maeneo ya Kent na Sussex huko Uingereza katika karne ya 17. Mchezo huu huchezwa zaidi katika nchi zilizowahi kutawaliwa na Mwingereza. Hapa Zanzibar kriketi ilianza kuchezwa rasmi mnamo mwaka wa 1890. Miaka sita baadaye mchezo huo ulizusha vita baina ya Uingereza na Zanzibar, vita vilivyodumu kwa muda wa dakika 37 na nukta 27 na ni vita vya muda mfupi kabisa hadi sasa katika historia ya vita duniani. Katika mwaka wa 1896 mlolongo wa manuwari za Kiingereza, bila ya kuomba ruhusa ya Sultan, zilitia nanga kwenye bandari ya Zanzibar ili wanamaji wake wende kuangalia mchezo wa kriketi uliokuwa unachezwa. Nahodha wa manuwari hizo Admeri Sir Harry Rawson aliwaamrisha mabahari wake wateremke ili wende kuangalia mchezo wa siku hiyo. Lakini Sultani, Seyyid Khalid bin Barghash, alikerwa kwa ujeuri wa Waingereza wa kutia nanga manuwari zao kwenye bandari ya Unguja bila ya kuomba ruhusa ya serikali yake. Ndipo alipoamrisha manuwari za Kiingereza zishambuliwe. Agosti 27, 1896 meli yake Sultani iliyokuwa ikiitwa Glasgow ilifyetua mizinga kuhujumu meli za kivita za Kiingereza. Hapo tena manuwari
za Kiingereza nazo zikaishambulia Unguja kando kando ya Forodhani. Kasri ya mfalme ilibomolewa na kuwa kifusi na inakisiwa watu na askari wasiopungua 500 waliuawa. Seyyid Khalid alikimbilia kwenye Ubalozi wa Ujerumani kutafuta hifadhi. Awali mchezo huo wa kriketi ulikuwa ukichezwa na walowezi wa Kiingereza. Baadaye pakawa panafanywa mechi kati ya walowezi hao wa Kiingereza na mabaharia wa Kiingereza waliokuwa wakitia nanga meli zao bandarini, Unguja. Klabu ya mwanzo ya kriketi Zanzibar ilianzishwa 1922 na hao wazungu waliokuwa wakiishi hapa visiwani. Ya pili ilikuwa klabu ya Ithnaasheeri. Baadaye zikafwatia klabu za makabila mengine ya Waarabu, ya Comorian yaani jamii ya Wangazija, nay a Wahindi waliokuwa wafuasi wa madhehebu ya Ismaili wakiongozwa na Aga Khan. Skuli nazo zilikuwa na timu za kriketi kuanzia Government School, King George VI Grammar Secondary School (sasa Lumumba College), Hindu Union na skuli ya Aga Khan. Hapa Zanzibar mchezo huu ukipendwa zaidi na Wahindi lakini hata wasio Wahindi nao wakiucheza na kuliwakilisha taifa. Miongoni mwa Wahindi waliokuwa maarufu katika miaka ya 1950 na miaka ya mwanzo ya 1960 walikuwa Baker Tejani, Harji Mawji, Rusi Madon, Gajendra Doshi,
55
Gulam Golo Mshamba na Ahmed Bachoo. Kuna wenye kuamini ya kwamba Mzanzibari aliyekuwa stadi kuliko wote alikuwa Harji Mawji anayefananishwa na Gary Sobers, mzalia wa Barbados aliyekuwa akichezea timu ya West Indies. Kama Sobers Harji Mawji alibobea katika kriketi. Ukija kwenye kudima ndiye yeye aliyekuwa bingwa; ukija kwenye mbio za kasi za wastani za kurushia mpira yeye alikuwa bingwa; ukija kwenye waliokuwa mastadi katika kuurusha mpira mpaka ukawa unaviringika basi ni yeye Harji Mawji aliyekuwa bingwa. Harji Mawji alikuwa na jengine lililomfanya apendwe apendeke. Alikuwa Mhindi
pekee aliyekuwa akichezea soka katika timu ya Kikwajuni tena Division One. Isitoshe alikuwa pia hodari wa volley ball. Mfano wake ni kama ule wa kina Ahmed aliyekuwa amebobea katika michezo ya hoki, kriket na soka. Wachezaji maarufu wa kriket wasio Wahindi walikuwa kina Chepe, Simba Makwega. Wawili hao walianza kuiwakilisha Zanzibar katika mchezo huu katika miaka ya 1940. Mwingine alikuwa Mzee Saadati aliyekuwa akifanya kazi Mahakama Kuu. Huyu alikuwa mchezaji mahiri na alimvutia sana bosi wake Sir John Gray. Kila siku ya mechi Sir John akimpa ruhusa Mzee Saadati kwenda kucheza kriketi.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
>
Safari moja katika miaka ya 1950 timu ya Comorian ilikuwa inacheza na kwa vile Mzee Saadati akichezea timu ya Comorian alienda kuombewa ruhusa na mwalimu wa timu hiyo Mzee Ahmed Iddi Mjasiri, aliyekuwa pia akifanya kazi Mahakamani. Kwa mshangao Sir John akauliza Who is Saadati? Akajibiwa Your staff, (mfanyakazi wako) Basi Sir John kwa kebehi alijibu: Fine, I will give him permission and I will be among the spectators.(Sawa, ntampa ruhusa na mimi ntakuwa miongoni mwa watazamaji.) Mzee Sadati alikuwa ni mfunguaji na akafungua yeye pamoja na Ahmed Mshangama Bwamkubwa Shoto. Katika mchezo huo timu ya Comorian ilikuwa inacheza na timu ya Ithnaasheri na siku hiyo Mzee Saadati mchezo ulimpa uso kwani mpira wa mwanzo alipeleka boundary (mpaka) na kuweza kufikisha mizunguko (round) 60. Katika mchezo mwingine uliobakia kwenye kumbukumbu ni ule mchezo wa timu ya Afrika Kusini iliyotembelea Afrika ya
Mashariki 1958 na kucheza na Zanzibar. Katika mechi hiyo Zaghloul Ajmi akiwa bado ni mwanafunzi wa Skuli ya Gulioni alichaguliwa kuwemo katika mchanganyiko (combined) ya Zanzibar. La kufurahisha ni kuwa siku ya mchezo huo wanafunzi wote wa Gulioni kuanzia wa chumba cha tano walipewa ruhusa ya kuondoka na mapema ili wende kushangilia. Zaghalouli alikuwa ni katika wenye kufungua na alifungua katika mchezo huo ambao alikutana na watupaji hatari wa Afrika ya Kusini akiwemo Nat Adcock, T.L Goddard, , H.J Tayfield, R. J. Westcott na C.B van Ryneveld. Kati ya hao ni wale ambao wakirusha zinazoitwa bounce za hatari. Mmojawao alikuwa Westcott na mipira yake yote ya mwanzo ilichezwa vya kutosha bila ya kukwepwa na Zaghloul, Zanzibar ilishindwa katika mechi hiyo lakini walikiri wachezaji wa Afrika Kusini kuwa kushindwa kwa Zanzibar kulikuwa ni honourable defeat yaani kushindwa kwa heshima au kushindwa kiume. Tukijaaliwa tutaendelea wiki ijayo kueleza zaidi kuhusu jinsi kriketi ilivyokua imeshamiri Zanzibar
riketi ilianza kwa kuchezwa kwa mtindo wa Test ikiwa ni mchezo mmoja kuchezwa kwa siku tano na mchezo mwengine ni wa siku moja Fifty Fifty (50-50) na siku hizi umekuja mtindo ambao umepata umaarufu mkubwa ujulikanao kama Twenty-Twenty (T20). Kriketi ni kama mchezo wa kabumbu lakini sio kabumbu kwani kriketi nayo huchezwa na wachezaji 11 kwa kila timu kwa mtindo tafauti. Katika mchezo mmoja wa kriketi hupambana timu mbili na kunakuwako waamuzi wawili wanaoitwa Empire. Siku hizi kumeongezeka mwamuzi wa 3 ambaye kama kuna utata wa uamuzi na kunatakiwa itolewe rufaa, mwamuzi huyo huangalia kwenye televisheni marejeo ya mchezo na hukata uamuzi wake ima kuubakisha uamuzi uliotolea kiwanjani au kuutengua. Timu itakayopata kura baada ya kurushwa fedha huamua ama kuanza kucheza au kwenda uwanjani kudima. Nahodha wa timu hutakiwa awe makini zaidi kujua iwapo kiwanja wanachokichezea kinatoa fursa kwa wapigaji au warushaji wa mpira. Ikiwa ni kwa wapigaji baada ya kushinda kwenye kura ataamua timu yao ianze na atawachagua watakaokwenda kufungua ikiwa ni wachezaji wawili na wengine tisa wakisubiri zamu zao zifike. Kiwanja cha kriketi kina ukubwa wa yadi 22 (20 cm) kwa marefu na futi 10 (3.0 m) mapana. Waamuzi hukaa katika kila upande mmoja. Anayerusha mpira hukaa upande wake na mchezaji ambaye huwa na bao la kuchezea hukaa na bao lake kusubiri mpira urushwe na nyuma ya mchezaji hukuweko golikipa wa mchezo huu ajulikanaye Wicketkeeper. Ukirushwa mpira na mpigaji akitoka alipo akenda alipo mwenzake huhesabiwa ni mzunguko mmoja (one round) na akipiga mpira ukatoka nje ya kamba maalumu iliyozungushwa kiwanjani hupata mizunguko minne (four runs). Na ukipigwa ukenda nje na kuvuka kamba pasi kutambaa hapo mpigaji hupata mizunguko sita (six runs) pasina kwenda yaani mmoja kutoka huku kwenda kule. Mchezaji hutolewa pale mpira uliorushwa akiupiga juu na ukadakwa au ukarushwa mpira na kumpiga mguu wa kushoto (lbw) kabla ya kuupiga, au kuviangusha vijiti (stumps) na akitolewa mchezaji mmoja hujiunga mchezaji mwengine kati ya wale tisa waliobaki nje wakisubiri zamu zao. Kila mrushaji mpira hurusha mipira sita kwa mara moja. Katika mchezo wa siku moja ujulikanao kama 50-50 katika mchezo mmoja kwa wastani hurushwa mipira 300. Mchezo wa kriketi hutaka mtu awe anajua hesabu kuweza kujua maendeleo yake na ili timu iweze kushinda ijipange pangaje.
56
57
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
uzi tulipata taarifa kuwa hatimaye Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesaini mkataba na kampuni moja ya Uholanzi kuhusu wa utafiti na pengine baadaye uchimbaji wa mafuta.
>
Hatua hii tulikuwa tukiisubiri sana kama si zaidi ya sana. Hapa si pahala pa kurudia misukosuko na mashaka ya uchimbaji wa nishati hiyo ambayo sio tu ni muhimu ila pia ni ya lazima kwa maendeleo na uchumi wa Zanzibar. Hakuna popote pale duniani ambapo nishati hii haikuweza kubadilisha hali za watu wake, ingawa kuna baadhi ya sehemu ambapo petroli na mazao yake yote yanayopatikana yamekuwa ni laana kwa nchi hizo. Lakini hizo si nchi nyingi. Kwa hivyo si mifano ya kutufanya tuogope. Nchi hizo chache ni mifano ya kutufanya tuwe na hadhari, tuwe macho kwa sababu nishati hiyo inaweza kuwa ya maumivu makubwa kwetu na vizazi vijavyo. Kwa hivyo, wakati tunapoanza kujiweka sawa na suala zima la uchimbaji wa mafuta jambo la kwanza kabisa ni kujitayarisha kwa miundombinu ya uchimbaji mafuta wa salama na wa maslahi kwa watu wetu. Ni ushauri wangu, kwa hivyo, kwamba kama ilikuwa hatujaanza basi natuanze haraka kutandika mipango na miundombinu ya kuhakikisha kuwa rasilmali hiyo inakuwa ni ya Wazanzibari wote na tusianze kama ilivyoanza kutokea Mtwara au Ogoni, Nigeria, au kwengineko. Katika hili pia kuna mfuko wa utajiri wa taifa (sovereign wealth fund) ambayo nchi ya Angola, kwa mfano, imeuanzisha. Hapa kuna mifano mikubwa ya nchi kama China, Qatar, Singapore, Abu Dhabi na sasa Mauritius ambazo zimepanua na kujichimbia kiuchumi kwa kubuni mashirika kadhaa ya uwekezaji wa kitaifa kwa maslahi ya nchi yetu.
58
59
Mashirika ya ndege kama ya Qatar, Singapore; makampuni Pili, ni wakati huu tunapopaswa kujitayariya uwekezaji tunaysha kwa mambo yote yanayohusu uchumi oyaona yanachipuka na uwekezaji wake. Hili ni suala la umuhimu huko China yote mkubwa na tuna mifano mingi ya kuiga duni matunda ya faida niani kama vile nchi za Qatar ilivyofanya kwa zinazotokana na gesi gesi asilia, au Oman ilivyofanya kwa mafuta au petroli lakini fedha na kadhalika. zinarudishwa kwa wazalendo kukuza Pia, huu ni wakati wa kujifunza juu ya suala la uwekezaji. uwekezaji maradufu ( re-investment) hatua ambayo ni muhimu katika kukuza utajiri ili Nimekuwa na fikra inayofanana na hiyo kwa tuweze kujitayarisha kukuza uchumi na nchi muda mrefu. Na fikra hii ilitokana pia na fikra isifadhaike pale mafuta yatapokwisha. inayofanana ya marehemu Ahmed Hassan Diria kuwa aliwahi kumshauri Rais Abeid Am> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03
na uhakika wa usafiri wa kubeba mazao na kuyaongeza thamani. Ni wazi kuwa kama Serikali ya Zanzibar ingewekeza katika eneo la kilimo Tanzania Bara
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >
>
TANZIA
>
N A M UA N D I S H I M A A LU M
aisha yanasonga mbele. Hayakusimama. Watu wanazaliwa na wanaendelea kuzaliwa siku hadi siku, ingawa watu hawa hutofautiana na watu kwa lugha na mataifa. Hivi ndivyo mwenyewe Muumba alivyofanya. Maamuzi yake ambayo hakika hayakuwa na ubaya wowote baada ya kumtayarisha binadamu huyu mazingira mazuri ya kuishi. Ni
binadamu hawa ndio maadui wakubwa kutokana na pumzi walizopewa bure na Muumba wakisahau hata siku ya mwisho siku, ambayo kila nafsi itauungama mbele yake Muumba. Dunia kweli ni uwanja wa fujo, na baada yote haya pumzi zitaziba na kuwa sasa ni zamu yako kuelekea kwake Muumba. Kwa hakika, hata na wale wanaokusin-
dikiza kwenye safari yako ya mwisho, nao itafika siku yao kama si leo basi kesho nao watakwenda katika njia hiyo hiyo uliyotangulia kuiandama na iliyotanguliwa kuandama na wa kabla yako. Hivyo mimi, kwa hakika, sitojutia kuwa Mtanzania mwenye asili ya Zanzibar, hata kama sina thamani yoyote katika taifa langu, kwani Mungu hakukosea
kuniteremsha kwa wazazi ambao ni Wazanzibari ambao baadae waliunganishwa na kuwa Tanzania, yumkini bila ya ridhaa yao na au kama waliridhia wenyewe, pasi kujua athari zake. Hapa Zanzibar, hata baada ya Serikali ya Mseto, bado watu wanazidi kuteseka na kubaguana kuanzia wao wenyewe hata kitaifa na kimataifa. Hebu jiulize,
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >
>
>
kuna sababu gani hata kufikia leo wahusika wa ajali ya meli ya Spice Islanders wakawa hawajachukuliwa na kupelekwa katika Mahakama ya Uhalifu dhidi ya ubinaadamu (ICC) kule mjini The Hague? Kwani hivi hawa wana tofauti gani na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto wa Kenya? Au pengine ni kwa kuwa wahanga wengi walikuwa ni nzige kutoka Pemba ambao hawana thamani katika taifa lao? Naandika kwa uchungu. Miaka miwili nyuma nilipoteza nuru ya moyo wangu mke wangu, ambaye ndio kwanza tulikuwa wanagenzi kwenye maisha ya kifamilia. Roho ya mke wangu ilikuwa miongoni mwa maelfu ya nyengine zilizozama usiku wa manane pasipokuwa na usaidizi wowote kwa uzembe na tamaa iliyotawala mkasa mzima wa kuzama kwa meli hiyo.
62
Spice Islanders na roho zote Nungwi, bali hata kwenye shimo la sahau. Taifa lisilokumbuka misiba yake, halioni thamani ya furaha yake. Ndiyo, sasa ni miaka miwili tokea meli hiyo yende kwenye mvungu wa bahari ya kina kirefu na roho za wapendwa wetu. Mayatima waliowachwa na wazazi wao wanataabika na wengine wakifa kidogo kidogo kutokana na kuathirika na mkasa mzima wa kupotelewa na wapenzi wao. Lakini hadi leo, hakuna CCM, Chadema, CUF au NCCR-Mageuzi ambao wamewahi kuishinikiza serikali angalau kuitambua tarehe 10 Septemba kama ni Siku ya Kumbukumbu ili japo kuwapa heshima wahanga hao. Miongoni mwa majibu wanayotoa wanasiasa hao ni kwamba Zanzibar haina utamaduni wa kuomboleza misiba yake milele kwa sababu ya mafungamano yake na dini ya Kiislamu. Lakini hili ni jawabu jepesi la kukwepa uwajibikaji. Ni ule ule tu usaliti wetu wa kawaida wa kutoana muhanga, tunapokosana kutolana sadaka dhahiri shahiri, basi angalau huzisaliti hisia na nyoyo zetu. Kwa kuunyamazia kimya msiba huu, sote kwa pamoja tunaisaliti Zanzibar yetu. Ni kweli kuwa Rais Ali Mohamed Shein aliunda Tume ya Uchunguzi baada ya ajali hiyo, lakini tangu mwanzo ilifahamika kwamba hicho kilikuwa kizungumkuti. Ulikuwa mchezo wa kuigiza, maana Tume ilipendekeza ya kuyapendekeza, lakini hakuna lililokuwa. Tuliwasaliti wahanga wa Spice Islanders. Leo hii maiti za watoto wadogo wasiokuwa na hatia, akinamama, vijana wabichi, waze na watu wazima, popote zilipo, naamini zinaamini kwamba zinajua nchi
yao na viongozi wao waziteua roho hizo ziwe chakula cha samaki. Ni kama vile waliambiwa: Kufeni, hamukuwa na thamani katika taifa lenu na ndio maana hata kaburi lenu lilikuwa ni meli!
Bado rikodi zipo zinazoonesha kuwa ile ni ajali iliyoweza kuepukwa. Hata pale abiria walipotoa ushauri hawakuziskilizwa kwani wengi wao walijua meli hiyo ilikuwa na mashaka makubwa kuvuuka kufika Pemba. Hadi leo, licha ya udogo wa Zanzibar, majibu ya wapi alipo nahodha wa meli hiyo ni kitendawili hadi leo. Hakuna ajuae maendeleo ya kesi hii ambayo imewagusa watu wengi, kwani kwa njia mmoja au nyengine hata vyombo vya habari vimesusia kutangaza maendeleo yake. Ni kama vile kila mtu kuanzia serikali inayoambiwa eti ndiyo mdhamini wa maisha na usalama wa raia wake, vyombo vya habari vinavyoambiwa eti ndiyo mdomo wa jamii, hadi asasi za kiraia zinazoambiwa eti ndiyo injini ya jamii inayowajibika na kuendelea, bali hata watu mmoja mmoja wameamua kuizika Mv
Lau serikali hii ingelikuwa kweli serikali ya watu, inayotokana na watu na kwa ajili ya watu, basi zamani ingelikuwa Ndiyo, tafsiri inabakia kuwa ni hiyo kwani imeshatangaza kwamba siku hii ni siku ya mapumziko na, kama si kukusanyika hata baada ya kufa kwao, hakuna fikira pamoja tukasoma khitima na kuwatakia zozote za kiutu zilizochukuliwa. Watoto dua maiti wetu, basi angalau kiongozi wa wao wanateseka bila misaada na wale waliopatwa na ulemavu wa kimwili na ki- nchi angelisoma risala ya kuwakumbuka saikolojia kutokana na kukumbwa na msi- na kulaani uzembe huu. ba huu mzito, hawana matibabu yoyote. Hawakuulizwa kala wala kalamu, zaidi ya Lakini waliokufa mule hawakuwa viongozi wa kisiasa, hawakuwa viongozi wa kijeshi, wengine tena baadhi yao tu kupata shilingi 500,000 miongoni mwa mamilioni hawakuwa watu mashuhuri. Walikuwa watu wa kawaida vitoto, mama zao, yaliyokusanywa na Ofisi ya Makamu wa baba zao, bibi na babu wanyonge tu wa Pili wa Rais. Mungu. Najua wako hawapendi kuyasikia sambe Miongoni mwa hao alikuwemo mke wankuyaona majumba yakiwa yameachwa gu. Na hata kama serikali yake hapa dunibila ya watoto au wazazi waliokuwamo ani imemsahau, mimi mumewe sitaacha kabla ya tarehe 10 Septemba 2011. Haya kumkumbuka. Serikali yetu mimi naye yote hayakuleta kimanzi kwa viongozi ndani ya nyumba mimi nikiwa Rais naye wetu angalau kuipa kisogo dunia na kuWaziri Mkuu haitamsahau daima. Kila wahurumia wahanga hawa masikini. Si siku hii itamtilia ubani na kumuombea wawakilishi, si wabunge waliokwenda dua. Itaulaani uzembe wa serikali ya akina katika majimbo yao kuwaulizia familia Dk. Shein, Maalim Seif Sharif na Balozi hizi zenye kumbukumbu ambayo inatSeif Iddi, ambayo inajifanya haina haja ambulika katika dunia kuwa ni miongoni naye.
63
Unaweza kutangaza biashara yako kupitia Zanzibar Daima Online, jarida la kila wiki mbili lenye wasomaji wengi wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili duniani kote.
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET
TOLEO 03 >