FOUNDER AND CEO SYG ( Start Young Global)!

Lina Shyma Gadi ni dada mwenye asili ya Tanzania anayeishi Uingereza, Lina anashahada ya Masoko na Matangazo (Marketing and Advetisement Systems) kutoka chuo kikuu cha Bedfordshire, Uingereza. Baada ya kumaliza na kuajiriwa kwa muda mfupi, Lina pamoja na vijana wenziwe akiwemo mdogo wake Natalie Jusnah Gadi maarufu DiamondLane London na Aaron Wallace walianzisha kampuni iitwayo Start Young Global kwa ajili ya kuwahamasisha wajasiriamali vijana na kubadilishana mawazo katika nyanja mbali mbali. Lina katika mchakato huu amafanikiwa kuendesha warsha ya ujasiria mali na kukaribishwa katika warsha mbali mbali kuzungumzia changamoto zinazo wakabili vijana katika kujiajiri, amewahi kukaribishwa katika nyumba ya bunge la Uingereza (House of Commons) kuzungumzia ajira na ujasiriamali kwa vijana, katika siku za karibu Lina anatarajia kuendesha maonyesho ya kwanza ya aina yake Uingereza kwa ajili ya wajasiria mali vijana chini ya miaka 30, kuonyesha na kutangaza biashara zao kwa dunia, hivi karibuni ametolewa katika gazeti la Yorkshire Times la Uingereza, soma hapa....!

!

! !

http://www.yorkshiretimes.co.uk/article/Plans-To-Put-On-The-UKs-First-YoungEntrepreneurs-Only-Exhibition.! Lina anashauku kubwa ya kushirikiana na vijana wenzie wajasiriamali na wale wenye nia ya kujiajiri kutoka pande zote za duniani katika kubadilishana mawazo na ushauri. Tembelea na ujiunge na mtandao wa SYG: startyoungglobal.com!

Lina Gadi akiwa na mshirika mwenza wa kibiashara Aaron Wallace, walipo karibishwa hivi karibuni kuchangia mada ya ujasiriamali kwenye kampuni MBTB Launch for young entrepreneurs.! !

! ! ! !

! ! ! ! !

Lina Gadi akitoa mada katika moja ya warsha iliyoendeshwa na SYG hivi karibuni mjini London Uingereza.!

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful