Taarifa kwa vyombo vya habari

:
Jumamosi, 28 Septemba 2013

Katibu wa Mambo ya Nje akaribisha ripoti ya IPCC juu ya Mabadiliko ya Tabia nchi

Jopo baina ya serikali na Umoja wa Mataifa katika Mabadiliko ya Tabia nchi (IPCC) limetoa ripoti ya tano ya tathmini; ripoti mpya katika sayansi ya tabia nchi kwa mara ya kwanza ndani ya miaka sita.
Mnamo Ijumaa, 27 Septemba 2013, IPCC ilichapa moja kati ya nakala tatu za ripoti ya tano ya tathmini, moja kati ya ripoti iliyosheheni tathmini za kisayansi juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Waziri wa Mambo ya Nje, William Hague alionyesha uhitaji wa haraka katika kushughulikia matokeo ya ripoti. Alisema; “Ripoti mpya ya kisanyansi ya jopo baina ya serikali na Umoja wa Mataifa katika Mabadiliko ya Tabia Nchi linathibitisha mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na shughuli za kibinadamu. Mazingira ya uwepo wa hali mbaya za hewa, yameongeza uwepo wa hatari katika maisha ya binadamu na mali, kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari, na kuyeyuka kwa barafu haraka zaidi ya ilivyotarajiwa. Ripoti ya IPCC inaonyesha wazi tusiposhughulikia sasa hivi kupunguza utolewaji wa gesi ya ukaa, yote haya yataongezeka kuwa mbaya zaidi muongo hadi muongo. Serikali, wafanyabiashara na watu binafsi wote wanauwezo wa kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi. Kadiri tunavyozidi kuchelewa ndivyo tunavyozidi kujiweka katika hatari na gharama zaidi kwa vizazi vya sasa na baadaye” Mwakilishi maalumu wa masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Neil Morisetti alitambua pia umuhimu wa ushahidi wa kina na kukubaliana na ripoti; “....inajenga msingi muhimu wa kuhakiki hitaji la kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi na hii itatumiwa na serikali duniani kuhabarisha namna ya kukabiliana na moja kati ya hatari kubwa tunayoikabili. Ushahidi mpana unaothibitisha kile ambacho tumekuwa tukifahamu kwa muda: dunia imekuwa ikiongezeka joto

kadiri ya mabadiliko ya tabia nchi. Hali ya hewa zisizo za kawaida zimekuwa zikijitokeza mara nyingi hivi sasa. Ni mpaka hapo ambapo tutachukua hatua kupunguza kusambaa kwa gesi za “greenhouse” na kipindi cha mpito cha gesi za ukaa za kiwango kidogo, matumizi bora ya rasilimali duniani, tunauwezekano mkubwa wa kushuhudia kuongezeka nyuzi joto mbili na uwezekano kabisa mpaka nyuzi joto tano katika joto la dunia mpaka mwisho wa karne hii. Hii inaashiria hatari katika uimara na ustawi wa dunia. Umuhimu wa kuchukuliwa hatua kidunia sasa lipo wazi” Ripoti inahitimisha uwepo wa ushahidi wa kisayansi ulio wazi kwamba vitendo vya binadamu vimesababisha ongezeko la joto katika mfumo wa tabia nchi katika karne iliyopita. Hii ni tofauti na namna ambavyo mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakitizamwa na kuhusishwa kwa upana wake. Dondoo kwa wahariri: Madokezo toka katika muhtasari wa AR5: Joto kidunia limezidi kwa nyuzi joto 0.9 toka mwaka 1901. Kiwango cha maji ya bahari kimeongezeka takribani mita 0.2 toka mwaka 1901, na kiwango cha kukua kinaongezeka. Theluji katika bahari ya Arctic katika kipindi cha joto imepungua kwa eneo takribani asilimia 40 tangu mwaka 1979. Tabaka la theluji katika mabara ya Greenland na Antarctic yamekuwa yakipungua uzito kama ilivyo kwa matabaka ya theluji kwingineko duniani. Majanga ya hali ya hewa yaliyokithiri ya hali ya hewa na tabia nchi yamekuwa yakiongezeka na yanategemewa kuongezeka zaidi katika muongo unaokuja. Ripoti kamili kwa watunga sera inapatikana: hapa.

Uingereza imethibitisha kupunguza uchafuzi wa hewa kwa asilimia 34 mpaka ifikapo mwaka 2020 na asilimia 80 ifikapo 2050 kulinganisha na viwango mnamo mwaka 1990. Malengo haya yamewekwa kisheria: Sheria ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (2008), na utendaji wa kiserikali dhidi ya hilo unakuwa unafatiliwa na kamati huru ya mabadiliko ya tabia nchi. Tunaendelea kuondosha hewa ya ukaa katika sekta ya nishati, usafirishaji na uchumi na kuweka motisha kupunguza matumizi ya ndani ya nishati. Muswada wa Nishati unaopendekezwa utawezesha teknolojia ya kutoa gesi ya ukaa kwa kiwango kidogo kushindana katika soko la umeme na kuvutia uwekezaji. Kimataifa, tunafanya kazi kuhakikisha kufunga mkataba wa dunia katika kupunguza uchafuzi wa hewa kupitia Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabia nchi (UNFCCC), kongamano la vyama mnamo mwaka 2015. Tumekubaliana kama sehemu ya Umoja wa Ulaya, kuingia katika kipindi cha pili cha makubaliano kadiri ya Mkataba wa Kyoto na wanahimiza Umoja wa Ulaya kufikia asilimia 30 ya kupunguza uchafuzi wa hewa kama malengo ya mwaka 2020 na asilimia 50 kwa mwaka 2030 kadiri ya makubaliano ya kimataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Sambamba na hili, Uingereza inatoa paundi Bilioni 3.87 kupitia mfuko wake wa kimataifa wa kusimamia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi (International Climate Fund) kusaidia nchi zinazoendelea, kudhihirisha utoaji mdogo wa gesi ya ukaa, kulinda misitu na kusaidia nchi masikini kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Dawati la Habari Kitengo cha habari na digiti-Ofisi ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola.

Taarifa zote mpya zinapatikana katika ukurasa wa Ofisi ya Mambo ya Nje gov.uk na tovuti: www.gov.uk/fco Fuatilia akaunti ya Waziri wa Mambo ya Nje kupitia facebook na katika twitter: @WilliamJHague Fuatilia Ofisi ya Mambo ya Nje kupitia akaunti ya twitter @foreignoffice Fatilia Ofisi ya Mambo ya Nje kupitia facebook na Google+ Bofya hapa matangazo au baruapepe kupata taarifa.

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na; Michael Dalali Afisa Miradi na Habari Ubalozi wa Uingereza Dar es Salaam Simu: +255 (0) 22 229 0269 Simu ya Mkononi: +255 (0)762 791 991 Baruapepe: michael.dalali@fco.gov.uk

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful