You are on page 1of 2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Pambika na Samsung yafanya droo ya kwanza kuelekea sikukuu za Mwisho wa Mwaka


Dar es Salaam, Tanzania, Novemba 18, 2013. Inawezekana ikawa bado hatujaanza kufikiria kuhesabu siku ngapi zimebaki kusheherekea Krismasi lakini hiyo haiwafanyi Samsung Tanzania kutoanza kuonyesha furaha za kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ambapo hapo jana kupitia promosheni ya Pambika na Samsung ilitangaza majina ya washindi wa kwanza waliojinyakulia zawadi mbalimbali. Droo hiyo ya kwanza imetoa washindi kutoka sehemu mbalimbali nchini, huku washindi wote watakabidhiwa zawadi zao katika sherehe Maalum za kuwakabidhi siku ya Jumatano katika eneo maarufu la kibiashara la Quality Centre jijini Dar es salaam. Droo hii ni ya kwanza ya Pambika na Samsung ambapo washindi hupatikana kwa kuinunua bidhaa za Samsung na kuzisajili katika huduma maalumu ya e-warranty. Napenda kuwapongeza washindi wote wa Pambika na Samsung katika droo yetu hii ya kwanza. Ushiriki wa wateja wetu kwa hii wiki ya kwanza imekuwa ya mafanikio makubwa na mwenendo wa promosheni yetu ni wa kuridhisha wenye kushika kasi kadri siku zinavyokwenda. alisema Bw. Sylvester Manyara, Meneja Masoko Rejareja wa Samsung Tanzania mara baada ya droo. Sumsung inashukuru kuendelea kuungwa mkono na mapokeo mazuri tunayoyapata toka kwa wateja wetu, bado tunahamasisha kila mmoja kushiriki katika promosheni hii ya Pambika na Samsung na kujiweka katika nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali zilizopo katika soko kila wiki kuanzia Jokofu la Samsung, jiko la kupashia chakula, jiko la umeme, deki ya DVD, luninga ya inchi 32 yenye teknolojia ya LED, kompyuta, muziki wa nyumbani, Galaxy 10.1 tablet na mashine za kufulia nguo kutoka Samsung aliongeza Bw. Manyara. Washindi wote wa wiki hii wametangazwa kupitia droo iliyofanyika chini ya uwangalizi wa msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) katika tukio lililofanyika makao makuu ya Samsung Tanzania jijini Dar es salaam. Droo zinafanyika kila Jumatatu ya kila wiki na washindi kukabidhiwa zawadi Jumatano. Ikiwa imeanza Novemba 7, 2013, Pambika na Samsung inalenga kumpa nafasi ya mteja wa Samsung kufurahia thamani ya kutumia bidhaa halisi za Samsung huku akipata faida za warranty ya miezi 24. Samsung tumejitolea kutengeneza bidhaa halisi zenye ubunifu na kukidhi soko la Afrika, bidhaa zote ni rafiki kwa mtumiaji na zinatoa nafasi kwa kila mtu kufurahia mkataba wa miezi 24 kwa ajili ya matengenezo bure. Pambika na Samsung inalengo la kuwazawadia wateja wetu zawadi za sikukuu za mwisho wa mwaka baada ya kuinunua na kusajili bidhaa yake. Promosheni hii ni moja kati ya njia nyingi za kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono kila siku. Alisema Bw. Manyara

Kupitia droo ya hii ya kwanza, Samsung wanategemea wateja kutoka maeneo mbalimbali ya nchi watahamasika zaidi na kushiriki katika promosheni hii katika wiki tano zilizobaki. Washindi wa wiki hii ni Beatrice Kessy (Dar es Salaam) ameshinda jokofu, John Mageretha (Dar es Salaam) ameshinda TV ya inchi 32, Erasto Mbwilo (Mkuu wa mkoa Manyara) ameshinda DVD player, Pius Antony (Dar es Salaam) ameshinda DVD player. Wengine ni Abasali Moledina (Dar es Salaam), Oscar Themu (Dar es Salaam), Siwema Edson (Mwanza) na Zulfika Hassan (Mbeya) wote wamejishindia DVD player kila mmoja, Khamis Khando (Dar es Salaam) ameshinda home theater system, Ally Abdallah (Dar es Salaam) ameshinda microwave, Christina Diweze (Dodoma) ameshinda laptop, Arnold Gumbo (Arusha) ameshinda microwave, Kennedy Manene (Mwanza) ameshinda Samsung home theater, Elawa Ramadhani (Moshi) ameshinda microwave. Baada ya kuinunua simu halisi za Samsung, mteja atatakiwa kusajili simu zao kupata huduma za miezi 24 bure kwa kutuma ujumbe mfupi wenye Namba za IMEI kwenda 15685. Kwa wale watakaonunua bidhaa nyingine za Samsung wanatakiwa wahakikishe mara baada ya kuinunua wanatakiwa wajaze fomu maalumu zinazopatikana katika maduka yote ya Samsung na mawakala wote nchi nzima alimalizia Bw. Manyara. Pambika na Samsung ni moja ya promosheni kubwa kuwahi kufanywa na Samsung nchini Tanzania. Promosheni hii ya kitaifa itawazawadia wateja wenye bahati bidhaa mbalimbali za Samsung na zawadi kubwa ya mwisho ni gari aina ya Mitsubishi Double Cabin ikiwa imejaa bidhaa za Samsung.

Kwa mawasaliano zaidi; Bertha Ikua bertha@spearheadafrica.com au 0759 252 252

Meneja

Huduma

kwa

Wateja