You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706 FAKSI: 255 22 2460735/2460700 Barua pepe: met@meteo.go.tz Tovuti: www.meteo.go.tz Unapojibu tafadhali nakili: Kumb. Na.: TMA/1622

S.L.P. 3056 DAR ES SALAAM

10 Februari, 2014

Taarifa kwa Umma: Matarajio ya kuwa na Vipindi vya Mvua kubwa, Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa.
Taarifa Na. Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Daraja la Taarifa: Kuanzia: Tarehe Mpaka: Tarehe Aina ya Tukio Linalotarajiwa 201402-01 Saa 11 Jioni Tahadhari 11 Februari, 2014 13 Februari, 2014

1. Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24) 2. Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0
Wastani (60%) 1. Vipindi vya Mvua Kubwa: Ukanda wa pwani mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Mbeya , Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa: Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya

Kiwango cha uhakika:

Maeneo yanayotarajiwa kuathirika 2.

Unguja na Pemba
Maelezo: Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga FOBANE kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka Pwani ya Somalia na misitu ya Congo kuelekea maeneo ya nchi yetu. Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari. Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi.

Angalizo: Maelezo ya Ziada

Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.