You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

M
Namba ya simu 2502572
Fax - +255252503734
E-mail:rpc.mbeya@tpf.com.tz
Unapojibu tafadhali taja

Ofisi ya Kamanda wa Polisi,


Mkoa wa Mbeya,
S. L. P. 260,
MBEYA.

MBR/C.5/900/B/VOL.I/44.
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141,
DAR ES SALAAM.

Tarehe: 11 Februari 2014.

YAH: TAARIFA YA ULINZI NA USALAMA KANDA NO 2 MKOA


WA MBEYA TAREHE 11.02.2014.
Tafadhali husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.
Pamoja na barua hii ninakutumia taarifa ya hali ya ulinzi na usalama Kanda no 2
Mkoa wa Mbeya ya masaa 24 yaliyopita kufikia tarehe 11.02.2014.
Naomba kuwasilisha tafadhali.

Kny

[ Barakael Masaki ACP ]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Nakala kwa: Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,


Makao Makuu ya Upelelezi,
S.L.P 9093,
DAR ES SALAAM. Kwa taarifa tafadhali.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
Mkoa wa Mbeya,
S.L.P 260,
MBEYA Kwa taarifa
1

S/N
1.

Tarehe
10.02.2014

Muda
18:00hrs

Maelezo ya kosa/Tukio

2.

10.02.2014

10:15hrs

MB/IR/1295/2014 KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA


MOSHI[GONGO]

TDM/TR/AR/03/2014 AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA


KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
Huko eneo la Kilimanjaro Kata na Tarafa ya Tunduma Wilaya ya
Momba Mkoa wa Mbeya Barabara ya Mbeya/Tunduma. Gari T.206
BVE aina ya Toyota Haice likiendeshwa na dereva asiyefahamika
jina wala makazi yake lilimgonga mtembea kwa miguu mtoto
asiyefahamika jina wala makazi yake jinsi ya kiume, umri kati ya
miaka 7-10 na kusababisha kifo chake wakati anapelekwa Hospitalini.
Dereva alikimbia na kutelekeza gari eneo la tukio. Kiongozi wa Zone
namba 13 Kanda B amekagua tukio. Upelelezi unaendelea.

Watuhumiwa
------

01.

Huko Mtaa wa Isyesye, Kata ya Itezi Tarafa ya Iyunga Zone namba


01 Kanda A Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika
doria/msako walimkamata SUZANA D/O MWANZA, miaka 29,
Msafwa, mkulima, mkazi wa Isyesye akiwa na pombe haramu ya
moshi [gongo] ujazo wa lita 12. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji
wa pombe hiyo.
3.

10.02.2014

10:00hrs

MB/IR/1294/2014 KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA


MOSHI[GONGO]

01.

Huko Mtaa wa Isyesye, Kata ya Itezi Tarafa ya Iyunga Zone namba


01 Kanda A Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika
doria/msako walimkamata EDINA D/O DAIMON, miaka 20, Kyusa,
mkulima, mkazi wa Isyesye akiwa na pombe haramu ya moshi
[gongo] ujazo wa lita 5. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa
pombe hiyo.
4.

10.02.2014

06:45hrs

LUP/RB/120/2014 KUPATIKANA NA BHANGI.


Huko katika Kijiji cha Nkungungu, Kata ya Lupa Tarafa ya
Kipembawe Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi
wakiwa katika doria/msako walimkamata LUSEKELO S/O SAMSON
@ MWAKABONGO,miaka 32, Kyusa, mkulima, mkazi wa Kijiji cha
Nkungungu akiwa na miche 16 ya bhangi katika shamba lake.
Mtuhumiwa ni mlimaji na mtumiaji wa bhangi. Kiongozi wa Zone
namba 23 Kanda D amekagua tukio na kushiriki kumkamata
mtuhumiwa, upelelezi unaendelea
.

A: Idadi ya watendaji.
Jumla ya askari 1,480 waliingia kazini, doria na malindo mbalimbali.
Jumla ya watumishi raia waliopo ni 21.

01.

Jumla ya vikundi vya ulinzi jirani vilivyopo Mkoa wa Mbeya 262, jumla ya vikundi
vilivyoshiriki ni 96 na walinzi 391 walishiriki katika doria/malindo mbalimbali.
Jumla ya askari Mgambo waliopo Mkoa wa Mbeya ni 2,257.
Jumla ya Polisi wasaidizi waliopo ni 23.
B: Migogoro mbalimbali.
Kisiasa Hakuna.
Wakulima na Wafugaji hakuna.
Wakulima/Wananchi na Wawekezaji Hakuna
Dini Hakuna.
Wafanyabiashara na Serikali [TRA] Baadhi ya maduka Jijini Mbeya pamoja na
baadhi ya Wilaya yalifungwa baada ya wafanyabiashara kupinga matumizi ya mashine
za Ki-elekroniki kutumika katika biashara zao kama walivyoagizwa na Mamlaka ya
Mapato nchini [TRA]. Hata hivyo hakuna matukio ya uvunjifu wa amani yaliyoripotiwa
kutokea. Ufuatiliaji unaendelea.
C: Mafanikio yaliyopatikana.

Mafanikio yaliyopatikana kupitia doria,misako na operesheni ni kama ifuatavyo:-

Bhangi - 01- Miche 16 ya bhangi Wilaya ya Chunya.


Dawa za kulevya {drugs} Nil
Pombe ya Moshi 02 Ujazo wa lita 17 eneo la Isyesye Jijini Mbeya.
Silaha Nil
Nyara za Serikali Nil
Wahamiaji haramu Nil
Noti bandia - Nil

D: Ukamataji wa makosa ya Usalama barabarani.


Jumla ya makosa yaliyokamatwa 126.
Jumla ya Makosa yaliyolipa faini 9112
Jumla ya magari yaliyokaguliwa kwa siku - 08.
Tozo lililopatikana kutokana na ukaguzi wa magari 215,000/=
Kesi zilizopelekwa Mahakamani 01.
Jumla ya tozo [Notification] Tshs 3,360,000/=
E: Watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa mbalimbali.
3

Jumla ya watuhumiwa waliokamatwa ni 27.


Jumla ya wahalifu wazoefu{harbitual} Mkoa wa Mbeya - 139.
Wahalifu wazoefu {Harbitual } waliokamatwa - Hakuna
Jumla ya wahalifu waangaliwa{Supervisee} Mkoa wa Mbeya - 82.
Wahalifu waangaliwa {Supervisee} waliokamatwa Hakuna
Jumla ya kesi zilizofikishwa Mahakamani 41
Kusomewa mashtaka 7
Jumla ya kesi zilizosikilizwa 16
Jumla ya kesi zilizotajwa 13
Watuhumiwa waliofungwa {Convicted} 01.
Watuhumiwa waliachiliwa huru {Acquited}- 4.
.