You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UCHUKUZI

MAMLAKA YA HALI YA HEWA


Simu: 255 22 2460706-8 Telefax: 255 22 2460735, 2460700 Barua pepe: met@meteo.go.tz S.L.P. 3056, DAR ES SALAAM

Tovuti: www.meteo.go.tz Tafadhali jibu: 26/02/2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YAKUTANA NA WANAHABARI KUTATHIMINI WARSHA ZA WANAHABARI NA UTEKELEZWAJI WAKE KATIKA USHIRIKISHWAJI NA USAMBAZAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA ZA UTABIRI WA MSIMU NA TAHADHARI Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imekuwa ikikutana na wanahabari katika kuandaa utabiri wa msimu ili kupata michango yao na kuifanyia kazi kadri inavyowezekana kwa lengo la kuhakikisha taarifa sahihi zinatolewa kwa wakati muafaka. Baada ya kukutana na wanahabari hao katika warsha zaidi ya tatu ikiwemo ile ya lugha itumikayo katika kutoa utabiri wa msimu, TMA imeona ni wakati muafaka sasa kwa Mamlaka kuweza kupata mrejesho ili kuweza kuboresha ushirikiano wake na vyombo vya habari katika kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa jamii Akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi alisema anavishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano ambao umewezesha taarifa za tahadhari ya hali mbaya ya hewa kuifikia jamii kwa wakati muafaka. Alisisitiza kwamba kikao hicho ni cha muhimu kwani pamoja na mambo mengine kitajadili changamoto wanazokutana nazo wanahabari katika kufikisha taarifa za utabiri kwa walengwa.Dkt Kijazi aliongezea kwa kusema kikao hicho kitatoa mapendekezo ambayo yataiwezesha Mamlaka kuboresha namna ambavyo taarifa za hali ya hewa zinafungashwa (packaging) ili wanahabari wazielewe na hivyo kuwafikia walengwa zikiwa sahihi na kwa wakati. Aliwaambia

wanahabari wawe huru wakati wowote kuulizia jambo lolote linalohusu hali ya hewa ili kupata ufafanuzi utakao wawezesha kutoa taarifa sahihi Mshiriki kutoka TBC1 Bi. Mwasu Sware akizungumza kwa niaba ya wanahabari amesema hivi sasa mamlaka ya hali ya hewa imejitahidi sana kuwa karibu na vyombo vya habari na hivyo kuzifanya taarifa za TMA kuwafikia wananchi kwa wakati. Lakini pia TMA inatakiwa kutumia lugha rahisi na nyepesi ambayo haina misamiati mingi ya kisayansi ili kuwasaidia waaandishi kuelewa na hivyo kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii. Alisema ipo haja pia kwa TMA kuwa na task team[ waandishi maalumu] ambao watakuwa karibu zaidi na mamlaka ili kuweza kufanya kazi ya kuandika na kuripoti taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Aidha, alisema ni vyema mamlaka ikawa na utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo na pia kubadilishana mbinu mbalimbali za kutoa taarifa ili pia ziweze kuwavutia wasomaji. Akifunga mkutano huo Dkt. Agnes Kijazi aliwashukuru wanahabari hao kwa michango waliyoitoa na kusema TMA itayafanyia kazi mapendekezo yote waliyoyatoa. Alitoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuendeleza kazi nzuri wanayoifanya ya kuwafikishia wananchi taarifa za hali ya hewa kwa wakati. Aidha alisem a TMA itajadiliana na vyombo vya habari ili kuona uwezekano wa kuongeza wigo wa utangazaji wa habari za hali ya hewa. IMETOLEWA NA MONICA MUTONI; OFISI YA UHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Picha Na 9131: Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi akifafanua jambo kwa wanahabari. Picha Na 1913: Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali nchini.