JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA.

RPC. Namba ya simu 2502572 Fax - +255252503734 E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz

Ofisi ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, S. L. P. 260, MBEYA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 12.03.2014.  

MWANAMKE MMOJA AMUUA MUME WAKE KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI. JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIWA WATU WANNE KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA KUISHA.

MWANAMKE MMOJA AMUUA MUME WAKE KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI. MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ETINA SILUMBA (44) MKAZI WA MPEMBA WILAYA YA MOMBA AMEMUUA MUME WAKE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MISHECK MWASHIUYA (52) MKAZI WA MPEMBA WILAYA YA MOMBA KWA KUMKATA KISOGONI NA KICHWANI NA KITU KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA NA KISHA KUMVUNJA SHINGO NA MGUU WA KUSHOTO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 10.03.2014 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU KATIKA KIJIJI CHA IPAPA, KATA YA IPUNGA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI. UCHUNGUZI UNAONYESHA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI. MTUHUMIWA KABLA YA KUTENDA TUKIO HILO INADAIWA KULIKUWA NA UGOMVI KATI YAKE NA MAREHEMU. MTUHUMIWA AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIMAPENZI KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIWA WATU WANNE KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA KUISHA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ULILE ERASTO (30) 2. ERNEST MJEMBE (40) 3. HAMIS MWANYOMBOLE (28) NA 4. HALIDI SAULI (33) WOTE WAKAZI WA SOWETO JIJI NA MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAFANYABIASHARA YA KUUZA POMBE BAADA YA MUDA KUISHA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA MAJIRA YA SAA 01:15 USIKU WA KUAMKIA TAREHE 12.03.2014 KATIKA ENEO LA MAMA JOHN, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUFUATA NA KUZINGATIA TARATIBU ZA KUENDESHA/KUFANYA BIASHARA ZAO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

Signed by: [AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful