PRESS LEO 13.03.2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC.
Namba ya simu 2502572
Fax - +255252503734
E-mail:- rp.cmbeya@tpf.go.tz

Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
S. L. P. 260,
MBEYA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA
HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 13.03.2014.

 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU
WATANO KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI KUTOKANA
NA MISAKO ILIYOFANYIKA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WATANO [05]
KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI KUTOKANA NA MISAKO
ILIYOFANYIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO [05]
KUHUSIANA NA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI. KATIKA TUKIO LA
KWANZA ALPHONCE PATRICK [19] MKAZI WA KIJIJI CHA MBALA WILAYA
YA CHUNYA ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI KETE 10 ZENYE UZITO WA
GRAM 50. TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 11.03.2014 MAJIRA YA SAA 15:13
ALASIRI KATIKA KIJIJI CHA MBALA, KATA YA MBALA, TARAFA YA
KWIMBA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
AIDHA WATU WENGINE WAWILI 1.KILLY SHUSHA [18] NA 2. MLAWA
SAKSON [18] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MAGAMBA WILAYA YA
CHUNYA WALIKAMATWA NA JESHI LA POLISI WAKIWA NA BHANGI GRAM
KUMI [10]. TUKIO AMBALO LILITOKEA TAREHE 12.03.2014 MAJIRA YA SAA
11:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI NA KATA YA
MAGAMBA, TARAFA YA
SONGWE, KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
KATIKA TUKIO JINGINE WATU WAWILI 1. CHAZALI INYAMAGOHA [45] NA
2. SAMWEL MTOKOMA [50] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISONGOLE
WILAYA YA ILEJE WALIKAMATWA WAKIWA NA MALI IDHANIWAYO
KUWA YA WIZI. CHAZALI INYAMAGOHA ALIKAMATWA AKIWA NA
MIFUKO MINNE [04] YA SIMENTI NA SAMWEL MTOKOMA ALIKAMATWA
AKIWA NA NONDO 55 MALI INAYODHANIWA KUWA NI YA WIZI KUTOKA
KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA VODACOM. TUKIO HILO
LIMETOKEA TAREHE 12.03.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA
KIJIJI HICHO CHA ISONGOLE TARAFA YA BULAMBYA, KUFUATIA
DORIA /MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI
KWA JAMII KUACHA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA KUTUMIA
NJIA ZA MKATO KWANI HUWEZI KUPAMBANA NA UMASIKINI WA KIPATO
KWA NJIA ZA MKATO BADALA YAKE WANANCHI WAFANYE KAZI HALALI
KWA LENGO LA KUPATA KIPATO HALALI IKIWA NI PAMOJA NA KUNUNUA
MALI HALALI KATIKA SEHEMU HUSIKA. PIA KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA
SAHIHI NA KWA WAKATI KUHUSIANA NA UHALIFU NA WAHALIFU ILI
WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful