JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.


RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260,
Fax - +255252503734 MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31.07.2014. WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA
AJALI YA GARI MATUNDASI WILAYANI CHUNYA. MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI JIJINI
MBEYA.


 MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA
KIFUSI CHA MCHANGA WILAYANI CHUNYA.


 MTOTO WA MIAKA KUMI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI
YA UMEME.


KATI KA TUKI O LA KWANZA:

WATU WANNE WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. PAULO
MWASANGA (18) MKAZI WA KITONGOJI CHA MATUNDASI „B‟ 2. WEDI
ANGOLWISE (21) MKAZI WA MATUNDASI 3. SALOME MWAKIBETE (13)
MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI SAMBILIMWAYA NA 4.
OBEDI MWAKAMELA (25) MKAZI WA MATUNDASI WAMEFARIKI DUNIA PAPO
HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 CHU AINA YA FUSO
TIPPER LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA KIPINDUKA KATIKA
KIJIJI CHA MATUNDASI WILAYANI CHUNYA.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:00
JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MATUNDASI “B”, KIJIJI CHA MATUNDASI,
KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA CHUNYA/MAKONGOLOSI.

GARI HILO LILIKUWA LIKITOKEA KIJIJI CHA SAMBILIMWAYA KUELEKEA
KIJIJI CHA MATUNDASI LIKIWA LIMEBEBA WACHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU NA
MASHABIKI. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 51 WALIJERUHIWA, KATI YAO 26
WALITIBIWA NA KURUHUSIWA NA WENGINE 25 WAMELAZWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA
TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

KATI KA TUKI O LA PILI :

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WILE PETER AMBAYE
ALIKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKI AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI DFP 0036 AINA YA BENZ MALI YA SHIRIKA LA UMEME
TANESCO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA PATRICK MHAGAMA (46) MKAZI
WA ILOMBA JIJI MBEYA KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI ASIYEFAHAMIKA JINA
WALA MAKAZI YAKE NA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA HUYO.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 31.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:45
JIONI HUKO NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA
GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA.


KATI KA TUKI O LA TATU:

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA PASCALIA JIFULA NGASA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA
KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA MCHANGA KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA
WILAYANI CHUNYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA
08:300 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA, KIJIJI CHA MWAMBANI
CHINI, KATA YA MWAMBANI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA
WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA, MTOTO HUYO ALIKUWA
AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE KWENYE GEMA LA MCHANGA NA NDIPO
KIFUSI KUMUANGUKIA NA KUMFUNIKA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA
MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO
ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.


KATI KA TUKI O LA NNE:

MTOTO WA MIAKA KUMI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JERRY JESTED,
MWANAFUNZI NA MKAZI WA MLOWO WILAYANI MBOZI ALIKUTWA AMEKUFA
CHUMBANI KWAKE BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 06:00
ASUBUHI HUKO KATIKA KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA
MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI
BAADA YA MAREHEMU KULAMBA NYAYA ZA UMEME AMBAZO ZILIKUWA
KARIBU NA KITANDA CHAKE HALI ILIYOPELEKEA KUPIGWA SHOTI NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA
MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO
ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA IKIWA NI PAMOJA NA
KUWEKA MBALI VITU VYA HATARI KWA WATOTO.


Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Sign up to vote on this title
UsefulNot useful