You are on page 1of 1

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO KATIKA SHULE YA

SEKONDARI YA WAMA- NAKAYAMA KWA MWAKA 2015

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatangaza nafasi za kidato cha Tano mwaka
2015 kwa wasichana katika Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama iliyopo Nyamisati
Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani kwa tahsusi zifuatazo: PCM, PCB na ECA.
WAMA ni Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na Mhe. Mama Salma Kikwete ili kusaidia
maendeleo ya wanawake na watoto. WAMA inamiliki na kuendesha shule maalum kwa ajili ya
watoto yatima na wasio na uwezo.
Hata hivyo kwa sasa tunapokea wanafunzi wachache watakaolipia ili kusaidia uendelevu wa
shule. Mtihani wa kujiunga na kidato cha tano utakaotolewa na shule yetu utafanyika Machi 21,
2015 katika Shule ya Sekondari Jangwani-Dar es Salaam.
Fomu za kujiunga zinapatikana katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
zilizopo mtaa wa Luthuli, Dar es Salaam au katika Tovuti ya Taasisi:
www.wamafoundation.or.tz
Shule ni ya bweni ya wasichana na ina mazingira mazuri ya kujisomea pamoja vifaa muhimu
vya kujifunzia.
Kwa Mawasiliano zaidi:
Piga Namba: 022-2126516, 0754-086896, 0754- 439183
Barua pepe: info@wamafoundation.or.tz
Tovuti: www.wamafoundation.or.tz